Writen by
sadataley
9:14 AM
-
0
Comments
Moja ya miundo mbinu inayojengwa kwenye mradi wa maji wa Ng’apa, mjini Lindi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji naUmwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akipata maelekezo kuhusu ramani ya ujenzi wa mradi wa Ng’apa kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa Mradi, Innocent Mgaya
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akiwa kwenye mazungumzo na Mhandisi Uendeshaji na Matengenezo, Yinus Krick kutoka Kampuni ya Lahmeyer na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi naUsafi wa Mazingira (LUWASA), Inj. Riziki Chambuso (katikati).
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akikagua moja ya miundo mbinu inayojengwa kwenye mradi wa maji wa Ng’apa, mjini Lindi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (LUWASA), Inj. Riziki Chambuso
………………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Majina Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi, mara baada ya ziara aliyoifanya jana mjini Lindi.
Prof.Mkumbo amefanya ziara hiyo kwania yakujua hali ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa, ambao unatekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Lindi (LUWASA),kama sehemu ya kufuatilia maagizo yaliyotolewa na Mhe. RaisJohn Magufuli miezi michache iliyopita wakati akiwa katika ziara yake yakikazi mkoani humo.
“Hali ya huduma ya maji Lindi si nzuri, ukizingatia inakidhi asilimia 40 tu ya mahitaji. Kwa mradi huu wa Ng’apa ukikamilika utatoa huduma ya maji kwa asilimia 100 kwa wakazi wa mjiwa Lindi, ikumbukwe Mhe. Rais alifanya ziara Lindi naakatoa maelekezo kuhusu mradi huu”, alisema Prof. Mkumbo.
Prof. Mkumbo alisema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais naamefurahishwa na maendeleo ya mradi huo, na kuwa maji yameshafika nakilichobaki ni kupelekwa kwenye chujio ambalo lipo kwenye matengenezo kabla ya kuanza kusambazwa kwa wananchi.
Huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi na LUWASA haina budi kutekeleza mradi huo kwa wakati kwania baya Serikali.
Wakatihuo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (LUWASA), Inj. Riziki Chambuso alisema mradi huo umefikia hatua nzuri na watatekeleza agizo la Rais kuwaifikapo mwezi Julai mradi utakuwa umekamilika na kuwapatia wakazi wa Lindi mjini maji.
Mradi wa Ng’apani moja ya miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kama sehemu yaahadi yake naunategemea kugharimu Sh. bilioni 29, kufikia sasa Sh. bilioni 22 zimeshatolewa. Ujenzi wa mradi huo, pia utahusisha upanuzi wa miundo mbinu ya maji kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na miundombinu hiyo kwa ajili ya kusambazia maji.
No comments
Post a Comment