Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, September 30, 2014

Watu 270 walazwa kwa kunywa togwa

Na Joyce Joliga, Mwananchi
Songea. Watu zaidi ya 270 wa Kijiji cha Litapwasi, Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma wamelazwa wengi wao wakiwa na hali mbaya katika Zahanati ya Lyangweni na Hospitali ya Misheni ya St Joseph, Peramiho baada ya kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu.

Tukio hilo lilitokea juzi mchana kwenye sherehe ya Kipaimara kwa mtoto Dickson Nungu (14) na kuzua hofu kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho ambao wanaonekana kutoamini kilichotokea.

Wingi wa wagonjwa hao umesababisha zahanati hiyo kuelemewa na kiasi cha wengine kulazwa chini kwenye udongo, barazani na kwenye miembe wakisubiri kupatiwa huduma ya kwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Mskhiela alisema polisi inawashikilia watu watatu kuhusiana na tukio hilo na vinywaji na mabaki ya chakula kilicholiwa vimezuiliwa huku sehemu ikichukuliwa sampuli ili kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi.

Alisema waliopatiwa matibabu na kuruhusiwa ni watu 50 huku 190 wakiwa bado wanatibiwa Lyangweni na wengine 30 wakilazwa PeramihoHata hivyo, Kamanda Mshkhiela alisema walioathirika wanaendelea kuongezeka.
Mtoto Nungu, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Litapwasi, alipata Kipaimara hicho na mara baada ya chakula cha mchana, waalikwa walipewa pombe za kienyeji na wengine togwa. Baada ya muda mfupi, waliokunywa togwa na chakula, kila mmoja kwa wakati wake alianza kujisikia maumivu ya tumbo na kuharisha mfululizo huku wengine wakitapika damu.

Mama mzazi wa kijana huyo, Philbeta Ngonyani (36), ambaye pia amelazwa katika Hospitali ya Misheni Peramiho alisema: “Nimefikishwa hospitalini jana (juzi) saa nane usiku nikiwa sijitambui kutokana na maumivu makali kwa kuharisha mfululizo baada ya kunywa togwa.”

Akielezea tukio hilo alisema, anakumbuka siku moja kabla ya tukio, (Jumamosi iliyopita) yeye na wenzake (majirani) walishirikiana kupika togwa na walianza kazi hiyo saa sita adhuhuri na kumaliza saa 10 jioni na kisha kuiweka katika chumba kimoja ili ipoe kisha walimkabidhi ufunguo wa chumba hicho mtu aliyemtaja kuwa ni jirani yao, Ridhiwan Shawa ili siku ya sherehe mtu atakayehitaji kinywaji ampatie.
Alisema, juzi mchana mara baada ya mwanaye kutoka kanisani, waalikwa walifika nyumbani kwake wakiwa na watoto wao na baadhi ya ndugu na jamaa zao kwa ajili ya kujumuika kumpongeza kijana huyo na vyakula mbalimbali vilipikwa kama wali, pilau na ugali.

Alisema mara baada ya kula, vinywaji vilitolewa na kijana wake na baadhi ya watu walipatiwa soda na wengine waliomba pombe za kienyeji na togwa. “Waliokunywa pombe na soda hawakudhurika lakini waliokunywa togwa wengi walianza kusikia maumivu ya tumbo na kuanza kuharisha na kutapika mfululizo na wengine kuharisha damu, baadhi walirudi nyumbani na wengine walikimbilia zahanati.”

Alisema yeye, mumewe Ines Nungu pamoja na kijana wao mwingine, Matson wanaumwa tumbo, kuharisha na kutapika.

Jirani ambaye pia amelazwa, Aloysia Ngonyani alisema alifikishwa hospitalini hapo juzi usiku wa saa saba akiwa na maumivu makali ya tumbo huku akihara na kutapika baada ya kunywa togwa.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Watu-270-walazwa-kwa-kunywa-togwa/-/1597296/2469654/-/129rcy5/-/index.html

Monday, September 29, 2014

TAMKO LA UKAWA JUU YA AMRI YA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KUHUSU MAMLAKA YA BUNGE MAALUM
UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI
(UKAWA)
TAMKO LA UKAWA JUU YA AMRI YA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KUHUSU MAMLAKA YA BUNGE MAALUM
&
RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA ILIYOWASILISHWA KWENYE BUNGE MAALUM NA MWENYEKITI WA KAMATI YA UANDISHI YA BUNGE MAALUM
Dar es Salaam, 26 Septemba 2014:
Hapo jana tarehe 25 Septemba, 2014, Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri kuhusu maombi yaliyofunguliwa na Bwana Saed Kubenea, mwandishi habari mwandamizi na mhariri wa gazeti la Mwanahalisi kutaka Mahakama Kuu itoe ufafanuzi wa mamlaka ya Bunge Maalum kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za nchi yetu. Katika amri yake hiyo, Mahakama Kuu imesema yafuatayo kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum:
(a)            “Kwamba kuna mgongano katika maana ya maneno yaliyotumika kwenye kifungu cha 25 cha Sheria hiyo kwenye toleo la Kiingereza la Sheria hiyo. Hata hivyo, licha ya mgongano huo, tafsiri sahihi ya maneno ya kifungu hicho ni kwamba:

(i)                            “Mamlaka ya ‘kujadili na kupitisha masharti ya Katiba inayopendekezwa’ maana yake ni mamlaka ya kutunga na kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi wa Tanzania ili kupigiwa kura ya maoni;

(ii)                          “Mamlaka hayo yatatekelezwa kwa kutumia Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalum na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Katika kufanya hivyo, Bunge Maalum linaweza kuboresha na/au kurekebisha Rasimu ya Katiba. Mamlaka hayo yanamewekewa mipaka, kama ilivyokuwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na tunu na maadili ya taifa yaliyopo kwenye kifungu cha 9(2) cha Sheria;

(b)            “Mahakama haina mamlaka ya kuamua aina na upeo wa maboresho na/au marekebisho ambayo Bunge Maalum linaweza kuyafanya kwenye Rasimu ya Katiba kwa sababu hilo ni suala la kisiasa na wala siyo la kisheria, ilimradi maboresho na/au marekebisho hayo hayaendi kinyume na matakwa ya kifungu cha 9(2) cha Sheria.”
Uamuzi huu ni muhimu kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu zifuatazo:
(1)             Tangu kuanza kwa Bunge Maalum mwezi Februari mwaka huu, kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya wajumbe wa UKAWA na wajumbe wa CCM na mawakala wao katika Bunge Maalum kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum kama yalivyoainishwa kwenye kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Wakati UKAWA imeshikilia msimamo kwamba mamlaka ya Bunge Maalum yana mipaka kisheria na Bunge hilo halina mamlaka ya kubadilisha misingi mikuu ya Rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi, CCM na mawakala wake imeshikilia msimamo kwamba mamlaka ya Bunge Maalum hayana mipaka na Bunge Maalum lina uwezo wa kufanya marekebisho au mabadiliko yoyote kwenye Rasimu ya Katiba. Uamuzi wa Mahakama Kuu unathibitisha usahihi wa hoja ya UKAWA kwamba mamlaka ya Bunge Bunge Maalum yana mipaka kisheria;

(2)             Kwa kusema kwamba Bunge Maalum lina mamlaka ya kufanya maboresho na/au marekebisho kwenye Rasimu ya Katiba, Mahakama Kuu imekataa dhana ya CCM na mawakala wake kwamba Bunge Maalum lina mamlaka ya kubadilisha Rasimu ya Katiba. Amri ya Mahakama Kuu haijataja kabisa neno ‘kubadilisha’ ambalo liliingizwa kwa nguvu kwenye Kanuni za Bunge Maalum. Kwa maana hiyo, kanuni ya 3 ya Kanuni za Bunge Maalum inayotafsiri neno ‘hoja’ kuwa ni pamoja na mamlaka ya Bunge Maalum kubadilisha Rasimu ya Rasimu inakwenda kinyume na matakwa ya kifungu cha 25 cha Sheria na kwa hiyo tafsiri hiyo ni batili;

(3)             Kama ilivyokuwa kwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu iliyokuwa inahusu suala la mgombea binafsi, Mahakama Kuu ya Tanzania imekwepa kutekeleza wajibu wake wa kutenda haki kwa kufuata Katiba na Sheria za nchi kwa kujificha nyuma ya kichaka cha ‘maamuzi ya kisiasa.’ Mamlaka ya Bunge Maalum yamewekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Mipaka yake imewekwa na Sheria hiyo pia. Mahakama Kuu, kama ilivyo kwa Mahakama nyingine zote, ilikuwa na wajibu wa kutafsiri Sheria hiyo kwa kutamka bayana aina na upeo wa mamlaka ya kisheria ya Bunge Maalum kufanya maboresho na/au marekebisho ya Rasimu ya Katiba. Badala ya kutekeleza wajibu wake huo, Mahakama Kuu imekwepa lawama za CCM na mawakala wake kwa kusema kwamba aina na upeo wa maboresho na/au marekebisho ya Rasimu ya Katiba utategemea matakwa ya kisiasa, yaani ya CCM na mawakala wake, badala ya kutegemea lugha ya Sheria yenyewe. Aidha, Mahakama Kuu imekwepa lawama za UKAWA kwa kukubali hoja kwamba mamlaka ya Bunge Maalum yana mipaka, hata hivyo bila kuifafanua mipaka hiyo;

KATIBA MPYA INATENGENEZWA KWA MTUTU WA BUNDUKI!!!

Hali ya kisiasa katika nchi yetu kwa sasa ni tete kwa kiasi kikubwa. Nchi yetu sasa iko chini ya utawala wa kijeshi usiokuwa rasmi. Kila mahali katika makao makuu ya mikoa, wilaya na majimbo, askari wa Jeshi la Polisi wakiwa na mabomu na risasi za moto, magari ya deraya, farasi na mbwa wametanda kila mahali ili kujaribu kuzuia maandamano na mikutano ya wananchi wanaopinga mchakato wa Katiba unaoendelea.

Mjini Dodoma, Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo linatumiwa na Bunge Maalum limezingirwa na vikosi hivyo vya Jeshi la Polisi. Katika hali hii, ni wazi kwamba mchakato wa Katiba umekuwa mateka wa Jeshi la Polisi, Bunge Maalum lenyewe ni mateka na Watanzania wote ni mateka wa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya mabavu. Katiba mpya inatengenezwa kwa mtutu wa bunduki. Katika hali tete kama hii, kitu cha ajabu kabisa ni kwamba Rais Jakaya Kikwete – kama ambavyo imekuwa kawaida yake sasa – amekimbia nchi na kwenda Marekani kwa ziara ya wiki mbili.

Kama ambavyo UKAWA imesema katika kipindi chote hiki, chochote kitakachotokana na mchakato huu wa kimabavu hakitakuwa na uhalali wowote wa kisiasa. Sasa, baada ya mabadiliko mbali mbali ya Kanuni za Bunge Maalum kuruhusu uchakachuaji sio tu wa Rasimu ya Katiba bali pia uchakachuaji wa maamuzi ya wajumbe waliobakia wa Bunge Maalum, ni wazi pia kwamba chochote kitakachotolewa na Bunge Maalum kwa sura ya Katiba inayopendekezwa kitakuwa batili kisheria vile vile.

Kwa sababu hizo, tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na nchi yao kupinga nchi yetu kugeuzwa kuwa dola ya kipolisi na nchi ili chini ya utawala wa kijeshi usio rasmi. Tunawaomba wanachama na viongozi wote wa vyama vya UKAWA kufanya maandalizi ya kupinga vitendo hivi kwa njia mbali mbali za kidemokrasia. Aidha, wanachama na viongozi wetu wafanye maandalizi kwa pamoja kwa ajili ya Uchaguzi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliotangazwa kufanyika tarehe 14 Desemba, 2014. Uchaguzi huo uwe ni fursa ya kwanza ya kuiondoa CCM katika utawala wa nchi yetu kabla ya kuiondoa kabisa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.




-----------------------------------------------------------
Mh. Freeman Aikaeli Mbowe
MWENYEKITI MWENZA




Mh. Profesa Ibrahim Haruna Lipumba
MWENYEKITI MWENZA



--------------------------------------------------------------------
Mh. James Francis Mbatia

MWENYEKITI MWENZA
CCM YAUMALIZA UPINZANI LUSHOTO MKOANI TANGA
  • Mzee Charles Kagonji arudi CCM
  • Uongozi mzima wa Jimbo la Mlalo warudi CCM
  • Kinana awapokea kwa mikono miwili
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiutangazia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano Sunga kurejea rasmi kwa Charles Kagonji (mwenye shati la kitenge) kwenye Chama Cha Mapinduzi akitokea Chadema,wengine katika picha hii ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama
 Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema.
Katika mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde,aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha
 Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji
 Mzee Charles Kagonji akishukuru kurudi nyumbani CCM
 Mzee Julius Kavurai aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Mlalo Chadema akiwapungia mkono wananchi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara wilayani Lushoto ya kujenga na kukiimarisha chama pamoja na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 inavyoendelea.
 Umati wa watu waliohudhuria mkutano.
 CCM juu!!!
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha juu kadi ya CCM tayari kumkabidhi Mzee Charles Kagonji ambaye ameorudi CCM kutokea Chadema.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM Mzee Charles Kagonji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Sunga jimbo la Mlalo wilayani Lushoto.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Mzee Charles Kagonji kwa uamuzi wake wa kurudi CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Ndugu Ismail Semkunde aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mlalo Chadema na kuamua kurejea CCM.
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama akihutubia wakazi wa kata ya Sunga kwenye mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Majid Hemed Mwanga (kulia) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mlalo Chadema Ndugu Ismail Semkunde.
TAASISI YA VYOMBO VYA HABARI KUSINI MWA AFRIKA(MISA-TAN) YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA NA KUTOA MATOKEO YA UTAFITI WA UPATIKANAJI WA TAARIFA KWENYE OFISI ZA UMMA NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akiwakaribisha wageni waalikwa na waandishi wa habari waliofika kweye mkutano wao uliofanyika Jana kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam kulia ni  Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew.
Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Jana imekutana na waandishi wa habari na wadau tofauti katika kuadhimisha Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.09.2014 katika ofisi zao zilizopo kinondoni Mkwajuni Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti (kulia) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28 kwa kila mwaka.
 Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wagene waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28 kwa kila mwaka. kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapicho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini.
 Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kitabu cha ripoti ya haki ya kupata taarifa halali katika sekta za umma.
  Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akitangaza taasisi iliyochukua tuzo ya Kofuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2014.
  Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akionesha tuzo ya Kufuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2014 iliyokwenda kwenye Idara ya Mahakama.
   Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akitangaza taasisi iliyochukua tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu kwa mwaka 2014 kwa kutoa taarifa bila kificho kwa mwaka 2014
 Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kulia) akimkabidhi tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu Kaimu Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda Komba(kushoto) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa jana jijini Dar es Salaam
 Kaimu Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda Komba akionesha tuzo hiyo kwa waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye ofisi za Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) zilizopo eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Shighuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda Komba akizungumza na vyombo vya habari baada ya taasisi yaokutwaa tuzo ya Ufungu wa Dhahabu.
 Afisa utafiti na maelezo wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Sengiyumva Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kwenye siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa ambayo uadhimishwa septemba 28 kwa kila mwaka.
 Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na waandhishi wa habari wakifuatilia shughuli zima iliyokuwa inaendelea kwenye ofisi za Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) zilizopo jijini Dar es Salaam.
Siku Ya Kimataifa Ya Haki Ya Kupata Taarifa
Maelfu waandamana Hong Kong kushinikiza mabadiliko ya kisiasa
Waandamanaji Hong Kong siku ya Jumapili
Waandamanaji Hong Kong siku ya Jumapili
 

Na Victor Melkizedeck Abuso REUTERS
Maelfu ya waandamanaji huko Hong Kong wamekabiliana na polisi, muda mfupi tu baada ya kiongozi wa serikali katika eneo hilo kutangaza kuaanzisha mazungumzo kuhusu mabadiliko ya kisiasa na uchaguzi katika eneo hilo.

Waandamanaji wanasema wanataka uhuru zaidi wa kisiasa katika eneo hilo na uchaguzi wa huru na haki.
Kiongozi wa eneo hilo Leung Chun-ying hata hivyo hajasema ni lini mazungumzo hayo yataanza ili kuleta mabadiliko hayo yanayoshinikizwa na waandamanaji hao wengi wao vijana.
Waandamanaji Hong Kong

Waandamanaji hao wamewashtumu polisi kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwasambaratisha, kupita kiasi wakati wa maandamano hayo waliosema ni ya amani.
Mwandamanaji akisaidiwa baada ya kulemewa na mabomu ya kutoa machozi

Wanafunzi wamekuwa katika mstari wa mbele kuongoza maandamano hayo, ambayo wanasema yataendelea hadi pale mabadiliko hayo yatakapofanyika.

‘Katiba itaibeba CCM Zanzibar’


 
Na Sharon Sauwa na Daniel Mjema, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mohamed Aboud Mohamed amesema Katiba inayopendekezwa, itaibeba CCM katika uchaguzi mkuu ujao visiwani humo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu bungeni jana, Aboud alisema katiba hiyo itawasaidia katika kujibu kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwani imejibu asilimia 90 ya kero hizo.

“Kwa asilimia zaidi ya 90 kero za muda mrefu za wananchi wa Zanzibar zimejibiwa. Kwa hiyo wananchi watajua kuwa tumeshughulika na kero zao kwa kuzipatia ufumbuzi,”alisema.

Aboud alisema watakwenda kwa wananchi wa Zanzibar wakiwa kifua mbele kufafanulia kero ambazo zimetafutiwa ufumbuzi na wajumbe wa Bunge la Katiba, wengi wao wakitokana na CCM.

“Mimi ninaamini kuwa wananchi wakipelekewa Rasimu ya Katiba hii inayopendekezwa na wakaiona kuwa imekidhi matakwa yao wataiunga mkono,”alisema Aboud katika mahojiano hayo.
Aeleza kuhusu urais 2015

Waziri huyo ambaye aliwahi kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar mara mbili (mwaka 2000 baada ya Dk Salmin Amour kumaliza muda wake na mwaka 2010 wakati Amani Abeid Karume alipokuwa akiondoka madarakani), alisema hatagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

“Sina nia wala dhamira ya kugombea tena urais. Mimi dhamira yangu kubwa ilikuwa ni kuiunganisha Zanzibar kazi ambayo Rais aliopo (Dk Ali Mohamed Shein) ameifanya vizuri,”alisema
Aboud alisema sifa ya Rais ni uadilifu na kuwaunganisha Wazanzibari na Watanzania kwa jumla, sifa ambazo zote amekuwa nazo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Shein. Hata hivyo, alisema kazi yoyote inayofanywa na mwanadamu inakuwa na upungufu, haiwezi kuwa kamili.

“Mimi nina uhakika matarajio ya Wazanzibari yamepata majibu katika Rasimu hii ya Katiba. Na ninaamini kuwa wataipokea vizuri. Lazima tufahamu kuwa Katiba ni mchakato,” alisema.

Aboud alisema kama kuna jambo ambalo hawakulipata katika mchakato wa sasa wa Katiba unaomalizika Oktoba 4 au hawakufikia mwafaka , kesho wanaweza kupata nafasi ya kulizungumzaAlipoulizwa kero zilizopatiwa ufumbuzi katika Katiba hiyo, Aboud aliitaja kero ya mafuta na gesi ambapo sasa Zanzibar itakuwa na uwezo wa kushughulikia.
Kwa habri zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Katiba-itaibeba-CCM-Zanzibar-/-/1597296/2467614/-/13sjm6b/-/index.html

Funga kazi Bunge la Katiba leo

Na Daniel Mjema, Mwananchi
Dodoma. Wiki ya kufa au kupona kwa Bunge la Katiba, inaanza leo mjini Dodoma wakati wajumbe watakapoanza kuzipigia kura ibara na sura za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

Shughuli hiyo itaanza huku kukiwa na hofu ya kutopatikana kwa theluthi mbili ya kura kwa wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar inayotakiwa kwa mujibu wa kanuni, sheria na Katiba ya nchi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, upigaji kura utafanyika kwa siku nne kuanzia leo hadi Oktoba 2, mwaka huu na iwapo itapitishwa, atakabidhiwa Rais kusubiri kupigiwa kura ya maoni mwaka 2016.

Habari kutoka bungeni zinadai kuwa wasiwasi wa kutopatikana kwa theluthi mbili uko zaidi upande wa Zanzibar hasa baada ya wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia Bunge hilo.

Hofu nyingine inatokana na suala la Mahakama ya Kadhi kutoingizwa, jambo ambalo limewagawa wajumbe huku kundi moja likiapa kupiga kura ya hapana iwapo haitaingizwa
Baadhi ya wajumbe wanataka Ibara ya 40 iingize vifungu vinavyotamka kuwapo kwa mahakama hiyo ili uamuzi wake kuhusu masuala ya ndoa, mirathi na talaka utambuliwe na sheria za nchi.

Hata hivyo, wajumbe wengine wanapinga suala hilo wakitaka ibara hiyo ibaki kama ilivyo ili Serikali isijihusishe na masuala ya uendeshaji wa jumuiya za dini.

Vilevile, Kifungu cha 22 (d) cha Rasimu kinachompa mwanamke haki sawa na mwanamume kumiliki ardhi kinapingwa vikali na baadhi ya wajumbe.

Pia baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar wanaona kuwa pamoja na kwamba karibu asilimia 90 ya mambo waliyokuwa wakiyalilia yameingizwa kwenye Katiba, bado Zanzibar haijapewa mamlaka kamili.

Hali hiyo imeifanya Kamati ya Uongozi chini ya Sitta kufanya vikao vya mashauriano mfululizo baina yao na wajumbe wa Kamati ya Uandishi ili kujaribu kuokoa jahazi.
Jana, vikao vya kamati 12 za Bunge ambavyo vilikuwa vianze saa 8:00 mchana vililazimika kusogezwa mbele kusubiri maelekezo kutoka Kamati ya Uongozi ambayo ilikuwa inakutana saa 9:00 alasiri.

Mahakama ya Kadhi yalitafuna Bunge


 
Na  Waandishi Wetu, Mwananchi
Dodoma/Dar. Suala la Mahakama ya Kadhi limechafua hali ya hewa bungeni mjini Dodoma baada ya wajumbe Waislamu kutishia kupiga kura ya hapana kama halitaingizwa katika Rasimu inayopendekezwa.

Wakati Waislamu wakishikilia msimamo huo, wajumbe ambao ni Wakristo nao wamejipanga kupiga kura ya hapana endapo Mahakama ya Kadhi itaingizwa katika Katiba inayopendekezwa.

Dalili za mpasuko huo zilianza kujitokeza jana asubuhi baada ya mjumbe mmoja, Jaku Ayub Hashim kuwasha kipaza sauti akitaka kuzungumza akisema ana jambo muhimu.

“Mheshimiwa tangu jana (juzi) ulisema utanipa nafasi ya mwanzo nizungumze,” alisema Jaku, lakini Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu alimtaka aketi chini na suala lake limesikika.

Suluhu akaendelea kuwapa wajumbe wengine kuendelea kuchangia na baadaye alimpa Jaku muda wa dakika saba ili kuwasilisha kile alichotaka kukizungumza ndani ya Bunge hilo.
Jaku alisema walipendekeza kifungu kinachotaka uamuzi unaohusu ndoa, talaka na mirathi iliyoamuliwa kwa misingi ya dini ingizwe kwenye Katiba inayopendekeza lakini hakimo.

“Ni kitu kidogo kabisa tuliomba kiongezwe lakini cha kusikitisha kikundi cha sanaa kimeingizwa. Mimi binafsi yangu sitaunga mkono wala mguu wala sitaipigia kura hii,” alisema Jaku.
Suluhu akamweleza kuwa angalizo lake limechukuliwa, na uongozi wa Bunge pamoja na kamati ya Uandishi wanajitahidi kuingiza kila kitu kinachowezekana, lakini kwa misingi na sheria za nchi.

Baadaye Sheikh Masoud Jongo alipopewa nafasi ya kuchangia, naye alitahadharisha kuwa mambo yaliyopendekezwa na Waislamu yasipoingizwa kama ilivyo kwa sasa, hawatakuwa tayari kwa lolote.

“Msimamo wetu sisi Waislamu kama mambo yetu tuliyoleta katika mapendekezo hayataingizwa, basi yatabomokea hapa na hatutakuwa tayari tena,” alisema Sheikh Jongo, kauli iliyowashtua wajumbe.

Akihitimisha majadiliano hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge alisema kamati yake imefanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwa masilahi ya Watanzania. Akiahirisha Bunge, Suluhu alisema kesho Bunge litaanza kwa kupitia baadhi ya mambo yaliyoibuka katika uhakiki kisha kupitisha azimio la upigaji wa kura. Kura zitapigwa kati ya kesho hadi Oktoba 2.

Baada ya kuahirishwa kwa Bunge, Sheikh mwingine, Hamid Jongo alimwendea Askofu mstaafu Donald Mtetemela na kumkumbatia, kisha kumvuta pembeni na kisha kuteta kwa dakika tano.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mahakama-ya-Kadhi-yalitafuna-Bunge/-/1597296/2467610/-/v0bk30z/-/index.html

Tibaigana: Wapinzani wana haki kuandamana


Alfred Tibaigana alipokuwa kazini siku chache kabla ya kustaafu. 
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba, Kamishna Tibaigana alisema suala la maandamano halikumsumbua kwa kuwa alielewa kuwa sheria inayaruhusu, hivyo alichokuwa akifanya ni kuwaita viongozi wa vyama vinavyotaka kuandamana na kufanya nao makubaliano ya namna maandamano hayo yanavyopaswa yafanywe kabla ya kuyaruhusu.

“Pengine hiyo ndiyo sababu sikuwahi kushambuliwa kwa maneno ya kejeli au matusi na wanasiasa kwa kuwa sikuwahi kuzuia maandamano yao bila sababu na hata kama kulikuwa na sababu niliwaita na kuwaeleza na tulikubaliana.

“Kikubwa ni kujenga tabia ya kuwaita viongozi wa waandamanaji na kujadiliana nao, vinginevyo wanaweza pia hata kukufikisha mahakamani wakipinga kuzuiwa maandamano yao,” alisema Tibaigana ambaye alikumbana na sakata la kudai maandamano wakati akiwa Kamanda kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam.
“Nilikuwa nawaita viongozi nakaa nao tunakubaliana. Hata kama ningeambiwa na kiongozi gani nisitoe kibali, kama hakuna sababu za kweli, nilikataa kwa kuwa kisheria mimi ndiye nawajibika kama vyama vikishtaki. Ili uzuie maandamano unapaswa kuwa na sababu za msingi ambazo ukiwaeleza waandamanaji wanakuelewa.”

Tibaigana anakumbuka jinsi CUF kilivyoandaa maandamano makubwa kushinikiza kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar baada ya kutoridhishwa na matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, lakini anasema kutokana na msimamo wake, haikuwa vigumu kwake kuruhusu jambo hilo.

 “Wakati wa uongozi wangu CUF ilikuwa na nguvu sana, lakini mimi sikuwa na tatizo nao. Walipotaka kibali cha kuandamana niliwapa bila woga na tuliishi vizuri,” anaeleza Tibaigana.

Vuguvugu la maandamano pia lilitanda wakati wa maandalizi ya ziara ya Rais wa zamani wa Marekani, George Bush nchini kutokana na wasomi na baadhi ya wanaharakati kutaka kufanya maandamano kupinga vitendo vya taifa hilo kubwa dhidi ya raia wa Palestina na sehemu nyingine ambako wananchi wasio na hatia walikuwa wakiuawa.

“Nilichofanya ni kukutana nao na kuwaeleza njia ambazo wangeweza kutumia katika maandamano hayo na hali ilikuwa shwari,” alisema Kamanda Tibaigana.

Katika kipindi chake cha uongozi wa Polisi Dar es Salaam, Kamanda Tibaigana pia alikumbana na vurugu za kidini ambazo zilisababisha askari mmoja kupoteza maisha, lakini anasema kwa kushirikiana na wadau wengine, walijipanga na hali ikawa shwari.
Alivyomng’ang’ania Ditopile

Moja ya matukio makubwa wakati akiwa Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam ni tukio la mkuu wa zamani wa Mkoa wa Tabora, Ditopile kumuua dereva wa daladala baada ya kutokea kutoelewana barabarani, hali iliyolazimu sheria kufuata mkondo wake. Jeshi la Polisi lilitakiwa limkamate mkuu huyo na kumfikisha mahakamani.

Ditopile alituhumiwa kufanya mauaji hayo Novemba 5, 2006. Akidaiwa kumuua kwa kumpiga risasi dereva wa daladala, Hassan Mbonde. Alikamatwa na kufikishwa mahakamani, lakini alifariki dunia Aprili 20, 2008 wakati kesi yake ikiendelea.
Kwa habari zaidi ingia Tibaigana: Wapinzani wana haki kuandamana

Sunday, September 28, 2014

KINANA AVUKA MILIMA NA MABONDE HADI LUSHOTO, MAELFU WAFURIKA MKUTANO WAKE WA HADHARA KATA YA MLOLA
 
 Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili Uwanja wa Sokoni, katika Kijiji cha Mlola 2,
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili viwanja vya Sokoni, katika Kijiji cha Mlola, kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja hivyo akiwa katika ziara yake ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM na pia kuzungumza na wananchi kuhusu kero mbalimbali kwa njia ya maswali na majibu, katika wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, leo, Septemba 27, 2014. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye ameambatana na Kinana kwenye ziara hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Nape wakisalimia wananchi baada ya kuwasili viwanja hivyo vya sokoni, katika Kijiji cha Mlola,
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipakia udongo wenye mbolea kwa ajili ya kuoteshea miche  kwenye kitalu cha kuoteshea miche ya miti katika mradi wa kutunza mazingira katika Kijiji cha Kwesimu, Lushoto. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Hanry Shekifu ambaye pia ni Mbunge wa Lushoto.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda mche kwenye kitalu cha kuoteshea miche ya miti katika mradi wa kutunza mazingira katika Kijiji cha Kwesimu, Lushoto
  Kinana akikagua kitalu cha kuoteshea miche ya miti Kijiji cha Kwesimu, Lushoto
Kitalu cha kuoteshea miche ya miti Kijiji cha Kwesimu, Lushoto
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoka kukagua ujenbzi wa zahanati ya Kijiji cha Mbweyi, Kata ya Malibwi, Lushoto akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimza utekelezaji wa ilani ya CCM katika wilaya ya Lushoto mkoa wa Tanga, leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
PRESIDENT KIKWETE VISITS CNN STUDIOS IN NEW YORK

President Jakaya Mrisho Kikwete chats with  Cable News Network (CNN) 's Richard Quest and Maggie Lake when he visited  CNN Studios at the  Time Warner Cente in New York.  
CNN is an American basic cable and satellite television channel that is owned by the Turner Broadcasting System division of Time Warner. 
The 24-hour cable news channel was founded in 1980 by American media proprietor Ted Turner.  Upon its launch, CNN was the first television channel to provide 24-hour news coverage, and was the first all-news television channel in the United States.
While the news channel has numerous affiliates, CNN primarily broadcasts from its headquarters at the CNN Center in Atlanta, theTime Warner Center in New York City, and studios in Washington, D.C. and Los Angeles. CNN is sometimes referred to as CNN/U.S. to distinguish the American channel from its international sister network, CNN International.
President Jakaya Mrisho Kikwete poses with CNN's Richard Quest and Maggie Lake when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York
President Jakaya Mrisho Kikwete presents  CNN's Richard Quest when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York. Right Ms. JulietRugeiyamu Kairuki, the Executive Director of the Tanzania Investment Centre. The Tour was jointly organized by the TIC and CNN as part of an on going partnership to promote Tanzania  as an attractive destination for investment and tourism. 
They also discussed  the forthcoming African Journalist of the year Awards Ceremony to be held in Dar es salaam later this year.
President Kikwete and his entourage take a souvenir photo in the CNN Studios during his visit
President Jakaya Mrisho Kikwete and  CNN's Richard Quest and Maggie Lake when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York.  This is where Richard Quest produces his world famous "Quest Means Business Programmes"
President Jakaya Mrisho Kikwete and his entourage are given a guided tour by  CNN's Richard Quest when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York.  
President Jakaya Mrisho Kikwete and his entourage are given a guided tour by  CNN's Richard Quest when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York.  
President Jakaya Mrisho Kikwete and his entourage in talks with Mr.  Ken Jautz (second left), the  Executive Vice President of CNN (Responsible for CNN/US) and Mr. Rani Raad (left  Executive Vice President & Chief Commercial Officer (CNN International) when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York.  The  CNN .executives engaged President Kikwete  on Tanzania's a investment Track record and the country's  impressive economic performance, as well as its  approach to responsible Journalism
 CNN memorabilia and TIC's promotional banner  on display during President Kikwete'svisit of  CNN studios in New York. STATE HOUSE PHOTOS

Jeshi la Marekani: Tunadhoofisha Islamic State nchini Syria

    
Ndege za kivita zikishambulia ngome za Islamic State
Ndege za kivita zikishambulia ngome za Islamic State  

Na Victor Melkizedeck Abuso
Jeshi la Marekani linasema mashambulizi ya angaa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Islamic State nchini Syria yanadhoofisha wapiganaji hao baada ya vituo vya mafuta walivyokuwa wanadhibiti kuteketezwa.

Hata hivyo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Martin Dempsey amesema mashambulizi ya angaa pekee hayawezi kutegemewa kuwamaliza kabisa wapiganaji hao nchini Syria na Iraq.
Aidha, Jenerali Dempsey amesema suluhu la kisiasa linahitajika nchini Iraq na Syria ili kupata amani ya muda mrefu katika nchi hizo mbili.
Siku ya Ijumaa, wabunge nchini Uingereza nao walikubali jeshi lao kujiunga na Marekani, Ufaransa na mataifa mengine ya Ulaya na kutoka Umoja wa Kiarabu kuwashambulia wapiganaji hao.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Martin Dempsey (Kulia)

Katika hatua nyingine, Marekani inasema wapiganaji wa jeshi huru la Syria linahitajika kupambana na wapiganaji hao wa Islamic State ardhini ili kudhibiti kabisa ngome za wapiganaji hao.
Zaidi ya Mataifa 40 yamejiunga na Marekani kuongoza mashambulizi dhidi ya wapiganaji hao ambao wanaedelea kusababisha mauaji ya raia na kuchukua maeneo zaidi.
Mwanajeshi wa Iraq

Siku ya Ijumaa, Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alishtumu mashamabulizi ya angaa nchini Syria bila ya kuishirikisha Moscow.