Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 31, 2015

Lembeli ashinda kura za maoni Chadema, Bulaya almanusura

Wabunge wawili waliohama CCM hivi karibuni, James Lembeli na Ester Bulaya wamepitishwa katika kura za maoni kuwania ubunge kupitia chama chao kipya. Wakati Lembeli akipitishwa kwa kura za kishindo kuwania ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini, Bulaya alishinda katika nafasi ya viti maalumu baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro cha Jimbo la Bunda Mjini. Wanasiasa hao sasa wanasubiri uteuzi wa Kamati Kuu ya Chadema utakaofanyika Agosti 5 na 6. Ushindi wa Lembeli Katika uchaguzi huo wa juzi, mbunge huyo wa zamani wa Kahama aliwabwaga wenzake 13 aliogombea nao akipata kura 168 kati ya 262 zilizopigwa, akifuatiwa na John Katibu aliyepata kura 45, Peter Shita (17) na Emmanuel Madoshi aliyepata kura 10. Wengine ni Muta Nyerere (4), Felician Maige (4), Zacharia Obadia (3), Tadeo Mwati (2), Arnold Mtajwaka (2), Prosper Denga (2), Deusdedit Madinda (1), Reuben Macheyeki (1). Victor Mbwana na Richard Makingi waliambulia patupu. Katika uchaguzi wa viti maalumu, Winfrida Mwinula alishinda kwa kura 34 akifuatiwa na Salome Makamba aliyepata kura 30. Bulaya Kama isingekuwa ni kura za maoni za viti maalumu zilizomfuta machozi, Bulaya alikuwa tayari ametupwa nje baada ya kuanguka katika Jimbo la Bunda Mjini. Bulaya aliyekuwa miongoni mwa makada saba wa chama hicho waliokuwa wanawania kuliwakilisha jimbo hilo, alipata kura 37 kati ya 182 zilizopigwa akiwa nyuma ya Pius Masururi aliyeibuka mshindi kwa kura 65 na Magembe Makoye aliyepata kura 40. Baadaye katika mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), uliofanyika baadaye usiku, Bulaya alipata kura 71 kati ya 110 zilizopigwa na kuwabwaga Godliver Masamaki aliyepata kura 31, Joyce Sokombi (4), Minza Shani (3), Dk Jane Nyamsenda (1) na Alice Wandya aliyeambulia patupu. Awali, Bulaya alikwaa kisiki baada ya jina lake kuwa miongoni mwa waliokatwa na kamati ya utendaji inayosimamia majimbo hayo wakidaiwa ni wageni katika chama; wapenda fujo na matabaka, akiwa pamoja na Chacha Nyamhanga, Sulemani Daudi lakini walirudishwa kundini baada ya kikao cha viongozi na watiania. Katika Jimbo la Bunda Vijijini, Sulemani Daudi aliibuka mshindi kwa kura 84 kati ya 127 zilizopigwana kuwashinda John Masenza aliyepata kura 14, Dk Lucas Webiro (11), Frank Mongateko (8), Edgar Chibura (5) na Mathias Bandio aliyepata kura moja. Chanzo:mwnanchi.co.tz

Nigeria yateua General mpya

Rais wa Nigeria Mhamadu Buhari Nigeria imemteua Generali mpya kuongoza kikosi cha kimataifa kilichoundwa kwa ajili ya kupamba na kundi la wanamgambo wa Boko Haram. Meja General Iliyasu Isah Abbah ataongoza kikosi hicho kitakachokuwa na askari takriban 9000 kutoka nchi tano. Nigeria imemchagua General huyo mpya kwa lengo la kupambana na wanamgambo hao wa kundi la kigaidi la Boko Haram. Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa na ofisi zake katika mji mkuu wa Chad N'Djamena na wanatarajiwa kuendesha operesheni zake kikamilifu kuanzia mwezi ujao. Nigeria na majirani zake wamekuwa wanajitahidi kupambana na wapiganaji wa Boko Haram ambao wameua watu wapatao elfu ishirini. Chanzo:BBC Swahili

Uganda:Mbabazi kuwania urais nje ya MNR

Mbabazi ametangaza atawania urais kama mgombea huru Waziri mkuu wa zamani wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi ametangaza kuwa hatawania urais kwa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu mwakani. Mbabazi ametangaza hilo muda mchache uliopita akiwa nyumbani kwake Kololo katika siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uwaniaji wadhfa katika chama hicho tawala. ''kamwe sitatoka NRM''. ''Lakini sitaweza kugombea urais katika tikiti ya chama hicho cha NRM ilihali vipengee vingi tu vya vya chama vinakiuka katiba ya nchi'' Chanzo:BBC Swahili

Burundi:Agathon Rwasa ni naibu wa spika

Agathon Rwasa achaguliwa naibu spika wa bunge la Burundi Hii leo bunge lipya lililochaguliwa nchini Burundi limewateua viongozi wake. Licha ya kupinga uchaguzi mkuu wa hivi majuzi kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa amekubali kuwa naibu wa spika. Wadhifa wa spika umekabidhiwa mwenyekiti wa chama kinachotawala CNDD FDD Pascal Nyabenda. Rwasa alijipatia kura 108 kati ya 112 baada ya kupata uungwaji mkono na chama cha CNDD-FDD. Baada ya uteuzi wa leo, imebainika wazi kuwa uongozi wa bunge hilo utatawaliwa na wanaume kutokana na kuondolewa sheria ya ndani walioweka kuwa lazima kuwe na uakilishi wa wanawake japo mmoja, katika uongozi wa bunge hilo. Rwasa alijipatia kura 108 kati ya 112 baada ya kupata uungwaji mkono na chama cha CNDD-FDD. Zaidi ya watu 70 walipoteza maisha yao baada ya makabiliano kati ya wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza na wapinzani waliomtaka asigombee kiti muhula wa tatu wa urais. Rais Nkurunziza alishinda kwa asilimia 70 ya kura Wapinzani walidai kuwa muhula huo unakiuka sheria za nchini. Naye rais Nkurunziza alishikilia kuwa muhula wa kwanza hakuchaguliwa na watu ,kwa hivyo haikuwa kinyume na sheria kwake kuwania muhula mwengine wa urais. Chanzo:BBC Swahili

Lowassa mgombea urais CHADEMA

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amechukua Fomu rasmi ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chadema. Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amesema baada ya kuchukua fomu hizo Lowassa atakuwa tayari kuzunguka nchi nzima kujitambulisha kwa wananchi kama mgombea rasmi wa Chadema. Lissu amesema uamuzi wa kumsimamisha mgombea huyo haukuwa wa kukurupuka bali umefuata uchunguzi wa muda usiopungua miezi mitatu na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa mgombea urais chini ya chama hicho. Amesema katiba ya Tanzania inasema pamoja na mambo mengine mtu pakee anayezuiwa kugombea urais ni yule aliyekutwa na hatia na Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo Chadema imepekua Nyaraka zote za kimahakama nchini na kujiridhisha kwamba Lowassa hana hatia yoyote inayoweza kumzuia kugombea nafasi ya urais. Chanzo:BBC Swahili

Thursday, July 30, 2015

‘Njia za asili za uzazi wa mpango zinatakatifuza maisha’

BARAZA la Maaskofu Katoliki Marekani limeathimisha juma la ‘Njia ya asili ya mpango wa uzazi, “BOM” na kubanisha kuwa njia hizo ni muhimu kwa ustawi wa maisha ya mwamini kiroho na kimwili. Maadhimisho hayo yaliyoanza Julai 19 hadi 25 mwaka huu yamelenga kuwawezesha waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusherehekea Injili ya familia kwa kuambata Injili ya Uhai, inayoheshimu na kuthamini mpango wa Mungu katika maisha ya mwanadamu. Kanisa linataka kuwasaidia waamini kutambua na kuthamini njia ya asili ya mpango wa uzazi kadiri ya mafundisho Kanisa ili kusimama kidete kushuhudia Injili ya Uhai, dhidi ya utamaduni wa kifo unaoendelea kusambaa duniani kwa kasi. Katika kipindi cha juma zima, Parokia zote nchini Marekani zimehamasisha njia ya asili ya mpango wa uzazi ili kuwasaidia waamini kufahamu na hatimaye kushuhudia Injili ya Familia inayoambata Injili ya Uhai, dhidi ya utamaduni wa kifo. Mnamo Julai 25, 1968 Mwenyeheri Paulo VI alichapisha Waraka wa Kitume ‘Humanae vitae’ yaani ‘Maisha ya mwanadamu’; Waraka ambao unachambua kwa kina na mapana utakatifu wa tendo ndoa katika maisha ya ndoa na familia, upendo wa dhati kati ya wanandoa na dhamana katika kulea na kuwatunza watoto ambao kimsingi ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Tarehe 25 Julai, 2015 inatangulia pia Kumbu kumbu ya Watakatifu Joakim na Anna, wazazi wake Bikira Maria inayoadhimishwa na Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 26 Julai. Huu ni wakati kwa familia ya Mungu nchini Marekani kujitaabisha kufahamu Sakramenti ya Ndoa ambayo kielelezo cha upendo wa dhati kati ya Bwana na Bibi na uaminifu unaopata chimbuko lake kutoka kwa Kristo kwa ajili ya mchumba wake Kanisa. Huu ni mwaliko kwa wanandoa kuhakikisha kwamba, wanatekeleza dhamana, wajibu na wito wao katika kuzaa, kulea na kuwatunza watoto ambao kwa hakika ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Njia ya asili ya mpango wa uzazi inawasaidia wanandoa kushirikiana kikamilifu katika mchakato wa utakatifu wa maisha, kwani njia hii inawawajibisha bwana na bibi katika maisha ya unyumba. Wanandoa wanapata nafasi ya kufahamiana zaidi na kutambua karama na vipaji ambavyo wamekirimiwa na Mwenyezi Mungu wanaposhiriki katika kazi ya uumbaji na malezi kwa ajili ya watoto wao. Chanzo:http://www.tec.or.tz

Muda wa uandikishaji BVR Dar waongezwa

Tume ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza kuongeza siku nne zaidi za uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia teknolojia ya BVR baada ya idadi kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam kuitikia wito wa zoezi hilo. Awali zoezi hilo lilikuwa likamilike kesho, Julai 31, lakini sasa litaendelea hadi Agosti 4, mwaka huu ili kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kujiandikisha. Kwa mujibu wa chombo hicho chenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za uchaguzi nchini, hadi jana, zaidi ya wakazi 1,000,000 walikuwa wamekwishaandikishwa jijini Dar es Salaam. Ikizingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Nec inatarajia kuandikisha jumla ya wakazi zaidi ya 2.8 milioni wa jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, hadi sasa jumla ya zaidi ya watu 18 milioni wamekwishajiandikisha wakati tume ilitarajia kuandikisha watu kati ya 22 milioni na 23 milioni.

Lowassa, Ukawa uamuzi mgumu

Siku moja baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangaza kuhama CCM na kujiunga na Ukawa kupitia Chadema, wasomi na wachambuzi wa masuala ya siasa wamesema pande hizo mbili zimefanya uamuzi mgumu ambao utanufaisha kila upande. Profesa wa Chuo Kikuu Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema uamuzi huo wa Lowassa ambaye alitangaza kujiunga na Chadema na kufafanua kuwa amejiunga na chama hicho kikuu cha upinzani kutekeleza azma yake ya kuwakomboa Watanzania na kuendeleza safari ya matumaini ni uamuzi mgumu. Alisema: “Lowassa amefanya uamuzi mgumu kutoka CCM lakini hata wapinzani wamefanya uamuzi mgumu kumpokea.” Alisema sababu kubwa ya Chadema kukubali kumpokea Lowassa ambaye leo anatarajiwa kuchukua fomu kuwania urais, wakati ilikuwa inamtuhumu kwa ufisadi inatokana na mwanasiasa huyo kuwa na watu wengi wanaomuunga mkono, hali ambayo itaibua ushindani mpya katika siasa nchini. Ni faida zaidi Profesa Mpangala alisema pamoja na Lowassa kutuhumiwa na viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa kwa ufisadi, uwepo wake ndani ya umoja una faida zaidi kuliko hasara. “Faida ya Lowassa kwenda Ukawa ni kubwa zaidi kuliko hasara ya kuendelea kumpinga na kumtuhumu kwa ufisadi. Ukawa wanatambua kuwa uwepo wa Lowassa utawapa kura nyingi katika uchaguzi ujao,” alisema. Profesa huyo alisema si jambo la ajabu kwa mwanasiasa kuhama chama, huku akitolea mfano mwaka 1995 jinsi Augustine Mrema alivyohama CCM kwenda NCCR kuwa, “Kama si nguvu ya Mwalimu Julius Nyerere pengine angekuwa rais,” alisema. Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu Huria (OUT), Dk Emmanuel Malya alisema katika siasa kinachotazamwa zaidi ni nafasi, na kwamba katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. “Ila ujio wa Lowassa Chadema lazima utazamwe, ni lazima chama hiki (Chadema) kimtazame kiongozi huyo anakuja na kitu gani? Pia, CCM nao hata kama hawatasema wazi, lakini kuondoka kwa Lowassa kutawatikisa kidogo,” alisema. Dk Malya alisema Lowassa alikuwa kiongozi katika Serikali iliyoundwa na CCM, hivyo ni lazima aeleze kilichomshinda kukifanya wakati huo na sababu za kutaka kuyafanya yaliyomshinda akiwa ndani ya Ukawa. Mhadhiri mwingine wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema: “Ukitazama kwa makini utagundua kila mmoja anambeba mwenzake, yaani Lowassa anaibeba Chadema na Ukawa na wao pia wanambeba yeye.” Alisema kama waziri mkuu huyo wa zamani atagombea urais kwa tiketi ya Chadema ni wazi kuwa mpambano utakuwa mkali kati yake na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kwa maelezo kuwa kuna baadhi ya mambo wanaendana. “Mtaji wa chama cha siasa ni watu na lengo kuu ni kuongoza nchi. Hakuna adui wa kudumu katika siasa. Kilichotokea ni jambo la kawaida tu ila tu watu wamestushwa maana hawakutegemea Lowassa kuwa atakihama CCM,” alisema. Lissu: Kwanini tumemkubali Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ametaja sababu mbili za Ukawa kumkaribisha Lowassa kuwa mgombea urais wakati chama hicho kilimtaja katika orodha ya mafisadi mwaka 2007. “Edward Lowassa ni mwanasiasa asiyeeleweka na aliyewagawa watu zaidi kwa sasa katika siasa nchini na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi Chadema tulimweka kwenye orodha ya mafisadi kutokana na kuhusika kwake na kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: ‘Kwa nini tumemkubali, siyo tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais? Na kwa nini washirika wetu wa Ukawa nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais? “Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama Taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipandevipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati, na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. “Sisi Chadema tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. “Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake Chadema na Ukawa, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa na sisi kuyafikia. “Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake; Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi? “Sisi Chadema na Ukawa tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwapo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono? Kwa nini Dk Slaa hakuonekana Katika mkutano wa kumtambulisha Lowassa, baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema hawakuhudhuria, kitendo kilichofafanuliwa jana kuwa walikuwa na majukumu mengine kichama. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba viongozi hao wamechukizwa na uamuzi wa chama hicho kumkubali Lowassa ajiunge Chadema, si za kweli. Viongozi ambao hawakuonekana katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Bahari Beach ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Naibu wake (Bara), John Mnyika na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu. “Kama mnavyojua kwa sasa kuna mambo mengi yanaendelea nchini likiwamo suala la uandikishaji wa wananchi katika daftari la wapigakura,” alisema Mwalimu huku akifafanua kuwa mchakato huo ni moja ya mambo yanayofuatiliwa kwa ukaribu na viongozi wa Chadema. “Mbona suala hili mnataka kulikuza sana. Ni kitu cha kawaida Chadema ni chama kikubwa na viongozi wake wana shughuli nyingi za kufanya,” alisisitiza. “Jana, (juzi) Dk Slaa hakuwapo wala Lissu, lakini katika mkutano wa leo (jana) Lissu kaja Dk Slaa hajaja. Na hata leo (jana) Mbowe ambaye tulikuwa naye jana leo hayupo. Kwa hiyo ni suala la utaratibu tu na si kila tukio lazima tuwe wote,” alisema. Kuchukua fomu Katika hatua nyingine, Mwalimu alisema leo Lowassa atachukua fomu za kuomba ridhaa ya kuwania urais kupitia Chadema katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kinondoni, Dar es Salaam. “Atachukua fomu kesho (leo) na kutakuwa na shamrashamra za aina yake,” alisema. Kingunge, Sophia wajitenga Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru na Waziri wa Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na Watoto, Sophia Simba wametoa kauli zinazoashiria kujitenga na uamuzi wa Lowassa kuondoka CCM. Simba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alisema bado ni mwanachama wa CCM na kuwa uamuzi wa Lowassa ni wa mtu binafsi. “Mimi haunihusu, bado ni mwanachama wa CCM, tafadhali msinisumbue,” alisema. Simba, pamoja na wajumbe wenzake wa Kamati Kuu ya CCM; Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi na Adam Kimbisa waliitisha mkutano wa waandishi wa habari kuipinga kamati hiyo kwa kulikata jina la Lowassa katika mchakato wa kumpata mgombea wa urais. Aidha, Kingunge ambaye wakati wa kusaka wadhamini katika mchakato wa awali wa urais ndani ya CCM alijitokeza hadharani kumuunga mkono Lowassa alisema hatua yake ya Mbunge huyo wa Monduli kuhamia Chadema ni uamuzi binafsi hivyo hawezi kuutolea maoni yoyote. “Kama ameondoka, basi anatakiwa aulizwe yeye na wala si mimi kwa sababu kila mtu ana maamuzi yake binafsi,” alisema. Chanzo:mwananchi.co.tz

Lissu wanaotaka kuondoka Chadema ruksa

MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho. Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema. Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze. Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.” “Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri. Tunamkaribisha kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya,” amesema Lissu. Akizungumza kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema, “…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.” “Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” ameeleza Lissu. Chanzo:mwnahalisi online

Spika Ndugai amshushia kichapo mgombea mwenzake

NAIBU Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai amemshushia kipigo mgombea mwenzake Dk.Joseph Chilongani na kusababishwa kuzirai na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa. Ndugai alimpiga kwa fimbo Dk. Chilongani kutokana na kitendo chake cha kutumia simu yake ya mkononi kurekodi matukio ya ubishani baina yao na Saimon Ngatunga. Akizungumza na gazeti hili, mdogo wa mgombea huyo Michael Chilongani alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni katika Kata ya Ugogoni mjini Kongwa wakati wakiwa kwenye kampeni ya kujinadi kwa wanachama. Amesema ndugu yake huyo amepigwa fimbo kichwani na tumboni na kusababisha kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa mbili ambapo alikimbizwa kituo cha polisi kwa ajili ya kupatiwa fomu namba tatu na kisha kupelekwa hospitali. Ndugai alimshushia kipigo mwenzake baada baada ya mgombea aliyetangulia kudai kwamba iwapo Chama kitampa ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge hatahakikisha anapambana ubadhirifu wa fedha katika halmashauri. ‘Baada ya fahamu kumrudia majira ya saa moja na nusu usiku, kaka alidai anasikia maumivu makali kwenye paji la uso pamoja na kichwani huku akipata shida kuzungumza,’ amesema. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa kabla ya Dk. Chilongani kujeruhiwa kwa fimbo na mgombea mwenzake alitaka kumpiga fimbo hiyo mgombea mwingine aliyejinadi kuwa atakomesha ubadhirifu katika halmashauri ambapo kamati ya ulinzi iliwahi kumzuia. Naye Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kongwa Peter Minja amesema kila mgombea ambaye anamalalamiko ayapeleke katika vikao husika. Kuhusu vurugu za ndugai kumpiga mwenzake amesema mpaka sasa hawajapokea malalamiko yoyote kwa utaratibu unaotakiwa na badala yake wamekuwa wakipokea malalamiko ya maneno. Alipotafuwa Mkuu wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kama amepokea taarifa za Ndugai kumpiga mwenzake amesema hana taarifa .Amesema hayupo ofisini na akiwa ofisini na kupata taarifa ataweza kuviarifu vyombo vya habari. NAIBU Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai amemshushia kipigo mgombea mwenzake Dk.Joseph Chilongani na kusababishwa kuzirai na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa. Ndugai alimpiga kwa fimbo Dk.Chilongani kutokana na kitendo chake cha kutumia simu yake ya mkononi kurekodi matukio ya ubishani baina yao na Saimon Ngatunga. Akizungumza na gazeti hili, mdogo wa mgombea huyo Michael Chilongani alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni katika Kata ya Ugogoni mjini Kongwa wakati wakiwa kwenye kampeni ya kujinadi kwa wanachama. Amesema ndugu yake huyo amepigwa fimbo kichwani na tumboni na kusababisha kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa mbili ambapo alikimbizwa kituo cha polisi kwa ajili ya kupatiwa fomu namba tatu na kisha kupelekwa hospitali. Ndugai alimshushia kipigo mwenzake baada baada ya mgombea aliyetangulia kudai kwamba iwapo Chama kitampa ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge hatahakikisha anapambana ubadhirifu wa fedha katika halmashauri. ‘Baada ya fahamu kumrudia majira ya saa moja na nusu usiku, kaka alidai anasikia maumivu makali kwenye paji la uso pamoja na kichwani huku akipata shida kuzungumza,’ amesema. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa kabla ya Dk. Chilongani kujeruhiwa kwa fimbo na mgombea mwenzake alitaka kumpiga fimbo hiyo mgombea mwingine aliyejinadi kuwa atakomesha ubadhirifu katika halmashauri ambapo kamati ya ulinzi iliwahi kumzuia. Naye Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kongwa Peter Minja amesema kila mgombea ambaye anamalalamiko ayapeleke katika vikao husika. Kuhusu vurugu za ndugai kumpiga mwenzake amesema mpaka sasa hawajapokea malalamiko yoyote kwa utaratibu unaotakiwa na badala yake wamekuwa wakipokea malalamiko ya maneno. Alipotafuwa Mkuu wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kama amepokea taarifa za Ndugai kumpiga mwenzake amesema hana taarifa . Amesema hayupo ofisini na akiwa ofisini na kupata taarifa ataweza kuviarifu vyombo vya habari. Chanzo:mwanahalisi online

Lowassa kuchukua fomu urais wakati wowote

EDWARD Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wakati wowote atachukua fomu kugombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Hatua ya Lowassa kuchukua fomu ya urais inakuja siku moja baada ya yeye na mke wake Regina Lowassa, kujiunga na chama hicho katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam ambamo aliahidi kuiongezea Chadema nguvu ya wanachama kuelekea ushindi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu kuiondoa CCM madarakani. Taarifa ya Lowassa kuchukua fomu hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam. “Kesho saa 5 asubuhi hapa makao makuu ya chama, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema. Kutakuwa na shamrashara nyingi sana. Na kutakuwa na matokeo mengi baada ya kesho,” amesema Mwalimu. Aidha, Mwalimu ametoa ufafanuzi kuhusu uwepo wa minong’ono kwamba Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Tundu Lissu, Mwanasheria wa chama hicho kwamba walisusia tukio la Lowassa kujiunga na Chadema. “Jana ilipita minong’ono mingi tu, katibu mkuu wetu yupo kwenye majukumu mengi. Katika kipindi hiki cha uchaguzi tuna mambo mengi. Hatuwezi wote kuwa pamoja. Tunagawanyika kulingana na programu tulizonazo,” amefafanua Mwalimu. Chanzo:mwanahalisi online

Lowassa, mkewe watua Chadema, wakabidhiwa kadi

Hatimaye ameingia Chadema. Ilianza kama uvumi lakini jana ilikuwa dhahiri baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangaza rasmi kukihama chama tawala, CCM na kujiunga na Ukawa kupitia Chadema, huku akisisitiza; “Sasa basi, imetosha.” Baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Lowassa alisema amejiunga na chama hicho kikuu cha upinzani ili kutekeleza azma yake ya kuwakomboa Watanzania na kuendeleza safari ya matumaini kupitia Ukawa. “CCM kimepotoka, kimepoteza mwelekeo na sifa za kuendelea kuiongoza Tanzania,” alisema Lowassa katika mkutano wa kumkaribisha Chadema uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Ledger Bahari Beach na kurushwa moja kwa moja na vituo kadhaa vya televisheni na redio. Dakika chache baada ya mkutano huo, CCM kupitia mitandao yake ya kijamii ilitangaza kuitisha mkutano wa wanahabari leo mchana kutoa taarifa muhimu, ikiaminika kuwa utakuwa wa kumjibu kiongozi huyo. Katika mkutano huo, Lowassa alitumia dakika 13 kueleza sababu za kujiunga Chadema, mbele ya wenyeviti wenza wa vyama vinavyounda Ukawa; Mbowe, Dk Emmanuel Makaidi (NLD), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF). Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Naibu wake (Bara), John Mnyika, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu hawakuonekana na hawakupatikana kuzungumzia sababu za kutokuwapo katika tukio hilo muhimu. Lowassa ambaye aliingia katika ukumbi huo saa 10.20 jioni akiwa ameambatana na mkewe, Regina, watoto wake, ndugu na jamaa, pia aligusia sakata la kampuni ya kufua umeme ya Richmond lililosababisha ajiuzulu wadhifa wa waziri mkuu mwaka 2008, kwamba alifanya hivyo kwa manufaa ya nchi na alishindwa kuvunja mkataba huo kutokana na amri kutoka mamlaka ya juu. Ahama na wimbo wake Wakati Lowassa akizungumza, wanachama wa Chadema walikuwa wakiitikia ‘peoples power’, na alipomaliza hotuba yake wanachama wao waliimba wimbo maalumu kuwa wana imani naye, “Tuna imani na Lowaasaa, oya oya oyaa.” Wimbo huo pia uliimbwa na wanachama wa CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho mjini Dodoma, baada ya jina mbunge huyo wa Monduli kutokuwamo kati ya wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu kuwania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ambayo ilikwenda kwa Dk John Magufuli. Mchakato CCM Katika hotuba yake, Lowassa aligusia jinsi mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ulivyogubikwa na mizengwe na kusisitiza: “Nimetumia muda huu kutafakari kwa kina yaliyotokea Dodoma na hatima yangu katika siasa nchini. Pamoja na yaliyotokea Dodoma azma yangu iko palepale ya kuanza mchakamchaka wa maendeleo ya kuiondoa nchi katika umaskini. “Najua sote tumevunjika moyo kwa yaliyotokea Dodoma na mazingira yaliyopelekea matokeo yale. Mchakato uligubikwa na mizengwe, ukiukwaji wa maadili, uvunjaji wa katiba na taratibu za uchaguzi za CCM.” Alisema mchakato huo ulisimamiwa kwa upendeleo wa dhahiri na chuki iliyokithiri dhidi yake... “Kikatiba Kamati ya Maadili si chombo rasmi na haina madaraka ya kuchuja na kupendekeza majina miongoni mwa wale wanaoomba kugombea urais kupitia CCM. Kilichotokea Dodoma ni kupora madaraka ya Kamati Kuu na kukiuka katiba ya CCM.” Alisema vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu viliitishwa na kuburuzwa ili vitekeleze azma ya watu binafsi bila kujali demokrasia, katiba, kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM. “Kibaya zaidi ni kile kitendo cha kuwanyima wagombea wote 38 haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu,” alisema. Alisema Watanzania walitarajia chama kinachoongoza nchi kiwe mfano wa utawala wa sheria na kinara katika kutetea misingi ya haki na demokrasia na siyo kuihujumu, lakini yaliyotokea Dodoma yameitia dosari nchi. Msimamo “Sikutendewa haki. Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa bado nina imani na CCM…, CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu,” alisema. Lowassa alisema hata Mwalimu Julius Nyerere alisema CCM siyo baba yake wala mama yake na kama Watanzania hawapati mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya chama hicho. “Baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuwa kuanzia leo ninaondoka CCM na kuitikia wito wa Ukawa kupitia Chadema kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya nchi yetu,” alisema. Richmond Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Lowassa alizungumzia sakata la Richmond akisema anashangazwa jinsi anavyohusishwa nalo licha ya kuwa ameshalitolea ufafanuzi na kuwataka wenye ushahidi waupeleke mahakamani. Alisema alijiuzulu uwaziri mkuu kwa niaba ya Serikali huku akisisitiza kuwa wakati huo waliingia mkataba na kampuni hiyo kutokana na shida ya umeme wakati huo, lakini baadaye waligundua kuwa ilikuwa na matatizo mengi na alipotaka kuvunja mkataba huo alizuiwa na mamlaka za juu. Alisema walikaa kikao na makatibu wakuu kujadili suala hilo na kwamba mmoja wa makatibu hao alitoka nje na kuzungumza na simu kwa zaidi ya saa moja, baada ya kurudi katika kikao alimueleza kuwa mkataba huo usivunjwe na kwamba ni amri kutoka mamlaka ya juu. Mbowe aweka msimamo Katika hotuba yake ya kumkaribisha Lowassa, Mbowe alisema wakati jina la waziri mkuu huyo wa zamani likikatwa CCM, alifurahi na kuamini kuwa atajiunga na upinzani. Alisema baada ya kuibuka kwa minong’ono juu ya Lowassa kuhamia Chadema, alipigiwa simu na viongozi wengi wa CCM wakimtahadharisha kuwa wasikubali ajiunge katika chama hicho. “Hata mimi niliwajibu kuwa hatuwezi kumpokea Lowassa, tena niliwajibu kwa Kiingereza, “over my dead body (sitampokea mpaka kufa)”. Lakini kumbukeni kuwa Chadema ni chama cha kujenga mshikamano na hakiwezi kuhukumu bila ushahidi,” alisema Mbowe. Akifafanua kauli ya ‘kula matapishi yake’, inayotokana na viongozi wa chama hicho kuwahi kumtuhumu Lowassa katika masuala mbalimbali ya ufisadi miaka ya nyuma alisema: “Hatuwezi kufikiri mambo mema mapya kwa kutafakari mambo mabaya ya zamani. Ni nani aliye mtakatifu mpaka awe na uwezo wa kushika jiwe na kumpiga mwenzake, hii si CCM tu hata Chadema au Lowassa.” Alisema Ukawa ikichukua dola haitaongoza nchi kwa kulipa visasi, bali kuwaletea Watanzania maendeleo huku akisisitiza kuwa kumleta Lowassa Ukawa haikuwa kazi rahisi kwani vilifanyika vikao vingi. “Lowassa ni waziri mkuu wa kwanza mstaafu kusema CCM si mama yake. CCM kimejenga hofu kwa wanachama wake. sisi Ukawa tunaamini nchi yetu inahitaji fikra na mtazamo mpya, tumevutana sana lakini tumeendelea kuwa kitu kimoja kwa masilahi ya Watanzania,” alisema. Mbowe alisema angekuwa mwendawazimu kumkataa Lowassa ambaye ana nguvu kubwa ya kisiasa kujiunga na Chadema wakati atakiletea chama hicho wanachama zaidi ya milioni moja na kusisitiza kuwa mtaji wa chama cha siasa ni watu. “Lowassa hujui tu minyororo uliyoifungua baada ya kuondoka CCM, umefungua minyororo ya watu wengine akiwamo Ole Medeye yule pale (akimwonyesha, Naibu waziri wa zamani, Goodluck). Siasa ni mchezo unaobadilika kulingana na wakati,” alisema. Alisema chama ambacho hakiamini katika mabadiliko si chama na kwamba Chadema hakiongozwi kwa kauli yake (Mbowe), bali katiba, kanuni, maadili na miiko. “Chadema hatupo kugombea vyeo, bali kulikomboa Taifa na kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa, hivyo viongozi na wanachama wa Chadema na Ukawa msihofu. Aliyeingia Chadema 1992 na mwaka huu wote wana haki sawa. Wapo watu tuliowatukana sana huko nyuma lakini hiyo haizuii kuwapokea,” alisema na kuongeza: “Watanzania ondoeni hofu maana tunapambana na mfumo si mtu, Lowassa na wenzake watatupa mbinu za kupambana na mfumo. Leo hii hata ukimchukua malaika na kumpeleka CCM baada ya mwezi mmoja atageuka ibilisi.” ‘Ampongeza’ Kikwete Mbowe alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo cha kuliondoa jina la Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM, kwa maelezo kuwa wakati wakimuondoa wapinzani walikuwa wakifurahia. Mbali na Mbowe, Dk Makaidi, Mbatia na Makamu Mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji walipongeza kitendo cha Lowassa kujiunga na Ukawa, huku Mbatia akisema Tanzania bila CCM inawezekana. “Sasa ni Tanzania kwanza na vyama baadaye. Hakuna machafuko yatakayotokea nchini lakini walioko madarakani wasituchokoze maana hoja za kupambana nao tunazo,” alisema Mbatia Ulinzi mkali Watu waliofika katika ukumbi huo, wakiwamo waandishi wa habari walikuwa wakikaguliwa kwa vifaa maalumu kabla ya kuingia ndani. Ukaguzi huo ulifanywa na walinzi wa Chadema (Red Brigade) na walinzi wa kampuni binafsi. Waandishi walioingia ndani ya mkutano huo waliitwa kwa majina yaliyokuwa yameorodheshwa mapema, hata walipokuwa ndani ya ukumbi walikaa maeneo waliyopangiwa na kutakiwa kutosimama hovyo. Chanzo:mwanancho.co.tz

Wednesday, July 29, 2015

Kiongozi wa kundi la Taleban amefariki

Habari kutoka kwa serikali ya Afghanistan zimeiambia BBC kuwa kinara mkuu wa kundi la wapiganaji wa Taliban, Mullah Omar amefariki. Lakini habari hizo bado hazijathibitishwa rasmi na kundi hilo. Kwa miezi kadhaa kumekuwepo na tetesi kuhusiana na kifo cha Mullah Omar. Kifo hicho kimetokea wakati ambapo serikali ya Afghanistan ilikuwa inajiandaa kuanza mashauriano ya amani na kundi hilo la Taliban. Waandishi wa habari wameitwa na serikali ili kuhudhuria kikao cha wanahabari jijini Kabul, ambao unatazamiwa kufanyika muda mchache ujao. Taarifa nyingine zinasema kuwa huenda alifariki miaka kadhaa iliyopita. Chanzo:BBC Swahili

LOWASSA AJIVUA GAMBA NA KUVAA GWANDA

Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa leo amejiunga na UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika hafla iliyohudhuriwa na waandishi wa Vyombo Mbalimbali vya habari. Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na Viongozi wote wanaunda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA akiwemo mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Maeuzi Mh James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel Makaidi. Lowassa ambaye aliambatana na mkewe Mama Regina Lowassa wote walikabidhiwa kadi ya kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema na Mh Freeman Mbowe. Katika Hotuba yake mara baada ya kutangaza kujiunga na Chadema Mh Lowassa ameongelea mambo mengi yaliyomshawishi kujiondoa CCM na kujiunga na UKAWA kupitia CHADEMA hosusani suala la mchakato wa kupata Mgombea Urais kupitia CCM lilivyotawaliwa na zengwe. Katika Hotuba yake Mh Lowassa amewaomba Watanzania wote wenye kulitakia mema Taifa Kujiunga na UKAWA kwa ajili ya kutimiza Safari ya Matumaini.

Obama awaonya viongozi wa Afrika

Rais wa Marekani Barrack Obama,amewasuta viongozi wa Afrika ambao wanaendelea kusalia madarakani hata baada ya katiba kutowaruhusu kuendelea kuwania tena wadhfa wa urais. Katika hotuba ya kwanza ya rais wa Marekani kwa muungano wa Afrika katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa,amesema kuwa Afrika haitapiga hatua iwapo viongozi wake watakataa kuondoka madarakani baada ya muda wao kuisha. Amemtaja hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano na anafahamika pakubwa kote duniani huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara Afrika, tofauti na marais wengi wanaoendelea kukwamia madaraka. Ameongezea kuwa wakati waandishi wanapofungwa huku wanaharakati wakitishwa,demokrasia huwepo tu kwa jina. Akimnukuu shujaa Nelson Mandela akisema kuwa unapoheshimu uhuru wa wengine watu wote huwa huru. Amesema kuwa ishara kuu ya maendeleo katika taifa ni vile linavyowachukulia wanawake wake. Amewaambia viongozi wa Afrika kwamba maendeleo ya bara hili yanategemea demokrasia,uhuru na haki za kibinaadamu. Anasema kuwa muda umewadia wa kubadilisha mtizamo wa Afrika kama bara duni lenye kulemewa na umaskini na mizozo. Aidha amepongeza umoja wa Afrika AU na shirika la Umoja wa mataifa katika mapambano dhidi ya makundi ya wapiganaji wa kiislamu kama vile, Boko Haram kaskazini mwa Nigeria na Al - Shaabab Afrika mashariki. Amemtaja hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano na nafahamika pakubwa kote duniani huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara Afrika, tofauti na marais wengi wanaoendelea kukwamia madaraka. Chanzo:BBC Swahili

Mwana wa Gaddafi ahukumiwa kifo

Mahakama moja nchini Libya imemuhukumu kumyonga mwana wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Gaddafi,Saif al Islam na wengine wanane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011. Walikuwa wameshtakiwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa mamlakani kwa kujaribu kazima maandamano wakati wa mapinduzi hayo. Saif al Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia teknolojia ya kanda ya video. Kwa sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji wa Zintan ambao wamekataa kumuachilia huru. Chanzo:BBC Swahili

Dk Salim: Chama chochote kinaweza kushika dola

Waziri mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema chama chochote cha siasa nchini kina nafasi ya kushika dola endapo kitafuata kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika. Dk Salim alisema hayo jana baada ya kufungua semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Utamaduni na Urithi kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM). Alisema demokrasia katika vyama vya siasa imezidi kukua na kwamba kikubwa kinachotakiwa ni kutumia njia bora na siyo kurushiana maneno ambayo hayana msingi. “Utakuta viongozi wa vyama wenyewe kwa wenyewe wanarushiana maneno, huyu hafai mara siyo raia wa nchi hii, sasa haya mambo kwenye siasa hayatakiwi. “Ni lazima kila kiongozi wa chama cha siasa atambue wajibu wake katika jamii,” alisema Dk Salim. Pia maadili ya viongozi katika Taifa yameporomoka, hivyo aliwaasa wananchi kuchagua viongozi bora kwa masilahi ya Taifa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. “Sasa kiongozi anagombea nafasi fulani kwa masilahi yake binafsi, siyo kwa wananchi na anawaomba wampigie kura,” alisema Dk Salim. Aliwataka wananchi kuwa watulivu na kuilinda amani katika kipindi hiki cha uchaguzi. Katika semina hiyo ya Urithi na Utamaduni wa Tanzania alisema nchi ina urithi lakini haujapewa kipaumbele. Alisema suala la uchumi na maendeleo ndilo lililopewa kipaumbele. Hata hivyo, alisema jamii haijachelewa na inaweza kuweka mikakati itakayofanya jambo fulani kutambulika zaidi. Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Profesa Abdallah Bujra alisema semina hiyo itakuwa ya siku tatu. Alisema Taifa haliwezi kupiga hatua bila suala hilo kutiliwa mkazo. Chanzo:mwananchi.co.tz

Lowassa ajiunga rasmi na Ukawa, akabidhiwa kadi ya uanachama Chadema

Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Lowassa ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar na kusema amekubali mwaliko wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Amesema kuwa CCM haikumtendea haki katika kupitisha majina ya wagombea urais hivyo hawezi kuendelea kubaki kwenye chama hicho ‘’ Niliwekewa mizengwe kuhakikisha Jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu’’. Waziri Mkuu huyo wa zamani ameeleza kuwa nia yake ni kuleta mabadiliko hivyo kujiunga na Chadema ni kuendeleza nia yake ya kuwatumikia Watanzania ‘’ CCM Si baba yangu wala Mama yangu, Watanzania kama wameyakosa mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM’’ Aidha ameongeza kuwa hajakurupuka kufanya uamuzi huo na kuendelea kubaki ndani ya CCM itakuwa ni unafiki ‘’ Sijakurupuka kwa uamuzi huu hivyo basi kuanzia leo natangaza rasmi kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA kupitia Chadema’’ alisema Lowassa. Hata hivyo muda mfupi baada ya kutangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimkabidhi Lowassa kadi ya uwanachama. Chanzo:mwananchi.co.tz

Tuesday, July 28, 2015

Lowassa akihama chama cha CCM

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa leo amejiunga rasmi na Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA na kuondoa hali ya sintofahamu miongoni mwa watanzania baada ya kutopata nafasi ya kuteuliwa na Chama cha mapinduzi ,CCM kupeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba. Akizungumza katika Mkutano uliowakusanya wanachama waliounda UKAWA, na waandishi wa habari, Lowassa alisema amekubali mwaliko wa kujiunga na UKAWA hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. Amesema baada ya kutafakari kwa kina baada ya yale yaliyotokea katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM mjini Dodoma kutoridhishwa nayo, ameamua kujiengua na chama hicho. ''Katiba ya CCM ilikiukwa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi,nilifanyiwa mizengwe,majungu na habari za uongo kuhakikisha kuwa jina langu halifikishwi kwenye kamati kuu na halmashauri kuu kwa ajili ya kujadiliwa licha ya kuwa nilikuwa nikiungwa mkono na Wanachama wengi zaidi kuliko wagombea wengine'' alisema Lowassa. Chanzo:BBC Swahili

Michango ya kampeni yawaliza wagombea CCM

Michango ya kampeni za kujinadi kwa wananchi katika majimbo mbalimbali nchini imelalamikiwa na baadhi ya wanachama wa CCM wanaowania kuteuliwa kugombea ubunge. Kutokana na ukali wa michango hiyo, baadhi ya wagombea wamelazimika kujitoa katika mchakato, wengine wakisema hawawezi kumudu kulipa fedha hizo kwa maelezo kwamba ni kiwango kikubwa. Michango hiyo inatofautiana baina ya jimbo moja na jingine. Hata hivyo chama hicho kimesema hakitishwi na wachache wasioridhishwa na uamuzi unaofanywa kwa masilahi mapana ya chama hicho. Akizungumzia malalamiko hayo jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: “Tunaendelea na mchakato wa kura ya maoni. Kila mtu yuko bize na kura, siwezi kuzungumzia watu wachache wasioridhika wakati wengi wanaendelea na utaratibu tuliojiwekea.” Wagombea watatu katika Jimbo la Bukoba Mjini wamelalamikia kuchangia gharama hizo ambazo kwa mujibu wa agizo la Kamati ya Siasa ya Wilaya, kila mmoja anatakiwa kutoa Sh2 milioni hadi ifikapo leo kabla ya kuanza kwa kura za maoni Agosti Mosi. Mmoja wa wagombea hao, George Rubaiyuka alidai kuwa kiasi hicho ni kikubwa na kwamba alikuwa tayari amelipa Sh200,000 huku mgombea mwingine, Dk Anatory Amani akiomba aongezewe muda ili akamilishe malipo hayo. Mgombea mwingine ambaye hajakamilisha malipo hayo ni Mujuni Kataraiya ambaye pia alipendekeza Kamati ya Siasa kuangalia upya kiwango kilichowekwa. Aliyekuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Chalinze, Imani Madega amekaririwa akisema hataweza kukamilisha ndoto yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kutokana na gharama kuwa kubwa. Kadhalika, mgombea ubunge Jimbo la Morogoro Mjini, Simon Berege alisema kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilikutana Julai 21 na kuchanganua gharama za uchaguzi na kila mgombea alitakiwa kulipa Sh6.9 milioni siku hiyohiyo tena zikiwa taslimu. Berege alisema baada ya uamuzi huo aliomba kupewa muda hadi siku ya pili kukamilisha lakini mgombea mwenzake alijitolea kumkopesha jambo ambalo hakuliafiki. “Ninaamini ukubwa wa gharama iliyowekwa na sharti la kutokushiriki kwenye kampeni hizo isipokuwa tu kwa kulipa fedha hiyo yote ama kwa awamu mbili na kuzuia mtu kufika kwenye mikutano ya kampeni kwa usafiri binafsi umefanywa kwa makusudi ili kufanikisha nia ile ya awali ya kuwa na mgombea mmoja,” alisema Berege. Alisema katika mikutano ya kampeni ambayo amekuwa hahudhurii, imekuwa ikitolewa taarifa kuwa amejitoa jambo ambalo si sahihi na kwamba amekuwa akiwasiliana na mkurugenzi wa uchaguzi wa chama akimweleza kuwa anaendelea kufanya jitihada za kutafuta fedha huku akitaka jina lake liendelee kutajwa katika mikutano ya kampeni. Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Milonge alisema hakuna mizengwe ya aina yoyote inayofanyika na kwamba chama kinamtambua Berege kuwa ni mgombea kwa kuwa fomu yake imejazwa kwa usahihi. Alisema Berege haonekani katika kampeni za kujitambulisha kwa wanachama na kwamba alipewa muda wa kutafuta fedha zilizotakiwa kwa ajili ya gharama za kampeni hiyo, hawezi kutajwa mpaka atakapoonekana katika kampeni. Kadi feki zalalamikiwa Huko mkoani Mbeya, wagombea ubunge wa jimbo jipya la Busokelo ambalo awali liliitwa Rungwe Mashariki, juzi wakiwa kwenye Kata ya Lufilyo walitaharuki baada ya kukamatwa kwa kadi 900 za CCM zilizodaiwa kuingizwa kwenye kata hiyo kwa lengo la kumpendelea mmoja wa wagombea. Hata hivyo, Katibu Msaidizi CCM Wilaya ya Rungwe, Simon Yawoo alisema kadi hizo zilitolewa kwa wanachama waliokuwa wakizihitaji kwenye kata hiyo na kwamba ni halali. Dk Mahiga alia rushwa Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Agustino Mahiga amekitaka chama hicho na Serikali kushughulikia tatizo la rushwa linalojitokeza wakati wa huu wa uchaguzi kwa uzito unaostahili kwa kuwa vitendo hivyo vinashusha heshima ya chama hicho tawala na kuchafua taswira ya nchi kimataifa. Dk Mahiga ambaye sasa ni mmoja wa makada 13 wa CCM wanaoomba kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge Iringa Mjini, aliwataka wananchi kushiriki katika vita hiyo ya rushwa na ufisadi katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kusaidia kuwapata viongozi bora watakaoongoza na kuliletea tija Taifa. Chanzo;mwananchi.co.tz

“Watanzania wanataka mabadiliko...watayatafuta nje ya CCM"

Kauli ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuwa Watanzania wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM inaweza kutimia mwaka huu. Mwalimu alikuwa akihutubia Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Dodoma wakati wa mchakato wa kumpata rais wa awamu ya tatu mwaka 1995. Alisema mambo mengi lakini aliwasisitizia wajumbe kuwa Watanzania wanataka mabadiliko na kwamba wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM. Huku akisikilizwa kwa umakini, Mwalimu alisema kuna mambo Watanzania wanataka uongozi wa awamu ya tatu uyafanye mojawapo ni kupambana na rushwa kwa kuwa Watanzania wengi wamechoka na rushwa. “Wajumbe wa zamani wa NEC watakumbuka nimepigia sana kelele rushwa wakati nikiwa mwenyekiti. Sasa hivi hali ya rushwa ni mbaya.” Aliongeza; “Pili, Tanzania ni masikini, nchi ni ya wakulima na wafanyakazi ambao si matajiri, nchi haijawa ya matajiri, chama hakijawa chama cha matajiri, tushughulikie kwa dhati matatizo ya wananchi, hali zao za uchumi, viwandani, mashambani, shuleni, hospitalini na ateuliwe mtu ambaye anajua nchi bado ya masikini, wakulima na wafanyakazi na awe anatambua hivyo.” Suala la tatu alilozungumzia ni kuhusu udini akisema umeanza kuzungumzwa kama vile ni sifa. Alisema zamani hawakuwa wanazungumzia udini wala kujali dini ya mtu kwa vile ni ya mtu mwenyewe anaijua na hawakuwa wanauliza dini ya mtu, kwa kuwa haiwahusu. “Tunataka nchi yetu ipate kiongozi safi, na kiongozi safi hawezi kutoka nje ya CCM, ninyi wapiga kura, mnaweza kutupatia kiongozi safi kwa kura zenu, sasa tupatieni kiongozi safi.”

Lowassa sasa rasmi Ukawa,muda wowote kutangazwa mgombea urais

Katika dakika za mwishomwisho wakati wa mchakato wa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, habari za mmoja wa wagombea aliyekuwa na nguvu katika kinyang’anyiro hicho, Edward Lowassa kwamba angeenguliwa zilivuma mno na kuibua swali la atakatwa hakatwi? Baada ya Kamati Kuu ya chama hicho (CC), kutangaza majina matano ya waliopitishwa katika hatua ya awali, bila ya jina lake kuwamo, likaibuka swali la pili; atatoka hatoki? Sasa jibu la swali hilo la pili limepatikana. Ametoka na sasa ni rasmi kwamba atakuwa mgombea urais kupitia Ukawa. Usiku wa kuamkia jana, Waziri Mkuu huyo wa zamani alihudhuria rasmi kikao cha Kamati Kuu ya Chadema katika kile kilichoelezwa kuwa ni kutambulishwa pamoja na kujadiliana mikakati ya kuing’oa CCM madarakani. Baada ya jana mchana, viongozi wa Ukawa, Mwenyekiti wa NCCR – Mageuzi, James Mbatia; Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba walikutana na waandishi wa habari Dar es Salaam na kumkaribisha rasmi Lowassa kwenye umoja huo huku wakitumia muda mrefu kumsafisha dhidi ya tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akihusishwa nazo. Atinga Kamati Kuu Chadema Mwandishi wetu alimshuhudia mbunge huyo wa Monduli akihudhuria kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chadema juzi usiku. Awali kikao hicho kilianza saa 9.30 alasiri katika Hoteli ya Ledger Bahari Beach, Dar es Salaam ambacho Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho walipata taarifa ya kufanyika kwa kikao hicho ghafla Jumamosi kati ya saa nne na tano usiku kwa kupigiwa simu, lakini hawakuambiwa ukumbi wala madhumuni ya kikao hicho zaidi ya kuambiwa kuwa wanatakiwa wawepo Dar es Salaam siku hiyo. Lowassa kikaoni Lowassa alialikwa kuhudhuria kikao hicho na aliwasili katika lango la kuingia kwenye hoteli hiyo saa 3.02 usiku akiwa ndani ya gari jeusi aina ya Toyota Lexus, akiwa amevalia suti nyeusi na shati jeupe na kupokewa na viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe. Baada ya hapo aliongozwa kuelekea katika Chumba cha Wageni Mashuhuri (VIP) na kukutana na viongozi wachache wa chama hicho wakiwamo Mbowe na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohammed. Mazungumzo hayo yalidumu kwa takribani dakika 18 na ilipofika saa 3.20 usiku, walitoka na kuingia katika ukumbi ambao kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilikuwa kinafanyika. Lowassa alishiriki kikao hicho kwa takriban dakika 98 na ilipofika saa 4.58 usiku, alitoka katika ukumbi huo akisindikizwa na Mbowe, Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa, Makamu Mwenyekiti (Bara), Profesa Abdallah Safari, Mohammed na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu ambao baadaye walirejea ukumbini kuendelea na kikao. Habari za ndani Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema baada ya Lowassa kuwasili na kutambulishwa kwa wajumbe, alipewa nafasi ya kuzungumza. Miongoni mwa mambo anayodaiwa kuwagusia ni pamoja na kashfa ya Richmond ambayo ilimlazimu kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008. Pia, inaelezwa kuwa wajumbe walitaka kujua utajiri wake na baada ya kupewa majibu, walijadiliana jinsi ya kuiangusha CCM katika Uchaguzi Mkuu. Ukawa wampokea, wamtetea Saa 18 baada ya Lowassa kutambulishwa katika Kamati Kuu ya Chadema, viongozi wengine wa Ukawa waliitisha mkutano wa wanahabari jana mchana na kumkaribisha rasmi katika harakati za kuing’oa CCM huku wakimsifia kuwa ni mchapakazi na mfuatiliaji wa karibu wa majukumu anayokabidhiwa. Hatua hiyo Ukawa juu ya mtazamo kwa Lowassa ambaye amekuwa akituhumiwa kwa kashfa mbalimbali na viongozi hao wa upinzani, inaonyesha dhahiri kwamba ameshapata baraka za kujiunga na umoja huo kupitia Chadema. Wakati wa sakata la Richmond, viongozi wa upinzani walikuwa wakimponda kiongozi huyo na Dk Slaa aliwahi kumuweka kwenye orodha aliyoiita ‘list of shame’. Viongozi hao walimtetea na kusema kuwa hakuna aliyewahi kuthibitisha tuhuma dhidi ya Lowassa na kuongeza kuwa mfumo wa CCM ndiyo wenye matatizo ya rushwa na si mtu. Profesa Lipumba alisema suala la ufisadi ni mfumo na si la mtu mmojammoja... “Sisi tunaponda ufisadi na mfumo wa kifisadi na chanzo kikubwa cha ufisadi ni mfumo ndani ya CCM, kwanza tuing’oe CCM, hapo ndipo tutakapoweza kuondoa ufisadi na kujenga msingi wa kupambana na ufisadi na rushwa iliyopo. “Lowassa alikumbwa na tuhuma za ufisadi mwaka 2008, leo ni 2015 lakini ufisadi umeongezeka au umepungua? Lowassa hayupo serikalini, Tegeta Escrow Akaunti imetokea wakati gani, Lowassa alikuwapo? Tatizo ni mfumo na jambo la kwanza ni kuing’oa CCM,” alisema. Makamu Mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji alihoji: “Mbona CUF iliwahi kupigana na kuuana na CCM mwaka 2000 lakini leo wameunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa? “Makaburu waliuana wakamfunga Mandela (Nelson) lakini alitoka gerezani na kukaa chini akazungumza nao, kipi cha ajabu? Msumbiji walipigana vita miaka 18, lakini walikubaliana, basi kama Lowassa anakubali kwamba Ukawa ni muhimu kwa Watanzania, amezinduka na kuona hata bora aende Ukawa akafanye mabadiliko.” Alisema kwenye siasa hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu, bali kuna kudumu kwa hoja ambazo zina masilahi kwa Taifa... “Wacha Mzee Lowassa aje, tumechoka kuonewa.” Dk Makaidi alisema kama Lowassa angekuwa mbaya kiasi hicho, basi angekuwa amekwisha shtakiwa kama ilivyo kwa viongozi wengine ambao tayari wameshahukumiwa vifungo kwa matumizi mabaya ya madaraka au rushwa. “Hata Lowassa mwenyewe aliwahi kuuliza mwenye uthibitisho kuwa yeye ni fisadi ajitokeze na kumhukumu lakini mpaka leo hakuna aliyefanya hivyo.” Alisema iwapo Lowassa ataamua kujiunga na Ukawa, wanamkaribisha kwa moyo wote kwani hakuna mwenye uthibitisho kuwa ni fisadi... “Mimi nasema sina wasiwasi, tunamkaribisha, sijaona ubaya wake.” Mbatia alisema Ukawa inamwalika kila Mtanzania aliye tayari kuuondoa mfumo kandamizi na dhalimu wa CCM na kwamba watashirikiana naye kujenga Taifa imara na kwamba Lowassa ni miongoni mwa wanaokaribishwa. “Tunachukua fursa hii kipekee kumwalika Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, mheshimiwa Edward Lowassa ajiunge na Ukawa na tuko tayari kushirikiana naye kuhakikisha tunaiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu ujao. “Tunaamini mheshimiwa Lowassa ana uwezo wa kuhamasisha umma kuikataa CCM yenye kusimamia mifumo isiyotenda haki. Ni mchapakazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa utendaji katika majukumu anayokabidhiwa.” Katika mkutano huo uliodumu kwa dakika 30, Mbatia alisema Ukawa inaamini kwa masilahi mapana ya Taifa inamhitaji kila Mtanzania ambaye yupo tayari kujiunga nao kuhakikisha Taifa linakuwa salama na lenye amani ya kweli ambayo msingi wake ni haki. “Katika kutafakari kwa kina masilahi mapana ya Taifa letu, Ukawa tunahitaji viongozi wenye sifa, uwezo na weledi katika kulinda, kuheshimu na kusimamia rasilimali za Taifa kwa masilahi ya Watanzania wote. “Viongozi wa aina hii hawawezi kuwa ndani ya CCM, maana mfumo wake haumpi kiongozi kutumia vipaji vyake au ubunifu wake katika kusimamia masilahi ya Taifa letu,” alisema. Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi Kuu ya CUF Buguruni na kuhudhuriwa na wenyeviti na makatibu wote wa Ukawa kasoro Dk Slaa, Mbatia alisema: “Hatutakubali kunyamaza pale sauti zetu zinaponyamazishwa kwa lazima bila sababu. Tusikubali kunyimwa fursa ambazo tuna uwezo nazo… tuwe tayari kushiriki michakato ya kidemokrasia ya kuleta mabadiliko na kupata viongozi bora.” Akizungumzia uamuzi wa kumpokea Lowassa, Profesa Lipumba alisema huo ni wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF na ambao uliafikiwa na Ukawa kwa ujumla. “Msimamo wa chama chetu tangu kwenye Baraza Kuu ni mmoja, kuwa sisi kuendelea kushirikiana na Ukawa na tupate mgombea mmoja. Tuna wagombea wazuri wa urais lakini tunataka kupata mgombea mmoja atakayeweza kutusaidia kupata rais na kuiondoa CCM,” alisema Profesa Lipumba. Alisema hata tamko la jana la Ukawa limetokana na baraka za Baraza Kuu la Uongozi la hicho. Alipoulizwa kuhusu chama chake kusuasua katika kinyang’anyiro cha kumpata mgombea wa urais kupitia Ukawa, Profesa Lipumba alisema chama hicho kilikuwa kinajadili suala hili kwa mujibu wa kanuni na taratibu zake. “Wakati wote nilipochukua fomu, nilieleza wazi kuwa nipo tayari kugombea urais na nitagombea kupitia Ukawa na iwapo atatokea mgombea mwingine nitashirikiana naye na huu ndiyo msimamo hata wa chama,” alisema. Kuhusu siku watakayomteua mgombea wa urais, Profesa Lipumba alisema mchakato huo utafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao kulingana na makubaliano ya Ukawa. ‘Ruksa’ kuchagua chama Haji alisema Lowassa atachagua chama cha kujiunga nacho na huko atafuata taratibu iwapo atachagua kugombea nafasi ya urais. “Kama atajiunga na chama A, B au C, basi chama hicho kitafuata taratibu zake, kama atajiunga na Chadema basi atafuata taratibu za huko lakini sisi vyama vingine tutamuunga mkono,” alisema. Alipoulizwa iwapo Ukawa inakaribisha kwa sababu anaonekana kuwa na nguvu ya kuiangusha CCM, Haji alisema Ukawa ndiyo yenye uwezo wa kuiangusha CCM na mgombea wa umoja huo ndiye anayeshika bendera. Mbowe kimya Tofauti na mikutano ya nyuma ya umoja huo, Mbowe jana hakuzungumza chochote licha ya kuulizwa maswali moja kwa moja kuhusu kauli zake za awali zilizowahi kuonekana bayana kumshambulia Lowassa. Hata alipofuatwa na wanahabari baada ya mkutano huo hakuzungumza chochote zaidi ya kueleza kuwa mambo yote yameelezwa kwa kina na wenzake. Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Mohamed alipotakiwa kuthibitisha taarifa za Lowassa kushiriki vikao vya Chadema na kwamba ameshajiunga na chama chao, alisema kwa kifupi: “Sitaki kuzungumzia lolote juu ya hilo.” Mgombea bado bado kwanza Akizungumzia sababu za kuahirisha kumtangaza mgombea mara kwa mara ikiwamo jana, makamu mwenyekiti huyo wa Chadema alisema wamekubaliana vyama vimalize utaratibu wa vikao vya kikatiba ili kupata wagombea na baadaye wakae pamoja na Ukawa kupitisha jina moja na kumtangaza mgombea mmoja. Alisema vyama vya siasa vinatakiwa kubadilika kulingana na hali halisi, hivyo kuna mambo ambayo yalitakiwa kufikiriwa zaidi kabla. Pamoja na suala la kumpata mgombea wa urais, alisema bado kuna masuala yaliyo mezani yakiwamo kuachiana majimbo mapya 26 na yale ya Mkoa wa Dar es Salaam yaliyoonekana kuwa na mvutano mkubwa wa nani atayawakilisha. Chanzo:mwananchi.co.tz

Monday, July 27, 2015

UKAWA: Lowassa mtu safi, wamkaribisha rasmi

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umemkaribisha Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli kujiunga na umoja huo. Rai ya kumtaka Lowassa kujiunga na UKAWA imetolewa leo Makao Makuu ya CUF, jijini Dar es Salaam katika mkutano uliohudhuriwa na Wenyeviti wenza wa UKAWA, Freeman Mbowe (Chadema), Emmanuel Makaidi (NLD), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR – Mageuzi). Mbali na kumkaribisha Lowassa, UKAWA wamesema mgombea urais kwa tiketi ya umoja huo atatangazwa wiki ijayo. Akizungumza katika mkutano huo Mbatia amesema, “Tunachukua fursa hii kipekee kumwalika Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mheshimiwa Edward Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana naye katika kuhakikisha kuwa tunaiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.” “Tunaamini Mheshimiwa Lowassa ana uwezo wa kuhamasisha umma kuikataa CCM yenye kusimamia mifumo isiyotenda haki. Ni mchapa kazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa utendaji katika majukumu anayokabidhiwa,” amesema Mbatia.Mbatia amesema hatua ya Lowassa kukaribishwa UKAWA imekuja baada ya Watanzania kushuhudia hadaa, udhalilishaji, upendeleo na ukandamizaji katika mchakato wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya CCM. Pia kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu, kanuni na katiba ya chama hicho. Pia, katika kujenga mshikamano ndani na nje ya vyama hivyo kuelekea na baada ya uchaguzi mkuu katika kuleta mabadiliko yatakayo toa katiba bora na kufikia maendeleo yatakayojenga demokrasia ya kweli na kuachana na uonevu, udhalilishaji, fitna na majungu yanayoendeshwa na CCM. Akizungumza kuhusu harakati zilizokuwa zikiendeshwa kwamba “Lowassa ni fisadi na hasafishiki” Lipumba amesema, “…masuala ya ufisadi ni masuala ya mfumo. Lowassa alitoka madarakani mwaka 2008. Lakini mpaka sasa ufisadi bado umeendelea kukua kwa kasi licha ya Lowassa kutokuwa serikalini.” “Mpaka sasa hakuna mashtaka mahakamani dhidi ya Lowassa. Tunawakaribisha Watanznia wote kujiunga na UKAWA kupitia chama chochote. Na zoezi hili ni lazima lifuate taratibu zetu ndani ya vyama,” amesisitiza Lipumba. Chanzo:mwanahalis online

Haki za binaadamu:Obama aionya Ethiopia

Rais Obama katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia amelionya taifa hilo kwamba linahitaji kuimarisha haki zake za kibinaadamu pamoja na uongozi bora. Akizungumza katika mkutano na wanahabari ,Barrack Obama amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kufana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na kwamba taifa hilo litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika. Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia. Vilevile Obama aliunga mkono maendeleo yalioafikiwa na Ethiopia kiuchumi pamoja na usalama wa kieneo. Chanzo:BBC Swahili

Siri nzito Ukawa, vikao vyaendelea mfululizo

Licha ya Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) kupokea taarifa ya Ukawa na kuamua chama hicho kiendelee kushiriki katika umoja huo, bado suala la mgombea urais wa vyama vinavyounda umoja huo limeendelea kuwa siri nzito. Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya CUF jana, zilisema kuwa katika kikao chake kilichoketi juzi na jana mjini Zanzibar, baraza hilo lilipokea taarifa ya Ukawa, kuithibitisha na kuamua chama hicho kiendelee na ushirikiano huo. Mkutano wa waandishi wafutwa Pamoja na hayo, jana kutwa nzima viongozi wa Ukawa walikuwa kwenye vikao mfululizo na hakukuwa na taarifa rasmi zilizopatikana na hata mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa jana jioni uliahirishwa bila kueleza utaitishwa tena lini. Ingawa taarifa ya mkutano wa Ukawa na wanahabari haikutaja ajenda, habari zilizoenea katika mitandao ya kijamii zilibainisha kuwa walikuwa wanakusudia ama kutangaza chama kilichopitishwa na Ukawa kusimamisha mgombea urais au kutangaza jina la mgombea mwenyewe pamoja na mgombea mwenza. Vyanzo mbalimbali ndani ya Ukawa, vilieleza kuwa ufunguo wa hatua hiyo ulikuwa unashikiliwa na CUF, ambayo hivi karibuni ilijitenga na umoja huo ili masuala yake yajadiliwe kwanza na vikao vyake vya maamuzi kabla ya kurejea kwenye meza ya majadiliano. Taarifa za uhakika kutoka katika kikao hicho kilichoketi Zanzibar kwa siku mbili, zilibainisha kuwa wajumbe waliafikiana kinyume na ilivyotarajiwa kuwa wangevurugana. Miongoni mwa mambo ambayo inadaiwa wameafikiana ni kuwa mgombea urais atoke Chadema na chama hicho kitoe mgombea mwenza. Jussa: Watanzania mtafurahi Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa baraza hilo, Jussa Ismail Ladhu alipoulizwa alisema ikiwa itaamuliwa mgombea mwenza wa Ukawa atoke CUF, hakutakuwa na shida kwa kuwa chama hicho kina wanasiasa wazuri, safi na makini na kwamba kitatoa mtu ambaye Watanzania wote watafurahi. “Ikiamuliwa kuwa mgombea mwenza atoke CUF, wananchi msiwe na wasiwasi, CUF ina hazina nyingi, itatoa mtu bora, itawapa chaguo ambalo Watanzania wote wataridhika nalo,” alisema Jussa. Pamoja na kuthibitisha kuwa Baraza hilo limeamua CUF iendelee kushiriki katika umoja huo, Jussa alisema kwenye mjadala matatizo kidogo yalikuwapo katika mgawanyo wa majimbo. Hata hivyo alisema baada ya kuweka vigezo vya kuwa na mgombea wa Ukawa, sasa hakuna shida kwa kuwa majimbo machache yaliyosalia utaratibu wake utatangazwa hivi karibuni. Kuhusu mgombea mwenza, Jussa alisema CUF ina nafasi kubwa ya kutoa mgombea huyo kwa sababu ndicho chama chenye nguvu Zanzibar na kina wanasiasa mahiri na makini. Wagombea wetu tunataka wawe ni wale watakaohakikisha kuwa Katiba Mpya inapatikana mara baada ya uchaguzi ili kuyaweka sawa mambo yanayohitaji kuwekwa sawa. Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba, mgombea urais na mgombea mwenza wanapaswa kutoka chama kimoja, hivyo kama Chadema itamtoa mgombea urais inabidi pia mgombea mwenza atoke chama hicho. Habari ambazo bado si rasmi zinasema kuwa mmoja wa viongozi wa CUF anaweza kuhamia Chadema ili kukidhi matakwa hayo ya Katiba. Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani alisema kuwa mambo katika Ukawa ni mazuri, wapo waliofikiri kuwa watavurugana, lakini wamekubaliana na sasa Watanzania wasubiri kupata wagombea safi katika ngazi zote. Bimani alisema CUF kitaendelea kushirikiana na vyama vingine vya upinzani nchini ili kuhakikisha demokrasia inazidi kukua. Vikao mfululizo Chadema Habari zaidi zilizolifikia gazeti hili zilisema mshirika mwingine wa Ukawa, Chadema jana viongozi wake walikuwa katika kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichoshirikisha wajumbe wachache, hasa wale wanaopatikana kwa kupigiwa kura ili kuweka mambo sawa. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene alikiri kuwapo kwa kikao hicho. “Kamati Kuu ya Chadema inaendelea kukutana jijini Dar es Salaam kwa kikao maalumu cha dharura kujadili mambo mbalimbali,” alisema Makene katika taarifa yake fupi aliyotuma jana usiku. “Mambo hayo ni pamoja na maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi mkuu, kupokea taarifa za mwenendo wa kura za maoni na uteuzi wa awali wa nafasi za ubunge wa majimbo na viti maalumu zinazoendelea nchini nzima,” alisema Makene. Habari za ndani ya kikao hicho kilichofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam, zilisema kuwa kilikuwa na jukumu la kupokea taarifa ya utafiti iliyofanywa nchini kote kuhusu mgombea anayekubalika zaidi. Ingawa hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu utafiti huo, lakini taarifa zinazoendelea kusambaa zinalitaja jina la waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa yuko mbioni kuhama chama chake cha CCM na kwenda Chadema, huku mgombea mwenza akitajwa kuwa atatoka upande wa Zanzibar CUF. Mgombea mwenza kuhamia Chadema Habari za ndani ya Ukawa zinasema chini ya makubaliano ya Ukawa ikiwa mgombea urais atatoka Chadema, mgombea mwenza akitoka chama kingine itabidi ahame chama chake ili aingie chama alicho mgombea urais ili kukidhi matakwa ya kikatiba. “Tutakaposhinda uchaguzi, kama makamu wa rais atatoka CUF itabidi kila akitoka katika ofisi ya makamu wa rais, kituo cha kwanza atasimama Makao Makuu ya CUF kwa ajili ya kupeleka taarifa na kupata baraka za chama katika masuala muhimu.” Chanzo chetu cha habari kinasema: “Ikiwa Ukawa tutashinda Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 na kupata nafasi ya urais, jambo la kwanza litakuwa ni kufanya Mabadiliko ya Katiba na kuruhusu demokrasia pana ya watu kuungana.” Alisema hakuna ajabu yoyote kwa rais kutoka chama kimoja na makamu wa rais kutoka chama kingine. “Hilo hata sasa linatendeka Zanzibar ambako Rais na Makamu wa Kwanza wa Rais wanatoka vyama tofauti na hakuna matatizo yoyote katika utendaji wa Serikali, kila mmoja anasimamia kwanza maslahi ya Taifa pili kuhakikisha sera za chama chake zinatekelezwa,” kilieleza chanzo cha habari. Lowassa atajwa Hii ndiyo ajenda ambayo imetawala mijadala kuhusu fununu za Lowassa kuhama CCM kwenda Chadema ili kukamilisha safari yake ya matumaini. Gazeti hili linafahamu kuwa mazungumzo na Lowassa yamekwishafikia hatua nzuri ingawa kulikuwa na viongozi wachache ndani ya Chadema waliokuwa wameshikilia msimamo wa kumkataa lakini kutokana na presha iliyopo ndani na nje ya chama wasingefua dafu. Mtei amkaribisha Huku mjadala kuhusu Lowassa ukizidi kukolea, mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemkaribisha mwanasiasa huyo na makada wengine wa CCM kujiunga na chama hicho kikuu cha upinzani. Akizungumza na Mwananchi jana, Mtei alisema kwa sasa Chadema na Ukawa wanahitaji kura za kutosha kuing’oa CCM, hivyo hata kura ya mtu mmoja ni muhimu. “Nimesikia Lowassa anatajwa kutaka kujiunga na Chadema, mimi namkaribisha aje, si yeye tu, aje na makada wengine wa CCM kwa kuwa tunapaswa kuimarisha nguvu za kuiondoa CCM madarakani,” alisema. Alisema Chadema ni chama cha Watanzania wote hivyo hakiwezi kumfungia milango Mtanzania mwenye sifa za kujiunga na chama hicho asijiunge. Hata hivyo, Mtei alisema makada hao wa CCM ambao wanataka kujiunga na Chadema endapo watakuwa na nia ya kupata uongozi, wajue kuna vikao vya kuwapitisha. “Tunawakaribisha Chadema makada wote wa CCM bila masharti na kama wana nia ya uongozi Chadema ina vikao vya kupitia kulingana na sifa zao na vikao vitakuwa na maamuzi ya mwisho,” alisema. Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao, alisema ana uhakika muungano wa upinzani ndio silaha kubwa ya kuing’oa CCM madarakani. “Uchaguzi uliopita Chadema tulishinda lakini tulichakachukuliwa lakini safari hii kupitia Ukawa tumejipanga kuhakikisha upinzani tunashinda kwa kiasi kikubwa,” alisema. Alisema hadi sasa Chadema na ukawa kwa ujumla wake kuna viongozi wenye sifa ya kushinda urais na wanakubalika nchi nzima. Chanzo:mwananchi.co.tz

Rais Obama afika nchini Ethiopia

Rais Obama akishuka kutoka ndani ya ndege ya Rais Rais Barack Obama wa Marekani hatimaye amefika nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya nchi za Afrika. Ni mara yake ya kwanza tangu aongoze taifa la Marekani akiwa raisi kuhutubia wanachama hamsini na mbili wa umoja wa Afrika katika makao makuu yake yaliyoko Addis ababa.Mazungumzo yao yakiwa yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita za wenyewe kwa wenyewe sudan ya kusini. Raisi Obama,aliwasili nchini Ethiopia akiwa anatokea mjini Nairobi ambako aliwaambia wakenya kuwa amna kikomo cha kile wanachokihitaji na kusisitiza kwa kutoa angalizo katika athari za ukabila na rushwa. Tamaduni mbaya kama unyanyasaji wa kijinsia,ndoa za kulazimishwa ,tohara kwa watoto wa kike na kutopeleka watoto shuleni. Chanzo:BBC Swahili

Bobbi Kristina mwanawe Whitney afariki

Bobbi Kristina afariki Dunia Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo. Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake. Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''. Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado.Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitliza kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufa. Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B. Chanzo:BBC Swahili

Sunday, July 26, 2015

Mlipuko mkubwa wawaua watu 10 Somalia

Takriban watu 10 wameuawa kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea katika hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Mwandishi wa BBC katika mji huo anasema kuwa lori moja lilitumiwa kushambulia hoteli ya Jazeera karibu na uwanja wa ndege wa taifa hilo. Wajumbe wa kimataifa wamekuwa wakiishi katika hoteli hiyo ambayo imelengwa katika siku za nyuma. Ripota wetu anasema kuwa ni moja ya mashambulizi mabaya kuwahi kushuhudiwa mjini Mogadishu. Anasema kuwa magari ya ambulansi yameanza kuokota miili. Chanzo:BBC Swahili

Obama awazima wengi kwa kukutana na Ruto

Obama awazima wengi kwa kukutana na Ruto Takriban saa ishirini hivi tangu rais wa Marekani Barack Obama awasili nchini Kenya swala ibuka limekuwa, Je atakutana na naibu rais wa Kenya bwana William Ruto au la ? Naibu rais Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007. Kesi dhidi yake inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC huko Hague Uholanzi. Wadadisi wa maswala ya kidiplomasia walikuwa wamebashiri kuwa rais Obama asingelikutana naye na ima atafanya hivyo itakuwa mkutano wa kisiri wala hakutakuwa picha yoyote kwani Ruto angali anatazamwa kama mshukiwa wa makosa jinai. Wakati huohuo , Bwana Ruto amenukuliwa mara kadhaa akikashifu hadharani swala la mapenzi ya jinsia moja. Yamkini majuma kadhaa yaliyopita, Ruto, alitangaza wazi kuwa, atapinga shinikizo za aina yoyote kutoka kwa serikali ya Rais Obama ya kutaka Kenya ihalalishe na kuwatambua watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja. Kulikuwa na dhana kuwa msimamo huo ungemfanya kutofautiana na rais Obama lakini hilo sasa limezikwa katika kaburi la sahau. Na alipowasili katika ikulu ya Nairobi alipokewa kwa taadhima kuu ya amiri mkuu wa jeshi na kupigiwa mizinga 21 ya heshima. Hata hivyo hii leo Naibu Rais wa Kenya, William Ruto ameamkuana na Rais Barrack Obama katika ikulu ya rais nchini Kenya. Ingawa ni salamu tu, kati ya Obama na Ruto, tendo hilo limekuwa na umuhimu mkubwa nchini Kenya na kuashiria uhusiano ulioko kati ya Kenya na Marekani. Awali kulikuwa na tetesi kuwa wawili hao hawangekutana kutokana na kesi inayomkabili Ruto katika mahakama ya uhalifu ya ICC. Ruto hakuwa katika wageni waliompokea Rais Obama alipotua nchini Kenya na tukio hilo lilichangia uvumi kuwa Ruto hangekutana na rais Obama. Baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya viliripoti kuwa Ruto hangeruhusiwa kukutana na Obama kwani ni mshukiwa kwa kuhusika katika vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini ambapo watu elfu moja waliuwawa na maelfu kuachwa bila makao. Hata hivyo Rais Uhuru Kenyatta alieleza awali kuwa Obama atakutana na Serikali ya Kenya na Ruto ni mmoja wa viongozi wakuu katika serikali hiyo. Kauli hiyo ilitiliwa mkazo na waziri wa nchi za nje, Amina Mohammed kwenye mahojiano ya kipekee na BBC aliposema kuwa hakuna sababu zitakazomzuia Ruto kukutana na Rais Obama. Aidha, Ruto amekuwa katika mstari wa mbele kupinga ndoa kati ya watu wa jinsia moja na kueleza kuwa Kenya haitahalalisha ndoa za aina hizo. Chanzo:BBC Swahili

Wiki ya mtikisiko

Ni wiki ya mtikisiko. Hivi ndiyo unavyoweza kuelezea hali itakavyokuwa nchini kutokana na matukio makubwa ya kisiasa yanayotazamiwa kutokea ndani ya wiki inayoanza leo ambayo yanaweza kubadili mwelekeo wa siasa za Tanzania. Hali hiyo inatokana na vuguvugu la kisiasa linalohusisha viongozi wenye ushawishi kuhama vyama vyao vya siasa na kutimkia kwenye vyama vingine, ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu. Ni wiki ambayo itapambwa na matokeo ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF kilichofanyika jana mjini Zanzibar kuhusu mustakabali wake ndani ya Ukawa, ikizingatiwa kuwa hivi karibuni chama hicho kiliamua kujiweka kando ya vikao vya umoja huo hadi vikao vya juu viamue. Hata hivyo, habari ambazo gazeti hili limezipata zinasema kuwa uwezekano wa chama hicho kujitoa ndani ya Ukawa ulikuwa mdogo kutokana na kuogopa hasira za wananchi wenye matumaini na umoja huo. Aidha, kulikuwa na taarifa kuwa kikao cha jana kilikuwa kinaangalia jinsi watakavyoshiriki katika umoja huo na kwamba kulikuwa na matumaini makubwa. Vile vile, hii ni wiki ambayo kura za maoni zinazoendelea katika vyama vikubwa vya siasa, kuonyesha baadhi ya vigogo wakiangushwa na kujaribu kutafuta upenyo wa madaraka katika vyama vingine. Pia, ni wiki ambayo chama kikuu cha upinzani, Chadema kimeamua kusogeza mbele tarehe za kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais kutoka jana hadi Ijumaa, katika kile kinachotazamwa kama kusubiri mchakato wa kumpata mgombea urais. Kana kwamba hiyo haitoshi, hii ni wiki ambayo minong’ono ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye jina lake limekatwa katika orodha ya wasaka urais wa CCM anaweza kuhamia Chadema. Tayari baadhi ya viashiria vya hali hiyo vimeanza kuonekana ambapo wiki iliyopita wabunge wawili wa chama tawala cha CCM, James Lembeli na Ester Bulaya waliachana na chama hicho na kujiunga na Chadema huku chama hicho cha upinzani kikitamba kujiandaa kuwapokea vigogo wengine zaidi. Kiashiria kingine cha mtikisiko ni hatua ya madiwani 18 wa CCM wilayani Monduli na wengine 10 wa UDP na CCM Bariadi kuhamia Chadema. Lakini pia wapo wabunge na madiwani wanaohama Chadema kwenda chama cha ACT-Wazalendo. Vuguvugu hilo la kisiasa limekolezwa na kauli za wanasiasa wawili vijana kwa nyakati tofauti, Godbless Lema na Zitto Kabwe kuwa wiki hii itakuwa ya mshikemshike kutokana na mambo yaliyopangwa kufanyika. Zitto: Ni wiki ya mabadiliko Akiandika kwenye kurasa zake za Facebook na Twitter jana, Zitto alisema, “Wiki ya kuanzia Jumatatu tarehe 27 Julai 2015 itashuhudia mabadiliko makubwa sana kwenye siasa za Tanzania. Kuimarika kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni jambo jema kwa nchi yetu.” Alipotakiwa kufafanua kauli yake, Zitto hakutaka kutaja matukio husika, lakini alisisitiza kuwa mtikisiko wa kisiasa utatokea na mazingira ya hali hiyo yataanza kubadilika kuanza kesho. “Na huu ujumbe nilioandika hauna uhusiano na chama cha ACT-Wazalendo,” alisema. Alipotakiwa kufafanua zaidi, alisema “Watanzania wasubiri mabadiliko ya siasa za Tanzania.” Lema asema ni mtikisiko Kwa upande wake Lema, akiwa jimboni kwake Arusha, alisema wiki hii itakuwa ya mtikisiko kwa CCM kwa sababu zaidi ya viongozi wake 950 kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na taifa watahamia Chadema. Akizungumza wakati wa kuwapokea vigogo watatu na wanachama 30 kutoka CCM jana, Lema alisema kuanzia kesho kimbunga cha viongozi na wana CCM kuhamia Chadema kitavuma kila kona ya nchi. Vigogo hao ni Diwani wa Kata ya Moshono, Paul Matthysen na mwenyekiti wa CCM Kata ya Terat, Simon Mollel wote wa jijini Arusha. Haya yametokea ikiwa ni siku chache baada ya katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Longido, Tostau Mollel kahamia Chadema, huku baadhi ya watiania wa udiwani na ubunge waliokamilisha maandalizi wakikacha kuchukua fomu za chama hicho. Miongoni mwa waliokacha kuchukua fomu bila kutoa sababu ni mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye, mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Robinson Meitinyiku, mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, Mathias Manga na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole, wote wakitajwa kuwa kwenye timu ya Lowassa. “Hii iliyoanzia Bariadi, Monduli, Longido na Arusha mjini ni mvua za rasharasha. Masika yataanza wiki ijayo (kuanzia kesho Jumatatu) kwa zaidi ya viongozi 950 wa ngazi mbalimbali watakapohama CCM na kujiunga Chadema,” alisema Lema. Alifananisha Chadema na kanisa au msikiti akisema milango yake iko wazi kuwapokea wanachama wa vyama vingine wanaotaka kutumikia umma kujiunga nacho kwa kutubu makosa yao na kusamehewa kabla ya kuingia kazini Oktoba 25, mwaka huu. Wabunge wanne Chadema watua ACT Wakati upepo ukivuma kutoka CCM kwenda Chadema, hali kama hiyo imekinufaisha chama kipya cha ACT-Wazalendo baada ya kuvuna wabunge watatu wa viti maalumu na diwani mmoja kwa mpigo kutoka Chadema. Wabunge hao ni Mhonga Ruhwanya (Kigoma), Chiku Abwao (Iringa ) na AnnaMaryStella Mallac (Mpanda) wote kutoka Chadema, huku mwingine ambaye jina lake tunalihifadhi kwa kuwa hatukumpata, akitimkia CCM. Wabunge hao wanaungana na Mbunge wa Kasulu mjini, (NCCR – Mageuzi ) Moses Machali aliyehama kutoka NCCR-Mageuzi kwenda ACT Wazalendo, hivi karibuni. Akizungumza na gazeti hili jana, Zitto alisema atawatangaza wakati wowote wabunge wengine sita kutoka CCM, Chadema na CUF. Kauli ya Chiku Abwao Akizungumza kwa simu akiwa India, Abwao alikiri kuhamia ACT-Wazalendo akidai kutoridhisha na mwenendo wa Chadema na hasa taarifa anazosikia za Lowassa ambaye amekuwa akituhumiwa mambo mbalimbali kuhusishwa na Chadema. “Mimi kwa historia yangu kitu kilichonipeleka upinzani ni kutafuta haki uwajibikaji na kupinga vitendo vya ufisadi na rushwa, lakini nimekishangaa chama changu katika suala hili,” alisema. “ Licha ya mambo ya sintofahamu yanayoendelea Chadema lakini hili la Lowassa kama kweli atajiunga na chama hiki basi suala litakuwa ni moja tu, ni chaneli ya kuingia Ikulu, lakini haya mambo mimi siyapendi kwa sababu ni mtu wa kupinga ufisadi na kupigania haki za wanyonge,” alisema Abwao Alisema ameamua kuhamia ACT-Wazalendo, kwa sababu ni chama pekee kitakachowakomboa Watanzania na kwamba ataenda moja kwa moja kugombea jimbo la Iringa Mjini badala ya Isimani. “Niliamua kwenda Isimani kipindi kile ili kuijenga Chadema, lakini safari hii nipo huku ACT-Wazalendo nitaenda kupambana na Mchungaji (Peter) Msigwa na yeyote yule atakayepitishwa na CCM,” alisema Abwao. Mhonga: Ni uamuzi tu Mhonga Rhuwanya alipouliwa alijibu kwa kifupi, “Kama ulivyosikia ndiyo hivyo hivyo, mimi ni mtu mzima na nina maamuzi yangu kwani chama siyo dini.” Alipoulizwa atagombea ubunge kupitia ACT-Wazalendo, alijibu, “Kwani mtu akihamia chama kingine ni lazima agombea ubunge… hata hivyo naweza kugombea tena.” Mallac aenda kupokewa Kwa upande wake, Mallac alisema alikuwa safarini kwenda Katavi kupokewa ACT-Wazalendo. “Niko njiani naelekea Katavi mkoani kwangu kupokewa rasmi na kiongozi wangu wa chama cha ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe,” uliosomeka ujumbe mfupi wa maneno. Zitto awapokea Zitto alisema huo ni mwendelezo wa chama hicho kuwapokea wabunge kutoka katika vyama mbalimbali na hivi karibuni atawapokea wengine katika mikoa ya Kagera, Tabora, Rukwa na Zanzibar. “Tabora wako wawili na Kagera mbunge mmoja wote wa CCM, kutoka wilaya ya Karagwe, pia Zanzibar wawili kutoka CUF na Chadema. Hawa wote wanasubiri mchakato wa kura za maoni umalizike ndipo tuwatangaze. “Hawa wabunge tuliowapokea ni sawa na asilimia 10 kati ya 50 niliosema, maana watu walikuwa wananiuliza, ‘Zitto ulisema utawapokea wa kiasi kadhaa mbona kimyaa?’ mambo ndiyo yameanza sasa.” Diwani Chadema atua ACT Katika hatua nyingine, aliyekuwa diwani wa Kata ya Segerea (Chadema), Azuri Mwambagi amejiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ya uhusiano mbaya kati yake na viongozi wa Chadema wa jimbo hilo. Mwambagi alisema kuwa amekuwa diwani wa kata hiyo kwa miaka mitano lakini hakukuwa na ushirikiano mzuri kati yake na uongozi wa jimbo hilo. “Kila ninachokifanya wenzangu wanasema sijafanya kitu na wanaamua kunizunguka kwa wananchi, hali hii imenichosha,” alisema Mwambagi. Katibu wa jimbo hilo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Anna alisema hata yeye amezisikia taarifa za diwani huyo kuhamia ACT- Wazalendo, lakini akakana kuwapo mizengwe aliyofanyiwa Mwambagi. “Tupo katika mchakato wa kura za maoni na yeye ameomba kuteuliwa kugombea udiwani Kata mpya ya Liwiti, kama anahisi alikuwa kiongozi bora enzi za utawala wake kwa nini asisubiri matokeo ya kura za maoni ndipo afanye uamuzi huo?” alihoji Anna. Chanzo:mwananchi.co.tz

Saturday, July 25, 2015

Waziri wa Fedha ajitosa ubunge Zanzibar

WAZIRI wa Fedha katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Saada Salum Mkuya, kwa mara ya kwanza ameingia katika kinyang’anyiro cha kusaka ubunge kwa uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Saada, mwanamama aliyesomea masuala ya uongozi wa fedha kufikia kiwango cha shahada, amejijengea jina kubwa kiutendaji kwa kuhimili vishindo vya kushika wadhifa huo ndani ya shutuma kali za ufisadi kugubika serikali ya CCM. Alirudisha fomu ya kugombea kiti cha Welezo, nje kidogo ya mjini Zanzibar. Welezo ni jimbo jipya la uchaguzi lililoundwa katika ugawaji mpya wa majimbo uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) mwanzoni mwa mwezi huu. Taarifa za ndani ya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, mjini hapa, zinasema kwamba Saada amepata washindani wawili ambao wenyewe viongozi wa chama hicho wanawaita kama “washindani wepesi mno.” Washindani wake watakaoshiriki kura ya maoni Agosti mosi, ni Abbas Hassan Juma na Zahor Salum Mohamed. Juma ni mdogo wa mwakilishi wa Kwamtipura, Hamza Hassan Juma aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya Amani Abeid Karume. Saada anatafuta ubunge ikiwa ni mara yake ya kwanza. Aliitwa kwenye siasa alipoteuliwa mbunge mwishoni mwa mwaka 2013 na moja kwa moja akateuliwa naibu waziri wa fedha akiwa chini ya Dk. William Mgimwa aliyekuwa mbunge wa Kalenga. Saada alipandishwa kuwa waziri kamili mapema mwaka 2014 baada ya Dk. Mgimwa kufariki dunia katika mazingira ya kutatanisha akiwa matibabuni nchini Afrika Kusini. Uongozi wake kama waziri umeshuhudiwa ukimpandisha chati kisiasa kwa kuwa jasiri na mahiri katika kujenga hoja za maelezo ya masuala ya mipango na utekelezaji wa bajeti ya serikali. Amefanikiwa kupitishiwa bajeti ya serikali pamoja na miswada ya inayohusu sheria mpya za kodi. Hata hivyo, jimbo analoomba kugombea, huenda likawa na mgogoro kwa vile ni moja ya majimbo manne yaliyoongezwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haijayaidhinisha kutokana na kutopata muda wa kuyachunguza kama vigezo vimetimizwa. Chanzo:mwanahalisionline.com

Chadema yaja na mbinu mpya kudhibiti mamluki

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimebuni mbinu mpya ya kudhibiti mamluki wanaochukua fomu za kugombea kupitia chama hicho kisha kutokomea nazo mitini. Sasa watakaopitishwa na kupewa fomu za chama hicho kugombea ubunge au udiwani, watatakiwa kusaini fomu maalumu mbele ya mahakama ili wakitokomea bila kurejesha fomu Tume ya Uchaguzi (NEC), wapandishwe mahakamani. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Magomeni, Jijini Mwanza. “Mwaka huu hakuna kupita bila kupingwa, wagombea wetu wote tutawasainisha mahakamani na wakishindwa kurudisha fomu, tutawashughulikia mahakamani,” amesema Dk. Slaa na kuongeza; “Waliochukua fomu hatutaki kesho mmoja amejitoa, kama unataka kujitoa ondoka leo, ruksa.” Mkutano huo umehudhuriwa na wabunge na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Makamu Mwenyekiti Bara, Prof. Abdallah Safari; Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee. Katika mkutano huo, wanachama wapya kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitambulishwa, wanachama hao ni James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Kahama Mjini na Ester Bulaya ambaye alikuwa Mbunge Viti Maalum kutoka Mkoa wa Mara. Kwenye mkutano huo Dk. Slaa amesema, sasa hivi Chadema ipo sehemu yote ya nchi hivyo hakuna mahali ambapo chama hicho kitashindwa kusimamisha mgombea na kwamba, Ijumaa wiki hii watamaliza uteuzi kwenye majimbo yote Tanzania. “Leo tumeingia kila kona ya nchi, uchaguzi uliofanyika wiki hii ni wa Tanzania nzima, hakuna mahali ambapo Chadema haipo tena, hatuzungumzi kabila, hatuzungumzi Magufuli ni mkabila, sehemu zote tunazungumza Utanzania,” anasema Dk. Slaa. Akizungumzia mahudhurio ya wananchi kwenye mkutano huo Dk. Slaa amesema, miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo hakuna aliyelipwa fedha wala kubebwa na magari kutolewa kule alikokuwa. “Hakuna aliyebebwa, hakuna aliyelipwa pesa, mmekuja hapa kwa miguu yenu tangu asububi, asanteni sana na Mungu awabariki,” amesema Dk. Slaa. Hata hivyo amesema, ukiumwa na nyoka hata utapoguswa na jani utalikimbia. Aliwafikirisha wananchi kwa kujiuliza, katika miaka 10 iliyopita, Watanzania walikuwa wanakunywa chai huku sukari ikiuzwa Sh. 500, je leo nani anaweza kunywa chai kwa sukari bei hiyo? Pia aliwakumbusha kuwa, miaka 10 iliyopita ikiwemo wafugaji waliweza kula nyama, leo bado wanaweza kula kula kilo ya nyama? Dk. Slaa amesema, mwaka 2005 wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa mgombea urais kupitia CCM, aliwaahidi Watanzania Maisha Bora kwa Kila Mtanzania lakini sasa maisha yamekuwa magumu kwa kila Mtanzania. Hata hivyo amesemea, mgomea wa CCM ni mzaliwa wa ukoo ule ule na kabila la CCM hivyo kuna kila sababu ya kuwaonda. Pia amesema, “tumekuja leo ili tuwaeleze kwamba Chadema tupo makini, kazi za chama hazisimami, tupo kwenye utekelezaji wa kazi za chama. Hata hivyo, amewaahidi wananchi kuwa, wakati utakapofika “tutadondosha nondo zetu.” Dk. Slaa amewahahakikishia wananchi kuwa, chama hicho hakiwezi kumeguka wala kusambaratika licha ya kuwepo kwa taarifa kwamba, yeye na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho hawasalimiani, Kwa kujiamini kiongozi huyo amesema, wamejihakikishai kushika dola, “haya sio maneno wala utani.” Msukumo mkubwa wa maisha Dk. Slaa amesema unatokana na mabadiliko ya uchumi ulio mbovu kwa miaka zaidi ya 50 baadaya Uhuru uliopatikana mwaka 1961. Amefafanua kuwa, wakati wa Rais wa Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, uamuzi ulianza matawini kwenda juu lakini sasa CCM imebadilisha na kuwa uamuzi wa kundi la watu wachache dhidi ya wananchi walio wengi. “La kwanza tunalolisimamia ni nchi irudi kwa wananchi, ukifanya hivyo yote yanaondoka; ufusadi, wizi rasilimali vyote vitakoma. “Mkikabidhi nchi kwa wachache hiki ndicho kinatokea, mwaka 2015 ndio mwisho. Katiba inasema serikali itapata madaraka yake kutoka kwa wananchi, CCM imepoka,” amesema. Akizungumzia ukombozi Dk. Slaa amesema, nchi inahitaji ukombozi na wananchi wapo tayari katika ukombozi na kuwa, Polisi, Wanajeshi na wengine ni watiifu na ndio maana wanawapenda na wanaungana nao katika safari ya ukombozi ambapo vyombo hivyo vitaendelea kuwepo, hofu kuwa upinzani unaleta vurugu haipo tena. Katika mkutano huo, Mbowe amewatoa hofu wananchi kwamba, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) uko imara, hadi atakapopatikana rais. Aidha, Mbowe alianza hotuba yake fupi baada ya kuwakabidhi kadi za uanachana Bulaya na Lembeli. “Hamtakiwi kuendelea kusikiliza maneno ya uzushi ambayo yanasemwa UKAWA umevunjika au kusambaratika, hayo sio kweli na kuhakikishieni hilo, hadi leo asubuhi nimewasiliana na viongozi wezetu wa UKAWA.” Amesisitiza kuwa, wananchi hawatakiwi kusikiliza maneno ya nje bali wawasikilize viongozi wao, kwani umoja wao bado unalengo lile lile la kuiondoa CCM madaraka. Amesema, UKAWA bado wanaendelea na mazungumzo ya amani na kwamba, bado wanamalizia mambao madogo ili wote waende sawa na kutoka na mgombea mmoja “Agosti 4 mwaka huu tutatoa taarifa ya nani rais.” Hata hivyo amesema, jambo la kwanza ambalo UKAWA italishughulikia ni kurudisha viwanja vyote ambavyo ni mali ya wananchi na sasa vipo chini ya CCM. Lakini pia amepiga marufuku mausula ya ukabila na kushangazwa katika Karne hii ya 21 kuwepo wapo kwa watu wanaozungumzia ukabila. Akizungumzia ukabila, alijaribu kuiga sauti ya Mwl. Nyerere ambaye katika hotuba zake alizokuwa akizungumzia ubaya wa kuubeba ukabila katika nchi hii. Mwanahalisi Online

Kigaila aula Chadema Dodoma Mjini

Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Oganaizeisheni na Mafunzo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),imeibuka kidedea katika kura za maoni kuomba ridhaa kugombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini. Kigaila amewabwaga kwa mbali wapinzani wake wanne ambao nao waliomba ridhaa ya kuchaguliwa katika kura za maoni ili kuweza kupeperusha bendera ya Chadema katika kusaka ubunge katika jimbo hilo. Pamoja na ushindi wa Kigaila, kada wa chama hicho, Josephine Kihoza ambaye alitangaza nia ya kuomba ridhaa ya kupitishwa katika kura za maoni ili awanie jimbo hilo naye alichomoza kwa kuwa mshindi wa pili huku akiwabwaga wenzake kwa mbali zaidi. Katika kura za maoni Kigaila alipata kura 168 huku mpinzania wake Joseph Kihoza akiwa na kura 25 na aliyefuatia alikuwa na kura 4 na wengine waliwa wakifungana kuwa na kura tatu tatu. Awali katika Mkutano mkuu maalum wa uchaguzi ulifanyika mjini hapa huku ukiwa chini ya usimamizi wa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi mzee, Eneck Mhembano ambaye aliwahi kupepeprusha bendera ya Chadema kwa kuwania nafasi ya ubunge mwaka 2010 na kuibuka mshindi wa pili wali aliwataka makamanda wa Chadema kuhakikisha wanashirikiana katika kufanya kazi za chama na kukijenga chama hicho. Amesema wakati yeye akigombea ubunge hapakuwa na wapinzania ndani ya chama kwa maana ya kupiga kura za maoni kama ilivyo sasa. “Mimi wakati nagombea hayakuwepo haya yote ya kura za maoni bali walikuja wakaniomba nigombee na wakanipa katiba ya Chadema nikaisoma vizuri na nikaielewa nikaingia ulingoni na nilipata kura nyingi nikawa waili dhidi ya mgombea wa CCM. “Lakini angalia kwa sasa chama kinakua hadi tunafanya kura za maoni ili kumpata mgombea mmoja sasa na sema ni lazima apatikane mmoja na hakuna mshindi hapa wa mshindi ni chadema wala siyo mtu.” Amesema Mbembano. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma Jella Mambo amesema kwa sasa chama kina kazi kubwa moja ya kuiondoa CCM madarakani kutokana na kushindwa kuwapatia maendeleo wananchi. Mbali na kushindwa kuwapatia wananchi maendeleo CCM imekuwa ilikumbatia wizi, ufisadi na masuala ya Rushwa huku watanzania wengi wakiendelea kuwa masikini. Kigaila wakati akitoa shukrani kwa wapiga kura alisema kazi kubwa ni kuhakikisha anaambana na ufisadi na manyanyaso ambayo wanafanyiwa wakazi wa Dodoma hususani katika masuala ya ardhi. Mwanahalisi Online

Rais Kikwete apewa Tuzo ya Utawala Bora

Rais Jakaya Kikwete ametunikiwa Tuzo ya Utawala Bora Afrika kwa mwaka 2015 kutokana na jitihada zake za kudumisha na kuimarisha utawala bora nchini. Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilieleza kuwa Rais Kikwete ametunikiwa tuzo hiyo na Taasisi ya African Archievers Awards yenye makao makuu nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete anaungana na Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini aliyekuwa wa kwanza kupewa tuzo hiyo mwaka 2011 kutokana na mchango wake wa kutetea haki za binadamu, usawa na amani. “Rais Kikwete ameteuliwa kutoka miongoni mwa watu 1,202 ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye jopo la kimataifa, linalojitegemea na lenye wajumbe kutoka Uingereza na Afrika Kusini kwa ajili ya uteuzi,” ilisema taarifa hiyo. Taarifa hiyo iliongeza kuwa, kutokana na tuzo hiyo, Rais Kikwete amealikwa kwenda kuipokea nchini Afrika Kusini kesho mjini Johannesburg. Hata hivyo, Rais Kikwete hataweza kwenda kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi, hivyo badala yake atakwenda Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro. Katika barua ya kumjulisha Rais Kikwete kuhusu uteuzi wake, Mtendaji wa African Achievers Awards, Rex Indaminabo alisema: “Uongozi wa African Achievers Awards unayo furaha kukujulisha juu ya uteuzi wako wa kupokea Tuzo katika kundi la Utawala Bora Afrika.” Mtendaji huyo aliongeza: “Ni kwa furaha na heshima kubwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri na Taasisi ya Uongozi na Menejimenti wanakupongeza kwa mafanikio haya.” Chanzo:mwananchi.co.tz

Fomu za urais Chadema kaa la moto

Wakati leo saa 10 jioni ndiyo muda wa mwisho uliopangwa kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais ndani ya Chadema, hadi sasa hakuna mwanachama hata mmoja aliyejitokeza kuzichukua. Badala yake zimetolewa kauli tofauti kuhusu kusuasua kwa mchakato wa kumpata mgombea urais hadi chama hicho kulazimika kusogeza mbele tarehe ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu. Hali hiyo inazidisha sintofahamu iliyougubika mchakato wa urais ndani ya chama hicho na ndani ya Ukawa, kuwa huenda kuna ‘mtu wa nne’ anayesubiriwa kutoka nje ya chama hicho, kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, wiki iliyopita. Likikariri chanzo cha kuaminika ndani ya Ukawa, gazeti liliandika kuwa huenda umoja huo na hasa Chadema, wanasubiri mgombea kutoka nje ya chama kwa kuwa hata baada ya wajumbe wa vikao vya mashauriano kukubaliana kuwa mgombea wa Ukawa awe Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, baadhi ya wajumbe kutoka katika chama hicho wanadaiwa kukataa kutangazwa kwake. Hata baadaye walipoulizwa nini msimamo wao kuhusu tetesi za mpango wa kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutoka CCM, viongozi na wabunge wa chama hicho walisema anakaribishwa mradi tu afuate kanuni na taratibu. Suala la mgombea urais wa Chadema na Ukawa limeendelea kuteka mjadala wa kisiasa nchini huku Watanzania wakisubiri kufahamu nani atateuliwa kupambana na yule wa CCM, Dk John Magufuli, hali inayosababisha baadhi ya watu kudai mchakato huo una mizengwe. Hata hivyo, Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa, Gaudence Mpangala alisema anadhani hakuna mizengwe inayowazuia baadhi ya wanachama wasiwanie nafasi hiyo kwa kuwa kanuni na taratibu za vyama ziko wazi. Alisema anachokiona ni kwamba wanachama hawajajipanga kuwania nafasi hiyo ya juu. Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Alexander Makulilo alisema wako watu ambao hawawezi kugombea nafasi ya urais kuwakilisha vyama vyao kwa sababu wanawaogopa viongozi wa juu wa vyama hivyo. “Jambo la msingi la kuangalia ni haki kutendeka katika kila mchakato katika uteuzi lakini watu wanawania nafasi kulingana na walivyojipanga,” alisema. Alisema wingi wa wagombea urais katika vyama si kigezo pekee cha kukua kwa demokrasia bali mchakato wa kuwapata wagombea hao ukiendeshwa kwa haki ndiyo demokrasia. Alisema kuwa hakuna ubaya hata kama kuna mgombea mmoja anayewania urais bali kinachotakiwa kuangaliwa ni ubora wa mchakato. Hakijaeleweka Katika mkutano wake uliofanyika mjini Mwanza Jumatano ambao ulipangwa kutumika kumtangaza mgombea urais wa chama hicho, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliwaomba Watanzania wavumilie wakati wanakamilisha taratibu za kumpata mgombea huyo. Pia, ilielezwa kuwa chama hicho kilikuwa kinasubiri mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF unaofanyika leo, huku taarifa nyingine zikisema chama hicho kilikuwa hakijampata mgombea mwenza kutoka Zanzibar. Wakati hayo yakiendelea, bado ratiba ya kuchukua fomu za urais na kurudisha ilikuwa inaonyesha ni leo na hakukuwa na dalili zinazoonyesha watu kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu, ambayo mara kadhaa viongozi wa chama hicho wametamka kuwa tayari wamempata mgombea anayefahamika ndani na nje ya nchi. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa aliliambia Mwananchi jana kuwa asingeweza kusema lolote kuhusiana na suala hilo kwa sababu alikuwa nje ya ofisi. “Wasiliana na watu walioko ofisini, wao wataweza kujibu vizuri swali lako,” alisema Dk Slaa. Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Dk Slaa aligombea urais na kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Gazeti hili lilipotaka kufahamu iwapo safari hii Dk Slaa amechukua fomu, alikataa kusema lolote akidai taarifa hizo zitapatikana kwa walioko ofisini. Wabadili ratiba Akizungumzia hali hiyo jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema kuna marekebisho yamefanyika katika tarehe hiyo ya mwisho kurejesha fomu ambayo yatatangazwa ndani ya simu mbili au tatu ambayo yalilenga kupisha mchakato wa kura za maoni. “Unajua viongozi wanatakiwa kusimamia kura za maoni majimboni, kwa hiyo tuliona kwanza tumalize hili, suala la mgombea urais lisubiri kwanza. Tunatarajia kutangaza tarehe mpya ya kurejesha fomu ndani ya siku mbili,” alisema Mwalimu na kuthibitisha kuwa hadi wanasimamisha shughuli hiyo hakukuwa na mwanachama yeyote aliyechukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais. Baadaye jioni jana, chama hicho kilitoa taarifa ya kusogeza mbele tarehe ya kurudisha fomu hadi Julai 31, 2015 saa 10 jioni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watiania wote watapaswa kurejesha fomu hizo katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, Dar es Salaam. Taarifa hiyo ilifafanua kuwa ratiba ya awali iliathiriwa na kitendo cha kusogeza mbele tarehe za uchukuaji na urejeshaji wa fomu za ubunge baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza majimbo mapya 26. “Hatua hiyo iliathiri ratiba ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi wa kugombea urais kupitia Chadema ambapo awali wanachama wenye sifa walipaswa kuanza kuchukua fomu 20-25 Julai, mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo. Mkutano Mbeya waahirishwa Katika hatua nyingine, ziara ya Dk Slaa aliyetarajiwa kuwasili na kuhutubia mkutano jijini Mbeya leo imefutwa hadi itakapotangazwa tena. Mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyasa (Chadema), Frank Mwaisumbe alisema sababu ya kufutwa ni viongozi wa kitaifa kuendelea na vikao vya ngazi ya juu jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa, Joseph China alisema ziara hiyo imefutwa kutokana na viongozi wakuu wa kitaifa kutingwa na vikao vya Ukawa. Viongozi wa kitaifa wa Chadema wakiwa Mwanza walitangaza kwamba wangefanya mikutano mingine, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam. Chanzo:mwananchi.co.tz

Obama leo kuhutubia wajasiriamali Kenya

Rais wa marekani Barack anatarajiwa kuhutubia kongamano la wajasiriamali akianza rasmi ziara yake katika eneo la afrika masharaki. Anatarajiwa kuzungumzia suala la ufisadi ambapo atataka kuwepo kwa jitihada kubwa za kupambana na ufisadi na pia kuwahutubia wafanyibiahara vijana nchini Kenya. Obama baadaye atatembelea eneo kulikotokea shambulizi la kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa marekani mjini Nairobi na pia kukutana na rais wa kenya uhuru kenyatta kwa mazungumzo ambapo wataangazia usalama wa kanda hiyo na tisho kutoka kwa kundi la kigaidi la Al shabaab. Marekani imekuwa ikiisadia kenya katika vita dhidi ya ugaidi na imewaua vongozi kadha wa kundi la al shabaab kwenye mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani. Chanzo:BBC Swahili

Marekani yakosoa ushindi wa Nkurunziza

Marekani yakosoa ushindi wa Nkurunziza Waziri wa masuala ya Nje wa Marekani John Kerry amekashifu matokeo ya uchaguzi ya Burundi yaliyotolewa hapo jana ambapo rais Pierre Nkurunziza alitangazwa kusajili ushindi mkubwa. Kerry ametaja uchaguzi huo kuwa ukiukaji mkubwa wa katiba na kejeli kwa mfumo wa haki huku akimlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa ghasia zilizotokea nchini humo wiki chache kabla ya kufanyika uchaguzi. Rais Nkurunziza alitangazwa mshindi na asilimia 70 ya kura Katika taarifa kwa vyombo vya habari saa chache zilizopita, waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amesema kuwa amesikitishwa kwa namna rais Nkurunziza ameiponda katiba ya nchi na kupuuza mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano iliyopita. Amesema kuwa rais huyo ametumia mbinu ghushi kung'ang'ania madarakani katika uchaguzi ambao sio huru wala wa haki. Kerry anasisitiza kuwa mazungumzo ya amani yafanyike Kerry amesisitiza kuwa ni lazima pande zote husika nchini humo zirudi katika majadiliano ya dhati na kuhusisha pia mashirika ya kijamii. Amesema kuwa hii ndio njia ya pekee ya kurejesha imani sio tu ya raia wa Burundi bali jamii ya kimataifa pia, na kuzuia ghasia zaidi nchini humo zilizosababisha watu kuikimbia nchi. Hapo jana tume huru ya uchaguzi nchini Burundi ilitangaza kuwa rais Nkurunziza amepata asilimia karibu sabini ya kura zilizopigwa katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne wiki hii. Kerry amesisitiza kuwa ni lazima pande zote husika nchini humo zirudi katika majadiliano Kura katika majimbo zinatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha wiki moja ijayo. Viongozi wakuu wa upande wa upinzani nchini Burundi walisusia uchaguzi huo,lakini majina yao yalisalia katika karatasi za kupigia kura. Kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa alimaliza katika nafasi ya pili akizoa asilimia kumi na tisa ya kura zilizopigwa. Chanzo:BBC Swahili

Obama returns to Kenya, reunites with father's family

NAIROBI, Kenya (AP) -- Fulfilling the hopes of millions of Kenyans, Barack Obama returned to his father's homeland Friday for the first time as U.S. president, a long sought visit by a country that considers him a local son. The president spent the evening reuniting with his Kenyan family, including his elderly step-grandmother who made the trip to the capital of Nairobi from her rural village. U.S. and Kenyan flags lined the main road from Nairobi's airport, and billboards heralding Obama's trip dotted the city. "I don't think that Kenyans think of Obama as African-American. They think of him as Kenyan-American," said EJ Hogendoorn, deputy program director for Africa at the International Crisis Group. Obama's link to Kenya is a father he barely knew, but whose influence can nonetheless be seen in his son's presidency. Obama has spoken candidly about growing up without his Kenyan-born father and feeling "the weight of that absence." A White House initiative to support young men of color who face similar circumstances has become a project dear to Obama, one he plans to continue after leaving the White House. In Africa, Obama has used his late father's struggle to overcome government corruption as a way to push leaders to strengthen democracies. He's expected to make good governance and democracy-building a centerpiece of his two days of meetings and speeches in Nairobi, as well as a stop next week in Ethiopia. "In my father's life, it was partly tribalism and patronage and nepotism in an independent Kenya that for a long stretch derailed his career," Obama said during a 2009 trip to Ghana, his first visit to Africa as president. "We know that this kind of corruption is still a daily fact of life for far too many." The president's father, Barack Obama, Sr., left Kenya as a young man to study at the University of Hawaii. There, he met Stanley Ann Dunham, a white woman from Kansas. They would soon marry and have a son, who was named after his father. The elder Obama left Hawaii when he son was just two years old, first to continue his studies at Harvard, then to return to Kenya. The future president and his father would see each other just once more, when the son was 10 years old. Obama's father died in a car crash in 1982, at age 46. "I didn't have a dad in the house," Obama said last year during a White House event for My Brother's Keeper, his initiative for young men. "I was angry about it, even though I didn't necessarily realize it at the time." Obama's first trip to Kenya nearly 30 years ago was a quest to fill in the gaps in the story of his father's life. In his memoir "Dreams From My Father," Obama wrote that at the time of his death, "my father remained a mystery to me, both more and less than a man." What Obama uncovered was a portrait of a talented, but troubled man. An economist for the Kenyan government, the senior Obama clashed with then-President Jomo Kenyatta over tribal divisions and allegations of corruption. He was ultimately fired by the president, sending him into a tailspin of financial problems and heavy drinking. The Kenyan leader Obama will meet with this weekend, Uhuru Kenyatta, is the son of the president his father confronted decades ago. Obama met most of his Kenyan family for the first time on that initial trip to his father's home country. As he stepped off Air Force One Friday, he was greeted by half-sister Auma Obama, pulling her into a warm embrace. The siblings then joined about three dozen family members at a restaurant at the president's hotel for a private dinner. Logistical constraints and security precautions prevented Obama from visiting Kogelo, the village where his father lived and is buried, on this trip. Sarah Obama, the step-grandmother he calls "Granny," still lives in the village. Despite the intense focus on the American leader's local roots, the White House has cast the trip as one focused on the relationship between the U.S. and Kenya, not the president and his family. Officials say Obama's agenda is heavily focused on trade and economic issues, as well as security and counterterrorism cooperation. The president is traveling with nearly two dozen U.S. lawmakers, along with 200 U.S. investors attending the Global Entrepreneurship Summit. Michelle Obama and daughters Malia and Sasha did not accompany the president. Auma Obama said she believed her late father would be proud to see his son return to Kenya as American president. "He'd be extremely proud and say, 'Well done,'" she said in an interview with CNN. "But then he'd add, 'But obviously, you're an Obama.'" Source:news.yahoo.com