Makamu wa rais nchini Cuba, Miguel DÌaz-Canel, ametajwa na viongozi wa ngazi za juu nchini humo kuwa ndiye kiongozi mtarajiwa ajaye anayekuja kumrithi ama kuchukua nafasi ya Raul Castro.
Miguel mwenye umri wa miaka 55 na ambaye kwa taaluma ni mhandisi wa zamani anatarajiwa kuchukua hatamu ya uongozi leo, baada ya zoezi la upigaji kura rasmi na mkutano wa kitaifa kuidhinisha uteuzi wake.
Makabidhiano ya madaraka utahitimisha miongo sita ya utawala wa Castro na ndugu yake marehemu Fidel, ambaye aliongoza mapinduzi ya mwaka 1959.
Raul Castro atasalia kuwa kiongozi mkuu wa Chama cha Kikomunisti mpaka hadi mwaka 2021 mpaka mkutano mkuu ujao na anatarajiwa kuendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika jamii yake.
Kwa tabia Miguel ni kiongozi mnyofu na tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa kuwa makamu wa raisi wa baraza la Congress la Cuba mnamo mwaka 2013 ingawa tangu wakati huo amekuwa ni mtu wa karibu wa Bw. Castro
No comments
Post a Comment