Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, November 30, 2014

Nchi nyingi za Afrika hazitafikia Malengo ya Milenia.

Rwanda president Paul Kagame addresses the 69th United Nations General Assembly at the U.N. headquarters in New York September 24, 2014.
Rwanda president Paul Kagame addresses the 69th United Nations General Assembly at the U.N. headquarters in New York September 24, 2014.
               
Nchi nyingi za bara la Afrika hazitaweza kufikia malengo ya milinia ifikapo mwaka 2015 kutokana na mwanya uliopo kati ya uchumi na maendeleo ya kibinadamu. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa juu ya nchi zenye maendeleo madogo, iliyowasilishwa Alhamisi.
Licha ya kukua kwa uchumi barani Afrika nchi nyingi hazitafikia malengo ya milinia (MDGS) mwakani. Afisa wa maswala ya kiuchumi kwa Afrika katika Umoja wa Mataifa Junior Davis anasema nchi nyingi za Afrika  hazijaweza  kutumia maendeleo ya kiuchumi kufanya mabadiliko  katika sekta zake za miundo mbinu.
Ripoti hiyo inataja nchi za Ethiopia, Rwanda, Uganda na Malawi kama nchi nne pekee za Afrika ambazo huenda zikafikia malengo hayo ya milenia  kwa sababu zimewekeza katika sekta za maendeleo, miundo mbinu, afya na elimu.
 Nchi ambazo ziko nyuma sana kimaendeleo ni Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambako maswala ya kiutawala bado ni tatizo na zitategemea uungaji mkono wa jamii ya kimataifa kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Miongoni mwa nchi 48 zisizo na maendeleo makubwa duniani, 34 zimo barani Afrika lakini tatu zimeondoka kwenye orodha hiyo, nazo ni Botswana, Cape Verde na Samoa.

Mapendekezo ya PAC juu ya wezi wa Escrow

MAAZIMIO YA BUNGE KUHUSU HOJA YA TAARIFA MAALUM YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI

MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA ‘ESCROW’ YA TEGETA

PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL

_____________________________________


 1.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi Maalum wa Malipo yaliyofanyika katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (‘CAG’) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (‘TAKUKURU’) imeonesha kwamba kwamba Harbinder Singh Sethi, James Rugemalira (VIP), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (‘TANESCO’) walihusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda kwa makampuni ya Pan African Power Solutions Ltd. (‘PAP’), na VIP Engineering & Marketing (‘VIP’);


KWA KUWA, kwa sababu ya kuhusika kwa watu hao na miamala iliyofanyika kwenye Akaunti ya Escrow imeliingizia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha za umma zinazotokana na kutokulipwa kwa kodi mbali mbali za Serikali na kushindwa kwa TANESCO kukokotoa upya kiwango cha malipo ya gharama za uwekezaji (‘capacity charges’) wa IPTL;


KWA KUWA, mabilioni ya fedha yaliyotolewa kwenye Akaunti ya Escrow yametumika kuwapa kile kinachoonekana kuwa ni rushwa baadhi ya viongozi na maafisa wa serikali kama vile Mawaziri, Majaji, Wabunge, Wenyeviti wa Kamati za Bunge, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi.


NA KWA KUWA, vitendo vilivyofanywa na watu hawa vinaashiria makosa mbali mbali ya jinai kama vile uzembe, wizi, ubadhirifu, kutakatisha fedha haramu, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na kupokea mali ya wizi;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na Taarifa Maalum ya Kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbali mbali unaoendelea;


2.    KWA KUWA, vitendo vya kijinai wanavyhohusishwa navyo viongozi wa umma na maafisa wa ngazi za juu serikalini vinakiuka pia maadili ya viongozi wa umma na kuwanyima viongozi na maafisa hao uhalali wa kuendelea kushikilia nafasi za mamlaka katika uongozi wa umma;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wawajibishwe, kwa kuishauri mamlaka yao ya uteuzi kutengua uteuzi wao;


3.    KWA KUWA, katika watu walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO;


NA KWA KUWA, Bunge na/au Kamati zake za Kudumu zina uwezo na mamlaka, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, ya kuwawajibisha viongozi hawa wa Kamati kwa kuwavua nyadhifa zao;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka, na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao Wenyeviti tajwa wa Kamati husika za Kudumu za Bunge;


4.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba katika watu waliotajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania;


KWA KUWA, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (‘Katiba’) imeweka utaratibu mahsusi wa kushughulikia nidhamu ya Majaji;


KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamtaka Rais kuunda Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Majaji;


NA KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamruhusu Rais kumsimamisha kazi Jaji au Majaji husika wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania;


5.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. ilishiriki kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwa njia haramu kutoka katika Akaunti ya Escrow na kupelekwa katika akaunti zilizofunguliwa na PAP katika benki hiyo;


KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba akaunti za PAP  katika Stanbic Bank Tanzania Ltd. zimekwishafungwa baada ya fedha zote zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow kumalizika na Akaunti ya ya VIP katika Mkombozi Commercial Bank imebakiza kiasi fulani cha fedha;


NA KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba kuna uwezekano fedha zilizotolewa kutoka kwenye akaunti za PAP na VIP zilipelekwa katika benki nyingine;


NA KWA KUWA, vitendo vya Stanbic Bank (Tanzania) Ltd., na benki nyingine kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwenye Akaunti ya Escrow ni vitendo vya jinai kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi ziitaje Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. na benki nyingine yoyote itakayogundulika, kufuatia uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu (institutions of money laundering concern);


6.    KWA KUWA, vitendo vya wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, hujuma ya uchumi na ufisadi vimeongezeka, kushamiri na kushirikisha viongozi wa kisiasa na maafisa wa serikali pamoja na wafanya biashara wakubwa;


KWA KUWA, kwa mujibu wa sheria iliyoiunda, TAKUKURU inashughulikia vitendo vya aina zote za rushwa zikiwemo rushwa ndogo ndogo (petty corruption) na rushwa kubwa na ufisadi (grand corruption) na matumizi mabaya ya madaraka;


NA KWA KUWA, kwa sababu ya majukumu yake mapana kisheria, TAKUKURU inaelekea kuelemewa katika vita ya kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa letu kiuchumi, kijamii na kisiasa;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Serikali iandae na kuwasilisha Muswada wa marekebisho ya Sheria iliyoiunda TAKUKURU kwa lengo la kuanzisha taasisi mahsusi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa;


7.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha jinsi ambavyo TANESCO imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kulipa gharama za umeme unaozalishwa na IPTL na hivyo kuathiri hali ya kifedha ya Shirika hilo;


KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba TANESCO itaendelea kulipa fedha nyingi kwa ajili ya gharama za umeme huo wa IPTL;


HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo.


8.    KWA KUWA, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya TANESCO na makampuni binafsi ya kufua umeme imeisababishia TANESCO hasara ya mabilioni ya fedha na hivyo kutishia uhai wake wa kifedha;


KWA KUWA, Bunge lilikwishaazimia kwamba serikali iwasilishe mikataba husika Bungeni au kwenye Kamati zake kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza vyema wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri serikali;


NA KWA KUWA, Serikali haijatekeleza Azimio hilo la Bunge hadi sasa;


HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali itekeleze Azimio husika la Bunge mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge.

RAIS Kikwete awasili nchini


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Rais Bw. Morris Mbena baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea


Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo


Novemba 29, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wafanyakazi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba


29, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP  Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bw. Rashid Othman baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana kwa furaha  na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru  Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Mama Maria Nyerere akiongea na Mama Salma Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya Rais Kikwete kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo


Novemba 29, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Dua ilisomwa na viongozi mbalimbali wa dini  baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza kuongea na wanahabari mara tu alipowasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia kwa furaha wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliyeongoza mapokezi hayo ya Ikulu 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu 

Polisi aliyemuua kijana mweusi ajiuzulu

   
Daren Wilson Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi nchini Marekani amejiuzulu.
Wakili wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.
Afisa huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya maandamano.
Michael Brown,kijana mweusi nchini Marekani alipigwa risasi na kuuawa
Gazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28 aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho kwamba ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.
Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali hata kidogo.''

ESCROW:Spika adaiwa kuwalinda washukiwa

   
Spika wa bunge la Tanzania Anne Makinda
Spika wa Tanzania Anne Makinda ameshtumiwa kwa kujaribu kuwatetea wale wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi ya Escrow.
Kulingana na wachambuzi,wasomi na wataalam wa sheria hatua yake ya kujenga mazingira ya kuwapendelea washukiwa huenda ikasaidia kuwalinda watu hao.
Wakili maarufu mjini Daresalaam Sylvanus Sylivand ameliambia gazeti la the Citizen kwamba spika makinda alitarajiwa kufuata mfano mzuri uliowekwa na wenzake katika kashfa za awali ambapo bunge lina uwezo wa kuwashinikiza mawaziri na waziri mkuu kujiuzulu.
Ni wazi kwamba bunge linaweza kuishauri serikali kuwachukulia hatua viongozi wanaoshukiwa lakini si lazima kwamba rais afuate agizo hilo.
Kulingana na Sylivand,ni wazi kwamba kuna kitu kinachofichwa ili kuendesha ajenda tofauti ambayo itasadia aibu iliopata serikali.
Bunge la Tanzania
Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma Paul Loisulie amesema kuwa bunge sharti lichukue hatua kama taasisi.
''Kile ambacho kimetokea bungeni kuna uwezekano mkubwa kitaligawanya bunge na wananchi.''.
Inaonekana kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wanajaribu wawezalo kuwatetea viongozi wanaoshukiwa bila kujali maslahi ya raia walio masikini.
Julius Mtatiro wa Chama cha Civic Front amesema kuwa CCM inataka kuwalinda viongozi wake wakuu ili raia wasielewe kuhusu kilichotokea baada ya Spika Makinda kuwataka baadhi ya washukiwa hao kupendekeza hatua ambazo zingefaa kuchukuliwa dhidi yao.
Kulingana na Profesa Kitila wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Wabunge wana uwezo wa kuwaweka katika mizani watu watatu pekee ,rais,waziri mkuu na Spika na kile kilichokuwa kikendelea bungeni ni fursa ya wananchi kufikiria sana kabla ya kuipitisha katiba mpya.

Thursday, November 27, 2014

Baridi yagandisha breki za ndege Siberia

   
Ndege hiyo ikisukumwa
Abiria waliokuwa wanafanya safari na shirika ka ndege la Serbia walilazimika kushuka katika ndege hiyo na kuisukuma baada ya breki zake kuganda na kushindwa kuondoka.
Ndege hiyo ilikuwa inaanza kuruka kutoka katika mji wa Kirusi wa Igarka,lakini ilishindwa kusogea baada ya hali ya hewa kuwa -52C.
Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo idadi yao kubwa walikuwa wafanyakazi wa ndege hiyo waliombwa kutoa msaada wa dharura wa kuisukuma ndege hiyo kwa hofu ya kutowachelewesha endapo watasubiri msaada Zaidi.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Katekavia baada ya muda ilimudu kuendelea na safari zake na baadaye kutua salama katika mji wa Krasnoyarsk.kwa muujibu wa mashuhuda wa tukio hili kiwango cha baridikwa muujibu wa mashuhuda wa tukio hili ,wanaeleza kuwa kiwango cha baridi kilishuka hadi kufikia nyuzi joto 52, na kugandisha mfumo wa breki za ndege hiyo .
Mkuu wa kitengo cha huduma za ndege hiyo Oxana Gorbunova, anaeleza kwama abiria hawakulazimishwa kuisukuma ndege hiyo bali kwa hiyari waliamua kusaidia kuisukuma ,japokuwa kitendo hicho hakiruhusiwi kwakuwa kitendo hicho kinaweza kuathiri bodi ya nje ya ndege hiyo ,na wanasheria nao wanachunguza endapo uwanja wa ndege,shirika la ndege,wafanyakazi wa ndege ama abiria endapo wamevunja sheria za usalama wa anga.
Uwanja huo wa ndege unatumiwa na abiria takribani elfu moja kwa mwaka ,wengi wao hufanya kazi katika makampuni ya mafuta yanayomilikiwa na Urusi.

Chanjo ya Ebola yaonesha matumaini

   
Chanjo ya Ebola katika majaribio,yafana
Wanasayansi wamepongeza matokeo ya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, na kusema dawa zinaonesha kuwa salama na itasaidia mfumo wa kinga ya mwili kuvitambua virusi hivyo.
Watu 20 waliojitolea kutoka nchini Marekani, walipatiwa kinga maradhi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola.
Utafiti wa chanjo hiyo ya ebola kama huenda ikaokoa maisha wa maelfu walio hatarini kuambukizwa virusi hivyo. Dr Anton Fauci ni mkuu wa Taasisi ya Marekani ya magonjwa ya kuambukiza :
"Kwa upande wa usalama na uwezo wa kuleta matokeo mazuri nadhani tunaweza kuita majaribio haya ya chanjo haikufanikiwa. Japokuwa katika mkondo wa awali imeonyesha mafanikio makubwa." Amesema Fauci
Hata hivyo watafiti wanasema matokeo hayo sio uthibisho kwamba chanjo hiyo inafanya kazi lakini kama majaribio ya awali yamekuwa na mafanikio basi chanjo ya eboal itatolewa kwa maelfu ya wafanyakazi wa afya huko Afrika Magharibi kuanzia mwezi Januari mwakani.
Zaidi ya watu elfu tano mia tano wamefariki kutokana na kuambukizwa virusi vya ebola.Kwa sasa chanjo imekuwa ikifanyiwa utafiti na kampuni GlaxoSmithKline.
Dr Colin Brown ni mtaalamu wa magonjwa ambaye amepokea habari za chanjo hiiyo kama habari njema.
"Kwa vile suala la usalama limepewa umuhimu tunayo furaha kwamba hakuna madhara yaliyotokana na chanjo. Ambapo imeonyesha wagonjwa wa awali wapatao 20 wakuwa na tatizo lolote. Ninadhani tutarajie kuona itasaidia hasa kwa upande wa wafanyakazi wa afya kujilinda wakiwa kazini. " Alisema Bwana Brown

KAMATI YA PAC YAMTAKA WAZIRI MKUU, MWANASHERIA MKUU, WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WAWAJIBIKE KUHUSU RIPOTI YA TEGETA ESCROW


Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

- Kamati imesema imejiridhisha pasipo mashaka kuwa, Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW.
-Kamati, kwa kuzingatia kielelezo namba 22, inathibitisha bila shaka kwamba, Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri na kwamba aliridhia muamala huu ufanyike. Ndiyo maana katika maelezo yake ya
Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alithibitisha kuwa fedha za Escrow hazikuwa fedha za Umma.

- Ripoti yasema ni jambo la kushangaza kuona kwamba, jambo kubwa na zito kama hili lingeweza kufanyika bila ya mamlaka za juu, hususan Mhe. Waziri Mkuu kufahamu.
-Yaongeza kuwa kwa uzito na unyeti wa jambo hili, vyovyote vile, Waziri Mkuu anapaswa kuwajibika kwa kauli zake na kwa kutokutekeleza wajibu wake wa kikatiba ipasavyo, ili kurejesha imani ya wananchi
kwa serikali yao na viongozi wao wa kisiasa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema.
MWANASHERIA MKUU
-Kamati imethibitisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki Kuu ya Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J. Kwa kutumia madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu
wa Serikali aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 107
na hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu.

- Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa kwamba mgogoro uliopelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya
ESCROW ulikuwa ni mgogoro wa Wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati ya TANESCO na IPTL. Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha
afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha.

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
- Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini amekuwa, mara kwa mara, akilipotosha Bunge tukufu na Taifa kwa ujumla kuhusiana na Fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW kwamba ndani ya
fedha hizo hakukuwa na fedha za umma. Hata mtu wa kawaida angeweza kujua kwamba washirika wa ‘Tegeta Escrow Account’ ni akina nani na masharti ya kutoka kwa fedha hizo kwenye akaunti ni yapi
kwa mujibu wa Mkataba wa uendeshaji wa akaunti hiyo.

-Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, aidha kwa makusudi ama kwa sababu anazozijua vizuri zaidi mwenyewe, Waziri wa Nishati ananukuliwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge, Kwa nguvu
kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo kinyume na masharti ya Mkataba wa Escrow.

-Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye alikuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi na Bwana James Rugemalira, tena katika ofisi ya Umma; na
pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa Nishati na Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya biashara kwa jina la IPTL.

-Iwapo Waziri wa Nishati na Madini angetimiza wajibu wake ipasavyo, Fedha za Tegeta ESCROW zisingelipwa kwa watu wasiohusika, na Nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama kodi za VAT,
Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 30.

-Kamati inapendekeza kuwa Mamlaka yake ya uteuzi itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana sababu hizo zilizoelezwa.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
-Kamati imethibitisha kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini alisema uongo Bungeni kwa kutamka kauli ambazo zilizokuwa na lengo la kupotosha umma kuhusu akaunti ya Tegeta ESCROW ikiwemo kutoa
kauli ambazo zingeweza kusababisha Nchi kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na
nchi ya Uingereza.

-Kamati inapendekeza kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutenguliwa uteuzi wake. Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri huyu afikishwe mbele ya
Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama Mbunge kwa kusema uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa wabunge wengine kuhusiana na kauli wanazotoa ndani ya Bunge lako tukufu.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
-Kamati imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliingia makubaliano ya kutoa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW bila kujiridhisha kikamilifu kuwa maamuzi ya hukumu ya ICSID 2 yalikuwa bado kutolewa na hivyo kusababisha fedha kutolewa bila kukokotoa upya gharama za ‘capacity charges’, jambo ambalo limesababisha kupoteza fedha za umma.
-Vile vile, Kamati imebaini kuwa, Katibu Mkuu hakufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kujiridhisha uhalali wa Kampuni ya Mechmar kuuzwa kwa Piperlink na baadaye kuuzwa kwa PAP, na hivyo kusababisha fedha za akaunti ya Tegeta ESCROW kulipwa kwa asiyestahili na kinyume cha Mkataba wa akaunti ya Escrow.
-Kwa maana hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, pengine kwa uzembe wake ama kwa kukusudia kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe zaidi, amesaidia uchotwaji na
hatimaye utakatishaji wa fedha haramu.

-Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya juu uliofanywa na Katibu Mkuu huyo, kushindwa kujiridhisha kama masharti ya Sheria ya kodi ya Mapato Sura ya 333, Kifungu cha 90(2) yalitekelezwa. Kifungu hicho kimsingi kinaitaka mamlaka ya ‘approval’’ ya uhamishaji wa Makampuni kutotambua Kampuni mpaka kwanza kodi za uhamishaji ziwe zimelipwa na hati za malipo ya kodi zimetolewa na mamlaka ya kodi.
-Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Katibu Mkuu huyu utenguliwe, na TAKUKURU wamfikishe mahakamani mara moja, kwa kuikosesha Serikali Mapato, matumizi mabaya ya ofisi na kusaidia utakatishaji wa fedha haramu.

Habari kwa hisani ya mtandao wa matukio daima

ESCROW:'Waziri mkuu awajabishwe'

   
Zitto Kabwe
Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.
Sakata hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu umezusha mjadala mzito katika bunge la Tanzania.
Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya viongozi.
Mizengo Pinda waziri mkuu wa Tanzania ametajwa kwenye ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni
Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Ripoti hiyo ilitokana na ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo ilianika ukiukwaji mkubwa wa taratibu wakati wa uchotaji wa fedha hizo pia mahojiano na mkurugenzi mkuu wa Takukuru na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Waziri Pinda amelimbikizwa lawama ikidaiwa kuwa alijua kuwapo kwa ufisadi huo na matamshi yake kuwa fedha hizo hazikuwa mali ya umma, wakati Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema ameonekana kutoishauri vizuri Serikali na pia kuagiza fedha hizo zitolewe kwenye akaunti hiyo.
Waziri Sospeter Muhongo amelaumiwa kwa kukosa kuchukua hatua wakati akijua kuwapo kwa sakata hilo, huku naibu wake, Stephen Masele akitiwa hatiani kwa kulidanganya Bunge.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.

Wednesday, November 26, 2014

Wasio na waume wakataliwa migahawani

   
Wanawake walio valia mabui mbui nchini saudia.wamiliki wa Migahawa wamewakataza wanawake wasio na waume kuingia katika maeneo hayo.
Migahawa nchini Saudi Arabia imeagizwa kuondoa maelezo yanayowataka wanawake ambao hawana waume kuingia.
Ombi hilo linatoka katika kitengo cha kukabiliana na haki za kibinaadamu ndani ya ufalme wa tafa hilo.
kitengo hicho kinasema kuwa maelezo hayo yanakiuka sheria.
Lakini mmiliki mmoha wa mgahawa amesema kuwa ameweka maelezo hayo kutokana na viwango vya juu vya wanawake wanaotongozwa katika migahawa hiyo.
Tutaondoa maelezo hayo iwapo tutaona kwamba visa kama hivyo havifanyiki tena katika migahawa.
Msemaji wa shirika hilo la kibinaadamu Khalid Al-Fakhri ameliambia gazeti la Saudia kwamba migahawa haina haki ya kisheria ya kuwatenga wanawake ambao hawajaolewa katika maeneo yao ama kusisitiza kwamba wako chini ya mlinzi.
''Haya maelezo yako kinyume na sheria na yanaonyesha maoni yalio na wamiliki wa migahawa hii'',na kuwataka wamiliki hao kubuni mbinu nyengine za kukabiliana na swala la wanawake kutongozwa katika maeneo hayo.
Gazeti hilo pia limemnukuu mwanamke mmoja akisema kuwa ''iwapo watatupiga marufuku kutoingia katika migahawa wanataka twende wapi? Na kuongezea kuwa ni migahawa pekee ambayo wanawake wa Saudia huenda pekee yao.

Tume ya Jaji Warioba yatingisha Dar


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza kwenye mdahalo wa Katiba uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema mambo yanayotokea sasa nchini, kama viongozi kuwa na akaunti nje ya nchi na kudai ni 'vijisenti', Serikali kuingia mikataba yenye utata isiyohojiwa popote ni matokeo ya nchi kuwa na Katiba yenye maswali mengi kuliko majibu.
Akizungumza katika mdahalo wa Katiba uliokuwa na mvuto wa aina yake kwa watu kushangilia kila mjumbe aliyakuwa anazungumza ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba huku akitumia zaidi mifano alisema mambo hayo yanaweza kuendelea kwa sababu hata Katiba Inayopendekezwa pia 'imeyabariki'.(P.T)

Katika mdahalo huo Jaji Warioba aligusia ufisadi wa Sh306 bilioni za Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha zilizokuwa zikilipwa na Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, kuwa ni matokeo ya kuwa na Katiba isiyo na majibu.
Huku akijinadi kuwa yeye ni mwanachama hai wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jaji Warioba alisema kuna 'CCM imara' na 'CCM maslahi' na kwamba tabia yake ya kutoa changamoto ya masuala mbalimbali imetokana na kujengwa na Mwalimu Julius Nyerere.
Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali na mmoja wa washiriki wa mdahalo huo kutoka Umoja wa Vijana wa CCM, Senga Abubakar aliyetaka kujua kama Jaji Warioba ataiunga mkono Katiba Inayopendekezwa, iwapo itapitishwa katika kura ya maoni.
Mdahalo huo ni wa tatu kufanywa na taasisi hiyo, baada ya ule wa pili uliofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl Novemba 2 mwaka huu na kuvunjika kutokana na kuibuka vurugu, huku Jaji Warioba akishambuliwa alipokuwa akihitimisha hotuba yake kwa kuhoji watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Julius Nyerere kupitisha hoja zao katika misingi isiyokubalika.
Tofauti na mdahalo wa pili, mdahalo wa jana ulikuwa na ulinzi mkali wa polisi na mamia ya washiriki walikaguliwa kabla ya kuingia ukumbini na kutakiwa kuandika majina ili idadi yao iweze kutambuliwa.
Katika mdahalo huo, Jaji Warioba aliambatana na waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole, Profesa Mwesiga Baregu, Joseph Butiku na Mohammed Yusufu Mshamba.
Huku akishangiliwa na mamia ya washiriki wa mdahalo huo, Jaji Warioba alisema, "Tume ya Katiba ilipendekeza miiko na kanuni za uongozi lakini Bunge Maalumu la Katiba limeyaondoa na kuyaweka katika msingi wa utawala bora.
"Hivi huwezi kuwa mzalendo na mwadilifu mpaka uwe kiongozi? Hii si misingi ya utawala bora ni misingi ya kitaifa na inamhusu kila mmoja wetu."
Alisema lengo la kuweka suala hilo ni kutaka zawadi wanazopewa viongozi ziwe za taifa, "Maana yake kama umepewa zawadi inakuwa ya taifa siyo ya kwako. Yaani kama umepewa dhamana ya uongozi na unapata 'vijisenti' viwe vya taifa."
Alisema kutokana na maoni waliyokusanya kutoka kwa wananchi na utafiti uliofanywa na Tume walibaini kuwa masuala hayo yakiwekwa katika sheria badala ya Katiba, sheria husika haitakuwa na nguvu.
MAGAZETI LEO JUMATANO

1_copy_27011.jpg

2_copy_c3a6f.jpg
3_copy_48c4e.jpg
4_copy_04cd8.jpg
5_copy_bfbf3.jpg

20_copy_88994.jpg
21_copy_c16c5.jpg
22_copy_999dc.jpg
23_copy_03edc.jpg
24_copy_2e4f1.jpg
25_copy_c192b.jpg
26_copy_2cfbe.jpg
Haya ni kwa hisani ya mtandao wa majid mjengwa

Klabu bingwa barani Ulaya

   
Timu ya Chelsea
Usiku wa kuamkia leo kindumbwe ndumbwe cha michuano ya Klabu Bigwa barani Ulaya kiliendelea na kushuhudia Chelsea ikitoa kipigo cha mbwa mwizi mbele ya mashabiki wa Schalke 04 ya Ujuremani pale ilipoishindilia magoli 5 bila majibu.
Manchester City ya England nao wakawabamiza wababe wengine wa Ujerumani Bayern Munich kwa kwa kuwafunga magoli 3 - 2 na kufufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku magoli yote matatu ya Man City yakitiwa kimiani Sergio Aguero.
Katika mechi nyingine Paris St. Germain ya Ufaransa waliwashikisha adabu Ajax ya Uholanzi kwa kuifunga magoli 3 - 1 huku Becelona kwa upande mwingine wakiisasambua Apoel Nicosia ya Syprus kwa kuishushia kichapo cha magoli 4 kwa yai.
CSKA Moscow ya Urusi na AC Roma zikatoka suluhu ya goli moja 1 - 1
Burudani hiyo itaendelea leo ambapo Liverpool ya England baada ya kufanya vibaya katika mechi zilizotangulia leo wanajaribu bahati yao wakiwa ugenini dhidi Ludogorets ya Bulgaria.
Arsenal nao watawakaribisha Borusia Dortmud ya Ujerumani huku vita vingine vikiwa ni kati ya FC Basel ya Uswis watakaopopepetana na Real Madrid. Malmo FF ya Sweden watakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia