Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, December 31, 2014

Azimio kuhusu Palestina lakataliwa

   
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limekataa azimio lililoandaliwa na Palestina ambalo limewasilishwa na Jordan linalopendekeza kusitishwa kwa mpango wa Israel wa kuyakalia maeneo ya Palestina kwa miaka miaka mitatu.
Jordan iliwasilisha azimio hilo baada ya kukubaliwa na nchi 22 za kiarabu ikiwemo mamlaka ya Palestina.
Kura tisa zilihitajika ili kupitisha azimio hilo lakini azimio hilo lilipigiwa kura nane pekee.
Nchi mbili zilipiga kura ya hapana kupinga azimio hilo ambazo ni Australia na Marekani zilizokataa mpango huo wa mwisho na kusema hautasaidia katika masuala ya usalama wa Israel.
Nchi tano hazikupiga kura ambazo ni Uingereza, Lithuania, Nigeria, Jamuhuri ya Korea na Rwanda, huku Urusi, China, Ufaransa, Argentina, Chad, Chile, Jordan na Luxembourg zikilipigia kura ya ndio azimio hilo.

Monday, December 22, 2014

Dkt. Bilal kuzindua majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Tanzania Jumatatu hii


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania) itakayofanyika kesho Jumatatu, tarehe 22 Disemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
 
Hafla hiyo itafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi – saa 6:00 mchana katika eneo lililopo nyuma ya Jengo la Mawasiliano (Mawasiliano Towers), barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam yalipojengwa majengo hayo. Aidha, majengo haya yapo karibu kabisa na kituo kipya cha daladala cha Ubungo.
 
Majengo yatakayozinduliwa ni Mahakama ya Mafunzo (Teaching Court); Vyumba vya Madarasa (Lecture Theatres); Maktaba (Library); Jengo la Utawala (Administration Block); Mgahawa (Cafeteria); na Nyumba za Watumishi (Staff Quarters).
 
Pamoja na Makamu wa Rais, viongozi wengine watakaohudhuria ni Mawaziri, Majaji, Makatibu Wakuu, Mawakili, Wabunge, Wahadhiri na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria.
 
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania ilianzishwa na Sheria ya Bunge (Sura 425) mwaka 2007 kufuatia jitihada na mapendekezo ya muda ya muda mrefu ya Tume na Kamati mbalimbali zilizofanya utafiti katika sekta ya sheria nchini na kuona umuhimu wa kuwa na chuo cha kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ili kuongeza ujuzi na stadi baada ya kupata mafunzo ya nadharia katika vyuo vikuu.
 
Ujenzi huo wa majengo ya kudumu ya Taasisi umeigharibu Serikali zaidi ya Tshs 16.1 bilioni na ulianza mwezi Oktoba, 2010 na kukamilika mwezi Juni, 2013. Ujenzi ulifanywa na Kampuni ya BECG (Beijing Engineering Construction Group) kutoka China na ulisimamiwa na kampuni ya Co-Architecture yenye makao makuu yake hapa nchini. Kampuni hizi ndizo zilizoshinda zabuni za kazi zao.
 
Wanahabari kutoka vyombo vyote mnakaribishwa katika hafla hiyo.
 
Mwisho.
 
Imetolewa na:
 
Wizara ya Katiba na Sheria
Dar es Salaam
Simu: 022 213 7823
0753214561 / 0658270460
Jumapili, Disemba 21, 2014
JK aongeza miezi sita kukamilisha maabara
Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewaongezea muda wa miezi sita viongozi na wasimamizi wa ujenzi wa maabara katika skuli za sekondari nchini, ili kuwawezesha kukamilisha kazi hiyo ipasavyo.

Aidha alitoa pongezi kwa wananchi wa Tanzania na viongozi kwa kazi kubwa waliyoifanya katika ujenzi wa maabara nchini.

Alisema anachangia shilingi milioni 200 katika Mfuko Maalum wa Dhamana (Endowment Fund For Excellence) wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

Alisema hayo jana wakati alipozungumza na uongozi, wahitimu na wana-jumuiya ya taasisi hiyo, baada ya ametunukiwa shahada ya uzamivu ya heshima (PhD honoris causa) ya taasisi hiyo katika mahafali ya pili yaliyofanyika Tengeru, Arusha.

Alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Mhe.Mohamed Gharib Bilal ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ni chombo cha elimu ambacho hutoa wahitimu wa shahada za uzamili na uzamivu (PhD) tu katika sayansi na teknolojia na ni moja ya taasisi mbili tu za aina hiyo katika bara la Afrika.

Pia alizungumzia maendeleo ya ujenzi wa maabara ya masomo ya sayansi nchini ambalo lengo lake ni kutekeleza agizo lake la kuhakikisha skuli zote za sekondari nchini zinajenga maabara ya kufundishia masomo ya sayansi.


Alitoa agizo hilo miaka miwili iliyopita, Novemba 2012 na akatoa miaka miwili kukamilisha kazi hiyo ifikapo Novemba 30 mwaka 2014.

Alitoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa ukosefu wa maabara kwa ajili ya masomo ya fikizia, kemia na biolojia ilikuwa moja ya sababu ya kuwakatisha tamaa wanafunzi nchini kupenda masomo ya sayansi.

Alisema umuhimu wa kujenga maabara uliongezwa kasi na ongezeko kubwa la skuli za sekondari ambazo ziliongezeka kutoka 828 mwaka 2004 hadi kufikia 3, 551 kwa sasa.

Kati ya hizo ni 88 zilizokuwa na vyumba vitatu kwa ajili ya masomo hayo matatu ya sayansi.
 
Alisema tathmini ya sasa inaonesha kuwa zinatakiwa zijengwe maabara kwenye skuli 3,463 ambazo ni sawa na vyumba 10,389 na kuwa tathmini hiyo inaonesha hadi Disemba 7, 2014, vilikuwa vimejengwa vyumba 3,867 vya maabara ambavyo ni sawa na asilimia 37.2 ya mahitaji ambavyo vimekamilika, vyumba 5,891, sawa na asilimia 56.7 ambavyo viko katika hatua mbali mbali za kukamilishwa na vyumba 631 ama sawa na asilimia 6.1 ambavyo ujenzi wake haujaanza.

MAHAFALI YA 10 CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idriss Ahmada Rai mara baada ya kuwasili katika ya Kampasi ya Chuo Tunguu kufungua Mahfali ya 10 yaliyofanyika chuoni hapo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.]

Baadhi ya walimu katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano katika mahfali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.]

Essebsi ajitangaza kushinda Tunisia

   
Mgombea Urais, akitangaza ushindi nchini Tunisia
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais nchini Tunisia yanaonesha kuwa Beji Caid Essebsi anaongoza kwa zaidi ya asilimia 55 ya kura
Licha ya Kujitangaza mshindi, mpinzani wake ambaye ameshika nafasi ya pili Moncef Marzouki amesema matokeo hayo yanakaribiana mno.
Wakati wafuasi wa Beji Caid Essebsi wakishangilia ushindi, kiongozi wa kampeni ya uchaguzi wa Bwana Essebsi, Mohsen Marzouk, amedai ushindi.
‘’…Kulingana na matokeo ya awali kutoka katika vituo vya kupigia kura tunaweza kusema kuwa Beji Caid Essebsi ameshinda katika duru ya pili...'' Anasema Marzouk.
Hata hivyo wakosoaji wake wanasema, ushindi wa bwana Essebsi ni ishara kurudi tena uongozi usioaminika.
Lakini mwenyewe anasema ni mtendaji ambaye ataimarisha nchi hiyo.
Uchaguzi huo unaonekana kama kilele cha mageuzi ya kisiasa ambayo nchi hiyo imepitia kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyotokea takriban miaka minne iliyopita.

Saturday, December 20, 2014

SERIKALI IMEJIDHATITI KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA MAWASILANO KWA NJIA YA MTANDAO (TEHAMA)

unnamed
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa), jijini Dar es Salaam.
unnamed1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.
unnamed2
Wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLa) wakifuatilia mazungunzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam

unnamed3
Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua wa kwanza kushoto, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) ya namana mikutano inavyofanyika kwa kutumia mtandao katika chumba cha mikutano wakati wa Ziara yake leo jijini dare s Salaam , wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondoleo jijini Dar es Salaam.
Serikali imejidhatiti katika kuboresha huduma za mawasilano kwa Njia ya Mtandao (TEHAMA) ili kurahisisha utendaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali.
Akiongea na wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi kwa watumishi na jamii kwa ujumla kujifunza na kuwasilisha mada mbalimbali kupitia mtandao.
Balozi Sefua amesema kuwa serikali na taasisi zake mbalimbali hazina budi kutumia wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao kufanya shughuli zake zote zinazotekelezeka kwa njia ya Videoconference na Mafunzo ya Masafa ili kupunguza gharama.
"Lengo kuu la Serikali ni kurahisisha mawasilino baina ya watumishi na jamii ili kupunguza usumbufu wa safari ndefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na pia kuokoa muda, na urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi" alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bwana Charles Sekondo, amesema ofisi yake imekuwa ikitekeleza majukumu kwa ufanisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia duniani katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali.
"Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao imerahisisha sana mawasiliano baina ya serikali, wizara, idara , wakala wa Serikali, pamoja na Sekta binafsi katika kuboresha uweledi kiutendaji kupitia utawala bora, anuai za jamii, maswala ya afya na mazingira" alisema Sekondo
Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea maeneo mbalimbali ya ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao ikiwemo Sehumu ya Huduma za Video Conference, Chumba cha Maabara za Kompyuta na kituo cha taarifa za maendeleo (TDCI).
Mtandao wa TaGLA,unajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wa wizara, idara na wakala wa serikali pamoja na sekta binafsi katika nyanja mbalimbali ikiwemo , mafunzo ya midahalo kwa njia ya video ya hapa nchini na nchi nyingine, midahalo kwa njia ya mtandao, mafunzo ya ana kwa ana na mafunzo kwa njia ya uongozi.
Chanzo: Mjengwa blog

Obama:Filamu ya Kim Jong Un ionyeshwe

    
Rais Obama wa marekani ametaka filamu ya ucheshi ya rais wa Korea kazkazini kuonyeshwa
Rais wa marekani Barack Obama ameimbia Korea Kaskazini kuwa Marekani itajibu kisa ambapo wizi wa mtandao ulioendeshwa dhidi kampuni ya filamu ya Sony Pictures hali iliyosababisha kufutiliwa mbali kwa maonyesho ya filamu inayomdhihaki kiongozi wa korea kaskazini kim jong- un.
Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa hatua hiyo haitakuwa rahisi kwa Marekani kutokana na kujitenga kwa Korea kaskazini.
Filamu ya Kumdhihaki rais wa Korea kazkazini Kim Jong Un iliozuiliwa na kampuni ya Sony Pictures kufuatia vitisho
Rais Obama amesema kuwa kampnui ya filamu ya Sony Pictures ilifanya makosa kwa kusitisha kuonyesha filamu hiyo.
Hata hivyo Sony ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwa kuwa kumbi nyingi kubwa za sinema nchini Marekani zilikataa kuonyesha filamu hiyo.
Sony imesema kuwa ina mipango wa kuionyesha filamu hiyo na kwa sasa inatafuta njia zingine za kuionyesha.

Uchaguzi wa masineta wafanyika Liberia

   
Uchaguzi wa msineta umeanza hii leo licha ya kuwa huenda ukasababisha kuenea kwa ugonjwa wa Ebola
Shughuli za upigaji kura zinaendelea nchini Liberia kuwachagua maseneta wapya licha ya kuwepo kwa hofu kwamba kura hiyo huenda ikachangia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.
Uchaguzi huo umehairishwa mara kadha lakini rais Ellen Johnson - Sirleaf anasema kuwa kura hiyo ni lazima ifanyike wakati huu ili kuzuia msukosuko .
Mikutano ya kisiasa ilipigwa marufuku kufuatia hatari iliyotokana na ugonjwa wa ebola ambao umewaua maelfu ya watu magharibi mwa afrika.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi nchini Liberia wanaamini kuwa kura hiyo ni hatari sana na kesi ya kuizuia isifanyike imepelekwa kwenye mahakama ya juu.

Korea kazkazini sasa yaionya Marekani

   
Rais wa Korea Kazkazini Kim Jong un .
Korea Kazkazini sasa inataka uchunguzi wa pamoja na Marekani kufanywa kuhusu wizi wa mtandaoni uliosababisha kampuni ya Sony Pictures kuahirisha maonyesho ya filamu ya ucheshi inayomdhihaki raia wa Korea kazkazini Kim Jong-un.
Imesema kuwa shtuma hizo za shirika la ujasusi nchini marekani FBI kwamba Pyongyang ndio iliotekeleza uovu huo inaliharibia jina taiafa hilo.
Chombo rasmi cha habari nchini humo kilimnukuu waziri wa maswala ya kigeni ambaye jina lake halikutajwa akisema kuwa taifa lake litachukua hatua kali iwapo Marekani itakataa ombi hilo.
Taifa la Korea Kazkazini hapo awali lilikuwa limeunga mkono uvamizi huo wa kampuni ya Sony likisema kuwa ni kitendo cha haki.
Rais Obama amesema kuwa Marekani itajibu shambulizi hilo la mtandaoni wakati utakapowadia.

SERIKALI YAZINDUA RASMI USAMBAZAJI TAKWIMU ZA PATO LA TAIFA, PATO LA MWANACHI LAONGEZEKA.


unnamed
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 leo jijini Dar es salaam.
unnamed1
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servicius Likwelile chapisho la lenye Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam.
Serikali imesema kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2007 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 26.8 ikilinganishwa na trilioni 20.9 za mwaka 2001, ambapo wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi milioni1,186,200/= mwaka 2001 hadi shilingi milioni 1, 561,050/= mwaka 2013.
Akizindua usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum ameeleza kuwa matokeo hayo ni sawa na ongezeko la ukubwa wa Pato la Taifa kwa asilimia 27.8.
Amesema ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri na kutengeneza fursa za kuwawezesha wananchi kufanya kazi za kujiajiri na hatimaye kupata kipato halali kwa kazi wanazofanya.
Mh. Mkuya amesema kuwa kukua kwa uchumi wa Tanzania kumechangiwa na kujumuishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo Sayansi na Teknolojia ambako kumetoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato hususan matumizi ya simu za kiganjani ambazo zimerahisisha mawasiliano na utafutaji wa masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
Amezitaja shughuli nyingine kuwa ni ukamilishaji wa miamala mbalimbali ya kibenki na mikopo ambazo zimekuzwa na sekta ya mawasiliano , kuongeza ajira na kupunguza muda wa kusubiri huduma za malipo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, amefafanua kuwa kuongezeka kwa thamani ya Pato la Taifa kunaiongezea Serikali uwezo kimapato kupitia kodi na kuiwezesha kugharamia ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
"Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya Binafsi ya mwaka 2012 unaonyesha asilimia 60 ya kaya zote nchini zinapata maji safi na salama hasa hususan maeneo ya mijini,zaidi ya asilimia 20 ya kaya zote nchini zinatumia nishati umeme haya ni mafanikio makubwa ya matokeo ya ukuaji wa uchumi nchini" Amesisitiza Mh. Mkuya.
Akizungumzia mchango wa Sekta Binafsi katika kukua kwa pato la taifa nchini amesema kuwa ajira zipatazo laki nne kati ya laki sita katika sekta iliyo rasmi zimepatikana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa imetumia Tafiti za Taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.
Amezitaja tafiti hizo kuwa ni pamoja na utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya wa mwaka 2007, Sensa ya Kilimo iliyofanyika mwaka 2008 na Takwimu nyingine za utawala kutoka katika Wizara na Idara za Serikali.
Aidha, amefafanua kuwa ukokotoaji wa takwimu hizo umefuata mfumo wa Umoja wa Mataifa wa kutayarisha takwimu za Pato la Taifa wa mwaka 1993 na 2008 kwa lengo la kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinalinganishwa na takwimu nyingine duniani.

KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA CHADEMA KILICHOKUTANA JB BELMONT JIJINI DAR

unnamed
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Freeman Mbowe kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dr. Wilbroad Slaa katikati pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara John Mnyika wakati wa kikao cha Kamati kuu kilichokutana jana kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam na kujadili mambo mbalimbali kuhusu harakati za chama hicho.
unnamed1
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Freeman Mbowe, Said Issa Mohamed Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Profesa Abdallah Safari wakiwa katika mkutano huo.
unnamed3
Mmoja wa wajumbe akizungumza katika kikao hicho.
 
Chanzo: Mjengwa Blog

Kenyatta asaini sheria kali ya usalama

   
Rais Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Mnamo siku ya Alhamisi, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria.
Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.
Sheria hizo mpya zilipitishwa na bunge licha ya pingamizi kubwa na vurugu kutoka kwa wabunge hao.
Vurugu katika bunge la Kenya wabunge walipokuwa wanajadili mswada wa sheria kali ya usalama
Vyombo vya habari vimesema baadhi ya vipengee vya sheria hio ninabana uhuru wa vyombo vya habari na hata kutishia kwenda mahakamani.
Mswada huo kabla ya kutiwa saini na kufanywa sheria,ulifanyiwa mabadiliko kadhaa katika vipengee ambavyo vilionekana na baadhi ya wabunge kama vilivyokua vikali na kwenda kinyume na katiba.
Polisi sasa watakuwa na jukumu la kuidhinisha taarifa au picha za uchunguzi wa maswala ya usalama na hasa kuhusiana na ugaidi.
Polisi pia ndio watapaswa kuidhinisha picha za waathiriwa wa ugaidi kabla ya kuchapishwa au kuonyeshwa katika vyombo vya habari.
Vyombo vya habaro vinasema haya yanakwenda kinyume na uhueu wa vyombo vya habari.
Adhabu itakayotolewa kwa watakaokiuka sheria hii ni hadi faini ya shilingi milioni tano au dola elfu sitini ama kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu.

Friday, December 19, 2014

Simu Kanisani? tafakari tena   

Kasisi Don

Kasisi mmoja nchini Italia, ameweka kifaa kanisani mwake kinachoweza kubana mawasiliano ya simu baada ya kuchoka kuwaomba waumini kuzima simu zao kila wakati alipokuwa anahubiri.
Alilazimika kuomba idhini ya polisi kuweka kifaa hicho baada ya kuchoka kusikia milio ya simu zikipokea ujumbe.
Mpango huo umesifiwa sana na waumini ingawa imewaudhi wenye maduka katika mji wa Naples wanaosema kifaa hicho kinatatiza masafa na mawasiliano yao na pia kifaa hicho kimeathiri mashine za kutoa pesa.
Wanasema kifaa hicho pia kinatatiza shughuli zao ambapo wateja huagiza bidhaa kupitia simu zao za mkononi.
Kasisi Don alikasirishwa sana na waumini wake kujibu simu zao wakiwa kanisani
Lakini kasisi Don Michele Madonna, anakana kwamba kifaa chake kinatatiza shughuli za wenye maduka akisema kinaathiri tu mawasiliano kwa simu kwa waumini walio kanisani peke yake.
'Nilinunua kifaa hicho kutoka kwa duka la vifaa vya elektroniki, na kuwauliza polisi ikiwa ilikuwa sawa kuweka kifaa hiicho kanisani mwangu. Ni kifaa kizuri sana kwa sababu kimemaliza tatizo la watu kupigiwa simu na kuzipokea wakiwa kanisani.
Mmiliki mmoja wa maduka alisema: 'Tangu kasisi Madonna kuweka kifaa hicho ndani ya kanisa , nimepata matatizo sana kutumia kadi yangu katika biashara yangu. ''
'Kadi hii haifanyi kazi vyema na ninapoteza sana pesa zangu.''
Kanisa la kasisi Don
Kasisi Michele Madonna aliamua kuchukua msimamo huo kwa sababu waumini walikuwa na mazoea ya kutumia simu zao kanisani wakati kasisi huyo akihubiri. Kilichomuudhi zaidi kasisi huyo ni watu kupokea simu kanisani na hata wakati wa mazishi.
Kasisi Don alinunua kifaa hicho kwa dola sitini.
Kabla ya kukinunua kifaa hicho alianza kwa kuwasihi waumini kutotumia simu zao kanisani kwa sababu zilitatiza shughuli zake. Alianza kwa kuweka mabango kanisani humo lakini ujumbe huo wengi hawakuuzingatia na hapo ndipo akalazimika kuweka kifaa hicho ambacho kinazuia watu kupokea au hata kutumia simu zao Kanisani.
Chanzo: BBC
Escrow:Je Kikwete atategua kitendawili?
   
Rais Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo atalihutubia taifa la nchi hiyo ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti yanayoligusa taifa hilo.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa na kijamii wanatabiri huenda hatua atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow itakuwa ni moja kati ya agenda muhimu atakayoitolea ufafanuzi.
Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya raia na wapinzani wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Watu wakubwa serikalini akiwemo waziri mkuu Mizengo Pinda walihusishwa na Kashfa ya Ecrow na kutakiwa kujiuzulu
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Baada ya uchunguzi kuwasilishwa katika mkutano wa bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba, kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hii na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika na wengine kuondolewa katika nyadhifa zao za kuteuliwa,tayari Mwanasheria mkuu wa serikali amekwisha jiuzulu na rais kukubali uamuzi huo.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilikuwa za juu mno. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hayo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao wawili lingepatikana.
Chanzo:BBC

Escrow:Tibaijuka asema ng'o hatajiuzulu

   
Waziri Anne Tibaijuka anayekabiliwa na kashfa ya Escrow amesema kuwa hatojiuzlu licha ya shinikizo.
Waziri wa Ardhi,nyumba na Maendeleo ya makaazi nchini Tanzania Professa Anne Tibaijuka amesema kuwa hayuko tayari kujiuzulu kutokana na kashfa ya ecsrow inayomkabili.
Kulingana na Gazeti la the Citizen Tanzania ,Tibaijuka ambaye pia ni mbunge wa Muleba kusini ameviambia vyombo vya habari kwamba hana hatia na kuongezea kwamba si haki kumshinikiza kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo ya kutolewa kwa takriban billioni 306 kutoka kwa akaunti ya Escrow.
''Ninasulubiwa bila kupewa fursa ya kusikizwa'',alisema kufuatia wito wa yeye kujiuzulu kutokana na maswala ya maadili.
Lakini Profesa Tibaijuka amesema kuwa atajiuzulu tu iwapo itabainika kuwa ana hatia na kuongezea kuwa billioni 1.6 alizopata kutoka kwa James Rugemalira hazikuwa chafu.
Waziri huyo amesema kuwa fedha hizo alipewa kama msaada wa kusaidia shule ya Babro Johnson School baada ya bodi ya wakurugenzi wa hazina ya Joha ambayo huendesha shule hiyo,kuomba msaada huo kutoka kwa bwana Rugemalira, mfanyibiashara wa Tanzania ambaye alikuwa na hisa chache katika kampuni ya Independent Power Tanzania.
Alizungumza siku mbili tu baada ya mwanasheria mkuu Frederick Werema kujiuzulu kutokana na jukumu lake katika kashfa hiyo.
''Sioni sababu ya mimi kujizulu kwa sababu kufikia sasa serikali haijasema kwamba nina hatia.
Nitajiuzulu tu iwapo itabainika kuwa nina hatia'',alizungumza katika hoteli ya Grand Hyatt.
Profesa Tibaijuka amesema kwamba kwa sababu hazina ya Joha haitumii fedha chafu yuko tayari kurudisha fedha hizo kwa bwana Rugemalira iwapo itajulikana kwamba fedha hizo zilitolewa kwa njia mbaya.
Waziri huyo amesema kuwa bwana Rugemalira alikubali kutoa ufadhili kwa masharti kwamba atafungua akaunti katika banki ya Mkombozi.
Ameongezea kuwa hakupewa fursa ya kujitetea wakati jina lake lililotajwa bungeni.
Chanzo:BBC

TAASISI YA NELSON MANDELA YAMTUNUKU RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE DIGRII YA UZAMIVU YA HESHIMA(PHD HONORIS CAUSA) DESEMBA 18, ARUSHA


1111

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Dkt.Mohamed Gharib Bilal akimtunuku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Digrii ya uzamivu ya Heshima(PHD Honoris Causa) wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho iiyofanyika katika chuo hicho mjini Arusha Desemba 18, 2014
RAIS AMTEUA MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI (TPDC)


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dokta James Mataragio kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014. Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-
ELIMU:- Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
 PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994
UZOEFU WA KAZI:- Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA 2001 – 2004,
 Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu 2000 – 2001,
Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 1999 – 2000,
Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi) 1994 – 1999 -,
Exploration Geologist, Anglo America Corporation. Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce. Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo. Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani. Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu. Dar es Salaam.
18 Desemba, 2014

MAGAZETI YASEMAVYO LEO IJUMAA
















Flora Mabasha adai talaka

   
Flora Mbasha
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha,amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-Es-Salaam,akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha.
Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu mkazi,Devota Kisoka.
Flora anadai kuomba kuvunja ndoa hiyo na apewe talaka ni kutokana na tabia ya mumewe kumpiga,kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.
Katika hati hiyo ya madaianaendelea kudai kwamba mgogoro wao waliwahi kuufikisha kwa ustawi wa jamii,kwa ajili ya upatanishi lakini ilishindikana wakashauriwa walifikishe suala lao mahakamani.
Flora anaiomba mahakama itoe talaka,iamuru aendelee kukaa na mtoto,matunzo ya mtoto yatoke kwa mbasha na wagawane mali walizochuma pamoja.
Chanzo: BBC

Kikwete kutegua kitendawili Escrow?

   
Rais Jakaya Kikwete

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo atalihutubia taifa la nchi hiyo ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti yanayoligusa taifa hilo.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa na kijamii wanatabiri huenda hatua atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow itakuwa ni moja kati ya agenda muhimu atakayoitolea ufafanuzi.
Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya raia na wapinzani wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Baada ya uchunguzi kuwasilishwa katika mkutano wa bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba, kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hii na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika na wengine kuondolewa katika nyadhifa zao za kuteuliwa,tayari Mwanasheria mkuu wa serikali amekwisha jiuzulu na rais kukubali uamuzi huo.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilikuwa za juu mno. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hayo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao wawili lingepatikana.
Chanzo: BBC

Thursday, December 18, 2014

SERIKALI YAKUBALI AZIMIO ARUSHA KUHUSU HIFADHI YA JAMII

IMG_7245
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Arusha).
Na Mwandishi wetu, Arusha
SERIKALI ya Tanzania imeridhia azimio la arusha kuhusi hifadhi ya jamii nchini Tanzania na kusema litatumika kama dira katika kunemeesha watanzania.
Azimio hilo ambalo limetoka baada ya mkutano wa siku tatu wa wadau mbalimbali wa hifadhi ya jamii kutoka bara la Afrika na mashirika ya kimataifa limeelezwa kuwa msingi mkubwa wa ajenda ya Tanzania kuhakikisha wananchi wake wanahaki sawa katika elimu, afya na mwendelezo wa kiuchumi.
Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba hifadhi ya jamii inasaidia kuwa na maendeleo endelevu kwa kuangalia maendeleo ya binadamu katika ujumla wake.
Mkutano huo wa siku 3 uliohusisha wataalamu 150 kutoka sekta mbalimbali nchini na barani Afrika wakiwemo watengeneza sera, watafiti na wataalamu wa masuala ya hifadhi.
Ukiwa umewezeshwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za uchumi EPRI iliyopo Afrika Kusini (EPRI) , mkutano huo umeelezwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salumkwamba umeweka misingi imara ya kuwa na hifadhi ya jamii endelevu inayojibu mipango ya maendeleo ya taifa.
IMG_7158
Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akisoma Azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya Jamii, alisema kuwa historia imejirudia ambapo yapata miaka 47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la Arusha lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni maadui wa taifa.
Kukiwa na wataalamu waliobobea katika mifumo ya hifadhi ya jamii kutoka Afghanistan, Bangladesh, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe ulifanikiwa kutengeneza hoja zitakazotumika kufanya hifadhi ya jamii Tanzania kuwa endelevu.
Waziri Mkuya alishukuru kwa ushiriki wa mkutano na jinsi ulivyokuwa wazi na jinsi wataalamu walivyoweza kutengeneza azimio ambalo linaenda kuwa msingi katika utengenezaji wa sera na sheria kuhusu hifadhi za jamii nchini Tanzania na afrika kwa ujumla.
Mada kadhaa ziliwasilishwa katika mkutano huo ambazo zilizaa majadiliano yenye manufaa kuhusu mwelekeo wa hifadhi za jamii,utengenezaji wa mifumo ya kuweza kuendelea kuwepo kwa hifadhi ya jamii na umuhimu wa uratibu ndani ya serikali kuu, mitaa na mashirika yanayiotoa huduma za hifadhi ya jamii.
IMG_7135
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) wakisikiliza azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya jamii wakati wa kufunga kongamano hilo.
Waziri huyo alisema kwamba wakati taifa linaelekea katika uchumi wa gesi utakaofanya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 masuala ya hifadhi ya jamii yatakahakikisha haki katika kugawa keki ya taifa na kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata huduma za elimu, afya, na za kiuchumi kwa haki, kwa kuwa mifumo hiyo pia itatakiw akuchochea ajira na ujasirimali huku ilkilinda afya za wahusika.
Kwa upande wake Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani aliisifu Tanzania kwa kuanza mapema kusimamia masuala ya kinga ya jamii ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii na misaada inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi.
Aidha, Dkt. Gulaid aliipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake licha ya kuwa na vivutio vizuri vya mlima Kilimanjaro, hifadhi ya Serengeti na visiwa vya karafuu.
IMG_7204
Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha na aliisifu na kuipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake.
“Wimbo huu wa Tanzania tofauti na nyimbo za nchi nyingine ambazo wao wanazungumzia askari, watumwa, watawala wakiwemo Malkia na Wafalme”alisema Dkt. Gulaid.
Dkt. Gulaid aliwahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa wote wapo salama na wapo kwenye mpango wa hifadhi ya jamii kwa kuwa wametambuliwa na kubarikiwa na wimbo wa taifa wa Tanzania ambapo wajumbe waliimba wimbo huo na kuhitimisha kongamano hilo.
DSC_1058
Washiriki wa Kongamano hilo wakiimba wimbo wa Taifa baada ya Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid kutoa ombi kabla ya kumalizika kwa kongamano hilo.
IMG_7109
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akisistiza jambo wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
DSC_1061
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitia saini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii huku viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakishuhudia tukio hilo.
IMG_7267
IMG_7269
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na washiriki wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akionesha nakala ya Azimio la Arusha alilosaini kwa niaba ya Serikali.
IMG_7271
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Wazri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum baada ya kusaini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii (katikati) kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb).
IMG_7272
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akipeana mkono na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) mara baada ya kusaini azimio hilo huku Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.
IMG_7102
Baadhi ya wajumbe wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.
IMG_7173
IMG_7003
IMG_7043
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) mara baada ya kumalizika kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
Chanzo:CCM BLOG