Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 5, 2016

Lutherans and Mennonites forge closer relations in practical ways

Lutherans and Mennonites are discovering practical ways of forging closer relations in their mutual commitment to deepen the healing and reconciliation they expressed six years ago, states a recent report, Bearing Fruit. The Lutheran World Federation (LWF) Task Force that followed up on the “Mennonite Action” at the July 2010 Assembly developed the report. The reconciliation action at the Eleventh Assembly in Stuttgart, Germany, was the outcome of the international dialogue between Lutherans and Mennonites, which was preceded by discussions at national level, dating back to the 1980s in France and Germany. The LWF Council endorsed the report of the task force at its June meeting, and recommended it to the member churches for study. Bearing Fruit says LWF’s action of asking Mennonites for forgiveness has given “rise to new forms of cooperation” and become “a source of inspiration for further joint study, celebration, reconciliation services and joint diaconal projects.” It reiterates the Lutheran communion’s commitment to its prayer for “forgiveness from God and from our Mennonite sisters and brothers” for the persecution of Anabaptists during the 16th century Reformation and for the “healing of memories and reconciliation” toward the future. The report is organized in three major parts. The first chapter focuses on how the reconciliation action affects the hermeneutic interpretation of the Lutheran Confessions and Confessio Augustana (CA) in particular. Chapter 2 elaborates on unresolved issues, such as the question of how Christians should relate to civil state and the use of lethal force, and how these can be explored in an atmosphere of mutual openness and willingness to learn from each other. The third chapter describes joint initiatives that were directly inspired by the Stuttgart Assembly action.

Mji wa Medina washambuliwa

Mripuko mkubwa umetokea katika mji wa Medina nchini Saudi Arabia,shuhuda wa tukio hilo anaeleza kwamba mtu aliyejitoa muhanga alifyatua kitufe cha kujilipulia karibu na msikiti mkubwa wa Mtume, ambapo msikiti huo ni mmoja wapo ya eneo takatifu kwa Waislamu. Kituo cha runinga mjini Saudia kilionesha picha za moto mkubwa uliokuwa ukiwaka kwenye maegesho ya magari huku magari yakiteketea na mwili mmoja wa binaadamu ulionekana karibu yake. Mpaka sasa hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali ya Saudi Arabia kuhusiana na tukio hilo,tukio jingine limetokea huku mtu mwingine wa kujitoa muhanga akiwa amejiripua katika msikiti wa madhehebu ya Shia upande wa Mashariki mwa mji wa Qatif, na mripuko wa tatu umetokea karibu na ubalozi wa Marekani mjini Jeddah. Askari wawili wa kulinda usalama wamejeruhiwa katika mojawapo ya matukio hayo.Mpaka wakati huu hakuna taarifa zozote kuhusiana na kundi lililo husika kupanga na kutekeleza mashambulizi hayo .Lakini kumekuwa na wasi wasi huenda wapiganaji wa Islamic State wakawa wanahusika. Kumekuwa na shutuma kuwa utawala wa Saudia kuwa sio wa halali na ambapo wamekuwa wakiiushambulia ufalme huo mara kwa mara katika siku za nyuma.

Sayari ya Juno yaikaribia Jupita

Ile Setelite ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda katika sayari ya Jupita sasa inakaribia kufika kwenye sayari hiyo.Wanasayansi wanakadiria setelite hiyo itafika muda mfupi ujao majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za afrika mashariki. Setilite hiyo kama itafanikiwa kufika ilipokusudiwa kwenye sayari hiyo inatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi ilivyoumbwa.

Monday, July 4, 2016

Shambulio la kujitoa mhanga Jedda

Taarifa kutoka nchini Saudi Arabia zinasema kuwa mshambuliaji wa kujitolea mhanga amejilipua karibu na tawi la ubalozi wa marekani katika mji wa Jedda. Ripoti zinasema kwa ni mshambuliaji tu aliyeuawa lakini baadhi ya taarifa zinasema kuwa walinzi wawili walijeruhiwa na shambulizi hilo. Shambuli kwenye tawi la ubalozi wa marekani mjini Jedda mwaka 2004 lilisababisha vifo vya watu 10. Utawala nchini Kuwait unasema umetibua mashambulizi matatu yaliyokuwa yamepangwa na kundi la Islamic State likiwemo lililokuwa limelenga msikiti wa washia. Wizara wa mambo ya ndani inasema kuwa idara za ulinzi ziliendesha oparesheni tatu ndani ya Kuwait na nje, ambapo watu kadha walikamatwa. Mwaka uliopita mshambuliaji wa kujitolea mhanga raia wa Saudi Arabia aliwaua watu 27 wakati alijilipua ndani ya msikiti wa washia nchini Kuwait.

Uingereza kuvutia makampuni ya biashara

Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ameeleza mipango ya wizara yake yenye lengo la kupunguza kodi muhimu ya faida katika biashara. Hatua ya Osborne ni sehemu ya mkakati wa kiuchumi katika harakati za kuvutia uwekezaji mpya, na hii inafuatia kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo iliamua Uingereza isite kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya. Osborne aliliambia gazeti la Financial Times kwamba anataka kupunguza kodi ya shirikishi kutoka asilimia ishirini hadi chini ya asilimia kumi na tano.mwandishi wa BBC wa masuala ya biashara ameeleza kwamba kura ya maoni ilikuwa ni mkakati wa kuisaidia Uingereza kuvutia uwekezaji kutoka kwa kampuni mbali mbali mpango ambao inawezekana haukufanikiwa kufuatia kura hiyo ya maoni

Mamia waandamana kupinga mauaji Kenya

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wanataka waliohusika waadhibiwe Mamia ya watu wameandamana jijini Nairobi, Kenya kupinga mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutekelezwa na maafisa wa usalama nchini humo. Maandamano hayo yamefanyika kufuatia kupatikana kwa miili ya wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri. Bw Kimani na Bw Mwenda walikuwa wameabiri gari la Bw Muiruri baada ya kuhudhuria kesi katika mahakama ya Mavoko 23 Juni, walipotekwa na watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa usalama. Inadaiwa walizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi wa utawala cha Syokimau. Miili yao ilipatikana katika mto wa Ol Donyo Sabuk, jimbo la Machakos, mashariki mwa jiji la Nairobi, ikiwa imefungwa mkono na ikionekana kuwa na ishara za majeraha. "Mauaji ya vijana hawa watatu yanafaa kumtia wasiwasi Rais Kenyatta," amesema Bw George Kegoro, mkurugenzi mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Tume ya Haki za Binadamu Kenya. "Kiongozi wa nchi ni sharti aunde jopo la uchunguzi kuhusu kutekwa na kutumiwa vibayakwa idara za polisi na rasilimali zake kwa manufaa ya watu binafsi na katika kutekeleza uhalifu ikiwa ni pamoja na, katika kisa hiki, mauaji ya kiholela." Hauhitaji Media PlayerPata usaidizi kuhusu Media PlayerBonyeza 'Enter' kuendelea au kurejea mwanzoni Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) kimewashauri wanachama wake kususia shughuli za mahakama kulalamikia kuuawa kwa wakili mwenzao, Bw Kimani. Waandamanaji wameanzia msafara wao eneo la Freedom Corner, uwanja wa Uhuru Park na kupitia katikati mwa jiji ambapo watafika pia makao makuu ya polisi na makao makuu ya idara ya mahakama. Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wanataka Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet na Waziri wa Usalama Joseph Nkaissery wajiuzulu. Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia visa vya ukatili wa polisi dhidi ya raia Kenya la IMLU, mwaka 2015 watu 125 waliuawa kiholela na maafisa wa polisi. Kati ya Januari na Aprili mwaka huu, watu 53 tayari wameuawa kwa mujibu wa IMLU. Maafisa watatu wa polisi waliotuhumiwa kuhusika katika kutoweka kwa Bw Kimani, Bw Mwenda na Bw Muiruri wamekuwa wakizuiliwa na walitarajiwa kufikishwa kortini leo.

Magufuli: AirTanzania kupaa tena kufikia mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa shirika la ndege la Tanzania litarejea angani ''kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016''. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ya Tanzania bw Gerson Msigwa ''Dkt. Magufuli amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti za kulifufua shirika la ndege la Taifa. Tayari mipango imefanywa kuhakikisha ndege mbili aina Bombadier Q400 zinanunuliwa na zitatua hapa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016.'' taarifa hiyo inaeleza. Tamko hilo ni ishara nzuri kwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania na vilevile kanda nzima ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikikabiliwa na gharama za juu za usafiri kutoka kwa mashirika ya kigeni. BIASHARA NA RWANDA Wakati huohuo rais Magufuli aliueleza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Rwanda kuwa China imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga reli ya kisasa yaani “Standard Gauge” kwa nia ya kurahisisha uchukuzi wa mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kwa manufaa ya wafanyabiashara. ''Tanzania imeamua kuipatia Rwanda eneo la kujenga bandari kavu kwa ajili ya mizigo ya wafanyabiashara wake na pia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itafungua ofisi mjini Kigali nchini Rwanda ikiwa ni juhudi za kurahisisha na kuongeza biashara kati ya nchi hizi mbili.'' Juhudi hizo bw Magufuli anasema ni kuwahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa bandari ya Dar es salaam ni salama kwao kupitisha mizigo na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha bandari hiyo na kurahisisha biashara kati ya nchi hizi mbili. Kwa upande wake rais Paul Kagame wa Rwanda alitoa wito kwa ''Tanzania na Rwanda pamoja na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana na sekta binafsi katika kutumia fursa nyingi za kibiashara zilizopo baina yake na kuwaletea manufaa wananchi''.

Saturday, July 2, 2016

Mahujaji Waislamu kuvalishwa bangili za kielektroniki

Saudia inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea Mecca kwa Hajj ya mwaka huu ambalo ni kongomano kubwa la Waislamu kutoka kote duniani. Hatua hiyo inafuatia mkanyagano uliotokea mwaka uliopita ambapo zaidi ya mahujaji 750 wanaaminikia kuuawa huku wengine 900 wakijeruhiwa. Bangili hizo zitakuwa na habari za kibinafsi za kila hujaji pamoja na zile za matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji hao. Takriban kamera 1000 pia zimewekwa. Bangili hiyo ya utambulisho itukuwa na habari muhimu kama vile pasipoti na anwani lakini pia zitatoa habari kwa mahujaji kama vile mda wa ibada pamoja na lugha tofauti kuwasaidia wale wasiozungumza lugha ya Kiarabu wakati huo. Bangili hizo zitakuwa haziingii maji na zitaunganishwa na programu ya ramani.

Mwanamke kujifungua 'mjukuu wake'

Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakanani na kuruhusiwa kufanya hivyo. Mwanamke huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya bintiye kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa. Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mamake amzalie watoto wake. Lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita. Hata hiyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu. Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28. Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliawaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.

Watu sita wauawa kwenye mabasi Mandera, Kenya

Watu wawili waliuawa baada ya basi jingine kushambuliwa Desemba 2015 Watu sita wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia mabasi mawili eneo la Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya. Vyombo vya habari nchini humo vinasema watu wawili walifyatulia risasi mabasi hayo yaliyokuwa kwenye msafara. Watu Zaidi ya 20 wamejeruhiwa. Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi anasema shambulio hilo limetokea siku moja tu baada ya Marekani kutoa tahadhari mpya kwa raia wake kuhusu usalama baadhi ya maeneo ya Kenya. Serikali ya Kenya ilikuwa imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mashambulio ya kigaidi huku mfungo wa mwezi wa Ramadhan ukikaribia kumalizika. Kamati ya usalama katika jimbo la Mandera ilikuwa pia imewaonya watu wasio wa asili ya Kisomali dhidi ya kusafiri eneo hilo kwa kutumia barabara wiki hii. Shambulio hilo la Ijumaa ndilo la tatu kutekelezwa kwenye mabasi ya uchukuzi wa umma Mandera. Desemba mwaka jana, watu wawili waliuawa baada ya basi kushambuliwa na watu wenye silaha. Abiria Waislamu waliwakinga wenzao Wakristo dhidi ya wanamgambo hao waliotaka kuwatenganisha wasafiri hao kwa msingi wa dini. Novemba 2014 watu wenye silaha waliua abiria 28 walioshindwa kukariri fungu la Koran. Eneo la Mandera limekuwa likishambuliwa sana na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabaab kutoka Somalia. Watu zaidi ya 60 wameuawa katika mashambulio yaliyotekelezwa na kundi hilo eneo hilo katika kipindi cha miaka miwili.

Uganda yavunja mkataba na kampuni ya Urusi

Park Geun-hye alizuru Uganda mwezi Mei Serikali ya Uganda imevunja mkataba wake na kampuni ya Urusi kuhusu mpango wa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta. Serikali ilikuwa imekamilisha mazungumzo na kampuni hiyo ya Rostec Global Resources Consortium. Lakini inasema baadaye kampuni hiyo ilianza kuongeza masharti mengine hata baada ya makubaliano ya mwisho kufikiwa. Uganda kukata uhusiano na Korea Kaskazini Mkataba huo sasa umekabidhiwa kampuni ya SK Engineering kutoka Korea Kusini. Kampuni hiyo iliibuka ya pili katika shughuli ya kutoa zabuni. Hatua hiyo imejiri wiki chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kuzuru Uganda.