TULIKOTOKEA......
KANISA LA KWANZA KUJENGWA-USHARIKA WA KWANZA KABISA
MAARUFU "POMERN" POMERINI
EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IRINGA DIOCESE
ADDRESS
P.O. Box 511,
IRINGA.
Phone +255 270 20 89
Fax +255 270 11
98
Website www.elctdira.org
IT’S ESTABLISHMENT
Iringa Diocese
was established in 26th
September, 1987 with registration number SO.6906
VISION STATEMENT
“…I came that
they may have life, and have it abundantly” (John 10:10b RSV)
MISSION STATEMENT
Iringa Diocese
exists to witness, live in Christian fellowship and to serve the people created
in the image of God Spiritually, Physically and Economically.
CORE VALUES
- Evangelization
- Christian nurture
- Unity in Christ
- Praise and worship
- To identify and uphold the life of poor and oppressed
- To work in partnership
LEADERSHIP
Bishop RT. REV. DR.
OWDENBURG MOSES MDEGELLA
Assistant to the Bishop REV. BLASTON TULUWENE GAVILE
General secretary MR. NAYMAN CHAVALLA
Treasurer MR. NOEL ILOMO
DEPARTMENTS
- Planning and Development Department
- Women and Family Nurture Department
- Mission and Evangelism Department
- Christian Education and Youth Department
- Theological Education by Extension Department
- Communication and Information Department
- Finance Department and
- Building Department.
- Training Unit
- Bega kwa Bega
- Mission to Normadic Societies
- Malaria and
- Pastors Spouses.
ON GOING PROJECTS
- Iringa Hope SACCOS- linked with Tumaini University where there are about 36 Congregations has joined SCCOS with the Capital of 120M
- Malaria Projects
- HIV/AIDS
- Ujana Project
- Afforestation -Sponsored by Lutheran Mission Cooperation (LMC)and
- Agriculture Demonstration Plots-under Institute of Agriculture Tumaini university Iringa-BKB, Paythrum
- Water project-St Paul Partners(SPP)-
- Furaha News Paper-Comin Soon!
CHURCH DISTRICT
The Diocese has Seven Church Districts namely;
- Northern Church District (Kihesa)
- Northwest Church District (Ilula)
- Western Church District(Kanisa Kuu)
- Southern west Church District (Ihemi)
- Southern Church District(Pomerini)
- Eastern Church District (Ipalamwa) and
- Southern east Church District(Idete).
CONGREGATIONS
The
Diocese has seventy nine Congregations
namely :-
- SOUTHERN CHURCH DISTRICT(POMERINI)
Pommern,Lukani,Kitowo, Ihimbo, Bomalang’ombe, Masisiwe,Mwatasi,Ugesa,Kipanga,
Usokami and Ukumbi.
- NORTHERN CHURCH DISTRICT (KIHESA)
Kihesa, Mlandege, MkimbiziNduli,ilambilole,Usolanga,Mtera,Mtwivila,Ikengeza,
Tumaini, Isimani and Migoli.
- SOUTHERN WEST CHURCH DISTRICT (IHEMI)
Ihemi,Ipogolo,Magulilwa,Ifunda,Kiponzelo,Masimike,Wasa,Mgama
nd Kitasengwa
- NORTHWEST CHURCH DISTRICT (ILULA)
Ilula,Luganga,Kipaduka,Image,Itungi,Irindi,Mbuyuni,Nyanzwa,Uhominyi,
Mbigili and Ilambo.
- SOUTHERN EAST CHURCH DISTRICT(IDETE).
Idete,Idunda,Muhanga,Kidabaga,MagomeNg’ang’ange,Kiwalamo,Idegenda,Wimbe,Itonya
and Ndengisivili.
- EASTERN CHURCH DISTRICT (IPALAMWA)
Ipalamwa, Makungu,
Kising’a, Mlafu, Ifuwa, Lulanzi, Kimala and Kilolo.
- WESTERN CHURCH DISTRICT(KANISA KUU)
Iringa Mjini,
Mkwawa,Kitapilimwa, Pawaga, Kidamali,Tungamalenga, Mlowa, Magubike and Kiwele.
HEALTH
The Dioceses has Ilula Hospital which is
Designated Hospital for Kilolo District and eight dispensaries;
- Pommern Dispensary
- Ideate Dispensary
- Ipalamwa Dispensary
- Ruaha Mbuyuni
- Ihimbo Dispensary
- Tungamalenga Dispensary and
- Image Dispensary.
- Lulanzi-
- Idunda-First aid
EDUCATION
The Diocese owns:-
- Iringa University
- Ilula Nursing School at Ilula to be introduced soon
- Pommern Secondary School at Pommern Village
- Lutangilo Secondary School at Idete
- ,Image Secondary School at Image
- Bomalang’ombe Secondary School at Bomalang’ombe
- Ipalamwa Secondary School at Ipalamwa
- Mtera Secondary School at Mtera and
- Malecela Secondary School at Kidatu Morogoro
HISTORIA YA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ni muungano waKilutheri katika nchi ya Tanzania. Mwaka 1938 makanisa
saba yaKilutheri yaliungana kama Muungano wa Makanisa ya Kilutheri, na tarehe 19 Juni 1963 yalikuwa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.
Lengo la KKKT ni kuwapa watu nafasi
ya kumfahamu Yesu Kristo ili kupata maisha ya milele. Kanisa
limejengwa juu ya msingi wa Yesu Kristo, limeongozwa na Neno la Mungu (Biblia) kama linapatikana katika Agano la Kale na Agano Jipya, na limeimarishwa katikasakramenti.
KKKT linaongozwa na Mkuu wa kanisa
(askofu Mkuu) na maaskofu ishirini kutoka dayosisi ishirini, wakiwa na
wanachama zaidi ya milioni .
Ofisi kuu wa KKKT imo katika mji wa Arusha. KKKT linalo uhusiano na All Africa Conference of Churches (AACC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Lutheran World Federation (LWF)
na Lutheran Mission Cooperation (LMC).
SEHEMU
YA HISTORIA YA DAYOSISI YA IRINGA
Makabila yanayoishi
katika eneo linalokaliwa na KKKT Dayosisi ya Iringa ni Wahehe ambao ni wengi
kuliko makabila mengine, Wabena, wakinga na wawanji.[1]
Makabila mengine ni Wagogo, Wambugwa, Wasagala, Watiliti pamoja na makabila ya
wahamiaji wakazi. Yapo pia makabila ya wafugaji waliohamia kwenye eneo hili,
kama vile wamasai, wabarbaig na wasukuma.
KKKT Dayosisi ya Iringa
ina historia inayorudi nyuma hadi mwaka 1899, mwaka ambapo Mmisionari wa Kijerumani
Mch. Wilhelm Neuberg alianzisha stesheni mahali paitwapo itonya katika milima
ya Udzungwa. Mchungaji huyu aliitwa na wenyeji wa eneo la Itonya kama “Mwambetani “kwa lugha ya kihehe
ikimaanisha mnavuna nini? Hii
ilitokea kwasababu kila alipohubiri alikuwa akiwauli mnavuna nini kutoka kwenye
neno ninalo hubiri.[2] Kazi
hii ya Injili iliyoanzishwa na Mch. Neuberg iliwezesha kutokea kwa sinodi ya
Ubena-Uhehe mwaka 1902.
Chanzo halisi
kilichosababisha Injili kuingia Itonya ni kwamba kulikuwa na mtu aliyeitwa
Mwamagelanga mzaliwa wa maeneo ya Idete alikuwa anafanya kazi katika mashamba
ya chai Lupembe huko Njombe. Mtu huyu aliamua kumuomba mmisionari mmoja kwa
kumwambia kuwa watu wa maeneo ya Itonya wanahitaji Injili, ndipo mmisionari huyo
aqliyeitwa Neuberg akawaambia wenzake na akakubali kupeleka Neno la Mungu katika
maeneo ya Itonya. Inasadikiwa kuwa Wakristo wa kwanza kubatizwa walikuwa Aron
Kikoti, Lupituko Mkemwa, Yehoswa Kikoti na ndio waliokuwa walimu na wahubiri
wakiwa wanapata posho ya shilingi tano kwa mwezi.[3]
Stesheni nyingine
ilianzishwa na Mch.Julius Oelke mahali paitwapo Ilutila katika milima ya
Udzungwa pia. Stesheni hii ilipewa jina la Kijerumani liitywalo Neustettin, lenye maana ya ‘stesheni
mpya’, hilo ni jina la mji mkuu wa eneo la Pommern katika Ujerumani ya
Mashariki ya wakati ule na katika nchi ya Poland ya sasa.
Kufika mwaka 1930
mmisionari mwingine wa Kijerumani aitwaye Mch. Herman Neuberg mtoto wa Mch.
Wilhelm Neuberg mwanzilishi wa stesheni ya Itonya alipewa wajibu wa kusimamia
eneo la Kikanisa la Ubena-Uhehe na ulanga makao yake yakiwa pale Pommern katika
nchi ya Wahehe mahali ambapo pia Herman Neuberg alizikwa baada ya kufariki
mwaka 1969.[4]
Mch. Martin Nordfeldt
kutoka Sweden, akisaidiana na Mch. Herbert Uhlin, alifika Ilula mwaka 1938.
Nordfeldt na Uhlin walikuwa wametumwa na chama cha wamisionari cha SEM (Swedish
Evangelical Mission). Kwenye utumishi wake Mchg Nordfeldt alishirikiana na
mtumishi mwenyeji, Mch. Yohana Nyagawa aliyekuwa mkuu wa kanisa la Ubena –Uhehe
mwaka1940 mpaka 1941. Juhudi za watumishi hawa ziliwezesha kuanza kwa ujenzi wa
nyumba ya ibada katika stesheni ya Ilula pamoja na ujenzi wa shule ya Ilula iliyosimamiwa
na na Mwl.Tulawona Luka. Baada ya hapo shule zaidi zilianzishwa, zikiwemo
Uhominyi- 1941, Balali – 1943, Ukwega – 1943, Ibumu – 1945, Ikokoto – 1946,
Lyasa – 1953, Ihimbo – 1954 na Kitowo – 1955. Baadhi ya walimu wa Kiafrika
walioshiriki kuanzisha shule hizi ni Yeremia Mlagala, Alexander Nyadzi, Yoeli Mhoka, Toplas Nsemwa, Enock Mkocha,
Yeremia Msola, Allan Chambile, Yoeli Lubazimwa, na Emmanuel Muyula. Kazi ya
injili iliyoanzishwa na wamisionari miongoni mwa Wahehe na Wabena iliwezesha
kuanzishwa pia kwa zahanati na shule ya Biblia. Kwa mfano, mwaka 1953 zahanati
ya kilutheri ya Pommern ilianzishwa na mtaalamu wa mataibabu aitwae Luhangano
Badi; na tarehe 3/2/1953 shule ya Biblia ya Kidugala ilianzishwa. Shule hii
ilipokea wanafunzi wanane wa kihehe waliokuwa wamepelekwa hapo kwa masomo ya
uinjilisti.
Kufika mwaka 1957 eneo
la Wahehe lilishakuwa na sharika tano za kilutheri ambazo ni Ihemi, Ilula,
Idete na Iringa Mjini na mwaka 1959 uliweka historia ya kipekee kwasababu ni
mwaka ambao Kanisa la Kiinjili katika Tanganyika ya kusini lilianzishwa, Kanisa
ambalo Rais wake alikuwa Mchg. John Nilsson. Tarehe 6/3/1960 ilikuwa ni siku ya
huzuni kwasababu Mchg. Yosefu Kiwope
alifariki dunia na kuzikwa pale Pommern, lakini mwaka uliofuata (yaani 1961)
mbinu mpya za kielimu na za kimatibabu ziliwekwa. Kwa juhudi za Kanisa la
Kilutheri zaidi zilianzishwa, kama vile shule ya msingi Pommern (1961 chini ya
uongozi wa Mwl. Philemon Chambile), na Bomalang’ombe (1963 chini ya uongozi wa
Mwl. Abel Chongola). Mwaka 1963 mmisionari Henrik Smedjebacka alichaguliwa kuwa
Rais wa Kanisa la Kinjili Tanganyika Sinodi ya Kusini, na mwaka 1964 Zahanati
ya Kilutheri Idete ilianzishwa. Mwaka uliofuata 1965 Mchg.Lupumuko Lugala
aliteuliwa kuongoza jimbo la Iringa-Uhehe na mwaka 1966 Mchg. Herman Neusberg
alizindua rasmi jengo la ibada lililoko Iringa mjini.
Mwaka 1967 Mmisionari
Ulla Svenson alifungua rasmi shule ya ufundi ya Kilutheri Mafinga na mwaka
huohuo Mchg. Lunogelo Vuhahula alichaguliwa kuwa mkuu wa Jimbo la Iringa –
Uhehe. Wakati huU eneo la Uhehe lilikuwa na jumla ya sharika saba, zikiwemo
sharika za Ismani na Masisiwe. Mwaka 1969 Mchg.Herman Neuberg alifariki dunia
na kuzikwa Pommern na mwaka 1970 Mchg. Allan Chambile alikabidhiwa wajibu wa kuongoza
jimbo la Iringa – Uhehe. Jimbo la Iringa lilianza rasmi mwaka 1977 na
Mchg.Israel Kiponda alichaguliwa kuliongoza. Kwenye mkutano uliofanyika Lupembe
mwaka 1979 palifanywa uamuzi ya kufuata
uongozi wa kiaskofu katika KKKT Sinodi ya Kusini na Katiba ilisomwa kwa
mara ya kwanza.
Katiba ilisomwa kwa
mara ya pili mwaka 1980 kwenye mkutano uliofanyika Mafinga na majukumu ya Askofu
yalikubaliwa rasmi. Kwenye mkutano uliofanyika Makambako mwaka 1981 Mch. Dk. Yuda
Kiwovele alichaguliwa kuwa Askofu wa kwanza wa iliyokuwa Sinodi ya Kusini na
Mch. Levi Nsemwa alichaguliwa kuwa Msaidizi wa Askofu. Viongozi wengine
waliochaguliwa ni Ndg. Obadia Kasumba (Katibu Mkuu) wa Sinodi ya Kusini, Henrick
Hult (Mtunza hazina) wa Sinodi na Mch. Nicholas Mwachusi kuwa (Mkuu wa jimbo la
Iringa).
Mwaka 1986 ulikuwa na
historia ya kipekee kwa kanisa la Kilutheri katika eneo la Iringa. Kwenye
mkutano uliofanyika Chimala tarehe 2-7 mwezi Novemba mwaka 1986 Jimbo la Iringa
liliagizwa lijiandae kuwa Dayosisi inayojitegemea. Kuhusiana na agizo hili
viongozi kadhaa wa Dayosisi iliyokuwa inaandaliwa kutokea walichaguliwa. Baadhi
ya viongozi hawa ni Mch. Nicholas Mwachusi, Mchg. Owdenburg Mdegella, Bw.
Tuluwene Kulanga na Mwinj. Gerson Munyi. Wakati huo huo Katiba ya Dayosisi mpya
ilikamilishwa na kukubaliwa na Mkutano Mkuu wa Dayosisi teule ya Iringa. Wachungaji
wa kwanza wenyeji ni Yohana Nyagawa,Joseph Kiwope.Yeremia Mlagala,Lutangilo
Mdegela,Iskaka Luvinga na Lupumuko Lugala.[5]
Kikao cha Halmashauri Kuu na cha Mkutano Mkuu wa KKKT vilivyofanyika Arusha na Korogwe mwaka 1986
vilikubali Dayosisi ya Iringa kuanza. Kibali hiki cha KKKT kiliwezesha viongozi
rasmi wa Dayosisi mpya ya Iringa kuchaguliwa, kwenye mkutano mkuu uliofanyika
tarehe 8/10/1986. Viongozi waliochaguliwa ni Mchg. Owdenburg Mdegella (Askofu
mteule), Mch. Nicholous Mwachusi (Msaidizi wa Askofu), Bw. Edward Mnyawami
(Katibu mkuu) na Mwinj. Gerson Munyi (Mtunza
hazina).
Baada ya viongozi hawa
kuchaguliwa, KKKT Dayosisi ya Iringa ilianza rasmi tarehe 01/01/1987 ikiwa na
majimbo matano (Iringa Mjini, Pommern, Idete, Ilula, na Ihemi) na sharika ishirini
na nne 24. Askofu Mdegella aliwekwa wakfu kuwa askofu wa kwanza wa Dayosisi ya
Iringa tarehe 27/9/1987, siku ambayo Dayosisi hiyo iliingia katika historia
kubwa ya kuzinduliwa rasmi na Mch. Nicholas Mwachusi kuingizwa kazini kama
msaidizi wa kwanza wa Askofu wa Dayosisi ya Iringa.
Miongoni mwa mambo ya
kukumbukwa katika Dayosisi Iringa ni lile la tarehe 20/11/1991 ambapo Dayosisi iliweka
historia mpya baada ya kumbariki Mtheolojia Tuseline Kihwele Madembo kuwa
mwanamke wa kwanza Mchungaji. Historia hiyo ya kipekee imerudiwa tena mwaka
1998 ambapo. Mch. Agnesi Kulanga amekuwa mkuu wa Jimbo mwanamke wa kwanza katika
Dayosisi ya Iringa. Mchungaji Agnes Kulanga ana historia ndefu katika kanisa
kwakuwa alishiriki mkutano mkuu wa kwanza wa KKKT mwaka 1963 huko Bukoba
uliojadili na kuunganisha makanisa saba na kuunda KKKT. Wakati huo aliwakilisha
vijana wa ukanda wa Kusini. Hadi kufikia mwaka 2012 Dayosisi ya Iringa ina
wachungaji wanawake 34.[6]
Makao makuu ya Dayosisi
ya Iringa yapo mjini Iringa. Kulingana na takwimu za mwaka 2012 Dayosisi ya
Iringa ilikuwa na jumla ya sharika sabini na nne (74) zinazounda majimbo saba
(7). Majimbo hayo ni Jimbo la Magharibi, Jimbo la Kaskazini, Jimbo la
Kaskazini-magharibi, jimbo la Mashariki, Jimbo la Kusini, Jimbo la Kusini-
Mashariki na Jimbo la Kusini- Magharibi. Hadi kufikia mwaka 2012 kulikuwa na
wakristo wapatao 102,652, wachungaji 168, wainjilisti 496, mitaa 676 na nyumba
za ibada 526.[7] Hii
ni ishara ya kukua kwa kanisa kwasababu Dayosisi hii ilipoanza mwezi Januari
1987 palikuwepo majimbo matano tu na sharika ishirini na nne tu. Majimbo
yaliyokuwepo mwanzoni ni Idete (sharika tano), Pommern (sharika tano), Iringa
mjini (sharika nne), Ihemi (sharika nne), Ilula (sharika sita).
Vilevile Dayosisi ya
Iringa kufika mwaka wa 2012 imepiga hatua kubwa katika elimu kwa kuwa na chuo
kikuu cha Tumaini –Iringa, Chuo cha Uinjilisti kwa wafugaji Ilambilole, shule
saba za sekondari ambazo ni Pommerini, Mtera, Malecela, Bomalang’ombe,
Ipalamwa, Image na Lutangilo, Kuna shule za awali nne. Pia kuna Hospitali moja ya
Dayosisi (Hosptali teule ya wilaya ya Kilolo (DDH). Kuna zahanati 8 ambazo ni
Pommerini, Ihimbo, Tungamalenga, Image, Ipalamwa, Idete, Idunda na Ruaha
Mbuyuni. Kuna vituo vya Dayosisi ambavyo ni Kituo cha Diakonia, Redio Furaha na
Lutheran Centre.[8]
Kuna Idara na vitengo,
ambavyo ni Kitengo cha Mahusiano (Bega kwa Bega), Mafunzo, Muziki, na Ukaguzi
wa Ndani. Idara zilizopo ni Idara ya Mipango na Maendeleo, Idara ya Uinjilisti
na Missioni, Idara ya Vijana na Elimu ya Kikristo. Idara ya Wanawake watoto na
Malezi ya Familia, Idara ya Habari na Mawasiliano, Idara ya Utabibu na Diakonia,
Idara ya Maandiko na Tafsiri ya Biblia, Idara ya Ufundi Majengo na Viwanja na
Idara ya Theolojia kwa Enezi (ETE). [9]
Idara ya ETE imekuwa na
mchango mkubwa katika Dayosisi ya Iringa kwa kuelimisha na kuongeza idadi ya
watumishi kwenye ngazi ya mtaa na sharika. Ilianzishwa mwaka 1985 katika usharika
wa Ihemi. Watumishi ambao wamekuwa wakiandaliwa ni katika ngazi ya wainjilisti,
wazee wa kanisa na wakristo raia. Dayosisi ya Iringa iliamua kuanzisha ETE kwa
makusudi kwaajili ya kuelimisha watumishi wake. Baba Askofu Dkt. O. Mdegella
akishirikiana na wamisionari toka chama cha missioni cha Sweden (Swedish
Evangelical Mission – SEM) ndio wanzilishi wa mpango huo. Wamisionari hao
ni Mchg. Stefano Holmstrom aliyepokea
wazo na baadaye Mchg. Dkt. Anders Petter Sjodin alipokea na kuendeleza kazi
hadi sasa kuna watumishi wengi ambao
wamepitia mafunzo hayo.[10]
Maandiko yaliyochapishwa
- KKKT
Dayosisi ya Iringa, Toleo maalumu la Jubilee Miaka 100 KKKT Dayosisi ya
Iringa (1899-1999): Inter Press of Tanzania, Dar es salaam
- KKKT
Dayosisi ya Iringa; Miaka 100 ya
Injili Uheheni 1899-1999, Wokovu umefika Kwako
3.
Mdegella Yockbeth; From Itonya to Pommern: Historical Development of the First Two Mission
Station; BD Research Paper. Makumira,
Tanzania 2007.
Taarifa
zilizo andikwa
- Taarifa
ya Maendeleo ya Idara ya Elimu ya Theolojia kwa Enezi (ETE), KKKT Dayosisi
ya Iringa, 2012
- Takwimu
za KKKT Dayosisi ya Iringa (Profile)
2012, Iringa
Mahojiano
- Mahojiano
na Mchungaji Agnes Kulanga 8/10/2012
VITABU NA MAANDIKO REJEA
[1]
Tazama; DIRA, Toleo maalumu la Jubilee Miaka 100 KKKT Dayosisi ya Iringa
(1899-1999), 9
[2]
Tazama Yockbeth L. Mdegella; From Itonya
to Pommern: Historical Development of the First Two Mission Station; BD Research
Paper. Makumira, Tanzania 2007.
[3]
Tazama KKKT Dayosisi ya Iringa; Miaka 100
ya Injili Uheheni 1899-1999, Wokovu umefika Kwako (Luka 19:9),13.
[4]
Tazama, Mwaduma, Dates and Important
Events of Iringa Diocese 1899-1999,1
[5] Tazama; DIRA, Toleo maalumu la
Jubilee Miaka 100 KKKT Dayosisi ya Iringa (1899-1999), 10.
[6] Tazama Takwimu za KKKT Dayosisi
ya Iringa (Profile) 2012; Mahojiano na
Mchungaji Agnes Kulanga 8/10/2012
[7] Tazama, Takwimu za KKKT Dayosisi
ya Iringa (Profile) 2012.
[8] Ibid
[9] Ibid
WACHUNGAJI WASTAAFU 2012/13
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
TAARIFA YA
KAMATI YA KICHUNGAJI YA MAASKOFU
ILIYOTOLEWA
15/01/2012 KATIKA KANISA KUU-IRINGA MJINI
TAMKO HII
ILISOMWA NA MWENYEKITI WA KAMATI ASKOFU DKT. HANCE MWAKABANA
Utangulizi
Mimi
nilipomaliza masomo yangu ya Theoligia
nilianza kazi hapa Iringa wakati huo nikiwa kijana kabisa.Nikiwa
masomoni niliandika juu ya Iringa katika andiko langu-kitabu kipo. Wakati ule
Iringa mjini ulikuwa usharika mmoja tu na sasa ni sharika nyingi . Hivyo
niliyoandika yamekuwa ya kuleta maendeeo na amani katika Kanisa.
Mwaka
jana mwezi wa tano tulikuja hapa na baadaye jopo la Maaskofu wa K.K.K.T
lilikuja hapa Iringa na kufanikiwa
kukutana pale katika kituo chetu cha
Huruma Centre 10/10/2011. Katika mkutano ile tulizungumza na Wachungaji na
baadaye wajumbe Halmashauri Kuu. Patano lilikuwa kamati ile ya maaskofu watatu
irudi tena baada ya miezi mitatu ili kuliweka sawa jambo hili, ifanye kazi kama
ilivyokuwa imepangwa awali.
Siku ya Jumatatu 09/01/2012 sisi watatu
tulikutana jioni pale Dar-es-Salaam na siku ya
Jumanne tuliwasili hapa Iringa.
Ujumbe wetu ulikuwa na
- BABA ASKOFU DKT. HANCE MWAKABANA- Mwenyekiti wa Kamati
- BABA ASKOFU DKT. MARTIN SHAO- Mjumbe
- BABA ASKOFU ELISA BUBERWA -Mjumbe
Jumatano
- Kukutana na viopngozi waandamizi wa Dayosisi (Managementi)
- Kukutana na watumishi wote wa Ofisi Kuu ya Dayosisi mmoja mmoja.
- Kukutana na Wanachuo –Watheolojia na Walimu pia tulikutana nao
Alhamisi
- Kukutana na Wakristo raia –waljitokeza wengi wa kutosha
- Kukutana na Baba Askofu
- Kukutana na wenye neno- waliweza kusema kwa uhuru mmoja mmoja na wakati mwingine kundi kwa kundi
Ijumaa
- Tulikutana na Wachungaji na wajumbe wa Halmashauri Kuu
Jumamosi
- Kumkutanisha na wenye neno au malalamiko dhidi ya Baba Askofu / Uongozi wa Dayosisi.
- Kukutana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu –Tuliwabadilishia ratiba kama mara nne hivi hivyo tulikutana nao mnano saa 4:30-6:35 usiku
MASWALI/MAMBO MATATU
A. Picha uliyo nayo ni picha ya
namna gani?
B. Je; umesikia haya yanayosemwa-
juu ya Dayosisi?- ndiyo yapo lakini hatujuwi ukweli wake.
-kusaidia
turudi katika amani, haya mambo yanatuumiza, turudishe heshima ya Dayosisi
yetu.
C. We kama mwanadayosisi
unashauri nini?
-Tufikie
mwisho, tupatane, tuyamalize, tupatane
-Kukuwakutanisha
wote wenye neno dhidi ya mwingine tana
ana kwa ana tumefanya hivyo.
PATANO
1. Tumesameheana na yamekwisha
2. Hatuta chafuana tena ,hatuta
lipizana visasi tena
3. Hatuta oneana tena ,tunataka
amani irejee kama awali
4. Tunataka maombi kama
shukrani kwa Mungu kwa tulipofikia,
tuombe toba Mungu kwani kila mmoja wetu amehusika kwa namana moja au nyingine.
5. Tuendelee kuishi kwa amani
katika Dayosisi yetu.
KUNA
MAMBO AMBAYO TUMEKUBALIANA YATEKELEZWE NA YATAENDELEA KUFANYWA NA DAYOSISI
(UONGOZI WA DAYOSISI).
o Tunaitangazia Dayosisi nzima
kuwa haya mambo yameisha; ahsante Mungu umetufikisha hapa. Tuombe toba na
kukiri
o Naomba nitangaze kwa ujasiri
kabisa kuwa mambo yameisha
o Tusikumbushane vidonda vilivyo
pita, tupo mwaka mpya tuanze upya.
o Kumbukumbu zipo, tusifufue
vidonda tena
o Tuwaambieni wengine pia kuwa
haya yameisha .Tuwaambie ndugu zetu na popote tutakapo kwenda na kazi iliyobaki
ni kuombeana tu
Tumetoa
nafasi ya kutosha kwani tumekuwepo kwa muda wa wiki moja sasa, tumetoa nafasi
kwa kwa wote wenye neno na
tumewakutanisha na wamepatana. Hivyo
hatutegemei mtu mwingine kujitokeza
kuamsha na kuanza kusema vinginevyo
tutajua huyo mtu ana nia yake nyingine na haitakii mema Dayosisi na
Kanisa letu kwa ujumla.
Tunawaomba
ninyi muwe wainjilisti kwa wengine ili warudi nyumbani kwani sasa nyumbani ni
salama na shwari hakuna tatizo lingine.Ndugu zangu ya kale yamepita tyugange yajayo.
Tuwe
waangalifu kuto hukumiana kati ya sisi na sisi kwani huwezi juwa mtu mwingine
anaweza akawa siyo wa Dayosisi ya Iringa na pengine si Mkristo wa Kanisa la
Kiinjili la Tanzania. Tunaamini yameisha kwani kila mmoja amepewa nafasi ya
kueleza na kujieleza katika kamati yetu. Tunashukuru kwa ushirikiano na umoja
wenu.
Ndimi
Mtumishi wenu,
ASKOFU DKT.HANCE MWAKABANA
MWENYEKITI WA KAMATI YA
KICHUNGAJI YA MAASKOFU
15/01/2012
15/01/2012
ASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA DAYOSISI YA IRINGA
DKT.O.M MDEGELLA
AZINDUZI WA USHARIKA WA NYAMHANGA
JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI(IHEMI)
1. HISTORIA YA USHARIKA WA NYAMHANGA.
Bwana Yesu Asifiwe.
Tunawasalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Nyamhanga ilikuwa moja kati ya Mitaa kumi na mbili (12) ya Usharika wa Ipogolo.
Msukumo wa kuanzishwa mtaa wa Nyamhanga ulitokana na mara kwa mara Washarika kukosa huduma za kiroho hasa nyakati za mvua nyingi ilikuwa vigumu kwa wazee, wagonjwa na watoto kuvuka korongo lililopo kati ya Usharika wa Ipogolo na eneo la Nyamhanga.
Mwanga ulianza kujitokeza pale mzee wa kanisa Dauson Mbembe alipombatiza ubatizo wa dharura mgonjwa mahututi ndugu Yohana Mnyihanga tarehe 12/10/1992.
Wakati huo Usharika ulikuwa unaongozwa na Mwinjilisti Yona Kinganga (Kaimu Mchungaji) baada ya Mchg Sawike kuhama.
Kutokana na tukio hilo kaimu Mchungaji alimwomba aliyebatizwa (ndg. Yohana Myihana) nyumba yake itumike kwa sala za asubuhi, alikubali na huduma hiyo ilikaanza tarehe 15/10/1992.
Huduma zingine ziliendelea kutolewa Usharikani Ipogolo.
Kaimu Mchungaji alipoona maendeleo ya sala za asubuhi zinaendelea vizuri, aliwaruhusu Washarika waliokuwa wakiishi eneo la Nyamhanga kuanza maandalizi ya kuanzisha mtaa ili huduma za kiroho ziweze kufanyika katika eneo hilo.
Mnamo mwaka 1993 sala za asubuhi zilihamia nyumbani kwa mzee Mbwilo (Baba Tula ) kukiwa na washarika wanane (08) chini ya uongozi wa mzee wa kanisa Ndugu Dauson Mbembe.
Uongozi wa maandalizi ya Mtaa huo ulibuni mbinu mbalimbali za kuanzisha Mtaa ikiwa ni pamoja na:-
- Kuanzishwa kwaya ya Upendo ambayo inaendelea na uimbaji hadi sasa.
- Kuwa na minada ya aina mbalimbali.
- Kuanzisha Uinjilisti wa nyumba kwa nyumba siku za Jumanne na Mikesha ya mara kwa mara.
- Kuundwa kwa kamati ya majengo.
Kwa kutumia mbinu tajwa hapo juu tarehe 13/8/1993 tulifanikiwa kununua kiwanja chenye ukubwa wa robo tatu eka (3/4) toka kwa mzee Pauli Kanuru kwa Tsh elfu tatu (3,000).Hatua hii ya kupata kiwanja iliwasukuma washarika kuanza kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.
Kiwanja hicho kipo mwambao wa daraja la Cagrielo, hakijapimwa na kinatumika kama shamba la viongozi wa kanisa.
Mnamo mwaka 1994 chini ya Mwenyekiti wa majengo Ndugu Awarywa Nnko tulipata kiwanja kilichopimwa.
Kutokana na kupatikana kwa kiwanja hicho uongozi uliamua kanisa lijengwe katika kiwanja hicho, ndipo washarika walipoanza shughuli za ufyatuaji wa matofali. Tunamshukuru Mungu kwa kuwatumia watumishi wake Ndugu Awarywa Nnko na Ndugu Chua kusimamia usombaji wa kuni za kuchomea matofali kwa trekta lililotolewa na Shirika la kilimo (EEC).
Trekta hili lilitumiwa pia kipindi hicho kusomba matofali ya awamu ya kwanza. Kazi ya ufyatuaji na uchomaji wa matofali ya awamu ya pili zilifanyika mnamo mwaka 1995. Kutokana na mzee Mbwilo kuhamia Makete sala za asubuhi zilihamishiwa nyumbani kwa mzee Dauson Mbembe kuanzia tarehe 14/7/1995.
Katika kipindi hiki Uongozi uliomba huduma ya shule ya Jumapili (Sunday School) ianze, uongozi wa Usharika ulikubali na watoto walianza ibada za Shule ya Jumapili tarehe 19/10/1996.
Kazi ya ujenzi wa kanisa ilianza rasmi tarehe 26/9/1996.
Ili kufanikisha ujenzi wa kanisa zilibuniwa mbinu au njia mbalimbali zikiwemo:-
- Kuanzisha mgahawa.
- Bahati na sibu iliyotupatia Tsh laki mbili na elfu hamsini (250,000)
- Wahisani R.C Ipogolo walitupatia Tsh elfu ishirini (20,000).
- Harambee iliyoongozwa na Mchg Agness Kulanga ilitupatia Tsh laki moja elfu thelathini (130,000).
- Makanisa rafiki wa Usharika wa Ipogolo toka Augustana Marekani walitupatia bati sitini (60) gage 28.
Kutokana na Ndugu Awarywa Nnko kupata uhamisho wa kikazi mwaka 1997, Ndugu Mathew Mlangi alichaguliwa kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Majengo.
Ndugu Mathew Mlangi alisimamia kamati hiyo ya Majengo, awamu ya pili ya usombaji wa tofali kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.
Ndugu Mathew Mlangi alienda masomoni nje ya nchi, na ndg Henry Mwaipopo alichaguliwa kuchukua nafasi ya uwenyekiti wa majengo, Ili kuharakisha ujenzi wa kanisa unaendelea bila kukwama.
Wakati ujenzi wa Kanisa unaendelea, Uongozi uliamua, ibada za shule ya Jumapili pamoja na mazoezi ya uimbaji yafanyike kwenye jengo la kanisa lililokuwa linaendelea kujengwa (pagale).
Uongozi wa Mtaa wakati huo ulipata changa moto nyingi kutoka kwa wamiliki wa kiwanja cha kanisa. Kanisa lililazimika kulipa fidia ya Tsh elfu ishirini na tano (25,000) kwa wamiliki wa eneo hilo kwa ajili ya vitindi na mlimao kama ilivyoamuliwa na ofisi ya Kata ya Kitwiru.
Tunamshukuru sana Mungu kupitia kwa msaidizi wa Askofu wakati huo Mchg Dr Richard Lubava na aliyekuwa Mchg wa Usharika wa Ipogolo Mchg Lusungu Msigwa waliweza kuishawishi ofisi ya bega kwa bega ambayo ilitupatia Tsh Milioni tatu laki nne elfu kumi tatu na mia nne (3,413,400), saruji mifuko mia moja (100), mbao mia moja (100), chokaa mifuko miwili (02) na waya za “Ringbeam”.
Mchango huu pamoja na michango ya washarika ilifanikisha kazi ya ujenzi wa kanisa kukamilika kuta, kupaua na kuchonga milango.
Shughuli hizi zilifanyika chini ya usimamizi wa mwenyekiti wa majengo Ndugu Henry Mwaipopo na mzee wa kanisa ndugu Dauson Mbembe.
Kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa kanisa tarehe 11/8/2002 ibada zote zilianza kufanyika yamhanga na ukawa mtaa unaojitegemea chini ya uongozi wa mzee wa kanisa Ndugu Dauson Mbembe, kukiwa na waumini sabini na mbili (72).
Huduma ziliendelea chini ya mzee wa kanisa Ndugu Dauson Mbembe hadi tarehe 30/11/2002 Mtaa ulipopata mwinjilisti, Regina Kibasa. Mtaa ulipopata mwinjilisti, washarika walipata hamasa, na mikakati ya maandalizi ya kuchonga mabenchi, kutengeneza samani za ofisi, kuingiza umeme na maji zilianza.
Michango ya washarika wa Mtaa huu, pamoja na minada ya ndani kazi zote hizo zilikamilika.
Baada ya Mtaa kukamilisha kazi zilizotajwa hapo juu, lilijitokeza wazo la kujenga nyumba ya mtumishi.
Washarika wa Mtaa huu, kwa michango yao na nguvu kazi wakishirikiana na vijana ishirini na moja (21) toka Usharika wa Augustana Marekani walifanikiwa kukamilisha kazi ya kujenga Msingi wa nyumba ya mtumishi.
Mnamo mwaka 2004, uongozi wa Mtaa uliandaa harambee, na Baba Askofu DKT Owdenburg Moses Mdegella ukiwa mgeni rasmi katika harambee hiyo kwa lengo la kuhamasisha.
Waalikwa wengine walikuwa, Kwaya kuu toka Usharika wa Kanisa Kuu, viongozi wa kanisa pamoja na viongozi wa Serikali, ndugu na marafiki.
Harambee hii ilichangisha kiasi cha Tsh laki nane themanini na mbili elfu na mia tatu (882,300/=). Kiasi kilichopatikana katika harambee hiyo kiliwezesha kukamilisha kazi ya ujenzi wa kuta, kupaua, Milango, kupiga plasta ndani.
Kazi hii ya ujenzi ilifanyika chini ya uongozi wa Mwilisti wa mtaa Regina Kibasa, wachungaji wa Usharika wa Ipogolo, Mchg Abass Tagamtwa na Mchg Nixon Mwitula.
Jengo la kanisa pamoja na nyumba ya mtumishi zilizinduliwa rasmi na Baba Askofu DKT Owdenburg Moses Mdegella tarehe 21/06/2009.
Mtaa wa Nyamhanga hadi kupata hadhi ya kuwa Usharika umeongozwa na watumishi hawa wafuatao:-
1. Mzee wa kanisa Dauson Mbembe 11/08/2012 – 30/11/2011
2. Mwinjilisti Regina Kibasa 30/12/2002 – 30/11/2009
3. Shemasi Regina Kibasa 01/11/2009 – 14/12/2009
4. Shemasi Gaitan Mkemwa 15/12/2009 – 20/09/2011
5. Mwinjilisti Aneth Mkongwa 2009 – Hadi sasa ni Mwinjilisti wa
Mtaa wa Stesheni
6. Mchg Nuru Makweta -20/9/2011 hadi sasa ni Mchg kiongozi wa Usharika huu mpya.
Makatibu waliotumika hadi kupata Usharika ni hawa wafuatao:-
1. Vicky Motto - 2002
2. Mathias .B. Masele – 2002 - 2006
3. Noel Chengula - 2006-Hadi sasa ni Katibu/Mtunza Hazina wa Usharika.
Tunamshukuru Mungu kwa kufanikisha upatikanaji wa viwanja vinavyoungana na eneo la kanisa. Viwanja hivi vilipatikana baada ya kanisa kulipa fidia ya Tsh Milioni saba laki moja na nne elfu mia tisa hamsini (7,104,950/=) kwa waliokuwa wamiliki wa viwanja hivyo tarehe 04/02/2012.
Tunawapongeza Wazee wa kanisa, Kamati ya majengo,Kamati ya ununuzi wa viwanja pamoja na wote walioshiriki katika kufanikisha upatikanaji wa viwanja hivyo.
Imeandaliwa na: KAMATI YA MAANDALIZI YA UFUNGUZI WA USHARIKA WA
NYAMHANGA:
Tarehe: 12/05/2013
2. RISALA
Baba Askofu wa Dayosisi ya Iringa. Msaidizi wa Askofu. Katibu Mkuu, Wakuu wa Majimbo, Wachungaji Wote, Viongozi wa Serikari na Waumini wote mliohudhuria katika ibada hii,
“ BWANA YESU ASIFIWE”
Baba Askofu.
Kwa niaba ya Washarika wa Usharika Mpya wa Nyamhanga, ambao baada ya muda mfupi ujao utaufungua, awali ya yote napenda kutoa shukurani zangu za dhati, kwanza kwako wewe Baba Askofu, Msaidizi wa Askofu, Katibu Mkuu, Wakuu wa majimbo, Viongozi wa Serikali na wote mliohudhuria katika ibada hii, kwa kumshukuru Mungu kutufikisha siku ya leo.
Pia napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Washarika wote wa Usharika wa Ipogolo na Wachungaji wote waliohudumu katika Usharika huo kwa kuuongoza Mtaa wa Nyamhanga hadi kufikia kuwa Usharika, na leo Baba Askofu utaufungua rasmi.
Ningependa Kuwataja Wachungaji waliohudumu katika Usharika wa Ipogolo, Nyamhanga ukiwa moja wa Mitaa ya Usharika huo. Wachungaji hao ni hawa wafuatao:-
(1) Mchungaji Agness Kulanga na msaidizi wake Mchg. Aleki Mhanga
(2) Mchungaji Damian Ngandango
(3) Mchungaji Lusungu Msigwa
(4) Mchungaji Abbas Tagamtwa
(5) Mchungaji Nixon Mwitula (Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Ipogolo hadi sasa) na wasaidizi wake wafuatao;- Mchg. Lunyiliko Muhile, Shemasi Gaitan Mkemwa, Mchg. Lucrecia Mbwilo, na Mchg. Nuru Makweta.
Wote hawa wamefanya kazi kubwa katika kuufikisha Mtaa wa Nyamhanga kuwa Usharika.
Baba Askofu, Mtaa wa Nyamhanga ulianza tarehe 11/08/2002 kwa juhudi za Waumini wa Mtaa huo kwa kushirikiana na Usharika wa Ipogolo.
Wakati Mtaa ulipoanza ulikuwa na Washarika 72, Washarika wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku na kufikiaWasharika 1,180 hadi Mtaa ulipofikia kupewa hadhi ya Usharika Mwezi Januari, 2013.
Baba Askofu, kuanzishwa kwa Mtaa wa Nyamhanga ilitokana na Waumini wa Mtaa wa huo na wakazi wa eneo hili kutaka kusogezewa huduma ya Kiroho katika eneo lao, kutokana na kikwazo cha Korongo lililoko kati ya eneo la Nyamhanga na Usharika wa Ipogolo kujaa maji wakati wa masika, Waumini wa eneo la Nyamhanga ilikuwa tatizo kwao kuvuka Korongo hilo na kwenda Ipogolo kuhudhuria Ibada,
Baba Askofu, Usharika huu wa Nyamhanga utakaoufungua leo, umetokana na Usharika wa Ipogolo, Nyamhanga ukiwa Mtaa moja wapo wa Mitaa kumi na mbili (12) ya Usharika huo wa Ipogolo.
Usharika wa Nyamhanga una Mitaa saba (7), Waumini 1,180, watu wazima ni Waumini 703, kati ya hao, Wanaume ni 266 , na Wanawake ni 439.
Watoto jumla yao ni 485, Wanaume ni 210, na Wanawake ni 275,
Baba Askofu, Usharika wa Nyamhanga una Mitaa Saba (7) kama nilivyokwisha eleza hapo awali, Mitaa hiyo ni:-
(1) Mtaa wa Stesheni – Nyamhanga una waumini 528
(2) Mtaa wa Kitwiru - 174
(3) Mtaa wa Kibwabwa - 125
(4) Mtaa wa Lugala - 221
(5) Mtaa wa Mseke - 65
(6) Mtaa wa Mosi - 11
(7) Mtaa wa Isimila – 56
Katika Mitaa hiyo Saba (7), Mitaa Mitatu (3) ni Mitaa ya Mission, Mitaa hiyo ni ifutatayo:-
(1) Mtaa wa Mseke
(2) Mtaa wa Mosi
(3) Mtaa wa Isimila
Baba Askofu, Usharika huu Mpya wa Nyamhanga una Wachungaji Wawili:
(1) Mchungaji Nuru Makweta – Ambae ni Mchungaji Kiongozi
(2) Mchungaji Lunyiliko Muhile
Baba Askofu, ninakuahidi kuwa mimi na Mchungaji mwenzangu, tutashirikiana na Waumini wote katika kuifanya kazi yaBWANA katika eneo hili la Usharika huu.
Kufunguliwa kwa Usharika huu wa Nyamhanga, kutaimarisha kueneza neno la Mungu na huduma yake katika eneo hili.
Pili, ni wajibu wa Usharika huu, nikiwa na maana ya Viongozi, Wahudumu na Watenda kazi wote wa Usarika huu wa Nyamhanga kuitangaza Injili kwa watu wote.
Baba Askofu, Usharika wa Nyamhanga pia una Mipango Kazi Kama ifuatavyo:-
(1) Kazi ya Kiroho:
Kazi kubwa iliyooko mbele yetu ni pamoja na;-
(a) Kueneza neno la Mungu katika eneo la usharika wa Nyamhanga
(b) Kushirikiana na Viongozi, Wahudumu na Watenda kazi wote wa Usharika katika kuitangaza Injili kwa watu wote, ili waweze kuokolewa kwalo na kumtumikia Mungu.
(c) Kufanya Uinjilisti wa nyumba kwa nyumba katika eneo hili la Usharika’
(d) Kuimasha na kuendeleza Sel – groups
(e) Kuandaa semina za neno la Mungu
(f) Kuandaa Mikutano ya Injili
(g) Kusomesha Wachungaji na Wainjilisti
(h) Tuna Mipango ya Kutembelea Sharika mbalimbali katika Dayosisi ya Iringa na nje ya Dayosisi kwa kutumia kwaya za Usharika wetu, katika kueneza Injili na pia kujifunza kutoka kwao.
(i) Kuimarisha huduma za Maombi.
Neno linasema,
“BWANA ASIPOIJENGA NYUMBA, WAIJENGAO WAFANYA
KAZI BURE,
BWANA ASIPOULINDA MJI YEYE AULINDAYE AKESHA
BURE”
(Zaburi 127: 1)
(2) Kazi za Kiuchumi:
Ili kazi ya Kiroho iweze kupata msukumo wa kwenda mbele, tuna Mipango Mkakati ya kazi za Kiuchumi kama ifuatavyo:-
(a) Kujenga ukumbi
(b) Kujenga Shule ya watoto wadogo (Kindergarten)
(c) Kujenga Hostel
(d) Kuendeleza Mradi wa upandaji Miti katika shamba lililopo Lugala
(e) Tuna mpango wa kujenga Maduka ya Biashara kuzunguka eneo la Kanisa
(f) Pia tuna Mpango wa ujenzi wa shule ya Ufundi
Mipango hii yote ni endelevu ( Mipango ya muda mrefu).
Baba Askofu,
Mahali popote pale hapakosi changamoto:
Usharika wetu kwa kuwa ndiyo unaanza, tuna changamoto zifuatazo:-
(1) Usharika una changamoto kubwa ya usafiri, hatuna chombo cha usafiri kwa
ajili ya kuifikia Mitaa yetu ambayo ipo mbali kutoka Makao makuu ya usharika, pamoja na kufanya shughuli zingine za kila siku.
(2) Tuna upungufu wa Majengo kwa ajili ya ofisi za idara mbali mbali katika
Usharika wetu.
Baba Askofu,
Kwa heshima nakuomba, karibu ufungue rasmi usharika wa Nyamhanga leo tarehe 12/05/2013.
“BWANA YESU ASIFIWE”
AMEN
NURU MAKWETA
MCHUNGAJI KIONGOZI – USHARIKA WA NYAMHANGA,
ASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI T ANZANIA
DAYOSISI YA IRINGA
DKT.O.M MDEGELLA
AZINDUZI WA USHARIKA WA NYAMHANGA
MATUKIO KATIKA PICHA
Radio Furaha 96.7 Fm wakifuatilia matukio tayari kurusha moja kwa moja (Live)
Bendi ikitumbuiza tayari kupokea maanadamano
MCHUNGAJI NURU AKISOMA RISALA KABLA YA UZINDUZI WA USHARIKA
KATIBU MKUU BW. NAYMAN CHAVALLA AKISOMA WAJIBU WA USHARIKA KATIKA UFUNGUZI HUO
BAADHI YA WACHUNGAJI WALIOSHIRIKI KATIKA UZINDUZI HUO
BABA ASKOFU AKIKAZIA JAMBO KABLA YA KUFUNGUA MLANGO WA KANISA HILO
MZEE WA KANISA BI OTTAVINA MYENZI AKISOMA MATANGAZO
WAKRISTO WAKIFUATILIA IBADA HIYO
WAZEE WAANDAMIZI WA USHARIKA HUO
MCHUNGAJI KIONGOZI WA USHARIKA HUO MCHG. NURU MAKWETA AKIWA TAYARI KWA KAZI
KWAYA KUU IKITUMBUIZA
WAZEE WA KANISA NA WENYEVITI WA KAMATI MBALIMBALI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
Monday, May 20, 2013
KWAHERI MAMA MCHUNGAJI ANN KATRIN PERSSON
Mama tunakushukuru sana kwa mapenzi mema ni maneo ya Baba askofu Dkt. O.M Mdegella wa K.K.K.T-Dayosisi ya Iringa
"Hongeara mama" ni maneno ya Mchungaji Sara Mdegella kwa mama Ann Katrinn Person
Hii ni zawadi yako Mungu akubariki sana
Ubarikiwe sana
Nashukuru sana ni maneo ya mama Mchungaji Runne Persson
Tunakutakia maisha mema na Mungu akipenda tutaonana
IFUATAYO NI SEHEMU YA HOTUBA YAKE
Ninawashukuruni sana! Kwanza ninashukuru kwa jioni hii njema kwa ninyi nyote mliofika kwa kuniaga taja…, ni neema ya pekee. Ninashukuru mno! Halafu ninataka kusema asante kwa moyo na upendo mmenionyesha wakati nimekuwepo hapa Iringa, DIRA. Wengine nimekaa nao sana, na wengine tumeonana kwa kifupi tu. Lakini ninataka kusema kwamba ukaribu wenu pamoja na ukarimu umenitia moyo sana na imenisaidia kujisikia kama nipo nyumbani hapa, asanteni sana.
Wenzangu wa ETE, Mchg. Vallence, Mchg. Sarah, Mchg. Ulime na Mary, kama mimi ninavyoona tumefanya kazi vizuri pamoja. Tumepanga kazi, tumezungumza, tumecheka na tumeomba pamoja ili kazi ya ETE isonge mbele na watu wapate nafasi kumfahamu Mungu wetu anayetaka watu wote wamfahamu Yesu Kristo katika maisha yake.
Pia ninasema asante Sarah, kwa muda huu tuliokuwa pamoja ofisini na kwenye safari zetu za kuzunguka majimboni kuwaona wenzi wa wachg. na wainj. Umekuwa tayari kunieleza mambo yote ambayo sikuelewa na sikufahamu, na umekuwa tayari kunijibu kila swali. Hii imekuwa msaada mkubwa kwangu na imenisaidia sana katika kazi yangu. Sasa naomba Mungu akubariki katika kazi ya kuchunga Usharika wako, wenzi wa wachungaji na wainjilisti.
Miaka hii michache nimejifunza mengi kutoka kwenu. Na kitu kikubwa hasa nimaana ya maisha ya maombi.
Ninaporudi nyumbani nitaendelea kutoa habari za kazi ya wenzi katika usharika wetu ili wafadhili wenu wapate changamoto kuendelea kujitolea kwa kupitia SEM.
Muda umeenda haraka, miaka 2 ½ imeshapita, na sasa livu yangu imekwisha na nimeitwa kazini nyumbani tena. Mwakani Mungu akipenda, ninataka kufika hapa tena kumtembelea Rune na ninyi nyote, nafikiri Mungu anapenda.
Mungu awabariki ninyi nyote na tutaendelea kuwa pamoja katika maombi, asanteni sana!
KATIBU MKUU AKIFURAHIA JAMBO KULIA KWAKE NI BABA ASKOFU DKT. O.M. MDEGELLA
KWAYA NA BENDI ZIKITUMBUIZA KUONGOZA MSAFARA KUELEKEA KANISANI
UBARIKIO WA MKUU WA JIMBO ULIOFANYIKA HUKO IHEMI KATIKA PICHA
BABA ASKOFU DKT. O.M MDEGELLA AKIWA NA MSAIDIZI WAKE TAYARI KUELEKEA KATIKA IBADA
MKUU WA JIMBO MTEULE AKIWA TAYARI KATIKA MSTARI TAYARI KUELEKEA KATIKA UBARIKIO WAKE
KATIBU MKUU BW. NAYMAN CHAVALLA AKIWA NA MKUU WA JIMBO MCHG. AGNES KULANGA
KATIBU MKUU AKIFURAHIA JAMBO KULIA KWAKE NI BABA ASKOFU DKT. O.M. MDEGELLA
KWAYA NA BENDI ZIKITUMBUIZA KUONGOZA MSAFARA KUELEKEA KANISANI
WAKUU WA MAJIMBO WAKIFUATILIA MATUKIO KATIKA IBADA HIYO
KATIBU MKUU BW. NAYMAN CHAVALLA NA MTUNZA HAZINA WA DAYOSISI BW. NOEL ILOMO KATIKATI WAKIFUATILIA JAMBO
"PONGEZI KWAKO BABA" NI MANENO YA MAMA MCHG. AIKAM CHAVALLA
HAPA MCHG. AIKAM CHAVALLA AKIWA TAYARI NA VAZI LAKE RASMI
Tuesday, May 21, 2013
TULIKOTOKA NI MBALI TUMSHUKURU MUNGU
Pichani Baba Askofu Dkt.O.M Mdegella akiwa na Msaidizi wake marehemu mchungaji Nicholaus Chusi mara baada ya kumtambulisha kama Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya iringa wanao onekana ni wake zao Mama Askofu ambaye kwa sasa ni Mchungaji Sara Mdegella na Mama Msaidizi wa Askofu Mwalimu Elitha Mkinywa
UBARIKIO WA WACHUNGAJI KUMI NA MASHEMASI
WATATU KATIKA USHARIKA WA MKWAWA 12.01.2014
No comments
Post a Comment