Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, April 3, 2017

UN yaongeza muda wa MONUSCO DRC

media
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linaloongeza muda wa ujumbe wa umoja huo MONUSCO nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kupunguza idadi ya askari wake.
MONUSCO imeongezewa muda hadi tarehe 31 mwezi Machi mwakani.
Kwa mujibu wa umoja wa mataifa azimio hilo limegusia suala muhimu lililokuwa linajadiliwa kuhusu kupunguza idadi ya askari, ambapo sasa imepunguzwa hadi askari 16,215.
Azimio limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kufanya tathmini ya majukumu ya MONUSCO kwa wakati huu kuona iwapo majukumu yote ni muhimu.
Wanachama wa baraza hilo wamemuonya raisi Joseph Kabila kwamba utawala wake lazima iheshimu mkataba wa kusirikiana uongozi na upande wa upinzani na kuruhusu uchaguzi muhimu kufanyika.
Balozi wa uingereza katika baraza la usalama la umoja wa mataifa Matthew Rycroft, ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza mwezi huu ameeleza kuwa ukosefu wa usalama na mvutano umeendelea kushuhudiwa katika kipindi chote nchini DRC.RFI
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment