Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, January 31, 2017

KAMPENI YA KUCHEZA OLIMPIKI 2020 KUZINDULIWA LEO UWANJA WA KARUME

UIKO
Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kushirikiana na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau leo Jumatatu Januari 30, kwa pamoja watazindua kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan.
Uzinduzi wa kampeni hizo unaopewa jina la ‘The Road to Tokyo 2020’ utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam saa 5.00 asubuhi ambako wadau na wafamilia wa mpira wa miguu wanakaribishwa.
Tayari timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali hizo za za Olimipiki.
Kambi hiyo imepigwa kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.
Tanzania haijapata kushiriki Michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu jambo ambalo limeisukuma TFF kuona kuwa ni fursa ya mpira wa miguu kuchezwa hivyo inashirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kufanikisha mipango na taratibu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA NNE 2016

 matokeo ya mtihani kidato cha nneBaraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.


Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

Mahamat rais mpya wa halmashauri kuu ya AU

Umoja wa Afrika umepata rais mpya wa halmashauri kuu ya Umoja huo. Naye ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat, aliyechaguliwa kwa  kura 39 kati ya 54 za nchi wanachama. 

Äthiopien Debatte der Präsidentschaftskandidaten der Kommission der Afrikanischen Union
(DW/C. Wanjohi)
Moussa Faki Mahamat, alizaliwa Juni 21 mwaka 1960 katika mji wa Biltime mashariki mwa Chad. Aliteuliwa kuwa Waziri mkuu Juni 2003 hadi Februari 2005, na ni mwanachama wa Chama cha Uokozi cha Kizalendo - Patriotic Salvation Movement. Kuazia 2007 hadi 2008 alikuwa rais wa Baraza la  Kiuchumi, Kijamii na  Kitamaduni, kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mwezi Aprili 2008.
Bw Mahamat, alisoma sheria katika chuo kikuu cha Brazzaville katika Jamhuri ya Congo. Wakati Hissene Habre alipochukua madaraka Juni 1982, Mahamat alikimbilia uhamishoni na akajiunga na Baraza la Mapinduzi la Kidemokrasi lililoongozwa na Acheikh Ibn Oumar. Lakini hakurudi Chad wakati Acheikh alipojiunga na serikali ya Habre 1988. Ilikuwa ni baada ya Habre kupinduliwa na  Idriss Deby ndipo Mahamat aliporudi nyumbani Juni 1999.
Äthiopien Debatte der Präsidentschaftskandidaten der Kommission der Afrikanischen Union
(DW/C. Wanjohi)
Mkutano wa kilele wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Ethiopia
Aliteuliwa Mkurugenzi mkuu wa  wizara mbili kabla ya  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Sukari la Taifa kati ya 1996 na 1999. Machi 1999 hadi Julai 2002 akateuliwa  kuwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Rais Deby, na alikuwa mkurugenzi wa kampeni ya Deby wakati wa uchaguzi wa Rais Mei 2001
Mpinzani mkuu wa  Mahamat katika duru ya mwisho ya upigaji kura alikuwa  Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Kenya Bibi Amina Mohammed. Senegal pia ilikuwa na mgombea  mwana diplomasia wa siku nyingi, Abdoulaye Bathily, aliyetolewa katika duru ya awali. Wengine katika orodha ya wagombea watano walikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Botswana Pelonomi-Venson Moitoi na Agapito Mba Mokuy kutoka Guinea ya Ikweta.
Nkosazana Dlamini-Zuma Amtseinführung Vorsitz Afrikanische Union (picture-alliance/dpa/J. Prinsloo)
Aliyekuwa rais wa zamani wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma

Wote wawili walikataliwa na Viongozi Wakuu  wa Umoja wa Afrika, wakati wa mkutano wao wa kilele mjini Kigali – Rwanda Julai 2016, baada ya kushindwa kupata uungaji mkono wa theluthi mbili kura ya siri.
Rais mpya wa Halamshauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, anachukua nafasi ilioachwa na Bibi Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika Kusini  aliyeshika wadhifa huo Julai 2012 akimpokea Jean Ping wa Gabon. Bibi Dhlamini-Zuma hakugombea tena .
Chanzo: Dw Swahili

MAGAZETINI LEO JUMANNE JAN 31,2017































RAIS MAGUFULI ALIVYOKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Malawi Peter Mutharika kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Rais wa Malawi Peter Mutharika pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kidemokrasia ya Sahrawi(SADR) Brahim Ghali katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. 

PICHA NA IKULU

Mualiko wa Trump wamueka malkia katika hali ngumu

Trump na Malkia

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrump na Malkia
Uamuzi wa waziri mkuu wa Uingereza Bi Theressa May wa kumualika rais Donald Trump wa Marekani umemuweka malkia katika hali ngumu, kulingana kiongozi wa zamani wa afisi ya maswala ya kigeni nchini humo.
Katika barua alioandika kwa gazeti la The Times, Lord Rickets amesema kuwa ombi hilo lilifanywa mapema mno.
Ombi la kutaka ziara hiyo ya Donald Trump nchini Uingereza kufutiliwa mbali limefaulu kupata zaidi ya saini milini 1.5.
Siku ya Jumatatu, maelefu ya watu nchini Uingereza waliunga maandamano dhidi ya agizo la usafiri la Donald Trump kuhusu mataifa saba ya kiislamu.
Mkakati huo wa uhamiaji wenye utata ulizua mjadala bungeni.
Lord Rickets ambaye alikuwa katibu wa maswala ya kigeni kutoka mwaka 2006-10 alisema kuwa sio jambo la kawaida kwa rais wa Marekani kualikwa kwa ziara ya kitaifa katika mwaka wa kwanza wa utawala wake.
Alihoji iwapo bw Trump alistahili heshima hiyo .
''Ingekuwa vyema kusubiri na kuona ni kiongozi wa aina gani kabla ya kumshauri Malkia kumualika.Sasa Malkia amewekwa katika hali ngumu sana'',aliongezea kiongozi huyo.

Barack Obama avunja ukimya

Marekani

Image captionRaisi mstaafu wa Marekani, Barack Obama
Ofisi ya rais wa zamani wa Marekani Barack Obama imetoa tamko na kusema kwamba raisi huyo wa zamani anakerwa na maandamano yanayoendelea nchini humo kupinga tamko la raisi Donald Trump kutaka kuweka vizuizi vya uhamiaji juu ya wasafiri kutoka kwa baadhi ya nchi za Kiislamu.
Msemaji wa rais Barack Obama, Kevin Lewis, amesema kwamba raisi mstaafu kimsingi hakukubaliana na wazo la ubaguzi dhidi ya watu kwa sababu ya dini yao.
Na kuongeza kusema kwamba wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kusikilizwa na viongozi waliochaguliwa na ndiyo matarajio yao pindi Marekani inaingia hatarini .

DC KILOLO ATAKA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI IPALAMWA ASILIPWE PESA ,MADIWANI WAMPA WIKI MBILI KUKAMILISHA MRADI

DC  Kilolo  Asaia Abdalaha  akifafanua  jambo
Mwenyekiti  wa Halmashauari ya  Kilolo  akifugua  kikao  kushoto  ni mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo.
Baraza la madiwani  Kilolo
Na MatukiodaimaBlog
BAADA ya  mradi  wa maji Ipalamwa  kujengwa chini ya  kiwango kwa bomba kupasuka ovyo kabla ya mradi  kukabidhiwa ,baraza   la madiwani  la Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  limempa muda  wa  wiki  mbili mkandarasi  wa kampuni ya Norcom Ltd kukamilisha mradi  wa maji wa Ipalamwa  kwa  ubora unaotakiwa zinginevyo mkataba  wake  utavunjwa.
Huku  mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  Asia  Abdalaha akiagiza Halmashauri hiyo  kutomlipa fedha  yeyote  mkandarasi   huyo hadi  hapo atakapokamilisha mradi  kwa  kiwango  kinachotakiwa  vinginevyo kama  kuna pesa  alilipwa awali basi  pindi  mkataba  wake utakapovunjwa atapaswa  kuzirudisha  fedha  hizo.
Wakitoa  maadhimio  hayo katika  kikao  cha  baraza  la  madiwani   kilichofanyika  juzi  katika  ukumbi  wa Halmashauri  ya  Kilolo  na  kuhudhuriwa na mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo ,madiwani  hao  walisema  kuwa wamechoshwa na mkandarasi  huyo  kuendelea kuchelewesha  mradi  huo  wa  maji na  kuwa sasa  wanaona  suala   hilo la kero ya  maji kijiji  cha Ipalamwa  lifike  mwisho  kwa  kumpa  muda  wa  mwisho  kwa ajili ya  kukamilisha mradi   huo .
Mhandisi   wa  maji  wa  wilaya ya  Kilolo Enock Basyagile   akijibu  hoja  za  baraza  la madiwani  juu ya  ucheleweshwaji  wa  mradi  huo   alisema  kuwa sababu ya  kuchelewa kwa  kazi hiyo ni  kutokana na  kukosekana  kwa   fedha kati ya Halmashauri na mkandarasi   ila  kwa   sasa  fedha  zimeingia na mchakato  wa  kufanya  kazi   hiyo  kwa  kununua  vifaa  vya mradi  huo  ikiwa ni  pamoja na mchakato  wa malipo kwa mkandarasi   huyo.
Mkuu wa  wilaya  ya  Kilolo Asia  Abdalah  alisema  hakubaliani  na  uamuzi  wa mhandisi    wa maji  wilaya  kutenga   fedha  ama  kufanya mchakato  wa malipo  ya Tsh  milioni 19 kwa  mkandarasi  huyo  aliyejenga  mradi  huo  chini ya  kiwango ila alitegemea  kuona mkandarasi  huyo anachukuliwa hatua kwa kufanya  kazi  chini ya  kiwango.
” Sikubaliani  hata  kidogo  na uamuzi  wa kumlipa fedha  mkandarasi  huyo ama  Halmashauri  kununua mabomba kwa ajili ya kukarabati  mradi ambao haujakabidhiwa  kwa  wananchi …..naagiza mkandarasi  huyo afanye  kazi hiyo  kwa gharama  zake na  asilipwe  pesa  yoyote  hadi mradi  utakapokabidhiwa “
 Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya  Kilolo Bw Vellance Kihwaga  alisema  sababu  kubwa ya  mradi   huo  kuendelea  kusumbua kwa mabomba  kupasuka  ni  baada ya  mkandarasi huyo  kwenda  kinyume na mkataba  wa kazi  hiyo kwa kuweza mabomba membamba  zaidi    kuliko  nguvu  ya maji   hivyo pindi  maji  yakifunguliwa mabomba  hayo   hupasuka .
Alisema  kutokana na ubovu   huo  wa mabomba  kamati ya  fedha  ilifanya  ziara ya  ukaguzi  wa  mradi  huo  toka  mwaka jana  na  kumwagiza mkandarasi  huyo kufanya marekebisho  kwa  kutoka mabomba   yote  yasiyo  na ubora na  kufunga mabomba  yenye ubora  na alikubali  kuifanya kazi   hiyo  ndani ya wiki mmoja na kamati  ilimpa  mwezi  mmoja  ila hadi  sasa ni  zaidi ya miezi 4 kazi   hiyo   haijafanyika .
 Mkurugenzi  mtendaji wa  Halmashauri ya  Kilolo Bw Aloyce Kwezi alisema  kuwa mkanadarasi  huyo bado  hajalipwa  fedha   yoyote  na  kuwa Halmashauri  haitamlipa fedha  hadi  hapo mradi  utakapokamilika na anapaswa  kufanya kazi  hiyo  kwa  gharama  zake na iwapo atashindwa  kwa muda  uliotolewa basi  halmashauri  itavunja mkataba  huo.
Wakati  huo  huo serikali  ya  wilaya ya  Kilolo imepiga  marufuku  wageni  kuingia katika  vijiji ama kata na  kuendesha  miradi  mbali mbali pasipo kushiriisha viongozi wa  ngazi  zote  za vijiji ama Halmashauri .
Chanzo: Mjengwa Blog