Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 24, 2015

Wana CCM Serengeti watua kwa Lowassa

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wamemwomba Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), kuchukua fomu ya kuwania urais muda utakapofika kwani wanaamini ni kiongozi anayefaa kuwania nafasi hiyo kupitia chama hicho. Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Vicent Nyamasagi, viongozi hao walitoa kauli hiyo jana Monduli baada ya kufika nyumbani kwa Lowassa kuwasilisha ombi hilo. Lakini pamoja na viongozi hao kuwasilisha ombi hilo, Lowassa hakutoa jibu la kukubali wala kukataa na badala yake alirejea kauli yake kwa kusema kuwa suala hilo ni kubwa, linahitaji maombi na baraka za Mwenyezi Mungu. “Historia yako inaonyesha ni mtu mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu, mapana na sahihi kwa masilahi ya nchi yetu. “Kwa hakika una sifa zote za kuwa rais wa nchi yetu, tunakuomba muda ukifika chukua fomu, wananchi wana imani kubwa na wewe,” alisema Nyamasagi. Aliongeza kuwa Watanzania wameshuhudia uwezo mkubwa wa Lowassa katika nafasi zote alizowahi kushika na ndiyo maana jina lake sasa ni tumaini pekee la wananchi. Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) wa Wilaya ya Serengeti, Patric Marwa, alisema hakuna kiongozi yeyote ndani ya CCM anayefanana na Lowassa kuweza kushika nafasi hiyo. “Hakuna kiongozi mbadala wa Lowassa kwa sasa, anajua historia ya chama chetu na nchi, katika maisha yake yote ya utumishi amekitumikia chama kwa uadilifu mkubwa,” alisema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, John Ng’oina, alisema wana imani na Lowassa na kuwa atasikia kilio cha Watanzania kumtaka achukue fomu kuwania urais. Hatua hiyo ya viongozi hao imekuja kutokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Februari Mosi mwaka huu ya kutaka wana CCM wenye uwezo washawishiwe wachukue fomu ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi ndani ya CCM. Chanzo:Mtanzania

Wasichana London wajiunga na IS Syria

Uturuki imeshutumu Uingereza kwamba imechukua muda mrefu kuijulisha nchi hiyo kuhusu wanafunzi wa kike watatu waliokuwa wakisoma London Uinger kwamba walisafiri kwenda nchini Syria kwa lengo la kujiunga na Islamic State. Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki. Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State limekuwa limeshtua wengi. Huku serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama ingepewa taarifa mapema Naibu Waziri Mkuu wa Bulent Arinc anatupa lawama moja kwa moja kwa Uingereza kwamba iliichelewa kuijulisha nchi hiyo kabla ya wanafunzi hao hawajaingia katika mji mkuu wa Instanbul. "Tumefuatilia na tumezuia watu wapatao elfu kumi ambao hapo awali waliripotiwa kwetu kutaka kuingia Uturuki kwa tuhuma za kutaka kuendesha shughuli za kigaidi. Tumetimiza wajibu wetu. Kama Serikali ya Uingiereza ingetujulisha mapema maafisa wetu wa usalama wangechukua hatua madhubuti. Tunaamini kuna haja ya kuanganisha nguvu kwa pamoja ili kuratibu na kupambana na ugaidi." Alisema. Wakati kukiwa na taarifa hizo za wanafunzi wa kike waliokuwa wakisoma London Uingereza kuingia nchini Syria kujiunga na Islamic State Nayo serikali ya Ufaransa kwa mara ya kwanza imezikamata hati za kusafiria za raia wapatao sita ambao wanatuhumiwa kwenda nchini Syria kujiunga na wapiganaji hao wa Islamic State. Waziri wa Mambo ya ndani wa ufaransa Benard Cazeneuve amesema kitengo cha ujasusi kinaamini kwamba watu hao walikuwa na mpango wa kusafiri na kwamba swala hilo linahusiana na mambo ya usalama. "Tunaamini hatua hizi zilizochukuliwa zimefanikiwa kwa sababu kama raia wa Ufaransa watakwenda kupigana Iraq na Syria watasababisha hatari kubwa kwa usalama wa taifa wakati watakaporudi. Wanaweza kuendesha vitendo vya kigaidi kwa kiwango kikubwa." Alisema.

Aliyewalawiti Watoto Kenya kuhukumiwa

Raia wa Uingereza aliyewadhalilisha kingono watoto wa kiume katika mji mdogo wa Gilgil nchini Kenya anatarajiwa kuhukumiwa leo Raia wa Uingereza Simon Harris, aliyedhalalisha kingono watoto waliokuwa wakirandaranda mitaani katika mji mdogo wa Gilgil nchini Kenya atahukumiwa leo nchini Uingereza. Hii ni baada ya mahakama ya Birmingham kumpata na hatia ya kudhalalisha kingono watoto wa kiume na kupatikana na picha za utupu za watoto. Harris mwenye umri wa miaka 55 alikuwa akiendesha mradi wa kutoa misaada kwa jamii na alikuawa mtu aliyeheshimika. Hatahivyo alitumia nafasi hiyo kuwashawishi watoto. Kwa takriban miaka 20 alikuwa akitumia gari lake kuzunguka katika mitaa ya Gilgil, nia yake ikiwa kunyemelea watoto wa kiume waliokuwa wakirandaranda mitaani, kwa kisingizio kuwa alijali na kushugulikia maslahi yao. Polisi wanasema waathirika 40 walijitokeza kutoa ushahidi. Hatahivyo ili kufanikisha utaratibu wa mahakama ushahidi wa 11 kati yao ndiyo uliotumika. Waathirika walitoa ushahidi katika mahakama hiyo ya Uingereza kupitia mtambo wa video uliowekwa nchini Kenya. Mjini Gilgil nilikutana na waathirika wawili. Vijana wenye umri wa miaka 30 ambao alimfahamu Harris wakati wakiwa na umri wa miaka 13. Waathirika hao waliomba majina yao halisi kuhifadhiwa na kwahivyo nimewapa majina John na Allan. John anaeleza jinsi alivyomjua Harris, ‘’ nilikua na umri wa miaka 13 wakati nilipokuja hapa mjini na kujiunga na watoto waliokuwa wakiraranda mitaani. Walikuwa wanamfahamu Harris na kila tulipoona gari lake tulimkimbilia, alikua akitubeba na kutupeleka kwake nyumbani’’. Naye Allan anasema umasiki mkubwa uliokuwa ukimwandama yeye na wenzake ulisababisha Haris kuweza kuwashawishi kwa urahisi, ’ kila tulipokwenda nyumbani kwa Harris ,tulijua kwamba tungepata chakula,mavazi mapya na pesa’’. Waathirika hao wawili walikubali kuandamana name hadi alikoishi Harris. Ni safari ya takriban kilomita 8 ,barabara yenyewe ni ya mchanga na mandhari ni ya kichani. Nyumba yake yenye paa la kijani iliyojulikana kama ‘’The green house’’ imesimama imara juu ya mojawapo ya milima modogo ya Gilgil. Eneo lenyewe limejitenga kwa kuwa mashamba ni makubwa na hakuna idadi kubwa ya wakaazi. Huenda mandhari hayo yalimsaidia kuficha yaliyokuwa yakifanyika hapo. Gari lake aina ya Land Rover ambalo alitumia kusafirisha watoto kutoka mjini limefungiwa ndani ya gereji. John na Allan wanasema kuwa makao hayo ni kumbukumbu ya kila mara kuhusu yale waliyopitia. ''Baada ya kula chakula alikuwa akituosha bafuni, anatupatia pombe kisha anaanza kutushikashika kila mahali,asubuhi ukiamka unajikuta umelala naye kitandani’’, anasema John. Kwake Allan hukumu dhidi ya Harris haitoshi, ‘’ ni vizuri atahukumiwa lakini serikali ya Uingereza inapaswa kutulipa fidia sisi waathiriwa kwasababu aliyotutendea yametufanya kutengwa katika jamii, hakuna anayetupenda ni vigumu sana kwetu hata kupata vibarua. Anasema. John anaeleza jinsi jamii imekuwa ikiwachulia, ‘’wanatuchukulia vibaya sana, wengi wanadhani tulikubali kudhalilishwa kwa hiari ili tupate pesa, hawaelewi kwamba tulikuwa watoto wadogo’’. Harris alifanya maouvu hayo wakati akiendesha mradi wa mkutoa misaada kwa jamii ambao alianzisha miaka ya 90. Hatahivyo udhalalisha huo uligunduliwa mwaka 2013 baada ya wanafilamu kutoka Uingereza kuandaa makala iliyoangazia maisha ya watoto waliokuwa wakirandaranda mjini Gilgil. Makala hiyo ilionyesha jinsi malalamishi ya watoto hao yalivyopuuzwa sio tu na wakaazi lakini pia maafisa wa utawala. ‘’ Watoto wa mitaani hawana sauti katika jamii, wanachukuliwa kama wanyama wa porini, hawapendwi na watu. Harris alifahamu hivyo na akatumia nafasi hiyo kuwadhalalisha kingono’’. Waathirika wawili niliozungumza nao waliweza kupata ushauri nasaha na kubadili tabia. Hivi sasa wanafanya kazi za vibarua kila vinapopatikana huku wakiwa na wingi wa matumaini kuwa siku moja jamii itawakubali kikamilifu. Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Uingereza ukasababisha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa Simon nchini Uingereza. Hii ni mara ya kwanza Uingereza kutumia sharia inayowezesha mahakama kufungua mashtaka dhidi ya raia wake kwa tuhuma za udhalalishaji wa kingono katika nchi ya kigeni.

IS yawateka wakristu 90 Syria

Kundi la Islamic State limewateka nyara watu 90 wa jamii ya wakristo kutoka katika kijiji kimoja kazkazini mwa Syria. Kisa hicho cha utekaji nyara kilifanyika mapema leo alfajiri, baada ya wanamgambo hao kuchukua udhibiti wa vijiji kadhaa kutoka kwa walinda usalama wa kabila la Wakurdi. Wanamgambo hao walivamia kituo cha Radio na kuchukua udhibiti wa mawasiliano na kuanza kutangaza Radioni, kuwa wamewateka nyara wale wanaojiita watetezi wa Dini. Kwa muda mrefu kundi la wakristo wachache walioko Nchini humo limekuwa likishirikiana na wapiganaji wa kabila la Wakurdi kukabiliana na wanamgambo wa IS. Awali Kundi la I S limekuwa likiharibu makanisa ya wakristo Nchini Syria. Wakristo hao wa makabila ya Assyria ambao wengi wamo serikalini, wanaiunga mkono utawala wa sasa wa Syria na wamekuwa wakipigana na wanamgambo hao wa Islamic State. Idadi ya Wakristo katika maeneo hayo imepungua kwa kasi mno kutokana na mauwaji dhidi yao.

Monday, February 23, 2015

Miatano waokolewa machimboni S: Afrika

Inakadiriwa kuwa wachimbaji wapatao mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya madini nchini Afrika Kusini. Moto mkubwa uliripuka mapema mwanzoni mwa wiki hii umbali wa zaidi ya kilomita mbili katika machimbo ya mgodi wa Kusasalethu Magharibi mwa mji wa Johannesburg. Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo . Moto huo unasadikiwa ulianza wakati wa kazi ya matengenezo ilipokuwa ikiendelea. Mwaka wa jana mgodi huo ulifungwa kwa muda wa wiki mbili ili kuwaondoa wachimbaji haramu ambao waliuvamia mgodi huo ambao wanshukiwa kuwa wao ndio walioanzisha moto huo.

Saturday, February 21, 2015

SERIKALI KUAJIRI WALIMU 35,000 - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimu zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu nchini. Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye shule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa. Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawana budi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo. Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara Waziri Mkuu alisema: "Mkoa mzima wa Iringa unahitaji kuwa na maabara 318 na zilizo tayari mpaka sasa ni 108. Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa na zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249 zilizokamilika," alisema. "RC inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo bado hazijaanza kujengwa zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alikuwa ameelekeza. Alisema hataongeza tena muda wa ujenzi," aliongeza. Alisema elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu wa kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN). Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe wasikivu ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye masomo yao. Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Afisa Elimu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Leonard Msigwa alisema ujenzi wa nyumba hizo nne ambazo zina pande mbili (four duplex houses) umegharimu sh. milioni 323.2. Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko, zina uwezo wa kubeba familia nane. Bw. Msigwa alisema ujenzi wa nyumba ulifanywa shirika la DESWOS la Ujerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na wananchi. Pia walisaidiwa kujengewa tenki la maji na mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya wasichana. Akifafanua kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Afisa Elimu huyo alisema hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Baiolojia lakini bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Alisema mfumo wa gesi na maji umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara. "Ujenzi wa maabara hadi sasa umekwishagharimu sh. milioni 52.8/- na katika kipindi cha Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya samani za maabara yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya sh. 8,940,000/-," alisema. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU, IJUMAA, FEBRUARI 20, 2015.

Papa atoa Ujumbe wa Kwaresima 2015

WAKATI Kanisa linajiandaa kuanza kipindi cha Kwaresima hapo Februari, 2015, ambapo waamini wanapata mwaliko wa kutubu na kumwongokea Mwenyezi Mungu, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Fransisko ametoa ujumbe wa kipindi hicho unaoongozwa na kauli mbiu “Imarisheni mioyo yenu” kwa kutambua kwamba, kila mtu anapendwa na Mwenyezi Mungu na anamfahamu kila mtu kwa jina na hata pale mwanadamu anapokengeuka, Mungu bado anamtafuta. Baba Mtakatifu Francisko anawapa changamoto waamini kuupokea na kuukumbatia upendo wa Mungu unaowatangulia daima kwa kutambua kwamba, Mwenyezi Mungu ndiye aliyeanza kwanza kumpenda binadamu na anaendelea kuliimarisha pendo lake na kwamba, ni wajibu wa waamini kuhakikisha kwamba, wanawasaidia jirani zao, kwa kuwashirikisha upendo ambao wamejichotea kutoka kwa Mungu na kuwawekea mbele yao, ili kuwahudumia hasa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Baba Mtakatifu anasema katika ujumbe wake wa Kwaresima kwamba, pale ambapo mwanadamu anaishi kwa raha mustarehe, anakuwa na kishawishi cha kuwasahau jirani zake wanaoteseka; katika shida na mahangaiko yao na kwa kutotendewa haki. Katika mazingira kama haya, moyo wa mwanadamu unatumbukia katika hali ya kutoguswa na mahangaiko yao, kishawishi kikuu kinachotoka kwa Shetani ambaye anaendelea kujiinua hadi amepata utambulisho wa kimataifa. Hapa Baba Mtakatifu anazungumzia tabia ya ubinafsi kama utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya wengine. Ni mtu yule tu ambaye aliwezeshwa kusafishwa miguu na Yesu anaweza kuwa ni sehemu yake kwa kushiriki kikamilifu katika kuwahudumia jirani zake. Lakini kwa wale wanaoelemewa na ubinafsi wao, wanajifungia ndani mwao, kiasi cha kushindwa kuwahudumia jirani zao. Wakristo wanapaswa kutambua na kuonja upendo mkamilifu ulioneshwa na Yesu mwenyewe aliyejitaabisha kuinama na kuwaosha mitume wake miguu; ni kielelezo cha pendo kuu ambalo Yesu analionesha kwa umaskini wa binadamu. Kuna haja kwa waamini kujiachilia mikononi mwa Yesu, ili aweze kuwaosha miguu, yaani kuonja upendo wake unaoponya licha ya mapungufu yanayoweza kujitokeza katika kumpenda Kristo. Watu wanaweza kuonja upendo huu, kwa njia ya Kanisa na ndani ya Kanisa Mkristo anaweza kumwachia Mwenyezi Mungu kumvika wema na huruma yake na hivyo kumwezesha kuwa na uwezo wa kuwaosha wengine miguu yao; kwa kujisadaka kwa ajili ya Mungu na binadamu. Baba Mtakatifu Fransisko anawaalika Wakristo kujenga na kudumisha moyo wa upendo na mshikamano wa dhati, ili kuachana na utamaduni usioguswa na shida pamoja na mahangaiko ya watu, kwa kutambua kwamba, wote ni viungo vya Fumbo la mwili huo mmoja, yaani Kanisa. Kila aliye wa Kristo ni sehemu ya Fumbo la Mwili wake, kumbe hapaswi kuwageuzia jirani zake kisogo. Baba Mtakatifu anasema… “na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.” Hii ndiyo dira ambayo Baba Mtakatifu Fransisko anapenda kuionesha katika maisha ya Jumuiya na Parokia mbali mbali. Anauliza maswali ya msingi, ikiwa kama wanajumuiya wanajisikia kuwa ni sehemu ya mwili huo mmoja? Mwili ambao kwa pamoja unapokea na kushirikishana kile ambacho Mwenyezi Mungu amewakirimia katika maisha. Mwili unaotambua na kuwawajibikia, maskini, wanyonge na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Au wote wanajifunika katika “blanketi” la upendo wa juma kwa kujishughulisha na malimwengu kwa kumsahau Lazaro ambaye ameketi pembeni mwa mlango wao uliofungwa? Baba Mtakatifu anawaalika Wakristo kumwilisha upendo katika uhalisia wa maisha yao, kwa kushikamana na Kanisa la mbinguni kwa njia ya sala, ili kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Kanisa linalosafiri hapa duniani na Kanisa la mbinguni; umoja unaojikita katika huduma na mafao ya wengi na kuhitimishwa kwa kumfahamu Mwenyezi Mungu. Kanisa linalosafiri na Kanisa la mbinguni yanashirikiana ili kuhakikisha kwamba, hakuna mtu duniani ambaye anateseka au kuomboleza, ili furaha ya ushindi wa Kristo Mfufuka iweze kufika hata mbinguni kama anavyosema Mtakatifu Theresa wa Lisieux. Kwa upande mwingine anasema Baba Mtakatifu, Kanisa kwa asili ni la Kimissionari na kwamba, linatumwa kwa watu wote na kamwe lisijitafute lenyewe na kwamba, Jumuiya ya Kikristo inachangamotishwa na Mama Kanisa kuhakikisha kwamba, inavuka mahusiano yanayojikita katika jamii inayowazunguka, kwa kuwaangalia maskini na wale walioko mbali zaidi. Jitihada hizi zinapaswa kutekelezwa na kila mwamini mmoja mmoja, kwa kushinda kishawishi cha kuwageuzia wengine kisogo kwa njia ya sala, matendo ya huruma, ili daima mioyo ya waamini iendelee kumwongokea Mwenyezi Mungu ambaye ni mwenye nguvu, mwingi wa huruma, makini na mkarimu, ambaye hawezi kujifungia ndani mwake! Imetafsiriwa na Padri Richard A. Mjigwa, C.PP.S Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatikani.

Friday, February 20, 2015

MAREKANI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUDHIBITI UINGIZAJI WA BIDHAA HARAMU NCHINI.           

kaw1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimsikiliza kwa makini Afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani, Emmanuel Nwankwo (wapili kushoto) katika mkutano wao uliofanyika jijini Washington DC katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Katika mazungumzo yao maafisa hao wa Marekani wanatarajia kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kumuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kaw2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwafafanulia jambo maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani katika mkutano wao uliofanyika jijini Washington DC katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Katika mazungumzo yao maafisa hao wa Marekani wanatarajia kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
kaw3 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (watatu kushoto), na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani. Waziri Chikawe alikutana na Maafisa hao wa Marekani, jijini Washington DC kujadiliana masuala mbalimbali likiwemo la Maafisa hao wakitarajia kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo jijini Washington DC katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI CHIKAWE ATUA NCHINI MAREKANI KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUPAMBANA NA VURUGU NA UGAIDI DUNIANI .

mula1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akikaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakati Waziri huyo alipowasili ubalozini hapo jijini Washington DC kujiandaa kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsalimia Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakati Waziri huyo alipowasili ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo katika Jiji la Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula3Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (katikati) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia) Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo wakati Waziri huyo alipowasili ofisini hapo, jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kulia) akizungumza na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya Waziri huyo kuwasili ubalozini hapo jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula5Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (kushoto) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini humo, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumpokea Waziri huyo aliyewasili jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

For Lent Pope Francis urges faithful: ‘Ask God for gift of tears’


Pope Francis celebrates Ash Wednesday Mass at  Basilica of Santa Sabina in Rome (Photo: CNS)
    
Francis says crying will make Lenten journey 'more authentic and without hypocrisy'
Lent is a journey of purification and penance, a movement that should bring one tearfully back to the loving arms of the merciful Father, Pope Francis has said at an Ash Wednesday Mass.
The Pope celebrated the Mass at the Dominican-run Basilica of Santa Sabina after a procession from the Benedictine monastery of St Anselm. He received ashes on the top of his head from Cardinal Jozef Tomko, titular cardinal of the basilica, and distributed ashes to the Benedictines, the Dominicans, his closest aides and a family of five.
When a priest places ashes on one’s head or forehead, he recited: “Remember that you are dust and to dust you shall return” or “Repent and believe in the Gospel.”
Both, Pope Francis said, are “a reminder of the truth of human existence: We are limited creatures, sinners always in need of repentance and conversion. How important it is to listen and accept these reminders.”

In his homily before the ashes were distributed, the Pope encouraged Catholics to ask God for “the gift of tears in order to make our prayer and our journey of conversion more authentic and without hypocrisy”.
The day’s first reading, Jl 2:12-18, described the Old Testament priests weeping as they prayed that God would spare their people. “It would do us good to ask, do I cry? Does the Pope cry? Do the cardinals? The bishops? Consecrated people? Priests? Do tears come when we pray?”
In the day’s Gospel reading (Mt 6:1-6, 16-18), Jesus warns his disciples three times against showing off the good works they do “like the hypocrites do”.
“When we do something good, almost instinctively the desire is born in us to be esteemed and admired for this good action, to get some satisfaction from it,” the Pope said. But Jesus “calls us to do these things without any ostentation and to trust only in God’s reward”.

Mwandishi aliyefungwa aachiliwa Burundi

   
Waandamana Burundi wakimuunga mkono mwandishi aliyeachiliwa kwa dhamana kwa tuhuma za mauaji
Makumi ya maelfu ya raia wameandamana katika mji mkuu wa Burundi ,Bujumbura wakimuungano mkono mwandishi maarufu ambaye amewachiliwa baada ya kufungwa jela.
Walioshuhudia wanasema kuwa yalikuwa maandamano makubwa kuwahi kufanyika katika mji huo kwa miaka kadhaa.
Bobo Rugurika anayekifanyia kazi kituo cha redio cha African Public Redio aliwachiliwa kwa dhamana.
Alishtakiwa mwezi uliopita kwa kuhusishwa na mauaji ya watawa watatu raia wa Italy baada ya kurusha mahojiano hewani na mtu anayedaiwa kuwa mmoja ya wauaji.
Mahojiano hayo yalihitilafiana na uchunguzi wa polisi kuhusu uhalifu huo na kumtuhumu afisa mmoja mwandamizi.
Kituo hicho cha redio kinaonekana kupendelea upinzani.

Marais wa EAC kukutana Nairobi, Kenya

   
Bendera ya Jumuia ya Afrika Mashariki
Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo mjini Nairobi, Kenya baada ya kutofanyika mkutano wa awali uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi wa Desemba mwaka jana mjini Nairobi.
Marais wote watano wa nchi wanachama wanatarajiwa kuhudhuria.
Katika mkutano huo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuia hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, wadhifa ambao alikuwa akabidhiwe mwezi Desemba mwaka jana, lakini hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kwenda kutibiwa nchini Marekani.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania
Marais wote watano wa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Jakaya Kikwete wa Tanzania na mwenyeji wa mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Mbali na masuala ya uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni mwa mataifa hayo, kujadiliwa katika kikaohicho, pia maombi ya nchi za Sudan Kusini na Somalia kuomba uanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki yatajadiliwa.

Thursday, February 19, 2015

Waziri Pinda : Tutaunganisha nguvu kwa mgombea urais atakayeteuliwa na chama.


IMG_4287
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi wa tarafa ya Pawaga leo.
IMG_4281
Waziri Mkuu Pinda akiwapungia mikono wananchi wa tarafa ya Pawaga leo.
IMG_4280
Wananchi wa tarafa ya Pawaga wakimshangilia Waziri Mkuu Pinda leo.
IMG_4249
Wananchi  wa tarafa ya Pawaga, Iringa wakimsikiiza Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Na Matukiodaima Blog
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewataka watanzania hasa wana Chama wa cha Mapinduzi ( CCM) kuwa na subira katika kumpata mwanachama atakayefaa kusimama kugombea urais kupitia CCM mwaka huu.
Kuwa tayari wengi sana wamejitangaza wazi wazi na wengine wamejitangaza kimya kimya kutaka kugombea Urais na kuwa yote heri ila chama kina utaratibu wake.
 ” Itafika wakati ambao kila chama kitasema huyu ndie mtu wetu ambae atapambana na vyama vingine …tunachosema sisi huyo atakayependekezwa ndie atakuwa mgombea wetu”alisema Waziri Pinda
Waziri Pinda alitoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa tarafa ya Pawaga Baada ya kuzindua skimu ya umwagiliji itakayowanufaisha wakazi wa vijiji vitatu kikiwemo cha Magozi, Ilolompya na Mkombilenga uliogharimu zaidi ya Tsh bilioni 1.6 fedha kutoka kwa wahisani na serikali.
Alisema kuwa utaratibu wa ndani ya chama anbacho wao ni watawala na wanaoendelea kuyafanya maendeleo yanaonekana watalazimika kumuunga mkono atakayeteuliwa na wale wote ambao hawajateuliwa watamuunga mkono atakayeteuliwa kwa makundi yote kuvunjwa na kuwa na Kundi moja pekee.
 Kuwa baada ya mgombea wa chama tawala kupatikana jukumu kubwa ni kuwaomba wapenzi wao wote kumchagua huyo aliyeteuliwa na chama.
Hivyo Waziri Pinda aliwataka wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura.
 Alisema kuwa zoezi hilo ambalo litawahusu wale wote wenye miaka kuanzia 18 na kuendelea linatarajia kuanza mwezi huu katika Mkoa wa Njombe na kuwa kila kata zoezi hilo litadumu kwa muda wa wiki mbili ama tatu .
 “Nawaombeni kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na pia kuipigia kura katiba inayopendekezwa muda ukifika sisi tunaamini ni katiba bora ambayo imegusa makundi yote yakiwemo ya wafugaji na wakulima pamoja na makundi mengine”
Kuwa wapo wapotoshaji ambao watafika na kuwadanganya juu ya katiba hiyo inayopendekezwa na wasiwasikilize.
 Alisema kazi kubwa imefanyika katika kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa mbali ya wao (UKAWA) kutoka nje wakati wa bunge hilo la katiba lakini wajumbe waliobaki walifanya kazi nzuri ya kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa hivyo kuwaomba wananchi kuipigia kura.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Pinda amewataka wakulima wa Mpunga Pawaga katika kuepuka na migogoro kati yao na wafugaji kuweka utaratibu wa kukusanya majani ya Mpunga na kuyapeleka majumbani kwao ili wafugaji wapate kununua kuliko kuyaacha mashambani na kuwafanya wafugaji kuingiza mifugo yao mashambani.

JK amtumia salamu za rambirambi Dkt. Shein kufuatia kifo cha Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Zanzibar.


salmin-awadh
Marehemu  Mh. Salmin Awadh enzi za uhai wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amempelekea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mheshimiwa Salmin Awadh Salmin, Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni katika Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Baraza hilo.
Mheshimiwa Salmin ambaye alikuwa pia Katibu wa Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Baraza la Wawakilishi, amefariki dunia ghafla mchana wa leo, Alhamisi, Februari 19, 2015, wakati akihudhuria kikao cha CCM kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Kisiwandui, mjini Zanzibar.
Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Rais Shein, “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Salmin Awadh Salmin, Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni katika Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Baraza hilo ambaye nimejulishwa ameanguka ghafla wakati akihudhuria kikao mjini Zanzibar.”
“Nimemjua Mheshimiwa Salmin kwa muda mrefu na hakuna shaka kuwa katika miaka 10 iliyopita tokea mwaka 2005 alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia Baraza la Wawakilishi ameliwakilisha vizuri Jimbo lake la Magomeni na watu wake, na ameonyesha uongozi katika Baraza la Wawakilishi na kutoa mchango mkubwa katika Chama chetu cha CCM. Tutaendelea kukosa mchango wake na busara zake za uongozi”, amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Nakutumia Mheshimiwa Rais salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo hiki kikubwa. Aidha kupitia kwako, nawatumia salamu za rambirambi wananchi wa Magomeni ambao wamepoteza Mwakilishi wao na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliopoteza mwenzao na kiongozi wao.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Kupitia kwako,vile vile, natuma pole nyingi sana kwa familia, ndugu na jamaa wa Mheshimiwa Salmin kwa kuondokewa na mhimili mkuu wa familia na mlezi. Wajulishe niko nao katika msiba huu mkubwa na kuwa msiba wao ni msiba wangu pia. Napenda pia uwajulishe kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyeji Mungu aiweke pema roho ya marehemu. Amen.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
19 Februari,2015

Mwili wa marehemu Salmin Awadhi ukipakiwa gari tayari kwa taratibu za mazishi hapo kesho, katika makaburi ya makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja,  mwili wa marehemu unategemewa kuagwa kesho saa tano katika ukumbi wa baraza la wawakilishi Chukwani Unguja na kusaliwa katika Masjid Muhammad kwa mchina na kuzikwa Kijiji kwao Makunduchi Unguja  






Mbunge wa Jimbo la Magomeni Hassan Chombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kifo chake walionana muda mfupi kabla ya kumkuta mauti, amekuwa na majonzi na kustuka na msiba huo. ni pigo kwake.  wakiwa nyumbani kwa ndugu wa marehemu mpendae kunakofanyika maziko hayo hapo kesho saa saba baada ya sala ya Ijumaa masjid Muhammad kwa mchina na kuzikwa makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.

 
PINDA ANZA ZIARA YA MKOA WA IRINGA.       
1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoani Iringa jana
2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma  ya kikundi cha Mangala  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoani Iringa jana.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Iringa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoan Iringa jana.
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua maabara ya Chuo Kukuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa wakati alipotembelea Chuo hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa jana 2015. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mkadala.
6
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akimsikiliza Mtalaamu wa Mifumo ya computer wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Ibrahimu Mwahu wakati alipokagua maabara ya chuo hicho akiwa katika zaiara ya mkoa wa Iringa jana. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa.
7
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa mkoa wa Iringa baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Iringa kwenye ikulu ya Iringa Februari 18, 2015. Kushoto ni Mkuu wamkoa wa Iinga , Amina Masenza. Mheshimiwa Pinda yuko katika ziara ya kikazi mkoani Iringa
8
Badhi ya viongozi wa mkoawa Iringa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao Februari 18, 2015 akiwa katika ziara mkoa wa Iringa jana.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Obasanjo ajiondowa kutoka chama tawala Nigeria cha PDP .

Polisi wakilinda usalama wakati waandamanaji mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria wakipinga kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu, Feb. 7, 2015.
Polisi wakilinda usalama wakati waandamanaji mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria wakipinga kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu, Feb. 7, 2015.
                
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, akumbwa na pigo kubwa wiki sita kabla ya uchaguzi mkuu kufuatia kujiondowa kwa Rais wa zamnani wa Olusegun Obasanjo kutoka chama tawala cha People’s Democratic, PDP.
Bw Obasanjo mkosaowaji mkubwa wa Jonathan hasa kutokana na namna anavyokabiliana na uwasi wa Boko Haram, na ulaji rushwa, alichana kadi yake ya uwanachama hadharani jana alipokua anazungumza na waandishi habari kutangaza uwamuzi wake mbele ya nyumbani kwake.
Katika taarifa iliyochapishwa na vyombo vya habari nchini Nigeria baba wa demokrasia ya nchi hiyo alisema “hivi sasa mimi ni Mnigeria wa kawaida na niko tayari kufanya kazi na yeyote bila ya kujali chama chake cha kisiasa.”
Bw Obasanjo ni mwanasiasa mashuhuri wa kikanda na kimataifa akiwa mmoja wapo wa waanzilishi wa chama tawala cha PDP, na mlezi wa kisiasa wa Johnathan.
 
Rais Goodluck Jonathan.
Rais Goodluck Jonathan.

Kiongozi huyo wa zaamani wa kijeshi aliyeleta mabadiliko ya kidemokrasia nchini mwaka  kwa kuacha uwongozi wa kijeshi na kugombania kiti cha rais 1999 kuleta utawala wa kiraia, alisema  Bila ya Nigeria hapatakuwepo na PDP tena, hivyo kile baadhi yetu tunabidi kutafakarfi ni namna ya kuifanya Nigeria kuwa na nguvu Zaidi.
Msemaji wa PDP Olisa Metuh  amesema chama cha pdp kimesikitishwa sana kutokana na kujiondowa kwa chifu Obasanjo katika wakati huu nyeti baada ya kupatiwa  jukwa la kuitawala nchi kwa miaka minane.
Gavana wa jimbo la Jigawa mwanachama wa PDP ameiambia Sauti ya Amerika
"Rais Obasanjo ni kiongozi wa nigerioa aliyepigania sana umoja wa taifa hili. Rais Goodluck Jonathan ni kama motto wake , aliyemfikisha madarakani. Kwa hivyo wote wawili ni sawa na baba na mtoto na wote wanawajibu ya kulinda nchi yao."
Katika mahojiano na jarida la Finacial Times wiki iliyopita Bw Obasanjo alimunga mkono mpizani mkuu wa Jonathan, Muhammadu buhari wa chama cha upinzani cha All progressive Congress APC, mtawala wa zamani wa kijeshi mnamo miaka 1980 na kuonekana mtu mwenye msimamo mkali zaidi kuhusiana na usalama na kupambana na  rushwa.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema kutokana na msimamo huo wa Obasanjon , chama cha PDP kilikuwa kinajitayarisha kumfukuza kutoka chama , lakini kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 77 alisema alipata habari kutoka vyanzo vyake na hviyo kuamua kujiondowa.
 
Wanajeshi wa NIgeria wapiga doria mjini Abuja
Wanajeshi wa NIgeria wapiga doria mjini Abuja

Jeshi la Nigeria kwenye ukurasa wake wa mtandao unamtuhumu Obasanjo kwa kuhusisha masuala muhimu ya usalama wa kitaifa na masula ya kijeshi katika jukwa la kisiasa.
Na tangu tume ya uchaguzi ya Nigeria kuahirisha uchaguzi mkuu kwa wiki sita hadi mwezi ujao kutyokana na kishinikizo cha jeshi wachambuzi na wananchi wamekuwa wakihoji jukumu la vikosi vya usalama katika kutayarisha uchaguzi.

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014.

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam Februari 13,2015 .Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik ©Ikulu
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Ghalib Bilal;
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda;
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa;
Waziri wa Nchi OWM- TAMISEMI, Mhe.  Hawa A Ghasia;
Naibu Waziri wa Elimu– OWM-TAMISEMI, Mhe. Kasimu Majaliwa;
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Anne Kilango Malecela;
Waheshimiwa Mawaziri wote mlioko hapa,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Said Meck Sadiki;
Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi Ombeni Sefue,
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Naibu Katibu Mkuu –OWM-TAMISEMI;
Katibu Mkuu- OWM-TAMISEMI;
Mabalozi
Wahisani wa Maendeleo;
Wakurugenzi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali;
Walimu, Wanafunzi, Wanahabari,
Mabibi na Mabwana.

Leo ni siku muhimu katika historia ya maendeleo ya elimu nchini.  Tunakutanishwa kwa ajili ya kufanya jambo kubwa, la kihistoria na la kimaendeleo la uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.  Uzinduzi wa Sera mpya unaashiria mwanzo wa ngwe mpya katika safari ya kuimarisha, kuendeleza na kuipaisha elimu nchini kufikia viwango vya juu vya kukidhi ubora na mahitaji ya taifa.  Ni kielelezo cha utashi na azma yetu ya kuboresha mfumo wetu wa elimu uende na wakati na kuiwezesha jamii kuzikabili ipasavyo changamoto na maendeleo na maisha yao.  Maisha bora kwa Mtanzania yanaanzia na kutegemea uwezekano wa kila Mtanzania kupata fursa ya kupata elimu iliyo bora, elimu itakayomuwezesha kutawala mazingira yake na kukabili changamoto za maisha.

         Nakupongeza sana Mheshimiwa Waziri, Dkt. Shukuru Kawambwa,  Katibu Mkuu, Prof. Sifuni Mchome pamoja na wataalamu wenu na wadau wengine wa elimu kwa kuongoza na kusimamia mchakato huu ulioanza kwa kupitia Sera mbalimbali zilizokuwapo katika sekta ya Elimu na kuzihuisha kwa kuandaa Sera hii.  Napenda pia kumtambua Naibu Waziri, Mheshimiwa Anne Malechela Kilango pamoja na upya wake katika Wizara.

Mheshimiwa Waziri;
 Nakushukuru pia kwa uamuzi wenu wa kuzindua Sera hii katika eneo la shule.  Tunapata fursa maridhawa ya kuoanisha kile kilichopo na kile tunachoazimia kutekeleza kwenye Sera.  Nimepata fursa ya kutembelea maabara na kuwaona vijana wetu wanavyopata elimu ya sayansi kwa vitendo.  Aidha, mnanipa nafasi ya kusema na walimu na wanafunzi ambao ndiyo wadau wakuu wa Sera hii ya Elimu.  Ni jambo la faraja kwangu kuona tulipofikia na mafanikio tuliyoyapata, kama haya niliyoyaona katika shule hii.  Inatupa kila aina ya sababu kuongeza bidii na kasi zaidi ya kufikia malengo makubwa zaidi.

         Vilevile, nakushukuru,  Mheshimiwa Waziri, kwa maneno yako ya utangulizi kuhusu Sera hii.  Kama ulivyokwishasema, Sera hii ni matokeo ya mapitio na uhuishaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1966 na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu ya mwaka 1999.  Kipindi cha zaidi ya kipindi cha miaka 14 ya utekelezaji wa sera hizo na maamuzi mengine kuhusu elimu kimekuwa cha mabadiliko mengi ya kijamii, kiuchumi na teknolojia ndani na nje ya nchi.  Uchumi wetu umekua na kutanuka na kuzua mahitaji mapya ya rasilimali watu na stadi mbalimbali ambazo hazikuhitajika siku za nyuma.  Aidha, mipango mitatu ya miaka mitano ya maendeleo kuelekea mwaka 2025 nayo imezaa mahitaji mengine.  Yote haya pamoja na maoni ya wadau mbalimbali yamezingatiwa katika Sera hii ya mwaka 2014.

Hali ya Sekta ya Elimu
Mheshimiwa Waziri;
Ndugu Wadau wa Elimu;
         Elimu ni kitu kinachomgusa na kumhusu kila mtu hapa Tanzania.  Sisi katika Serikali, tunatambua wajibu wetu na nafasi yetu maalum kwa upatikanaji wa elimu nchini.  Kwa ajili hiyo, elimu ni jambo la kipaumbele cha juu, ni la kufa na kupona.  Ukweli wa usemi wangu huo unajihidhirisha katika uwekezaji mkubwa tunaoufanya katika kuendeleza elimu.  Bajeti ya Elimu ndiyo iliyo kubwa kuliko zote kwa miaka mingi  na imekuwa ikiongezeka.  Kwa mfano, mwaka 2005/2006 zilitengwa shilingi bilioni 669.5 wakati mwaka 2014/2015 zimetengwa shilingi trilioni 3.1.  Katika kipindi hicho, bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka kutoka  shilingi bilioni 56.1 hadi shilingi bilioni 345. Kwa sababu hiyo idadi ya wanafunzi wanaofaidika imeongezeka kutoka 16,345 mwaka 2005 hadi 98,000 mwaka 2014.  Shule za msingi zimeongezeka kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,343 mwaka 2014 na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi nayo kukua kutoka milioni 7.54 hadi milioni 8.23.  Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka 531 mwaka 2005 hadi 4,576  mwaka 2014.  Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804.056 mwaka 2014.

Upanuzi huu mkubwa na wa kihistoria  umetokea pia kwenye vyuo vya elimu ya ufundi stadi ambapo vyuo vimeongezeka kutoka 184  hadi 744 kati ya mwaka 2005 na 2014.  Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 50 kati ya mwaka 2005 na 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka 2014.  Leo hii tunapokutana hapa, hatuna tena tatizo na fursa ya kupata elimu kwa elimu ya msingi,  sekondari, ufundi na elimu ya juu.

Mwaka 2005, urari wa wanafunzi kati yetu na wenzetu wa Afrika Mashariki ulikuwa wa chini mno kwa upande wetu.  Kenya walikuwa na wanafunzi wa sekondari 925,341 na wa vyuo vikuu 108,407  ikilinganishwa na Tanzania iliyokuwa na wanafunzi 524,325  wa sekondari na 40,719 wa vyuo vikuu.  Uganda ilikuwa na wanafunzi 728,393 wa sekondari na 124,313 wa vyuo vikuu.  Sasa hali ni tofauti.  Kwa mwaka 2013, kwa mfano, Kenya ilikuwa na wanafunzi wa sekondari 2,104,300 na wanafunzi wa vyuo vikuu 324,600.  Katika mwaka huohuo, Uganda walikuwa na wanafunzi wa sekondari 1,362,739 na wa vyuo vikuu 140,403.  Ongezeko hili linatuweka katika hali nzuri ya ushindani tunapoelekea katika ushindani wa soko la pamoja ndani ya Afrika Mashariki ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.  Jukumu letu ni kuimarisha ubora wa elimu yetu na hasa iwe ni ile inayokidhi mahitaji ya soko la ajira nchini, Afrika Masharini na dunia.
 Juhudi zetu hizi za kuendeleza elimu zimetambulika duniani na kutupatia heshima kubwa zikiwemo tuzo mbalimbali.  Tumekuwa nchi ya kupigiwa mfano katika kutekeleza Malengo ya Milenia (MDGs) yanayohusu fursa ya watoto kupata elimu ya msingi, na usawa wa kijinsi baina ya watoto wa kiume na wa kike kupata elimu ya msingi na sekondari.  Haya na mengine mazuri tuliyofanya ni mambo ya kujivunia.  Ni mafanikio yanayotokana na utekelezaji mzuri wa Sera tatu za elimu ya Msingi, Ufundi na Elimu ya Juu zilizokuwepo.

Ndugu Wadau wa Elimu;
         Mafanikio hayo makubwa nayo yamezua changamoto mpya mbalimbali.  Miongoni mwake ipo ile ya malengo ya Elimu kuwa sawa na goli linalohama kila unapolikaribia.  Hali hii haipo hapa nchini kwetu pekee, bali ipo kote duniani.  Nimebahatika kutembelea nchi nyingi na kuona yanayofanyika. Hali kadhalika nimesoma yanayoendelea kwenye nchi mbalimbali kuhusu elimu.  Ukweli ni kwamba hakuna nchi duniani ambayo imemaliza changamoto zote zihusuzo elimu.  Katika kila nchi kuna mjadala unaoendelea kuhusu ubora wa elimu.  Na, sababu ni moja, uboreshaji wa elimu ni jambo endelevu.  Iko hivyo kwa nchi zinazoendelea kama yetu na hata zile zilizoendelea.  Tofauti yetu ipo kwenye aina ya changamoto zilizopo.  Nchi zilizoendelea hazina matatizo yanayozikabili nchi zinazoendelea.

Ni jambo la kutia moyo kuwa tangu uhuru mpaka sasa matatizo mbalimbali yanayoisibu elimu yametambuliwa na kushughulikiwa.  Katika awamu hii ya uongozi wa nchi yetu tumetoa msukumo maalum tena mkubwa katika kutafuta majawabu ya changamoto zinazokabili sekta ya elimu nchini.  Bahati nzuri tumepata mafanikio kwenye nyanja nyingi.  Nimekwishaelezea jinsi idadi ya shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vya ufundi na vyuo vikuu vilivyoongezeka.  Mambo hayo yameongeza sana fursa za elimu nchini.  Hivi leo watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaweza kuwa shule labda wakatae wenyewe au wakatazwe na wazazi au walezi wasioona mbali.  Watoto wote wanaofaulu darasa la saba wana hakika ya kwenda sekondari na vyuo vikuu vina nafasi wazi zinazosubiri wanafunzi wenye sifa kuzijaza.

Kimsingi tunaweza kusema kuwa suala la watoto  na vijana wetu chini kupata fursa ya kupata elimu inayolingana na umri wao siyo tatizo kubwa tena la kutuumiza vichwa.  Hata hivyo, kazi kubwa inayohitajika kuendelea kufanyika ni kuhakikisha kuwa elimu wanayopata watoto na vijana wetu ni bora.  Kwa ajili hiyo, hatuna budi kuendelea kuboresha mazingira ya kutolea elimu.  Walimu wa kutosha wawepo kwa masomo yote.  Tena wawe ni walimu wanaoyamudu vyema masomo wanayofundisha.  Hali kadhalika, huduma za msingi kwa maisha na utendaji kazi wa walimu ziboreshwe pamoja na maslahi yao.

Vifaa vya kufundishia na vile vya kusomea na kujifunzia vipatikane kwa uhakika.  Majengo ya kufundishia na huduma mbalimbali shuleni na vyuoni yawepo ya kutosha tena yaliyo bora.  Pamoja na hayo, mifumo na miundo ya uendeshaji na usimamizi wa elimu nchini iendelee kuboreshwe zaidi na zaidi.

Sera Mpya na Matumaini Mapya

Ndugu Wadau wa Elimu;
         Sera Mpya ya Elimu inatupa mwanzo mpya na matumaini mapya ya kututoa hapa tulipo sasa na kutupeleka mbele kwenye neema na mafanikio makubwa zaidi.  Mahali ambapo nyingi ya changamoto zinazotukabili sasa zitakuwa hazipo ila zitakuwepo zile za kupeleka elimu yetu mbele zaidi.  Sera mpya inatambua umuhimu na nafasi ya elimu kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake.  Sera inatambua kuwa Elimu ni silaha ya ukombozi kwa Watanzania dhidi ya umaskini na madhila yake.  Ni nyenzo ya uhakika ya kutupeleka kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.   Kwa sababu hiyo, Sera inasisitiza umuhimu wa kuendelea kupanua fursa kwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule aende shule.  Sera Mpya inatoa dhima kwa taifa kuanza safari ya kumuwezesha kila mtoto anayeanza darasa la kwanza aweze kupata elimu ya sekondari ya mpaka kidato cha nne.  Hili ni lengo la muda mrefu kwamba elimu ya msingi iwe mpaka kidato cha nne badala ya darasa la saba kama ilivyo sasa.  Hili ni lengo ambalo halitakamilika mara baada ya uzinduzi huu.  Yanahitajika maandalizi makubwa.  Katika kuanza safari ya kuelekea huko, Serikali imeamua kufuta ada ya elimu ya sekondari kuanzia mwaka 2016 ili wale waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wasishindwe kusoma.

         Sera Mpya ya elimu imeweka msisitizo wa pekee kwa kila mtoto kupata elimu ya awali kabla ya kupata elimu ya msingi.  Tumedhamiria pia kuwekeza zaidi katika stadi za Kuandika, Kusoma na Kuhesabu (KKK) katika miaka miwili ya elimu ya msingi.  Azma yetu ni kujenga msingi imara wa elimu kwa wanafunzi nchini ambao hutegemea sana upatikanaji wa stadi hizo.  Watoto wanapoimarishwa vya kutosha kwa upande wa kusoma, kuandika na kuhesabu, aghalabu humudu vyema masomo yao shuleni.  Aidha, itasaidia kurekebisha upungufu uliopo sasa.

Ndugu Wadau wa Elimu;    
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba ili tuweze kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi lazima tuongeze matumizi ya sayansi na teknolojia nchini.  Tunaweza kufanya hivyo tu kwa kuwa na wanasayansi wengi.  Sera hii inasisitiza kuimarishwa kwa muundo na utaratibu wa ufundishaji wa masomo ya Hisabati, Sayansi na Teknolojia katika ngazi zote.  Kazi hii tayari tumekwishaianza na tunaendelea nayo kwa ari na nguvu.  Tumetoa msukumo mkubwa katika ujenzi wa maabara na naamini, Juni, 2015 tutafikia malengo yetu.

Tunapanua mafunzo ya walimu wa sayansi.  Tutakapotekeleza mradi wa matumizi ya computer mashuleni tutakuwa tumepiga hatua kubwa muhimu.  Sera hii imetoa mwongozo kwa changamoto nyingine nyingi muhimu ambazo zimetolewa maoni na wadau mbalimbali.  Kwa mfano, Sera inaelekeza sasa kutumika kwa utaratibu wa kila somo kitabu kimoja kwa shule zote badala ya utaratibu wa awali wa kila shule kuwa na kitabu chake.  Sera inatoa msisitizo kuwa elimu ni huduma na inaelekeza kuwekwa kwa utaratibu utakaodhibiti upangaji wa ada katika shule za binafsi kwa utaratibu wa kuweka ada elekezi (indicative fees) kwa msingi wa gharama halisi kwa mwanafunzi (Student Unit Course).  Hii itatoa ahueni kwa wazazi na walezi na kuwawezesha kumudu gharama za kusomesha watoto wao katika shule za binafsi.

         Suala la ubora wa elimu inayotolewa tumeliwekea mkazo wa kipekee katika sera hii mpya.  Tutaimarisha mfumo wetu wa usimamizi na ukaguzi wa shule zetu kwa lengo la kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa.  Tutajenga uwezo wa Wizara kwa kutenga fedha za kutosha kwa shughuli za ukaguzi, kuajiri wakaguzi wa kutosha na kuwapatia vitendea kazi vya kuwawezesha wakaguzi kufanya kazi zao kwa ufanisi nchi nzima.  Madhali tumeshapata mafanikio ya kutosha kwenye kupanua fursa ya kupata elimu, sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye kusimamia ubora wa elimu inayotolewa.

Wito kwa Wadau

Mheshimiwa Waziri;
Ndugu Wadau wa Elimu;
         Mafanikio yote tuliyoyapata katika Sekta ya Elimu yamepatikana kutokana na ushirikiano wa wadau wote wakiwemo walimu, wazazi, wananchi wetu wote na wadau wa maendeleo.  Mafanikio haya hayana budi kuenziwa na kuendelezwa.  Tunapoanza utekelezaji wa Sera Mpya ya Elimu, hatuna budi kukumbushana tena wajibu wetu na kushirikiana kufikia malengo yetu haya mapya.
         Mdau mkubwa wa kwanza katika elimu ni mzazi na mlezi ambao ndiyo viongozi wa kaya wanazotoka wanafunzi wetu.  Ninyi mnao wajibu wa kipekee wa kuwahamasisha na kuwahimiza watoto wenu kupenda shule kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kuwawezesha kusoma.  Jihusisheni na elimu ya watoto wenu, na jengeni uhusiano na walimu wao katika kufuatilia maendeleo ya watoto wenu.  Wakati mwingine inashangaza sana kuona wazazi na walezi kutojali kujua maendeleo ya watoto wao shuleni.  Hawakagui maendeleo yao, wala hawajihusishi na kamati za elimu za shule za watoto wao na kata wanazoishi.  Njia bora ya kutatua changamoto za elimu za nchi ni kwa kila mmoja wetu kushiriki katika kutatua changamoto zilizoko katika shule iliyoko katika eneo lake analoishi.

         Walimu ni wadau wenye wajibu wa kipekee sana.  Jukumu lao la kuwafumbua macho na kuwaongezea upeo wa ufahamu wa vijana wetu pamoja na kuwandaa kuwa raia wema halina mfano wake.  Halina badala yake.  Mnafanya kazi nzuri lakini mnatakiwa kufanya vizuri zaidi leo na siku za usoni.  Elimu ni kitu chenye unyumbufu mkubwa na mabadiliko mengi na hasa siku hizi.   Lazima muende na wakati.  Ni ninyi waalimu, pengine kuliko watu wengi wengine  mtakaoumba Tanzania ya kesho iliyo bora kupitia elimu mnayowapa wanafunzi.  Ninyi walimu ndiyo wa kutusaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii na nchi yetu.  Nawaomba sana muendelee kujizatiti katika kutambua uzito wa majukumu yenu na kuyatekeleza.  Sisi Serikalini tutaendelea kufanya kila lililo katika uwezo wetu kuboresha maslahi yenu na mazingira yenu ya kazi.

         Nawaomba pia wamiliki wa shule, hususan shule zinazomilikiwa na mashirika ya dini na watu na makampuni binafsi nanyi mtimize ipasavyo wajibu wenu.  Tunatambua na kuthamini mchango wenu mkubwa katika utoaji wa elimu.  Nawaomba mkumbuke kuwa Elimu ni haki ya mtoto hivyo mjiepushe na upendeleo na ubaguzi. Elimu ni huduma, hivyo mtoze ada zinazohimilika.  Aidha, hamna budi kuzingatia mitaala na miongozo inayotolewa na Wizara ya Elimu na Taasisi zake kuhusu elimu.  Serikali inawahakikishia kuwa tutaendelea kuweka mazingira rafiki ya kuwawezesha kutimiza wajibu wenu huo wa kutoa huduma ya elimu.  Ni kwa sababu hiyo tumewatambua katika Sera hii na mmeshirikishwa kwa ukamilifu katika mchakato wote wa kuitunga.  Naomba tuendeleze ushirikiano wetu katika utekelezaji wa Sera hii.

         Sina budi kuwashukuru pia wadau wetu wa maendeleo kwa michango yao muhimu iliyotuwezesha kufikia mafanikio makubwa katika Sekta ya Elimu. Tunapowashukuru, tunawaomba waendelee kushirikiana nasi tunapoianza safari yetu hii ya kutekeleza Sera Mpya ya Elimu.  Utekelezaji wa Sera hii utahitaji rasilimali nyingi na hivyo tutashukuru kupata mchango wao katika kuongezea nguvu jitihada zetu.  Mchango wao utatuwezesha kupata matokeo makubwa kwa haraka.

Hitimisho

Mheshimiwa Waziri;
Ndugu Wadau wa Elimu;
         Ni jambo la faraja kubwa kwangu kwamba, katika kipindi changu cha uongozi kwa ushirikiano wetu tumeweza kupata mafanikio makubwa na ya kujivunia katika kuendeleza Elimu nchini.  Sera hii tunayoizindua leo ni mojawapo ya mafanikio hayo.

         Naamini kuwa tuliyoyafanya yamechangia kwa kiasi kikubwa kuzikomboa kaya nyingi kutokana na kutoa fursa kwa watoto wengi zaidi wa Watanzania kupata elimu ikiwa ni pamoja na watoto wa kike.  Bado tunayo kazi kubwa ya kufanya mbele yetu. Bahati nzuri, tunayatambua na tunaendelea kuyafanya.  Sera ya Elimu tunayoizindua leo inatoa mwongozo na kutupa mwelekeo mzuri wa namna ya kufanya yanayotakiwa kufanyika sasa na miaka 10 ijayo.    Uzinduzi wa Sera hii mpya ya elimu, na yale yaliyomo katika sera hii ni ushahidi tosha wa dhamira yangu na ya wenzetu wote tulioshirikiana kutayarisha sera hii kuona elimu nchini ianzidi kuimarika na kuwa bora zaidi.

         Napenda sasa, kwa heshima na taadhima kubwa kutamka kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 imezinduliwa rasmi.
         Asanteni sana.

Chanzo: Ikulu

LAZARO NYALANDU ALIPOZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI, ARDHI NA MAZINGIRA YA NORWAY .


Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ( katika kati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen (kushoto) wakiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) Kabla ya Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Waziri waWizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway kwenye Mkutano uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen ( kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu baada ya Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27, PAUL MAKONDA NA FREDRICK MWAKALEBELA NDANI .

 
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Wanging'ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging'ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang'ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, FEBRUARI 18, 2015.
 

Obama:Vita ni dhidi ya magaidi si Uislam.

   
Rais Barack Obama wa Marekani
Rais Barack Obama ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi waliouchafua Uislamu.
Bwana Obama amesema ni sharti dunia ikabiliane na itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya imani ya kidini .
Ameyasema hayo katika mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana na makundi ya aina hiyo.
Rais Obama ameeleza kuwa manung'uniko waliyonayo vijana lazima yashughulikiwe ili kuondokana na hisia za makundi yenye misimamo mikali ya kiitikadi.
Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi sitini wanahudhuria mkutano huo ambao umekuja kufuatia mashambulio ya makundi ya Kiislam katika nchi za Denmark, Ufaransa na Australia.
UN YATAKA JUHUDI ZAIDI KUKABILI MAUAJI YA ALBINO.

DSC_0233
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na binti wa miaka 19 ambaye ni mlemavu wa ngozi na kutosikia, Masalu Masuka ambaye anaishi katika kituo cha watoto walemavu cha Buhangija baada ya kukimbia kwao Bariadi kukwepa wauaji wa albino. Binti huyo alijifungua mtoto wake akiwa kituoni hapo bila msaada wa muuguzi.
Na Mwandishi wetu
MRATIBU wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la umoja huo (UNDP), Alvaro Rodriguez amehimiza serikali kuchukua hatua zaidi kukabili mauaji ya watu wenye albinism.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo kufuatia taarifa ya kutekwa na kuuawa kwa binti mwenye albinism wa umri wa mwaka mmoja, Yohana Bahati, alisema pamoja na juhudi zilizopo sasa za kukabili mauaji dhidi ya watu wenye albinism lazima ziongezwe.
Maiti ya Yohana Bahati (1) aliyetekwa Februri 15 mwaka huu imekutwa katika kijiji cha Shilabela Mapinduzi , kilomita chache kutoka nyumbani kwao Ilelema.
Mwili huo umekutwa na polisi katika hifadhi ya Biharamulo jana Februari 17, 2015 majira ya saa 9 alasiri huku ikiwa imenyofolewa miguu na mikono.
Mama yake, Ester Jonas (30) bado hoi hospitalini Bugando akitibiwa majeraha yaliyotokana na mapanga wakati akijaribu kumuokoa mtoto wake.
DSC_0386
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho hivi karibuni mkoani humo.
Aidha dada yake Tabu bahati (3) bado yuko katika ulinzi wa polisi wakati dada yao mkubwa Shida Bahati (12) akiwa kwa ndugu zake kijiji kingine.
Alisema katika taarifa yake kwamba katika kipindi cha miezi miwili Tanzania imeshuhudia kutekwa nyara kwa watoto wawili katika kanda ya ziwa.
Desemba mwaka jana mtoto Pendo alitekwa na kusababisha kizaazaa kikubwa lakini pamoja na juhudi za kumtafuta mtoto huyo mpaka leo hajulikani alipo.
Taarifa hiyo imesema kwamba Umoja wa Mataifa unasikitishwa na vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watoto hao wawili.
Mashambulio dhidi ya watu wenye albinism yanaelezwa kuwa yanasababishwa na imani za kishirikina na kwamba kutoka mwaka 2000 hadi sasa watu wenye albinism 74 wameshauawa.
“ Mashambulizi haya yanaambatana na ukatili mkubwa, na wakati serikali inafanya kila juhudi kukabili tatizo hili, juhudi kubwa zinastahili kufanywa ili kukomesha mauaji na kulinda kundi hilo dogo la watu ambao wako katika hatari kubwa “ inasema sehemu ya taarifa hiyo.
DSC_0351
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma ujumbe unaosema “DREAM BIG” kwenye T-shirt ya mtoto Agnes Kabika mwenye ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho hivi karibuni.
Umoja wa Mataifa umesema kwamba mashambulio dhidi ya albino hayavumiliki, si halali kwa namna yoyote na yanaweza kukomeshwa.
Wakati taifa hili linaelekea katika uchaguzi, yapo madai kuwa maisha ya watu wenye albinism wako katika hatari kubwa.
Mratibu huyo amesema kwamba pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kukabiliana na wimbi hilo la mauaji hayo, Umoja wa Mataifa unataka Mamlaka husika kuhakikisha haki za raia zinalindwa na utawala wa sheria unazingatiwa.
“ Tunataka mwaka 2015 kuwa mwaka ambapo haki za Watanzania wote zitaheshimiwa wakiwemo albino” Taarifa imesisitiza.
Mratibu huyo wa umoja wa Mataifa amesema kwamba amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa na chama cha Maalbino nchini TAS.
Amesema Mkuu huyo wa mkoa alimhakikishia kwamba wanafanya kila linalowezekana kukomesha madhila dhidi ya maalbino, huku TAS ikitaka kuhakikisha kwamba huu ni mwaka wa kukomesha mauaji.
Aidha Mratibu wa The Same Sun (UTSS) nchini, Vicky Ntetema, amemweleza mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa mashaka yake wakati taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu.
RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27.
 
  • Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

 Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

 Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

 Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

 Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

 Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

 Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

 Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).
 
(mwisho)
 
IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

JUMATANO, FEBRUARI 18, 201‎5.