Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 8, 2017

Wazungu Wamuwekea Ulinzi Mkali Samatta

ANATUSUA! Baada ya dau lake la usajili kupanda na kuwa euro milioni tatu (Sh bilioni 7.1), Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) limemtaja straika Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji kuwa ni mmoja kati ya wachezaji hatari wa kuchungwa .

Awali dau la Samatta lilikuwa ni euro milioni 2.2 (zaidi Sh bilioni 5) lakini baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao, dau lake limepanda.

Samatta ameisaidia timu yake kutinga hatua ya robo fainali ya Europa League huku yeye akifunga mabao sita katika mechi tano zilizopita, hii ni kwenye Europa mechi moja na nne za ligi na sasa wanajiandaa kuvaana na Celta Vigo kwenye hatua hiyo.

Kupitia ukurasa wao wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter ambao unatambulika kwa jina la Uefa Europa League, Uefa wameandika: “Mtu wa kuchungwa? Mbwana Samatta amefunga mabao sita katika mechi tano za mwisho kwa timu ya Genk.”

Mabao hayo sita ambayo Samatta alitupia ni dhidi ya KAA Gent alitupia mara mbili katika ushindi wa mabao 5-2 huku manne akifunga kwenye ligi, timu ambazo kazifunga ni Club Brugge ambayo alitupia mara mbili, Westerlo bao moja, kama ilivyo kwa KSC Lokeren.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment