Writen by
sadataley
11:32 AM
-
0
Comments
Akizungumza katika Ibada ya misa takatifu katika Kanisa la Maria Imamakulata, Jimbo Katoliki la Mpanda, Pinda alisema bado ana uwezo wa kuchangia katika taifa na jamii kwa kuwa ana afya njema.
Mbali na hilo, Pinda aliwaeleza waumini hao kuwa amefanya kazi serikalini kwa miaka 40, hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kipindi hicho chote alichofanya kazi.
“Katika kipindi cha utumishi nikiwa serikalini, miaka ishirini na mbili nimefanya kazi nikiwa Ikulu na miaka 15 kazi ya siasa, yaani ubunge pamoja na miaka mitatu nimefanya katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” alisema Pinda.
Aidha aliwaomba viongozi wa dini wawaombee viongozi wa Serikali wawe na nguvu na afya za kuliongoza taifa na pia waiombee nchi amani na utulivu izidi kuendelea.
Pinda aliwataka waumini wa kanisa hilo kuwapeleka watoto wao kusoma katika Seminari ya Mtakatifu Paulo ili jimbo hilo liwe na mapadri wengi, huku akieleza kuwa amevutiwa na matokeo ya ufaulu kwa kidato cha pili kwa miaka miwili mfululizo.
Naye Paroko wa Kanisa hilo, Monsinyori George Kisapa, alimshukuru Pinda kwa michango yake mbalimbali ya maendeleo aliyoitoa kwenye jamii na kwenye kanisa wakati na baada ya uongozi wake.
Alisema anaungana na Pinda kuwataka wazazi wawapeleke watoto wao kusoma shule za seminari ingawa si lazima kila anayesoma huko atakuwa padre.
Alisema seminari inasaidia kwa kiasi kikubwa kupata viongozi bora wa baadaye kama alivyokuwa waziri huyo mstaafu, ambaye alisoma katika Seminari ya Kaengesa mkoani Rukwa.
No comments
Post a Comment