Dar es Salaam. Kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mechi mbili za kirafiki dhidi ya Burundi uliopigwa mjini Bukoba wiki juzi.
Shime alisema mechi hizo dhidi ya Burundi na ujao dhidi ya Ghana utampatia picha halisi ya mikakati ya kufanya kama benchi la ufundi.
“Ninaisubiri kwa hamu mechi ya Ghana kwakuwa wenzetu wana timu nzuri za vijana, ninaamini itatupa changamoto nzuri,”alisema Shime, aliyewahi kuinoa Mgambo Shooting ya Tanga.
Leo, Serengeti itacheza na Ghana katika mchezo mwingine wa kirafiki kabla ya kwenda Morocco ambako itaweka kambi ya sanjari na kucheza mechi za kujipima nguvu.
“Mechi zina umuhimu mkubwa, kabla hatujakwenda Morocco tunataka kujua wapi tumefika ili tupange programu nzuri na ya uhakika. Kumbuka tumebaki na wiki sita kabla ya mashindano tunapaswa kuwa makini,”alisema
Mshambuliaji Yohana Mkoma alisema mechi za kirafiki zitawaongezea hali ya kujiamini kabla ya kwenda Gabon.
“Tumefanya mazoezi kwa muda kwa hiyo mechi za kirafiki zinatujenga kama wachezaji, tukicheza mechi nyingi zaidi tutakuwa tayari kwa mashindano,”alisema Mkomolo ambaye aliifungia Serengeti mabao manne katika mechi za kufuzu
Tanzania imepangwa Kundi B katika mashindano Afcon 2017 ikiwa pamoja na Niger, Angola na mabingwa watetezi Mali.
No comments
Post a Comment