Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 31, 2015

WORLD COUNCIL OF CHURCHES AT A PRESENCE TO ACCOMPANY VULNERABLE COMMUNITIES

They are there every day, each month of the year – as they have been for the last 13 years. They have become a natural element in the chaos of life in Israel and Palestine. Their presence is appreciated. They provide safety and stability. Their sole weapon is a pen, or a camera. They see and listen; they analyze and report back. The Ecumenical Accompaniment Programme in Palestine and Israel (EAPPI) has existed since 2002 and contributes to curbing violence and promoting respect for international law. Their presence is an expression of practical solidarity with vulnerable groups – both Palestinians and Israelis. The author travelled to the Holy Land in March 2015 with a high-level delegation representing WCC leadership of the Central Committee. EAPPI is a concrete response to an appeal to the World Council of Churches from church leaders in Jerusalem in 2002. They wrote in a letter: “We would respectfully request protection of all people in order to assist the re-establishment of mutual trust and security for Israelis and Palestinians. Further, we would call on all peace-loving people from around the world to come and join us in a manifestation for just peace”. The World Council of Churches took the appeal to heart, and together with local churches and churches in Europe and the US they created the accompaniment programme, which is based on presence in the country and on analysing and reporting back on events there. “Over 70 churches, ecumenical bodies and specialized ministries in 22 countries from Africa, Asia, Europe, North America and Latin America actively participate in the programme. Almost 1,500 accompaniers have participated. We will soon receive the 58th group,” says Manuel Quintero Pérez, coordinator for EAPPI at the WCC. The accompaniers are recruited locally. Since the beginning, there has been incredibly strong support and commitment among member churches. An accompanier must be at least 25 years old but not yet 70, have experience working with people, and speak English fluently. Three recommendations are required in order to be accepted. The assignment is three months long; accompaniers work on international teams and live in places such as Hebron, Jericho or Jerusalem. Solidarity visit to the Holy Land In conjunction with the World Council of Churches’ solidarity visit to the Holy Land in March 2015, we meet around ten different accompaniers. We meet one team in Jericho, a Norwegian and a Swede who constitute one of the teams stationed in the city. They explain that the day before, they were alerted that the army was demolishing homes. They received the information via text message and promptly proceeded to the area. The trips are long, and it is sometimes difficult to find their way. They arrive and meet a Bedouin family with many young children; the family has been asked to leave the area and sit out in the scorching heat and glaring sun with no shelter. They plead to be allowed to take the children to a shady area but are denied their request. The accompaniers stay with the family, give them water and try to talk to the army for the sake of the children. But their home is leveled to the ground; everything they own is destroyed, including food, clothing and school books. The children go to a school that the UN established in the area, and the school books are a requirement for attendance. No school books, no school. When we meet the family the next day again with the accompaniment team, the hard-hit family greets the team warmly. They readily open up and tell us about the previous day. They show us the rubble of what was their home yesterday. Now, nothing is left. “By all means, we want to talk about it. Talking helps us process the traumatic events of yesterday. The fact that the World Council of Churches is focusing on accompaniers brings hope for the future – someone cares, someone is there as support in this mangled and tattered part of the world,” says the father of the family. This is one life story among thousands, perhaps millions, of life stories. The accompaniers are tasked with seeing, analyzing and reporting back.

Buhari aongoza katika matokeo ya awali Nigeria

Matokeo ya awali ya kura zilizopigwa siku ya jumamosi huko Nigeria zinaonesha kuwa kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni rais Goodluck Jonathan. Generali Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) anaonekana kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos. Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao. Huku zaidi ya nusu ya matokeo yakiwa yametangazwa mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari yuko mbele ya rais wa sasa Goodluck Jonathan. Hata hivyo matokeo bado hayawezi kutabiriwa kwa kuwa majimbo yenye watu wengi kama Lagos na Rivers hayajatangaza matokeo yake. Mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali. Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.

Jamii itoe ushirikiano kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini

JAMII imetakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi nchini katika kutoa taarifa zitakazo fanikisha kukamatwa kwa wote walioshiriki mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Pereira Silima bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mhe. Al -Shaimaa Kwegyir, Mbunge wa Viti Maalum aliyehoji kuchelewa kwa taarifa ya kupatikana kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Emmanuel. "Pendo alitekwa kutoka mikononi mwa mama yake mzazi, hii changamoto ni kubwa sana, tunaomba jamii itusaidie kutoa taarifa zitakazo saidia kufanikisha kukamatwa kwa wahusika, tushirikiane kwa pamoja kukomesha tatizo hili" alisema Mhe. Silima "tangu kutekwa kwa mtoto Pendo watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi akiwemo baba mzazi, uchunguzi bado unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani hivi karibuni, ila Pendo bado hajapatikana" aliongezea Mhe. Silima Aidha akijibu Swali la msingi la Mhe. Salumu Barwany, Mbunge wa Lindi Mjini, aliyehoji idadi ya kesi za mauaji ya walemavu wa ngozi na sababu za kuchelewa kutolewa hukumu. Mhe. Silima alisema kesi 10 zinaendelea kisikilizwa mahakama mbalimbali "kati ya mwaka 2006 hadi 2015 jumla ya matukio 56 ya uhalifu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaliripotiwa nchini. Matukio 41 yalihusisha vifo 43, matukio 13 yalihusisha majeruhi 13 na matukio 2 ya kupotea kwa watu wenye ulemavu wa ngozi" alifafanua Mhe. Silima "kesi 46 kati ya matukio 56 zilifikishwa Mahakamani ambapo kesi 10 zenye watuhumiwa 12 zilitolewa hukumu ya kifo na kumi ziko chini ya upelelezi. Aidha kesi 26 watuhumiwa wake waliachiwa huru kwa kukosa ushahidi" aliongezea Mhe. Silima Kuchelewa kwa hukumu au upelelezi wa baadhi ya kesi zilizotajwa kunachangiwa na sababu mbalimbali kama vile matokeo ya uchunguzi wa DNA toka Mamlaka ya Uchunguzi na/au mashahidi kutopatikana kwa urahisi na kwa wakati.

Wagombea urais Nigeria mchuano ni mkali

Huku nusu ya matokeo katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria yakiwa yametangazwa, mgombea kutoka chama kikuu cha upinzani, Muhammadu Buhari, anaongoza dhidi ya rais aliye madarakani, Goodluck Jonathan. Lakini majimbo ya kusini yenye idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers bado hayajatangaza matokeo na mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali. Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.

Mwendesha mashitaka auawa Uganda

Watu wenye silaha wamemuua mwendesha mashitaka mkuu katika kesi ya watuhumiwa wa Kiislam wanaotuhumiwa kuua watu kadha katika mashambulio ya bomu mwaka 2010. Mwendesha mashitaka huyo Joan Kagezi ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi mwendesha mashitaka msaidizi nchini Uganda ameuawa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa katika pikipiki wakati akiendesha gari kurudi nyumbani mjini Kampala. Kesi inayoendelea inawahusu watu kumi na watatu wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha al-Shabaab Wanatuhumiwa kuua watu zaidi ya sabini wakati wakiangalia Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 katika mgahawa mmoja na katika uwanja wa klabu ya rugby. Wiki iliyopita Marekani ilisema ilipata "habari za kuwepo uwezekano wa shambulio" katika maeneo ya mji ambayo raia wa mataifa ya magharibi wanakutana. Serikali ya Uganda imesema Marekani ilionya juu ya uwezekano wa kuwepo kwa mtu anayejitoa mhanga akijaribu kuingia nchini humo. Msemaji wa serikali amesema Uganda ilikuwa katika kitisho kwa sababu imechangia askari wengi katika jeshi la Umoja wa Afrika linalolinda amani nchini Somalia wakipambana na kundi la al-Shabab ndani ya Somalia.

Aliye waua Waingereza wawili kunyongwa

Mahakama ya Malaysia imemkuta na hatia ya mauaji mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya wanafunzi wawili wa udaktari kutoka nchini Uingereza.Mauaji hayo yanadaiwa kufanyika August mwakajana katika kisiwa cha Borneo. Jaji wa mahakama hiyo amesema mahakama imeidhishwa na ushahidi dhidi ya mshitakiwa na kuona anastahili adhabu. Hukumu hiyo inayomkabili Zulkipli Abdullah anadaiwa kuwaua Neil Dalton na Aidan Brunger. Kwa mjibu wa hukumu hiyo ya mauaji, Abbdullah atanyongwa hadi kufa.

Monday, March 30, 2015

Matokeo ya uchaguzi Nigeria leo jioni

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni. Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi." Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega. Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo. Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.

Sunday, March 29, 2015

Kesi ya Mtikila vs Mahakama ya Kadhi kusikilizwa Machi 30 yapangiwa Jaji .

Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Machi 30, mwaka huu kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Mchungaji Christopher Mtikila, akipinga kitendo cha Serikali kupeleka Muswada bungeni wa kutunga sheria ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi, kwamba uko kinyume na Katiba ya nchi. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Richard Mziray. Katika kesi hiyo kupitia hati yake ya madai iliyopewa usajili namba 14 ya mwaka huu, Mtikila: 1.Ameiomba mahakama itoe amri kwamba wale walio kwenye mamlaka ya Serikali akiwaemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Mary Nagu; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira na wenzao watoe sababu kwa nini wasifungwe kifungo kisichopungua miaka mitano endapo watashindwa kujieleza. 2.Itoe amri ya vigogo hao kufungwa kifungo hicho kutokana na kuchezea Katiba ambayo ni sheria mama ya nchi. 3.Ameiomba mahakama itoe amri kwamba Mahakama ya Kadhi na Jumuia ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC) itangaze ni haramu kwenye ardhi ya Tanzania. 4.Anadai kuwa suala la serikali kuandaa muswada wa Kiislamu na kuuwasilisha bungeni na kitendo cha Bunge kukubali ni sawa na uhaini. Anadai kuwa kitendo hicho ni sawa na uvunjifu mkubwa wa viapo walivyoapa viongozi hao wakati wa kushika madaraka ya umma na ni kinyume cha ibara ya 19 ya katiba ya nchi inayoeleza kwamba masuala ya dini na kuabudu yatakuwa ni ya mtu binafsi na kwamba uendeshaji wa mambo au taasisi za kidini hazitakuwa sehemu ya mamlaka ya nchi. Chanzo: http://www.wavuti.com/2015/03/kesi-ya-mtikila-vs-mahakama-ya-kadhi.html

Rais Kikwete: Serikali haitaanzisha Mahakama ya Kadhi

Rais Kikwete amesema serikali haiwezi kuanzisha wala kuiendesha na kuihudumia Mahakama ya Kadhi na ameongeza kuwa hilo ni jukumu la Waislamu wenyewe na kwamba hawazuiliwi kuianzisha Mahakama hiyo na kwamba hayo ndio yalikuwa makubaliano. Pia,Rais Kikwete amesema tamko la viongozi wa dini kuhusu suala la katiba mpya, limemshangaza, limemfedhehesha na kumsikitisha sana. Rais Kikwete ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya amani cha viongozi wa dini wa mkoa wa Dar-es-salaam. Chanzo: ITV

Wednesday, March 25, 2015

Awaua wanawe na kuwaweka ndani ya Jokofu.

Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi kufuatia mauaji ya wanawe wawili waliopatikana wamefungikiwa ndani ya jokofu. Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamke huyo mama wa watoto wanne aliwatumbukiza wanawe wawili wenye umri wa miaka 11 na mwengine mwenye umri wa miaka 14 ndani ya jokofu baada ya kuwaua. Aidha miili ya mvulana 11, na msichana 14, ilipatikana imewekwa kwenye karatasi za plastiki ilizisivunde. Yamkini miili hiyo ilipatikana na maafisa wa idara ya mahakama waliokwenda nyumbani kwa mama huyo kwa nia ya kumfurusha baada ya kushindwa kugharamia kodi ya nyumba . Walishtuka kupata miili ya watoto hao na mara moja wakawaarifu maafisa wa polisi katika jimbo hilo. Wanawe wawili waliosalia walikuwa kwa jirani na walichukuliwa na kupewa usalama. Uchunguzi na upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanyika ilikubaina kiini haswa cha vifo vyao. Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo James Craig ametaja kitendo cha mwanamke huyo kuwa cha kuogofya mno. Jirani ya mwanamke huyo Tori Childs, aliliambia shirika la habari la AP kuwa watoto hao wawili waliopatikana walikuwa wametoweka kwa takriban mwaka mzima . Majirani wengine walisema kuwa mwanamke huyo alikuwa taabani haswa baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba, na kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 36 alikuwa kanakwamba anakabiliwa na upungufu fulani maishani mwake.

Nyota wa 'Empire' wadaiwa kuwa wapenzi

Nyota wawili wa filamu ya 'Empire' Adre Lyon na Anika Calhoun ni watu wa familia moja katika filamu hiyo lakini katika maisha ya kawaida wawili hao wamedaiwa kuwa wapenzi. Kulingana na mtandao wa TMZ nchini Marekani wawili hao walionekana katika harusi moja wakiwa pamoja na wengi waliohudhuria sherehe hiyo ya kukata na shoka wanasema nyota hao walionekana kupendana. Katika filamu hiyo ya Empire ambayo ni filamu ya msururu iliyowavutia wengi mwaka huu wawili hao wanaigiza kama mtoto na mama yake wa kambo.

Kinasa sauti cha ndege chaharibika

Waziri wa maswala ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amesema kuwa kifaa cha kunasa sauti kwenye ndege kilichopatikana hapo jana Jumanne baada ya kuanguka kwa ile ndege ya Ujerumani katika milima ya Alps kimeharibika. Lakini Bwana Cazeneuve anasema kuwa kifaa hicho bado kitatoa taarifa kwa watalamu wanaojaribu kubaini kilicho sababisha kuanguka kwa ndege hiyo, ambayo iliwauwa abiria wote 150 na wahudumu waliokuwemo kwenye ndege hiyo. Shughuli za utafutaji wa ndege hiyo zimerejelewa baada ya usiku kumalizika. Ndege za helikopta zinaonekana zikipaa katika maeneo hayo huku maafisa wa polisi wakiendelea kuchunguza mabaki ya ndege . Maafisa wakuu wanaonya kuwa kupata mabaki ya miili ya abiria itachukua muda mrefu kutokana na hali mbaya ya anga katika eneo hilo. Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Barcelona na kuelekea mji wa Duesseldorf. Kansela wa Ujerumani pamoja na Rais wa Uhispania na waziri wake mkuu, wanatarajiwa kuzuru eneo la ajali hiyo hii leo Jumatano.

Tuesday, March 24, 2015

NINAPOITAFAKARI CCM NA SERIKALI YAKE NACHANGANYIKIWA KABISA

"Masikio hayawezi kuvuka kichwa, kiongozi wa serikali usiyetaka kuambiwa ukweli na chama nenda kalale, acha kazi." Hii ni kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Nnauye aliyoitoa wakati akikemea ule aliouita uzembe wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. Nape na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana bado wanaendelea kupaza sauti kuwa baadhi ya wateule wa mwenyekiti wao wa chama, Jakaya Kikwete hawaendani na kasi ya kutumikia jamii.Mwaka jana waliibuka na kibwagizo kuwa, serikali yao inayoongozwa na Rais Kikwete ina rundo la mawaziri mizigo, utashi wao ukawa ni kumtaka mwenyekiti awatimue wasikigharimu chama. Wakati kionjo hicho cha mawaziri mizigo kikionekana kupoa, wameibua kingine kinachoitwa waziri mzururaji; wakimaanisha Nyalandu. Wametoa hoja ang'olewe akalale kwa kuwa ameonesha kuishindwa nafasi ya uwaziri. Wamesema wazi kuwa, masikio hayazidi kichwa, tafsiri ni kwamba wanaoingoza serikali ni masikio ya CCM ambacho ndiyo kichwa cha rais hadi katibu tawala. Hapa ndipo ninapoitafakari CCM na serikali yake kiasi cha kuchanganyikiwa. Kwa nini? Nape na Kinana wanaposema karibu kila walikopita wamekutana na migogoro ya ardhi ikiwahusisha wananchi, hifadhi za taifa na kwa upande mwingine wawekezaji na waziri yupoyupo tu; anazurura, kuna kitu cha kutafakari. Najiuliza; Kinana anapomuona mzururaji Rais Kikwete aliyemchagua katika nafasi hiyo ya uwaziri anakuwa wapi, kalala? Nape anapomuona Nyalandu kuwa ameshindwa kutekeleza jukumu lake; Rais Kikwete, kasafiri? Nachanganyikiwa kabisa! Ukifuatilia ziara za Nape na Kinana zinazoitwa za kujenga chama kila walipopita viongozi hao hotuba zao nyingi zimejaa ukosoaji kwa baadhi ya watendaji wa serikali, kwa vinywa vyao wamekiri hadharani kuwa udhaifu huo unakidhoofisha chama chao. Jambo la kujiuliza; hivi kichwa (CCM) na masikio (watendaji) havina ushirikiano ndiyo maana jamii inashuhudia mkanganyiko huo wa kimtazamo? Ikiwa viungo hivi havishirikiani katika utendaji, wananchi wanavigawanyaje ili kinachoonekana dhaifu wakichukie? Tangu lini mchongoma ukazaa machungwa? Kamwe chemchemi ya maji haiwezi kutoa maji matamu na maji machungu. Naomba nisikilizwe hoja zangu kwa makini.CCM ya Nape na Kinana, mwenyekiti wake ni Rais Kikwete ambaye ni mkuu wa uteuzi wa karibu nafasi zote nyeti za nchi hii, nafasi hizohizo ndizo zinazopigiwa kelele na wasafisha chama kuwa ni dhaifu ki-utendaji! Kwa nini tusifike mbali zaidi ya fikra hizo, tuvuke mipaka ya ufahamu mpaka tuusogelee ukweli kuwa anayewaangusha siyo Nyalandu na uzururaji wake bali aliyemteua ambaye ni mwenyekiti wa CCM. Nashangaa kuaminishwa kuwa chama kinaweza kuwa mtetezi wa wanyonge kwa kiwango wanachoonesha akina Kinana, kuipita serikali ambayo inaongozwa na mwenyekiti wa Kinana. Hivi mashauriano ya chama kifanye nini hawa akina Nape wanayafanyia nyumbani kwao au ofisini? Wanajipangia watakavyo au vikao vya chama na ridhaa ya viongozi wa ngazi za juu akiwemo mwenyeti ndiyo vinavyotoa baraka ya ziara na kupokea mrejesho wa kilichofanywa na watumwaji! Ikiwa chama kinaongozwa kwa mfumo, iweje rais ambaye ni mwenyekiti asijue kuwa, Nyalandu ni mzururaji na kumtimua kazi mara moja! Waliitwa mawaziri mizigo wakaendelea kudunda kwenye nafasi zao; Nyalandu kaambiwa aache kazi lakini bado anapanda ndege na kulipwa mshahara unaotokana na kodi za wananchi. Naomba Nape awaambie wananchi wafanye nini ili watenganishe kichwa na masikio kwa sababu wamechoshwa na umaskini. Asipofanya hivyo ipo siku wataamua kukata shingo, wakiondoe kichwa pamoja na masikio yake kisha wavitupe jalalani! Nachochea tu.CHANZO: GLOBAL PUBLISHER

David Cameron: Awamu mbili zatosha!!

Waziri mkuu wa Uingereza, hataendelea tena na wadhfa wake huo, iwapo atarudi madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei. David Cameron, ameiambia BBC kuwa, anadhani awamu ya tatu inaweza kuwa ni kipindi kirefu kwake kukaa madarakani na kiongozi mpya ni vizuri kuchaguliwa. Chama kikuu cha upinzani cha Leba kimemshutumu Bwana Cameron kwa kuonyesha uzembe na kushinikiza muhula wa tatu, kwa chama chake cha Conservative, hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao.

Ndege ya Ujerumani yaanguka nchini Ufaransa

Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa. Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.

Friday, March 20, 2015

Christian Love and Dialogue Can Influence Middle East Crisis

Rampant religious fanaticism in the Middle East calls Lutherans and other Christians to secure a shared future for all through love and dialogue, said Bishop Dr Munib A. Younan, President of The Lutheran World Federation (LWF). Younan made these remarks on 19 March, when he delivered a public lecture on “Reformation and Politics” at the Near East School of Theology (NEST) in Beirut, Lebanon. The bishop of the Evangelical Lutheran Church in Jordan and the Holy Land (ELCJHL) emphasized that Lutherans don’t seek to “Christianize” politics but to improve society through engagement. “Although Christians are numerical minorities in the Middle East, we can have tremendous influence to utilize for the benefit of all persons and communities in our region,” Younan said in his paper focusing on “Lutheran Contributions to the Political Life of the Middle East.” He was responding to a presentation by Rev. Dr Margot Kässmann, the Evangelical Church in Germany (EKD) special envoy for the 2017 Reformation Jubilee. “Constitutional development is a central concern for the rebuilding of the Middle East. In that process, Arab Christians emphasize commitment to equal citizenship with equal rights and equal responsibilities,” Younan said. The LWF president said Lutherans should know that Martin Luther, who triggered the Protestant Reformation 500 years ago, would find the suffering being endured by the people of Iraq and Syria reason to involve himself in such a crisis. Luther would question the false distinction between religion and politics, promote interfaith engagement, address the Israeli-Palestinian conflict as a factor contributing to the current religiously-sanctioned fanaticism and promote moderation, the bishop noted. “As a leader from a minority movement himself, Luther would no doubt understand us when we say that our danger is not in living with the ‘Other’ but when fanatics seek to persecute us,” Younan said in his address. He pointed to the historic document From Conflict to Communion: Lutheran-Catholic Common Commemoration of the Reformation in 2017 to illustrate Lutheran ecumenical accountability, which emphasizes unity, transformation, the power of Jesus Christ and joint witness. “Together, we show that the church of Jesus Christ is indeed always engaged in reform and renewal,” he said. The waves of violence that have overtaken the Middle East have disproportionately affected the small Christian communities there, Younan said, adding that all communities are potential victims of the ongoing violence. “Lutheran reflections on the proper authority of church and government can help shape how all communities in the Middle East move forward toward a shared future,” he concluded. The ELCJHL bishop is on the board of NEST, an inter-confessional Protestant institution that trains pastors and other church workers in the Middle East for ministry in the churches and their related organizations.

WORLD COUNCIL OF CHURCHES DELEGATION EXPRESSES SOLIDARITY WITH UKRAINE

A ten-person delegation organized by the World Council of Churches (WCC) visited Ukraine from 17 to 20 March, reporting that “the delegation has heard a consistent call for the World Council of Churches and the ecumenical movement to inform the international community about the situation in Ukraine, to promote a more adequate humanitarian response to the human suffering resulting from the conflict, and to support and strengthen the efforts of the churches and faith communities of Ukraine for justice and peace.” According to a WCC communiqué issued on 20 March, “Delegation members had the opportunity to visit a displaced persons’ shelter in Kiev and were able to encounter people who had been obliged to flee from the fighting. Delegation members were also able to travel close to the conflict zone, near Lisichansk, and to witness for themselves the destruction and disruption resulting from the crisis. The delegation also heard of the central role being played by churches in providing humanitarian aid in the affected regions, though the unmet needs still remain very great.” The visit was facilitated by the WCC member church in Ukraine, the Ukrainian Orthodox Church (Moscow Patriarchate). The delegation met with representatives of the Ukrainian Orthodox Church (UOC) and the All Ukrainian Council of Churches and Religious Organizations (AUCCRO), a group encompassing almost every church tradition in Ukraine as well as the Muslim and Jewish communities The communiqué describes the UOC as “the majority church in Ukraine – with congregations in all parts of the country and on both sides of the line of conflict”. It has “officially declared and reiterated its commitment to the territorial integrity and unity of Ukraine”. Members of the delegation included WCC general secretary Rev. Dr Olav Fykse Tveit; Conference of European Churches president Bishop Christopher Hill; the WCC president for Europe, Archbishop emeritus Anders Wejryd; Moderator of the General Synod of the Protestant Church in the Netherlands, Rev. Karin van den Broeke; and a vice-moderator of the WCC central committee, Metropolitan Gennadios of Sassima

Ujumbe wa WhatsApp wasababisha talaka

Mwanamume mmoja nchini Saudia amempa talaka mkewe kutokana na ujumbe wake katika mtandao wa WhatsApp. Kulingana na gazeti moja la kiharibu Al Hayat, mwanamume huyo amedai kwamba mkewe aliandika ujumbe unaosema ''naomba kuwa na subra ya kutosha ili kuweza kuishi na wewe''. ''Nilimpigia mmoja ya ndugu zangu kumuuliza iwapo ujumbe ule ulikuwa unanilenga mimi'', alisema mwanamume huyo.Watu wa Familia yangu walithibitisha hilo na nilisikia aibu kubwa kwamba mabibi za marafiki zangu pamoja na watu wa familia yangu wanaona ninaaibishwa.Hata sielewi alikuwa akimaanisha nini''.Amesema kuwa ndo yake ilikuwa taabani na kwamba kitendo hicho hakikustahili kufanyika.Si mara ya kwanza amenichafulia jina katika mtandao wa kijamii.Niliamua kumpa talaka kabla ya kuyatamgaza maisha yangu katika mitandao ya kijamii.'', Khalid Al Habibi ,naibu mkurugenzi wa kituo cha kijamii kinachojihusisha na watoto mayatima anasema kuwa mitandao ya kijamii ni chanzo kikuu cha talaka.

Kenya na Uingereza kukabili ugaidi

Uingereza imesema itasaidiana na Kenya katika kukabiliana na makundi ya kigaidi ili kuboresha amani kama njia bora ya kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond amesema hayo baada ya Kenya na Uingereza kutia saini mkataba wa maelewano baina ya mashirika ya biashara na viwanda vya nchi hizo mbili. Hamond amesema ukosefu wa usalama unatishia kuvuruga biashara kati ya nchi hizo mbili. Wafanyabiashara wa Uingreza na Kenya wamepongeza kutiwa saini kwa mkataba wa kibiashara kati ya nchi zao. Hafla hii iliongozwa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond na mwenzake wa Kenya Amina Mohamed. Ijapokuwa utawala wa Uingereza kwa siku nyingi walikuwa wamejitenga na mahusiano ya moja kwa moja na serikali ya rais Kenyatta, punde baada ya kuchaguliwa kwake mwaka 2013 kutokana na tuhuma za kuhusika na mauaji yaliyoikumba Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007. Kuwasili kwa Hamond nchini Kenya kuliashiria kuwa Uingereza imeanza kuukubali utawala wa Rais Kenyatta. Bwana Hamond alisisitiza kuwa biashara itafanikiwa tu chini ya mazingra bora ya usalama. '' Tunafahamu vyema kuwa kwenye amani kuna mawasiliano na ushirikiano na pia biashara baina ya watu''alisema Hammond Zaidi ya raia elfu ishirini na tano wa Uingereza wanajihusisha na shughuli mbalimbali za kikazi na kibiashara nchini Kenya. Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Kenya balozi Amina Mohamed alisema kuwa hatua ya Uingereza kuwapiga marufuku raia wao kuzuru Kenya kutokana na msururu wa mashambulizi ya kigaidi kumeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii. Hatua hiyo ilisababisha mikahawa mingi kufungwa na wafanyakazi wengi wa hotelini walipoteza ajira kutokana na uhaba wa wageni. ''Kinachotuuma kwa hakika ni hatua ya serikali ya Uingereza kuendelea kutoa onyo kwa raia wake wasiingie Kenya ilhali hivi vita dhidi ya Ugaidi sio vyetu pekee'' alisema Amina. Vivyo hivyo suala la Kenya kuandikisha mkataba mpya na Uingereza mkataba utakaowaruhusu wanajeshi wa Uingereza kuendelea kufanya mazoezi nchini Kenya lilijipenyeza katika ajenda. Balozi Amin Mohamed amesema '' mashauriano yanaendelea lakini uamuzi utakaochukuliwa utazingatia katiba ya Kenya na sheria za Uingereza''. Hammond pia alikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kujadili masuala ya ushirikiano wa kibiashara na kidiplomasia kati ya Kenya na Uingereza. Kabla na baada ya uchaguzi wa mwaka 2013 Serikali ya Uingereza ilikuwa imejitenga na Kenya wakati huo kesi ya jinai ikimkabli rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu, ICC. Lakini Uingereza sasa imelegeza msimamo baada ya kesi iliyokuwa ikimkabili Rais Kenyatta kutupiliwa mbali kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi hiyo.

USA:Netanyahu amekiuka mpango wa amani

Msemaji wa serikali ya Marekani, Josh Earnest, amesema waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekiuka dhamira yake ya awali ya kuundwa kwa mataifa mawili kama suluhu ya mgogoro wa Israel na Palestina mwanzoni mwa wiki hii, na kwamba Marekani inautathmini msimamo wake upya. Matamshi ya waziri mkuu huyo wa Israel ya kutotaka kuwepo kwa taifa la Palestina yanaonekana na wengi kama ndio yaliyomsaidia kushinda katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne. Netanyahu amekiambia kituo cha televisheni cha Marekani, MSNBC, kwamba bado anabaki na dhamira ya kuundwa kwa taifa la Wapalestina, huku akikana taarifa za kubadili msimamo katika sera yake. Bwana Netanyahu ameiambia MSNBC kwamba anataka Marekani na Israel kuendelea kuwa washirika wakubwa:

Mancity kumtema Yaya Toure na wengine

Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City watamuuza Yaya Toure msimu huu katika mpango unaolenga kuwauza wachezaji wengine wa kilabu hiyo kwa lengo la kununua wachezaji chipukizi watakaoongozwa na mchezaji Kevin De Bruyn wa Wolfsburg. Kushindwa kwa kilabu hiyo na Barcelona katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya kumethibitisha kwamba mabadiliko makubwa yanahitajika katika kilabu hiyo. Katika wachezaji kumi na moja walioanzishwa katika mechi dhidi ya Barcelona ni Sergio Aguerro mwenye umri wa maka 26 aliye chini ya umri wa miaka 27. Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet Kompany,Fernandinho na David Silva wakiwa na maisha marefu katika kilabu hiyo ,waliosalia huenda wakauzwa. Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary Sagna,Martin Demichelis,Alkesandar Kolarov ,Samir Nasri na James Milner ambaye kandarasi yake inaisha hatma yao haijulikani. Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumatano usiku,Gale Clichy,Pablo Zabaleta,Jesus Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin Dzeko huenda pia wakauzwa. Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili kujiunga na kilabu ya New York City nchini Marekani.

J Goodluck:Tutalimaliza Boko Haram

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema ana matumaini kwamba katika muda wa mwezi mmoja kundi la wapiganaji wa kiislamu Boko Haram halitodhibiti sehemu yoyote. Wanamgambo hao waliokiri ushirikiano na kundi la Islamic State liliziteka sehemu kubwa ya eneo la kaskazini mashriki mwa Nigeria. Lakini operesheni ya kieneo imesadia serikali kudhibiti miji na vijiji kadhaa. Rais Jonathan anayewania kuchaguliwa tena katika siku nane zijazo ametetea jitihada zake za kukabiliana na ukosefu wa usalama na amesema anaamini atashinda katika uchaguzi huo. Kiongozi huyo amesema Boko Haram linazidi kuwa dhaifu na litasamabaratishwa. Ameeleza kwamba silaha mpya ilizopata nchi hihyo pamoja na ushirikiano na nchi jirani zimesaidia kuwasukuma wanamgambo hao nje ya miji na vijiji. Alipoulizwa ni wapi walikokimbilia, alieleza kwamba wakati wengi wamemiminika katika mipaka ya nchi hiyo, anadhani wengine wamekimbilia katika msitu wa Sambisa ulio ngome yao kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Thursday, March 19, 2015

Tanzania yapitisha muswada wa ajira

Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa mwaka 2014 ,ambapo pamoja na mambo mengine unaainisha vipengele muhimu vya ajira kwa wageni na wazawa.Hata hivyo bunge hilo limesisitiza serikali kupitia taarifa za waomba ajira wageni ili kubaini uwezo kuhusu ajira wazoomba na mienendo yao kijamii. Sheria hiyo pia inawataka watanzania kuwepo katika ajira zote kutokana na sifa zao.huku wageni wakianishiwa aina ya ajira kulingana na mahitaji ili kuleta ushindani sahihi katika soko la ajira nchini humo. Sheria hiyo inalenga kuvutia waombaji wenye ujuzi kutoka nje kulingana na mahitaji,huku pia ikitoa fursa kwa wazawa.Akichangia muswada huo kabla ya kupitishwa mbunge wa Karatu Yohana natse anaeleza jinsi wazawa wanavyopaswa kunufaika zaidi Gaudensia Kabaka ni waziri wa kazi na ajira wa Tanzania na hapa amesema kuwa vibali vya kazi kwa wageni na suala la uraia kwa mjibu wa sheria hiyo ni mambo ambayo hayataenda pamoja,bali kinachotakiwa ni kutumiza masharti yote mawili. Kupitia muswada huu,bunge limesema kuwa ni moja ya hatua itakayosaidia ajira wa vijana wa Tanzania ambayo baadhi yao wanakosa ajira kutokana na mazingira ya kipaumbele kuwa kwa wageni na si wazawa kama ilivyo katika mataifa mengi duniani ambayo kutoa fursa kwa wenyeji na kisha wageni baadaye.

Alshabaab:US yathibitisha mauaji

Wizara ya ulinzi nchini Marekani imethibitisha kwamba imemuua mojawapo ya viongozi wa kundi la wapiganaji wa Somalia Al Shabaab kupitia kombora. Adan Garaar alituhumiwa kupanga shambulio katika jumba la kibiashara la West Gate nchini Kenya miaka miwili iliyopita. Maafisa nchini Marekani wanasema aliuawa kusini mwa Somalia ijumaa iliyopita. Marekani imekuwa ikikagua operesheni hiyo kabla ya kuthibitisha kwamba Garaar ndiye aliyekuwa akilengwa. Nchi hiyo imewalenga viongozi wengine wakuu katika kundi hilo la wapiganaji wenye itikadi kali za kiislamu kwa mkombora akiwemo kiongozi wa zamani wa kundi hilo, Ahmed Godane.

Usalama:Japan na China kukutana

China na Japan wanafanya mkutano wa kwanza wa kiwango cha juu wa usalama katika muda wa miaka minne. Mkutano huo unaofanyika Tokyo unajumuisha maafisa kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi. Mazungumzo hayo yalisitishwa mnamo mwaka 2011 kutokana na hofu kuhusu visiwa vinavyozozaniwa mashariki mwa bahari ya China. China inasema Japan imeshindwa kuomba msamaha kwa uchokozi wake wakati wa vita vya dunia vya pili. Pande zote zimesisistiza umuhimu wa mazungumzo ya kweli kudumisha amani.

Mapigano makali yashuhudiwa Yemen

Mapigano makali yanashuhudiwa nje na ndani ya uwanja wa ndege katika mji wa Aden nchini Yemen. Taarifa zinasema maafisa wa polisi waaminifu kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Ali Abdullah Saleh, walishambulia sehemu moja ya uwanja wa ndege, lakini wakakabiliwa na makundi ya usalama yanayomuunga mkono rais wa sasa, Abed Rabbo Mansour Hadi. Milipuko kadhaa imetokea katika uwanja huo na abiria waliagizwa kushuka kwenye ndege iliyokuwa inatarajiwa kuondoka kuelekea Cairo. Washambuliaji watatu waliuwawa katika mapigano huku kumu kati yao wakitiwa mbaroni. Aden ni ngome kuu ya rais Abdrabbuh Mansour Hadi, aliyekwepa nyumbani alikokuwa anazuiliwa katika mji mkuu Sanaa baada ya waasi wa madhehebu ya kishia - Houthi kulidhibiti kikamilifu eneo hilo mnamo mwezi Januari.

Wednesday, March 18, 2015

‘Kura ya maoni iko palepale’

SERIKALI imesema haiwezi kubadili msimamo wake kuhusu upigaji wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, licha ya kuwepo maoni ya viongozi wa dini ambao wanataka jambo hilo lisitishwe. Kaimu Kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, Samuel Sitta alisema jana mjini hapa kuwa pamoja na kuwepo kwa tofauti kati ya Jukwaa la Wakristo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, msimamo wa Serikali uko pale pale. Sitta, ambaye anakaimu shughuli za serikali bungeni kutokana na kutokuwepo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema Serikali inakubaliana na maoni ya Kardinali Pengo kuwa waumini waachwe waamue wenyewe kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Alisema kama viongozi wa dini wamegawanyika hakuna namna ya kuwafanya wawe na kauli moja, lakini akasisitiza kuwa jambo la msingi ni kuachwa kwa mtu aamue mwenyewe aina ya kura atakayopiga. Hivi karibuni Pengo alitofautiana na Baraza la Maaskofu (TEC) na Jukwaa la Wakristo ambao wanataka upigaji wa kura ya maoni usitishwe, kwa maelezo kuwa wananchi hawajapewa muda wa kuisoma na kuielewa katiba hiyo na kama Serikali itang’ang’ania ni vyema waumini wa kanisa wapige kura ya hapana. Sitta, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Kutunga Katiba (BMK) alisema Serikali haiwezi kuwakadiria waseme nini au mambo yao yaishe vipi. “Demokrasia yoyote huwa na mawazo ambayo yanatofautiana. Msimamo wa serikali ni ule ule kwamba tutaendelea mpaka kupiga kura ya maoni,” alisema Sitta. Mwanasiasa huyo mkongwe alisema; “Wananchi wataamua wenyewe na wale watakaoona kwamba wameshawishiwa na wakuu wao wa dini kufuata hilo tamko hawawezi kuwazuia na wale watakaoona kuwa hakuna suala la imani ni utashi wa kisiasa nao watakuwa na msimamo wao.” Sitta alisisitiza kuwa ratiba ya Serikali haibadilishwi na tofauti ya kimtizamo kutoka kwa viongozi hao na kwamba Kura ya Maoni itapigwa Aprili 30 kama ilivyopangwa. Mvutano ulioibuka hivi karibuni kati ya Kadinali Pengo na viongozi wengine wa madhehebu ya Kikristo, umeibua mjadala mzito kwenye jamii huku wengine wakieleza kuwa viongozi hao wanawayumbisha wananchi. Kauli ya Pengo imekuja huku tayari tamko ambalo lilitolewa na TEC limesambazwa makanisani na tayari lilishasomwa katika baadhi ya parokia na vigango. Msimamo wa Kadinali Pengo ni kwamba wananchi waisome na waielewe Katiba hiyo, kwani ndiyo wajibu wa msingi ambao Wakristo wanao kwa sasa ili kupiga kura inayostahili wakati ukifika. Kuhusu agizo la waumini kuikataa Katiba Inayopendekezwa, Kadinali Pengo katika maoni yake anaeleza kuwa wao wakiwa viongozi wa watu, hawana mamlaka wala uwezo huo, bali wenye uwezo ni wananchi wenyewe. Hata hivyo, Kadinali Pengo alitaka tamko hilo lisambazwe kwenye parokia na vigango vyote vya Jimbo Kuu la Dar es Salaam ili waumini wasomewe, wauelewe kwanza, ili hatimaye waweze kufanya uamuzi sahihi wakielewa ni nini wanachokitakiwa kukifanya. Jukwaa la Wakristo linaundwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT).

Makamu wa rais wa S Leone afutwa kazi

Rais wa Sierra Leone Ernest Koroma kushoto na makamu wake Sam Sumana Kulia Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo. Siku ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani kumpatia hifadhi ndani ya ubalozi wa Marekani nchini humo akihofia maisha yake. Awali wanajeshi waliizunguka nyumbani yake na kumpokonya silaha mlinzi wake . Kumekuwa na wasiwasi kati ya rais na bwana Sam Sumana. Hivi majuzi aliondolewa katika chama tawala cha All People Congress kwa udanganyifu na kuchochea ghasia. Hatahivyo amekana madai hayo.

Kanisa laidhinisha ndoa za jinsia moja

Kanisa la Presbyterian nchini Marekani ambalo lina takriban wanachama millioni 2 ,limebadilisha sheria yake ya ndoa na kuwajumuisha watu wa jinsia moja. Kanisa hilo ambalo linashirikisha idadi kubwa ya wanachama wake duniani lilitoa tangazo hilo baada ya idadi kubwa ya magavana wa majimbo yake 171 kuidhinisha mabadiliko hayo. Sheria yake mpya sasa itasoma kwamba ndoa ni makubaliano ya kipekee kati ya watu wawili ikilinganishwa na makubaliano kati ya mume na mke. Sheria hiyo ilioidhinishwa na baraza kuu la kanisa hilo mwaka uliopita ilikubaliwa na zaidi ya nusu ya majimbo ya kanisa hilo. Mkutano wa makundi katika jimbo la New Jersy ulikuwa wa 86 kuidhinisha sheria hiyo. Uamuzi huo unatarajiwa kuzua mgawanyiko mkubwa kati ya wanachama wa kanisa hilo ambao wanapinga sheria hiyo. Mwaka uliopita baraza kuu la kanisa hilo lilitoa idhini kwa wachungaji wake kuwafungisha ndoa wapenzi wa jinsia moja katika majimbo ambayo ndoa hizo zinaruhusiwa.

Upinzani wampongeza Netanyahu Israel

Kingozi wa Upinzani nchini Israel Yitzhak Hertzog amempongeza waziri mkuu Netanyahu kwa ushindi wa chama cha Likud Kiongozi wa upinznai nchini Israeli Yitzhak Hertzog amempongeza Benjamin Netanyahu kwa ushindi wake katika uchaguzi wa ubunge nchini humo na kumtakia kila la kheri. Netanyahu anelekekea kushinda nafasi ya kuhudumu kwa mara ya tatu kama waziri mkuu wa Israeli na hatamu yake ya nne kwa jumla. Chama chake cha Likud kimepata ushindi wa asilimia 24 ya kura zilizopigwa dhidi ya asilimia 19 ya chama cha mrengo wa kushoto - Zionist Union. Sasa Netanyahu analenga kuunda serikali thabiti na imara ya mseto na vyama vidogo vya mrengo wa kulia. Katika kampeni yake ya kuwania kuchaguliwa kwa awamu ya tatu alisisitiza kuhusu usalama wa kiatifa wa Israel. Akizungumza na wafuasi wake, bwana Netanyahu amewashukuru kwa jitihada zao za kumuunga mkono.

Tuesday, March 17, 2015

Kenya, Nigeria zagoma kuiazima Tanzania BVR

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amesema ofisi yake ilijaribu kuazima vifaa vya kielektroniki vya Biometric Voters Registration (BVR) katika nchi ya Kenya na Nigeria kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura, lakini nchi hizo zilikataa. Uamuzi wa NEC wa kutaka kuazima vifaa hivyo ni kutokana na mchakato wa uandikishaji kukwama kwenda kama ulivyopangwa kutokana na BVR 250 zilizopo kutokuwa na uwezo wa kuandikisha wapiga kura wote nchini. Kitendo hicho kinaweza kusababisha Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu kushindikana kwani mpaka sasa ni mkoa wa Njombe pekee uandikishaji unaendelea kufanyika ambako utamalizika Aprili 12, 2015. "Tulitaka kuazima Kenya lakini wakasema wanavitumia hata kama wamemaliza uchaguzi lakini mchakato wao wa uandikishaji unaendelea kutokana na kwamba watu wao wanapofikisha umri wa kuandikishwa wanawaingiza katika daftari lao," alisema Jaji Lubuva na kuongeza: "Tulikwenda Nigeria nako walitueleza wanazitumia. Kuazimana siyo jambo geni kwetu na huu ndiyo ukweli wake." Kuhusu mchakato wa uandikishaji mkoani Njombe alikoweka kambi alisema: "Uandikishaji huku unakwenda vizuri licha ya kauli mbalimbali na mimi nimekuwa nikiwahamasisha kujitokeza na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa." Katika uchaguzi wa Ghana uliofanyika mwaka 2013 mfumo wa BVR ulitumika na kuonyesha mafanikio makubwa. Hata hivyo, Malawi iliukataa mfumo huo katika uchaguzi wa mwaka 2014 baada ya kuonyesha udhaifu mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 2005. Katika mahojiano maalumu na viongozi, wahariri na waandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen makao makuu ya kampuni hiyo Tabata Relini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema, NEC ilianza mchakato huo bila vifaa ikitegemea kuazima. "Tulipokwenda Kenya na TCD (Kituo cha Demokrasia Tanzania) kuangalia walivyofanikisha mchakato huo wakatueleza kuwa NEC walikuja hapa kuazima BVR za kuandikisha... tulikuwa na mawaziri pale yaani ilikuwa aibu na walitueleza kama hadi Novemba hamjanunua hamuwezi kuandikisha. Walisema walikuwa na BVR 15,000 Kenya na waliandikisha wapiga kura milioni 14 kwa zaidi ya siku 45 hadi 60, sisi tuna matatizo, matatizo. "Wanatupa wasiwasi mkubwa, ikiwa lengo ni kuandikisha wapiga kura wote haiwezekani tukawa na kura ya maoni Aprili 30, lakini ukiwa unahitaji lazima uandikishe kwanza halafu ufanyike uhakiki wake, lakini muda huo hautoshi? Kauli hiyo ya Profesa Lipumba kuhusu kusimamishwa kwa kura ya maoni pia ilitolewa Februari 12 na viongozi wa vyama 22 vya siasa walipokutana na NEC kujadili mchakato huo wa uandikishaji kwa kutumia BVR. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: "Mchakato huu ni muhimu na kama hautafanyika vizuri tutaichafua nchi yetu. Wadau washirikishwe na waridhike kwani kusipokuwa na uwazi kutaleta shida huko mbele." Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: "Ilitakiwa kutuhusisha katika hili mwanzo hadi mwisho. NEC wanatuonyesha hardware (vifaa vya kompyuta) badala ya software (programu ya kompyuta) zinavyofanya kazi ambayo tuna haja ya kuifahamu. Nani anatuuzia hizo hardware na nani anatuuzia software hizo?" Profesa Lipumba alisema: "Serikali inatakiwa kujikita zaidi katika uandikishaji wapiga kura lakini Serikali haina fedha, bajeti ya Sh144 bilioni haipo sasa itakuwaje tunaingia katika kura ya maoni? Mchakato wa Katiba Kuhusu mchakato wa Taifa kupata Katiba Mpya chini ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, Profesa Lipumba alisema hakuna matumaini hayo na kinachofanyika ni kutaka kuhalalisha utaratibu ambao haukuwa na uhalali kutoka kwa wananchi. Alisema Februari mwaka 2013 wakati Rais Kikwete akizindua Vitambulisho vya Taifa, alisema vitambulisho hivyo vingeweza kutumika pia katika kupiga kura lakini hakuna utaratibu wowote uliotumika kuhakikisha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na NEC wanashirikiana. Profesa Lipumba alisema baadaye Jaji Lubuva alinukuliwa akisema kazi ya uandikishaji itafanywa na tume yake na si mtu yeyote kwani haiwahusu. Alisema bajeti ya mchakato huo ni Sh297 bilioni lakini alipotizama katika kasma ya tume kulikuwa na Sh7.01 bilioni, fedha za maendeleo na fedha za tume hazikuonekana. "Ukienda kuchambua fedha ziko wapi huzioni, mimi nikauliza mbona bajeti ni kubwa lakini haijulikani iko wapi? Hata ukifanya ukaguzi unatakiwa kujua fedha hizo, katika maombi yake Tume iliomba Sh144 bilioni kwa ajili ya Kura ya Maoni lakini nayo haionekani katika vitabu vya Serikali sasa unajiuliza mchakato huo utakwendaje na fedha zimekwenda wapi?" alihoji na kuongeza: "Suala la muda halitekelezeki, awali tume ilisema uandikishaji ungeanza Septemba mwaka jana lakini ilishindwa, Desemba ikifanya majaribio ya uandikishaji na katika Jimbo la Kawe wameandikisha wapiga kura kama 15,000 na ushee katika maeneo ya Bunju na Mbweni. Walisema wamevuka malengo lakini ukienda katika takwimu za Sensa za mwaka 2012 za Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) haziendani. Bunju wapo 51,000 lakini hawa wameandikisha 15,000 wanasema wamevuka lengo sasa hapa kuna ukweli wowote?" "Makambako walisema wataandikisha wapiga kura kama 31,000 lakini kwa Sensa ya mwaka 2012 ina wapiga kura zaidi ya 53,000 sasa utasemaje umevuka lengo na Jaji Lubuva alishatamka kwamba daftari la mwaka 2010 limechakaa hivyo wakisema tutumie daftari hilo haiwezekani."CHANZO:MWANANCHI

Iraq:Kaburi la Saddam limeharibiwa

Wanajeshi wa Iraq na wapiganaji wanaopigana na wanamgambo wa Islamic State karibu na mji wa Tikrti wanasema kuwa kaburi na la rais wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein karibu limeharibiwa kabisa. Aidha zinaonesha picha za Saddam zikiwa zimeondolewa na mahala pake kuwekwa picha za viongozi wa wapiganaji ikiwemo picha ya jenerali wa Iran Qassem Soleimani anayewashauru wapiganaji wanaopigana vita na islamic state. Mwaka uliopita jamii ya wasunni wanaokaa katika eneo hilo liliondoa mwili wa kiongozi huyo wa Iraq ambaye kungolewa kwake madarakani na majeshi ya muungano yaliongozwa na Marekani iliitumbukiza taifa katika vita ambavyo vimechacha hadi leo. Haijulikani hadi wa leo ulizikwa wapi mwili huo. Mwandishi wa BBC nchini Iraq anasema kuwa kuna shauku kuwa huenda wapiganaji wa Shia ndio walioharibu kaburi hilo ilikulipiza kisasi cha mateso waliyopita mikononi mwa kundi la Islamic state na wapiganaji wa Sunni.

Prince Harry kuondoka jeshini Juni

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Harry amesema anaangalia mustakhabali mwingine wa maisha baada ya kuthibitika kuwa ataacha jeshi mwezi Juni. Taarifa kutoka makazi ya kifalme ya Kensington imesema Prince Harry atamaliza utumishi wake wa miaka kumi jeshini baada ya wiki nne kwenda kutumikia katika jeshi la ulinzi la Australia, kuanzia mwezi April. Mrithi wa nne katika mfuatano wa warithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza amesema uzoefu wake jeshini utabakia katika maisha yake yote. Prince Harry amesema bado alikuwa akitafakari ajira yake. Prince Harry ameshiriki mapigano mara mbili nchini Afghanistan, vita vya karibuni kabisa ni pale aliposhiriki mwaka 2012 akiwa rubani wa helikopta ya kijeshi aina ya Apache. Prince Harry ametajwa kuwa rubani aliyetoa msaada mkubwa kwa wapiganaji wa ardhini kwa kuwajali.

Jeshi la Nigeria latwaa mji wa Bama

Jeshi la Nigeria limesema limeurejesha mji wa Bama uliko kaskazini mashariki mwa Nigeria kutoka kwa wapiganaji wa Kiislam wa kundi la Boko Haram. Wapiganaji wa Boko Haram walikuwa wakiudhibiti mji wa Bama, ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno tangu mwezi Septemba mwaka jana. Mike Omeri, msemaji wa Rais Goodluck Jonathan, amethibitisha kuwa majeshi ya Nigeria yaliingia Bama. Alipoulizwa na BBC ni kwa nini imechukua wiki mbili kuutwaa tena mji huo kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge, amesema jeshi lilikosa zana muhimu.

Watu 12 wamenyongwa Pakistan

Pakistan imewanyonga watu kumi na wawili kutoka magereza tofauti kote nchini. Ni idadi kubwa ya mauaji kutekelezwa kwa siku moja tangu serikali iondoe marufuku ya hukumu hiyo kuu mnamo mwezi Desemba. Pakistan imewanyonga takriban watu arobaini tangu kuanza tena kutumika hukumu hiyo kufuatia shambulio la Taliban dhidi ya shule moja huko Peshawar ambapo watoto wapatao 150 waliuawa. Serikali imesema kuwa,asilimia kubwa ya waathiriwa ni watu waliopatikana na hatia ya ugaidi mauaji na makosa mengini kama uhaini. Pakistan imewanyonga takriban watu arobaini tangu kuanza tena kutumika hukumu hiyo Msemaji wa wizara ya waswala ya ndani ,amesema kuwa takriban watu 8000 wamehukumiwa kinyonga nchini humo. Aidha wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanasema kuwa asilimia kubwa ya hukumu hizo haziwezithibitishwa iwapo ilitimiza vigezo vya kimataifa vya haki kwa watuhumiwa.

Sunday, March 15, 2015

Sanamu ya Gandhi yafunuliwa London

Sanamu ya shaba ya mgombea uhuru wa India, Mahatma Gandhi, imefunuliwa rasmi mjini London katika medani ya bunge la Uingereza. Mamia ya watu walihudhuria kutazama sherehe hiyo huku bendi ikipiga muziki wa Kihindi na bendera za India zikipepea. Kwenye sherehe hiyo, Waziri Mkuu, David Cameron alimuelezea Gandhi kuwa kati ya watu mashuhuri kabisa katika historia ya siasa duniani; na alisema sanamu hiyo inampa makaazi ya daima nchini Uingereza. Sanamu hiyo iko kando ya sanamu za viongozi wa zamani kama Winston Churchill, ambaye alipinga harakati za Gandhi kuania uhuru kutoka Uingereza. Gandhi aliuliwa mwaka wa 1948 miezi michache baada ya India kupata uhuru.

TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA, MAHAKAMA YA KADHI NA HALI YA USALAMA NA AMANI YA NCHI.

Sisi Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo Tanzania linaloundwa na Taasisi za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) tuliokutana leo tarehe 10.03.2015, tumepata nafasi y a kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi. Baada ya kutafakari yote hayo, Jukwaa limefikia maazimio yafuatayo: Kuhusu uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi: Suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini kama tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari 16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka mi singi ya Taifa hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini. Pia mjadala unaoendelea unavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Ibara ya 19. Kwa kuendelea kujadili suala hili katika Il ani za Vyama vya Siasa, Majukwaa ya Kisiasa na Bungeni, limeligawa Taifa letu, Serikali, Bunge, Mahakama na wananchi. Mahakama ya Kadhi imekuwa likiendelea kutumiwa na wanasiasa kama mtaji wao wa kujipatia madaraka kwa gharama za kuleta chuki za kidini. Kw a dhamiri safi, Jukwaa linatamka wazi kuwa mjadala unaoendelea kati ya Serikali na vikundi vya kidini kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kikatiba na kisheria ufungwe na badala yake ziachiwe taasisi husika za kidini kuamua juu ya masuala hayo bila kuih usisha serikali wala waumini wa dini nyingine. Kuhusu Katiba inayopendekezwa: Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu; na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe. dha, Katiba In ayopendekezwa haijajibu bado matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali (Muundo wa serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya Rais, uwiano wa mihimili ya dola n.k). Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa ilipit ishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake!!! Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezw aHivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wing i kupiga kura ya HAPANA kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu. Hali ya usalama wa nchi ulivyo sasa: Jukwaa linasikitishwa na viashiria pevu vya ugaidi vilivyoanza kujitokeza nchini kwa takribani miaka mitano iliyopita. Kumekuwa na vitendo vinavyoashiria kuchipuka kwa ugaidi kama vile uvamizi wa vituo vya polisi, kuporwa silaha na mauaji ya polisi, mafunzo ya kareti katika nyumba za Ibada, mafunzo ya itikadi kali za kidini kwa watoto (Kilimanjaro), tukio la Amboni Tanga, mauaji ya v iongozi wa dini (Buselesele, Zanzibar, Arusha), uchomaji wa nyumba za Ibada na kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini. Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino): Jukwaa linasikitishwa na mwendelezo wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (m aalbino) na ukatili unaosababisha ulemavu wa kudumu wa maalbino katika nchi yetu. Hali hii inatishia utulivu, amani na umoja wa kitaifa tuliokuwa nao kama taifa la mfano barani Afrika. Jukwaa linawaasa wananchi kuacha tabia hii ya kuua albino. Jukwaa linaa mini kuwa kukosekana kwa uwajibikaji wa viongozi wa serikali na kuongezeka kwa wigo wa kipato kati ya walionacho na wasionacho kunachangia ongezeko la vitendo hivyo viovu. Jukwaa linajiuliza: mbona tembo na ng’ombe wakiuawa operesheni maalum zinafanyika na viongozi wanawajibika, kwa nini maalbino wakiuawa viongozi hawawajibiki? Kutokana na hayo yote, Jukwaa linatilia shaka dhamira thabiti ya uongozi wa Chama Tawala na Serikali yake katika kuvitokomeza vitendo vya kigaidi, mauaji ya albino na uvunjifu wa am ani unaoendelea hasa kutokana mikakati hafifu na udhaifu mkubwa uliojitokeza wakati wa kuyashughulikia masuala hayo. Kwa kuwa Chama Tawala na Serikali wameshindwa kusimamia misingi iliyolea taifa kama serikali isiyo ya kidini na taifa lenye amani; umoja na utulivu; Jukwaa linawaelekeza waumini wote na wenye mapenzi mema wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao kufanya maamuzi yanayolitanguliza Taifa badala ya kutanguliza mazoea, mapokeo, itikadi na usha biki wa chama fulani cha Siasa. YATOSHA KWA SIKU MAOVU YAKE: MATHA YO 6:34 Imetolewa na: CCT,TEC na CPCT

Kesi ya rais wa Kenya yafungwa rasmi

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta . Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu. Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha. Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo. Mawakili wake walishindwa kuiondoa kesi yake.

Saturday, March 14, 2015

Kesi ya rais wa Kenya yafungwa rasmi

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta . Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu. Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha. Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo. Mawakili wake walishindwa kuiondoa kesi yake.

Kesi ya rais wa Kenya yafungwa rasmi

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta . Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu. Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha. Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo. Mawakili wake walishindwa kuiondoa kesi yake.

Kesi ya rais wa Kenya yafungwa rasmi

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta . Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu. Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha. Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo. Mawakili wake walishindwa kuiondoa kesi yake.

Friday, March 13, 2015

Matokeo ya Mechi za ligi ya Europa

Mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku jana aliisaidia timu yake ya Everton kupata ushindi dhidi ya Dynamo Kiev ya Ukraine wa magoli 2 kwa moja. Matokeo mengine ya mechi za mkondo wa kwanza wa ligi hiyo Villarreal ya Hispania ilishikishwa adabu na ndugu zao Sevilla baada ya kuchapwa jumla ya magoli 3 - 1. Zenit Saint Petersburg ya Urusi wakaiadhibu Torino ya italia kwa magoli 2 kwa 0. Nayo Fiorentina ya italia ikitoka sare ya goli moja kwa moja na AC Roma pia ya Italia. Napoli ya Italia wakawapa kipigo cha mbwa mwizi Dynamo Moscow ya Urusi cha magoli 3 kwa moja. Wolfsburg ya Ujerumani wakawa mwiba mkali kwa Inter Milan ya Italia pale ilipowashindilia magoli 3 kwa 1. Mechi za mkondo wa pili wa ligi ya Europa zitaendelea siku ya Alhamis ya wiki ijayo March 19 mwaka huu.

Mji wa Tikrit wadhibitiwa

Katika mapigano makubwa na makali yanaondelea dhidi ya wanamgombo wa Islamic State, majeshi ya Iraq na yale Shia yamezidi kupata ushindi na kuurudisha tena mji wa Tikrit. Majeshi ya nchi hiyo yamesema imewachukua usiku mzima kupambana katika eneo la kaskazini, mashariki na magharibi kando ya mji, kuingian katikati mwa mji. Kwa mujibu wa ripoti moja, kwa sasa wapiganaji mia moja na hamsini wa kundi la Islamic State wameendelea kuwepo katika mji huo wa Tikrit, ambao ni makao makuu ya jimbo la Salahuddin. Mkuu wa operesheni za kijeshi katika jimbo hilo Luteni Jenerali Abdul-Wahab al Saadi amesema operesheni hiyo itaendelea mpaka wapiganaji hao wa Islamic State watakapoondolewa. ''...Mapambano kuusafisha mji wa Tikrit yanaendelea, tumeanzisha operesheni kadhaa za kijeshi- kiasi cha operesheni tano au sita hivi. Wakati huu tunapozungumza operesheni za kijeshi zinaendelea na zitaendelea mpaka tutakapolikomboa jimbo zima la Salahuddin. Mungu akipenda...'' Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Baghdad, Waziri mkuu wa Iraq, Haider al Abadi, ameelezea kufurahishwa kwake kutokana na majeshi ya nchi hiyo kuendelea kupata ushindi dhidi ya wapiganaji hao wa Islamic State, mjini Tikrit. Ushindi mkubwa tulioupata ni kuunganisha nchi, umoja kwa ajili ya kuushinda ugaidi katika ardhi ya Iraq, kuwashinda wote wanaotaka kuwadhuru watoto wetu, nchi yetu na watu wetu. Huu ni ushindi halisi tulioupata leo...''.

Tuesday, March 10, 2015

Man U yatolewa kombe la FA na Arsenal

Timu ya Arsenal usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA baada ya kuwalaza mahasimu wao Manchester United kwa jumla ya mabao 2 -1. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Danny Welbeck aliyerejea Old Trafford akiwa na Arsenal ndiye aliyepigilia msumari wa moto kwenye kidonda baada ya kupachicha goli la pili lililoipeleka moja kwa moja Arsenal kwenye hatua ya nusu fainali.

DR MTITU ATANGAZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA AMPONGEZA MBUNGE MGIMWA

MVUTANO mkali ubunge jimbo la Kalenga baada ya mpinzani wa Jackson Kiswaga kutoka kata ya Nzihi Msomi Dr Evaristo Mtitu kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Kalenga linaloongozwa na Godfrey Mgimwa (CCM) Akizungumza na wadau mbalimbali Dr. Evaristo Andreas Mtitu alisema kuwa amelazimika kujitokeza kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka huu kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema). Dr Mtitu alisema kuwa yeye ni mzaliwa Kidamali kata ya Nzihi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa alizaliwa mwaka (1974) na kusoma Shule ya msingi Nyamihuu olevel Ulayasi secondary 1995. Alevel Mzumbe high school morogoro 1998, Pia baada ya hapo alijiunga na Stashahada ya ualimu Chuo cha ualimu Morogoro 2001. Shahada ya kwanza ya Elimu, Chuo kikuu DSM, 2006. Shahada ya uzamili katika elimu, Chuo Kikuu cha Charles Darwin, Australia, 2009. Dr Mtitu pia alisema amehitimu Shahada ya uzamivu (Doctor of Philosophy) katika elimu Chuo Kikuu cha VICTORIA cha Wellington, New Zealand, 2014. Akielezea kazi ambazo amepata kufanya katika nchi kuwa ni pamoja na ualimu Shule za sekondari , mkufunzi vyuo vya ualimu Tandala na Klerruu huku kwa sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania aliyebobea katika taaluma ya mitaala ya elimu na ufundishaji, Katika Nyanja ya utandawazi alisema yeye ni mtafiti, elimu ya geography, sera mipango na uongozi katika elimu na nadharia ya upembuzi. Hivyo alisema kuwa lengo lake la kutaka ubunge jimbo la kalenga ni kushirikiana na wana Kalenga katika kuleta maendeleo . Kipaumbele chake ni kuboresha elimu na huduma za afya ,miundo mbinu huku akimpongeza mbunge wa sasa Bw Mgimwa kuwa amejitahidi kufanya kazi kulingana na uwezo wake kwa muda mfupi ila bado kuna haja ya kumuunga mkono kwa kumsaidia zaidi kwa kuliunganisha jimbo hilo na wahisani wa ndani na nje. Kujitokeza kwa Dr Mtitu katika kata hiyo ya Nzihi kutafanya kata moja hiyo kuwa na wagombea wagombea watatu hadi sasa wanaotaka ubunge kutoka kata hiyo .

Mke wa Gbagbo miaka 20 gerezani

Mahakama nchini Ivory Coast imemhukumu aliyekuwa mke wa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani. Simone Gbagbo amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011. Simone Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu mjini The Hague Uholanzi. Katika ghasia hizo watu takriban elfu tatu walifariki dunia.

Sunday, March 8, 2015

Tanzania:'Chinja chinja' alikuwa mlevi

Mohammed Emwazi ,mtu ambaye alibadilika na kuwa ''chinja chinja'' wa kundi la islamic state kwa jina 'jihad John' Mohammed Emwazi, alifurushwa kutoka nchini Tanzania kwa kuwa mlevi na mtu anayetoa matusi.,afisa moja wa polisi ameiambia BBC. Emwazi anasema alitishiwa na kuhojiwa chini ya maagizo ya shirika la upelelezi la Uingereza MI5 alipoenda nchini humo mwaka 2009.

Thursday, March 5, 2015

Balozi wa Marekani ashambuliwa

Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akibwata kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya jumuiya yao. Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi. Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayatarishi maisha yake. Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote . Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi. Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kam hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini Seoul mnamo mwaka 2010. Mkuu wa polisi Yoon Myung na amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine kumhusu . Naye msemaji wa baraza la maridhiano na ushirikiano ambaye alikuwa ndiye muandaaji wa mkutano huo, ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi madhubuti . Balozi Lippert, ni mshauri wa muda mrefu wa Raisi Obama na mambaye pia aliwahi kuwa msaidizi wa katibu mkuu wa ulinzi katika masuala ya mahusiano na bara la Asia,na alipata nafasi ya kuwa balozi Korea Kusini mwezi October mwaka wa jana. Lippert amewahi pia kushika wadhifa wa afisa wa usalama wa taifa katika paresheni maalum na alitwaa medali ya nyota ya shaba nyeusi wakati alipoitembelea Iraq. Korea Kusini na Kaskazini walitengana tangu mwaka 1950-53 baada ya vita vya Korea nab ado kiufundi wako vitani kwakuwa mapigano yalisitishwa kwa suluhu . Marekani na Korea Kusini wameunganisha nguvu za kijeshi na wiki hii wako katika mazoezi kufuatia hali tata ya kiusalama kutoka kwa wakomunisti walioko Kaskazini . Pyongyang wanadai kuwa wana fanya mazoezi kwa kujiweka tayari na uvamizi wowote utakao tokea wakati huo huo Korea Kusini na Marekani wao wanadai kuwa mazoezi yao ni kwa kujihami tu . Marekani inakadiriwa kuwa na vikosi vya askari wake wapatao30,000 vya kudumu vilivyopiga kambi Korea Kusini.

Wanne wahukumiwa kifo mauaji ya Albino jijini Mwanza

Mahakama kuu ya Tanzania Mwanza imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne akiwemo mume wa marehemu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua zawadi Mangidu [22] wa kijiji cha Nyamalulu kata ya Kaseme wilayani Geita. Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Joaquine De-Mello katika ukumbi uliokuwa umefurika wasikilizaji wakiwemo ndugu wa upande wa washtakiwa na baada ya kutolewa hukumu baadhi ya ndugu wa washtakiwa walitokwa na machozi Waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa ni Masalu Kahindi[54]Ndahanya Lumola[42]Singu Nsiyantemi[49]na Nassor Said[47] ambaye alikuwa mume wa marehemu Zawadi Mangindu wote wamepatikana na hatia ya kula njama na kushiriki kumuua zawadi kwa kukusudia ambaye alikuwa mlemavu wa ngozi. Katika hukumu yake Jaji De-mello alisema alikuwa amezingatia kwa makini na tahadhari kubwa katika kufikia uamzi huo baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mashahidi 12 waliitwa na kutoa ushahidi pamoja na ule wa Utetezi na kisha kujiridhisha kuwa pasipo kuacha shaka yoyote washtakiwa walitenda kosa hilo. Aliongeza kuwa katika hukumu zilizotangulia pia zimebainisha kuwa mauaji ya walemavu wa ngozi yamekuwa yanatekelezwa na mtandao mkubwa na siyo rahisi kuubani bila umakini na kuomba katika kesi zijazo pia wanunuzi wa viungo na wagangawanaopiga ramili nao wafikishwe mahakamani kwani uzoefu unaonyesha wauaji hufikishwa mahakamani kwani nao ni wauaji. Huku wasilikizaji wakifuatilia kwa umakini hukumu hiy wakati akiisoma Mheshimwa Jaji De-mello aliisisitiza kuwa Ushahidi uliotolewana Magdalena Shimba mama mzazi wa marehemu na shahidi Semeni [14]waliothibitisha mahakamani kuwaona na kuwatambua washtakiwa wa kwanza na wanne kwenye eneo la tukio pamoja na mazingira yaliyoelezwa mahakamani yanaifanya mahakama pasipo kuacha shaka yoyote. Awali upande wa Mashtaka wakati ukiongozwa na wakili wa serkali Hezron Mwasimba akisaidiana na wakili Janeth Kisibo ulidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa kwa pamoja kwa makusudi walishirikiana kula njama na kutenda kosa la kumuua Zawadi Mangidu[22] aliyekuwa mlemavu wa ngozi hapo Machi 11 mwaka 2008 saa moja usiku katika kijiji cha Nyamalulukata ya Kaseme Wilayani Geita walitenda kosa hilo na pia kumjeruhi mtoto Chausiku aliyekuwa na umri wa miezi 9 wakati huo kwa panga katika mkono wake akiwa mtoto wa mareheu. Upande wa mashtaka uliendelea kudai washtakiwa walikamatwa kwa nyakati tofauti baadaye na taratibu za kisheriazilizingatiwa ikiwemo kupewa nafasi ya kutoa maelezo ya onyo na kutoa Ungamo na baadaye walifikishwa mahakamani ambapo Jamhuri iliwezakuita mashaihdi 12 na kutoa ushahidi hivyo kuiomba mahakama kuu kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili kuwa fundisho kwa watu wengine aina hiyona kuwa ilidaiwa viungo hivyo hutumiwa kuwawezesha watu kupata utajiri ikiwemo wa madini. Hata hivyo wakati wa kesi hiyo malumbano makubwa yalitokea wakati upande wa utetezi ukipinga maelezo ya Ungamo na Onyo kutopokea kama kilelelezo na mahakamawkwa madai wastahkwia walishinikizwa kukiri maelezo hayo hatua iliyomfanya Jaji kuingilia kwa kusema kuwa mazingira ya yaliyochukuliwa maelezo hayo ya ungamo na Onyo yanaashiria washtakiwa hawakulazimishwa hivyo mahakama kuu kuyapokea kama sehemu ya ushahidi. Wakati kesi hiyo ilidaiwa na upande wa mashatka kuwa washtakiwa wanadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 250,000 kati ya shilingi 1,250,000 kutoka kwa wakala wa kununua viungo hivyo baada ya kuvifikisha ilibainika viungo vya marehemuhavikuwa na kiwango cha ubora unaotakiwa hivyo Wakala wao alikataa kumalizi a kaisi cha shilingimilioni 1 kilichokuwa kimebakia ambaye alitajwa mahakamani kwa jina la Hamis Hamad mkazi wa mkoani Shinyanga ambaye hakuweza kupatikana. Ilidaiwa kuwa baada ya mlemavu wa ngozi kuuawa viungo vyake hufanyiwa utambuzi wa ubora wa viungo vyake ambapo wembe,radio na sarafu ya shilingi kumi hutumiwa katika kutambua ubora wake na kiungo kikigusishwa kwenye radio ,radio hukwaruza kwa kupiga kelele na hata kuzima ubora huo ndio unaotakiwa lakini kisipotoa ishara hizo basi kinakuwa hakina kiwango cha ubora unaoatakiwa hakihitajiki. Jaji De-mello alihitimisha kwa kuamru washtakiwa kunyongwa hadi kufa ,..na haki ya kukata rufafa ilkuwa wazi kwao hivyo kuufanya ukumbi mzima kukaa kimya na baada ya kutoka nje ya ukumbi wengi walijitokeza kuunga mkono hukumu hiyo,na imekuja huku kukiwa na tukio la mtoto Yohana bahati naye kuuawa mkoani humo.

B Fasso:Mwili wa Sankara kufukuliwa

Serikali Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara . Watu wa familia ya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani. Mjane wa marehemu Miriam,akizungumza kupitia njia ya simu kutoka Paris amesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji yake. Bwana Sankara aliuawa mnamo mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaore kuchukua mamlaka. Blaise Campaore aling'atuliwa mamlakani katika mapinduzi ya raia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita. Serikali mpya inayoongozwa na Michael Kafando ,imesema kuwa italiangizia swala hilo wakati ilipochukua hatamu. Mwili wa Sankara ulizikwa katika kaburi lisilotambulika katika makaburi yaliopo mashiriki mwa mji wa Ouagadougou.

Wednesday, March 4, 2015

Tiketi za kielektroniki zasitishwa

Serikali ya Tanzania imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki ( kununua kwa kutumia njia za mitandao) kwenye Uwanja wa mkuu wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 3, 2015 hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura, uamuzi huo umetangazwa jana (Machi 3, 2015) jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB. Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu 60,000 na ndio uwanja wa kisasa zaidi uliojengwa na Serikali kwa ubia na watu wa Jamhuri ya China.Ni moja ya viwanja vinavyotumika kwa ajili ua mechi za ligi kuu na za kimataifa. TFF , kwa kushirikiana na moja ya benki kuu nchini Tanzania (CRDB), iliamua kuanzisha mfumo wa kununua tiketi kwa mashabiki kwa njia ya mtandao ili kuepusha usumbufu kwa mashabiki wa soka na pia kuzuia tiketi feki au ulanguzi kutoka kwa wachuuzi wa kawaida. Hata hivyo, zoezi hilo, ambalo lilianzishwa pia katika viwanja vingine tofauti ikiwa kama sehemu ya majaribio, lilipata baadhi ya dosari ndogondogo, kama vile changamoto za mtandao huku baadhi wakilalamika kuwa wanapata usumbufu wanaponunua tiketi ,wakati mwingine aidha kukoseana au kuchelewa kuleta majibu kama muamala umefanikiwa au la.

Jihadi John bado kitendawili

Waandishi wa BBC ndio wa kwanza kukutana na baba wa Mohammed Emwazi, maarufu kwa jina la Jihadi John ambae amekuwa akionekana katika kanda za video Islamic State akiwachinja mateka. Jasem Emwazi amehojia na maafisa wa serikali ya Kuwait ambao wanajaribu kukusanya taarifa za mtoto wake. Mwandishi wetu, Mark Lowen, kutoka Kuwait amekutana na baba ya Mohamed Emwazi Jasem Emwazi hakuonyesha hisia zozote pindi alipoingia ofisi ya wakili wake nchini Kuwait kukutana na waandishi wa BBC ambao ndio wa kwanza tangu mtoto wake alipojitambulisha kama mpiganaji katika picha za video za Islamic State. Akiwa amevaa vazi jeupe, alininyooshea mkono. Nami nikasalimiana nae kwa lugha ya kiarabu na yeye akanijibu, lakini alitoka chumbani muda mfupi tu baada ya kukataa kufanyiwa mahojiano. Wakili wake amesema bwana Emwazi yuko katika hali ya mshtuko na kuongeza kwamba amehojia na maafisa wa serikali ya Kuwait kwa muda wa zaidi masaa mawili na kuachiliwa bila jina lake kutajwa kwamba ni mshukiwa. Mke wake na binti yake hawakuhojiwa, alituambia wakili huyo. Bwana Emwazi alirudi nchini Kuwait kutoka Uingereza mwaka jana mwezi wa Novemba, wakili wake amesema taarifa za vyombo vya habari kwamba amerudi hivi karibuni ni za kupotosha. Ameongeza kusema kwamba bwana Emwazi hafanyi kazi hapa kama taarifa hizo zinavyodai. Alipoulizwa ni lini bwana Emwazi alizungumza na mwanae, au iwapo aliitambua sauti yake katika picha za video, wakili huyo alisema hatapenda kuzungumzia maswala binafsi.

Monday, March 2, 2015

SERIKALI IKO MBIONI KUUGAWA MKOA WA MBEYA

SERIKALI imeyapokea maombi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) cha Mkoa wa Mbeya yanayopendekeza mkoa huo ugawanywe na kupata mikoa miwili ya Mbeya na Songwe. Akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (Jumamosi, Februari 28, 2015) kwenye uwanja wa Saba Saba wilayani Chunya, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema Serikali imeridhia maombi hayo kutokana na ukubwa wa mkoa huo ambao una kilometa za mraba 63,000. "Tumekwishapokea maombi ya kuugawanya mkoa wa Mbeya kwa sababu mkoa huu una eneo la kilometa za mraba 63,617 zilizogawanyika katika Wilaya 8 na Halmashauri 10. Hili ni eneo kubwa sana kiutawala, siyo rahisi kuusimamia na kusukuma maendeleo," alisema. Alisema kamati hiyo imeshauri mkoa huo ugawanywe katika wilaya nne nne ambapo mkoa mpya wa Songwe utakuwa na wilaya za Ileje, Momba, Mbozi na Chunya. Wamekubaliana kuwa makao makuu yatakuwa Mbozi lakini ninyi wa chunya mmeenda mbali zaidi kwa kuigawa Chunya kwenye wilaya mbili za Songwe na Chunya ambapo chunya itaenda Mbeya," alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa. Alisema katika kikao hicho ilikubaliwa kwamba makao makuu ya wilaya mpya ya Songwe yatakuwa Mkwajuni. "Nimekubali maombi haya kwa sababu yatapunguza gharama za uendeshaji, na kama itashindikana kupata wilaya mpya basi itabidi tuwape Halmashauri ya Songwe," alisema. Mkoa wa Mbeya una wilaya nane ambazo zimegawanyika katika tarafa 27, kata 262, vijiji 842 na mitaa 252. Idadi ya wakazi kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni 2,707,410. Akizungumzia kuhusu mpango wa maji katika wilaya hiyo, Waziri Mkuu alisema bado kuna changamoto kubwa ya kufikisha maji vijijini ambako upatikanaji wake uko kwenye asilimia 46. "Tuna mpango wa kuchimba visima vikubwa vitatu na mwakani tuna mpango wa kuchimba visima vingine virefu 11, tunachohitaji ni fedha na usimamizi," alisema. Alivitaja vijiji viyakavyopata visima hivyo ni Makongorosi, Mkwajuni, Kapalala, Isangawana, Galula, Lupa na Matwiga. Vingine ni Kambikatoto, Tanile, Bitimanyanga na Mapogoro. Wakati huohuo, Waziri Mkuu amezindua maabara tatu katika shule ya sekondari ya Saza ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Shanta. Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Chunya, Bi. Sophia Kumbuli alisema ujenzi wa maabara hizo tatu umegharimu sh. Milioni 268.5 vikijumuisha pia ununuzi wa samani, uwekaji wa mfumo wa maji na gesi. "Kati ya hizo sh. Milioni 23.5 ni za ununuzi wa vifaa vya maabara na kemikali na sh. Milioni 245 ni ujenzi wa jengo, samani na uwekaji wa mfumo wa maji na gesi," alisema. Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Mbozi ambapo mbali ya kuzungumza na wananchi, atazindua maabara Vwawa sekondari, atakagua ghala la nafaka la NFRA na kupokea taarifa ya uzalishaji na usambazaji wa miche ya kahawa kwenye kituo cha TACRI – Mbimba.

WAPUUZENI WANAOTUMIA VIBAYA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuna baadhi ya watu wamegeuza mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya kuwa wa kisiasa badala ya kujikita kuwafahamisha wananchi mazuri yaliyomo. Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akiwahutubia wakazi wa Kata ya Lwangwa kwenye Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe akiwa kwenye siku ya nne ya ziara yake mkoani Mbeya kukagua shughuli za maendeleo. "Katiba inayopendekezwa imezingatia maslahi ya kila kundi kwenye jamii hivyo zipuuzeni kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa Katiba hiyo haijakidhi malengo ya Kitaifa," alisema. Alisema mabadiliko yaliyofanywa kwenye Katiba hiyo ni asilimia 20, huku asilimia iliyobakia ni sehemu ya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Jaji Warioba. Alisema ili kukabiliana na kauli za kiupotoshaji, Serikali imeanza kusambaza nakala za Katiba inayopendekezwa hasa kwenye mikoa ya pembezoni. "Jumla ya nakala 300 za Katiba Inayopendekezwa zitasambazwa kwenye kila Kata ambapo makundi yenye uwezo wa kutoa elimu sahihi kuhusiana na Katiba inayopendekezwa yatapatiwa nakala hizo ili kuwaelimisha wananchi," alisema Waziri Mkuu. Wakati huohuo, akiwa Tukuyu mjini, Waziri Mkuu alizindua ofisi za Halmashauri hiyo baada ya jengo la zamani kupata nyufa kutokana na tetemeko la ardhi. Pia alizindua maabara tatu kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya Kayuki. Akingumza na maelfu ya wakazi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Tandale jana jioni, Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha wakazi zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakapoanza. Alisema ni muhimu wananchi watumie fursa hiyo ya kujiandikisha kwa sababu kadi zinazotolewa ndiyo zitatumika kwenye upigaji kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu. "Usipojiandikisha sasa hutaweza kupiga kura kumchagua kiongozi unayemtaka wakati huo ukifika. Hata ukiwa na kitambulisho au barua gani hutaruhusiwa kwa sababu taarifa zako zitakuwa hazimo kwenye daftari la wapigakura." "Hili zoezi limeanza sasa pale Njombe na litafanyika nchini kote, ni vema tukijitokeza kwa wingi na kujiandikisha wakati waandikishaji watakapokuja hapa Tukuyu," alisema Waziri Mkuu. Katika hatua nyingine, Mbunge wa Rungwe Magharibi, Prof. Mwakyusa aliiomba Serikali iingilie kati mradi wa maji wa masoko kutokana na mradi huo kukwama kwa muda mrefu. "Mradi huu umelenga kuwanufaisha wanachi wa vijiji 15, mkataba ulisainiwa tangu 2009 na mradi ulipaswa kukamilika mwaka 2011 lakini hadi leo hakuna hata tone la maji," alisema Prof. Mwakyusa. Aliiomba Serikali pia iingalie barabara ya kutoka Tukuyu hadi Busokelo yenye urefu wa km. 86 kwani ni mkombozi wa mazao mengi yanayozalishwa kwenye Halmashauri ya Busokelo. "Hii barabara ni ahadi ya Mheshimiwa Rais kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami na imeingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi. Kwa vile muda uliobakia ni mfupi, tunaomba iwekewe japo jiwe la msingi ili Rais ajaye akumbuke kuikamilisha," alisema. Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Chunya na kuzindua maabara, kufungua mradi wa maji wa Mbuyuni. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMAPILI, MACHI MOSI, 2015.