Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, November 30, 2016

Bashir: Ni rahisi kufanya kazi na Donald Trump

Rais Omar el Bashir wa Sudan

Image copyrightREUTERS
Image captionRais Omar el Bashir wa Sudan
Kiongozi wa Sudan Omar el Bashir amempongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump akisema kuwa itakuwa rahisi kushirikiana naye, kulingana na gazeti la Emirati al Khaljee.
''Bw Trump anaangazia maslahi ya raia wa Marekani, ikilinganishwa na wale wanaozungumzia kuhusu demokrasia ,haki za kibinaadamu na uwazi'',alisema rais Bashir katika mahojiano na gazeti hilo.
Aliongezea kwamba: Tunaweza kushirikina na watu wenye sura mbili lakini huyu hapa mtu mwenye uwazi wa anajua anacholenga.
''Nina hakika itakuwa rais kushirikiana na Trump ikilinganishwa na wengine kwa sababu ni mtu anayeangazia maswala moja kwa moja na mfanyibiashara ambaye anaangazia maslahi ya anaoshirikiana nao'',alisema Bashir. 
Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya ICC kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika eneo la Drafur amekana mashtaka hayo.
Alichukua mamlaka mwaka 1989 kupitia mapinduzi na ameshutumiwa kwa kuwa na uongozi wa kiimla tangu wakati huo.

Iran nyuklia: Mkurugenzi wa CIA amuonya Trump

Brenann

Image captionJohn Brenann
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani CIA amemuonya rais mteule wa Marekani Donald Trump kwamba kusitisha makubaliano ya mpango wa nyuklia na Iran itakuwa ''hatari na upuuzi''.
Katika mahojiano na BBC ,John Brennan pia alimshauri rais huyo mpya kuwa na tahadhari kuhusu ahadi mpya za Urusi akiilaumu Moscow kwa mateso yanayoendelea nchini Syria.
Katika kampeni yake ,bw Trump alitishia kufutilia mbali mpango wa mnyuklia nchini Iran mbali na kuashiria kufanya kazi kwa karibu na Urusi.
Bw Brenan atajiuzulu mnamo mwezi Januari baada ya kuhudumia shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne.
Katika mahojiano ya kwanza na vyombo vya habari vya Uingereza ,Brennan alitaja maswala kadhaa ambapo alisema kuwa utawala mpya unafaa kuzingatia kwa busara na heshima, ikiwemo lugha inayotumiwa kuhusu ugaidi, uhusiano na Urusi, mpango wa kinyuklia wa Iran na vile siri za shirika hilo hutekelezwa.

Yusuph Kileo akwaa tuzo ya TEHAMA

Tanzania


Image copyrightYUSUPH KILEO
Image captionYusuph Kileo mwana usalama wa mtandao akwaa tuzo ya TEHAMA

Kila mwisho wa mwaka kumekua kukitolewa tunzo za utambuzi wa michango mbali mbali ya wana TEHAMA maeneo mengi ambapo mwaka huu Tuzo 31 zilitolewa jijini Nairobi Nchini kenya.
Moja ya Tunzo ilikua mwana usalama mtandao bora wa mwaka ambapo Mtanzania Yusuph kileo, Mtaalam wa maswala ya usalama mtandao na uchunguzi wa makosa ya Digitali ameitwaa tuzo hiyo ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika mataifa mbali mbali barani afrika.
Kileo amekua chachu ya kuimarisha usalama mitandao maeneo mengi , si tu barani Afrika bali pia nje ya bara la Afrika. na amekiri tuzo aliyo ipata itamuongezea hari ya kujituma zaidi katika maswala ya usalama mtandao.
Aidha, Katika kuzungumzia hali ya usalama mtandao hivi sasa Yusuph Kileo ameeleza, Si shwari na bado hairidhishi kwani bado mashambulizi mtandao yanaonekana kuendelea kujitokeza maeneo mengi duniani.
Kileo amefafanua ya kua kipi hiki pekee cha kuelekea mwisho wa mwaka mashambulizi milioni hamzini yametegemewa hiku idadi kubwa tayari ikiwa imesha fikiwa.
Miongoni mwa waathirika ni pamoja na Mabenki, makampuni ya simu , mashule, hospitali na maeneo mengine mengi.
Kirusi kipya kinacho muwezesha mashine za kutolea fedha kutoa fedha zenyewe bila ya mhalifu kua eneo la tukio ni miongoni mwa yaliyo jitokeza kwa kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka huku kirusi cha RANSOMWARE bado kikiumiza kichwa wana usalama mitandao hasa baada ya kupiga hodi barani afrika.
Kirusi ambacho kina mnyima mtumiaji halali wa vifaa vya digitali kutumia kifaa chake hadi alipe kiwango cha pesa.
Kileo amesisitiza yote yanayo jiri imekua yana ambatana na wizi mtandao ambapo fedha imekua ni tegemeo kuu - Kileo ameonya kama hali hii haita angaziwa kuna hatari ya Uchumi wa mataifa mengi kuyumba kutokana na wizi mtandao unaoendelea kuchukua sura mpya kila siku.

Rais Magufuli azuru gereza la Ukonga ghafla

Tanzania

Image copyrightGOOGLE
Image captionAmiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,akiwa katika gereza la Ukonga.
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar -Es - Salaam na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini humo na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.
Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi.
Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini mwake kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli''
Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini DSM.
Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa wakitumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.
Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini Tanzania.

Tuesday, November 29, 2016

SHULE TATU ZA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA DAYOSISI YA IRINGA ZAPATA VYETI MAALUM TOKA WIZARA YA ELIMU KWA KUWA MIONGONI MWA SHULE ZINAZOMILIKIWA NA WATU BINAFSI ZINAZOENDELEA KUFANYA VIZURI.






Habari kwa hisani ya Katibu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Iringa

Chadema Kukusanya Bilioni 13.9 Kwa Mwaka Kupitia Kadi Mpya za Wanachama Zitakazoanza Kutolewa Mwakani

Chadema imetangaza kuwa Januari itaanza kutumia kadi mpya za uanachama za kielektroniki, zitakazoiwezesha kukusanya Sh13.9 bilioni kwa mwaka na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali.

Mkakati huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika mkoani Morogoro. Tofauti na Mbowe, viongozi wengine wa chama hicho walioko mikaoni ni Edward Lowassa aliyeko Dodoma na Frederick Sumaye ambaye yupo Singida.

Mbowe alisema mfumo huo utasaidia pia kudhibiti baadhi ya viongozi wasio waaminifu, wanaotumia mwanya wa kuuza kadi na kushindwa kuwasilisha fedha kwenye hazina ya chama.

Alisema kwa mfumo huo mpya, kama Chadema itakuwa na wastani wa wanachama 100,000 katika wilaya moja na kila mmoja kulipa ada ya Sh1,000 kwa mwaka, maana yake itaingiza Sh100 milioni.

Kwa hoja hiyo ya Mbowe, ikiwa chama hicho kitakuwa na wastani wa wanachama 100,000 katika kila wilaya za Tanzania Bara ambazo ni 139, Chadema itakuwa na uwezo wa kukusanya Sh13.9 bilioni kila mwaka.

Vyama vya siasa vinapata ruzuku kwa mujibu wa sheria na ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilibainisha kuwa jumla ya Sh67.7 bilioni zililipwa na Serikali kwa vyama vya siasa katika mwaka kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka wa fedha 2009/2010 mpaka 2012/2013. Fedha ambazo kwa mujibu wa CAG zilikuwa hazijakaguliwa kisheria.

Ikilinganishwa na mkakati mpya wa Chadema, fedha hizo ni ndogo katika kuhudumia shughuli za chama nchi nzima.

Mbowe alisema Chadema imeamua kuhakiki wanachama wake ili ifikapo Januari iwe tayari imemaliza kazi hiyo na kuingia rasmi katika mfumo mpya, utakaokisaidia kuondokana na dhana ya utegemezi wa ruzuku kutoka serikalini.

Alisema ili chama kipige hatua na kuondokana na utegemezi wa ruzuku serikalini, wamekusudia kuingia katika mfumo wa kupata mapato kutoka ndani ya wanachama kupitia ulipaji wa ada.

Mbowe alizungumza na wanachama hao kutoka ngazi za vitongoji, vijiji, kata na wilaya waliohudhuria mkutano mkuu maalumu wenye lengo la kuwakumbusha mambo mbalimbali ya kuimarisha chama hicho baada ya Serikali ya Rais Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara.

“Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, Chadema itakuwa tayari imefanya utambuzi wa wanachama wake kwa kuwatambua katika kila mtaa, kitongoji, kijiji, kata na jimbo kupitia mfumo mpya wa kadi za eleketroniki ifikapo Januari 2017,” alisema Mbowe.

Alisema katika baadhi ya maeneo ya mikoa hapa nchini, kadi za uanachama za Chadema ni lulu na zimekuwa zikiuzwa hadi Sh5,000 badala ya 500.

Alieleza kuwa mapato ya chama lazima yatokane na ada za wanachama na siyo ruzuku ya Serikali, kwa kuwa utegemezi wa ruzuku ni hatari kwa uhai wake.

“Hii ruzuku inayotolewa na Serikali inatolewa kwa sababu ya CCM na CCM bila ruzuku hakiwezi kujiendesha,” alidai.

Mbowe alisema kila jimbo linapata fedha za ruzuku kulingana na idadi ya kura ilizopata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, akitolea mfano Jimbo la Mlimba kuwa Mbunge Suzan Kiwanga alishinda kwa kura 40,000 wakati urais Chadema ilipata kura 38,000 huku katika udiwani wakipata kata tisa kati 16.

“Kutokana na ruzuku, Mlimba itapata Sh163,688 kila mwezi. Unaweza kuona fedha za ruzuku kutoka ndani ya chama ni ndogo sana ambapo Mkoa wa Morogoro unapokea kiasi cha Sh2.2 milioni kila mwezi.

“Kufikia mwaka 2017 kupitia programu ya Chadema msingi, tumekusudia kukijikita zaidi kusaka wanachama kutoka ngazi ya mitaa, vitongoji na balozi na tutaanza uchaguzi ndani ya chama.

“Tumebaini kuwa baadhi ya maeneo Chadema tumeshindwa kupata wenyeviti wa Serikali ya vitongoji na vijiji, kukosa madiwani na wabunge kutokana na kukosa misingi imara wa wanachama,” alisema Mbowe
.

RAIS DKT.MAGUFULI AMWANDALIA RAIS EDGAR LUNGU DHIFA YA KITAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

     Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa hiyo ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake Ikulu jijini Dar es salaam.
 Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa
 Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.(P.T)
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akisherehesha hafla hiyo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akigonganisha glasi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Wimbo wa Taifa 
 Viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Zambia ukipigwa
 Viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Zambia wakiwa wamesimama kwa wimbo wa Taifa 
 Sehemu ya Mawaziri waliohudhuria wakiwa wamesimama
 Viongozi wakiwa wamesimama
 Makatibu wakuu na sehemu ya ujumbe wa Zambia
 Wageni waalikwa na viongozi wa vyama vya siasa
 Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliohudhuria
 Wageni mbalimbali
 Mabalozi mbalimbali
 Mabalozi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje 
 Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali
  Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali na maafisa wa Wizara ya Mambo ya nje
 Viongozi wa taasisi mbalimbali
 Viongozi wa kidini na wageni mbalimbali
 Makatibu wakuu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace Mujuma
 Rais Dkt Magufuli akigonganisha glasi na mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia
 Mrisho Mpoto na Banana Zorro na Mjomba band akitumbuiza
 Mrisho Mpoto akighani wimbo maalumu
 Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 
 Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 
 Rais Edgar Lungu akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
 Rais Edgar Lungu akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Rais Edgar Lungu akisindikizwa na mweyeji wake Rais Dkt Magufuli
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakiondoka baada ya dhifa
Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu Dkt.  Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakifurahia jambo mara baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam.
 PICHA NA IKULU

KINANA AKUTANA NA UJUMBEA WA CPC YA CHINA

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya Mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (Wakwanza kushoto),  alipokutana naye na kufanya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam.
Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. Wapili ni Kaimu Balozi wa China hapa Nchini, Gou hao Domg. Na walioketi kulia, ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Katibu wa NEC, Sisa na Ushorikiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chama.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akimsalimia  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo kabla ya kuanza mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Kaimu Nalozi wa China hapa nchini, Gou Hao Dong, alipowasili katika ukumbi wa Sekretarieti kwa ajili ya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (katikati)
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akijiandaa kukaa tayari kwa mazungumzo na Jia Bo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alipowasili ukumbini. Madabida ndiye Mwenyeji wa ujumbe huo wa China.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akiiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo katika picha ya pamoja na ujumbe wa CCM na CPC, baada ya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. 
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akiagana na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Hao Dong, baada ya mazungumzo.
Balozi wa China hapa nchini, Gou Ho Dong akiagana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana baada ya mazungumzo hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog.