Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, February 18, 2016

Waziri Simbachawene asimamisha wakurugenzi kazi Tanzania.

Rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli ambae utawala wake unapambana na ufisadi. Rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli ambae utawala wake unapambana na ufisadi. Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais, tawala za mikoa na Serikali za mitaa nchini Tanzania, TAMESEMI- George Simbachawene, amewasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wakurugenzi kutoka halimashauri za Manispaa tano katika mikoa tofauti nchini kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa. Inadaiwa kuwa wakurugenzi hao wamekuwa wakishirikiana na maafisa wa ukaguzi wa hesabu kutoka ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali, CAG, kwa lengo la kuandikiwa hati zisizo na dosari pindi inapobainika kuwa wana kasoro. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es Salaam Jumatano, waziri Simbachawene amezitaja halmashauri hizo kuwa Misenyi mkoa wa Kagera,Nanyumbu mkoa wa Mtwara, Mbogwe Geita, Kilolo Iringa na Tunduma mbeya. Aidha Simbachawene amemvua madaraka na kuagiza mamlaka husika imsimamishe kazi ili kupisha uchungizi mkurugenzi wa halimashauri ya mji wa Tunduma, Halima Mpita , kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo kuwatumia watoto wake kwenye shughuli za halimshauri na kuwalipa posho pamoja na kuisababishia Serikali upotevu wa mapato ya ushuru wa magari yanayopita kwenye mpaka wa Tunduma. Chanzo:VOA SWAHILI
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment