Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, April 30, 2015

Roach :Mayweather hakutaka hili pambano.

Kocha wa bondia Manny Pacquiao ,Freddie Roach ana wasiwasi huenda bondia Floyd Mayweather asitokeea kwenye mpambano wa mei 2. Roach amesema “Sidhani kama mabondia wana hofu ila sidhani kama Mayweather alitaka kupigana alilazimishwa kupigana pambano hili na hakulitaka. "Sijui kwanini amekua mkimya sana kwenye mpambano huu maneno yake yana woga” Hata hivyo Mayweather hakushangazwa na kauli hizo za kocha huyo na kudai "nitakuepo niliongea uchafu siku za nyuma lakini hili pambano linajiuza lenyewe”. Pambano hili limeteka hisia kwa washabiki wa masubwi duniani kote huku homa ya mchezo ikiwa inapanda kila muda unavyozidi kukaribia pambano hilo hapo Mei 2.

Mayweather Vs Pacquiao:Nani bingwa?

Japo tayari ni tajiri ,Mayweather ambae jina lake la utani ni Money, inatarajiwa atapokea zaidi ya dolla millioni $150m na Pacquiao kama millioni $100m. Pacquiao yeye ametoka jamii ya kimaskini huko Ufilipino na kuna wakati katika maisha yake ya utotoni ambapo hata angelala njaa. Sasa wa kuangalia kwenye TV kando, wengi wa mashabiki wa huko Marekani wangependa kuona makonde yakirushwa 'LIVE' kwa hivyo wamekubali kutoa ada ya hadi $100 kwa kichwa kushuhudia wakiwa 'LIVE' nje ya ulingo. Wenye uchu wa kushuhudia pambano hilo 'LIVE' lakini hawajapata tiketi wako tayari kuzipata kwa walionanazo huku dau likiwa limepandishwa kwa kiwango atakacho muuzaji huyo mchuuzi. Wafilipino kumshangilia Pacquiao Wakati huo huo wito umetolewa kwa wakaazi wa kisiwa kimoja cha Philippines kwamba watumie kawi kwa kipimo kidogo ili kuihifadhi ndio waitumie kumwangalia katika runinga zao hapo Jumapili shujaa wao m-Filipino mwenzao , Manny Pacquiao (36) atakapokuwa akipambana na Mmarekani Floyd Mayweather (38) kwenye ulingo wa shindano la ndondi linalotajwa kuwa kubwa zaidi mnamo siku za hivi karibuni. Wakaazi hao wameshauriwa na kampuni ya umeme nchini humo Palawan kuzima vifaa vya matumizi mengine ya nyumbani kama friji, kutotumia mashine za kufua nguo, wala kutopiga pasi ili kuhifadhi kawi hiyo siku hiyo itumike tu kuwashia Runinga zao. Ushauri huo umetolewa kwani kisiwa hicho hukumbwa na upungufu wa umeme mara kwa mara, hivyo ni sharti wafuate maagizo hayo ili wasikose kushuhudia na kumshangilia kinara huyo wao ataeshiriki pambano hilo litakalo fanyika huko Las Vegas Jumamosi usiku saa za Marekani. Ndilo pambano lililovutia fedha zaidi kuwahi kutokea.

Akutwa hai kwenye kifusi, Nepal

Watoa huduma za uokoaji huko mji mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya funikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko la ardhi kukumba taifa hilo siku tano zilizopita. Licha ya kuwa chini ya maporomoko hayo kwa siku hizo tano isaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida. Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake.Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi. Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo. Wengi wa wanavijiji wangali wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa huku mashirika ya kutoa misaada ya kisema huenda ikachukua siku nyengine 5 kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa miundo mbinu. Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415 kuisaidia Nepal katika kipindi cha miezi 3 ijayo.

Thursday, April 23, 2015

Wafuasi wa dhehebu wauawa Angola

Wanachama kadha wa dhebu moja lililojihami wameuawa kwenye mapigano na vikosi vya usalama nchini Angola. Chama kikuu cha upinzani nchini humo cha UNITA kilisema kuwa huenda watu 200 waliuawa huku chama tawala cha MPLA kikisema kuwa ni watu 13 waliuawa. UNITA kinaitaka serikali ya Angola kuchunguza vifo vya waumini wa dhebu la Seventh Day Light of the World ambalo lilijitenga kutoka kanisa la Seventh Day Adventist. Dhehebu hilo linamini kuwa dunia itaisha mwishoni mwa mwaka huu na limetoa witu kwa wafuasi wake kuondoka makwao na kuelekea milimani.

Timu 4 zatinga nusu fainali,Ulaya

Timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali. Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico Madrid. Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali. Nayo Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona.

Jeshi laapa kuwashinda Boko Haram

Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa linafanya oparesheni ya mwisho kwenye msitu moja ambao unaaminiwa kuwa ngome kuu ya wanamgambo wa Boko Haram. Msemaji wa jeshi (Chris Olukolade) alithibitisha kuwa opaesheni zinaendelea kwenye msitu wa Sambisa karibu na mpaka na Cameroon. Serikali ya Nigeria inasema kuwa Boko Haram wako mbioni na jeshi limeapa kuwashinda kabla ya kuapishwa kwa rais mpya Muhammadu Buhari tarehe 29 mwezi Mei. Inaaminika kuwa zaidi ya wasichana 200 wa shule ambao walitekwa nyara mwaka mmoja uliopita kutoka mji wa Chibok huenda wameshikiliwa ndani ya msitu huo

Monday, April 20, 2015

Jacob Zuma aapa kukabiliana na ghasia

Rais Jacob Zuma amewatembelea watu walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo. Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita.Amesema kuwa ghasia hizo ni kinyume na maadili ya taifa la Afrika kusini. Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika maeneo yenye mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini. Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini. Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini. Nchini Harare Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alilaani ghasia hizo. Ghasia hizo zilianza baada ya mfalme mmoja wa Kizulu, Goodwill Zwelethini, kusema kuwa raia wa kigeni sharti waondoke Afrika Kusini. Akiongea katika kambi hiyo iliyoko mjini Durban kiongozi mkuu wa jimbo la Gauteng, David Makhura, anasema kuwa uhasama na ghasia hizo zinazoshuhudiwa, haundamani na uhuru wa miaka mingi ambayo Afrika Kusini ilipigania.

IS latoa video ya mauaji ya wakristo

Wanamgambo wa kundi la Islamic State wametoa kanda ya video wanayosema inaonyesha mauaji ya takriban Wakristo 30 kutoka Ethiopia waliokamatwa na washirika wa IS nchini Libya. Picha za kundi moja zimeonyesha wakikatwa vichwa katika ufukwe wa bahari huku picha nyengine zikionyesha kundi jingine la raia hao wakipigwa risasi kichwani katika jangwa. Maandishi katika kanda hiyo yanasema kuwa waathiriwa ni wanachama wa kanisa la Ethiopia. Kanda hiyo ya dakika 29 inaonyesha alama ya kundi la mawasiliano la IS kwa jina Al-Furqan na inafanana na ile iliotolewa hapo awali na kundi hilo ikiwemo ile iliochapishwa mwezi Februari ambayo ilikuwa ikiwaonyesha wapiganaji wa kundi hilo wakiwakata vichwa wakristo 21 wa Misri katika ufukwe wa bahari nchini Libya.

Dawa ya magugu yauwa watu Nigeria

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inavoelekea dawa ya kuuwa magugu ndio chanzo cha vifo vya watu 18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana. Katika siku chache zilizopita wakaazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache baada ya kuhisi macho hayaoni sawasawa na kuumwa na vichwa. Baadae wanazimia. Msemaji wa WHO alieleza kuwa ukaguzi uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu. Alisema kwa sasa mawazo yao ni kuwa vifo hivyo vilisa-babishwa na dawa ya kuuwa magugu.

Friday, April 17, 2015

Mahakama yakunjua makucha Tanzania

Katika hukumu nadra kutolewa nchini Tanzania, mahakama Kuu Kanda ya Tabora imeiagiza halmashauri ya wilaya ya Urambo, kulipa fidia ya shilingi milioni 25 kwa Mwamini Adam na mumewe Idrisa Jafari kutokana na madhara waliyopata baada ya uzembe uliofanywa na daktari wa hospitali ya wilaya hiyo alipokuwa akimfanyia upasuaji Mwamini. Katika uamuzi wa shauri hilo la madai Namba 13/2011 uliotolewa hivi karibuni, Mahakama Kuu imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa Mwamini shilingi milioni 20 kutokana na kilema alichopata kwa kuondolewa mfuko wa uzazi na kukatwa utumbo. Pia, mahakama imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa Jafari fidia ya shilingi milioni tano ikiwa ni gharama za uendeshaji wa shauri hilo. Akisoma hukumu, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Amir Mruma alikubaliana na madai ya walalamikaji kuwa madhara waliyopata kutokana na uzembe uliofanywa na Dk Jackob Kamanda ni makubwa. Jaji Mruma alisema haipingiki kwamba huo ni uzembe uliofanywa na mtumishi, hivyo mwajiri anapaswa kulipa gharama. Aliagiza kuwa kiwango hicho cha fedha kitalipiwa riba ya asilimia saba kila siku kuanzia tarehe ya uamuzi ulipotolewa hadi siku mlalamikiwa atakapolipa fedha hizo. Mwamini na mumewe walifikisha malalamiko yao Mahakama Kuu, wakidai kulipwa fidia ya shilingi milioni 505 kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wakati wa upasuaji kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mgonjwa. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Anatory Lukonge wa Hospitali ya Itigi ambako walibaini kitambaa tumboni mwa Mwamini, aliieleza mahakama kuwa walipomfanyia upasuaji walikuta utumbo umeshikana na kizazi huku juu yake kukiwa na kitambaa. Dk Lukonge alisema walikitoa kitambaa hicho lakini kutokana na sehemu ya kizazi kuharibika, iliwalazimu kukiondoa huku akidai kuwa hali hiyo ilisababishwa na uzembe wa daktari aliyemfanyia upasuaji.

Wageni waendelea kushambuliwa A Kusini

Kumekuwa na mashambulizi zaidi usiku dhidi ya biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kutawanya umati kusini mwa mji wa Johannesburg ambapo gari na nyumba vilichomwa moto. Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa karibu raia mia mbili wa kigeni walikimbilia usalama kwenye kituo cha polisi lakini wakaondoka muda baadaye. Usalama umedumishwa kufuatia mashambulizi yaliyowalenga raia wa kigeni ambapo watu watano wameuawa. Rais Jacob Zua amelaani ghasia hizo na maandamano ya amani mjini Durban siku ya Alhamisi yalihudhuriwa na zaidi ya watu elfu kumi.

Wednesday, April 15, 2015

ANGLICAN CHURCH OF KENYA CALLS FOR UNITY TO DEFEAT TERRORISM

The primate of the Anglican Church of Kenya, Rev. Dr Eliud Wabukala, in his message for Good Friday called for unity in order to defeat the terrorist threat faced by the country. The Anglican Church of Kenya is a member church of the World Council of Churches (WCC). Wabukala’s remarks came in a pastoral letter following the al-Shabaab attack on 2 April at Garrissa University, Kenya, that killed nearly 150 people, including many Christians. In his letter Wabukala said, “Let us resolve today that these deaths, and those of other Kenyans who have died previously at the hands of al Shabaab, will not be in vain.” “We call on the government to do all in its power to protect the lives of its citizens and we call on the world community to recognize that this latest outrage is not just an attack on Kenya, but part of an assault on world peace. The time has come for the world to unite as never before in defeating this growing menace,” Wabukala added. Wabukala went on to say that while government has a vital role to play in dealing with terrorism, the hearts and minds of ordinary people are even more important. He said, “Let us covenant together before God that we will never ever surrender our nation or our faith in Christ to those who glory in death and destruction. We will not be intimidated because we know and trust in the power of the cross, God’s power to forgive our sins, to turn death into the gate of glory and to make us his children for ever.”

Drogba arejesha alichojaaliwa kwa jamii.

Mshambuliaji wa timu ya Chelsea F.C. Didier Drogba amezindua hospitali ya kwanza, kubwa na ya aina yake kati ya tano alizo wahi kuahidi kuzijenga kama sehemu ya kujitolea kwa jamii yake . Hospitali hiyo iko wilaya ya Attécoubé katika mji wa kibiashara wa Abidjan, hospitali hiyo imemgharimu nguli huyo wa kandanda kiasi cha dola milioni moja za kimarekani ili kukamilisha mjengo huo wa afya ;na hospitali hiyo ni maalumu kwa wanawake na watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu . Hospitali hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba mia nane (800) huduma kadhaa zinapatikana ikiwamo chumba cha uchunguzi, wodi ya wazazi,kitengo cha watoto,jengo la x-ray ,jengo la kisasa la maabara,duka kubwa la dawa,jengo la kulaza wagonjwa na jengo tengefu la wagonjwa. Inakadiriwa hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa elfu hamsini kwa mwaka na hii ni kwa muujibu wa katibu mkuu wa asasi ya Didier Drogba Foundation , Guy Roland Tanoh ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo. Hospitali zingine nne zilizo katika ahadi za mwanasoka huyo ziko katika hatua za ujenzi za mwisho mwisho kukamilika ambazo ziko nchini Ivory Coast katika miji ya Yamoussoukro, San Pedro, Man na Korhogo na zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao. Asasi hiyo ya Drogba foundation inaandaa chakula cha hisani mjini London mwezi huu wa April tarehe 18 ili kupata fedha za kukamilisha miradi hiyo. Mshambuliaji huyo wa timu ya Chelsea na pia timu ya Elephants anabakia kuwa mchezaji na mfungaji bora na wa mfano wa kuigwa nchini mwake pamoja na kwamba amestaafu kuichezea timu yake ya taifa,ambayo iliutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Africa mwaka huu nchini Equatorial Guinea mnamo mwezi wa February. Kazi nzuri Didier Drogba! .

Hillary Clinton atangaza kugombea urais

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton ametangaza rasmi kuingia katika kinyang'anyiro cha urais wa nchi hiyo katika uchaguzi wa 2016 ambapo anataka kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Marekani. Alizindua ukurasa wake wa kampeni katika mtandao wa internet, Jumapili, akiwaambia Wamarekani kuwa anataka kuwa "kiongozi" wao. Bibi Clinton aliingia katika mbio za kuomba kuteuliwa na chama cha Democratic kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008 lakini alishindwa kwa Bwana Barack Obama. Akiwa mgombea anayepewa nafasi na wanachama wa Democratic alitarajiwa kutangaza azma yake ya kugombea miezi kadhaa iliyopita. Katika video kupitia ukurasa wake wa kampeni, Bibi Clinton alitangaza: "Nagombea urais". "Wamarekani wamepambana na nyakati ngumu za uchumi," amesema, "lakini hali imebaki kuwanufaisha walio juu. "Kila siku Wamarekani wanataka kiongozi na nataka kuwa kiongozi," amesema Bibi Clinton pia alikuwa mke wa rais wakati mumewe Bill Clinton alipokuwa rais wa Marekani.

Thursday, April 9, 2015

Mchezaji wa EPL anaswa kwa wizi London

Mchezaji wa zamani wa ligi kuu ya premia ya Uingereza Andrea Dossena amekamatwa kwa kuiba bidhaa dukani. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Leyton Orient anadaiwa kuwa aliiba katika duka moja la kifahari la Harrods lililoko jijini London. Awali Andrea aliwahi ichezea timu ya Liverpool. Andrea alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha Brompton Road, Knightsbridge. Andrea alikamatwa akiwa na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 31. Hata hivyo waliachiliwa kwa dhamana hadi mwishoni mwa mwezi huu. Dossena alijijengea sifa si haba alipokuwa Anfield , ikiwa ni pamoja na kuifungia dhidi ya Manchester United na Real Madrid . Liverpool ilitoa pauni milioni saba mwezi Julai 2008, kumsajili Dossena . Raia huyo wa Italia ameiwakilisha nchi yake katika mechi 10 alijiunga na Napoli januari mwaka wa 2010 Aidha aliwahi ichezea Sunderland mwaka 2013-14.

Leodgar Chila Tenga aula CAF.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF). Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA. Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani. Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA. NB: Kesho alhamisi saa 5 kamili asubuhi kutakua na mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa TFF uliopo Karume, makocha wa Twiga Stars na She-Polopolo wataongelea maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa siku ya ijumaa.

Saturday, April 4, 2015

Mbowe: Kila chama Ukawa ruksa kuandaa wagombea.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema kila chama ndani ya umoja huo kiko huru kutoa fomu na kuandaa wanachama wake watakaoshindanishwa katika mchakato wa kuwapata wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu. Tamko hilo lilitolewa na viongozi wakuu wa Ukawa baada ya kumalizika kwa kikao cha siku mbili kilichofanyika Shangani, Zanzibar kujadili hali ya kisiasa na utaratibu wa kuwapata wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge na urais. Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe alisema wagombea wa umoja huo watapatikana kwa kuzingatia sifa na uwezo wa kila mmoja na nia ya kweli ya kuleta mabadiliko katika nchi. “Hakuna chama kinachozuiwa kutoa fomu kutafuta wagombea katika mchakato wa ndani wa chama kabla ya Ukawa kufanya uteuzi wa mwisho,” alisema Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema. Kuhusu mvutano Kauli ya Mbowe inakuja wakati kukiwa na wasiwasi miongoni mwa wanachama na wajumbe wa kamati ya ufundi ya Ukawa kutokana na mvutano wa kila chama kutaka majimbo fulani ambako kila kimoja kinadhani kinakubalika. Hata hivyo, Mbowe alisema Ukawa inaendelea kuimarika tangu kuasisiwa kwake na hakuna mpasuko kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. “Hakuna mushkeli, uhusiano wetu Ukawa unaendelea kuimarika na tutahakikisha tunasimamisha mgombea mwenye sifa na uwezo wa kutuletea ushindi, hatutagubikwa na masilahi ya vyama, tunataka masilahi ya Ukawa kwanza vyama baadaye. “Ni ndoto Ukawa kumeguka kwa sababu tumetambua umoja ni nguvu na wenzetu wanasubiri kuona tunameguka,” alisema Mbowe katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad. Gharama za uchaguzi Alipoulizwa kuhusu gharama za uchaguzi ndani ya Ukawa, Mbowe alisema ni mapema kueleza hilo lakini hawatarajii kumwaga fedha kama wanavyofanya baadhi ya wagombea wa chama tawala katika kutafuta nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo urais wa Muungano... “Ukawa tunajiamini, tuna uwezo wa kushinda dola.” Awali, Mwenyekiti wa CUF ambaye pia mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kikao hicho kimepata mafanikio makubwa na kusisitiza kuwa wagombea wa Ukawa watatangazwa baada ya kukamilika mchakato ndani wa vyama. Alisema kwa mwelekeo wa kisiasa baada ya kufanya tathmini, Ukawa ina nafasi kubwa ya kuingia Ikulu ya Muungano na Zanzibar mwaka huu kutokana na CCM kushindwa kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Alisema lengo kubwa la Ukawa ni kuwa na Tanzania mpya yenye maendeleo na sera ya maisha bora kwa Watanzania wote na kuwataka wananchi kuwa tayari kuyapokea mabadiliko ya kiutawala baada ya Uchaguzi Mkuu. Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alisema chama chake si msindikizaji katika Ukawa na nia yake ni kuona mabadiliko ya kiutawala yanatokea. Aliwataka Watanzania kuwa tayari kufanya uamuzi mgumu. “Tayari nimeota ndoto Ukawa wanakamata madaraka ya nchi mwaka huu,” alisema Makaidi.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kuzindua Kanda mpya ya Kusini itakayoundwa na mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.

Akizungumza na NIPASHE juzi, Ofisa wa chama hicho Kanda ya Kusini, Filbert Ngatunga, alisema mwanzo Kanda ya Kusini ilikuwa inaundwa na mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Ruvuma na makao makuu yake yalikuwa mjini Songea mkoani Ruvuma. Alisema kutokana na maboresho yaliyofanywa na chama hicho, waliamua Mkoa wa Ruvuma kuuhamishia katika Nyanda za Juu Kusini na hivyo kuungana na mikoa ya Njombe, Mbeya, Iringa na Rukwa na hivyo kanda hiyo kuundwa na mikoa mitano. Aliongeza kazi hiyo itafanyika Aprili 11 na 12, mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika. Alisema kabla ya uzinduzi huo, kutakuwa na vikao vya ndani na kufuatiwa na mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mashujaa.

BLOGGERS WAMUOMBA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ASIPITISHE MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA MTANDAONIMUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015

Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni. Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo. MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015 Umoja huu (TBN) ulishtushwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kwa hati ya dharura kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo tulihitaji maridhiano na wadau na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa kutumia mitandao na yapi yanakubalika. Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutoka na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea habari. Hali kadhalika tulishuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu zenye uzito za kwanini sheria hii isipite kwa hati ya dharura na kuhoji kwanini sheria hii ipite kwa dharura bila ya kupata majibu. Muswada huu ambao kati ya makosa mengi uliyonayo kubwa moja wapo ni majukumu makubwa aliyopewa Mkuu wa Kituo chochote cha Polisi kuwa na uwezo wa kupekuwa na kuchukua vielelezo/data pale anaposhuku kuna suala la uhalifu unaohusu mtandao. Swali ni kuwa kwanini polisi apewe mamlaka ya kumsulubisha mtuhumiwa katika hatua ya mwanzo bila uthibitisho wa sahihi? Mbali na hapo, sisi kama waandishi ulimwenguni kote tunatakiwa kufuatilia maadili ya kazi zetu. Maadili ya mwandishi yeyote yule ni kutunza usiri wa chanzo cha habari yake pale inapotakiwa lakini katika sheria hii sisi kama bloggers, sheria hii inakiuka hili kwa kutulazimisha kutaja vyanzo vya habari. Kupitia sheria hii, bloga yeyote yupo hatarini kutokana na kwamba sheria inaainisha ni kosa la jinai kutoa ujumbe unaoweza kumuudhi mtu kihisia. Aidha, tunamuomba Mheshimiwa Rais pia asipitishe Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2013. Muswada huu unavinyima uhuru vyombo vya habari vinavyotangaza takwimu mbalimbali. Kama ilivyo Ibara ya 7(4) ‘‘Chombo chochote cha habari ambacho kinachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au upotoshaji, au kinatangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa.’’ Hii iki maanisha kuwa hata blog zetu ziko hatarini kuelekea katika kulazimika kufanya kazi za kuisifia serikali na kutangaza takwimu zilizopitiwa na serikali tu, jambo ambalo litaharibu ukuaji wa uhuru wa habari nchini. Tunamkumbusha mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa na kupokea habari. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika IMETOLEWA NA; Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network-TBN) 04/03/2015. http://www.tbn.or.tz/

Chadema wasafiri kwa chopa kusaka majimbo Kanda ya Ziwa.

Mwanza. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Ziwa Magharibi, kimeanzisha operesheni maalumu kwa ajili ya kusaka ubunge katika majimbo yote yaliyoko kwenye kanda hiyo ambayo yanashikiliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Operesheni hiyo inayojulikana kama ‘tigitigi’, ilianza juzi kwa kutumia usafiri wa helikopta katika majimbo kadhaa, ikiwamo Jimbo la Sengerema linaloshikiliwa na mbunge wa sasa, William Ngeleja. Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Geita Alphonce Mawazo ni miongoni mwa makada wa chama hicho waliofika katika jimbo la Sengerema juzi, wakiambatana na kada wa chama hicho anayetaka kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo, Hamis Tabasamu. Akihutubia kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji tofauti kwa muda wa dakika 30 katika kila kijiji, Mawazo alisema wameanzisha operesheni hiyo kwa lengo la kushinda ubunge kwenye majimbo yote yaliyoko kwenye kanda hiyo ili kuleta ukombozi wa kweli kwa wananchi. “Wananchi naomba niwambie tumeanza na Jimbo la Sengerema, tutapambana hadi hatua ya mwisho ili kulikomboa jimbo hili. Tunataka Kanda ya Ziwa iwe ya mfano, tutazunguka kata zote na vijiji vyote katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza, Tabora, Shinyanga na Mara kuelimisha wananchi,” alisema Mawazo na kuongeza’ “Pia naomba wananchi mjitokeze kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili tuweze kupata nafasi ya kufanya mabadiliko ya kweli mwezi Oktoba. Ndugu zangu mapambano yameanza hakuna kulala, huu ni wakati wetu Chadema,” alisema. Naye mtangaza nia wa jimbo hilo, Hamis Tabasamu ambaye aliwahi kuwa diwani wa Sengerema, alisema kuwa watafungua ofisi 78 za Chadema kwenye jimbo hilo ili wananchi waweze kuwa na sehemu za kutoa malalamiko yao kwa viongozi na kuhudumiwa. Alisema muda uliopo sasa ni wa kufanya mabadiliko na kwamba kazi ya kutafuta ukombozi Sengerema imeanza, hivyo ni jukumu la wananchi wa eneo kuunga mkono jitihada za chama hicho za kuwaletea maendeleo endelevu. “Mimi ni mtangaza nia wa jimbo hili nipo tayari kushirikiana na nyie kuleta mabadiliko ya kweli Sengerema. Tutafungua ofisi 78 hapa na kazi zitafanyika kila kona ya jimbo hili ili tuweze kuing’oa CCM hapa. Nia na sababu ya kuing’oa CCM tunazo kwa kuwa ni ukweli kwamba haijafanya kitu chochote katika uongozi wake eneo hilo,”alisema Tabasamu.

Friday, April 3, 2015

Zimbabwe:ZANU-PF chamtimua Bi Mujuru

Aliyekuwa makamu wa rais nchini Zimbabwe Joice Mujuru amefukuzwa katika chama tawala ZANU-PF. Chama hicho kinasema alipanga njama za kumuondoa mamlakani rais Robert Mugabe mbali na kukiharibia jina chama hicho- madai ambayo ameyakana hapo mbeleni . Bi Mujuru alipigana vita vya Guerilla pamoja na Mugabe miaka ya sabini dhidi ya uongozi wa weupe na alionekana kama mrithi wake,kabla ya kukosana naye mwaka uliopita swala lililomfanya kufutwa kazi kama makamu wa rais mnamo mwezi Disemba. Waandishi wanasema alishtumiwa sana na mke wa Mugabe, Grace ambaye anaongoza wanawake katika chama hicho.

Kanisa Katoliki linautazamaje ushoga?

Kadinali Raymond Burke mwenye asili ya Marekani ameenguliwa na Papa Francis katika wadhifa wake wa mwenyekiti wa bodi katika kanisa katoliki,ametoa onyo kwamba kuna viashiria vya kanisa hilo kuupigia chapuo ushoga, kauli hii Burke aliiotoa wakati alipokuwa akihojiwa na tovuti moja ya Italy ya La Nuova Bussola Quotidiana mara baada tu ya kuenguliwa kwenye wadhifa wake. Mwandishi wa BBC anasema hii ni ishara nyingine ya jinsi viongozi wa dini waandamizi wanavyochukulia hatua juu ya masuala kama vile ushoga na talaka , wakati wengine wanatakiwa kuyachukulia mambo kwa utuvu na uangalifu wa hali ya juu.

Thursday, April 2, 2015

NEC ITATOA RATIBA KAMILI KUHUSU BVR NA KURA YA MAONI – PINDA.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwa serikali imeiagiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa ratiba kamili kuhusu zoezi la uandikishwaji Wapiga Kura kwa BVR pamoja na hatma ya Kura ya Maoni ya Katiba Mpya. Pinda ameyasema hayo wakati akiahirisha Bunge majira ya saa 6 usiku wa kuamkia Alhamis tarehe 02 April, 2015 ambapo amedai kuwa tayari serikali imekwisha lipia pesa zote kwa ajili ya mashine zote za kuandikishia (BVR). “Serikali imekwishatoa pesa kwa ajili ya mashine zote za BVR kilichobaki ni kwa Tume kupanga ratiba yao, tuna imani kuwa mashine zote zikifanya kazi zoezi la uandikishwaji wapiga kura litamalizika kwa wakati” Amesema Pinda Amesema ameongea na Mwenyekiti wa tume hiyo leo (April 01) na imemuhakikishia kuwa itatangaza ratiba nzima kabla ya Pasaka. Kuhusu ugawaji wa Katiba Pendekezwa amesema kuwa tayari nakala 1,141,300 kwa upande wa Tanzania Bara na nakala 210,000 kwa upande wa Zanzibar zimekwisha sambazwa. Kuhusu muswada wa mahakama ya Kadhi, Pinda amesema serikali imefurahishwa na uamuzi wa muswada huo kuondolewa kwa kuwa itapata muda wa kutosha kujadiliana na wadau na kutoa elimu zaidi kuhusu umuhimu wa Mahakama hiyo. Bunge limeahirishwa hadi tarehe 12 Mei, 2015 kwa ajili ya mkutano wa 20 likiwa limejadili na kupitisha miswada 14 kati ya 21 iliyokuwa imepangwa katika mkutano huu uliomalizika leo. Kabla ya kuahirishwa, bunge limefanya maamuzi ya kupitisha muswada wa uhalifu wa kimitandao huku likiwa na wabunge wasiofikia nusu ya wabunge wote kama inavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni.

Maaskofu wamjibu Rais Kikwete

Siku tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa tamko la Jukwaa la Wakristo (TCF) kuwataka waumini wao kupigia kura ya 'hapana' Katiba Inayopendekezwa lilikuwa la hasira, viongozi hao wamejitokeza tena na kusisitiza kwamba msimamo wao huo utabaki kama ulivyo. Katika tamko pamoja walilolitoa jana baada ya kukutana juzi mjini Dodoma, viongozi hao wamemtahadharisha Rais Kikwete kuwa kuendelea kupigia debe Katiba Inayopendekezwa na kuruhusu Mahakama ya Kadhi, kunaweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko na hali ikiwa hivyo Serikali ndiyo itakayolaumiwa. Tamko hilo limesainiwa na viongozi walewale waliosaini lile la awali la Machi 12, mwaka huu ambao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet.(P.T) Tamko hilo la maneno 921, limeendelea kuwataka waumini wao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya 'hapana,' msimamo ambao tayari umeibua msuguano baina yao na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyesema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamulia waumini wao aina ya kura wanayostahili kupiga. Pia, Jukwaa hilo limewataka viongozi wakuu wa Serikali –Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais Kikwete wasifurahi kwamba ujumbe wao umewafikia viongozi wa dini waliozungumza nao hivi karibuni, kwa kuwa watu waliokutana nao si wawakilishi rasmi na hawana uwezo wa kutoa uamuzi au kukubaliana juu ya jambo la kitaifa. "Maaskofu tuliokutana hapa (mjini Dodoma) hatuna hasira na wala hatuongozwi na hasira wala mihemko katika kufikia maamuzi tunayofanya kama ambavyo wengine wanavyotutafsiri, tunafikia maamuzi yetu baada ya maombi na sala na tunasukumwa na upendo kwa wananchi ili kujenga Taifa lenye umoja, amani, utulivu na maelewano," lilisema tamko hilo likihitimishwa kwa maneno ya Biblia kutoka Mithali 29: 1, "Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla, wala hapati dawa." Jumamosi iliyopita, Rais Kikwete akifungua mkutano wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali ikijumuisha viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, alisema msimamo wa TCF kuhusu kuipigia kura ya 'hapana' Katiba Inayopendekezwa ni wa hasira na usiokuwa na tija kwa maendeleo ya Taifa. "Nimeyasoma matamko hayo yote kwa umakini, imenishangaza, imenisikitisha na kunihuzunisha. Siamini kwa nini wamefikia huko kwa kuunga au kutokuunga mkono," alisema Rais Kikwete. Rais Kikwete alisema: "Waacheni waumini waamue Katiba wanayoitaka wao... hayo matamko niliyoyasoma yamejaa hasira kwa Serikali kupeleka bungeni Muswada wa Mahakama ya Kadhi." Maaskofu hao walikuwa Dodoma kufuatilia kwa kina Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964 unaotambua Mahakama ya Kadhi. "Muswada huu unapendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi ambao utawasilishwa bungeni leo kwa hati ya dharura na hivyo kuufanya umma wa Watanzania kutokujua maudhui yaliyomo katika muswada huo wakati bado hoja zetu za msingi tulizopeleka kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge na kwa Waziri Mkuu hazijajibiwa," Ilieleza taarifa hiyo. "Tunamtaka Rais aagize muswada huu uondolewe bungeni na usijadiliwe tena kwa kuwa utafiti wa Tume ya kurekebisha sheria ulishaonyesha madhara ya uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi. Vinginevyo, kuendelea kujadiliwa kwa muswada huu maana yake ni kwamba Serikali inajihusisha na itagharimia mahakama hiyo." Chanzo:Mwananchi

Buhari ahidi kutokemeza Boko Haram

Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa linalokabili nchi. Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani. "Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao." Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu. "Tumebaini matatizo makubwa matatu. Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe. Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi, miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii." Anasema rais huyo mteule wa Nigeria.

Wednesday, April 1, 2015

Kwanini Buhari alimbwaga Goodluck ?

Raia wa Nigeria wameshazoea kuwa rais anayeongoza hawezikushindwa katika uchaguzi wa Nigeria! Lakini leo Nigeria imefungua ukurasa mpya. Rais aliyeko madarakani Goodluck Jonathan amesalia akijutia maamuzi yake baada ya raia wa taifa hilo kubwa zaidi Afrika kiuchumi kumpigia kura mpinzani wake mkuu Muhammadu Buhari . Hizi hapa sababu 5 ambazo zinaelezea kwanini raia wa Nigeria walimng'oa Goodluck Jonathan mamlakani. 1: Haikuwa rahisi kuiba kura Katika Uchaguzi uliopita mwaka wa 2007 ,tuhuma za wizi wa kura za urais ziliibuka huku wadadisi na wachunguzi wakuu wakisema waziwazikuwa kura hazikuwa za huru wala haki. Ripoti ya wachunguzi huru katika uchaguzi wa mwaka wa 2011 ilisema kuwa haukuwa wa uhuru japo ilisema kuwa idadi ya wizi ilikuwa imepungua mno. Kufuatia ripoti hiyo tume huru ya uchaguzi nchini humo ilijiandaa na kuziba mianya iliyokuwa imebainika. Tume hiyo ilinunua mashine za kuwasajili wapiga kura kwa njia ya kielektroniki na ving'amuzi vilivyotumika kubaini data ya mpiga kura. Chama cha rais Goodluck Jonathan People's Democratic Party (PDP) kilikuwa kimepoteza ufuasi mkubwa katika majimbo yaliyokuwa ngome yake. 2 Boko Haram Uchaguzi huo umetangazwa huku raia wengi wa Nigeria wakikabiliwa na changamoto ya usalama wao haswa wakiwa mijini. Hii inafwatia tishio la kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram ambao walikuwa wanaonekana ni kama wameishinda maarifa vyombo vya usalama wa kitaifa. Boko Haram iliwaua zaidi ya watu elfu 20,000 na kuwalazimisha wenyeji zaidi ya milioni tatu kutoroka makwao. Rais Jonathan hakuwa na jibu dhidi yao na alionekana mnyonge hadi majuzi majeshi ya muungano wa mataifa jirani yaliposhirikiana na jeshi la Nigeria na kuwavamia wanamgambo hao wa kiislamu. Kura hizi zimefanyika zaidi ya majuma 6 baada ya kuahrishwa kufuatia tishio la kundi hilo lililokuwa limeapa kusambaratisha uchaguzi. 3 Muungano wa Upinzani Chama cha PDP kiliundwa kwa muungano wa viongozi kutoka matabaka ya kaskazini na vilevile kusini mwa taifa hilo. Hata hivyo kufuatia utepetevu wa rais Jonathan viongozi wengi waliokuwa nguzo ya umoja huo walitawanyika. Muungano wa viongozi wa upinzani chini ya nembo ya chama cha All Progressives Congress (APC)kuliwasaidia kukusanya kura zote katika kapu moja. Kampeini za chama tawala zilikumbwa na madai ya hiyana na unafiki lakini vyama vya upinzani havikulegeza kamba . 4 Uchumi mkubwa zaidi Afrika Ijapokuwa Nigeria inasifika kuwa taifa kubwa zaidi barani Afrika kiuchumi ,ukiwauliza raia wa Nigeria iwapo wamenufaika kwa njia yeyote ile watakuambia kuwa hawajanufaika kwa hali yeyote ile. Takriban nusu ya raia wa nigeria wanaishi kwa hali duni ya uchochole na umaskini. Wengi wao wanalaumu ufisadi wa viongozi na ubadhirifu wa mali ya umma. Uchumi wa Nigeria umekuwa kwa kiwango cha asilimia 5% kwa mwaka kutokana na mauzo ya mafuta lakini raia wengi hawakutaka kuendelea na utawala wa Goodluck. 5 Ni wakati wa Mabadiliko Wafuasi wa chama cha upinzani APC walichagua kibwagizo chao kikuu kuwa ''Mabadiliko''. Na huenda wanigeria hawakuwa wanataka kuendelea na hali ilivyokuwa wakati huu. PDP imekuwa madarakani tangu mwaka wa 1999, utawala wa kiimla ulipomalizika. Mwaka huu 2015 Wapiga kura wameamua kumchagua kiongozi atakayekuwa na msimamo dhabiti na uwezo wa kukabiliana dhidi ya matatizo chungu nzima yanayowasakama Hata hivyo kinachosubiriwa na wengi ni kuona iwapo rais Buhari ataleta mabadiliko kweli alivyowaagiza wapiga kura.

Palestina yapewa uanachama wa ICC

Wapalestina wamepata uanachama wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita miezi mitatu baada ya ombi lao kukubaliwa. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Palestina Riad Malki anatarajiwa kutoa taarifa baada ya kuhudhuria sherehe za makaribisho kwenye mahakama hiyo mjini Hague. Uanachama wa ICC unaiwezesha Palestina kuifungulia Israeli mashtaka ya uhalifu wa kivita lakini pia utachangia wanamgambo wa Hamas nao kufunguliwa mashtaka. Serikali ya Palestina inasubiri kutoa malalamishi dhidi ya Israel kuhusu madai ya uhalifu wa kivita mnamo mwaka 2014 katika eneo la Gaza na hatua ya Israel kujenga makaazi katika ardhi yake.

Buhari:Ni ushindi wa kidemokrasi Nigeria

Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Nigeria Muhammadu Buhari anasema kuwa ushindi wake unamaanisha kuwa taifa hilo linafuata mfumo wa kidemokrasi. Buhari alimshinda mpinzani wake Goodluck Jonathan,kwa kura millioni 2 idadi ambayo wachanganuzi wanasema kuwa itazuia harakati zozote za kuanzisha kesi. Ni mara ya kwanza kwa rais wa taifa hilo kushindwa katika uchaguzi. Bwana Buhari ,kiongozi wa zamani wa kijeshi alichukua mamlaka mnamo mwaka 1980 kupitia mapinduzi. Hatahivyo alifanya kampeni za kidemokrasia kwa lengo la kutaka kusafisha siasa katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika. Katika hatua ya kidemokrasia,rais anayeondoka Goodluck Jonathan alimpigia simu Buhari kukubali ushindi na vilevile kutoa taarifa akiwataka wafuasi wake kukubali matokeo.