Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 12, 2017

RC Makonda Agoma Kuona Mwili wa Seth Katende.


Seth Katende
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amevuta hisia za waombolezaji katika tukio la kuuaga mwili wa mtangazaji wa EFM Radio ya jijini Dar es Salaam, Seth Katende pale aligoma kuangalia mwili wa marehemu kutokana na machungu aliyonayo kwa msiba huo. Mkuu wa mkoa alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kutoa salamu za rambirambi katika msiba huo.
Makonda alisema hataki kuondoka na picha ya kwamba marehemu, Seth amelala kwenye jeneza na hayupo tena, bali aondoke na picha ya kutoamini kifo chake na ya kwamba bado yupo na anaendelea kupambana kutimiza ndoto zake.
Alisema marehemu alikuwa mtu wa karibu kwake na mara zote walikuwa wakishirikishana masuala mbalimbali ya kimaisha na kimaendeleo na alipenda moyo wake wa kujituma na kujitoa ili kutimiza malengo yake. Mkuu wa mkoa alisema msiba huo umemgusa sana kwani yeye ni sehemu ya familia ya akina Seth hivyo ameguswa na msiba huo.
Marehe Seth (31) maarufu kwa jina la Bikira wa Kisukuma aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni cha EFM alifariki Julai 9, 2017 katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es Saam. Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Thehabari.com
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment