Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, May 28, 2016

Bomu Uganda 2010: Wahusika wafungwa maisha Jela

Watu 5 waliopatikana na hatia ya mashtaka ya ugaidi kufuatia shambulio la bomu la mwaka 2010 katika mji mkuu wa Uganda Kampala ambalo liliwaua watu 74 wamepewa hukumu ya kifungo cha maisha jela. Miongoni mwao ni Issa Ahmed Luyima ,mpangaji mkuu wa mashambulio hayo yaliodaiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi la al-Shabab. Watu wengine wawili waliopatikana na hatia ya ugaidi walipatiwa hukumu ya kifungo cha miaka 50 jela. Akitoa hukumu hiyo,jaji Alfonse Owiny-Dollo alisema hakuamini kwamba hukumu ya kifo itazuia visa kama hivyo. Kupatikana kwao na hatia ni mara ya kwanza kwa washukiwa wa kundi la wapiganaji wa al-Shabab nje ya Somalia. Watu wengine sita ambao pia walishtakiwa waliachiliwa kwa mashtaka ya ugaidi na mauaji ,lakini mmoja wao alipatikana na hatia ya shtaka la kiwango cha chini.

Friday, May 27, 2016

Obama rais wa kwanza Mmarekani kuzuru Hiroshima

Rais wa marekani Barrack obama atakuwa rais wa kwanaza wa taifa hilo kuzuru mji wa Hiroshima nchini Japan hivi leo, eneo la mlipuko wa bomu la kwanza la atomiki duniani. Rais Obama anatarajiwa kuweka shada la maua katika eneo hilo, kuwakumbuka watu 140,000 walioaga dunia, kutokana na shambulizi hilo lililotekelezwa na marekani.

Viongozi wa G7 kuimarisha uchumi wa dunia

Viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani maarufu kama G7, wanasema uimarishaji wa uchumi duniani ni swala linalofaa kupewa kipau mbele. Katika taarifa kwa vyombo vya habari baada ya mkutano wa viongozi hao nchini Japan, G7 imeahidi kuhakikisha kuwa masoko ya kimataifa yamesalia kuwa wazi, na kuzuia mbinu zozote za ulinzi wa soko, dhidi ya ushindani wa masoko ya nje.

Trump apata wajumbe wa kutosha Marekani

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump amefikisha idadi ya wajumbe ya kupata uteuzi wa chama hicho kulingana na chombo cha habari cha AFP. Bw Trump ambaye aliwashinda wagombea wengine 16 wa chama hicho ameripotiwa kupata wajumbe 1,238 mmoja zaidi ya inavyohotajika. Chama cha Republican kinataraijiwa kukamilisha uteuzi wao katika mkutano wa chama hicho utakaofanyika huko Cleveland mnamo mwezi Julai. Iwapo atathibitishwa ,bw Trump atakabiliana na aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Hillary Clinton au seneta wa Vermont Bernie Sanders ambao wanashindania uteuzi wa chama cha Demokrat. Siku ya Jumatano,bilionea huyo wa New York alipanga kufanya mjadala na Bernie Sanders katika runinga mjini California kabla ya uchaguzi wa mchujo wa tarehe 7 mwezi Juni. Bw Sanders alikubali kushiriki katika mjadala huo katika ujumbe wake wa Twitter uliosema: ''Game on''.

Monday, May 9, 2016

'Malkia wa Pembe' afikishwa kortini Tanzania

Kesi dhidi ya mwanamke mfanyabiashara raia wa China anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandaoa wa kihalifu wa ulanguzi wa pembe barani Asia imeahirishwa kwa wiki mbili nchini Tanzania. Alifikishwa mahakamani Jumatatu asubuhi mjini Dar es Salaam. Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, aliendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia. Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa takriban miaka 14. Anakana mashtaka hayo. Mahakama imeambiwa kwamba faili ya kesi yake bado imo mikononi mwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Maafisa wa serikali Tanzania walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan mnamo Oktoba mwaka jana kama ufanisi mkubwa. Taifa hilo la Afrika mashariki limepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Jumba la ghorofa laporomoka Mombasa

Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre, yenye ghorofa sita, iliporomoka usiku wa kuamkia Jumatatu. Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa mkasa huo. Jumba la Nyali Centre huwa na kituo cha mazoezi na mgahawa maarufu. Polisi, maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) wamefika eneo hilo kufanya uchunguzi zaidi.

Saturday, May 7, 2016

Nendeni zenu, Uturuki yaifokea EU

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema serikali yake haitabadilisha sheria zake dhidi ya ugaidi kama masharti ya Muungano wa Ulaya ikiwa Uturuki inataka raia wake kuondolewa visa ya usafiri ndani ya Ulaya. Kwenye taarifa kwa runinga, kiongozi huyo alitoa maneno makali akisema kila mtu afuate njia yake, matamshi yaliyoonekana kuelekezwa kwa Muungano wa Ulaya. ''Tunachukua njia yetu nanyi chukeini yenu'',alisema Reccep tayyip Erdogan Bwana Erdogan amesema kwamba Uturuki inakabiliwa na tisho la ugaidi. Waziri mkuu, Ahmet Davutoglu aliyeongoza mazungumzo ya muafaka na Muungano wa Ulaya alitangaza kujiuzulu hapo Alhamisi baada ya kutofautiana na Rais. Kwenye hotuba hiyo Rais amesema atawasilisha mapendekezo ya kubadilisha mfumo wa utawala kutoka kwa Waziri Mkuu hadi Rais mwenye Mamlaka kupigiwa kura ya maoni.

Usitishaji mapigano Aleppo warefushwa kwa masaa 72

Usitishaji wa mapigano wa muda katika eneo la mapigano nchini Syria katika mji wa Aleppo umerefushwa kwa masaa mengine 72 kuanzia leo Jumamosi(07.05.2016),wakati mapigano yakiendelea upande wa kusini. Urefushaji wa kusitisha mapigano kwa ajili ya Aleppo unakuja wakati shutuma za kimataifa zinaongezeka kuhusiana na mashambulizi mabaya ya anga yaliyosababisha umwagikaji wa damu katika kambi kwa ajili ya watu waliokimbia makaazi yao kaskazini mwa Syria, ambayo serikali na mshirika wake Urusi wamekana kuhusika nayo. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema usitishaji huo tete wa mapigano umerefushwa "ili kuzuwia hali kuwa mbaya zaidi" dakika chache kabla ya usitishaji wa awali wa saa 48 kwa ajili ya mji huo kumalizika. "Hali ya utulivu katika jimbo la Latakia na mji wa Aleppo umerefushwa kutoka usiku wa manane Mei 7 kwa masaa 72," wizara ya ulinzi imesema katika taarifa. Marekani yathibitisha Marekani -- ambayo imekuwa ikifanyakazi pamoja na Urusi kuweka mbinyo kwa serikali kuzuwia ghasia na kufufua makubaliano ya kihistoria ya nchi nzima ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwezi Februari --- pia ilithibitisha kurefushwa huko. Watu wakipita katika vifusi vya majengo yaliyoshambuliwa mjini Aleppo "Wakati tunakaribisha urefushaji huu , lengo letu ni kupata kufikia mahali ambako hatutakuwa tunahesabu masaa na kwamba kusitishwa kwa uhasama kunaheshimiwa nchi nzima Syria," amesema msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani John Kirby. Jumuiya ya kimataifa ina matumaini kwamba kupungua kwa mapigano kunaweza kuimarisha mazungumzo yanayolegalega ya amani kumaliza miaka mitano ya vita ambavyo vimeuwa zaidi ya watu 72,000 na wengine milioni kadhaa kukimbia makaazi yao. Utulivu umerejea katika mitaa ya Aleppo baada ya kusitisha mapigano kuanza usiku wa manane siku ya Alhamis, na kuwapa wakaazi unafuu kidogo kutoka wiki mbili za mapigano ambayo yamesababisha kiasi ya raia zaidi ya 280 kuuwawa. Lakini kusini mwa mji huo, mapigano ya hapa na pale baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa Jihadi pamoja na washirika wao yamewauwa zaidi ya watu 70 kutoka kila upande, shirika linaloangalia haki za binadamu nchini humo limesema jana Ijumaa,(06.05.2016). Al-Nusra na washirika wao wapiganaji wa itikadi kali ya Kiislamu walikamata kijiji cha Khan Tuman na vijiji vinavyozunguka eneo hilo chini ya masaa 24, kwa mujibu wa shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Uingereza, baada ya majeshi yanayoiunga mkono serikali kuwafurusha kutoka eneo hilo mwezi Desemba. Wanawake na watoto wanaripotiwa kuwa miongoni mwa wale waliouwawa katika mashambulizi ya Alhamis katika kambi karibu na mpaka na Uturuki, ambapo pia watu 50 wamejeruhiwa. Mamun al-Kahatib , mkurugenzi wa shirika la habari linalounga mkono waasi mjini Aleppo, ameshutumu kile alichosema kuwa ni "ndege za utawala" kwa kushambulia kambi hiyo katika kijiji cha Al-Kammouna siku ya Alhamis -- shutuma ambazo serikali mjini Damascus inakana.

Friday, May 6, 2016

Kampuni ya simu ya Hong Kong yaingia katika soko la Afrika Mashariki

Kampuni ya simu kutoka Hong Kong limeamua kuingia kwenye soko la Afrika Mashariki. Kampuni hiyo kwa jina Zuri imebaini kuwa inashirikiana na ile ya Despec kuzindua simu za kisasa nchini Kenya, Tanzania na Uganda. Zuri inasema kuwa itazindua simu aina nne kwenye soko hilo. Simu hizo ni C41, C46, C52 na S56. Mkurugenzi mkuu wa Zuri, Vikash Shah, amesema kuna nafasi kubwa ya ukuaji katika eneo la Afrika Mashariki ambapo matumizi ya simu za kisasa (smartphones) yanaendelea kuongezeka. Simu ya C41 ina urefu wa inchi 4 yenye uwezo wa megabite 512 na inapatikana kwa rangi nyeusi na nyeupe. C46 ina urefu wa inchi 4.5 ikiwa na megabite 512 na kamera yenye uwezo wa Megapitzel 8. Simu ya C52 nayo ina urefu wa inchi 5 ikiwa na uwezo wa gigabite 1 na kamera ya megapitzel 8. Simu ilio kubwa kabisa ni ile ya S56 ilio na urefu wa inchi 5.5 na hyenye uwezo wa kuchuka sim card 2 kwa wakati mmoja na inayotumia mfumo wa Android 5.1 Lollipop. Mkurugenzi mkuu wa kampuni shirika ya Despec, Riyaza Jamal, amesema kuwa wana nia ya kuleta simu za kisasa kwenye soko la Afrika Mashariki ambazo ni tofauti na zingine zozote. Anasema mikakati ya mauzo iliowekwa na Zuri, pamoja na ujumbe unaoenezwa bila kusahau ubora wa bidhaa zao kwa pamoja zitachochea mauzo makubwa kwenye eneo hilo la Afrika Mashariki.

Rolling Stones wamtaka Trump kutocheza muziki wake

Wanamuziki wa The Rolling Stones wamemtaka mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Demokrat Donald Trump kuwacha kucheza muziki wao wakati wa kampeni zake za urais. Bendi hyo imetoa taarifa ikisema kuwa mgombea huyo wa uraisi hana ruhusa ya kucheza nyimbo zao na wametaka asitishe kufajnya hivyo mara moja. Bendi ya Rolling Stones haijatoa ruhusa kwa kampeni ya Trump kutumia nyimbo zao na sasa inaitaka kampeni hiyo kukoma kutumia muziki wake mara moja. Mgombea huyo amekuwa akicheza nyimbo hizo katika mikutano yake ya kampeni kwa miezi kadhaa sasa.Kibao chao kilichovuma mwaka 1969 ''You Cant Always Get What You Want'' kimekuwa maarufu. Bendi hiyo sio ya kwanza kutoa lalama kama hizo kwa nyota huyo wa runinga na mfanyibiashara. Mnamo mwezi Februari ,Adele alitoa taarifa akijiondoa katika uhusiano wowote na Trump baada ya kucheza muziki wa nyota huyo ''In The Deep'' katika mikutano yake. Mwanamuziki huyo alitoa taarifa akiweka wazi kwamba hajampatia ruhusa mgombea huyo kutumia muziki wake kwa kampeni zake za kisiasa.