Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 31, 2016

International affairs facilitator reflects on pilgrimage

With a background in international conflict resolution, peace-building and reconciliation, Professor Emily Welty is uniquely suited to her role as acting moderator of the Commission of the Churches on International Affairs (CCIA) of the World Council of Churches (WCC). She facilitated the commission’s work most recently during its annual meeting in Geneva from 7 through 14 March. The CCIA is an advisory body within the WCC comprising 35 people nominated by churches and regional ecumenical organizations. The CCIA engages the capabilities of member churches in a shared ecumenical response to international affairs related to peace and justice. This year’s CCIA meeting focused especially on matters of religion and violence, the COP25 conference on climate change, the refugee crisis and “the economy of life.” “The dynamics of groups are fascinating, and in a group like this there are cultural differences beyond the usual mix of personality styles,” Welty observes. “It is an honour and a privilege to be asked to take this responsibility, yet it is also a truly humbling experience.” Welty asks herself, “What does it mean when one person is silent during a discussion? And what if a whole segment of participants hold themselves back from open dialogue? I try to be aware of these dynamics as the commission interacts.” The consensus approach to decision-making, a protocol in the WCC for more than ten years, can be puzzling for newcomers used to traditional systems of parliamentary procedure. Welty sees the consensus methods as “a good tool for getting a sense of where the group is going as it deliberates.” Director of Peace and Justice Studies at Pace University in New York, Welty is one of the youngest leaders ever to serve as chairperson or interim chair of a WCC commission. She was elected vice moderator of the CCIA following the 10th Assembly of the WCC at Busan, Republic of Korea, in 2013. She has been serving as acting moderator due to the ill health and demission of the original moderator Rev. Dr. Mvume Dandala. A lay member of the Presbyterian Church (USA), Welty hold degrees from the church-related College of Wooster in the US state of Ohio, American University in Washington DC and the University of London where she earned her doctorate at the School of Oriental and African Studies. She is the co-author (with Matthew Bolton, Meghana Nayak and Chris Malone) of “Occupying Political Science: The Occupy Wall Street Movement from New York to the World.” For Welty, one of the most significant moments in this year’s meeting was the day on which the CCIA visited the Geneva headquarters of the United Nations and attended a session of the Human Rights Council (HRC). The day before their visit, WCC commissioners heard a presentation by UN special rapporteur for human rights Heiner Bielefeldt. The next day, they heard him give his formal report to the HRC. “It is important for commissioners to see and experience the UN,” she says. “A visit like this humanizes the UN for people. It underlines the accessibility of the institution.” Welty expresses her appreciation as an interim moderator for the opportunity to meet with leaders of other ecumenical commissions: “From the viewpoint of an average commission member, one seldom has a sense of what all the other commissions are doing – Faith and Order, mission and evangelism, education, and so on. I had never had access to the moderators’ meeting until recently, and it increased my appreciation for the broader work of the ecumenical movement beyond my own commission.” She welcomes the WCC’s current theme of “a pilgrimage of justice and peace,” finding it “integral to who we are.” “We are part of a process,” she says. “Not just the commissions, but the member churches and other partners and Christians in many places. At the same time, the idea of pilgrimage provides a dynamic and a notion of what we’re walking toward, and how we’re endeavouring to walk. It’s not just that peace and justice are our goal, but they are our preferred means of being, of acting together.” “So far as the CCIA is concerned,” Welty adds, “we see ourselves as being on the pilgrimage of justice and peace.”

Hotuba ya Rais Kenyatta yavurugwa

Hotuba ya taifa ya rais wa kenya Uhuru Kenyatta, imetatizwa kwa muda bungeni baada ya wabuge kadha wa upinzani kupuliza firimbi. Wabunge hao walianza kupuliza firimbi na kuvuruga hotuba ya rais punde tu alipoanza kuitoa. Mmoja wa wabunge akizindikizwa nje Ilimbidi spika wa bunge kuwasihi wabunge ambao walionekana kuendelea kupuliza firimbi. Hata hivyo utulivu ulirejea baada ya spika kuwatupa nje wabunge waliokua wakizipuliza hizo firimbi, na rais akaendelea kutoa hotuba yake kwa taifa.

Wafadhili wasitisha ufadhili kwa bajeti ya Tanzania

Mataifa 10 ya Magharibi yamesema hayataendelea na ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania. Baadhi ya nchi hizo ni Sweden na Ireland. Nchi hizo zinaendelea na msimamo huo ikiwa ni siku chache baada ya shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani (MCC) kuondoa msaada wake wa dola 472 za ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa Tanzania. Bodi ya MCC ilisema hatua yake ilitokana na mzozo kuhusu uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar na utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao. Mataifa yaliyositisha ufadhili wao kwa bajeti ya Tanzania hata hivyo hayajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Ubalozi wa Sweden umethibitisha kwamba taifa hilo limesitisha ufadhili wake kwa bajeti ya Tanzania, lakini ukasisitiza kwamba hatua hiyo haihusiani na yaliyojiri katika uchaguzi wa visiwa vya Zanzibar. Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC Uchaguzi wa Zanzibar waikosesha hela Tanzania "Mwaka uliopita, Sweden ilikuwa moja ya nchi zilizositisha ufadhili wake kwa bajeti ya Tanzania kutokana na tuhuma za ufisadi kuhusiana na sekta ya kawi [na mkataba wetu na serikali ulifika kikomo mwaka jana],” ubalozi huo umeambia BBC. “ Sweden inafurahishwa na juhudi za serikali kukabiliana na ufisadi na iko tayari kuanzisha majadiliano na serikali ya Tanzania na wafadhili wengine kuhusu mikakati ya kufadhili bajeti ya Tanzania siku zijazo.” Ubalozi wa Ireland pia umethibitisha kwamba ni kweli taifa hilo halifadhili tena bajeti ya Tanzania. Ufadhili wake wa mwisho ulitolewa mwaka wa kifedha wa 14/15, malipo ambayo yalifanyika Juni 2015 na kwa sasa hakuna malipo yaliyoratibiwa ya mwaka wa kifedha wa 15/16. "Mpango ulimalizika Juni 2015 na hakuna mipango mingine ya kutoa ufadhili kwa bajeti (ya Tanzania),” ubalozi wa nchi hiyo umesema. Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua ya nchi hizo ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.

Aliyewakinga wakristo kutoka kwa al shabab atuzwa

Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa. Rais Kenyatta alihutubia taifa Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi. Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab. Rais Kenyatta amemtuza Mwalimu Farah heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi. Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu na wale wasio waislamu. Al Shabaab: Wanawake waislamu waliwafunika Hijab wakristo Waislamu waokoa wakristo waliotekwa na al Shabab Hapo ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu waliponga'amua nia ya wapiganaji hao ilikuwa ni kuua wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga abiria wakristo miongoni mwao ilikuokoa maisha yao. Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya kukataa kugawanywa kwa makundi. Kwa bahati mbaya Mwalimu Farah alifariki mwezi Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa takriban mwezi mmoja. Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na magaidi wa Al Shabab. Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya Makkah kutekwa. Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa waislamu. Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili mwaka uliopita lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.

Chama chatishia kumuondoa Zuma madarakani

Chama cha Democtratic Alliance nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka katiba. Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kamtaka alipe pesa zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi. Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimu rais Jacob Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi yaliofanywa na mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika na mabadiliko yaliofanyiwa nyumba yake ya Nkandla. Mamilioni ya madola yalitumika katika kile kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na zizi la ngombe

Wednesday, March 30, 2016

Wanawake 14 wapokea tunzo ya Marekani ya Wanawake Shujaa

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry pamoja na Balozi wa masuala ya wanawake Cathy Russell wakipiga picha na washindi wa tunzo ya "Wanawake Shujaa" 2016. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, aliwakabidhi wanawake kumi na wanne kutoka nchi mbali mbali za dunia tunzo ya Wanawake Shujaa, kwa kuonyesha uongozi katika kutetea haki, haki za binadam, demokrasia, usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake. Mmoja kati ya walopokea tuzo hiyo maarufu inayotolewa kila mwaka na Marekani, ni mwanaharakati wa kichina, Ni Yulan, aliyezuiliwa na serikali yake kusafiri hadi Washington. Miongoni mwa wanawake watatu kutoka Afrika ni Vicky Ntetema, mtanzania aliyetunukiwa tuzo hiyo kwa jitihada zake za kufichua mbinu zinazotumika kuwauwa na kuwakata viungo watu wenye ulemavu wa ngozi – albino. Waziri Kerry amesema, “Mwaka huu tunatambua kundi la wanawake walonesha ushujaa katika fani tatu muhimu. Kufichua na kupinga ghasia kwa misingi ya ngono, wanapambana na ulaji rushwa na kuimarisha utawala wa sheria na wanaohamasisha haki za kisheria na haki za binadamu kwa wote.” Huu ni mwaka wa 10 tangu kuanzishwa kwa tunzo ya “Women of Courage”, ambapo hasi sasa wanawake 101 wamepokea tunzo hiyo kutokana na mafanikio yao.

Afrika yakabiliwa na madeni ya kimataifa

Miongoni mwa mataifa yanayokumbwa na tishio zaidi la kuongezeka kwa viwango vyao vya ukopaji kimataifa ni pamoja na Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Afrika ya Kati, Chad, Ghana na Mauritania. Baadhi ya mataifa ya Afrika yanakabiliwa na malimbikizi ya madeni. Hayo ni kwa mujibu wa wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi duniani. Mataifa katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara yaliyokopa kimataifa sasa yanakabiliwa na hali ngumu kiuchumi huku thamani ya bidhaa ikiporomoka. Wataalamu wa uchumi wameelezea wasiwasi wao kuwa jinamizi la malimbikizi ya madeni limerejea kuyazonga mataifa ya Afrika, miaka ishirini tangu kufanywa kampeni duniani kote kufutilia mbali madeni yaliyoyakumba mataifa mengi masikini. Julien Marcilly, mchumi mkuu wa mashirika ya Coface nchini Ufaransa yanayotoa bima kwa mataifa yanayokabiliwa na madeni makuu kote duniani kuyaepusha dhidi ya kushindwa kulipa, amesema, watu hawakutarajia hali ya sasa kujitokeza na inazua wasiwasi mkubwa. Mpango wa shirika la fedha duniani IMF ulioanzishwa mwaka 1996 hadi sasa umeidhinisha dola bilioni sitini na nane kusaidia mataifa 36 yasiyojiweza kulipa madeni yao ya kimataifa, 30 kati ya mataifa hayo yanatoka Afrika. Kinachotia hofu ni kwamba mataifa hayo yanaendelea kukopa madeni kwa viwango vya juu. Baada ya kupata afueni ya kulipiwa madeni yao na mpango wa shirika la fedha duniani, baadhi ya mataifa yalifurahia uhuru wa bajeti zao kunawirisha uchumi ambao tayari ulikumbwa na bei za juu za bidhaa. Mchumi kutoka Tanzania Dr. Len Kasoga anasema hali hii imechangiwa na Afrika kuagiza bidhaa nyingi zaidi kuliko inazouza katika masoko makuu ulimwenguni miongoni mwa changamoto zaidi. Chinesische Kleinunternehmer in Afrika Katika miaka michache iliyopita, mataifa katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara yameshiriki uuzaji wa bondi kama njia ya kujipatia fedha kuendeleza bajeti zao, mengine yakishiriki kwa mara ya kwanza. Hata hivyo ripoti ya karibuni kutoka shirika la viwango la Standard and Poors inasema si njia bora zaidi ikizingatiwa baadhi ya nchi ziliuza bondi zake wakati viwango vya thamani ya bondi vimeshuka. Thamani ya sarafu za Afrika yadorora Ripoti hiyo imeonya kuwa hali imebadilika na mataifa husika yatahitajika kutumia fedha zaidi katika miaka mitatu ijayo kulipa madeni yao, na kwamba mataifa mengi katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara yatakumbwa na uamuzi mgumu kati ya kupunguza matumizi yao kifedha na kulazimika kulipa madeni kwa riba za juu siku za baadaye. Wakati huu madeni mengi yalitolewa na mashirika ya kibinafsi wala si shirika la fedha la kimataifa IMF au benki ya dunia. Shirika la Standard and Poors linasema kudorora kwa thamani ya sarafu za mataifa katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara, kunakohusishwa na kupungua kwa bei za bidhaa, kumechangia kuongezeka kwa viwango vya madeni katika sarafu za kimataifa. Utafiti uliofanywa na idara ya fedha nchini Ufaransa umeonyesha mpango wa shirika la Kimataifa la Fedha kwa ushirkiano na benki kuu ya dunia ulipunguza madeni ya mataifa 30 ya Afrika kutoka asilimia 119 hadi 33 kila mwaka. Miongoni mwa mataifa 30 yaliyopata msaada kuwawezesha kulipa madeni ya kimataifa, 13 yameongeza viwango vyao vya mikopo kwa asilimia kumi kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliongoza orodha hiyo kwa silimia 25, ikifuatwa na Niger kwa asilimia 23 na Malawi kwa asilimia 19. Miongoni mwa mataifa yanayokumbwa na tishio zaidi la kuongezeka kwa viwango vyao vya ukopaji kimataifa ni pamoja na Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Afrika ya Kati, Chad, Ghana; Mauritania, Sao Tome na Principe. Idara ya fedha nchini Ufaransa imesema hakuna njia ya mkato kuhusu mzozo wa madeni unaokumba mataifa ya Afrika. Huku ikionya mataifa mengine huenda yakarejelea hali ya awali miaka 20 kabla ulimwengu kufutilia madeni ya mataifa yasiyojiweza. Kwa mujibu wa Carlos Lopez ambaye ni katibu mkurugenzi katika tume ya kiuchumi ya Afrika ndani ya Umoja wa Mataifa, jumla ya madeni ya Afrika yamechukua asilimia 38 ya sehemu ya ukuaji. Ameongeza kuwa madeni yataongezeka katika mataifa ambayo nidhamu zao kudhibiti bajeti ni dhaifu

Iran: Makombora sio mazungumzo ndio ngao

Kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Khamenei, amesema wale wanaonadi kuwa hatma ya taifa lake siku zijazo inategemea mazungumzo badala ya makombora ya masafa marefu, wanadanganya. Amesema raia wa Iran ambao walitoa tetesi hiyo hawajui au ni wasaliti. Kiongozi huyo wa kidini amekariri kuwa sasa ni wakati wa mazungumzo na kutengeneza makombora. Matamshi hayo ya Ayatollah yanajiri siku chache baada ya rais wa zamani wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani kudai kuwa hatma ya taifa hilo siku zijazo inategemea mazungumzo na wala sio makombora. Ayatollah Ali Khamenei, aliisifu kikosi cha Revolutionary Guards ambacho kinaongoza harakati za makombora na ulinzi wa taifa kwa kuiinua jina la Iran kwa kufanya majaribio ya silaha kali. ''katika ulimwengu huu wa sasa wenye kila mtu anajifanya mbabe itakuwa vigumu kwa Jamhuri ya Iran kuendelea na mazungumzo ya kidiplomasia huku kila taifa likijihami,lakini kwa sasa hakuna taifa lolote litakalothubutu kuishambulia Iran'' alisema Ayatollah Khamenei, kupitia kwa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wake. ''Maadui wetu wanaendelea kuimarisha ulinzi wao na makombora yao kila kukicha itakuwaje tufikirie kuwa enzi za ubabe wa makombora umekwisha ? Iran bado inahitaji makombora asema kiongozi wa Iran Ayatolla Khamenei Matamshi yake yalitafsiriwa kumlenga aliyekuwa rais wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani, ambaye majuzi tu alichapisha kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa ulimwengu wa siku za usoni sio ulimwengu wa makombora bali itakuwa ni siku za mazungumzo ya kidiplomasia. Aidha matamshi yake yanawadaia siku moja tu baada ya Marekani,Uingereza Ufaransa na Ujerumani zilipoishtaki Iran katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kukiuka mapatano ya kinyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu zaidi dunia.

Mtekaji nyara awekwa rumande Cyprus

Mwanaume aliyejisalimisha kwa polisi wa Cyprus baada ya kuteka nyara ndege ya Egypt Air amefikishwa mahakamani. Seif Eldin Mustafa amewekwa rumande kwa siku 8 ilikuruhusu uchunguzi ukamilishwe. Mahakama hiyo ya Larnaca inapanga kumfungulia mshukiwa huyo mashtaka ya utekaji nyara, na kutishia maisha ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya Egypt Air. Hakuruhusiwa kuzungumza ila alionesha alama ya ushindi alipokuwa akiondolewa mahakamani. Maafisa wakuu wa Cyprus wanasema kuwa wanaona dalili kuwa Mustafa anamatatizo ya kiakili wakisema tukio hilo la utekaji nyara halihusiani kwa njia yeyote na ugaidi. Hakuruhusiwa kuzungumza ila alionesha alama ya ushindi alipokuwa akiondolewa mahakamani. Ndege hiyo ya EgyptAir MS181 ilikuwa ikibeba abiria 55, ikiwemo raia 26 wa kigeni waliotoka Alexandria kueleka Cairo. Wengi wa wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo waliwachiliwa baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Lanarca lakini mtekaji huyo aliwazuia watu saba kabla ya kisa hicho kukamilika kwa amani. Waziri wa maswala ya nje wa Cyprus Ioannis Kasoulides alisema kuwa bw Mustafa aliomba kuzungumza na mkewe wa zamani ambaye aliletwa katika uwanja wa ndege na polisi kabla ya kuanza kutoa matakwa mengine ya ''yasiyo na maana''.

Pele aishtaki Samsung anadai dola milioni 30

Gwiji wa soka ya Brazil Pele ameishataki kampuni ya kutengeza bidhaa za kielektroniki ya Samsung kwa kutumia mfano wake katika matangazo ya kibiashara bila idhini. Pele anataka kampuni hiyo ya Korea Kusini imlipe dola milioni $30 pesa za Marekani. Pele anadai kuwa Samsung imekuwa ikitumia mfano wake katika tangazo la runinga aina ya ultra high-definition katika jarida la New York Times bila idhini yake. Mbrazil huyo mwenye umri wa mia 75 ambaye majina yake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, aliwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya Chicago Marekani Pele anatambulika kama baba wa kizazi kipya cha wasakataji kabumbu anafahamika kote duniani kwa ustadi wake wa kucheza mpira. Aliongoza timu ya Brazil iliyotwaa kombe la dunia la mwaka wa 1958 na 1970. Aidha Pele alichezea timu iliyotawala kombe la dunia mwaka wa 1962. Umaarufu wake haukuishia tu katika ushindi wa kombe la dunia, la, Pele anakumbukwa kwa kuisaidia klabu yake ya Santos kutwaa ubingwa wa Copa Libertadores mara mbili mbali na kunyakua kombe la Intercontinental . Baada ya kustaafu soka ya kimataifa Pele alihamia Marekani ambapo alijenga jina kama nembo ya mpira wa kandanda ligi ya taifa NASL ilipokuwa ikijaribu kupata umaarufu katika miaka ya 1970. Yamkini Samsung walitumia mfano wake hata baada ya kuvunja majadiliano naye mwaka wa 2013 walipokuwa wamemtaka awape ruhusa ya kutumia mfano wake kuuza runinga zao. Nyota huyo sasa anatumia sura yake kunadi bidhaa mbali mbali na pia kushiriki maonesho kadha kujichumia mkate wake wa kila siku.

Trump asema hatomuunga mgombea mwengine

Mgombea aliye kifua mbele katika chama cha Republican Donald Trump ameondoa ahadi yake ya kumuunga mkono mgombea wa chama hicho iwapo hatoshinda uteuzi wa uchaguzi huo wa mwezi Novemba. Wapinzani wa bwana Trump Ted Cruz na John Kasich wamekataa kutangaza iwapo watamuunga mkono atakayeteuliwa na chama hicho. Wagombea wote wa Republican walitia sahihi kutekeleza ahadi hiyo mwezi Novemba. Ni ishara ya mwisho ya msuguano kati ya Bwana Trump na Bwana Cruz ambaye wamekuwa na mgogoro unaowahusisha wake zao. Kamati inayomuunga mkono Bwana Cruz imechapisha picha ya utupu ya mkewe Trump Melania kutoka mwaka 2000. Akimjibu, bwana Trump alituma ujumbe wa Twitter wa picha isiopendeza ya mkewe Cruz Heidi. Bwana Trump amesema kuwa amechukuliwa vibaya na viongozi wa chama cha Republican.

Tuesday, March 29, 2016

Meneja wa kampeni ya Donald Trump ashtakiwa

Meneja wa kampeni ya mgombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump , ameshtakiwa kwa kumshambulia mwandishi wa habari katika mkutano wa kampeni. Bwana Corey Lewandowski ameshtakiwa kwa shambulio dhidi ya aliyekuwa mwandishi wa Breitbart Michelle Fields. Mnamo tarehe 8 mwezi Machi Bwana Lewandowski alimvuta na kumuangusha chini alipojaribu kuuliza swali na kujeruhiwa mkono. Bwana Lewandowski anapanga kukana shtaka hilo,ilisema timu ya kampeni za bwana Trump

Obama: Wanahabari ndio waliomjenga Trump

Rais Barack Obama wa Marekani amelaumu vyombo vya habari kwa kukua kwa umaarufu wa mgombea wa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump. Akihudubia hafla maalum kwaajili ya waandishi wa habari wa siasa bw Obama alisema sharti waandishi wa habari nao wawajibike kwani haitoshi tu ''kumpa mtu kinasa sauti '' Bwenyenye huyo mbishi ambaye alijenga jina lake na kupata utajiri mkubwa kutokana na kuendesha na kumiliki migahawa katika maeneo mengi tu duniani anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican kuwania urais. Trump, na wapinzani wake wanaowania tikiti ya chama chao cha Republicans wameratibiwa kukabiliana katika mdahalo wa runinga baadaye leo usiku. Shirika la habari la CNN linaanda madahalo huo kabla ya kura za mchujo za jimbo la Wisconsin zinazoratibiwa kufanyika juma lijalo. Japo hakumtaja Trump kwa jina ilikuwa bayana kuwa ndiye aliyelengwa na ujumbe wa Obama. Japo hakumtaja Trump kwa jina ilikuwa bayana kuwa ndiye aliyelengwa na ujumbe wa Obama. Anaposafiri ughaibuni, Obama anasema watu humuuliza nini kinachoendelea katika siasa za Marekani kwani' sio mahali unakotarajia siasa zisizokuwa za kawaida'' Wanasiasa waandishi habari na umma kwa jumla wana wajibu wakati wa siasa kali kama hizi zinazoshuhudiwa kwa sasa Marekani. Aliwashauri waandishi habari kupiga msasa habari wanazochapisha. Haiwezekani kuwa mwanasiasa anaahidi vitu ambavyo tunajua wazi kuwa hawezi kutimiza ilahali anaendelea kupeperushwa hewqani ,lazima nanyi mchukue jukumu la kuuliza maswali magumu na kutofautisha mbivu na mbichi. Katika siku za hivi punde Trump alikashifiwa na wapinzani wake kwa kumgoa mkewe mpinzani wake ambaye ni gavana wa jimbo la Texas Ted Cruz. Trump atakabiliana na mpinzani wake mkuu Ted Cruz katika uchaguzi wa jimbo la Wisconsin Aprili tarehe 5.

Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC

Tanzania imehuzunishwa na hatua ya bodi ya shirika la changamoto za milenia (MCC) kusitisha msaada Tanzania imehuzunishwa na hatua ya bodi ya shirika la changamoto za milenia (MCC) kusitisha msaada wake wa awamu ya pili wa dola milioni 472.8 ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja pesa za Tanzania. Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga ameelezea kushtushwa kwake na hatua hiyo ya bodi ya MCC akisema "imepuuza hatua kubwa tu zilizopigwa kidemokrasia" nchini humo. ''Inasikitisha kuwa demokrasia yetu inatathminiwa tu na matokeo ya uchaguzi wa visiwani Zanzibar,'' Kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar Bw Mahiga anasema kuwa Tanzania, ilifanya kila kitu kuambatana na sheria na katiba ya nchi wala hakuna tatizo ama ukiukwaji wa sheria. Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) yafuta msaada kwa Tanzania Mabalozi wakashifu uchaguzi wa Zanzibar Mahiga anasema kuwa huo ni uamuzi wao na kwa sababu hela hizo ni zao wanauhuru wa kuzitumia watakavyo ila anahoji kwanini uamuzi huo uliafikia bila ya majadiliano na serikali ya muungano ya Tanzania. Bw Mahiga amesisitiza kuwa Tanzania ilifwata katiba yake kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar Kuhususiana na kupitishwa kwa sheria ya uhalifu wa mitandao bwana Mahiga anasema sheria hiyo ilikuwa inalenga kupambana dhidi ya ugaidi. Waziri huyo ameonya kuwa watu wanaoishi vijijini ndio watakaoathirika zaidi kwani fedha hizo zilikuwa zimepangiwa kueneza umeme mashinani. Katika kutoa uamuzi wake, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ilisema kuwa Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili. Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote Kupitia taarifa, bodi hiyo ilisema kuwa: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa sheria ya Uhalifu wa Mtandao.” Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”

Monday, March 28, 2016

Let yourselves be moved by hope, Pope says at Easter Vigil

Vatican City, During the Easter Vigil, Pope Francis told attendees not to be overcome by sadness in the face of life’s difficulties, but to be open to hope, which is not the absence of problems, but is a gift from God when we allow him to enter our lives. “We, like Peter and the women, cannot discover life by being sad, bereft of hope,” the Pope said March 26. He urged the faithful not to “stay imprisoned within ourselves, but let us break open our sealed tombs to the Lord so that he may enter and grant us life. Let us give him the stones of our rancor and the boulders of our past, those heavy burdens of our weaknesses and falls.” As we anticipate Jesus’ Resurrection from the dead, the first stone which must be moved aside is “the lack of hope which imprisons us within ourselves,” he said. The Pope then prayed that the Lord would free us from the trap of being “Christians without hope, who live as if the Lord were not risen, as if our problems were the center of our lives.” Pope Francis spoke to the thousands present inside St. Peter’s Basilica for the Easter Vigil, which is celebrated the night before Easter in anticipation of Jesus’ rising from the dead. The vigil began in the atrium of the basilica with the traditional blessing of the fire and the preparation of the Easter candle. The Pope then led a procession with the lit candle to the main altar, where he continued with the rest of the Mass. In the course of the celebration, Francis administered the Sacraments of Christian Initiation – Baptism, Confirmation and the Eucharist – to 12 newcomers in the Catholic Church, hailing from Italy, Albania, Cameroon, Korea, India and China. Those being baptized included Yong Joon Lee, the Korean ambassador to Italy, and his wife Hee Kim. In his homily, the Pope noted how the women in the Gospel, after going to anoint Jesus' body, had run to the disciples and told them about how they had found the tomb empty. Peter and the others did not initially believe the women, yet Peter ran to the tomb anyway, he said. “There was doubt in Peter’s heart, together with many other worries: sadness at the death of the beloved Master and disillusionment for having denied him three times during his Passion,” he said. But still, something in Peter’s behavior had changed. Instead of staying sedentary and remaining at home with the others, Peter rose, refusing to succumb to the somber atmosphere in the days following Jesus’ death or to be overcome by his doubts. Peter, the Pope said, “was not consumed by remorse, fear or the continuous gossip that leads nowhere.” “He was looking for Jesus, not himself. He preferred the path of encounter and trust. And so, he got up, just as he was, and ran towards the tomb from where he would return amazed.” This, Francis observed, “marked the beginning of Peter’s resurrection, the resurrection of his heart.” Without giving in to sadness or darkness, Peter “made room for hope: he allowed the light of God to enter into his heart, without smothering it.” Like Peter, the women also had the same experience of awe when they went to Jesus' tomb with oil and met the angel, who told them that the Lord had risen, Francis said, adding that like them, we can't allow ourselves to be overcome by a lack of hope. Pope Francis stressed that there will always be problems “both within and without,” which won’t go away. What’s important, he said, is to place them in the light of the Risen Lord, “and in a certain sense, to evangelize them.” The resurrection of the Lord is “the foundation of our hope,” he said, clarifying that this hope is neither “mere optimism, nor a psychological attitude or desire to be courageous.” Rather, he said, Christian hope “is a gift that God gives us if we come out of ourselves and open our hearts to him.” Hope will never disappoint us because we have been given the Holy Spirit, the Pope said, noting that the Spirit doesn’t seek to make things look appealing or “remove evil with a magic wand.” The Holy Spirit, he said, “pours into us the vitality of life, which is not the absence of problems, but the certainty of being loved and always forgiven by Christ, who for us has conquered sin, death and fear.” Pope Francis emphasized that each person, after having met Jesus, is then sent out by him to proclaim the Easter message, and “to awaken and resurrect hope in hearts burdened by sadness, in those who struggle to find meaning in life.” However, he cautioned that we shouldn’t proclaim ourselves, but must rather be “joyful servants of hope” who announce the Risen Lord through our lives and the ways in which we love. “Otherwise we will be only an international organization full of followers and good rules, yet incapable of offering the hope for which the world longs,” he said. Francis concluded his homily by telling attendees that their hope can be strengthened by following the angel’s advice to the women in the Gospel: “Remember what [Jesus] told you.” He urged them to always remember Jesus’ words and deeds, “otherwise we will lose hope.” He urged everyone to “open our hearts to hope and go forth,” praying that the constant memory of Jesus’ works and words would be “the bright star which directs our steps in the ways of faith toward the Easter that will have no end.”

Zaidi ya 69 wafa kwa mlipuko Pakistani

Zaidi ya watu sitini na tisa wamekufa na wengine kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye eneo la wazi la kupumzikia lenye shughuli nyingi katika mji wa Lahore nchini Pakistan. Polisi wanasema mlipuaji mwenye kujitoa mhanga alijilipua karibu na eneo la kuchezea watoto mahali wazazi walipokuwa wamejikusanya ambao baadhi yao walikuwa wakisherehekea siku kuu ya Pasaka. Wengi ya waliokufa na kujeruhiwa katika tukio hilo ni watoto. Tayari kundi la Talbani la Pakistan la Jamaat ul Ahrar limekiri kuwa ndilo linalohusika na shambulizi hilo. Msemaji wa kundi hilo amesema walikusudia kuwalenga Afzal ni mmoja ya wakazi wa mji wa Lahore yeye alikuwa ni miongoni mwa waliosaidia kuwasaidia majeruhi baada ya mlipuko kutokea. " Nimewabeba zaidi ya watoto ishirini ambao walipelekwa hosptalini. Nilisaidia kubebe miili mitatu na kupakia kwenye gari la polisi. Wakati mlipuko ulipokuwa unatokea watoto walikuwa wakicheza kwenye uwanja huo wa wazi. Leo jamii ya wakristo walimaliza mfungo na kusherehekea Pasaka. Wakristo wengi walifika hapa katika tukio hili. Siwezi kuelezea jinsi tukio hilo la kusikitisha lilivyokuwa." Naye Tariq Fatimi ambaye ni mshauri wa Waziri Mkuu wa Pakistani ameiambia BBC kuwa tukio hilo ni la kinyama bila kujali ni nchi gani imelengwa. " Hata kama shambulizi hilo limetokea Peshawar au Lahore au Brussels au Paris au London, Sisi sote tunapaswa kuwa pamoja kwa sababu huu ni uhalifu ambao hauathiri nchi moja pekee, au jamii moja lakini inaathiri wanadamu wote."

Sunday, March 27, 2016

Iran yakana kuidukua Marekani

Iran imekanusha kuwa iliidhinisha mashambulio ya mitandao dhidi ya Marekani, baada ya mahakama mjini New York, kuwashtaki raia saba wa Iran, kwa kufanya udukuzi huo. Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Iran, (Hossein Jaberi Ansari), alieleza kuwa Marekani haina haki ya kushtaki raia wa nchi nyengine, bila ya kutoa nyaraka za ushahidi. Alisema Marekani yenyewe ina historia ya kufanya udukuzi dhidi ya Iran. Wadukuzi hao wameshtakiwa kwa mashambulio kwenye mitandao ya mabenki kadha ya Marekani, na bwawa la New York, baina ya mwaka 2011 na 2013. Washtakiwa wote wanaishi Iran, na waandishi wa habari wanasema, haikuelekea kuwa watapelekwa Marekani kukabiliwa na mashtaka

Sanders apania kupunguza uongozi wa Clinton US

Bernie Sanders apania kupunguza uongozi wa Clinton Mbombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Democrat Bernie Sanders atajaribu kupunguza uongozi wa Hillary Clinton katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea wa chama cha Democrat siku ya Jumamosi katika kura za Hawaii na Alaska katika jimbo la Washington. Bwana Sanders bado hajakata tamaa lakini Hillary tayari amejishindia wajumbe 1691 kati ya wajumbe 2,383 wanaohitajika kushinda. Bado anaendelea kuvutia makumi ya maelfu katika mikutano yake ya kampeni huku akiitisha mageuzi ya kisiasa . Bi Clinton amesema kuwa ana kura milioni 2.6 zaidi ya Sanders.Kura ya Jumamosi ni ya wagombea wa chama cha Demokrat pekee . Bwana Sanders ametumia wiki yote akiwa magharibi mwa pwani akitafuta uungwaji mkono miongoni wale wanaounga mkono mabadiliko na wale wa mrengo wa kushoto.

Wagombea warushiana matusi Marekani

Wagombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican Ted Crus na Donald Trump walirushiana cheche za matusi katika mjadala Wagombeaji wawili wa Urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamegombana vikali na kurushiana matusi juu ya wake zao. Seneta wa Texas, Ted Cruz, amemlaumu mpinzani wake, mfanyabiashara Donald Trump kwa kuzusha uvumi kuwa yeye alikuwa mzinifu na kumdanganya mkewe, Heidi. Bwana Cruz alisema uvumi huo ni takataka na akasema kuwa anaelewa kuwa uvumi ulianzishwa na Bwana Trump ambaye alisema hastahili kuwa Rais. Bwana Trump alisisitza kuwa hakuhusika vyo vyote na uvumi huo. Mjadala wa wagombea urais nchini Marekani Mapema juma hili, Bwana Trump alimlaumu Seneta Cruz kwa kuweka picha za mkewe, Melania, akiwa uchi kwenye mtandao ili kumharibia sifa.

Rais kuongoza kwa muhula mmoja Benin

Rais mpya aliyechaguliwa nchini Benin, Patrice Talon, anasema anataka kupunguza muda wa rais anaoweza kuongoza, kuwa muhula mmoja tu wa miaka mitano. Bwana Talon, ambaye alimshinda waziri mkuu katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais juma lilopita...amesema muda mfupi wa uongozi utasaidia kile alichoelezea kuwa rais kuridhika na kutokuwa na hima akiongoza muda mrefu. Alisema atakuwa na mawaziri 16, karibu nusu tu ya idadi ya zamani. Rais anayestaafu, Thomas Boni Yayi, ametumikia mihula miwili. Msimamo wa rais mpya wa Benin ni tofauti na viongozi wengine wa Afrika, ambao hivi karibuni wameongeza muda wao wa uongozi.

Saturday, March 26, 2016

Kiongozi wa IS auwawa Syria

Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika itifaki ya kundi la wapiganaji la Islamic State ameuawa katika oparesheni iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu, vyombo vya habari vya Marekani vimesema. Maafisa wa ulinzi wameliambia shirika la habari la NBC kwamba Abdul Rahman Mustafa al- Qaduli,raia wa Iraq anayejulikana kama Hajji Iman aliuwawa katika uvamizi mwezi huu. Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash Carter alitarajiwa kuthibitisha kifo cha mwana jihad huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo. Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli. Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu mwaka 2014. Alijiunga na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya uongozi wa marehemu Abu Musab al-Zarqawi akihudumu kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul kulingana na Marekani. Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.

Akamatwa kwa kuipelelezea Korea Kusini

Raia wa Marekani aliyekamatwa nchini Korea Kaskazini amesema kuwa aliiba siri za kijeshi za Korea kaskazini ili kuisaidia Korea Kusini katika taarifa na waandishi wa habari ilioandaliwa na Pyongyang. Kim Dong Chul mwenye umri wa miaka 62 alikiri kufanya hivyo siku ya ijumaa,akiomba msamaha kwa kupeleleza. Bwana Kim awali aliwaambia waandishi kwamba yeye ni raia wa Marekani aliyezaliwa nchini Korea Kusini na kwamba alikamatwa mwezi Oktoba kwa kufanya upelelezi. Bwana Kim amesema kwamba alikutakana na maafisa wa upelelezi kutoka Korea Kusini mwaka 2011 ili kuifanyia uchunguzi,kulingana na shirika la habari la KCNA kutoka nchini Korea Kaskazini. Alikamatwa wakati alipokuwa akichukua habari za kijasusi za kijeshi na zile za kinyuklia kutoka kwa mtu ambaye hakutajwa.

Friday, March 25, 2016

Imam wa Glasgow ampongeza muuaji

Kiongozi wa dini katika msikiti mkubwa wa Glasgow nchini Uskochi amempongeza mtu mmoja mwenye itikadi kali ambaye alinyongwa kwa kutekeleza mauaji nchini Pakistan. Imam Maulana Habib Ur Rehman wa msikiti wa katikati mjini Glasgow alitumia mtandao wa WhatsApp kumuunga mkono Mumtaz Qadri. Qadri alinyongwa mnamo mwezi Februari baada ya kumuua mwanasiasa mmoja ambaye alipinga sheria kali ya kufuru. Katika taarifa Imam huyo alisema kuwa ujumbe huo ulieleweka vibaya. Alisema kuwa alikuwa anatoa maoni yake yanayopinga watu kunyongwa. Katika Ujumbe ulioonekana na BBC ,imam Maulana Habib Ur Rehman anasema ''amekasirishwa'' na ''kusumbuliwa'' kuhusu habari za kunyongwa kwa Qadri,na baadaye kuandika ''rahmatullahi alai'' ikiwa ni baraka za kidini zinazopewa mtu anayefuata dini. Katika ujumbe mwengine anasema ''siwezi kuficha uchungu wangu leo''. Mwislamu wa haki aliadhibiwa kwa kufanya kile amacho taifa zima lilishindwa kukifanya. Qadri aliajiriwa kama mlinzi wa gavana wa mkoa wa Punjab nchini Pakistan Salman Taseer kabla ya kumgeukia mwaka 2011 na kumpiga risasi mara tisa. Baada ya kumpiga risasi Qadri alidaiwa kuwaambia waandishi kwamba anafurahia alichofanya na kwamba amemaliza ''kufuru''.

Washukiwa sita wakamatwa Brussels

Polisi wamekuwa wakiwasaka washukiwa wa ugaidi Ubelgiji na Ufaransa Polisi nchini Ubelgiji wamewakamata washukiwa sita mjini Brussels huku uchunguzi ukiendelea kuhusu mashambulio ya Jumanne yaliyosababisha vifo vya watu 31. Watu hao walikamatwa katika mtaa wa Schaerbeek. Polisi bado hawajatoa majina yao na pia hawajasema iwapo walihusika katika mashambulio hayo. Kwingineko Ufaransa, mshukiwa ambaye inasadikika alikuwa akipanga shambulio amekamatwa karibu na mji wa Paris, maafisa wamesema. Mashambulio hayo ya Brussels yamehusishwa na mashambulio ya Paris ya Novemba mwaka jana. Kundi linalojiita Islamic State (IS) limekiri kutekeleza mashambulio yote mawili. Kwa Picha: Mashambulio ya Brussels Mchezaji wa DR Congo anusurika Brussels Watu waliokamatwa mtaa wa Schaerbeek walikamatwa baadaye Alhamisi, na walinaswa baada ya msako wa nyumba kwa nyumba katika eneo hilo. Wakazi walisema walisikia milipuko wakati wa msako huo wa polisi lakini chanzo chake hakijabainika. Aidha, Alhamisi jiobi polisi wa Ufaransa nao walifanya msako katika mtaa wa Argenteuil, kaskazini magharibi mwa Ufaransa baada ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo ambaye inadaiwa alikuwa anapanga shambulio Waziri wa usalama Bernard Cazeneuve alisema mshukiwa huyo, mwenye asili ya Ufaransa, alikuwa kwenye hatua za mwisho za kutekeleza mpango wake, na kuongeza kwamba bado hakujapatikana uhusiano kati yake na mashambulio ya Brussels au ya Paris. Watu 130 walifariki Novemba mwaka jana baada ya wanamgambo kushambulia maeneo kadha mjini Paris.

Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu

Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameosha miguu ya wahamiaji waislamu mjini Rome katika tukio la unyenyekevu linaloambatana na itikadi ya kuanza kwa msimu wa Pasaka. Papa Francis alitembela makao ya wahamiaji, mjini Roma na kuendesha misa ya kuanza kwa msimu wa pasaka. Ziara yake katika kituo hicho cha kutathmini uhalali wa wahamiaji cha (Castelnuovo di Porto), inawadia huku uhasama na taharuki ikienea kote barani ulaya kuhusiana na kuwepo kwa wahamiaji waislamu hususan kufuatia mauaji ya Paris mwezi Novemba na ya hivi punde huko Brussels Ubelgiji. Papa Francis alikashifu mauaji yaliyotokea Ufaransa na Ubelgiji akisema kuwa hizo ni njama za watu wenye kiu cha kumwaga damu ya binadamu. Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alilaumu mtazamo wa watuhumiwa hao kuhusu maafa waliyosababisha. Aidha papa mtakatifu aliwashauri watu wa dini tofauti duniani kuishi kwa amani. ''Haijalishi iwapo tunaimani tofauti la muhimu kwetu sote ni tuishi kwa amani sisi ni ndugu alisema papa mtakatifu.

Thursday, March 24, 2016

Wabunge wahojiwa Takukuru

SIKU moja baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, kupangua wenyeviti na makamu wenyeviti kwa kuwaondoa kwenye kamati walizokuwa wanaziongoza, hatimaye Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), imewahoji wabunge watatu ambao wanatajwa kuhusika na mgawo wa fedha. Uamuzi huo umekuja baada ya gazeti la MTANZANIA kuripoti hatua ya baadhi ya wabunge kuhongwa fedha na baadhi ya mashirika ya umma. Taarifa kutoka ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zililiambia MTANZANIA kwamba tangu juzi baada ya kuripotiwa kwa taarifa hiyo maofisa wa taasisi hiyo wamekuwa na kibarua cha kuwahoji wabunge hao. “Ni kweli tumewahoji wabunge watatu hadsi sasa kutokana na tuhuma za rushwa na suala hili tunalichukulia uzito wa pekee kwani Bunge ni mhimili unatakiwa kuwa safi. “… siwezi kuwataja kwa sasa kwani hatua hii inaweza kuharibu uchunguzi wetu ambao kwa sasa upo katika hatua za awali na tunaamini tunaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na wale ambao watabainika tutawafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria,” alisema mmoja wa maofisa wa Takukuru ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. Juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai, alifanya mabadiliko ya baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge huku akiwaondoa wenyeviti na makamu wevyeviti watano katika kamati walizokuwa wakiziongoza. Katika mabadiliko hayo yaliyowagusa jumla ya wabunge 27, Spika Ndugai, ametoa maelekezo ya kujazwa kwa nafasi zilizoachwa wazi za wenyeviti na makamu wenyeviti walioguswa na panga pangua hiyo na kusititiza utekelezaji wa maagizo yake kuanza mara moja. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Bunge, Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Umma, uamuzi wa Spika umezingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuundwa kwa Kamati za Bunge hapo Januari mwaka huu. Taarifa hiyo ilieleza kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa Spika ya kuteua wabunge na kuunda kamati za Bunge, alizingatia kanuni ya 116 (3) ya kanuni za kudumu za Bunge kuwaondoa viongozi watano wa kamati na kwamba kamati ambazo zitaathirika na uamuzi wake zitapaswa kufanya uchaguzi wa viongozi walioondolewa kwa mujibu wa kanuni ya 116 (10) ya kanuni za kudumu za Bunge. Wenyeviti walioguswa la rungu la mabadiliko yaliyofanywa na Spika Ndugai ni Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata (CCN) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini aliyehamishiwa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), ambaye alikuwa Mwenyekitiwa Kamati ya Uwekezaji na Mitaji (PIC), aliyehamishiwa kamati ya Katiba na Sheria. Mwingine ni Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Mary Mwanjelwa (CCM), ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ambapo amejikuta akihamishiwa kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Makamu wenyeviti walioondolewa kwenye kamati zao ni Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni (CCM), ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), ambaye aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC). Sambamba na hao, wabunge wengine 22 nao wamehamishwa kutoka kamati walizokuwa kwenda katika kamati nyingine. Taarifa za Bunge ambazo gazeti hili limezipata zimeeleza kuwa mabadiliko hayo yamelenga kuwaondoa waliokuwa wakilalamikiwa kuhusu mienendo yao ya kikazi kwenye kamati walizokuwa, huku wengine wakihamishwa kwa ajili ya kwenda kujenga taswira mpya ya kamati zinazonyooshewa vidole. MTANZANIA lilikariri taarifa za kibunge zilizoeleza kuwa taasisi zilizofikiwa na wabunge wanaotuhumiwa kuombwa rushwa kuwa ni Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura). Ndugai afafanua Jana Spika Ndugai, alitoa ufafanuzi katika Kituo cha Redio cha Clouds FM, wakati akizungumzia suala la kujiuzulu kwa wajumbe wawili na tuhuma za rushwa. Alisema wao kama Bunge suala hilo wataliachia mamlaka zenye dhamana ya kuchunguza tuhuma hizo na uchunguzi ukikamilika taarifa zitatolewa. “ Nimepokea barua za wabunge wawili wa kamati ambao wameomba kujiuzulu nimeshangazwa na kujiuzulu kwao kwa kuwa wao hawajatuhumiwa… nitazipitia barua zao na kuzitolea majibu,”alisema Ndugai. Alisema jana wangewaita wabunge hao ili kuweza kusikiliza hoja zao na wao kama Bunge hawafanyi uchunguzi wowote kuhusu hali hiyo. “Sisi kama Bunge hatufanyia uchunguzi wowote dhidi ya mbunge yoyote kwa sasa ila vyombo vya dola vinaweza kuwa na utaratibu huo sasa au baadaye kidogo. “Hata wakichunguza hawaripoti kwa Spika ila tunawaomba Watanzania wazidi kuwa na imani na Bunge lao na watuombee na tunaamini Bunge la 11 litawafanyia kazi vizuri,” alisema Spika Ndugai. Alisema suala la mabadiliko ya kamati ni la kawaida kama ilivyo kwa timu ya mpira kwa lengo la kuimarisha timu. Makosa ya kususia vikao Baada ya taarifa hizo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Dk. Chegeni naye juzi aliwasilisha dokezo la kamati yake ofisini kwa Spika lililoeleza kuwa kamati yake iliyokutana jana katika ukumbi wa Saadan uliopo jengo la LAPF, Kijitonyama baada ya kumaliza majukumu yake ya kibunge ilijadili tuhuma za rushwa ilizoelekezewa. Dokezo hilo lilieleza kusikitishwa na tuhuma hizo na kwamba wajumbe waliazimia kulitaka Bunge kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo na kwamba kuanzia jana wanasitisha kufanya kazi yoyote ya kamati hadi uchunguzi utakapokamilika. Kutokana na hali hiyo Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya, alisema ni kosa kisheria wabunge kusitisha shughuli za Kamati za Bunge bila idhini ya Spika. Mwandumbya aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kuhusu Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kulitaka Bunge kufanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wenyeviti wa kamati mbalimbali ambapo tuhuma hizo zilisababisha wenyeviti kusimamishwa wadhifa huo hali iliyoifanya kamati hiyo kudai kuwa watasitisha shughuli za kamati kuanzia juzi Mwandumbya, alisema mwenye mamlaka ya kusitisha vikao vya Kamati ya Bunge ni Spika pekee yake kwa mujibu wa sheria huku akielezea kazi za mbunge kuwa ni pamoja na ushiriki wa vikao vya kamati. “ Mbunge yoyote moja ya majukumu yake ni kushiriki kwenye kamati …hivyo kitendo cha kusitisha vikao bila idhini ya spika ni kosa kisheria,” alisema Mwandumbya. Alisema pamoja na hali hiyo kamati hiyo jana iliendelea na shughuli zake kama kawaida na waliongozwa na mwenyekiti wa muda, hivyo hakuna taarifa walizopata za kusitisha kikao. Alisema kuhusu suala la Mbunge wa Kigoma Mjini , Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), kuandika barua za kujiuzulu ili kupisha uchunguzi dhidi ya wenyeviti wanaotuhumiwa kwa rushwa alisema Spika Ndugai, amepokea barua zao na atazitolea majibu. “Spika amepokea barua zao atatoa majibu na mbunge anayesusia shughuli za kamati anakaidi shughuli halali za Bunge ,”alisema Mmwandumbya. ACT-Wazalendo na uchunguzi Nacho Chama cha ACT-Wazalendo kimesema uamuzi wa kuwahamisha kamati viongozi na wajumbe wa kamati zilizotuhumiwa kupokea rushwa hautoshi. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wa Spika wa Bunge kufanya mabadiliko ya baadhi ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa, Yeremia Maganja, alisema kuwa ACT- Wazalendo haikubaliani na uamuzi huo kutokana na kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuendeleza utamaduni mbovu. Alisema kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge ndiyo chombo kikuu chenye madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake katika utekelezaji wa majukumu yake.Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Mchina akiri kuiba siri za Marekani

Miongoni mwa siri nyingine, Su na wenzake walisaka siri kuhusu ndege aina ya F-22 Mwanamume mmoja kutoka Uchina amekiri kuhusika katika njama ya kuiba siri kuu kuhusu mifumo ya kijeshi ya Marekani. Su Bin anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita, ndege za kubeba mizigo na silaha. Wizara ya haki ya Marekani imesema kupitia taarifa kwamba Bw Su alilenga kufaidi kifedha. Bw Su, mwenye umri wa miaka 50, alikamatwa akifanya kazi nchini Canada mwaka 2014. Alidaiwa kuwa na kampuni ya Kichina ya teknolojia ya uchukuzi wa ndege iliyokuwa na afisi Canada na alikamatwa akijaribu kupata uraia wa Canada. Alikiri kufanya kazi na watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la Marekani kuunda ndege zake. Sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela na faini ya $250,000 (£170,000).

Afisa mwingine wa jeshi auawa Burundi

Afisa mwengine wa ngazi ya juu katika jeshi la Burundi ameuwawa usiku wa jana katika hali ya kutatanisha katikati mwa jiji la Bujumbura. Meja Didier Mihimpundu ameuawa saa chache baada ya kuuawa kwa kamanda wa kambi moja muhimu mjini Bujumbura Kanali Darius Ikurakure akiwa kwenye makao makuu ya jeshi mjini Bujumbura . Kamanda wa kambi ya Bujumbura Kanali Darius Ikurakure ameuawa Meja Didier Muhimpundu aliuawa karibu saa mbili ya usiku . Polisi wanasema alipokea simu na kuondoka ndani ya baa moja mjini Bujumbura kabla ya kufyatuliwaa risasi. Uhasama nchini Burundi ulianza baada ya rais Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wa tatu Hadi sasa waliomuuwa afisa huyo aliyekuwa msimamizi wa idara ya afya ya jeshi , hawajafahamika kwa mujibu wa naibu msemaji wa polisi Moise Nkurunziza. '' Meja Muhimupundu alipigiwa simu na mtu akiwa katika baa, halafu alipotoka kutaka kukutana na mtu huyo, wakampiga risasi, na akafariki papo hapo,'' ''Uchunguzi umeanzishwa kujua vema watu hao waliofanya ukatili huo , na hivo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria kuadhibiwa. alisema Nkurunziza. Saa moja kabla ya Meja Muhimpundu kuuwawa, kulisikika milio ya risasi Kaskazini mwa jiji katika mtaa wa Carama . Wakaazi sehemu hiyo wanathibitisha polisi mmoja aliuwawa katika ufyatulianaji huo wa risasi. Katika kipindi cha miezi minane , maafisa wakuu jeshini wasiopungua watano wameuawa katika jiji la Bujumbura Hata hivo polisi imekanusha taarifa hizo na kutaja kuwa alitekwa. '' Polisi huyo alitekwa na watu waliokuwa katika gari la watu binafsi, ambao walikuwa wamevalia sare za kijesh.'' ''Taarifa za kuuliwa kwake si sahihi hazina ukweli maana haijaonekana maiti yake'' alisema msemaji wa polisi Nkurunziza. Awali jana mchana aliuwawa Kamanda wa kambi moja muhimu ya kijeshi hapa nchini Luteni Kanali Darius Ikurakure akiwa ndani ya makao makuu ya jeshi hapa mjini Bujumbura. Mauaji hayo ya mfululizo yameanza kutafsiriwa kama ulipizanaji kisasi katika jeshi lenye mchanganyiko wa makabila na kutishia uwiano wa vikosi vya ulinzi. Mauaji hayo ya mfululizo yameanza kutafsiriwa kama ulipizanaji kisasi katika jeshi Msemaji wa Jeshi Clement Cimana .ameonya kuhusu hali hiyo'' Makao Makuu ya jeshi yanalaani vikati ukatili wowote wa aina hii,uongozi wa jeshi unawatolea wito wanajeshi popote walipo kubaki wanashikamana na kuwaepuka watu wanaojaribu kuwagawanya kwa lengo la kusambaratisha jeshi la Burundi.'' Katika kipindi cha miezi minane , maafisa wakuu jeshini wasiopungua watano wameuawa katika jiji la Bujumbura, lakini mauaji ya sasa yameibuka baada ya siku kadhaa za utulivu nchini.

Wednesday, March 23, 2016

Marekani yatahadharisha raia wake Ulaya

Polisi Ubelgiji wanawasaka washukiwa zaidi maeneo mbalimbali Marekani imewaonya raia wake walio Ulaya na wanaopanga kuzuru bara hilo kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulio mengine ya kigaidi. Tahadhari hiyo imetolewa baada ya mashambulio kuua watu 34 katika mji wa Brussels Jumanne. Wizaya ya mashauri ya kigeni ya Marekani imesema makundi ya kigaidi huenda yakatekeleza mashambulio karibuni. “Makundi ya kigaidi yanaendelea kupanga mashambulio ya kuteketelezwa karibuni kote Ulaya, yakilenga hafla za michezo, maeneo ya kitalii, migahawa na uchukuzi,” taarifa ya wizara hiyo ilisema. Raia wa Marekani wanaozuru Ulaya wametakiwa kuwa macho zaidi maeneo yenye watu wengi au wanapotumia mifumo ya uchukuzi wakati wa sikukuu ya Pasaka. Miji mingi Marekani imeimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege na vituo vya treni na mabasi. Serikali hata hivyo imesema bado haina habari za uhakika kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulio Marekani. Washukiwa wanaodaiwa kutekeleza shambulio uwanja wa ndege wa Zaventem Kundi linalojiita Islamic State (IS) limedai kuhusika katika mashambulio Brussels. Taarifa iliyopakiwa mtandaoni na kundi hilo ilisema maeneo hayo yaliyoshambuliwa “yaliteuliwa kwa umakinifu mkubwa” na kuonya kuwa kutatokea mabaya zaidi kwa mataifa yanayopinga kundi la Islamic State.

Burundi: Mkuu wa jeshi auawa kambini

Afisa mmoja muandamizi wa jeshi la Burundi ameuwawa leo ndani ya makao makuu ya jeshi la Burundi. Kanali Darius Ikurakure alikuwa Kamanda wa kambi ya kijeshi ya Muzinga, nje kidogo ya jiji la Bujumbura. Kambi ya Muzinda iko kilomita 30 kutoka mji mkuu wa Bujumbura. Kanali Ikurakure alikua msatari wa mbele katika harakati za kuzima maandamano na ghasia dhidi ya rais Pierre Nkurunziza Kanali Ikurakure alikua msatari wa mbele katika harakati za kuzima maandamano na ghasia zilizotokea baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu mamlakani. Duru kutoka kwa jeshi la burundi zinasema kuwa kanali huyo alipigwa risasi na mwanajeshi mwenza.

Obama amtaka Castro asiiogope Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama ameeleza matumaini yake kwamba hali ya Cuba itaimarika, kwenye hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga. Kiongozi huyo wa Marekani, ambaye ndiye wa kwanza kuzuru Cuba akiwa bado madarakani katika kipindi cha miaka 88, alitoa hotuba hiyo kutoka ukumbi wa Grand Theatre mjini Havana. Bw Obama alisema alifika Cuba “kuzika masalio ya Vita Baridi” na miongo mingi ya uhasama. Alimwambia Rais wa Cuba Raul Castro kwamba hafai kuiogopa Marekani na pia hafai kuogopa “usemi wa watu wa Cuba”. Obama na Castro wajibizana Cuba Bw Obama alisema wakati umefika kwa Marekani na Cuba kuacha nyuma yaliyopita na kusonga mbele “kama marafiki na majirani na kama familia, pamoja” kwa siku za usoni zenye ufanisi. Jumatatu, viongozi hao walijibizana kwenye kikao na wanahabari Amewataka raia wa Cuba kuacha nyuma vita vya kifalsafa na kujieleza sio kwa kupinga Marekani bali kwa kujieleza wao binafsi ama raia wa Cuba. "Licha ya siasa hizi zote, watu ni wale wale na Wacuba ni Wacuba,” alisema. Aidha, amehimiza kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara vilivyowekewa nchi hiyo na Marekani miaka 54 iliyopita. Tamko hilo lilishangiliwa sana na raia wa Cuba. Ni Bunge la Congress pekee linaloweza kuidhinisha kuondolewa kwa vikwazo hivyo. Bw Obama alikamilisha ziara yake ya siku tatu kwa kuungana na Rais Castro kutazama mechi ya besiboli uwanja wa Baada ya kuondoka Cuba, Bw Obama ameelekea Argentina siku ambayo inalingana na maadhimisho ya miaka 40 tangu kutokea kwa mapinduzi yaliyoingiza mamlakani utawala dhalimu wa kijeshi. Baadhi ya makundi yanapanga maandamano kushutumu Marekani ambayo inadaiwa kusaidia jeshi wakati wa mapinduzi hayo ya 1976.

Tuesday, March 22, 2016

Trump aahidi kuvunja mkataba wa nyuklia

Trump ndiye anayeongoza miongoni mwa wagombea wa Republican Mgombea Urais katika chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesema kuwa akichaguliwa kuwa Rais hatua ya kwanza atakayochukua juu ya masuala ya kigeni ni kuvunjilia mbali mkataba wa nyuklia. Mkataba huo ambao Trump anauzungumzia na kukerwa nao ni ule wa Marekani na Iran. Ushindi wa Trump ni hatari kwa dunia Iran yaanza kutekeleza mkataba wa nyuklia Bw Trump, ambaye kwa sasa yuko mstari wa mbele katika kinyang'anyiro hicho katika chama chake aliliambia kundi lenye ushawishi mkubwa linalounga mkono Israel kuwa mapatano hayo ya Iran ni hatari kwa Marekani. Amesema pamoja na madhara kwa Marekani lakini pia unaweza kuihatarisha Israel na Mashariki ya Kati.

Obama na Castro wajibizana Cuba

Rais Obama na mwenyeji wake Raul Castrol Rais Barack Obama na mwenyeji wake Raul Castrol wamejibizana kuhusu suala la haki za binadamu na vikwazo vya kibiashara baina ya Marekani na Cuba. Hata hivyo Rais Obama amehimiza Cuba kuendelea na mageuzi ya kisiasa na haki za binadamu kama inataka kurejesha ambao kwa miaka mingi umedorola baina ya mataifa hayo mawili. Katika siku ya pili ya ziara yake ya Kihisitoria nchini Cuba, rais Obama amesema kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo la Kikomonisti kutategemeana na uharaka wa mataifa hayo mawili kuondoa tofauti zao hasa katika suala la haki za binadamu. Obama amesema kuwa Marekani haioni kama Cuba ni tishio kwa Marekani na kwamba ziara yake nchini humo ina lengo la kuweka misingi mipya kati ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Rais Obama baada ya mazungumzo ya mjini Havana na mwenyeji wake Raul Castro, amesema kutokuwepo harakati za kupigania haki za binadamu nchini Cuba ni jambo litakalo mpatia ugumu kushawishi bunge la Congress kuondoa vikwazo vilivyopo dhidi ya Cuba.

Mabalozi wakosoa uchaguzi wa Zanzibar

Tume ya uchaguzi imesema asilimia 67.9 ya wapiga kura walijitokeza Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani wamekosoa uchaguzi wa marudio uliofanyika visiwani Zanzibar Jumapili. Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein ametangazwa mshindi wa uchaguzi huo na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Chama cha Wananchi (CUF) kilisusia uchaguzi huo. Mabalozi wa Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Uhispania, Sweden, Uswizi, Uingereza na Marekani wamesema uchaguzi huo haukufaa kufanyika bila ya kuwepo kwa maafikiano kuhusu suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani humo. “Ili uchaguzi uwe wa kuaminika, ni lazima ushirikishe wote na uwe unaakisi nia ya watu,” mabalozi hao wamesema kupitia taarifa. “Tunakariri wito wetu kwa Serikali ya Tanzania kutoa uongozi Zanzibar na kufanikisha suluhu kupitia mashauriano kati ya vyama, kwa lengo la kudumisha amani na umoja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mabalozi hao walionekana kutoa wito kwa Rais John Magufuli kusaidia katika utatuzi wa mzozo huo. Kiongozi huyo hata hivyo tayari amesema kwamba hataingilia mzozo katika visiwa hivyo. Shein Image caption Dkt Shein baada ya kupiga kura yake Bungi, Unguja Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na ZEC, Dkt Shein alipata kura 299,982 ambazo ni sawa na asilimia 91.4 ya kura zilizopigwa. Mgombea urais wa chama cha ADC Hamad Rashid Mohammed aliibuka wa pili na kura 9,734 (3.0%). Bw Seif Sharif Hamad wa CUF alipigiwa kura 6,076 (1.9%) licha ya kwamba chama chake kilisusia uchaguzi huo.

Monday, March 21, 2016

Obama afanya ziara ya kihistoria Cuba

Obama amesema ziara yake itatoa nafasi ya ushirikiano zaidi Rais wa Marekani Barack Obama ameanza ziara ya kihistoria nchini Cuba, akiwa ndiye rais wa kwanza wa Marekani kuzuru taifa hilo katika kipindi cha miaka 88. Ziara hii ya siku tatu ndiyo kilele cha mazungumzo ya miaka miwili yaliyonuia kurekebisha uhusiano kati ya Marekani dola kubwa zaidi duniani na jirani yake yenye mfumo wa ujamaa. Rais Obama atakutana na Rais Raul Castro. Punde baada ya kuwasili Obama alitembea kwenye barabara za mji wa kale wa Havana na pia kuwahutubia wafanyikazi wa ubalozi mpya wa Marekani. Kiongozi huyo amesisitiza ziara yake inatoa nafasi kushauriana na raia wa kisiwa hicho. Pia ameahidi kuangazia masuala ya haki za binadamu, kuwepo mageuzi ya kisiasa japo maafisa wa Cuba wamesema hakuna ajenda ya kujadili vile nchi hiyo inaweza kukubalia vyama vingi vya kisiasa. Cuba inataka zaidi kuondolewa vikwazo vyote vya kiuchumi na Marekani. Baada ya kuwasili Cuba, Rais Obama aliandika kwenye Twitter akiwasalimu raia wa Cuba na kusema anasubiri kukutana nao na kusikia kutoka kwao.

Sunday, March 20, 2016

Wacuba wajitayarisha kumpokea Obama

Serikali ya Cuba na wananchi wanamsubiri kwa hamu Rais Barack Obama akianza ziara yake ya kihistoria kisiwani humo siku ya Jumapili, akiwa rais wa kwanza wa Marekani kulitembelea taifa hilo jirani katika kipindi cha miaka 90 iliyopita. Wananchi wamegawika kutokana na ziara hiyo, baadhi wakiwa na matumiani kwamba ni tukio la kihstoria kupelekea kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani, na kuna wale wanaoamini hakuna kitakacho badilika chini ya utawala wa kikomunisti. Kuna Wacuba kama Yosleny Borroto, anaechukulia ziara hiyo ya kwanza na kiongozi wa Marekani tangu miana ya 1920 ni ishara ya mabadiliko makubwa katika nchi yake. "Amekua moja wapo ya marais wa Marekani wanaotaka kutusaidia.. kutusiadia ili nchi yetu ipate maendeleo." alisema Borroto. Rais Obama anafuatana na baadhi ya wafanyabiashara ikiwa ni ishara ya kuzungumzia masuala ya mikataba mipya ya biashara ingawa vikwazo vya kiuchumi vitaendelea kutekelezwa hadi bunge la Marekani kukubali kuviondowa Lakini wakati huo huo kuna Wacuba wenye wasi wasi kama Oscar Casanella Saint Blancard, anaehisi analengwa na serikali kutokana na urafiki wake na wapinzani. Ana hofu kwamba kuanzishwa kwa uhusiano kamili wa kidiplomasia kati ya Washington na Havana hautamanisha mabadiliko makubwa bali yake anadhani kutakua na matatizo zaidi. "Suala la kwanza, serikali ya Cuba itakua na tabia gani baada wa ziara, haitotosha kuondowa vikwazo hivyo vya marekani. Kwa sababu kuna vikwazo vya serikali ya Cuba dhidi ya watu wa Cuba, na ninadhani hivyo ndivyo hatari zaidi ." alisema Casanella. Nao wapinzani wakuu wa serikali wamefurahishwa na juhudi za rais Obama. Mpizani Miriam Leiva anasema akiweza kukutana na rais Obama basi atamuambia "nina kushukuru kwa sera zako kuelekea kisiwa chetu ambazo zitaleta afuweni kwa maisha ya Wacuba". Maafisa wa white House wanasema miongoni mwa vipaumbele vya ziara yake ni kukutaka na wanaharakati wanaotetea demokrasia huko Cuba.

Marudio ya uchaguzi chini ya ulinzi mkali Zanzibar

Visiwa vya Zanzibar vyenye mamlaka ya ndani nchini Tanzania Jumapili (20.03.2015)chini ya ulinzi mkali vimekuwa na marudio ya uchaguzi uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani cha CUF. Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ilibatilisha matokeo ya uchaguzi wa awali hapo tarehe 25 mwezi wa Oktoba kwa madai ya udanganyifu.Lakini wanadiplomasia wamesema hawakuona ushahidi wowote ule wa kuwepo kwa udanganyifu mkubwa unaodaiwa kutokea. Chama kikuu cha upinzani (CUF) kimesema kilikuwa kimeshinda uchaguzi huo na kimeonya juu ya uwezekano wa kuzuka ghasia katika visiwa hivyo vya bahari ya Hindi iwapo uchaguzi huo ungeliendelea kufanyika Jumapili. Chama cha CUF kimewahimiza wafuasi wake kuususia uchaguzi huo wa rais,wawakilishi na serikali za mitaa jambo linalomaanisha ushindi bwerere kwa chama tawala cha CCM. Vyama vingine vidogo vinashiriki uchaguzi huo lakini uchaguzi visiwani Zanzibar kwa kawaida unakuwa wa ushindani mkali kati ya CCM na CUF. Hali ya usalama ilikuwa imeimarishwa kwenye vituo vya kupigia kura.Chaguzi za nyuma visiwani humo zilikuwa zimechafuliwa na vurugu. Takriban vituo vingi vya kupigia kura vilikuwa vimefunguliwa kwa wakati hapo saa moja asubuhi ambapo wapiga kura waliunda misururu kwa amani lakini idadi ya walijotokeza kupiga kura inaonekana ni ndogo katika ngome za CUF ambapo wafuasi wa chama hicho wameitikia wito wa chama chao kuususia uchaguzi huo. Mfuasi wa chama tawala CCM ambacho kinaunga mkono marudio hayo ya uchaguzi Amina Hassan amesema " Nina furaha kupiga kura tena. Tutapata ushindi wa vishindo " Mwanachama wa upinzani Yussuf Juma ameupuzilia mbali uchaguzi huo kuwa ni wa kiini macho.Amekaririwa akisema "Ni kupoteza wakati na rasilmali kupiga kura tena.Tumewasikiliza viongozi wetu waliotutaka tusipige kura na tumeamu kuususia." Rais anayetetea wadhifa wake Ali Mohamed Shein alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kupiga kura katika kituo kilioko Mji Mkongwe mji mkuu wa Zanzibar ambao ni wa kihistoria. Shein amesema ana furaha kutumia haki yake ya kidemokrasia na kuongeza "sio sahihi kwa upinzani kususia lakini wana uhuru wa kufanya hivyo." Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imesema kumekuwa hakuna ucheleweshaji katika kuwasilishwa kwa visanduku na makaratasi ya kupigia kura na kwamba waangalizi wa uchaguzi wa ndani ya nchi na wale wa Afrika wako mahala pao isipokuwa wale wa Umoja wa Ulaya ambao hawakushiriki. Kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba visiwani Zanzibar kumekuja baada ya mgombea wa CUF Seif Sharrif Hamad kujitangaza mshindi kabla ya matokeo kutangazwa rasmi. Viongozi wa CUF wamesema hatua hiyo ilikuwa imesanifiwa ili kuzuwiya ushindi wa chama chao na kuipatia ushindi mwengine CCM ambacho kinahodhi madaraka Tanzania bara. Serikali ya Zanzibar ilipiga marufuku kwa muda usafiri wa baharini kati ya visiwa hivyo na Tanzania bara hapo Jumapili kwa kile maafisa wa serikali walichosema ilikuwa ni hatua iliokusudia kuhakikisha kwamba uchaguzi huo hauvurugwi. Takriban wapiga kura 500,000 visiwani Zanzibar walikuwa pia wakistahiki kupiga kura zao katika uchaguzi wa Oktoba kumchaguwa rais wa Tanzania na licha ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar,Rais mpya wa Tanzania John Magufuli aliapishwa mwaka jana. Vituo vya kupigia kura vinatazamiwa kufungwa saa kumi jioni na matokeo yanatarajiwa kutolewa hata Jumatatu.

Moja kwa Moja: Uchaguzi wa marudio Zanzibar

14:00 Wawafahamu wagombea wote wa urais walio kwenye karatasi za kura visiwani Zanzibar? Kuna wagombea 14. Majina yao ndiyo haya: 1 Khamis Iddi Lila ACT-W 2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA 3 Hamad Rashid Mohamed ADC 4 Said Soud Said AFP 5 Ali Khatib Ali CCK 6 Ali Mohamed Shein CCM 7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA 8 Seif Sharif Hamad CUF 9 Taibu Mussa Juma DM 10 Abdalla Kombo Khamis DP 11 Kassim Bakar Aly JAHAZI 12 Seif Ali Iddi NRA 13 Issa Mohammed Zonga SAU 14 Hafidh Hassan Suleiman TLP 13:00 Mji Mkongwe (Stone Town) ambao ni maarufu sana kwa watalii hauna watu wengi. Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela amepiga picha hizi zinazoonesha mtaa huo ukiwa kama mahame. 11:15 Mwandishi wa BBC Halima Nyanza aliyeko Zanzibar anasema idadi ya watu waliojitokeza katika baadhi ya vituo ni ndogo, tofauti na uchaguzi wa awali Oktoba 25, mwaka jana. Baadhi ya mitaa imeonekana kutulia huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika baadhi ya maeneo. 10:30 Mgombea urais wa chama cha ADC Hamad Rashid amepiga kura yake kituo cha Tondooni Wawi wilaya ya Chake-Chake, mkoa wa Kusini Pemba. Amesema: "Nina imani ya kuwa Rais, nikikosa nitakuwa Makamu wa Rais". 10:00 Mwanamke akitumbukiza kura kwenye kijisanduku kituo cha Kiembe, Samaki. Upigaji kura unaendelea. 08:50 Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein amezungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja. Mwanzo amezungumzia hatua ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi huo. Kuhusu amani na utulivu, amesema anaamini kutakuwa na utulivu visiwani. Hauhitaji Media PlayerPata usaidizi kuhusu Media PlayerBonyeza 'Enter' kuendelea au kurejea mwanzoni 08:13 Kumbuka, Chama cha Wananchi (CUF) kilitangaza kwamba hakitashiriki uchaguzi wa marudio unaoendelea leo. Chama hicho kinaamini kilishinda uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na mgombea wake Maalim Seif Hamad anafaa kutangazwa mshindi. Tume ya uchaguzi Zanzibar hata hivyo ilitangazwa kwamba hakuna aliyejiondoa rasmi kutoka kwa uchaguzi wa leo. Lubuva: Magufuli hafai kuingilia kati Zanzibar 08:00 Maafisa wa usalama wakishika doria mjini Chake kisiwani Pemba.

Saturday, March 19, 2016

Mripuko wa kujitowa muhanga wauwa watano Instabul

Watu watano akiwemo mripuaji wa kujitowa muhanga wameuwawa Jumamosi (19.03. 2016) katika shambulio linalotuhumiwa kufanywa na wanamgambo wa Kikurdi katika wilaya kuu ya utalii na maduka mengi katikati ya mji wa Istanbul. Polisi ya Uturuki yazingira mtaa wa Istiklal kufuatia mripuko Instanbul (19.03.2016) Polisi ya Uturuki yazingira mtaa wa Istiklal kufuatia mripuko Instanbul (19.03.2016) Mripuko huo wa kujitowa muhanga ambao ni wa nne nchini Uturuki mwaka huu umetokea katika mtaa wa Istiklal eneo kubwa la njia ya waendao kwa miguu ilioambatana na maduka ya kimataifa na ofisi zndogo za ubalozi wa nchi za kigeni mita chache tu kutoka mahala ambapo kwa kawaida polisi huegesha mabasi yao. Afisa wa mwandamizi wa Uturuki ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba uchunguzi wa awali unadokeza kwamba chama kilichopigwa marufuku cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) au kitengo kinachohusiana nacho kimefanya shambulio hilo. Afisa huyo amesema mshambuliji huyo aliripuwa bomu kabla ya kufika shabaha yake kutokana na kuwahofia polisi na kuongeza kwamba alikuwa amepanga kujiripuwa katika eneo lenye watu wengi zaidi. Polisi wenye silaha waliuzingira mtaa huo wa maduka ambapo magari kadhaa ya kubebea wagonjwa yalikuwa yamekusanyika.Helikopta za polisi zilikuwa zikizunguka juu ya anga la eneo hilo na watu walikuwa wakikimbia kwa hofu kwa kujipenyeza kwenye vichochoro pembezoni mwa mtaa huo. Gavana wa mji huo Vasin Sahin amesema mripuko huo umetokea nje ya ofisi ya serikali ya mitaa wakati waziri wa afya Mehmet Muezzinoglu amesema watu 36 wamejeruhiwa katika shambulio hilo wakiwemo wageni 12. Waziri huyo hakufafanuwa juu ya uraia wa wageni waliojeruhiwa lakini shirika la habari la kibinafsi la Dogan limesema takriban raia watatu wa Israel ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa wakiwemo watoto wawili.Nayo talevisheni binafsi ya NTV imesema raia mmoja wa Iran ni miongoni mwa majeruhi. Wengi wabakia nyumbani wakihofia usalama Mmojawapo wa wahanga wa shambulio la Ankara la mwezi wa Machi. Mmojawapo wa wahanga wa shambulio la Ankara la mwezi wa Machi. Mtaa wa Istiklal ambao kwa kawaida umechangamka na watu waliofurika kwa manunuzi ya mwishoni mwa juma leo ulikuwa tulivu kuliko ilivyo kawaida kutokana na kwamba watu wengi wamebakia majumbani kufuatia mfululizo wa mashambulizi yaliosababisha maafa. Mripuko wa kujitowa muhanga kwa kutumia gari umeuwa watu 37 mjini Ankara mwezi huu. Mripuko kama huo mwezi uliopita umeuwa watu 29 katika mji mkuu huo wa Uturuki.Kundi la wanamgambo wa Kikurdi limedai kuhusika na miripuko hiyo yote miwili. Mwezi wa Januari mshambuliaji wa kujitowa muhanga ameuwa takriban watu 10 wengi wao wakiwa ni watalii wa Kijerumani katika kitovu cha historia mjini Istanbul ambapo serikali inalilaumu kundi la Dola la Kiislamu kwa kuhusika. Uturuki ambayo ni mwanachama wa Jumuiya Kujihami ya NATO inakabiliwa na vitisho vingi vya usalama.Ikiwa kama sehemu ya ushirika unaoongozwa na Marekani nchi hiyo inapambana na kundi la Dola la Kiislamu katika nchi jirani ya Syria na Iraq. Pia inapambana na wanamgambo wa PKK wa chama cha wafanyakazi cha Kurdistan kusini mashariki mwa nchi hiyo ambapo usitishwaji wa mapigano wa miaka miwili na nusu umesambaratika mwezi wa Julai mwaka jana na kutibua matumizi ya nguvu mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa tokea miaka ya 1990. Vitendo vya kinyama Waziri wa Afya wa Uturuki Mehmet Muezzinoglu amesema "Sisi kama taifa kwa bahati mbaya hivi sasa tunakabiliana na ana kwa ana na hali isiokuwa na kikomo,vitendo visivyopimika ambavyo ni vya kinyama vyenye kukana maadili ya kibinadamu na vya usaliti." Katika kampeni yake ya matumizi ya silaha PKK kihistoria imekuwa ikishambulia vikosi vya usalama moja kwa moja na kusema kwamba haiwalengi raia katika mashambulizi hayo.Hata hivyo kutokana na mashambulizi yao ya hivi karibuni inaonyesha kwamba imekuwa ikibadili mbinu. Uturuki imeimarisha usalama mjini Ankara na Istanbul kuelekea tamasha la Newroz la majira ya machipuko hapo Machi 21 ambapo Wakurdi nchini Uturuki kwa jadi wamekuwa wakilitumia kuyakinisha utambulisho wao wa kikabila na kudai haki zaidi. Ubalozi mdogo wa Ujerumani ulioko katika wilaya ulikotokea mripuko umefungwa siku za hivi karibuni kwa sababu ya wasi wasi wa kiusalama.

It's official – Mother Teresa will be canonized September 4

Vatican City, After months of anticipation, the date of Mother Teresa’s canonization has finally been announced. It falls on Sept. 4, which this year will also mark a special jubilee for workers and volunteers of mercy. Though it's been rumored for months that Mother Teresa’s canonization will take place Sept. 4, the Vatican made the date official during a March 15 consistory of cardinals. Mother Teresa was born Agnes Gonxha Bojaxhiu Aug. 26, 1910, in Skopje, Macedonia. After joining the Sisters of Loretto at age 17, she was sent to Calcutta, where she later contracted tuberculosis, and was sent to rest in Darjeeling. On the way, she felt what she called “an order” from God to leave the convent and live among the poor. After she left her convent, Mother Teresa began working in the slums, teaching poor children, and treating the sick in their homes. A year later, some of her former students joined her, and together they took in men, women and children who were dying in the gutters along the streets. In 1950, the Missionaries of Charity were born as a congregation of the Diocese of Calcutta. In 1952, the government granted them a house from which to continue their mission of serving Calcutta's poor and forgotten. She died Sept. 5, 1997, and was beatified just six years later by St. John Paul II Oct. 19, 2003. In addition to Mother Teresa, the consistory also decided on the canonization dates of four other blesseds: Bl. Maria Elisabetta Hesselblad, Bl. Jose Sanchez del Rio, Bl. Stanislaus of Jesus Mary and Bl. Jose Gabriel del Rosario Brochero. The canonization of Bl. Jose Sanchez del Rio is also noteworthy. He will be made a saint Oct. 16, alongside Bl. Jose Gabriel del Rosario Brochero. Blessed José Luis Sánchez del Río was brutally tortured and killed when he was 14 years old during the 1924-1928 religious persecution by Mexican President Plutarco Elías Calles. José Luis had enlisted in the ranks of the Cristeros, under the command of General Prudencio Mendoza. He was martyred by the Federal Army Feb. 10, 1928. According to the story, the soldiers cut off the soles of his feet and forced him to walk barefoot to his grave. Moments before he was killed, the boy shouted, “Viva Cristo Rey!” or “Long live Christ the King!” His character was one of the main protagonists in the 2013 film “For Greater Glory.” Blessed Jose Gabriel del Rosario Brochero, frequently referred to as the “gaucho priest,” will be Argentina's first saint. Born March 16, 1840, the priest suffered from leprosy throughout his life, and is known for his service to the sick and the dying. He died in 1914 and was beatified by Pope Francis Sept. 14, 2013. Sweden will also receive a new saint in Bl. Maria Elizabeth Hesselblad, who will be canonized June 5 alongside Polish Blessed Stanislaus of Jesus and Mary Papczynski. Born in the small village of Faglavik, in Sweden’s western coast province of Alvsborg June 4, 1870, Bl. Maria Elisabeth was a nurse and a convert to Catholicism. After her conversion, she went on to found a new order of Bridgettines, called the Most Holy Savior of Saint Bridget. She died in Rome April 24, 1957, and was beatified April 9, 2000, by St. John Paul II. Blessed Stanislaus of Jesus and Mary Papczynski is a Polish priest born in 1631 and beatified by Benedict XVI in 2007. Often referred to as the “Father Founder,” Bl. Stanislaus is known for his writings and constant encouragement to contemplate God’s mercy and to turn to Mary Immaculate for guidance and protection. In addition to founding the Congregation of Marian Fathers of the Immaculate Conception of the Most Blessed Virgin Mary, the priest also experienced visions of Holy Souls in Purgatory, and urged penance and prayers on their behalf.

Ndege yaanguka na kuwauwa abiria 62 Urusi

Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 62 imeanguka ilipukuwa ikitua katika mjini ulio kusini mwa Urusi wa Rostov-on-Don. Hakukuwa na manusura kati ya abiria 55 na wahudumu saba waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Ndege hiyo aina ya Boeng 737 iliyokuwa ikitoka Dubai ilimilikiwa na shirika la Flydubai. Ndege ya Flydubai ilioanguka nchini Urusi Ndege hiyo ilizunguka kwa karibu masaa mawili kabla ya kufanya jaribio la pili la kutua kufutia hali mbaya ya hewa. Ilianguka mita mia kadha kutoka kwa barabara ya uwanja ambapo ilivunjika na kushika moto.

Mshukiwa mkuu wa shambulio la Paris akamatwa

Maafisa wa polisi nchini Ubelgiji wakimkamata mshukiwa Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameonya kuwa mitandao ya kigaidi barani Ulaya inaendelea kuimarika licha ya kukamatwa kwa mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris. Salah Abdeslam alikamatwa wakati wa uvamizi uliofanywa na kikosi cha kupambana na ugaidi nchini Ubelgiji katika wilaya ya Molenbeek mjini Brussels baada ya kupigwa risasi kwenye mguu. Mtu mwingine ambaye pia anashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi hayo ya mwezi Novemba alijeruhiwa na kukamatwa na kwa ujumla watu watano walikamatwa. Bwana Hollande alisema kuwa vita havitakwisha hadi kila mmoja aliyehusika kwenye shambulizi la Paris akamatwe. Watu 130 waliuawa wakati wa shambulizi hilo.

Friday, March 18, 2016

Simba aingia jijini Nairobi na kujeruhi mzee

Visa vya simba kutoka mbugani Nairobi vimekuwa vikiripotiwa hivi karibuni Simba aliyetoka katika mbuga ya taifa ya wanyama ya Nairobi amemshambulia mzee mmoja jijini humo mapema asubuhi. Simba huyo alitoka mbugani na kuonekana karibu na eneo la City Cabanas, katika ya Mombasa Road. Afisa wa mawasiliano wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) Bw Paul Udoto ameambia BBC kwamba mzee aliyejeruhiwa ni wa umri wa miaka 63 na amepewa matibabu ya dharura katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kisha akakimbizwa hospitalini kwa matibabu kamili. Hata hivyo, Bw Udoto amesema mzee huyo hayuko hatarini. Kwa mujibu wa afisa huyo, simba huyo huenda alikerwa na kelele za magari yaliyokuwa yakipita. SimbaImage copyrightAFP Image caption Maafisa wa usalama wakitafuta simba waliodaiwa kuonekana barabara ya Ngong majuzi Vikosi vitatu vya maafisa wa KWS vilitumwa kumdhibiti na kwa mujibu wa Bw Udoto, simba huyo anaelekezwa ndani kwenye mbuga. Maafisa wanaendelea kushika doria kubaini iwapo kuna simba wengine walitoka mbugani. Visa vya simba kutoka mbugani vimekuwa vikiripotiwa siku za karibuni. Mwezi mmoja uliopita, simba wanne waliingia maeneo ya makazi eneo la Langata. Wiki mbili zilizopita, simba wawili walidaiwa kuonekana karibu na barabara ya Ngong.

Umoja wa Ulaya kuafikiana na Uturuki kuhusu wakimbizi

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajaribu kufikia muafaka muhimu na Waziri Mkuu wa Uturuki wa kuutatua mgogoro wa wahamiaji baada ya kukubaliana kuhusu msimamo wa pamoja katika mkutano wa kilele mjini Brussels Belgien EU-Gipfel Angela Merkel Lars Lokke Rasmussen und Mark Rutte Rais wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk anawasilisha mapendekezo hayo yenye utata kwa Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, ambayo Uturuki itatakiwa kuwapokea wahamiaji wote na wakimbizi wanoingia kutokea Ugiriki, kabla ya kushiriki katika mkutano na viongozi wote 28 wa Umoja wa Ulaya. Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu amesema mpango huo unaopendekezwa ni wa wazi na kuaminika lakini akaongeza kuwa Utruruki haitawahi kuwa gereza la wazi kwa wahamiaji. Ulaya inautegemea muafaka huo kupunguza wimbi kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa la wahamiaji milioni 1.2 tangu mwanzo wa mwaka wa 2015, linalosababishwa na vita vya Syria, lakini Uturuki itatangaza gharama kubwa kabla ya kukubali mpango huo. Licha ya wasiwasi katika mataifa mengi ya Umoja wa Ulaya kuhusu rekodi ya haki za binaadamu ya Uturuki, nchi hiyo imedai kuharakishwa kwa jaribio lake lililokwama kwa muda mrefu la uwanachama wa Umoja wa Ulaya, kupewa msaada zaidi wa mabilioni ya euro na kukubaliwa kuwa na usafiri huria. Griechenland Mazedonien Flüchtlinge bei Idomeni Wahamiaji wakiwa njiani kuelekea Macedonia kutoka kambi ya wakimbizi ya Idomeni, Ugiriki Kansela wa Ujerumani amesema mpango huo ni fursa nzuri ya kuzuia biashara ya wasafirishaji watu. "Masharti kadhaa yatastahili kuwekwa kwa ajili ya ulinzi wa wakimbizi kulingana na viwango vya kimataifa. Hii ni sehemu ya mkakati huo, na ili kuwa na usafiri huria bila Visa, viwango Fulani vya sheria ya kimataifa lazima vishirikishwe katika sheria ya Uturuki ikiwa hilo halijafanyika tayari". Wakosoaji pia wameibua wasiwasi kuwa muafaka huo huenda ukakiuka sheria za kimataifa ambazo zinazuia kufukuzwa kwa jumla kwa wakimbizi. Mgogoro wa wahamiaji umeendelea kuigawa Ulaya, wakati kukiwa na hofu kuwa mkataba wake wa Schengen wa usafiri huria huenda ukavunjika kwa sababu mataifa wanachama yataweka uthibiti wa mipaka na pia kuchipuka kwa vyama vinavyotafuta umaarufu kupitia hisia za kupinga uhamiaji. Lakini baadhi ya viongozi wa Ulaya wameelezea wasiwasi kuwa muafaka huo – ambao Umoja wa Ulaya utamchukua mkimbizi mmoja wa Kisyria kutoka ardhi ya Uturuki kwa kubadilishana na kila Msyria atakayechukuliwa tena na Uturuki kutokea Ugiriki – huenda ukawa kinyume cha sheria. Lengo la mpango huo ni kuwahimiza Wasyria kuomba hifadhi katika Umoja wa Ulaya wakati wakiwa wangali kwenye ardhi ya Uturuki, badala ya kuhatarisha maisha kwa kutumia maboti ya wasafirishaji haramu wa watu katika Bahari ya Aegean. Muafaka huo pia utaipa msaada muhimu Ugiriki ambako maelfu ya wakimbizi wamekwama katika mazingira duni baada ya nchi za Balkan kufunga mipaka yao na kuwazuia kuingia Ujerumani na nchi za Skendinevia

Trump kufanya hotuba kuu badala ya mdahalo Jumatatu

Trump anapanga kufanya kile alichokiita hotuba kuu Jumatatu badala ya kufanya mdahalo na wapinzani wake wawili waliobaki kwa uteuzi wa chama chao. Mgombea wa chama cha Republikan, Donald Trump, anasema anapanga kufanya kile alichokiita hotuba kuu Jumatatu badala ya kufanya mdahalo na wapinzani wake wawili waliobaki kwa uteuzi wa chama chao. Trump alikuwa akitarajiwa kushiriki kwenye mdahalo wa shirika la habari la Fox huko Salt Lake City Utah, na Seneta wa Texas Ted Cruz na Gavana wa Ohio John Kasich, lakini alisema jana jumatano kwamba warepublikan wamepata midahalo ya kutosha na hatahudhuria. Kasich naye alitangaza kwamba bila ya Trump kuwepo naye hatashiriki kutokana na kukosa washiriki, shirika la habari la Fox liliamua kufuta mdahalo huo. Cruz yuko nyuma ya Trump kwa wajumbe 673 dhidi ya 410 alimshambulia mfanyabiashara huyo na kumwita Ducking Donald akimaanisha “anakwepa na kukimbia” na kuwaambia waunga mkono wake waende kwenye mtandao uitwao "duckingdonald.com."

Mahakama yasimamisha uteuzi wa Lula Brazil

Mahakama moja nchini Brazil imesimamisha uteuzi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Luiz Inacio Lula da Silva kama mkuu wa utumishi wa uma na mrithi wake Dilam Rousseff. Agizo hilo la mahakama mjini Brasilia linajiri mda mfupi baada ya Lula kuapishwa katika wadhfa huo. Mapema ,wafuasi wake na wale wanaompinga walifanya maandamano nje ya jumba la rais. Wakosoaji wa Lula wanamtuhumu kwa kuchukua wadhfa huo ili kukwepa mashtaka ya ufisadi yanayomkabili. Kulikuwa na maandamano katika miji kadhaa ya Brazil usiku kucha.Rais Rousseff anakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi kufuatia madai ya kutoa hongo yanayhusishwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Petrobras.

EU wafikia makubalino dhidi ya wahamaiji

Viongozi wa Umoja wa ulaya walioko kwenye mkutano nchini Brussels wameamua kwa pamoja kuwasilisha pendekezo moja kuhusu Uturuki, katika kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi. Katika mapendekezo ya mpango uliowekwa, wahamiaji wanaoingia Ugiriki kutoka Uturuki watarudishwa huku Uturuki ikipewa msaada wa kifedha na wakati huo huo raia wake kuweza kuingia barani ulaya bila visa. Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel alilizungumzia baada ya mkutano huo wa umoja wa ulaya na Uturuki uliofanyika nchini Brussells. Amesema Uturuki imekubali kukabiliana na umiminikaji wa wahamiaji kwa kupokea wakimbizi ambao wanarudishwa kutoka fukwe za Ugirikri ,fursa ambayo ni nzuri ili kwa kuwa inawaweka pembeni wafanya biashara haramu wa binadamu.Hata hivyo suala hili linapaswa kuwa wazi kisheria,suala ambalo lilipewa mkazo zaidi katika mkutano huo.Tumekubaliana kuwa kila muhamiaji anayetoka katika fukwe ataweza kusikizwa yeye binafsi. Ingawa chancellor wa Ujerumani ,Angela Merkel alisisitiza kuwa Ugiriki inahitaji msaada wakati ambao maelfu ya wakimbizi wamekwama nchini mwake.Raisi wa Ufaransa ,Francois Hollande, unahitaji makubaliano ambayo yataisaidia Ugiriki pamoja na Uturuki.

Thursday, March 17, 2016

Waandamana dhidi ya uteuzi wa Lula Brazil

Raia wa Brazil nchini Sudan Kusini wamefanya maandamano katika miji kadhaa wakipinga hatua ya rais Dilma Rousseff ya kumteua mtangulizi wake Luiz Inacio Lula da Silva kama mkuu wa wafanyikazi. Katika mji mkuu wa Brasilia ,maafisa wa polisi waliwarushia waandamanaji maji yenye pilipili nje ya jumba la rais. Lula anachunguzwa katika kashfa kubwa ya ufisadi.Saa chache baada ya hatua hiyo ,jaji wa kijimbo anayeongoza uchunguzi dhidi ya Lula alitoa mawasiliano ya simu yaliorekodiwa yakionyesha kwamba bi Lula alimpatia wadhfa huo ili kumkinga dhidi ya kukamatwa. Kiongozi huyo wa Brazil ambaye yeye mwenyewe anakabiliwa na mashtaka alitetea uteuzi huo.Amesema kuwa Lula ana ujuzi mkubwa kama mpatanishi wa kisiasa ambaye atasaidi kuupiga jeki uchumi. Pia alisema kuwa rais huyo wa zamani anaweza kushtakiwa na mahakama ya juu. Sauti hiyo ya mawasiliano ilizua hisia kali katika bunge la Brazil huku kukiwa na visa vya ghasia baada ya viongozi wa upinzani kumtaka rais huyo kujiuzulu.

Ripoti: Ushindi wa Trump ni hatari kwa dunia

Shirika moja la kimataifa limesema ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa miongoni mwa hatari 10 kuu zaidi zinazokabili dunia. Shirika hilo la Economist Intelligence Unit linaonya kuwa iwapo Bw Trump atashinda urais Marekani, hilo huenda likavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani. Hata hivyo, shirika hilo halimtarajii Bw Trump, anayeongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican, kumshinda Bi Hillary Clinton ambaye shirika hilo linasema "ana uwezekano mkubwa sana kuwa mgombea wa chama cha Democratic". Ushindi wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya kivita katika bahari ya South China Sea. Kuyumba kwa uchumi wa Uchina au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na kusababisha “vita baridi” vipya ni miongoni mwa mambo ambayo yanachukuliwa kuwa hatari zaidi ya ushindi wa Bw Trump. "Kufikia sasa, Bw Trump ametoa maelezo machache sana kuhusu sera zake, na huwa anabadilisha sana msimamo wake,” EIU wanasema kwenye ripoti yao ya utathmini wa hatari zinazokabili dunia. Utathmini huo huangazia pia athari za jambo fulani na uwezekano wa jambo hilo kutokea. Al-Shabab wamtumia Trump wakitafuta wafuasi EIU hutumia kipimo cha moja hadi 25, na Bw Trump ana alama 12, sawa na hatari ya "kuongezeka kwa ugaidi wa kijihadi kuathiri uchumi wa dunia”. "Amekuwa na msimamo mkali sana dhidi ya biashara huria, pamoja na Nafta, na ameituhumu Uchina mara nyingi kuwa taifa linalofanyia mchezo sarafu,” EIU inasema. Shirika hilo limeonya kuwa matamshi yake makali dhidi ya Mexico na Uchina hasa yanaweza kusababisha vita vya kibiashara. Bw Trump amependekeza ua ujengwe kati ya Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji na pia ametetea kuuawa kwa jamaa za magaidi. Aidha, amependekeza kuvamiwa kwa Syria ili kuangamiza kundi la Islamic State. EIU wanasema pendekezo msimamo wake kuhusu mzozo Mashariki ya Kati pamoja na pendekezo kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani vinaweza kutumiwa na makundi ya itikadi kali za Kiislamu kuwatafuta wafuasi zaidi.

Magufuli apiga simu kituo cha runinga

Rais wa Tanzania John Magufuli amewashangaza wengi baada ya kupiga simu katika kituo cha runinga asubuhi. Rais huyo alipiga simu wakati wa kipindi cha Clouds 360 kueleza kufurahishwa kwake na kipindi hicho. Tangu kuingia madarakani Novemba mwaka jana, kiongozi huyo hajafanya mahojiano yoyote ya moja kwa moja na kituo chochote cha habari. “Mimi nawapongeza sana kwa kweli,” alisema Dkt Magufuli, kabla ya kuendelea na kutaja majina ya watangazaji wa kipindi hicho na kusema huwa wanachambua vyema magazeti. Alisema aliwapigia simu kuwapongeza. Mmoja wa watangazaji hao alichukua fursa hiyo kumuuliza swali Dkt Magufuli. Magufuli: Vijana sharti wafanye kazi Magufuli amteua Kikwete mkuu wa chuo Swali lilihusu kutolewa kwa zawadi kwa wanawake lakini Dkt Magufuli alishangaa ni kwa nini hawakuwapa wanaume zawadi. Baada ya kumaliza kuzungumza, Dkt Magufuli alimkabidhi simu mkewe Janet ambaye pia alieleza furaha yake kuhusu kipindi hicho. “Yaani mnatupa faraja, huwa tunacheka sana na mzee wangu hapa,” alisema Bi Magufuli. Kituo hicho cha runinga baadaye kilipakia simu ya watangazaji hao wakiwasiliana na rais kwenye Instagram Baadaye alirejesha simu kwa Dkt Magufuli ambaye kwa utani aliwashauri watangazaji wakati mwingine wajitokeze na wachumba wao. "Sam (Sasali) na mke wake, Babbie (Kabae) aje na mume wake na wewe Hudson (Kamoga) uje na mke wako hapo. Siku nyingine mwakaribishe hapo,” alisema.

Obama amteua Merrick Garland kuwa jaji wa mahakama kuu

Makamu Rais Joe Biden, kushoto, akimsikiliza Rais Barack Obama akimtangaza Jaji Merrick Garland kuwa mteuzi wake katika Mahakama Kuu, Washington, March 16, 2016. Makamu Rais Joe Biden, kushoto, akimsikiliza Rais Barack Obama akimtangaza Jaji Merrick Garland kuwa mteuzi wake katika Mahakama Kuu, Washington, March 16, 2016. Rais Barack Obama amemteua jaji wa mahakama ya rufaa ya serikali kuu Merrick Garland kujaza nafasi ya Mahakama Kuu iliyoachwa wazi baada ya kifo cha Jaji Antonin Scalia mwezi uliopita. Akitambulika kama mtu mwenye sera za kadiri, Garland, mwenye umri wa miaka 63 kwa sasa ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa katika eneo la Washington DC. Maseneta saba Warepublican walioko katika baraza la seneti la sasa ni miongoni mwa wale waliomwidhinisha Garland kushika nafasi aliyo nayo sasa mwaka 1997. Rais Obama alisema alitafuta jaji ambaye ana misingi mitatu mikuu: "mawazo yaliyo huru, mwenye sifa zisizopingika, na umahiri usiopingwa katika sheria." Kifo cha ghafla cha Jaji Scalia Februari 13 sio tu kilisababisha upungufu katika mahakama kuu yenye majaji tisa, lakini pia mvutano wa kisiasa baina ya Rais Mdemokrat na Baraza la Seneti linalodhibitiwa na Warepublican. Saa chache baada ya kufariki kwa Scalia, kiongozi wa Warepublican katika Seneti, Mitch McConnell alisema "nafasi hiyo isijazwe mpaka apatikane rais mpya" na akaahidi kwamba seneti haitaitisha kikao cha kuidhinisha uteuzi wa Obama. Warepublican wanatumaini kuwa mgombea wao urais atashinda uchaguzi wa Novemba na hivyo kuwa na nafasi ya kufanya uteuzi utakaorejesha mahakama kuu kuwa na wingi wa wakonsevativu. Obama ambaye atakuwa madarakani mpaka mwishoni mwa Januari 2017, alisema ni wajibu wake wa kisiasa kufanya uteuzi wa mahakama kuu haraka iwezekanavyo.

Clinton na Trump waongoza nafasi ya urais Marekani.

Mgombea urais anayeongoza wa chama cha Republican Donald Trump ameshinda majimbo matatu katika upigaji kura wa awali uliofanyika Jumanne ikiwemo jimbo muhimu la Florida na kumsababisha Seneta wa jimbo hilo Marco Rubio kujitoa katika kinyang’anyiro cha kampeni za urais na hivyo kujiongezea wajumbe mbele ya seneta wa Texas, Ted Cruz. Jimbo pekee ambalo Trump alishindwa katika uchaguzi huo wa Jumanne ni Ohio, ambapo Gavana John Kasich alipata ushindi mkubwa kwa mara ya kwanza kwenye jimbo lake. Bilionea mfanyabiashara Trump, alishinda jimbo la Florida kwa wingi wa asilimia 19, lakini ushindi wake wa kiasi katika jimbo la North Carolina na Illinois, ulimsaidia Cruz kupata wajumbe zaidi kwenye siku hiyo. Trump na Cruz pia walifungana katika kinyang’anyiro hicho kwenye jimbo la Missouri. Hivi sasa kinyang’anyiro hiki kimebaki kwa Ted Cruz na Donald Trump wa Republican ambapo wote wanatoa wito wa chama kuungana pamoja. Kwa upande wa wademokrat Hillary Clinton alipata ushindi muhimu wa majimbo manne kati ya matano. Profesa wa chuo kikuu cha Georgia Athens Dr.Lioba Moshi amezungumza na VOA akieleza kwamba uchaguzi huo umechukua sura mpya kwa chama cha republican kwa sasa kwa sababu njia yake haiko wazi pamoja na kuongoza chama chake kwasababu upande mmoja wa chama chake asilimia 60 ya wananchi waliofanyiwa uchunguzi wansema hawamuungi mkono. Na katika mkutano mkuu wa chama cha Republikan huko Cleveland kutakuwa na sokomoko kubwa anaongeza Dr.Lioba kwasababu wanaweza warepublikan wa wapinzani wa Trump wanaweza wasijitoe mpaka mwisho na kuendelea kumpinga ambapo upigaji kura unaweza kufanyika tena.

Obama aongezea Korea Kaskazini vikwazo

Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia majaribio silaha za nyuklia na makombora hivi majuzi. Msemaji wa ikulu ya White House amesema Marekani na jamii ya kimataifa hawatavumilia “shughuli haramu za nyuklia” zinazotekelezwa na Korea Kaskazini. Awali, ikulu ya White House iliishutumu Korea Kaskazini ikisema inawatumia raia wa Marekani kama rahani katika juhudi za kuendeleza ajenda yake ya kisiasa. Korea Kaskazini yaamrisha majaribo zaidi ya mabomu Korea Kaskazini yajibu vikwazo vya UN Hii ni baada ya Korea Kaskazini kumhukumu mwanafunzi Mmarekani kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola. Bw Otto Warmbier, mwenye umri wa miaka 21, alikiri kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akikaa pamoja na kundi jingine la watalii mjini Pyongyang. Marekani imeitaka Korea Kaskazini kumwachilia huru mwanafunzi huyo mara moja.

Trump asema huenda fujo zikazuka Marekani

Trump ameshindwa katika mchujo jimbo la Ohio Mfanyabiashara tajiri Marekani Donald Trump, amesema anafikiri kutatokea fujo iwapo ataongoza kwa wajumbe kisha chama chake cha Republican kitakosa kumuidhinisha awanie urais. Bw Trump alishinda mchujo katika majimbo matatu zaidi, likiwemo jimbo la Florida mnamo Jumanne, ingawa alishindwa katika jimbo jingine muhimu la Ohio. Hatua yake ya kushindwa Ohio huenda ikawawezesha wahafidhina wadhibiti wa chama cha Republican, ambao hawajafurahishwa na mtazamo wake, kumpendekeza mgombea mwingine kwenye mkutano mkuu wa kuidhinisha wagombea Julai. Hayo yakijiri, Bw Trump amesema hatashiriki mdahalo katika runinga ya Fox News wiki ijayo akisema ametoshena na midahalo. Katika chama cha Democratic, Hillary Clinton ameimarisha uongozi wake na kumshinda mpinzani wake wa pekee Bernie Sanders katika majimbo manne yaliyofanya mchujo Jumanne.

Ripoti: Tanzania nyuma kwa furaha duniani

Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi za mwisho kwa viwango vya furaha kwa mujibu wa Ripoti ya Viwango vya Furaha Duniani ya 2016 ambayo imetolewa leo. Orodha hiyo iliandaliwa kwa kuangazia pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi maishaji, uhuru kutoka kwa ufisadi, na ukarimu miongoni mwa mengine. Mataifa yaliyo kwenye kundi la mataifa kumi ya mwisho ni Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria huku Burundi ikishika mkia. Tanzania imo nambari 149 kati ya nchi 157 ikiwa na alama 3.695 kati ya alama 10 na Rwanda nambari 152 na alama 3.315. Uganda imo nambari 146 na alama 3.739, Malawi nambari 132 na alama 4.156, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imo nambari 125 na alama 4.272 na Kenya nambari 122 na alama 4.356. Somalia imo nambari 76 na alama 5.44. Ripoti hiyo imetolewa mjini Roma, Italia huku ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha Siku ya Furaha Duniani ya Umoja wa Mataifa tarehe 20 Machi. Orodha hiyo imetayarishwa na shirika la maendeleo endelevu ya Sustainable Development Solutions Network (SDSN) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa. Denmark inaongoza kwa viwango vya furaha duniani ikiwa na alama 7.526 ikifuatwa kwa karibu na Uswizi, Iceland na Norway. Finland, Canada, Uholanz, New Zealand, Australia na Sweden zinafunga kumi bora. Marekani imo nambari 13 na Uingereza nambari 23.

Wednesday, March 16, 2016

Mwanafunzi Mmarekani afungwa jela Korea Kaskazini

Otto Warmbier alisema alifanya kosa kubwa zaidi maishani mwaka Mahakama ya Juu nchini Korea Kaskazini imemhukumu mwanafunzi Mmarekani kifungo cha miaka 15 jela na kazi ngumu, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti. Amehukumiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola. Otto Warmbier, 21, alikiri kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akiishi na kundi la watalii mjini Pyongyang. Alikamatwa Januari alipokuwa akijaribu kuondoka Korea Kaskazini. Baadaye alijitokeza kwenye runinga akionekana kukiri makosa hayo na kusema kundi moja la kanisa lilikuwa limemuomba abebe kitu cha kukumbuka kutoka kwa safari yake. Korea Kaskazini wakati mwingine huwafunga jela wageni kama njia ya shinikizo kwa mataifa yanayoipinga. Image copyrightfacebook profile Warmbier, 21 alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Virginia. Wakati wa kukamatwa kwake tarehe 2 Januari, shirika la habari la serikali la KCNA lilisema alikuwa ameingia Korea Kaskazini akiwa na lengo la “kuvuruga umoja wa taifa” na kwamba alikuwa amedhibitiwa na kuelekezwa na serikali ya Marekani. Warmbier alipokuwa akikiri makosa Akiongea kwenye runinga Februari, huku akitokewa na machozi, alisema alitenda “kosa kwa kuondoa bango la kisiasa kutoka eneo la kusubiri wafanyakazi katika hoteli ya Yanggakdo”. “Lengo langu lilikuwa kudhuru kujitolea na bidii ya watu wa Korea. Hili lilikuwa lengo la kijinga sana,” alinukuliwa akisema. Alisema ndilo kosa kubwa kabisa alilowahi kulifanya maishani.

Uchaguzi Marekani: Rubio ajitoa, Clinton na Trump waongeza kasi

Seneta Mrepublican Marco Rubio wa Florida amejitoa katika kuwania ugombea urais kwa chama hicho baada ya kushindwa kwenye jimbo lake wakati Gavana wa Ohio John Kasich amepata ushindi muhimu katika jimbo lake na kumpa nguvu mpya katika kinyang'anyiro kwa upande wa ware publican baada ya kura za awali Jumanne. Donald Trump ambaye anaongoza kwa upande wa chama hicho alijiongezea kasi kwa kupata ushindi mkubwa katika jimbo la Florida, huku Seneta wa Texas Ted Cruz na Kasich wakiwa nyuma yake. Trump pia alishinda katika majimbo ya Illinois na North Carolina. ​Baada ya kushindwa katika jimbo lake, Rubio alisema anashukuru wote waliomwunga mkono, akiongeza kuwa haikuwa "mpango wa Mungu" kwa yeye kuwa rais mwaka 2016. Ohio ni jimbo lenye wajumbe wengi katika mkutano mkuu wa uteuzi wa chama cha Republican hivyo ushindi wake unampa Kasich nguvu mpya katika kampeni yake. Akizungumza baada ya ushindi wake alibashiri kuwa atakuwa mshindani mkuu katika chaguzi zijazo za awali kuwania ugombea. Kwa upande wa Wademokrat, Hillary Clinton alimshinda Seneta Bernie Sanders kwa kura nyingi katika majimbo muhimu ya Florida, North Carolina na Ohio na hivyo kuchukua wajumbe wengi kutoka majimbo hayo. Clinton alisema Jumanne ilikuwa "Super Tuesday" nyingine kwake, na kumpa hongera Sanders kwa kile alichosema ni kampeni ya nguvu. Clinton ameongeza sana idadi yake ya wajumbe kuelekea mkutano mkuu wa chama cha Democrat huku Sanders akiendelea kupambana vikali kujaribu kumpiku Clinton ingawa wachambuzi wengi wanasema bila shaka Clinton hatimaye atakuwa mgombea rasmi wa chama cha Democrat.

Putin aamrisha jeshi lake liondoke Syria

Urusi imesema jeshi lake liliopo Syria linajitayarisha kuondoka na kurudi nyumbani kufuatia amri iliyotolewa na Rais wa Urusi Vladimir Putin, baada ya kuanza kwa mazungumzo ya amani ya mzozo wa Syria mjini Geneva. Syrien russische Kampfjets Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya Rais Putin kutoa amri ya kuondoka kwa baadhi ya wanajeshi waliopo nchini Syria. Amri aliyoitoa siku yaliyoanza mazungumzo ya amani yanayofanyika mjini Geneva. “Ushirikiano wa jeshi la Urusi pamoja na jeshi la Syria na vikosi vengine vya kizalendo, vimefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa na ya kushangaza katika mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa,” amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin. Aidha Putin ameongeza matumaini yake ni kwamba kujiondoa kwa jeshi la Urusi itakuwa ni "ishara nzuri" kwa pande zote zinazopigana. Kuanza kwa mazungumzo hayo kunampa Putin nafasi nzuri ya kutangaza kusitisha kampeni yake ya mashambulizi ya anga iliyoendelea kwa miezi mitano na nusu nchini humo na ambayo ililisaidia kwa kiasi kikubwa jeshi la Rais wa Syria Bashar al- Asaad kukamata baadhi ya maeneo muhimu nchini humo na kujiongezea nguvu kabla ya kuanza mazungumzo. Baadhi ya wanajeshi wa Urusi watasalia kuwepo Hata hivyo Putin ameweka wazi baadhi ya wanajeshi wa Urusi watabakia katika kambi ya kijeshi ya eneo la Latakia pamoja na bandari ya Tartus nchini humo. Aidha Shirika la habari la Syria limemnukuu Rais Asaad akisema, Urusi itasitisha mashambulizi yake ya anga, lakini baadhi ya wanajeshi wake watabakia nchini humo. Ikulu ya Syria imesema viongozi hao wawili walizungumza kwa njia ya simu na kufikia aumuzi huwo. Licha ya kuondoshwa kwa baadhi ya wanajeshi wa Urusi, jeshi la Syria limesema litaendelea na kampeni yake ya kuyashambulia makundi ya kigaidi, ya Dola la Kiislamu-IS pamoja na la Al-Nusra. Aidha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakubaliana na uwamuzi uliyochukuliwa na Urusi wa kuanza kuondoa wanajeshi wake nchini Syria. Mashambulizi yaliyodumu miezi mitano na nusu Urusi ilianza mashambulizi ya anga nchi Syria mwezi Septemba kwa madai ya kutaka kuliondoa kundi la kigaidi linalojiita dola la kiisilamu IS linalodhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo, lakini kampeni hiyo ya kijeshi kwa kiasi kikubwa ilikuwa na lengo la kumsaidia Rais wa Syria Bashar al-Asaad. Ingawa Urusi imeweza imeweza kwa kiasi kikubwa kuingilia kati mapigano yanayoendelea nchini Syria, wanadiplomasi wanasema hakuna hakika iwapo itaweza pia kumshinikiza Rais Asaad kukubali kufikia makubaliano yatakayoleta suluhu ya mgogoro huwo. Katikaripoti yake kwa wanachama wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Steffan de Mistura amesema kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Febuari 27, yanaweza kuvunjika kirahisi na kwa maana hiyo yanahitaji kulindwa. Mazungumzo ya mjini Geneva, yaliyoitishwa na Umoja wa mataifa yalianza jana, ambayo ni siku iliyotimia miaka mitano tokea kuanza kwa mzozo wa Syria, ikiwa ni jitihada za hivi karibuni za kusitisha mapigano yaliyosababisha vifo vya zaidi watu 270,000 na kupelekea mamilioni wengine kupoteza mkaazi yao. DW SWAHILI

Rais Magufuli asema hasara ya mishahara hewa inafikia billioni 2.5 kwa mwezi

Rais wa Tanzania John Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni nchini humo huku akizungumzia upotevu mkubwa wa mapato ya serikali unaotokana na kuwepo watumishi hewa Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu hao wa mikoa rais Magufuli amesema tatizo la wafanyakazi hewa limekuwa likigharimu serikali fedha nyingi, ambapo ametolea mfano wa uchunguzi uliofanywa katika mikoa miwili ya Dodoma na singida na kubaini takriban wafanyakazi hewa 202 katika halmashauri 14. Amesema kutokana na hali hiyo na ikichukuliwa taswira ya nchi nzima, hasara inayokisiwa inayotokana na malipo ya mishahara hewa ya wafanyakazi nchini Tanzania inafikia shilingi billioni 2.5 kila mwezi huku serikali ikitumia shilingi bilioni 549 kwa mwezi kwa ajili kulipa watumishi wake hivyo amewataka kuzisimamia vyema halmashauri zao. Wakuu wa mikoa wote 25 walioapishwa baadaye wamesaini kiapo cha uadilifu kilichosimamiwa na kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Salome Kaganda, huku makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwatahadharisha juu ya kusimamia vyema matumizi ya fedha za maendeleo. Rais Magufuli pia amewaapisha kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA, Alphayo Kidata na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru, Valentine Mlowola aliyewathibitisha kazini hivi karibuni baada ya kukaimu kwa muda nafasi hizo. VOA SWAHILI