Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, October 18, 2016

Mahakama ya katiba Katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo imeidhinisha ombi lililozusha mzozo la tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi wa Novemba ili orodha ya usajili wa wapiga kura iwekwe sawa.

Uchaguzi mkuu unazidisha hali ya wasiwasi Congo

Image copyrightAFP

Kiongozi wa mahakama ya katiba, Benoit Lwamba Bindu amesema mahakama hiyo inatambua kuwa kuna matatizo ya kiufundi na imeamrisha 'kucheleweshwa kwa sababu zinazoeleweka.' 
Imesema tume hiyo ni lazima ichapishe kalenda mpya ya uchaguzi wa urais ambao awali ulipangwa kufanyika Novemba 27. 
Tume ya uchaguzi Congo iliwasilisha rufaa mahakamani ya kuchelewesha uchaguzi huo mnamo mwezi September. 
Kufikia sasa imesema huenda uchaguzi usiweze kuandaliwa hadi mwishoni mwa mwaka 2018, jambo linalozusha wasiwasi kuwa hofu na ghasia zitaongezeka.

Madaraka na Uongozi 

Rais Joseph Kabila alitarajiwa kujiuzulu Desemba baada ya muda wake kikatiba kumalizika baada ya kuhudumu kwa mihula miwili madarakani.
Upinzani unasema kuwa Kabila anajaribu kuendelea kushikilia madaraka kwa kuchelewesha uchaguzi. 

Ghasia katika maandamano ya kuipinga serikali ya rais KabilaImage copyrightAFP
Image captionGhasia katika maandamano ya kuipinga serikali ya rais Kabila

Mahakama ya juu imesema, rais Kabila anaweza kusalia madarakani mpaka kiongozi mpya atakapo chaguliwa.
Watu kadhaa wameuawa katika mji mkuu Kinshasa mwezi Septemba baada ya vikosi vya usalama kupambana na maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali.
Pia siku ya Jumatatu, chama tawala na washirika wengine katika mazungumzo ya kitaifa wamekubaliana kuhusu azimio kuwa uchaguzi wa urais, wabunge na madiwani unapaswa kufanyika April 2018, uamuzi ambao huenda ukapingwa na vyama vikuu vya upinzani nchini, ambavyo vimesusia mazungumzo hayo ya kitaifa. 
Vyama vikuu vya upinzani vimetaka jumuiya ya kimataifa na Umoja wa mataifa kuwajibika zaidi na Muungano wa Afrika katika kuidhinisha mazungumzo yalio na hadhi kubwa zaidi na yanayojumuisha pande zote kuhusu kuandaa uchaguzi mkuu, na vimeitisha maandamano ya Oktoba 19 iwapo hakuna hatua itakayo pigwa. 
Vimetaka pia tume ya uchaguzi, na mahakama ya kikatiba zifanyiwe mabadiliko, vikieleza kuwa zinampendelea Kabila. 
Tangu Congo ijinyakulie uhuru kutoka Ubelgiji mnamo 1960, hapaja shuhudiwa mageuzi ya uongozi kidemokrasia kwa amani.

Shirika la utangazaji la NBC nchini Marekani limemfuta kazi mtangazaji Billy Bush ambaye amekuwa akiendesha kipindi cha Today.

Billy BushImage copyrightAP
Image captionBw Bush ameomba radhi kutokana na aliyoyasema wakati wa mahojiano hayo
Mgombea urais wa chama cha Republican alikuwa anahojiwa na Bw Bush miaka kumi iliyopita alipotoa matamshi ya kudhalilisha kuhusu wanawake.
Ukanda wa mahojiano hayo yaliyofanyika mwaka 2005 ulifichuliwa majuzi na gazeti la Washington Post.
Baada ya kufichuliwa kwa ukanda huo, viongozi wengi wakuu wa chama cha Republican walijitenga na Bw Trump ambayo yamezua utata.
Kwenye video hiyo, Bw Bush anasikika akicheka baada ya matamshi ya Bw Trump.
Billy Bush, 45, ambaye ni mpwa wa rais wa zamani George H W Bush, alikuwa awali amesimamishwa kazi baada ya kufichuliwa kwa video hiyo.
Amekuwa mtangazaji wa kipindi cha Today kwa miezi miwili pekee.
"Ingawa alikuwa mgeni tu katika waandaaji wa kipindi cha Today, amekuwa na NBC kwa muda mrefu. Tunamtakia kila la heri," shirika la NBC limesema kupitia taarifa.
Mke wa Donald Trump, Melania, amemshutumu Bw Bush akisema alimchochea mumewe kusema mambo mabaya kuwahusu wanawake.
Bw Bush mwenyewe aliomba radhi tarehe 7 Oktoba akisema binafsi pia aliaibishwa na tabia yake alipokuwa akifanya mahojiano hayo.

Friday, October 14, 2016

JUHUDI ZA MWALIMU NYERERE KATIKA KUKUZA NA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII NCHINI.

Na Beatrice Lymo- MAELEZO
“Uhai wa wanyamapori ni jambo linalotuhusu sisi sote katika Afrika, viumbe hai wa porini wakiwa katika mapori waishimo sio muhimu tu kwa ajili ya kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na mustakabali wa maisha yetu baadaye”
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema hayo wakati akitoa tamko la Arusha kuhusu Uhifadhi wa wanyamapori kipindi Tanganyika inapata Uhuru mwaka 1961.
Alisema kwa kukubali dhamana ya wanyamapori, watanzania watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wajukuu na watoto wa kitanzania wanaweza kufurahia urithi mkubwa wa thamani hiyo adimu ya wanyamapori.
Juhudi za uhifadhi na kulinda rasilimali, malikale na kuendeleza shughuli za ufugaji nyuki pamoja na kukuza Sekta ya Utalii ikiwa ni jukumu la Wizara ya Maliasili na Utalii zilikuwepo hata kabla ya ukoloni ambapo jamii nchini zilitenga mapori kwa ajili ya kuabudia na kutambika.
Kuingia kwa wakoloni nchini kuliambatana na kutunga Sheria za uhifadhi wa rasilimali za maliasili na malikale ambapo ni Sheria ya kuhifadhi Majengo ya kihistoria ya mwaka 1937, Sheria ya Makumbusho ya mwaka 1941, Sheria ya Usimamizi wa Misitu ya mwaka 1957, Sheria ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1959, Sheria ya Hifadhi za Taifa ya mwaka 1959 na Sheria ya kuhifadhi wanyama ya mwaka 1959.
Chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kuanzia mwaka 1961 Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa na Sera na Sheria tofauti kulingana na mabadiliko yaliyokuwa yakitokea duniani katika nyanja za kiuchumi, kiteknolojia, kiasiasa na kijamii.
Juhudi za Baba wa Taifa katika kuhakikisha Sekta ya utalii ambapo ilikuwa na idara moja mwaka 1961 kuanza kuwa na Sera ya uhifadhi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii nchini zinaonekana.
Mabadiliko na matukio makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya uhuru mwaka 1961 yalipelekea jitihada za makusudi za kuwezesha wazawa kielimu ili kuweza kuchukua nafasi za utendaji na uongozi ambazo awali zilishikiliwa na wageni.
Aidha, mwaka 1967 kufuatiwa kupitishwa Azimio la Arusha chini ya uongozi wa Baba wa Taifa mali binafsi zilitaifishwa na kuundwa kwa mashirika na taasisi za umma ambapo Wizara iliunda mashirika ya umma ikiwemo Shirika la Wanyamapori, Shirika la Viwanda vya mbao, Shirika la Utalii Tanzania, Shirika la kuhudumia wasafiri na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kukuza na kuimarisha sekta ya utalii nchini.
Katika mabadiliko hayo ndani ya Wizara, juhudi za Mwalimu Nyerere zilipelekea Serikali kujitoa katika kuendesha shughuli za kibiashara na kujikita katika kusimamia Sera na uwezeshaji.
Kadhalika katika suala la ulinzi wa rasilimali za maliasili, Serikali ilirithi mfumo wa ukoloni ambapo Serikali ilikuwa ndiye mlinzi na mwendelezaji mkuu wa rasilimali za maliasili, malikale na utalii ambapo mabadiliko ya kisera na mwelekeo wa uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali ulifanyika miaka ya 1991 kwa kuhimiza ushirikishwaji wa jamii katika uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za maliasili, malikale na utalii.
Ushirikishwaji jamii katika shughuli za maliasili na utalii ulichangia katika Wizara kuanzisha vitengo mbalimbali ikiwemo kitengo cha Ugani katika idara na taasisi zake ikiwa na lengo la kuimarisha na kukuza sekta ya utalii nchini.
Vilevile, katika suala la ajira na jinsia katika wizara, wakati nchi inapata uhuru sekta za maliasili hususani wanyamapori, misitu, malikale na nyuki zilikuwa maalumu kwa wanaume ambapo juhudi za Mwalimu Nyerere ziliwezesha kupatikana kwa ajira ikihusisha jinsia zote mbili, ambapo sekta ya utalii ikaajiri mwanamke kwa mara ya kwanza mwaka 1970.
Katika sekta ya nyuki wanawake wawili waliokuwa na astashahada ya ufugaji wa nyuki waliajiriwa mwaka 1975, sekta ndogo ya misitu iliajiri mwanamke wa kwanza mwenye shahada mwaka 1976, katika sekta ndogo ya wanyamapori mwanamke aliajiriwa mwaka 1967 na katika sekta ya mambo ya kale mwanamke aliajiriwa mwaka 1978 kwa ngazi ya cheti na 1981 kwa ngazi ya shahada.
Kama Mwalimu Nyerere, Rais John Pombe Magufuli naye ameonyesha kukerwa na vitendo vya ujangili na biashara haramu ya kuuza meno ya tembo. Katika hotuba zake Mhe. Rais Magufuli amekuwa akisisitiza utunzaji wa maliasili kwa ajili ya maendelo ya Taifa.
Pia katika kuongeza tija na kufanya maamuzi kwa kutumia taarifa zilizofanyiwa utafiti, wizara ilianzisha vyuo vya ulinzi, uhifadhi na uendelezaji wa maliasili, malikale na utalii ambapo chuo cha viwanda vya misitu kilianzishwa mwaka 1975, chuo cha ufugaji nyuki Tabora mwaka 1978 pamoja na vyuo vya elimu ya wafanyakazi Rongai na Sao Hill vilivyoanzishwa mwaka 1979 kwa lengo la kutoa elimu ya awali ya uoteshaji miche na kuhudumia misitu.
Katika kukuza na kuimarisha sekta ya utalii nchini Mwalimu Nyerere aliweza kutekeleza majukumu ya wizara kulingana na mabadiliko ambayo yamekuwa yakitokea nchini na duniani katika nyanja ya kiuchumi, kisiasa kiteknolojia na kijamii.
Juhudi hilo zilipelekea wizara kuongeza vituo vya malikale na kutangaza maeneo tofauti kama urithi wa Taifa, mashamba ya miti yaliongezeka, misitu ya asili pamoja na hifadhi za Taifa kuongezeka.
Mbali na hayo juhudi za Mwalimu katika kukuza na kuimarisha sekta ya utalii mara baada ya uhuru zilichangia katika ongezeko la mikusanyo ya malikale ambapo wakati wa uhuru wizara ilihifadhi jumla ya mikusanyo 10,151 ya fani za Akiolojia, mila, historia, bayolojia na nyaraka mbalimbali.
Aidha baada ya uhuru kutokana na tafiti zilizofanywa na watafiti wazawa na wageni kutoka nje ya nchi hadi juni, 2011 wizara imefanikiwa kuhifadhi nchini urithi wa malikale unaohamasisha wenyeji jumla ya mikusanyo 337,361.
Katika suala la ongezeko la idadi ya watalii wanaongia nchini ndani ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere idadi ya watalii iliongezeka kutoka watalii 9,847 mwaka 1960 hadi watalii 103,361 mwaka 1986.
Mbali na hayo katika kuendeleza jitihada za kukuza na kuimarisha sekta ya utalii nchini, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, kwenye Sherehe ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba Wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, Singida mwaka 2005 alisema kuwa sekta ya utalii ni muhimu katika ukuzaji wa uchumi wetu hivyo ni budi kuitunza na kuithamini.
“Ukweli unaojionyesha ni kwamba kama tukijikita katika sekta hii tunaweza kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi katika nchi yetu, nategemea kwamba sekta hii inaweza ikatuongezea mchango wake katika pato la Taifa hivyo tutumie rasilimali zilizopo kuwavutia watalii na wawekezaji wengine kuingia katika sekta hii”, aliongeza Rais Mkapa.
Alibainisha kuwa hifadhi ya mazingira ni eneo ambalo linahitaji nguvu za pamoja na za haraka katika kuepusha athari zinazoweza kutokea kama hatujali na kutilia maanani hivyo jamii inahitaji kuhifadhi misitu, vyanzo vya maji na kupanda miti kwa wingi ili kuzuia nchi kuwa jangwa.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi hivi karibuni alitoa wito kwa watanzania kuongeza juhudi katika kusaidiana na Serikali kupiga vita ujangili hapa nchini kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo.
Rais mstaafu huyo, alisema kumekuwa na tatizo la mauaji ya wanyamapori hapa nchini ambayo ni dhambi na ni kinyume na kusudio la Mungu kwa kuwa wanyama hao wana haki ya kuishi kama viumbe wengine.
“Kumekuwa na matukio mengi ya uuaji wa wanyamapori ikiwemo tembo na faru na hivyo kupunguza rasilimali ya taifa kwa vizazi vijavyo na pia kitendo hicho ni kinyume na kusudio la Mungu hivyo ni vizuri kuwatunza, kuwapenda, kuwaendeleza na kuwalinda wanyama hao kwani ni moja ya vivutio vinavyochangia pato la Taifa” aliongeza Rais Mstaafu Mwinyi.
Nae Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar aliwataka Wananchi kutumia vivutio vya utalii vilivyopo ili kuweza kukuza utalii wa ndani kwani kwa pamoja taifa litaendeleza juhudi za kukuza sekta ya utalii kwa kauli mbiu ya “Utalii kwa wote” ili iendelee kuwa na mchango mkubwa katika soko la ajira, kuingiza fedha za kigeni na katika kukuza Pato la Taifa kwa jumla.
Sambamba na hilo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alisema asilimia 80ya mapato ya fedha za kigeni zinazoingia nchini kupitia Sekta ya Utalii inaweza kubakia kuwa ndoto kama suala la amani na utulivu halitazingatiwa na kupewa nafasi yake chini ya usimamizi wa Jamii kwa mashirikiano na Serikali Kuu.
Alisema hakutakuwa na mgeni wala mtalii atakayekuwa na shauku ya kutaka kuingia nchini sambamba na kufifia biashara ya Utalii endapo amani na utulivu uliopo utachezewa na hatimae kutoweka kabisa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa kumekuwa na changamoto zilizohusu masuala ya Maliasili na Utalii zilizojitokeza wakati wa kampeni ikiwemo ujangili ambao lazima Idara husika inashiriki, Migogoro ya mipaka kati ya vijiji na Hifadhi, Upotevu wa mapato hivyo kuahidi kuzifuatilia changamoto hizo ili kuweza kukuza na kuimarisha sekta ya utalii nchini.
Mbali na hayo wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la Jamhuri Rais Magufuli aliwataka mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje kutumia fursa walizo nazo katika kutangaza utalii wa nchi ili kuweza kuongeza pato la Taifa.
Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kutekeleza majukumu yake licha ya mabadiliko na changamoto mbalimbali na inatarajiwa kuwa rasilimali za maliasili, malikale na utalii zitaendelea kuchangia kwa kiwango kikubwa juhudi za kukuza uchumi wa Taifa.
Hakika Mwalimu Nyerere mchango wake kwa sekta ya utalii haiwezi kusahaulika, itakumbukwa vizazi hadi vizazi. Utalii ukitiliwa mkazo na kuboresha miundombinu ya kuwawezesha watalii kufika na kukaa bila taabu ni dhahiri watalii wataongezeka na hivyo kukuza Pato la Taifa.
Chanzo:Mjengwa Blog

Mfalme wa Thailand Bhumibol kuombolezwa mwaka mmoja

Watu walia kuomboleza Mfalme Bhumibol Adulyadej Bangkok, Thailand, Alhamisi 13 Oktoba 2016.

Image copyrightAP
Image captionWatu wengi waliokuwa nje ya hospitali alimokuwa amelazwa Mfalme Bhumibol walilia kwa huzuni baada ya kifo chake kutangazwa

Raia wa Thailand wameanza kuomboleza kufuatia kifo cha Mfalme Bhumibol Adulyadej, ambaye alikuwa nguzo ya uthabiti wa kisiasa nchini humo wakati wa utawala wake uliodumu miaka 70.
Mfalme Bhumibol Adulyadej, ambaye ndiye mfalme aliyetawala muda mrefu zaidi duniani, alifariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 88.
Umati mkubwa wa waombolezai walikesha Bangkok wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyeusi, na wengi sasa wanarejea katika barabara za mji.
Mwili wa mfalme huyo utapelekwa katika hekalu la Temple baadaye leo.
Maombolezi rasmi yatadumu kwa mwaka mmoja.
Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn anatarajiwa kwa mfalme mpya, lakini ameomba shughuli yake kurithi madaraka icheleweshwe kidogo.

Maelfu wamejitokeza barabara za Bangkok kusubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo 14 Oktoba 2016
Image captionMaelfu wamejitokeza barabara za Bangkok kusubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo
Waombolezaji barabarani (14 Okt 2016)Image copyrightAP
Image captionRaia wa Thailand ambao walimchukulia mfalme huyo kuwa nguzo ya uthabiti wamesikitishwa na kifo chake.

Baraza la mawaziri lilitangaza siku ya Ijumaa kuwa siku ya mapumziko.
Bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kwa siku 30 zijazo.
Serikali imewaomba watu wavalie mavazi ya rangi nyeusi na kujiepusha na hafla za "furaha" kipindi hicho.
Tovuti za habari nchini humo zimegeuza rangi za kurasa zake kuwa za rangi nyeusi na nyeupe.
Viongozi mbalimbali duniani wamekuwa wakituma salamu za rambirambi.
Maelfu ya waombolezaji wamefika katika barabara za mji wa Bangkok wakisubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo kutoka hospitali ya Siriraj hadi Kasri Kuu Ijumaa adhuhuri.
Mwanamfalme anayetarajiwa kuwa mrithi wa ufalme ataongoza shughuli za kuosha maiti ya mfalme huyo, tambiko la Kibuddha, Ijumaa jioni, maafisa wa kasri wamesema.

Bangkok 14 Oktoba 2016
Image captionWengi wanavalia mavazi ya rangi nyeusi Bangkok
Mfalme Bhumibol AdulyadejImage copyrightEPA
Image captionMamia ya watu wamejitokeza kuomboleza nje ya kasri la Grand Palace, Bangkok
Bangkok (14 Okt 2016)Image copyrightREUTERS
Image captionMfalme huyo alipendwa sana na raia wa Thailand ambao walimchukulia kama mteule wa Mungu

Mfalme Bhumibol alichukuliwa kama nguzo ya uthabiti kwenye taifa hilo lililokumbwa na misukosuko ya kisiasa na mapinduzi ya serikali.

Mfalme Bhumibol AdulyadejImage copyrightEPA
Image captionWengi waliomboleza hadharani baada ya habari za kifo chake kutangazwa

Thailand bado inatawaliwa na jeshi ambalo lilitwaa mamlaka kupitia mapinduzi 2014. 
Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn anatarajiwa kuwa mfalme mpya, amesema tangazo hilo litatolewa baadaye.
Amethibitisha kwamba atatekeleza majukumu yote kama mfalme mtarajiwa, lakini akawataka raia waomboleze kifo cha babake kwanza. 

Maha VajiralongkornImage copyrightAFP
Image captionMwanamfalme Vajiralongkorn hajafahamika sana na raia wa Thailand

Mwanamfalme Vajiralongkorn, 64 hajafahamika sana na raia wa Thailand na hajapendwa sana na raia kama babake.
Ameishi muda mwingi nje ya nchi, sana Ujerumani.