Writen by
sadataley
1:42 PM
-
0
Comments
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy
Gwajima akifunga warsha ya siku tatu iliyolenga kuwajengea uwezo
madaktari nchini kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic
Surgery).
Baadhi
ya washiriki wakimsikiliza Dk Gwajima wakati wa kufunga mafunzo hayo
leo ambayo yamefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Profesa
Rafique Parkar akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya upasuaji wa
matundu madogo, Dk. Ibrahim Mkoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Muhimbili, Profea Lawrence Museru.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru
akimkabidhi cheti cha ushiriki Dk. Paul Kisanga wa Hospitali ya Selian
mkoani Arusha leo.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Watoto katika hospitali ya Muhimbili, Zaitun
Bhokary akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Profesa Museru.
Daktari
bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar
(kushoto) akimfanyia upasuaji mmoja wa kinamama mwenye matatizo ya uzazi
leo. Kulia ni Dk. Vicenti Tarimo akishirikiana na Profesa Parkar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia upasuaji mubashara katika ukumbi wa mikutano, Muhimbili leo.
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeze
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuendesha warsha ya siku tatu
kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic surgery) kwa madaktari
kutoka hospitali mbalimbali nchini.
Warsha
hiyo ilianza jumatano na imemalizika leo Ijumaa na kuwashirikisha
madaktari kutoka hospitali ya za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki,
Tumaini, Regency na Agha kan. Madaktari wengine ni kutoka hospitali za
umma zikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya
Mbeya, Mwanza, Arusha, Morogoo na Dodoma.
Pongezi
hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara hiyo Dk.
Dorothy Gwajima kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara, Dk. Mpoki Ulisubisya
wakati akifunga warsha hiyo.
Dk
Gwajima amewataka washiriki wa warsha hiyo kupeleka ujuzi waliojifunza
kwa madaktari wengine ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanakwenda
kutibiwa katika hospitali ya Muhimbili.
“Kwa
niaba ya wizara napenda kuipongeza Muhimbili kwa kuandaa mafunzo haya,
sisi wizara tunawaunga mkono na msifikiri tumewasahau la hapana kwani
tunatambua uwezo wa madaktari. Heshima ya hospitali itabaki pale pale
kwani Muhimbili kitovu cha uwanzishwaji wa HospitaOceac road, Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Mifupa ya Moi,” amesema Dk
Gwajima.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amewashukuru
madaktari kutoka hospitali za binafsi na umma kwa kushiriki kwenye
mafunzo hayo.
“Tumeanzisha
mafunzo haya na napenda kuwahakikishia tutaendelea kuandaa warsha kwa
kada nyingine ili kuwajengea uwezo madaktari wa hospitali za mikoa na
wilaya nchini,”amesema Profesa Museru.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar
ameishauri uongozi wa Muhimbili kuendelea kutoa mafunzo hayo na
kuendesha ufapasuaji wa njia ya matundu madogo kwa wagonjwa waliopo
mikoani kwani wengi wao hawana fursa ya kupatiwa huduma hiyo.
Washiriki walikabidhiwa vyeti baada ya mafunzo hayo kufungwa.
Katika
hatua nyingine, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kutumia njia ya
matundu madogo wanaendelea vizuri na baada ya afya zao kurejea katika
hali ya kawaida wataruhusiwa kurejea nyumbani.
Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji hadi leo wamefikia wanane.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
No comments
Post a Comment