Writen by
sadataley
8:20 AM
-
0
Comments
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akizungunza wakati wa utambulisho wa mradi wa Uzungwa Scarp leo |
Kaimu meneja wa Hifadhi ya Uzungwa Carp Yusiph Tango akitambulisha mradi wa uhifadhi wa misitu ya hifadhi ya Uzungwa Carp leo mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kilolo |
Kaimu meneja wa hifadhi ya misitu ya Uzungwa Scarp Yusuph Tango akitambulisho mradi wa uhifadhi wa misitu katika hifadhi ya Uzungwa Scarp leo |
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah katikati akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama pamoja na kaimu meneja wa hifadhi ya misitu ya Uzungwa Scarp Yusuph Tango wa tano kulia mara baada ya kutambulisha mradi wa Uzungwa Ccarp wa kuhifadhi misitu
Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imepongeza jitihada zinazofanywa na mradi wa Uzungwa Scarp katika kuhifadhi na kuhamasisha utalii ktika hifadhi hiyo na kutaka kasi ya uhamasishaji wa utalii izidi kutolewa.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi wa Uzungwa Scarp leo ,Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa jitihada za serikali ya wilaya hiyo ni kuona lango la utalii katika wilaya ya Kilolo linafunguliwa ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kukuza uchumi wao.
Alisema kuwa wilaya ya Kilolo yenye hifadhi zaidi ya moja ikiwemo hifadhi ya misitu ya Uzungwa Scarp na ile ya Hifadhi ya Taifa ya misitu ya Udzungwa ila bado kasi ya utalii inaweza kuongezeka na kuwa na maslahi zaidi kwa wananchi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa moja kati ya mipango ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuona Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na kupitia utalii kuna uwezekano viwanda zaidi kuanzishwa Kilolo.
Hata hivyo aliagiza hifadhi ya Mistu ya Uzungwa Scarp kuandaa eneo la kuwagawia wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za kitalii badala ya kuendelea kuhamasisha utalii bila kuwa na hoteli za watalii kufikia.
Aidha alisema ili uhifadhi huo uwepo ni lazima suala la uharibifu wa mazingira kusimamiwa kwa kuona moto hauharibu mazingira ya hifadhi hiyo.
Hivyo alisema serikali ya wilaya itahakikisha inatoa ushirikiano mkubwa kwa hifadhi hiyo na nyingine ili kuhakikisha wananchi hawaharibu mazingira ovyo ama kuingia ndani ya hifadhi hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Vallence Kihwaga pamoja na kupongeza hifadhi hiyo na wahisani wa UNDP kujitolea kujenga daraja la kuunganisha kijiji cha Uluti bado alitaka wananchi kutafutiwa shughuli nyingine kama za ufugaji wa samaki ili kupunguza kasi ya uwindaji hifadhini.
Alisema iwapo wananchi wataanzishiwa miradi ya ufugaji wa samaki ama mifugo mingine wataacha kuingia hifadhini kuwinda wanyama.
Kaimu mhifadhi wa hifadhi ya Uzungwa Scarp Yusuph Tango alisema kuwa hifadhi hiyo kijografia ipo Kilolo ,Mufindi na Kilombero na kwa Kilolo ina vijiji 7 na jumla ya vijiji vyote kwa Kilolo,Mufindi na Kilombero vinavyo pakana na hifadhi ni 19 na vyote vinanufaika na hifadhi hiyo kwa kusaidiwa shughuli mbali mbali za kimaendeleo.
Alitaja fursa zilizopo kuwa ni utalii na utafiti,ajira,uwekezaji kama Hoteli, Ufungaji nyuki,uzalishaji wa maji ya kunywa na nyingine nyingi.
Habari na Matukio Daima Blog
No comments
Post a Comment