Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, September 30, 2016

Viongozi wamlimbikizia sifa Shimon Peres mazishini Jerusalem



Walinzi wa bunge la IsraelImage copyright
Image captionWalinzi wa bunge la Israel wabeba jeneza lenye maiti ya Bw Peres
Viongozi mashuhuri duniani wamemsifu rais wa zamani wa Israel Shimon Peres, ambaye amezikwa leo siku tatu baada yake kufariki akiwa na umri wa miaka 93.
Waziri Mkuu wa israel Benjamin Netanyahu amemweleza kama "mtu muhimu kwa dunia".
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwepo kwa kiongozi wa Wapalestina Mahmoud Abbas katika mazishi hayo ni ukumbusho wa "shughuli ambayo haijakamilishwa ya kutafuta amani".
Bw Abbas amekuwa miongoni mwa wageni mashuhuri kutoka nchi za nje waliohudhuria mazishi hayo Jerusalem.
Usalama uliimarishwa na polisi wanasema watu kadha walikamatwa.
Akihutubu wakati wa mazishi hayo, Bw Netanyahu amesema ingawa Israel na dunia yote kwa jumla watu wanamuomboleza Peres, ameacha matumaini duniani.
"Shimon aliishi maisha yenye lengo," amewaambia waombolezaji katika makaburi ya Mlima Herzl, Jerusalem.
"Alipanda na kufikia makuu. Aligusa wengi kwa maono yake na tumaini. Alikuwa mtu humo kwa Israel. Alikuwa mtu muhimu kwa dunia."
'Mwenye kuota zaidi'
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, aliyesaidia kufanikisha mikataba ya amani ya Oslo kati ya Israel na Wapalestina mapema miaka ya 1990 jambo lililopelekea Shimon Peres kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel, amesema kiongozi huyo alikuwa Mwisraeli "mwenye kuota zaidi".
"Alifikira sana mambo ambayo wengine wetu tungefanya. Alianza maisha kama mwanafunzi mwerevu zaidi wa Israel, alikuwa baadaye mwalimu wake bora zaidi na baada ya hapo mtu mwenye kuota zaidi."

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuImage copyright
Image captionWaziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Rais Barack Obama amemlinganisha Bw Peres na watu wengine mashuhuri wa karne ya 20 ambao amesema alifanikiwa kukutana nao. Wengine amesema ni Nelson Mandela na Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Bw Obama pia amemtaja Bw Abbas ambaye ameonekana kupeana mkono na kuzungumza kwa muda mfupi na Bw Netanyahu. Mara ya mwisho wawili hao kukutana hadharani ilikuwa 2010.
Juhudi za kutafuta amani zilitishwa Aptili 2014.
Bw Abbas alikuwa mmoja wa washiriki wa mazungumzo ya amani upande wa Palestine Liberation Organisation (PLO), mjini Oslo na ndiye aliyetia saini mkataba huo mwaka 1993.
Afisa mmoja mkuu wa Wapalestina ameambia shirika la habari la AP kwamba alitaka kutuma ujumbe mzito kwa Waisraeli kwamba Wapalestina wanataka amani na wanafurahia juhudi za wapenda amani kama vile Shimon Peres.

Shimon Peres (kushoto) Mahmoud Abbas (kati) na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Misri Amr Moussa miezi michache baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa OsloImage copyright
Image captionShimon Peres (kushoto) Mahmoud Abbas (kati) na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Misri Amr Moussa miezi michache baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa Oslo
Msemaji wa Hamas, kundi la Wapalestina lenye msimamo mkali ambalo hutawala Gaza, alikuwa amemtaka Bw Abbas "kutohudhuria mazishi ya mhalifu Shimon Peres".
Bw Peres hulaumiwa kutokana na urushaji wa mabomu 1996 katika eneo la Qana kusini mwa Lebanon ambao ulisababisha vifo vya watu 100 waliokuwa wametafuta hifadhi kambi ya Umoja wa Mataifa.

Ulinzi mkali umewekwa mjini JerusalemImage copyright
Image captionUlinzi mkali umewekwa mjini Jerusalem
Bw Barack Obama akihudhuria mazishi hayoImage copyright
Image captionBw Barack Obama akihudhuria mazishi hayo
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ambaye alisaidia kupatikana kwa Mkataba wa amani wa OsloImage copyright
Image captionRais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ambaye alisaidia kupatikana kwa Mkataba wa amani wa Oslo
Mwanamfalme Charles wa Uingereza na Rais Francois Hollande wa UfaransaImage copyright
Image captionMwanamfalme Charles wa Uingereza na Rais Francois Hollande wa Ufaransa

Wageni mashuhuri waliohudhuria:
  • Barack Obama, Rais, Marekani
  • Bill Clinton, rais wa zamani, Marekani
  • Mwanamfalme Charles, Uingereza
  • Boris Johnson, Waziri wa mambo ya nje, Uingereza
  • Tony Blair, waziri mkuu wa zamani, Uingereza.
  • Malcolm Turnbull, Waziri Mkuu, Australia
  • Justin Trudeau, Waziri Mkuu, Canada
  • Donald Tusk, Rais, Baraza la Umoja wa Ulaya
  • Francois Holland, Rais, Ufaransa
  • Joachim Gauck, Rais, Ujerumani
  • Matteo Renzi, Waziri Mkuu, Italia
  • Jenerali Nakatani, waziri wa zamani wa ulinzi, Japan
  • Jawad Anani, waziri wa ngazi ya juu, Jordan
  • Enrique Pena Nieto, Rais, Mexico
  • Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu, Nato
  • Mark Rutte, Waziri Mkuu, Uholanzi
  • Valentina Matviyenko, spika, bunge la juu, Urusi
  • Mfalme Felipe VI, Uhispania
  • Ban Ki-moon, Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa

Shimon Peres alikuwa nani?

  • Alizaliwa 1923 Wisniew, Poland, eneo ambalo sasa hufahamika kama Vishneva, Belarus
  • Alichaguliwa kwenye Knesset (Bunge la Israel) mara ya kwanza mwaka 1959
  • Alihudumu katika serikali 12, mara moja kama rais na mara mbili kama waziri mkuu.
  • Alitazamwa kama mpenda vita miaka yake ya awali - aliongoza mashauriano ya kuitafutia silaha Israel ilipokuwa bado taifa changa
  • Alikuwa kwenye serikali iliyoidhinisha sera ya kujengwa kwa makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina yaliyotekwa na Israel
  • Hata hivyo, alitekeleza mchango muhimu katika kupatikana kwa Mkataba wa Amani wa Oslo, mkataba wa kwanza kati ya Israel na Wapalestina, uliosema wangefanya juhudi "kuishi kwa amani pamoja".
Chanzo:BBC SWAHILI

Rodrigo Duterte asema "anafurahia kuua" sawa na alivyofanya Hitler

Rodrigo Duterte akiwa Davao


Image copyrigh
Amesema anaweza kuua walanguzi wengi wa dawa hizo za kulevya sawa na alivyofanya Hitler akiua Wayahudi.
"Hitler aliua Wayahudi milioni tatu ... kuna waraibu milioni tatu wa dawa za kulevya. Ninaweza kufurahia sana kuwaua," amesema.
Wayahudi zaidi ya milioni sita waliuawa na Wanazi chini ya Hitler.
Bw Duterte amekuwa akiongoza kampeni kali ya kuua walanguzi na watu wanaotumia dawa za kulevya tangu achukue madaraka mwezi Juni.
Takwimu rasmi zinaonesha watu zaidi ya 3,000 wameuawa kwenye operesheni za polisi au na makundi ya kiraia.
Miili ya waliouawa huachwa hadharani, ikiwa na mabango yaliyoandikwa makosa waliotuhumiwa kutekeleza.
Rais huyo awali amesema anaweza kufurahia sana "kuua wahalifu 100,000" kupunguza viwango vya uhalifu Ufilipino.
'Maneno ya kukera'
Bw Duterte alikuwa akiongea Davao, mji ambao alikuwa meya zamani ambapo alitekeleza sera kali ya kuunga mkono makundi ya kuua wahalifu.


Manila, 21, Agosti 2016Image copyrig
Image captio

Ameambia wanahabari kwamba amekuwa akioneshwa na baadhi ya wakosoaji wake kama "binamu wa Hitler".
"Hitler aliua Wayahudi milioni tatu, kuna waraibu milioni tatu. Ninaweza kufurahia sana kuwaua," amesema.
"Angalau Ujerumani walikuwa na Hitler. Wafilipino hawawezi."


Rodrigo Duterte akibusu bendera Manila (7 Mei 2016)Image copyright

Amesema angependa sana "kumaliza tatizo hilo nchini mwangu na kuokoa vizazi vijavyo".
Matamshi yake yameshutumiwa na makundi ya Wayahudi, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Thursday, September 29, 2016

test

test

Friday, September 23, 2016

Watoto wa Tanzania wana afya nzuri ya maungo duniani

Watoto wa Tanzania wana afya nzuri ya maungo kuliko wenzao duniani Taifa la Tanzania ndilo lenye watoto wenye afya nzuri ya maungo duniani, kulingana na utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Australia. Viwango vya afya ya maungo ya watoto milioni 1.1 walio kati ya umri wa miaka tisa hadi 17 kutoka mataifa 50 vilifanyiwa ukaguzi. Watoto hao walifanyiwa zoezi la kukimbia umbali wa mita 20,ambalo hukagua afya yao ya maungo. Grant Tomkinson, mmoja ya watafiti wakuu wa chuo cha Kusini mwa Australia ameiambia BBC kwamba watoto wa Tanzania waliibuka washindi kutokana na utendaji wao.

Wakristo na Waislamu waonyesha umoja Kibera Kenya

Makanisa na misikiti katika kitongoji duni cha kibera jijini Nairobi yanapata umbo jipya, baada ya kupakwa rangi ya manjano kama ishara ya umoja na uwiano baina ya waislamu na wakristo. Mradi huo unaoendelezwa katika kitongoji duni cha kibera mjini Nairobi, ambacho ndiyo mojawapo ya mtaa mkubwa wa mabanda barani Africa, unalenga kuangamiza dhana ya ubabe wa kidini, unaosababisha mivutano na ugaidi miongoni mwa vijana kwa misingi ya dini. Mradi huo, colour-in-faith unatumia sanaa kubadilisha jamii, na lengo la waasisi ni kuusambaza kote nchini Kenya. Kasisi Albert Loresha aliyeongoza zoezi la kupaka rangi anasema, ulikuwa wakati wa kufahamiana kati ya waislamu na wakristo, wakati wakipaka kuta za kanisa hilo rangi. Kanisa la Kianglikana, lango lake na pia kuta, zimepakwa rangi ya manjano. Kuta za msikiti pia zimepakwa rangi ya manjano, zoezi lililofanywa na wakristo. Wakaazi wa Kibera wakishirikiana katika kupaka rangi mskiti Kibera kuonyesha umoja kati ya uislamu na ukristoImage Wakaazi wa Kibera wakishirikiana katika kupaka rangi mskiti Kibera kuonyesha umoja kati ya uislamu na ukristo Katika mtaa wa Kibera, umaskini ukosefu wa usalama na pia mivutano baina ya waumini wa dini tofauti hushuhudiwa mara kwa mara. Kuna misikiti 14, na takriban kanisa mia saba. Imamu Yusuf Nasur Abu Hamza, ''wakati mwingine waislamu huwa wanahisi kama wakristo wanapendelewa na serikali''. Msimamizi wa mradi huu Nabila Alibhai anasema, kuwashawishi viongozi wa kidini kushiriki katika mradi huu, halijakuwa jambo rahisi, haswa kutokana na ukiritimba wa kamati za maeneo ya ibada.

Wednesday, September 21, 2016

Magufuli avunja bodi ya udhamini wa pensheni Tanzania

Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof Hasa Mlawa na kuvunja bodi ya udhamini wa mfuko huo. Taarifa kutoka ikulu imesema uamuzi huo utaanza kutekelezwa mara moja. "Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF utafanywa baadaye," taarifa hiyo imesema.