Wakati zoezi la kusikiliza Malalamiko yanayotolewa na Kinamama dhidi ya kinababa wanaodaiwa kutelekeza watoto bila huduma likifikia tamati leo ,Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda amekiri zoezi hilo kuwa gumu huku idadi ya watu ikiongezeka kila kukicha.
Akizungumza na akina mama na akina baba walioitikia wito wa kusikiliza malalamiko dhidi yao,Makonda amesema akina mama elfu 17 wamejitokeza katika zoezi hilo lililoanza april 9,tayari akina mama elfu saba mia mbili wamesikilizwa huku zaidi ya elfu 10 bado hawajasikilizwa.
Aidha Makonda amesema akina baba wote waliokaidi wito wa kupatanishwa ili watunze watoto wao majina yao yatakabidhiwa kwa Kamanda mambo sasa ili washughulikiwe kuanzia jumatatu ijayo.
Aidha Makonda amesema kutokana na changamoto zilizojitokeza ataunda kamati itakayojumuisha wanasheria,maafisa Ustawi wa jamii,na polisi ili kuaandaa mapendekezo yatakayowasilishwa bungeni kwa ajili ya marekebisho ya sheria.
No comments
Post a Comment