Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, April 21, 2016

Malkia Elizabethi atimiza 90

Malkia Elizabeth ametimiza miaka tisini ya kuzaliwa.Malkia atasheherekea siku hii kwa kukutana na wananchi wake katika matembezi atayafanya huko Windsor. Malkia Elizabeth ametawala kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza, muda unaokadiriwa kufikia zaidi ya sitini na nne.

Somalia yazuia raia wake kwenda Sudan

Somalia inatazamia kuwazuia vijana ambao hufanya safari hatari kwenda Ulaya Somalia imewaambia raia wake kuwa hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchini Sudan, ambacho ni kituo maarufu kwa wahamiaji wanaosafiri kwenda Ulaya kinyume na sheria. Afisa mkuu wa uhamiaji Abdullahi Gafow, alisema kuwa wasomali ambao wataruhusiwa kusafiri kwenda Sudan ni wale wanaohusika na masuala ya kidiplomasia. Bwana Gafow alisema kuwa anatazamia kuwazuia vijana wa kisomali ambao hufanya safari hatari kwenda Ulaya. Mamia ya wahamiaji wengi wao rais wa Somalia, wanaripotiwa kufa maji mapema wiki hii wakati mashua yao ilizama katika bahari ya Mediterranean.

Vurugu zaendelea nchini Zambia

Polisi nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni. Watu Zaidi ya mia mbili na hamsini wamekamatwa baada ya maduka mengi yanayomilikiwa na wanyaruanda kuvamiwa.Uvamizi huo ulitokea baada ya wanyaruanda kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja. o Padre Charles Chilinda ameiambia BBC kuwa kanisa lake linafanya jitihada zote ili kuweza kuwasaidia wahanga ambao wamekwenda kuomba hifadhi kanisani. "Kitu ambacho tunaweza kuwapa ni kwamba watakuwa na usalama wa kutosha kuwa hapo,tutaenda kuwaangalia na kuwaeleza kuwa hawa sio wazambia ambao wanagombana nao.hali hii haikubaliki ,kila mtu aliyepo katika ardhi ya Zambia analindwa na katiba ya Zambia.Ni jukumu letu kudumisha Amani na tushirikiane katika kulitokomeza hili"

Monday, April 18, 2016

Mahakama Kuu ya Marekani kuamua hatima ya wahamiaji wasio na stakabadhi

Mahakama kuu ya Marekani leo inatathmini hatima ya takriban wahamiaji milioni 4 wakati majaji wanaposikiliza hoja za ufunguzi kwa kesi ya kihistoria inayopinga amri ya kiutendaji ya Rais Barack Obama kuhusu uhamiaji. Uamuzi wa mahakama hiyo utaathiri pakubwa amri za kiutendaji katika siku zijazo na unakuja wakati swala la uhamiaji linazungumziwa sana kwenye kampeni za mwaka huu. Kesi hiyo maarufu US vs. TEXAS imeiomba mahakama kutathmini iwapo Rais alivuka mamlaka yake ya kikatiba wakati alipotoa amri ya kutowarudisha makwao wahamiaji wasio na stakabadhi. Uamuzi wa kesi hiyo utaathiri maamuzi kwenye majimbo mengine 25 yanayopinga amri ya rais kuhusu uhamiaji.

Daraja la kisasa kuzinduliwa Kigamboni

Tanzania inatarajia kufungua daraja la kingamboni, daraja la ndefu zaidi Afrika Mashariki aina ya cable-stay kwa maana daraja linalobeba uzito kwa nyaya au kamba. Daraja hilo linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Rais John Pombe Magufuli kesho na kuunganisha mkondo wa kurasini jijini Dar es salaam hadi eneo la Kigamboni. Daraja hilo limegharimu zaidi dola milioni 140, na litachukua nafasi ya feri inayosafirisha watu na magari kati ya kigamboni na kivukoni upande wa mjini Dar.

Korea Kaskazini kulipua bomu la nyuklia

Korea Kaskazini ilifanyia majaribio bomu la haidrojeni Januari mwaka huu Korea Kusini imesema imepata dalili kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la tano la bomu la nyuklia, Rais Park Geun-hye amesema. Hakufafanua zaidi kuhusu dalili hizo, lakini ameagiza jeshi la nchi yake kuwa tayari, shirika la habari la nchi hiyo limesema. Kumekuwa na ripoti katika vyombo vya habari nchini Korea Kusini kwamba kumeongezeka shughuli katika kituo cha majaribio ya silaha za nyuklia cha Korea Kaskazini cha Punggye-ri, ambapo majaribio ya awali yalitekelezwa. Iwapo Pyongyang itaendelea na kufanyia majaribio bomu la nyuklia, basi itakuwa ni kukaidi zaidi vikwazo vikali ilivyoongezewa na Umoja wa Mataifa mwezi jana. "Tupo katika hali ya kutatanisha, hatujui iwapo Korea Kaskazini inaweza kufanya uchokozi kama njia ya kujitetea kutokana na kutengwa na jamii ya kimataifa na pia kuimarisha uungwaji mkono ndani ya nchi,” Bi Park aliambia maafisa wake wakuu wa jeshi, shirika la habari la Yonhap liliripoti. Korea Kaskazini yatishia kuishambulia Marekani Mhubiri wa Canada afungwa maisha Korea Kaskazini Mwezi Januari, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la nne la silaha za nyuklia na baadaye ikarusha kombora baharini. Hatua hiyo iliongeza hali ya wasiwasi katika rasi ya Korea. Waangalizi wanasema huenda jaribio hilo la bomu likafanywa kabla ya mkutano mkuu wa chama tawala cha Workers' Party mjini Pyongyang mwezi Mei. Wataalamu wanaamini Korea Kaskazini haina uwezo wa kiteknolojia wa kuweka silaha ya nyuklia kwenye kombora, ingawa imepiga hatua kubwa katika mpango wake wa nyuklia miaka ya karibuni.

Waliotarajia Mugabe aanguke waambulia patupu !

Afya ya rais Mugabe imekuwa ikidhohofika katika miaka ya hivi karibuni Je unaikumbuka picha hii ? Haya basi , Maafisa wa usalama wa kitengo cha kumlinda rais wa Zimbabwe Robert Mugabe walilazimika kumsogelea kwa karibu mno kiongozi huyo mkongwe katika tukio lililowaudhi raia wengi waliofika katika uwanja wa kitaifa jijini Harare kwani hata wenyewe hawakuweza kumtazama ''baba wa taifa'' Yamkini kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 92 aliingia katika uwanja wa kitaifa akiwa kwenye gari rasmi la Kijeshi Maafisa wa usalama wa kitengo cha kumlinda rais wa Zimbabwe Robert Mugabe walilazimika kumsogelea kwa karibu mno Hata hivyo baada ya kukagua gwaride la jeshi maafisa hao wa usalama walipanga kikamilifu njia ya kumstiri rais Mugabe asije akakungua na kuanguka kama ilivyokuwa mwaka uliopita Bw Mugabe alikuwa akiongoza taifa katika kuadhimisha miaka 36 ya uhuru kutoka kwa minyororo ya ukoloni. Rais Mugabe aliwaomba radhi wafanyikazi wa serikali waliostaafu kwa kuchelewa kupata malimbikizi ya marupurupu yao Bw Mugabe alikuwa akiongoza taifa katika kuadhimisha miaka 36 ya uhuru ''Bila shaka malipo yenu na mishahara ya siku za usoni itawafikia kwa muda ufaao'' alisema rais Mugabe. Mugabe aliwataka wazimbabwe waache ukabila na ufisadi iwapo wanaitaka Zimbabwe iimarike kiuchumi tena. Taifa hilo limekumbwa na udhaifu wa sarafu yake baada ya sera ya serikali ya kuwapokonya wakoloni wazungu mashamba na kisha kuyagawanyia waafrika weusi ambao ndio wengi kukosolewa vikali na mataifa ya magharibi yakongozwa na Uingereza.

Sunday, April 17, 2016

Papa Francis arejea na wahamiaji Vatican

Wahamiaji wakielekea kuabiri ndege iliyombeba Papa Francis Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewachukua wahamiaji 12 kutoka Syria na kwenda nao Vatican baada yake kutembelea wahamiaji katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki. Wahamiaji hao kutoka familia tatu wote ni Waislamu, na miongoni mwao kuna watoto sita. Nyumba za familia hizo zilishambuliwa kwa mabomu wakati wa vita nchini Syria. Vatican imesema kupitia taarifa kwamba Papa Francis amechukua hatua hiyo kuwaonesha wahamiaji kwamba wanakaribishwa. Maelfu ya wahamiaji kwa sasa wamekwama katika kisiwa cha Lesbos kufuatia mkataba wa mwezi jana kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki ambao unalenga kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya. Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu Papa Francis: Donald Trump 'si Mkristo' Kwa Picha: Maisha ya Papa Francis Wahamiaji wote walioondoka na Papa walikuwa tayari wanaishi Lesbos kabla ya mkataba huo kuanza kutekelezwa, Vatican imesema. Chini ya mwafaka huo baina ya EU na Uturuki, wahamiaji wanaofika kwa njia haramu katika visiwa vya Ugiriki kutoka Uturuki baada ya tarehe 20 Machi watakuwa wakirejeshwa Uturuki iwapo hawatafanikiwa kuomba hifadhi. Kwa kila mhamiaji wa Syria anayerejeshwa Uturuki, EU itampokea mhamiaji mwingine kutoka Syria aliyeko nchini Uturuki. Awali, Papa Francis aliambia wahamiaji wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Moria, baadhi wakikabiliwa na uwezekano wa kurejeshwa Uturuki, kwamba "hamjaachwa peke”.

Tetemeko la ardhi laua watu 77 Ecuador

Zaidi ya watu 77 wamefariki katika tetemeko la kubwa ardhi kuwahi kukumbwa Ecuador katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja . Makamu wa rais wa nchi hiyo ametangaza hali ya tahadhari katika mikoa sita nchini humo, huku maafisa wa huduma za dharura wamepelekwa kusaidia . Maafisa katika kituo cha Marekani cha utafiti wa kijiologia wamesema tetemeko hilo la ardhi lilikuwa la kiwango cha 7.8 kwenye vipimo vya Richter. Kitovu chake kilikuwa takriban kilomita 27 kutoka kwa mji wa pwani uitwao Muisne mji ambao kwa kawaida hauna wakaazi wengi. Taarifa katika mitandao ya kijamii nchini humo zaelezea jinsi mapaa ya majengo na hata baadhi ya madaraja na vivukio vya watembea miguu vilivyoporomoka kutokana na tetemeko hilo. Tetemeko hilo la ardhi lilikuwa la kiwango cha 7.8 kwenye vipimo vya Richter. Stephan Kuffner mwandishi habari anayeishi katika mji mkuu wa nchi hiyo Quito maili 200 kutoka eneo la tukio ameelezea jinsi watu walivyokimbilia kutoka nje ya majengo wakati ardhi ilipanza kutingisika.. Awali Kituo cha kutoa onyo la uwezeano wa kutokea mafuriko, Pacific Tsunami Warning Centre kimesema huenda kukawa na mawimbi makali yatakayoweza kufikia maeneo yaliyokilomita 300 kutoka mahali tetemeko hilo lilipotokea.

Barabara ya kwanza ya juu kujengwa Dar-es-Salaam

Mradi wa ujenzi ukizinduliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara Jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018. Sherehe ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika kando ya eneo la makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Mameya wa Jiji la Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida. Barabara hiyo ya juu itakuwa ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake umepangwa kugharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3. Barabara ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam. Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema barabara hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali yake ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam, ambao kwa mwaka 2013 pekee utafiti umeonesha ulisababisha upotevu wa shilingi Bilioni 411.55 Rais Magufuli amebainisha juhudi nyingine za kukabiliana na msongamano wa magari Jijini Dar es salaam kuwa ni pamoja na kujenga barabara ya njia sita ya Dar es salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na Flyover tano, ujenzi wa barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo na ujenzi wa daraja jipya la Salander lenye urefu wa kilometa 6.23 kuanzia Coco Beach hadi hospitali ya Agha Khan. Juhudi nyingine ni ujenzi wa awamu ya pili wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Kilwa, Chang'ombe na Kawawa, na ujenzi wa awamu ya tatu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Nyerere - Gongo la Mboto na Uhuru - Azikiwe. Aidha, Rais Magufuli amezungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, kuwa serikali yake imelazimika kusimamisha kuanza kwa huduma hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa mzigo mzito wa viwango vikubwa vya nauli, na amewahakikishia wananchi wa Dar es salaam kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika. Dkt. Magufuli pia amezungumzia usafi wa Jiji la Dar es salaam kwa kuwataka viongozi wa Manispaa zote za Jiji, kuhakikisha wanatafuta namna ya kudhibiti utupaji hovyo wa takataka ikiwemo kutoza faini kubwa kwa watakaokamatwa wakitupa takataka hovyo.

Friday, April 15, 2016

Wagonjwa 400 wa kansa Uganda kupelekwa Kenyan

Mashine pekee ya tibaredio nchini Uganda imeharibika Uganda imetangaza kwamba wagonjwa 400 wanaohitaji matibabu ya kansa watapelekwa Kenya baada ya mashine pekee ya kuwahudumia wagonjwa nchini humo kuharibika. Wagonjwa hao ni kati ya jumla ya wagonjwa 17,000 wanaohitaji huduma ya tibaredio. Waziri wa afya nchini humo Dkt Chris Baryomunsi aliambia bunge la nchi hiyo Alhamisi kwamba hospitali ya kibinafsi ya Aga Khan jijini Nairobi imejitolea kusaidia wagonjwa 400 kutoka Uganda wanaohitaji matibabu. Gazeti la kibinafsi la Daily Monitor, likinukuu maafisa wa serikali, linasema nchini Uganda kuna visa 32,000 vya kansa. Asilimia 55 (sawa na wagonjwa 17,600) wanahitaji huduma ya tibaredio. Mashine ya matibabu ya kansa Uganda yaharibika Kwa mujibu wa Dkt Baryomunsi, serikali itagharimia usafiri na malazi huku hospitali ya Aga Khan nayo ikigharimia matibabu. Mashine pekee nchini humo ilikuwa katika hospitali kuu ya Mulago ambayo ndiyo taasisi kubwa zaidi ya matibabu nchini Uganda na hushughulikia magonjwa makubwa. Mashine ya tibaredio iliyokuwa Mulago ambayo ni aina ya Cobalt 60 hutoa miali nururishi, yaani Radioactive, kuangamiza seli za saratani katika mwili wa mgonjwa. Ilinunuliwa mwaka wa 1995 na imekua ikiharibika mara kwa mara, licha ya kukarabatiwa.

Clinton na Sanders wajibizana vikali New York

Clinton amekuwa seneta New York naye Sanders ni mzaliwa wa jimbo hilo Wagombea urais waliosalia katika chama cha Democratic, Hillary Clinton na Bernie Sanders, wamejibizana vikali katika mdahalo uliofanyika katika jiji la New York. Kila mmoja ametilia shaka uwezo wa mpinzani wake kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala kama vile kudhibiti benki Wall Street, kudhibiti umiliki wa silaha na ujira wa chini. Jimbo la New York litafanya mchujo wake Jumanne. Bw Sanders amemkosoa Bi Clinton kwa kuunga mkono vita vya Iraq na kutetea mikataba ya biashara huru. Sanders amshinda bi Clinton huko Wyoming Lakini naye Bi Clinton amemtuhumu Bw Sanders na kusema hawezi kutekeleza hata sera zake mwenyewe, mfano kuvunja udhibiti wa benki kuu za Wall Street. Sanders ameshinda majimbo saba kati ya manane yaliyofanya mchujo karibuni Wote wawili wana uhusiano mkubwa na jimbo hilo la New York. Bw Sanders alizaliwa huko naye Bi Clinton amekuwa seneta wa jimbo hilo kwa miaka minane. Mdahalo huo wa runingani umefanyika eneo la Brooklyn. Bw Sanders ameshinda majimbo saba kati ya manane yaliyofanya mchujo karibuni jambo lililomuwezesha kupunguza uongozi wa Bi Clinton katika mchujo wa chama hicho. Clinton anajivunia uongozi mkubwa Bi Clinton hata hivyo bado anajivunia uongozi mkubwa. Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika mwezi Novemba.

Sudan Kusini kujiunga na Afrika Mashariki

Rais Magufuli ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anatarajiwa kutia saini mkataba wa kuiingiza rasmi nchi hiyo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Kiir atatia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo. Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita. Sudan Kusini yajiunga na Afrika Mashariki Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo baadaye. Sudan Kusini ilikubaliwa kujiunga na EAC mwezi uliopita Baada ya kujiunga rasmi leo, Sudan Kusini inatarajiwa kufungua mipaka yake kwa ajili ya biashara. Tayari kampuni na asasi nyingi za kifedha kutoka Kenya zimefungua vbiashara nchini Sudan Kusini. Wengi wanatarajia hatua ya leo itafungua fursa zaidi za kibiashara kati ya Sudan Kusini na nchi wanachama wa jumuiya. Wadadisi wengine wanaamini kuwa baadhi ya miradi ambayo Sudan Kusini ingetaka kujumuishwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miundo msingi ikiwemo reli na mabomba ya mafuta.

Magufuli amfuta kazi mhariri wa magazeti ya serikali

Dkt Magufuli amemteua Bi Abdallah kuwa kaimu Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw Gabriel Nderumaki. Bi Tuma Abdallah, ambaye amekuwa mhariri mtendaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN), ameteuliwa kuwa kaimu. Hakuna maelezo yoyote zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Bw Nderumaki. TSN huchapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, habari Leo, Habari Leo Jumapili na Spoti Leo.

Monday, April 11, 2016

Ukame walazimu treni ipeleke maji kilomita 300

Gari la moshi la dharura lililobeba lita nusu milioni ya maji inatarajiwa kuwasili Magharibi mwa India kukata kiu ya wenyeji wa eneo hilo lililokumbwa na ukame. Gari la moshi hilo linaloitwa ''Treni ya maji'' linavuta mabehewa 10 makubwa yaliyojaa maji. Mabwawa ya maji yaliyokuwa yanategemewa kwa uhifadhi wa maji yamekauka baada ya ukosefu wa mvua Hilo ndilo treni la kwanza kati ya mia zilizopangwa kupeleka maji Magharibi mwa India. Mabehewa 100 ya maji yatasafirishwa umbali wa kilomita 300 hadi Latur katika jimbo la Maharashtra Kusini. Jimbo hilo linakumbwa na ukame mbaya sana katika kipindi cha karne moja iliyopita. Mabehewa 100 ya maji yatasafirishwa umbali wa kilomita 300 hadi Latur katika jimbo la Maharashtra Kusini. Mabwawa ya maji yaliyokuwa yanategemewa kwa uhifadhi wa maji yamekauka baada ya ukosefu wa mvua kwa kipindi kirefu. Ukame huo umesababisha hata hospitali katika eneo hilo la Kusini kuahirisha operesheni ya wagonjwa kwa sababu ya uhaba wa maji.

Obama ajutia makosa ya Marekani nchini Libya

Rais Obama amekiri kwamba Marekani ilikosea katika kutatua mzozo Libya Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya. Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake. Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi. Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake. Eneo la Sirte, alikozaliwa Gaddafi, lilishambuliwa sana na majeshi ya muungano Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011. Bastola ya dhahabu ya Gaddafi ilienda wapi? Obama acheza densi ya tango Argentina Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti. Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida. Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.

Nyoka mkubwa zaidi duniani afa

Chatu huyo aliyepatikana katika eneo lililokuwa likijengwa nchini Malaysia karibu na mti mkubwa uliokatwa katika kisiwa cha Penang. Joka hilo linakisiwa kuwa takriban mita 8 hivi sawa na futi 26 lilipatikana siku ya Alhamisi iliyopita. Kwa bahati mbaya joka hilo lilikufa jumapili lilipokuwa likizaa. Chatu huyo aliyepatikana katika eneo lililokuwa likijengwa nchini Malaysia Afisa anayesimamia ujenzi katika kisiwa hicho cha Penang, Herme Herisyam aliiambia BBC. Kulingana na daftari za kumbukumbu za Guinness, joka anayeshikilia rekodi ya dunia anaurefu wa mita 7.67. Chatu huyo anayeitwa Medusa ana uzani wa kilo 158 na anaishi katika jumba moja mjini Kansas City, Missouri Marekani. Bw Herisyan anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250. Hata hivyo joka huyo wa Malaysia ambaye alikuwa mkubwa zaidi yake hakuwa amepimwa na kuthibitishwa kuwa mrefu zaidi kabla ya kufa kwake. Bw Herisyan anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250. Hata hivyo katika harakati za kumuokoa kutoka maficho yake inakisiwa kuwa aliumia na hivyo akafa kabla hajafikishwa kwenye hifadhi ya wanyama alikotarajiwa kutuzwa hadi ajifungue.

Watumishi hewa wamponza mkuu wa mkoa Tanzania

Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wafanye uchunguzi kuwatambua watumishi hewa Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa. Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa. Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza. Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini. Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa Abdul Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja. "Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema Dkt Magufuli. Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani.

Sunday, April 10, 2016

Mkuu wa kanisa Anglikana agundua babaake sio Welby

Kiongozi wa kanisa Anglikana duniani Justin Welby Kiongozi mkuu wa Kanisa la Kianglikana duniani, ametangaza kuwa babaake mzazi ambaye alikuwa anamfahamu sio yeye. Askofu huyo wa Cantebury, Justin Welby, amesema alifahamu mwezi uliopita kuwa babake mzazi alikuwa balozi wa Uingereza Sir Anthony Montague Browne, ambaye alifariki miaka mitatu iliyopita na wakati mmoja alihudumu kama msaidizi wa Sir Winston Churchil. Askofu huyo alikuwa akidhani Gavin Welby ambaye alifariki mwaka wa sabini na saba alikwa babake. Justin Welby ametaja habari hizo kama za kushangaza na alifanya majaribio ya DNA baada ya kupata habari hizo kutoka kwa gazeti moja nchini Uingereza. Matokeo yake yalifananishwa na yale yaliyopatikana katika nywele za babake.

Wasomali wa UK wakutana kupigana na Itikadi kali

Raia wa Uingereza walio na mizizi yao nchini Somalia wanakutana mjini Bristol mashariki mwa Uingereza kujadiliana kuhusu kuwazuia watu wa jamii hiyo kuwekwa itikadi kali. Waandalizi wanasema kuwa vijana wengi wa Kisomali kutoka Uingereza wamejiunga na makundi ya itikadi kali nchini Syria,Iraq na Somalia kwenyewe. Kundi la wapiganaji wa kisomalia al-Shabab huwaonyesha wapiganaji wake raia wa Kisomali katika hatua yake ya propaganda. Mkutano huo unawakutanisha wawakilishi wa jamii,makundi ya kidini wanaharakati na maafisa wa polisi.

Korea Kaskazini yaujaribu mtambo wake wa makombora

Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya mtambo wake mpya, ambao unaweza kurusha makombora kutoka bara moja hadi jiingine, katika juhudi za kuimarisha uwezo wake wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani. Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vinasema kuwa zoezi hilo liliongozwa na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un. Jaribio hilo ni katika harakati za hivi karibuni za utawala wa Pyongyang wa kuunda zana za nuklia tangu ilipofanya jaribio lake la nne la makombora ya nuklia January mwaka huu. Hatua hiyo iliiushurutisha Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa wito kwa utawala wa Pyongyang kujiepusha na vitendo vyake vya uchochezi.

Rais wa Zanzibar atangaza baraza la mawaziri

Hatimaye Rais wa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar ametangaza Baraza lake la Mawaziri akiwemo Hamad Rashid kutoka Chama cha Upinzani cha ADC. Hamad Rashid Mohamed aliwahi kuwa mwanachama machachari wa Chama cha Upinzani, CUF kilichosusia uchaguzi wa marudio kwa madai kuwa kiliporwa ushindi katika uchaguzi wa awali uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2015. Hamad Rashid alifukuzwa katika CUF akagombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change na kuambulia nafasi ya pili. Hata hivyo hakufikia asilimia 10 ya kura zote ili apate nafasi ya kuwa makamu wa kwanza wa rais kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar iliyopatikana baada ya mvutano mkubwa kati ya Chama cha CUF na CCM. Hii ndio Orodha ya baraza hilo la mawaziri: 1-ISSA HAJI USI GAVU-OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI. 2-HAROUNA ALI SULEIMAN-OFISI YA RAISI KATIBA,SHERIA,UTUMISHI WA UMMA. 3-HAJI OMAR KHERI-OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ. 4-MOHAMED ABOUD-OFISI YA MAKAMO WA PILI YA RAISI. 5-DR.KHALID SALUM MOHAMED-WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO. 6-MAHMOUD THABIT KOMBO-WAZIRI WA AFYA. 7-RIZIKI PEMBE-WAZIRI WA ELIMU. 8-AMINA SALUM ALLY-WAZIRI WA VIWANDA NA MASOKO 9-ALI KARUME-WAZIRI WA UJENZI,MAWASILIANO NA UCHUKUZI. 10-HAMAD RASHID-WAZIRI WA KILIMO MALIASILI MIFUNGO NA UVUVI. 11-RASHID ALI JUMA-WAZIRI WA HABARI, UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO 12-NURDIN KASTIKO-WAZIRI WA UWEZESHAJI,WAZEE,WANAWAKE NA WATOTO 13-SALMA ABOUD TALIB-MAJI, ARDHI,NISHATI NA MAZINGIRA. MANAIBU WAZIRI:- 1-HAROUS SAID SULEIMAN-AFYA 2-JUMA KHAMIS MAALIM-KATIBA 3-CHUM KOMBO-HABARI 4-LULU MSHAM KHAMIS-KILIMO 5-JUMA MAKUNGU JUMA-ARDHI 6-MOHAMED AHMED SALUM-UJENZI 7-MMANGA MJENGO MJAWIRI-ELIMU

Friday, April 8, 2016

Afisa wa Mbabazi ajitokeza, asema alijificha Tanzania

Bw Mbabazi alimaliza wa tatu katika uchaguzi uliofanyika 18 Februari Aliyekuwa meneja wa usalama wa kampeni ya waziri mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi ambaye alidhaniwa kwamba alifariki baada ya kutoweka miezi mitatu iliyopita amejitokeza. Bw Christopher Aine alijisalimisha kwa nduguye Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Salim Saleh. Bw Aine aliambia kituo cha runinga cha NTV cha Uganda kwamba amekuwa mafichoni jijini Dar es Salaam, Tanzania na kwamba aliamua kuondoka Uganda kutokana na wasiwasi uliotanda baada ya makabiliano ya Ntungamo tarehe 13 Desemba. Makabiliano hayo yalikuwa kati ya vijana waliovalia fulana za chama tawala cha NRM na waliokuwa wakiimba nyimbo za chama hicho na maafisa wa usalama wa Bw Mbabazi katika wilaya ya Ntungamo, magharibi mwa Uganda. Bw Aine alitoweka siku mbili baada ya makabiliano hayo. Mahakama yatupilia mbali kesi ya Mbabazi Uganda Besigye ashtakiwa kwa kuingia Kampala Amesema alijaribu kuwasiliana na Bw Mbabazi na Mkuu wa Polisi Jenerali Kale Kayihura ili wafanikishe kujitokeza kwake lakini hakufanikiwa kwa sababu aliacha simu zake nyumbani alipoondoka Tanzania. Serikali ya Uganda iliahidi zawadi ya shilingi 20 milioni za Uganda kwa mtu ambaye angetoa habari ambazo zingesaidia kupatikana kwake. Jenerali Saleh ameambia wanahabari kwamba Bw Aine atakaa nyumbani kwake yeye akiendelea na mashauriano na serikali kuhakikisha uhuru wake.

Ruto: Waathiriwa wa ghasia lazima wapate haki

Naibu wa rais nchini Kenya William Ruto amevihutubia vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu kesi iliokuwa ikimkabili kuhusiana na ghasia zilizotokea katika uchaguzi wa mwaka 2007 katika mahakama ya ICC ifutiliwe mbali. Ruto amesema kwamba serikali haitapumzika hadi waathiriwa wa gjhasia hizo ambapo takriban watu 1200 walifariki wapate haki yao. ''Sababu ambayo iliofanya kesi hiyo kuanguka ni kwamba hatukuwa na hatia''.

Simu mpya aina ya Smartphone zaingia Dar es Salaam

Kampuni ya Zuri ilio na makao yake mjini Hong Kong imezindua rasmi simu aina ya Smartphone katika soko la Tanzania.Kampuni hiyo pia imeisajili kampuni ya DESPEC kama msambazaji rasmi wa simu hizo nchini Kenya Tanzania na Uganda. Kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo,uzinduzi huo uliofanyika mjini Dar es Salaam siku ya Jumatano unamaanisha kwamba simu za smartphone za Zuri kama vile C41,C42,C52 na S56 zinapatikana nchini Tanzania. ''Tumeona kwamba kuna fursa nzuri ya bidhaa zetu Tanzania...tunawasihi raia wa Tanzania kujipatia simu zenye ubora ili kukwepa gharama zinazokuja na simu baada ya kununua mbali na maswala mengine ya kiafya yanahuhusishwa na simu zenye kiwango cha chini',afisa mkuu wa simu za Zuri Bwana Vikash Shah,amesema. Kulingana na The Citizen Tanzania,Mkurungenzi wa kampuni ya DESPEC Bw Riyaz Jamal anaamini kwamba kwa kuongeza Zuri katika soko la simu kutawasaidia raia wa Tanzania kupata simu zenye ubora na zilizo na bei ya chini. ''Wateja wanatafuta bidhaa za simu zilizo bora duniani,tunaamini kwamba Zuri itaturuhusu kupata mauzo mazuri nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla'',alisema Jamal.

Papa Francis kutoa tamko muhimu kuhusu ndoa

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo anatarajiwa kutangaza wazi msimamo wake kuhusu ndoa, njia za kupanga uzazi na malezi ya watoto. Tangazo hilo linatarajiwa kuwa kwenye ripoti ya mikutano miwili mikuu ya kutoa maamuzi kuhusu sera za kanisa hilo, maarufu kama sinodi. Wengi wanatumai kwamba ripoti hiyo itafungua njia kwa kanisa hilo kutoa sakramenti ya komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale waliooa tena, jambo ambalo wahafidhina katika kanisa hilo wamekuwa wakipinga. Ripoti hiyo ni matokeo ya kazi aliyoifanya Papa huyo kwa miaka mitatu. Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya kidini Caroline Wyatt anasema ripoti hiyo ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Apostolic Exhortation (Ujumbe wa Papa kwa Waumini) ni nyaraka yenye zaidi ya kurasa 200. Ripoti hiyo ya sasa imepewa kichwa The Joy of Love (Furaha ya Upendo). Baadaye, aliwaita maaskofu na makadinali kwa mikutano miwili ya sera za kanisa mjini Roma. Kwenye mkutano huo, aliwahimiza kujadiliana na hata kutofautiana kuhusu masuala ambayo hugawanya waumini wa kanisa hilo katika nchi nyingi. Masuala hayo ni pamoja na kutoa komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale walioolewa tena, njia za kupanga uzazi na pia Wakatoliki ambao ni wapenzi wa jinsia moja. Mwandishi wetu anasema ripoti hiyo itaonyesha wazi msimamo wa Papa Francis. Baadhi tayari wanasema itashangaza wengi, huku Papa akijitosa katika bahari ya mafundisho ya kanisa Katoliki kuhusu familia. Wahafidhina hawamtaki abadilishe imani na msimamo wa kanisa, lakini watu wenye msimamo huru wanatumai kwamba ataliambia kanisa liwe na huruma na kuwakumbatia wale watu walio kwenye familia wasiokumbatia kikamilifu mafundisho ya kanisa. Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu Papa: Uoga utawafanya Wakristo wafungwa Papa Francis aingia Instagram Baadhi katika kanisa Katoliki wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za kumruhusu padri au askofu kuamua faraghani kwa kuzingatia uzito wa kila kisa, iwapo Mkristo aliyepewa au kupeana talaka na kuoa au kuolewa tena anaweza kukumbatiwa kwenye kanisa na kuruhusiwa kupokea komunyo. Ingawa wale wanaotaka kanisa likumbatie mambo ya kisasa kama vile Kadinali Walter Kasper wa Ujerumani wanaunga mkono sera hii, wahafidhina wanasisitiza kwamba itadunisha uzito wa msingi uliowekwa na Yesu kwamba ndoa haiwezi ikavunjwa. Wakati wa kumalizika kwa sinodi ya mwaka jana, Papa Francis aliwakosoa viongozi wa kanisa aliosema wamelifumbia macho suala hilo na kusema kwamba kuendelea kusisitiza kuheshimiwa kwa mafundisho ya dini kikamilifu ni kukosa kutilia maanani dhiki wanayopitia watu wengine katika familia. Kwa Picha: Maisha ya Papa Francis Nyaraka hiyo ya papa inatarajiwa kutoa wito wa kuwepo kwa maandalizi mema zaidi kabla ya ndoa na pia kusisitiza mtazamo wa sinodi kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja haziwezi zikawekwa kwenye kiwango sawa na ndoa za watu wa jinsia tofauti.

Waumini KKKT Mufindi wahama Dayosisi wakimpinga Askofu

Dar es Salaam. Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini, Jimbo la Mufindi wametoa tamko la kuhamia Dayosisi ya Iringa kwa madai ya kuchoshwa na mgogoro wa siku nyingi baina yao na Askofu wao, Isaya Mengele. Mbali na mgogoro huo, tamko hilo lilidai kwamba hawawezi kuendelea kubaki Njombe kwa madai kuwa jimbo hilo linapaswa kuwa Iringa kulingana na mipaka ya kimikoa. Juzi, waziri wa zamani, Joseph Mungai aliandika barua kwa Mkuu wa KKKT, Dk Frederick Shoo akimwomba achukue hatua za haraka katika mambo matano likiwamo la kuzingatia hoja za Wakristo wa jimbo hilo anaodai wanatengwa na kunyanyaswa na Askofu Mengele. Akizungumza tamko hilo jana, Askofu wa KKKT Jimbo la Iringa, Dk Owdenburg Mdegela alisema amelipokea na ameamua kuwapokea kwa mikono miwili huku akiwasihi watulie kusubiri usuluhishi utakaofanywa na viongozi wa kanisa hilo. Akisimulia hali halisi, Dk Mdegela alisema Februari 26, waumini hao walitaka kuandamana hadi Arusha ili kumuomba Askofu Shoo aingilie kati mgogoro huo. Alisema kabla ya kufanya maandamano hayo, waumini hao walikwenda Iringa kumsihi awapokee jambo lililomfanya awatulize akiahidi kuzungumza na Askofu Mengele ili kumaliza tatizo lililopo. “Niliwaomba watulie, nikawasiliana na Askofu Mengele nikimsihi aumalize mgogoro huu kwa mazungumzo. Hata hivyo, mgogoro huu ni wa kihistoria na unahitaji hekima na maombi kuumaliza,” alisema Dk Mdegela. Alisema Machi 8 waumini hao walimfuata tena safari hii walimpelekea tamko kwamba wameamua kuihama dayosisi yao na kuhamia Iringa. Dk Mdegela alisema hatua ya waumini hao ilimuudhi Askofu Mengele ambaye aliamua kumfukuza kazi Mkuu wa Jimbo la Mufindi, Mchungaji Anthony Kipangula na hivyo kuwaudhi zaidi waumini. Mchungaji Kipangula alipopigiwa simu alikiri kuwapo kwa tatizo la muda mrefu baina ya waumini na Askofu Mengele. “Kwa sasa nipo Mwanza, hivyo sitaweza kuongea zaidi masuala ya jimbo japo mgogoro huu ni wa muda mrefu, waumini wanataka wahamishiwe Iringa na si kuendelea kuwapo Njombe,” alisema. Katika tamko lao, waumini hao walidai kuchoshwa na mgogoro huo na kwamba hawatatambua uongozi wa Askofu Mengele. Katiba barua yake, Mungai alimuomba Dk Shoo kuunda tume ili ichunguze mgogoro huo na kusikiliza pande zote mbili. Askofu Mengele alipopigiwa simu kuzungumzia tatizo hilo, alipokea lakini ilikatika na alipopigiwa tena haikupatikana.

Wednesday, April 6, 2016

MUNGAI ACHARUKA AMFIKISHA ASKOFU MENGELE KWA MKUU WA KKKT

KUHANI MKUU WA KKKT Salaam KATIKA Jina la Bwana wetu Yesu Kristo BAADA ya kushindwa kukupata kwa SIMU; NAJITAMBULISHA kwako KUWA mimi ni Joseph James Mungai MKRISTO wa KKKT Jimbo la Mufindi. Tumewahi kukutana. Nilipokuwa Waziri wa Elimu nilimuwakilisha Rais Mkapa kwenye Sherehe YENU ya KUMUAGA Baba Askofu Kweka. Nimewahi kuwa Mbunge wa Wilaya ya Mufindi miaka 35. Nimewahi pia kwa nyakati tofauti kuwa Waziri wa Kilimo; Waziri wa Elimu; & Waziri wa Mambo ya Ndani ya NCHI. Aidha nimewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Ndani ya Kanisa nimewahi kuwa Mjumbe wa Halmashsuri Kuu ya Dayosisi ya Kusini. Kama MKRISTO wa kawaida niliyewahi, kwa Rehema ya Mungu, kuwa katika uongozi wa Nchi na wa Kanisa; na aidha kama Mzee wa Miaka 72; NAKUSHAURI UCHUKUE HATUA BILA KUCHELEWA YA kufanya mambo matano (5) yafuatayo: (1) Uzingatie Hoja za WAKRISTO wanaoteseka wa Jimbo la Mufindi tunaotengwa na kunyanyaswa na Askofu Mengele wa Dayosisi ya Kusini: (2) Uunde bila kuchelewa zaidi Tume ya Kanisa kwenda kusikiliza Hoja za kila upande (3) Utambue kuwa kwa wakati huu wa mpito Jimbo la Mufindi baada ya kunyanyaswa na kutengwa na Askofu Mengele limejihifadhi chini ya ulezi wa Dayosisi ya Iringa; (4) Kwa hiyo basi UAGIZE kuwa Dayosisi ya Kusini kutokana na yenyewe kulitenga Jimbo la Mufindi katika VIKAO VYA UAMUZI imepoteza uhalali wa kuamua jambo lolote kuhusu Jimbo la Mufindi mpaka mgogolo uliopo uishe chini ya UONGOZI WA KANISA. Kwa hiyo uamuzi wa jana wa kumuvua Uchungaji & Ukuu wa Jimbo Mchungaji Kipangula ni batili hata kwa Akili ya KAWAIDA. (5) Kwa NIABA y a KKKT uelekeze RASMI kuwa kwa sasa kondoo wa Jimbo la Mufindi tulionyanyaswa na kutelekezwa na Askofu Mengele wa Dayosisi ya Kusini TUKO chini ya ulezi wa Baba Askofu MDEGELA wa Dayosisi ya Iringa (DIRA) na HALMASHAURI KUU ya Dayosisi hiyo. Kwa SHALOM na kwa Heshima Kuu Nawasilisha. Aidha nawakumbusha Maaskofu wangu miliongoze Kanisa kwa nguvu ya Biblia na SIYO kwa nguvu ya Polisi kama Dola. Wa Salaam katika Jina Kuu la Yesu Kristo Joseph J Mungai M K R I S T O WA KKKT JIMBO LA MUFINDI MKOA WA IRINGA Cc: Baba Askofu MDEGELA Dayosisi ya Iringa Cc: Baba Askofu Mengele Dayosisi ya Kusini Chanzo:www.matukiodaima.co.tz

Shinikizo laongezeka kumtaka Zuma ajiuzulu

Shinikizo la kumtaka Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ajiuzulu linazidi kuongezeka, licha ya bunge la nchi hiyo kupinga hoja iliyotolewa na upinzani ya kutokuwa na imani naye na kumtaka ajiuzulu. Muungano wa makanisa, wanataaluma pamoja na mashirika mengine, yameanzisha kampeni dhidi ya Rais Zuma, ambaye ameomba radhi na kukiri kosa baada ya mahakama ya juu ya Afrika Kusini kutoa uamuzi kuwa kiongozi huyo alikiuka katiba kwa kutumia mamilioni ya Dola, katika fedha za umma kwa ajili ya kuyafanyia ukarabati makaazi yake binafsi. Muungano huo umesema utajadili mipango yake baadae leo. Waziri wa zamani wa fedha wa Afrika Kusini, Trevor Manuel na Ahmed Kathrada, mwanaharakati mkongwe dhidi ya ubaguzi wa rangi na aliyekuwa rafiki wa karibu wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, wamemtaka Rais Zuma ajiuzulu wadhifa wake. Bunge la Afrika Kusini ambalo limetawaliwa na wanachama wa chama tawala cha African National Congress-ANC, hapo jana lilipiga kura kupinga hoja ya upinzani ya kumuondoa madarakani Rais Zuma, kutokana na kashfa ya rushwa iliyokuwa inamkabili. Wabunge 233 walipiga kura kupinga hoja hiyo, huku wabunge 143 wakipiga kura kuunga mkono hoja, kwa sababu hawana imani naye. Hakuna mbunge yeyote ambaye hakupiga kura. Hoja iliwasilishwa bungeni na chama cha upinzani Hoja hiyo ilipelekwa bungeni na chama cha upinzani cha Democratic Alliance-DA, baada ya uamuzi uliotolewa wiki iliyopita na Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini. Mbunge wa ANC, John Jeffery ameliambia bunge kwamba uamuzi uliotolewa na mahakama haukutoa sababu za mjadala kuhusu kuondolewa Zuma madarakani. Wabunge wa Afrika Kusini Wabunge wa Afrika Kusini Hata hivyo, kiongozi wa chama cha DA, Mmusi Maimane, amesema kuwa suala la rushwa limekiathiri chama chote cha ANC, kama saratani. ''Kwa kweli ni aibu sana kwamba bunge limevunja tena sheria sawa na hiyo. Sisi kama wapinzani hatuwezi kukaa hapa pamoja na chama kisichofata taratibu za kikatiba. Lazima tueleweke wazi kwamba hatutakubaliana na makosa ya kuipindua demokrasia ya taifa letu. Hapana haiwezekani kuwa hivyo spika,'' alisema Maimane. Mchakato huo ulionekana kama pigo kwa Zuma, ambaye amekuwa rais wa kwanza wa Afrika Kusini kukabiliwa na mjadala bungeni wa kutokuwa na imani naye. Imeripotiwa kwamba Rais Zuma ambaye amenusurika hoja ya kushtakiwa, alitumia kiasi cha Dola milioni 16 ambazo ni fedha za umma kukarabati makaazi yake binafsi kwenye mji wa Nkandla. Rais Zuma alidai kuwa amezitumia fedha hizo za walipa kodi kwa kufanya ukarabati ambao ulihusisha bwawa la kuogelea, eneo la mifugo, mabanda ya kufugia kuku, kituo cha wageni pamoja na eneo la kufanyia burudani.

Iran, Pakistan na Saudia zaongoza kwa kunyonga

Ongezeko la idadi ya watu wanaonyongwa ulimwenguni lilisababisha watu zaidi kuuawa kwa njia hiyo mwaka uliopita ikilinganishwa na kipindi chochote tangu mwaka 1989,shirika la haki za kibibaadamu la Amnesty International limesema. Takriban watu 1634 walinyongwa mwaka 2015,ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Iran,Pakistan na Saudia Arabia walihusika na asilimia 89 ya watu wote walionyongwa duniani. Jumla hiyo haishirikishi China ambapo Amnesty International imesema kuwa maelfu zaidi waliuawa lakini rekodi zake zikafichwa. Kwa upande mwengine,kundi hilo limesema kuwa kwa mara ya kwanza mataifa mengi duniani yalifutilia mbali hukumu ya kunyonga. Mataifa ya Fiji,Madagascar ,Congo Brazaville na Suriname yalibadilisha sheria zao mwaka 2015,huku Mongolia ikipitisha sheria mpya itakayoanza kutekelezwa baadaye mwaka huu. Vifaa vinavyotumiwa na serikali ya China kuwashinikiza watu kukubali makosa Amnesty imesema kuwa China bado inaongoza miongoni mwa mataifa yanayonyonga watu.Inakadiriwa kwamba maelfu ya watu walinyongwa huku maelfu ya wengine wakipewa hukumu ya kunyongwa mwaka 2015.

Moyo wa nguruwe wapandikizwa kwa nyani

Upandikizaji wa moyo wa nguruwe kwa nyani Wanasayansi wanasema kuwa wameuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili. Matokeo yake yanaweza kupiga jeki matumaini ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao. Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili unaofanyiwa upasuaji huo. Lakini wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga. Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia. Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu,kulingana na mwandishi mwenza Muhammad Mohiuddin,kutoka kwa taasisi ya kitaifa ya Moyo ,Pafu na Damu huko Maryland,alikiambia chombo cha habari cha AFP. Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.

Ted Cruz amshinda Trump mchujo Wisconsin

Cruz ameshinda upande wa Republican, naye Sanders akashinda Democratic Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Ted Cruz ameshinda mchujo wa chama hicho katika jimbo la Wisconsin, hilo likiwa pigo kubwa kwa Donald Trump. Katika chama cha Democratic, Bernie Sanders alipata ushindi mkubwa dhidi ya Hillary Clinton anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa. Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na katika kura za maoni chama cha Republican, lakini kuna wasiwasi kwamba huenda akashindwa kupata wajumbe wa kumuwezesha kuidhinishwa moja kwa moja kuwa mgombea. Wapinzani wa Bw Trump wanatumai kwamba hilo likifanyika basi wanaweza kubadilisha mambo katika mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha wagombea mwezi Julai. Katika mkutano huo, iwapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya nusu ya wajumbe, ni viongozi wa chama ambao watakuwa na usemi katika kuamua mgombea. “Leo ni siku muhimu sana, inatoa ujumbe kwa watu wa Marekani,” Bw Cruz amewaambia wafuasi wa chama hicho Milwaukee. “Tunashinda kwa sababu tunaunganisha chama cha Republican.” Bw Cruz huenda asipate wajumbe wa kutosha kumuwezesha kushinda uteuzi moja kwa moja, lakini viongozi wa chama cha Republican wanamuunga mkono katika juhudi za kumzima Bw Trump. Image copyrightReuters Bw Trump kwa upande wake amesema kwamba ana matumaini kwamba atafanikiwa licha ya kushindwa Wisconsin na akamshambulia mpinzani wake. "Ted Cruz ni mbaya kushinda kikaragozi, yeye ni kama kirusi, anatumiwa na viongozi wa chama kutupokonya uteuzi,” maafisa wa kampeni wa Bw Trump wamesema kupitia taarifa. Viongozi wa chama wana wasiwasi kwamba Bw Trump hatakuwa na nguvu sana katika kukabiliana na mgombea wa Democratic uchaguzini iwapo ataidhinishwa na pia kwamba anaweza kuathiri wagombea ubunge wa Republican uchaguzini. Kura za maoni zinaonesha hapendwi na wanawake, watu wa Hispania na vijana. Katika upande wa Democratic, ushindi wa Sanders jimbo la Wisconsin umemuongezea nguvu kabla ya mchujo muhimu New York na Pennsylvania. Seneta huyo wa Vermont, akiwahutubia wafuasi wake Wyoming, amesisitiza kwamba kampeni yake inaendelea kushika kasi na kwamba atabadilisha mambo. "Mabadiliko kamili huwa hayafanyiki kutoka juu kwenda chini, huwa yanatoka chini kwenda juu,” amesema. Bi Clinton yuko mbele sana kwa wajumbe na wadadisi wengi wa kisiasa wanasema ana uwezekano mkubwa wa kushinda uteuzi wa chama cha Democratic licha ya kushindwa majimbo kadha karibuni. Ingawa Bw Trump alishindwa mchujo huo wa Jumanne Wisconsin, bado ana muda wa kujikwamua.

Rais wa zamani wa Israel kusalia jela

Katzav alifungwa jela miaka saba Bodi ya kutathmini na kutoa msamaha kwa wafungwa nchini Israel imekataa kumwachilia huru rais wa zamani wa nchi hiyo Moshe Katzav. Katzav ametumikia miaka minne ya kifungo chake cha miaka saba jela alichohukumiwa baada ya kupatikana na makosa ya ubakaji. Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema Bw Katzav ameendelea kujitazama kama mwathiriwa na kulalamika kuhusu gharama kubwa ambayo familia yake imelipia. Bodi hiyo imesema hajaonekana kujutia kitendo chake wala kuonyesha huruma kwa wanawake aliowashambulia. Bw Katzav alihudumu kama rais wa Israel kuanzia 2000 hadi 2007.

Tuesday, April 5, 2016

ICC: Ruto na Sang hawana kesi ya kujibu

Bw Ruto alikuwa ameshtakiwa pamoja na mwanahabari Joshua Sang Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imeamua Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto hana kesi ya kujibu kuhusiana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yanamkabili. Aidha, imeamua pia kwamba mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, hana kesi ya kujibu. Bw Ruto alikabiliwa na mashtaka ya mauaji, kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Alikana mashtaka hayo na mawakili wake walitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi. Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo. Majaji wamesema upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang. Desemba mwaka 2014, mwendesha mashtaka aliondoa mashtaka sawa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta akisema mashahidi walikuwa wametishiwa na kubadilisha ushahidi wao. Bw Ruto na Bw Kenyatta walikuwa kwenye mirengo pinzani wakati wa uchaguzi wa 2007 lakini waliunda muungano wa kisiasa na wakashinda uchaguzi mkuu wa 2013.

Zuma aponyoka kura ya kutokuwa na imani naye

Zuma anusurika kura ya kutokuwa na imani naye Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amepenyoka kura ya kutokuwa na imani naye bungeni. Zuma alipata kura kutoka kwa wabunge 233 wanaomuunga mkono dhidi ya 143 za wabunge ambao hawakuwa na imani naye. Awali naibu spika alikuwa amewataka wabunge wapaze sauti hadharani kuhusu iwapo alikuwa anaunga mkono kura ya kutokuwa na imani au la. Hata hivyo upinzani ulishinikiza kura hiyo iendeshwe kwa njia halisi sawa na kura zingine. Wachanganuzi wa maswala ya kisiasa nchini Afrika kusini walikuwa wanatarajia matokeo hayo kutokana na idadi kubwa ya wabunge wa chama tawala cha ANC. Bunge la Afrika Kusini liliamua kusikiza na kujadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma kufuatia shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani. Spika wa bunge la Afrika Kusini bi Baleka Mbete, alikubali hoja hiyo ijadiliwe kufuatia mahakama ya juu ya Afrika Kusini kumpata rais Zuma na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake. Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema kilienda mahakamani kikitaka rais Zuma ashurutishwe kulipa fedha zilizotumika kinyume cha sheria kufanya ukarabati katika makazi yake ya Nkandla. Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.

Magufuli kuzuru Rwanda ziara ya kwanza nje

Hiyo itakuwa ziara ya kwanza ya Magufuli nje ya Tanzania tangu Oktoba Rais wa Tanzania John Magufuli amepangiwa kufanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi hiyo tangu kuingia madarakani mwaka jana. Dkt Magufuli anatarajiwa kuzuru nchi jirani ya Rwanda Jumatano na Alhamisi, kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Paul Kagame. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania, Dkt Magufuli na Bw Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha huduma za pamoja mpakani katika mpaka wa Tanzania na Rwanda. Kagame kuiga Magufuli katika matumizi Baadaye, wataelekea Kigali ambapo watafanya mazungumzo ya pamoja. Dkt Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 mjini humo. “Ikizingatiwa kwamba hii ndiyo ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu achukue madaraka Oktoba 2015, ziara hii inaashiria umuhimu ambao Tanzania inaweka katika kuimarisha uhusiano wake na majirani zake.” Rais Magufuli amekuwa mapumzikoni nyumbani kwake eneo la Chato, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Uwanja wa ndege wa Brussels wafunguliwa tena

Ndege ya shirika la ndege la Ubelgiji kuelekea katika mji wa Ureno wa Faro imeondoka katika uwanja wa ndege wa Brussels Jumapili ikiwa ni ndege ya kwanza ya abiria kuruka tokea miripuko ya kigaidfi Machi 22. Ndege ya shirika la ndege la Ubelgiji kuelekea katika mji wa Ureno wa Faro imeondoka katika uwanja wa ndege wa Brussels Jumapili ikiwa ni ndege ya kwanza ya abiria kuruka kutoka uwanja huo tokea miripuko ya mabomu ya kujitowa muhanga katika ukumbi wa kuondokea hapo Machi 22. Usalama katika uwanja huo umeimarishwa kwa taratibu mpya za ukaguzi wa abiria. Ndege nyengine mbili zimepangwa kuondoka baadae katika kitovu hicho cha usafiri wa anga barani Ulaya ambapo kilikuwa kikishughulikia safari 600 kwa siku.Baadae ndege ya shirika la ndege la Ubelgiji moja itaelekea Athens Ugiriki na nyengine itakwenda mjini Turin,Italia. Arnaud Feist Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uwanja wa Ndege wa Brussels ameziita safari hizo za Jumapili kuwa "ishara ya matumaini " kufuatia "siku za kiza kabisa katika historia ya usafiri wa anga nchini Ubelgiji." Pia amewashukuru wafanyakazi wote kwa ushujaa wao. Akizungumza katika hafla iliofanyika katika uwanja huo amesema "ziada ya kuwa ni uwanja wa ndege wamezidi kuwa familia iliyoungana." Uharibifu katika uwanja huo ulikuwa mkubwa sana kutokana na miripuko miwili ya kujitowa muhanga karibu na eneo la ukaguzi wa abiria lililokuwa limejaa watu siku kumi na mbili zilizopita na kuuwa watu 16 na kujeruhi wengine wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani. Mripuko mwengine siku hiyo hiyo umetokea katika kituo cha reli ya chini ya ardhi mjini Brussels na kuuwa watu wengine 16. Kundi la Dola la Kiislamu limedai kuhusika na miripuko yote hiyo. Feist amesema uwanja huo mkubwa kabisa nchini Ubelgiji utakuwa umerudi katika uwezo wa kufanya kazi kwa asilimia ishirini ifikapo Jumatatu na kuweza kuwahudumia abiria 800 kwa saa. Hapo Jumamosi alisema anataraji huduma kamili katika uwanja huo zinaweza kurudishwa kufikia mwanzoni mwa mwezi wa Julai wakati wa msimu wa mapumziko wa majira ya kiangazi. Hatua mpya za usalama katika uwanja huo zinakusudia kupunguza nafasi za kurudiwa kwa mashambulizi hayo. Polisi Jumapili walikuwa wakikaguwa magari kabla ya kuwasili.Hema kubwa limewekwa nje ya ukumbi wa uwanja wa ndege huo kukaguwa vitambulisho vya wasafiri, hati za kusafiria na mikoba yao kabla ya kuruhusiwa kuingia ndani ya jengo la uwamnja huo. Eneo la kuegesha magari nje ya ukumbi wa uwanja wa ndege limefungwa na maafisa wamesema kutakuwa hakuna usafiri wa reli na ule wa umma kuelekea katika uwanja huo katika kipindi cha hivi karibuni. Washambuliaji wa kujitowa muhanga waliingia katika eneo la ukaguzi uwanjani hapo wakiwa na mikoba iliosheni mabomu na misumari na miripuko hiyo imesababisha kuanguka kwa dari la uwanja huo na kuvunja madirisha. Mashambulizi hayo yamezusha mjadala mkubwa miongoni mwa maafisa wa usafiri wa anga katika nchi nyingi juu ya iwapo kufanya ukaguzi wa kawaida katika sehemu za kuingilia kwenye kumbi za uwanja wa ndege.

Rais Rousseff kujitetea kwa mara ya mwisho leo

Wakili mkuu wa Rais wa Brazil Dilma Rousseff atawasilisha hoja za mwisho mbele ya kamati inayochunguza uwezekano wa kiongozi huyo kushitakiwa. Mwanasheria Mkuu Jose Eduardo Cardozo anatarajiwa kuwasilisha hoja mbele ya kamati hiyo yenye wanachama kutoka vyama mbalimbali vya siasa kwa mara ya mwisho kabla kupiga kura kuhusu ikiwa ipendekeze rais Rousseff ashitakiwe kwa madai ya kubadilisha mahesabu katika akaunti ya serikali kuficha matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Brazil. Kikao hicho kinatarajiwa kuanza mwendo wa saa moja na nusu usiku. Mapendekezo ya kamati hiyo yaliyopangwa kutangazwa Aprili 11 hayana mafumgano lakini yatatoa muelekeo wa jinsi kura itakavyopigwa katika baraza la wawakilishi kuhusu mustakabali wa Rousseff. Theluthi mbili ya kura za wajumbe wa baraza hilo, yaani kura 342, zinahitajika kuipeleka kesi ya rais huyo katika baraza la seneti. Kwa mujibu wa gazeti la Folha toleo la Jumapili, baraza la wawakilishi linatarajiwa kupiga kura Aprili 17. Ratiba hiyo inampa rais Rousseff siku chache tu kutafuta uuungwaji mkono na kuokoa wadhifa wake. Kufuatia makubaliano yaliyofanyika kwa njia ya siri, anatarajiwa hivi karibuni kutangaza nafasi za uwaziri na nafasi za ajira serikalini zitakazotolewa kama zawadi kwa kuungwa mkono na bunge. Hatima ya Lula kujulikana Rousseff pia wiki hii atajua ikiwa mahakama ya juu kabisa ya Brazil itakubali rais wa zamani wa taifa hilo anayekabiliwa na kashfa, Luiz Inacio Lula da Silva, atajiunga na baraza lake la mawaziri. Lula ni muhimu katika kuviunganisha vyama vya mrengo wa kushoto na kuvishawishi kuunda muungano unaopinga rais Rousseff kufunguliwa mashitaka, lakini amezuiwa kwa sababu anashutumiwa katika kesi inayohusiana na kashfa kubwa ya ubadhirifu wa fedha na hongo katika kampuni ya mafuta ya serikali, Petrobras. Gabriel Petrus, mchambuzi katika shirika linalojihusisha na masuala ya siasa la Barral M Jorge Associates, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wiki hii pande zote mbili zitacheza karata zao kwa bidii na kuchukua hatua kwa umakini. "Wiki ijayo tutapa matokeo ya mapambano haya," akaongeza kusema mchambuzi huyo. Rousseff anatuhumiwa kwa kuchakachua mahesabu ya akauti za serikali, madai ambao wachambuzi wengi wanayaona kuwa madogo na hayatoshi kuweza kumfungulia mashitaka. Hata hivyo rais huyo pia yuko katika kiti moto kwa mdororo wa kiuchumi na kashfa ya rushwa ya kampuni ya mafuta ya Petrobas. Huku umaarufu wa serikali yake ukiwa asilimia 10 na bunge likiwa halina uwezo wa kupitisha sheria, Rousseff tayari anaonekana hana nguvu.

Ugiriki yaanza kuwarejesha wahamiaji Uturuki

Ugiriki imeanza kuwarejesha Uturuki wahamiaji walioko nchini humo ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya ambayo yamekosolewa na makundi ya haki za binadamu Griechenland Die Situation der Flüchtlinge auf Lesbos Kundi la kwanza la wahamiaji hao limewasili nchini Uturuki asubuhi ya leo. Isaac Gamba anaarifu zaidi katika taarifa ifuatayo. Boti ya kwanza iliyobeba wahamiaji waliokuwa nchini Ugiriki, imewasili asubuhi hii katika bandari ya Dikili nchini Uturuki, ikisindikizwa na walinzi wa pwani ya nchi hiyo. Boti hiyo, Nazli Jale ni moja ya mbili zenye kupeperusha bendera ya Uturuki, ambazo zimeondoka alfajiri ya leo jumatatu tarehe 04.04.2016 katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos zikiwa zimewabeba wahamiaji 131. Mabasi maalumu kwa ajili ya kuwabeba mamia ya wahamiaji hao kwa ajili ya kusafirishwa kupelekwa nchini Uturuki nayo pia yaliwasili katika bandari za Lesbos na Chios nchini Ugiriki mapema asubuhi. Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Efkan Ala amesema nchi yake iko tayari kuwapokea watu 500 ingawa serikali ya ugiriki imetoa majina ya watu 400 tu . Hata hivyo idadi hiyo inaweza kubadilika. Baadhi ya wahamiaji wawasilisha maombi ya hifadhi katika dakika za mwisho. Chanzo cha kipolisi kutoka katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki ambacho kimekuwa njia kuu ya watu wanaotafuta hifadhi barani ulaya wakitokea nchini Uturuki kimesema kumekuwepo na harakati katika dakika za mwisho za maombi ya watu wanaotafuta hifadhi ya kisiasa barani ulaya miongoni mwa wahamiaji 3,300 walioko nchini humo. " Tuna idadi ya zaidi ya watu 2,000 ambao tayari wameonesha nia ya kutafuta hifadhi ya kisiasa na tunahitaji kuona utaratibu unaofaa kwa ajili ya kushughulikia suala hilo'' amesema Boris Cheshirkov ambaye ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi katika kisiwa cha Lesbos, na kuongeza kuwa shughuli hiyo itafanyika kulingana na taratibu zinazohusiana na masuala ya hifadhi ya kisiasa nchini Ugiriki kwa wale ambao wanahitaji kuelezea juu ya kuwepo na haja ya kulindwa. Griechenland Flüchtlinge auf Lesbos Wahamiaji wameanza kusafirishwa kutoka bandari ya Mytilini Wahamiaji hao pia wanatarajiwa kusafirishwa kurejeshwa nchini Uturuki kutoka katika visiwa vingine ambavyo pia vimeshuhudiwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji, kama vile Chios ambako maafisa wa shirika la kulinda mipaka ya Umoja wa Ulaya walionekana kuwasili hapo jana. Idadi kamili ya wahamiaji wanaotarajiwa kurejeshwa Uturuki haijawekwa wazi Hata hivyo maafisa wa serikali ya ugiriki hadi sasa hawajaweka wazi kuhusiana na idadi kamili ya wahamiaji watakaorejeshwa nchini Uturuki katika utekelezaji wa makubaliano hayo ingawa shirika la habari la nchi hiyo limekaririwa katika taarifa yake likisema kuwa kiasi ya wahamiaji 250 kutoka Bangladesh, Pakistan, Sri Lanka na kutoka mataifa ya Afrika watakuwa wakirejeshwa kila siku kati ya siku za Jumatatu na Jumatano. Yiorgos Kyritsis, msemaji wa kitengo kinachoratibu masuala ya wahamiaji nchini Ugiriki, amesisitiza kuwa operesheni ya jumatatu tarehe 04.04.2016 itawahusu wale tu ambao hawajawasilisha maombi ya kuomba hifadhi ya kisiasa. Makundi ya haki za binadamu tayari yamekosoa makubaliano yanayohusu kurejeshwa kwa wahamiaji hao, yaliyofikiwa kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya, yakihoji kama yamefuata sheria na pia kuzingatia maadili. "Hatujui kwa kweli kipi kitatokea" alisikika Peter Sutheland ambaye ni afisa mwandamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi. Makubaliano hayo yalisainiwa mwezi Machi mwaka huu mnamo wakati mataifa ya ulaya yakikabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia huku zaidi ya wakimbizi milioni moja wakiwasili barani humo kutoka katika mataifa ya Mashariki ya Kati na kwingineko katika kipindi cha mwaka jana. Chini ya makubaliano hayo Uturuki iliahidiwa kupata msaada zaidi wa kifedha na raia wake kusafiri bila viza katika mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Monday, April 4, 2016

Magufuli afuta sherehe za sikukuu ya muungano

Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kufuta sherehe za sikukuu Rais wa Tanzania John Magufuli ameahirisha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Muungano na badala yake akawataka Watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani au wakiwa katika shughuli zao binafsi. Siku hiyo hata hivyo bado itasalia kuwa ya mapumziko kama kawaida. Agizo hilo la Dkt Magufuli aidha linaathiri shamrashamra za mwaka huu pekee. Siku hiyo huadhimishwa tarehe 26 Aprili kila mwaka kukumbuka siku sawa na hiyo mwaka 1964 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja). Magufuli aamua sikukuu iwe siku ya kazi Magufuli: Vijana sharti wafanye kazi Dkt Magufuli amesema fedha ambazo zilipangwa kutumika kwa ajili ya kugharimia vinywaji, vyakula, gwaride, halaiki, burudani mbalimbali na hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni mbili za Tanzania zitumike kupanua barabara ya Mwanza Airport katika eneo linaloanzia Ghana Quarters hadi uwanja wa ndege wa Mwanza. Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi kutatua msongamano wa mkubwa wa magari ambayo umekuwa ukiathiri shughuli eneo hilo. Dkt Magufuli amekuwa mapumzikoni nyumbani kwake eneo la Chato, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

CUF: Hatumtambui Shein kama rais Zanzibar

Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimesema hakimtambui Dkt Mohamed Ali Shein aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi uliopita. Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakizungumza kwa mara ya kwanza tangu kufanyika kwa uchaguzi huo ambao chama hicho kilisusia, wamesema hawamtambui Dkt Shein kama rais wa visiwa hivyo. “Tangu mapema, tangu Jecha (Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha) alipofuta uchaguzi, tulisema waziwazi kwamba haikuwa halalali. Walipoitisha uchaguzi wa marudio, tulisema waziwazi uchaguzi huo sisi hatuutambui na tukawataka wananchi wasipige kura,” amesema Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad. Bw Hamad alikuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na ambao matokeo yake yalifutwa na tume. “Kama Rais ametokana na mchakato ambao hamkuutambua nyinyi tangu mwanzo, sasa leo kuja kusema hatumtambui kwa nini iwe ni haramu? Hatumtambui.” Chama hicho kimesema kitatumia njia za kidemkrasia kulalamika dhidi ya Dkt Shein na serikali yake. Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC Mabalozi wakosoa uchaguzi wa Zanzibar Aidha, kimeiomba jamii ya kimataifa kuwawekea vikwazo watu binafsi waliofanikisha uchaguzi huo wa marudio ambao chama hicho kimesema ulikuwa “uongozi haramu”. Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama Twaha Taslima amesema chama hicho hakiko tayari kuwa sehemu ya serikali mpya. "CUF haitoshirikiana na serikali itakayoundwa kwa sababu ni kinyume na katiba ya Zanzibar, kinyume na sheria ya uchaguzi na haikutokana na ridhaa ya watu," amesema. Wiki iliyopita, Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC) lilisitisha ufadhili wa $472milioni kwa Tanzania likilalamikia uchaguzi visiwani Zanzibar na utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao. Pesa hizo zilikuwa za kutumiwa katika miradi ya kusambaza umeme. CUF imesema upo uwezekano wa kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo ka ikiwa uchaguzi huo utarudiwa basi usimamiwe na ujumbe wa kimataifa kwani wasimamizi wa ndani wamepoteza uhalali Chama tawala visiwani humo kimebeza tamko hilo la CUF ana kusema kuwa Wazanzibari ni watu makini na kwamba hawawezi kumnyima ushirikiano Rais wao ambaye anafanya kazi kuwaletea maendeleo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai ameiambia BBC kwamba Rais Shein anao pia uwezo wa kutengeneza serikali hata bila ushiriki wa chama cha CUF "CUF wanafanya upotoshaji. Katiba haijamfunga Rais kukamilisha utengenezaji wa serikali yake. Na hivi tunapozungumza, muda si mrefu atakamilisha serikali yake na atajumuisha Wazanzibari na kufanya nao kazi" alisema Vuai. Hii ni mara ya kwanza kwa Chama cha CUF kutoa tamko tangu kurudiwa kwa uchaguzi ambao waliususia

Uchunguzi: Viongozi 18 wa Afrika waliotajwa

Viongozi na watu wengine maarufu 18 wa Afrika wametajwa katika nyaraka zilizofichuliwa hapo jana zikiwahusisha na kampuni moja ya kisheria nchini Panama inayowasaidia kufungua kampuni katika mataifa yasiotoza kodi kwa minajili ya kukwepa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi kimataifa. Kwa mujibu wa nyaraka za siri zilizopatikana na gazeti moja la Kijerumani na kusomwa na Idhaa ya BBC, kampuni hiyo ya Mossack Fonseca imewasaidia viongozi hao wa Afrika washirika wao na jamaa zao wamekuwa wakiitumia kampuni hiyo kuficha asili ya mali yao. Hati hizo zinaonyesha kuwa mabilioni ya pesa zilitolewa barani Afrika na kuwekezwa katika kampuni hewa ughaibuni. Kwa baadhi yao akiwemo rais wa zamani wa Sudan Ahmad Ali al-Mirghani, na Naibu jaji mkuu wa Kenya bi Kalpana Rawal, na mwanaye aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, Kojo Annan kampuni hizo hewa zilitumika kununua nyumba katika mitaa ya kifaharai mjini London Uingereza. Msaidizi wa karibu wa Mfalme wa Morocco Mounir Majidi -alitumia kampuni kama hiyo kununua mashua ya kifahari mwaka wa 2006. Mawakili wake wanasema kuwa biashara hiyo ilikuwa halali. Mpwa wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ,Khulubuse Zuma ametajwa kama mmiliki wa kampuni iliyotwaa hati ya kuchimba mafuta katika maeneo mengi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo mwaka wa 2010. Image copyrightPA Image caption James Ibori aliyekuwa gavana wa jimbo la Delta anatumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha 2012 Msemaji wake amekanusha kuwahi kumiliki kampun hewa. Viongozi wengine na jamaa zao walikataa mwito wa BBC wa kuwataka wajieleze. James Ibori aliyekuwa gavana wa jimbo la Delta anatumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha mnamo mwaka wa 2012. Kampuni hewa 4 zinazohusiana naye zilitumika kutakatisha fedha ambazo baadhi zilitumika kununua ndege ya kibinafsi iliyogharimu takriban dola milioni $20,000,000.

Wahamiaji waanza kufurushwa Ugiriki

Uturuki inatarajia kupokea wahamiaji 500 Maboti ya kwanza yaliyowabeba wahamiaji ambao wanafurushwa kutoka Ugiriki na kupelekwa Uturuki yameanza safari chini ya mpango wa EU unaotarajiwa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya. Mamia ya wahamiaji wameonekana wakiabiri feri katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki mapema Jumatatu. Wanapelekwa Dikili, magharibi mwa Uturuki. Maafisa wa Uturuki wamesema wanatarajia kupokea karibu watu 500. Mkataba kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki umeshutumiwa vikali na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na kuna wasiwasi pia kuhusu maandalizi duni. Wahamiaji nchini Ugiriki wamelalamika kwamba hawana habari za kutosha kuhusu utaratibu wa kuomba hifadhi na wengine wamesema hawafahamu kwamba wanaweza kurejeshwa Uturuki. Idara ya EU inayohusika na kuwasindikiza watu na kuwavusha bahari ya Aegean ina chini ya asilimia kumi ya wafanyakazi inaohitaji kutekeleza jukumu hilo, shirika la habari la Associated Press limeripoti. Feri nyingine inayobeba wahamiaji kuwapeleka Uturuki inatarajiwa kuondoka kisiwa cha Chios nchini Ugiriki baadaye Jumatatu. Chini ya mkataba huo wa EU, wahamiaji wanaowasili kwa njia haramu Ugiriki wanatarajiwa kurejeshwa Uturuki wasipowasilisha maombi ya kutafuta hifadhi au maombi yao yakikataliwa. Kwa kila mhamiaji wa Syria anayerejeshwa Uturuki, EU inapangiwa kumpokea mhamiaji mwengine wa Sryia ambaye ombi lake limekubaliwa. Uturuki itanufaika kifedha na kisiasa kutoka kwa umoja huo chini ya mkataba huo. Tangu kutiwa saini kwa mkataba huo mwezi Machi karibu watu 400 wamekuwa wakiwasili kila siku visiwa vya Ugiriki. Wahamiaji milioni moja waliingia Ulaya kupitia Ugiriki kwa kutumia maboti kutoka Uturuki mwaka jana.

Kiongozi wa ugaidi Nigeria akamatwa

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limemkamata kiongozi wa kundi wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye uhusiano pia na kundi la kigaigi la Al Qaeda.taarifa ya msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo. Kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kundi la Ansaru tawi la Boko Haram kunafuatiwa kusakwa kwa muda mrefu ambapo Marekani walitoa ahadi ya zawadi ya dola millioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kutiwa nguvuni Khalid al Barnawi. Ansaru ni kundi maarufu kwa utekaji wa raia kutoka nchi za Magharibi na limekuwa likituhumiwa kwa mauaji ya raia kadhaa wa kimagharibi pia.Brigedia Jenerali Rabe Abubakar ameiambia BBC kuwa kukamatwa kwa Barnawi ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi. “Ndiyo tumemkamata gaidi.Yeah, kukamatwa kwake ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi,na si ndani ya Nigeria tu bali duniani kote pia. Ni mtu mhimu sana katika makundi ya kigaidi Nigeria na Duniani,na tunajitahidi kuhakikisha hatuishii kumkamata yeye tu bali na wengine.

Viongozi 72 duniani wahusika na kampuni ya siri

Nyaraka za siri zilizopatikana zaonesha kuwa viongozi 72 kote duniani wanatumia kampuni moja kutakatisha fedha kukwepa kodi Stakabadhi za siri za shirika moja la kisheria la Panama zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani zimeonyesha viongozi zaidi ya 72 wakuu wa nchi wa zamani na wale waliopo madarakani wanahusika na kampuni hiyo ya kisiri iliyowasaidia wateja wao kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa. Kwa mujibu wa nyaraka za siri zilizopatikana na gazeti moja la Kijerumani na kusomwa na Idhaa ya BBC, kampuni hiyo ya Mossack Fonseca imewasaidia watu duniani kote kufungua kampuni kwenye visiwa ambavyo havitozi kodi. Hati hizo zinaonyesha kuwa dola bilioni kadhaa zilitakatishwa na benki moja ya Urusi kwa kumuhusisha mtu mwenye uhusiano na rais Urusi Vladimir Putin. Image copyrightReuters Image caption Viongozi 72 duniani washirikishwa na kampuni ya siri ya Panama Nyaraka za kampuni hiyo ya Mossack Fonseca zinaonesha kampuni zote zilizofunguliwa kwenye visiwa vinavyotoa misamaha ya kodi zilifuata sheria na miiko ya ufunguaji biashara. Mossack Fonseca imesema inasikitika kuwa kuna ambao wametumia vibaya huduma zake.

CUF kuzungumzia hali ya siasa Zanzibar

Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar leo kinatarajiwa kutangaza mikakati yake na msimamo kuhusiana na mzozo wa kisiasa wa Zanzibar. Hata hivyo msimamo huo unatarajiwa kuzungumzia mufaka katika ya chama cha CUF na CCM ambao ulileta uundwaji wa serikali kati ya vyama hivyo viwili. Chama cha CUF visiwani Zanzibar bado kinaendeleza msimamo wake kususia kutambua matokeo na serikali iliyoundwa kufuatia uchaguzi wa marudio. Hivi karibuni shirika la misaada la Marekani MCC lilisitisha msaada wa dola 487 kwa madai ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Saturday, April 2, 2016

Wakenya wakumbuka shambulio la Garissa

Wananchi wa Kenya wamekuwa na kumbukumbu ya kwanza ya shambulio la Chuo Kikuu cha Garissa wakati wapiganaji wanne wa itikadi kali walipowaua watu 148. Mamia walikusanyika katika eneo la shambulio hilo mashariki ya Kenya kukumbuka mkasa huo ambalo ni shambulio baya kabisa la kigaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo likitekelezwa na wapiganaji wanne wa kundi la Al Shabab la Somalia lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda. Wapiganaji hao hatimae waliuwawa na kikosi cha makomandoo wa Kenya baada ya saa 12 na serikali ilikosolewa vikali kwa kuchelewa kuchukuwa hatua ya kukabiliana na shambulio hilo licha ya kuwepo kwa kambi ya kijeshi karibu na eneo hilo la tukio. Kenya imekabiliwa na wimbi la mashambulio ya wapiganaji wa itikadi kali tokea ilipotuma wanajeshi wake nchini Somalia hapo mwezi wa Oktoba mwaka 2011 kuisaidia serikali dhaifu ya nchi hiyo katika mapambano yake na wanamgambo wa Al Shabab. Chuo kikuu hicho kilifunguliwa tena hapo mwezi wa Januari baada ya ukarabati mkubwa wa majengo yaliojaa tundu za risasi lakini ni wanafunzi 150 tu kati ya 700 waliorejea madarasani.Wengine wamehamishiwa katika Chuo kikuu cha Aden Duale mbunge wa Garissa amesema katika kumbukumbu hiyo kwamba vikosi vya Kenya vitaendelea kubakia nchini Somalia hadi hapo jukumu la kuleta utulivu katika nchi hiyo litakapotimilizwa. Hata hivyo wazungumzaji wengine katika kumbukumbu hiyo wamesema familia za wahanga zinapaswa kulipwa fidia.Mwakilishi wa wanawake wa Kaunti ya Garissa Shukran Gure amesema "Wakati umefika kwa serikali kuwafidia wanafunzi waliouwawa katika shambulio hilo.Huo ni wajibu wa serikali." Paul Wekesa mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni mwanafunzi wa masomo ya elimu wa mwaka wa pili ambaye alishuhudia shambulio hilo anakubali kwamba serikali inapaswa kutowa fidia ya aina fulani kwa familia za wanafunzi waliopoteza maisha na msaada wa masomo kwa wale walionusurika. Amesema yeye mwenyewe aliweza tu kunusurika kwa sababu alikuwa ameamka na mapema ili kusoma na alikuwa macho wakati shambulio hilo likianza. Akiwa pamoja na kundi jengine la wanafunzi alikwenda kuchunguza sauti za risasi ambapo walikuja kukutana na mtu mwenye bunduki aliyewafaytulia risasi. Mwanafunzi mmoja alikufa papo hapo na wengine walikimbia kwa kuukwea uzio wa senye'nge huku risasi zikiwaandama. Kwa mujibu wa mchambuzi wa kisiasa Patrick Gathara kwa umma kuna masuali mengi yanayohitaji majibu kuhusu serikali kuchelewa kuchukuwa hatua,kushindwa kuzuwiya shambulio hilo licha ya kuwepo kwa tahadhari za kijasusi na ukweli kwamba hakuna mtu aliyefunguliwa mashtaka kwa uzembe wa usalama. Amesema Kenya ni nchi ilioko hatarini.Watu hawaamini kwamba kimsingi wako salama licha ya kile inachosema serikali. Ameongeza kusema kwamba "hakuna ushahidi serikali imejifunza kutokana na makosa yake." Ukiwa ni mwaka mmoja tokea shambulio hilo vyuo vikuuu vya Kenya vimekuwa katika hofu ambapo mara nne kumetokea mikanyangano katika taasisi mbali mbali baada ya wanafunzi kudhania kwamba wamesikia milio ya risasi au mabomu ambapo mamia walijeruhiwa na wawili kupoteza maisha yao.

Hans-Dietrich Genscher afariki dunia

Mwenyekiti wa heshima wa chama cha waliberali, FDP Hans Dietrich Genscher amefariki mjini Bonn akiwa na umri wa miaka 89. Kwa muda wa miaka mingi Genscher pia alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani. Hans-Dietrich Genscher anderer Ausschnitt Tumekuja kwenu ili kuwapa taarifa kwamba mnaruhusiwa kusafiri nchi za nje." Ni kauli hiyo hasa itakayomfanya mwanasiasa Genscher aendelee kukumbukwa. Aliitoa kauli hiyo mjini Prague katika majira ya kiangazi mnamo mwaka wa 1989. Alikuwa amesimama kwenye roshani alipoyasema hayo yaliyoleta furaha kubwa kwa raia wa iliyokuwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Ujerumani- waliokimbilia kwenye ubalozi wa Ujerumani magharibi na kuendelea kukaa kwenye ubalozi huo kwa siku kadhaa. "Ulikuwa wasaa wa kusisimua kuliko mwingine wowote katika wadhifa wangu wote wa kisiasa. Niliweza kuwaelewa watu kwa sababu mimi mwenyewe niliondoka Ujerumani Mashariki nilipokuwa katika umri kama wao. Walikuwa na wasi wasi, lakini nilipowaambia kwamba njia ilikuwa wazi kwa ajili yao,walipiga shangwe ambazo sikuweza kuzifikiria, na huo ndio ulikuwa mwanzo wa mwisho (wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Ujerumani"), alikumbuka Genscher. Hans-Dietrich Genscher wakati akitangaza mjini Prague, kuwafungulia milango raia wa Ujerumani Mashariki kuingia Magharibi. Hans-Dietrich Genscher wakati akitangaza mjini Prague, kuwafungulia milango raia wa Ujerumani Mashariki kuingia Magharibi. Nyadhifa alizozitumikia Katika maisha yake Hans Dietrich Genscher alizitumikia nyadhifa mbalimbali za kisiasa, lakini jina lake liliambatana sana na wadhifa wa waziri wa mambo ya nje. Tayari mnamo mwaka wa 1974 watu wengi walimwita Genscher wakili mahiri wa kuleta urari baina ya magharibi na mashariki. Kutokana na mkutano juu ya usalama na ushirikiano barani Ulaya, Genscher alihamasika kuziundua sera yake juu ya kuondoa mvutano baina ya mashariki na magharibi mnamo miaka ya 80. Genscher aliutekeleza mpango maalumu wa ziara za kidiplomasia. Baada ya majeshi ya Urusi kuivamia Afghanistan mnamo mwaka wa 1979 Genscher alichukua msimamo mkali dhidi ya Urusi lakini wakati wote aliuacha wazi mlango wa mazungumzo. Alisimama kidete katika siasa ya kuondoa mvutano baina ya magharibi na mashariki lakini kwa uvumilivu. Kutokana na dalili za mabadiliko ya kisiasa kujitokeza nchini Urusi, Genscher aliweza kuona fursa kwa manufaa ya nchi mbili za kijerumani na kwa ajili hiyo alitoa mwito kwa viongozi wa Ujerumani Mashariki kubadilika kimawazo. Ndoto ya Genscher ilikuwa ya kweli baada ya nchi mbili za kijerumani kuunga tena. Hans-Dietrich Genscher ni nani hasa? Hans Dietrich Genscher alizaliwa mnamo mwaka wa 1927 karibu na mji wa Halle katika Ujerumani Mashariki. Baada ya nchi mbili za Ujerumani kuungana tena Genscher alirejea mara kwa mara katika mji wake wa uzawa . Genscher alikuwa mwasheria aliekuwa mwingi wa fahari alipotunukiwa shahada ya heshima ya uzamifu na chuo kikuu cha Leipzig. Baada ya masomo ya sekondari mnamo mwaka wa 1946 Genscher alisomea sheria kwenye chuo hicho na kwenye chuo cha mjini Halle. Wakati akiwa mwanachama wa chama cha waliberali, mwanasiasa huyo alishuhudia mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Ujerumani Mashariki. Mnamo mwaka wa 1952 Genscher aliondoka Ujerumani Mashariki na kwenda Bremen ambako alikuwa wakili. Alijiunga na chama cha waliberali cha FDP katika jimbo hilo la Bremen. Na haraka sana alianza kupanda ngazi. Mnamo mwaka wa 1965 aliingia katika bunge la Ujerumani na alikuwamo katika bunge hilo hadi mnamo mwaka wa 1998. Wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani Genscher alikabiliwa na mtihani mgumu wa kwanza. Mnamo mwaka wa 1972 magaidi wa kiarabu waliwateka nyara wanamichezo wa Israel mjini Munic. Katika juhudi za kujaribu kuwakomboa wanamichezo hao walikufa. Genscher alitaka kujiuzulu, lakini Kansela wa wakati huo kutoa chama cha Social Demokratik Willy Brandt alimkatalia. Lakini muda tu kutoka hapo Hans Dietrich Genscher aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje na pia alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama chake cha FDP. Alikiongoza chama hicho kwa muda wa miaka 11. Lakini uongozi wa serikali ya Ujerumani ulibadilika wakati huo. Uongozi wa Social Demokratik ulifikia mwisho na chama cha CDU kiliingia madarakani-Helmut Schmidt aliondoka na Helmut Kohl aliingia. Kuunda mseto na CDU ulikuwa uamuzi mgumu kwa Genscher, na alithibitisha mara kwa mara katika mahojiano kwamba ilimwuia vigumu kuutamatisha mseto na Social Demokratik yaani na Helmut Schmidt. Ndugu wa chama hawakupendelea mseto na CDU na chama cha FDP kiliingia katika mgogoro mkubwa. Genscher amefariki Ijumaa mjini Bonn.

Zuma akubali makosa kuhusu ukarabati Nkandla

Mahakama ya Kikatiba ilimtaka Zuma alipe gharama ya ukarabati Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba uliompata na hatia kuhusiana na ukarabati uliofanywa katika makao yake ya kibinafsi eneo la Nkandla. Akihutubia taifa hilo moja kwa moja kupitia runinga, Bw Zuma amesifu mahakama hiyo na kusema imedhihirisha kuwepo kwa uhuru wa mahakama nchini humo. Amesema uamuzi wa mahakama hiyo ni wa kihistoria kuhusu uamuzi wa mkaguzi wa hesabu za umma aliyewasilisha kesi dhidi yake mahakamani. "Mahakama imeamua kwamba uamuzi wa mkaguzi wa hesabu za umma ni wa mwisho na anayetaka kubadili hilo lazima apitie kwa mahakama," amesema Bw Zuma. Kiongozi huyo amesema atakubali kulipia ukarabati uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla kama ilivyoamua mahakama. "Nimekuwa nikisisitiza kwamba niko tayari kulipia ukarabati usiohusiana na usalama katika mahakama yangu, taasisi rasmi ikifanya hesabu hiyo na kutoa uamuzi," amesema. Zuma taabani kwa matamshi dhidi ya wanawake Chama chatishia kumuondoa Zuma madarakani Bw Zuma amesema pia kwamba anakubali kwamba hatua yake ya kukosa kutii uamuzi wa mkaguzi wa hesabu za umma ni makosa na ukiukaji wa katiba. Hata hivyo amesisitiza kwamba hakufanya hivyo makusudi. "Awali, nilifuata njia tofauti ambayo ni sahihi kisheria wakati huo, lakini baadaye imebainishwa kuwa kinyume cha katiba. Kama Mahakama ya Kikatiba ilivyosema, nilifuata njia tofauti nikifuata uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Western Cape. Uamuzi huu baadaye ulibatilishwa baada ya rufaa na mara moja nilianza kufuata uamuzi wa Mahakama ya Rufaa," amesema. "Nia yangu haikuwa kutaka kujinufaisha kupitia ufisadi au kutumia mali ya umma kujifaidi au kufaidi familia yangu. Hivyo, nimeamua kulipia gharama ya vitu vinavyotakikana utathmini ukifanywa." Amesema kuna mafunzo ya maafisa wa serikali kujifunza kwa ajili ya siku za usoni. Ameeleza kuwa mradi huo wa Nkandla umefichua udhaifu wa mfumo wa ununuzi wa mali ya umma. Amekiri kwamba gharama ya ukarabati wa makao yake iliongezwa sana jambo ambalo halikufaa kufanyika.

Wabunge 9 wa chama tawala Gabon wajiuzulu

Rais Ali Bongo wa Gabon Wabunge tisa wa chama tawala nchini Gabon wamejiuzulu kulingana na ripoti za shirika la habari la AFP. Hatua hiyo inaongeza uvumi kwamba huenda chama kipya kikabuniwa kumkabili raisi Ali Bongo katika uchaguzi mnamo mwezi Agosti. Kiongozi wa bunge Guy Nzouba Ndama ambaye aliongoza bunge hilo tangu 1997 alitangaza kujiuzulu kwake siku ya Alhamisi.

Watatu washtakiwa kashfa ya Stanbic Tanzania

Watatu hao wamewekwa rumande hadi Ijumaa wiki ijayo Maafisa watatu wamefikishwa kortini Dar es Salaam leo wakishtakiwa kuhusiana na kashfa ya udanganyifu wa riba ya mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 600 ambazo zilikopwa na serikali ya Tanzania kutoka kwa benki ya Standard ya Uingereza. Walioshtakiwa ni aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw Harry Kitilya, aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Sinare pamoja na aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw Sioi Graham Solomon. Pamoja na makosa mengine, washtakiwa wote wameshtakiwa kwa makosa ya kula njama na kujipatia fedha kwa udanganyifu, kughushi nyaraka na utakatishaji wa fedha haramu kinyume na sheria. Wote wamekana mashtaka hayo. Washtakiwa wote watatu wamepelekwa rumande baada ya kukosa dhamana na kesi hii itatajwa tena tarehe 8 Aprili 2016. Kashfa hii ilitokana na kitendo cha Benki ya Standard kukubali kuipokesha Serikali ya Tanzania kiasi cha Dola milioni 600 mwaka 2012 kwa masharti ya kulipwa riba ya asilimia 1.4. Lakini Benki ya Stanbic, tawi la Tanzania iliongeza asilimia moja na hivyo kufanya serikali kutakiwa kulipa riba ya asilimia 2.4.

Friday, April 1, 2016

Mahakama Uganda yahalalisha ushindi wa Museveni

Mahakama ya juu kabisaa nchini Uganda Alhamisi imetupilia mbali shauri linalopinga kuchaguliwa tena kwa rais Yoweri Museveni mwezi Februari, na kusema mchakato huo ulikuwa wa haki na wa wazi. Shauri hilo liliwasilishwa na mgombea wa upinzani Amama Mbabazi, ambaye alitoa hoja za kucheleweshwa kwa vifaa vya kupigia kura, vitisho na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani. Shauri hilo pia linadai kuwepo na ushahidi wa udanganyifu, ikiwa ni pamoja na kupiga kura mara nyingi, na kuundwa kwa vituo haramu vya kupigia kura Februari 18. Jaji Mkuu wa Uganda Bart Katureebe alikataa pingamizi hilo, akisema hakukuwa na ushahidi kwamba ushindi wa Museveni ulikuwa wa udanganyifu. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71 alieitawala Uganda tangu 1986, alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia karibu 61 ya kura. "Tume ya uchaguzi ilimtangaza Museveni kihalali kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi wa rais," alisema Jaji mkuu Katureebe wakati akisoma hukumu mbele ya mahakama iliyokuwa imefurika mjini Kampala. "Hatuoni ushahidi wowote wa kuridhisha kuhusiana na madai ya kupiga kura mara nyingi," aliongeza, na kukataa madai ya upinzani ya kuwepo na vituo tofauti vya kujumlisha kura za uongo. "Hakukuwepo na vituo haramu vya kujumlisha matokeo ambavyo tume ya uchaguzi ilipokea matokeo kutoka kwake," ilisema hukumu hiyo. Polisi waliojihami kwa silaha nzito walitawanya mjini Kampala kuzuwia maandamano ya vurugu ya wafuasi wa upinzani kupinga hukumu hiyo. Mwandishi wa DW mjini Kampala Lubega Emmanuel ameripoti kuwa jeshi hilo lilitumia nguvu kuwatawanya wafuasi kadhaa wa upinzani waliokuwa wameanza kujikusanya katika maeneo mbalimbali ya jiji kuandamana. Mgombea alieshika nafasi ya tatu Amama Mbabazi, waziri mkuu wa zamani alieshinda juu ya asilimia moja tu ya kura, aliwasilisha pingamizi dhidi ya matokeo ya uchaguzi, lakini jopo la majaji tisa wa mahakama ya juu kabisaa nchini Uganda limelikataa pingamizi hilo kwa kauli moja. "Tunapata tabu kuamini kuwa mafanikio finyu ya mlalamikaji kwenye vituo vya kupigia kura yalitokana na kutokuwepo kwa mawakala wake," ilisema hukumu hiyo. Mpinzani wa karibu zaidi wa Museveni, Kizza Besigye, alikamatwa mara kadhaa wakati wa kampeni za uchaguzi na katika siku ya uchaguzi yenyewe, jambo ambalo alisema lilimzuwia kuwasilisha pingamizi sawa la kisheria. Anaendelea kuzuwiwa katika kifungo cha nyumbani. Polisi inasema yuko chini ya "kifungo cha uzuwiaji" ili asichochee vurugu. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Badru Kiggundu, ambaye pia ndie alisimamia chaguzi mbili zilizotangulia, ambazo Museveni alishinda, alitoa ushahidi wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo. Kiggundu aliomba radhi mahakamani kwa matatizo mengi yaliowakabili wapigakura katika mji mkuu and wilaya jirani ya Wakiso, zote zikiwa ngome kuu za upinzani, ambako vifaa vya kupigia kura vilipelekwa kwa kuchelewa au kutofikishwa kabisaa. Chini ya sheria ya uchaguzi ya Uganda, mtu anaedai kuwepo na kasoro na kutaka matokeo ya uchaguzi wa rais yafutwe, anapaswa kuthibitisha kwamba kasoro hizo ziliathiri matokeo kwa kiasi kikubwa. Mashauri mawili sawa yaliowasilishwa na Besigye mwaka 2001 na 2006 akitaka kubadilitishwa kwa ushindi wa Museveni yalitupiliwa mbali kwa misingi sawa na kusababisha ukosoaji mkubwa. Baadhi ya serikali za mataifa ya magharibi yaliomsifu Museveni huko nyuma kwa kusaidia mapambano dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu nchini Somalia, zimemkosoa hivi karibuni kwa ukandamizaji dhidi ya wakosoaji wake na kuwanyanyasa wapinzani. Mchambuzi wa siasa nchini Uganda Nicholas Ssengoba, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa ushindi wa Museveni unaakisi ugumu ulioukabili upinzani katika kukusanya ushahidi. Mara baada ya shauri kuwasilishwa mahakamani, wezi walivunja ofisi mbili za mawakili wa Mbabazi na kuiba baadhi ya ushahidi. Mbabazi alisema wizi huo yumkini ulipangwa na jeshi la polisi, tuhuma ambazo serikali ilizikanusha.

Trump ‘ajipendekeza’ kwa wakuu Republican

Bw Trump anaongoza kwa wajumbe chama cha Republican kufikia sasa Mgombea urais anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amechukua hatua ya kushangaza akijaribu kuimarisha uhusiano uliodorora kati yake na wakuu wa chama hicho. Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York ametembelea Kamati Kuu ya Taifa ya Republican. Trump ayumbayumba kuhusu utoaji mimba Amechukua hatua hiyo siku moja baada ya kuwakera viongozi hao kwa kusema kwamba hatatii makubaliano ya kuunga mkono mgombea mwengine, iwapo yeye mwenyewe hatashinda uteuzi wa chama hicho. Bw Trump, anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa, amekosoa kile anachosema ni juhudi zisizo za kidemokrasia za kutaka kumpkonya ushindi katika mkutano mkuu wa kuidhinisha mgombea mjini Cleveland mwezi Julai.

Rwanda yataka ufafanuzi kuhusu kifo cha waziri

Jacques Bihozagara alihudumu wakati mmoja kama balozi Ubelgiji Serikali ya Rwanda imeitaka Burundi kutoa ufafanuzi kuhusu kifo cha waziri wa zamani wa Rwanda aliyefariki baada ya kuzuiliwa na Burundi kwa miezi minne akituhumiwa kufanya ujasusi. Jacques Bihozagara, aliyekuwa wakati mmoja waziri na balozi wa Rwanda, alifariki tarehe 30 Machi, muda mfupi baada ya ufikishwa katika zahanati ya gereza la Mpimba. Chanzo cha kifo chake hakijatangazwa rasmi. Mkurugenzi anayeangazia masuala ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya Rwanda Eugene Ngoga, amesema: “Jacques Bihozagara ni mmoja tu kati ya Wanyarwanda wengi nchini Burundi ambao wamefariki katika hali isiyoeleweka katika kipindi cha miezi saba iliyopita. Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda inataka maelezo ya ufasaha kutoka kwa watawala Burundi kuhusu hali iliyopelekea kifo cha Bw Bihozagara na ufafanuzi kuhusu sababu za kuzuiliwa kwake tangu Desemba mwaka jana”. Rwanda pia imeitaka Burundi kusaidia familia ya marehemu kusafirishwa mwili wake hadi nyumbani kwake. Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji alikuwa awali ameandika na kusema kifo cha Jacques kilikuwa ni "mauaji". Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.

Waliokufa kuangukiwa daraja India wafikia 23

Moja ya magari yaliyoangukiwa na sehemu ya barabara hiyo Mamia ya waokoaji wakiongozwa na majeshi, wahandisi, matabibu wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha katika mji wa India wa Calcutta kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye barabara ya juu iliyoanguka ikijengwa. Maafisa wanasema hadi sasa watu 23 wamekufa na mamia kujeruhuwa na wengine wakiwa bado wamefukiwa na kifusi. Inasadikiwa watu wengi wamefukiwa ambapo hadi sasa tayari watu 23 wamethibitishwaa kufariki na mamia wengine kujeruhiwa ambao wanapatiwa matibabu. "Kulikuwa na watu wengi waliokuwa wamesimama chini ya bara bara hiyo inayopita juu kwa juu kulikuwa na bajaji na taxi nyingi zote zimefukiwa," anasema mmoja wa walioshuhudia mkasa huo Mkurugenzi Mkuu wa Kikosi cha Kukabiliana na majanga nchini India O P Singh anasema waokoaji wamekuwa wakikata zege ili kuwafikia watu waliokuwa wamezikwa baada ya kuangukiwa na kifusi. Kampuni iliyokuwa inajenga barabara hiyo ya juu kwa juu amesema watatoa ushirikiano kwa maafisa wa upelelezi katika uchunguzi wa tukio hilo. Msemaji wa kampuni hiyo K P Rao anasema bado hawajafahamu nini kilichosababisha

Korea Kaskazini yawa gumzo mkutano wa nuklia

Korea kaskazini imekuwa gumzo wakati wa mkutano wa dunia juu ya usalama wa nyuklia unaofanyika mjini Washngton. Baada ya kukutana na Rais Xi Jinping wa China, Rais Barack Obama amesema wote wanawajibu wa kulifanya eneo hilo la rasi ya Korea kuwa eneo huru lisilo na nyuklia na kuiweka vikwazo zaidi dhidi ya Pyongyang. Hali ya wasiwasi imetanda juu ya jaribio la Korea kaskazini kuendelea silaha za nyuklia na majaribio yake ya teknolojia ya makombora. Awali Rais Obama alikutana na viongozi wa Japan na Korea kusini kuweka msimamo wa pamoja juu ya suala la usalama katika rasi hiyo ya Korea. Pamoja na kwamba nchi ya pili kwa nuklia duniani Urusi haijahudhuria mkutano huo, Rais Obama alifanya mazungumzo na Rais Xi Jinping of China ambapo amesema yeye pamoja na Rais XI wamekubaliana kuondoa nuklia katika eneo la rasi ya Korea na kutekeleza vikwazo vipya vilivyopitishwa na Umoja wa Matiafa kwa lengo la kuipa shinikizo jipya Korea Kaskazini. Kwa upande wake Rais Xi amesema China inataka kuongeza mawasiliano na kuratibu jambo hilo ambapo nchi zote mbili zimekubaliana kukutana kila mwaka kuzungumzia masuala ya usalama wa nyuklia. Wamesema pia watafanya kazi kwa pamoja kuzuia malighafi za kutengeneza nuklia na kuratibu juhudi za kuzuia malighafi hizo kuangukia mikononi mwa magaidi. Hata hivyo kasoro moja katika mkutano huo ni kutokuwepo kwa Rais Vladimir Putin. Urusi na Marekani wanamiliki karibu asilimia 90 ya silaha za nyuklia hivyo Mosco kukataa kuhudhuria mkutano huo unaweza kufanya makubaliano yatakayofikia isiyatekeleze.