Writen by
sadataley
7:46 AM
-
0
Comments
Mtoto mmoja kati ya watano anaishi katika hali ya umaskini katika nchi tajiri duniani
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetangaza katika ripoti yake kwamba mtoto mmoja kati ya watano katika nchi tajiri au zilizostawi anaishi katika katika hali ya umaskini.
Unicef imeripoti kuwa, kuna idadi kubwa ya watoto maskini katika nchi zilizostawi yaani nchi tajiri na kwamba, Marekani na New Zealand pia ni miongoni mwa nchi hizo ambazo zinafanya vibaya kuhusu ustawi na afya ya vijana.
Shirika la Unicef limesema kuwa, asilimia 20 ya watoto katika nchi za Marekani na Uingereza hawapati vyakula salama na lishe bora ya kutosha.
Sarah Cook Mkurugenzi Unicef wa Ofisi ya Innocenti iliyochapisha ripoti hii amesema kuwa, serikali katika nchi zote zinapasa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa, mianya inapunguzwa na mafanikio yanapatikana.
Ujerumani na nchi za Nordic zimetajwa katika ripoti ya Unicef kuwa zenye idadi kubwa ya watoto ambao hawapati lishe bora na ya kutosha. Aidha idadi ya mabarobaro wenye matatizo ya kiakili inaongezeka katika nchi nyingi zilizostawi huku kukiwa na kiwango kikubwa cha tatizo la kunenepeana ovyo
No comments
Post a Comment