Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, August 31, 2014

Pacific Koreans infected with 'Francis syndrome' after papal visit


Pope Francis celebrated Mass in Daejon, South Korea for the Solemnity of the Assumption on Aug. 15, 2014. Credit: Alan Holdren/CNA.
Pope Francis celebrated Mass in Daejon, South Korea for the Solemnity of the Assumption on Aug. 15, 2014.
.A former Korean ambassador to the Holy See spoke of the effects of Pope Francis' recent visit to South Korea, saying that all of Asia now feels a long-term challenge to imitate his humble ways.

“All the media in Korea are already speaking of 'Francis syndrome,'” former ambassador Thomas Han told CNA Aug. 26.

“The Korean people, having been deeply impressed by Pope Francis' person and his lifestyle, seriously reflect upon the meaning of their lives and seek to see the things in life that really matter.”

Han explained that leaders “at every level of society” now feel an “unspoken pressure to make their own the leadership style the Korean people have witnessed in Pope Francis.”

“Therefore, it is safe to say that such 'Francis syndrome' will surely serve as a momentum for the Koreans to promote the culture of love, thereby contributing to authentic humanization of the Korean Peninsula in the long term.”

Pope Francis traveled to Seoul, South Korea Aug. 14-18, where he met with youth participating in the 6th Asian Youth Day, as well as with government officials, local Church leaders and heads of other faith traditions.

Marking the first time a Roman Pontiff has visited the peninsula since John Paul II went in 1989, the voyage has had an impact on the entire Asian continent, particularly the youth, who were touched by the Pope's heart-to-heart way of communicating, and those affected by the Sewol ferry disaster that happened earlier this spring.

With the presence of Pope Francis in their midst, Koreans “were excited to verify what they had heard about him through the media,” Han observed.

“In a word, Pope Francis has at last satisfied their quenchless thirst for true leadership. His coherence between words and actions, his simple lifestyle, his humility, the way he embraced the poor, the disabled, the outcasts greatly impressed them.”

It is rumored that following the Pope's visit, many in Korea are now beginning to purchase the compact Kia Soul he chose to pick him up from the airport, following his request to have the smallest car possible.

As the smallest car in Korea, the vehicle was considered unsuitable for such a globally significant figure, and left many chuckling when they saw the pontiff drive away in the boxy car.

What the Korean people saw in the Pope was “a witness to hope,” the former ambassador explained. “The hope that with the leadership of Pope Francis the world can be made a better place to live in.”

Speaking on the particular impact Pope Francis made on the Asian youth, Han noted that they viewed him as the Good Shepherd who came “not to be served but to serve and to give his life to redeem many people.”

“They have been excited to be with Pope Francis who rekindled the very special love that had been displayed by Christ toward the young man in the Gospel” and who “launched them as leading actors in humanization and evangelization of society.”

Drawing attention to how the Asian continent currently is home to over 60 percent of the world’s population, Han noted that along with this number come “flagrant inequalities” both in terms of one’s possessions, as well as in the exercise of political power.

“More than half of the 900 million absolute poor in the world who survive on less than $1.25 a day are in Asia,” he stated, observing also how “Women experience a very low level of gender equality in the world” and “the deprivation of the right to life of the unborn child is widespread.”

Going on, Han observed that many “are denied the right to religious freedom” and that “cultural and religious diversity sometimes leads even to animosity and conflict between peoples.” He also pointed out current threats to peace, including increasing militarization and continuous environmental pollution.

“It is thus timely for Pope Francis to come to encourage the Catholic Church in Asia to strengthen its efforts to humanize and evangelize the Asian continent facing such realities,” he said.

Noting the significance of choosing Korea for his first trip to Asia, the former ambassador explained that Pope Francis’ presence in a country suffering division for 70 years signifies that he came “to Korea and to Asia as Pontiff, that is, as a builder of bridges with God and between peoples.”

He came “as apostle of true peace, to encourage the Catholics and all the other Asians to dialogue and work together to overcome all the inhuman situations that occur on the Continent to build a more equitable society, a more stable peace in the world.”

In this context, Pope Francis’ visit represents “a challenge to Korea as a nation and the Catholic Church therein to assume a greater role in pursuing authentic human development of peoples in Asia as well as in the Korean Peninsula,” Han observed.

“Both Korea and the Catholic Church well deserve to play such a role and (are) ready to embrace such a challenge,” he said. “The Pope’s visit will stimulate the ongoing renewal of the Catholic Church’s determination to take the lead in evangelization of Asia as well as the Korean Peninsula.”

At the same time, he continued, it will serve “as an effective catalyst to Korea’s constant willingness to assume its own responsibility for the humanization of Asia as well as the Korean Peninsula by promoting the culture of love, justice and peace.”

CHADEMA YATOA UFAFANUZI JUU YA GHARAMA ZA FOMU NA UMRI WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI BAVICHA


TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI JUU YA GHARAMA ZA FOMU, UMRI WA KUGOMBEA, KAMPENI ZA UCHAGUZI NDANI YA BARAZA NA USAILI WA WAGOMBEA
Wakati zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbali mbali ndani ya Baraza zikiendelea, tunapenda wanachama hususani vijana kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo:
1. ADA YA FOMU YA KUGOMBEA
Tunapenda kuwajulisha wananchama wote wanaochukua fomu za kuomba nafasi za uongozi wa Baraza kuwa gharama za fomu ni kama ilivyoandikwa kwenye fomu yaani Shilingi 50,000/= kwa nafasi zote. Nafasi hizo ni:
i) Mwenyekiti
ii)Makamu mwenyekiti Bara na Visiwani
iii)Katibu Mkuu wa Vijana
iv)Naibu Katibu Mkuu wa Vijana Bara na Visiwani
v)Mratibu wa uhamasishaji
vi)Mweka Hazina
vii)Wajumbe watano wanaowakilisha Vijana Baraza Kuu
Viii)Wajumbe ishirini wanaowakilisha vijana katika Mkutano Mkuu wa Chama.
2. UMRI WA KUGOMBEA
Kwa mujibu wa kanuni za Baraza, mgombea yoyote anapaswa kumaliza kipindi cha uongozi wake, kama atachaguliwa, akiwa bado na umri wa ujana yaani miaka na kwamba asiwe amezidi miaka 35. Hivyo ni lazima mgombea yoyote asiwe amezidi umri wa miaka 30 wakati anagombea. Kwa maana hii, wagombea wote wa nafasi za uongozi wa BAVICHA Taifa wanapaswa kuwa ni wale waliozaliwa tarehe 10.09.1984 na kuendelea kwani mtu atatambulika kuwa kiongozi wa Baraza Taifa kuanzia tarehe hiyo na si vinginevyo.
Ndio maana tunaendelea kusisitiza kuwa moja ya viambatanisho muhimu vya kwenye fomu ya kugombea kiwe kimojawapo kati ya cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria au kitambulisho cha kupiga kura na si tofauti na hapo.
3. UREJESHAJI WA FOMU
Hapo awali tulielekeza kuwa siku ya mwisho ya kurejesha fomu ni tarehe 25.08.2014 Saa kumi na nusu jioni na kwamba fomu hizo zirejeshwe makao makuu ya BAVICHA Dar es salaam ama ofisi ndogo za BAVICHA Zanzibar. Tunapenda kuendelea kusisitiza kwamba muda wa mwisho ni kama ilivyopangwa. Hata kama uko mkoani, hakikisha fomu yako inafika makao makuu ya Baraza ndani ya muda uliopngwa.
4 USAILI WA WAGOMBEA
Baraza linapenda kuwafahamisha wale wote wanaokusudia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwa tarehe 4 na 5 Mwezi Septemba 2014 ndio siku za usahili. Usahili huu utafanyika Jijini Dar es salaam na wagombea wote wanapaswa kufika na vyeti vyao halisi. Gharama za kuwepo Dar es salaam pamoja na usafiri zitakua juu ya wagombea wenyewe.
5 KAMPENI ZA UCHAGUZI NDANI YA BARAZA
Kama ilivyoelezwa hapo awali, Katiba ya chama, Mwongozo wa Baraza, taratibu za uchaguzi za chama toleo la mwaka 2012, na mwongozo wa dhidi ya rushwa wa mwaka 2012, kwapamoja ndio zinaongoza uchaguzi huu.
Pamoja na mambo mengine ya kuzingatia, muda wa kampeni ni wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi na si tofauti na hapo. Tunapenda kuwasisitiza vijana wote wa CHADEMA hususani wenye nia ya kugombea kuwa makini katika masuala haya. Tusingependa kuona vijana wanafifisha ndoto zao za kugombea nafasi ndani ya baraza kwa kukiuka tu taratibu hizi.
Imetolewa leo tarehe12.08.2014 Jijini Dar es salaam na;
Ester Daffi
Naibu Katibu Mkuu – BAVICHA

SPIKA BUNGE LA NIGER ATOROKA KWA KASHFA YA KUUZA WATOTO, ALISHATANGAZA KUWANIA URAIS 2016

Spika wa Bunge la Niger ametoroka nchini humo baada ya kamati ya bunge hilo kuafiki kukamatwa kwake kuhusiana na kashfa ya kuwauza watoto. 
     Hama Amadou, ambaye tayari ameelezea azma yake ya kugombea urais mwaka 2016, anasema kuwa madai hayo dhidi yake yamechochewa kisiasa.
Mke wa pili wa spika huyo na watu wengine 16 walikamatwa mwezi Juni baada ya kutuhumiwa kuwauza watoto wachanga Kusini Mashariki mwa Nigeria. Watoto hao huuzwa kwa maelfu ya dola kila mtoto.

Mwandishi wa BBC nchini Niger anasema kuwa kesi hiyo imetoa fursa tosha kwa chama tawala kumuondoa Bwana Amadou kutoka katika chama hicho tangu kukosana na muungano tawala.

Kashfa hii pia imewashtua wengi katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu hasa kwa kuwa ni kosa kuonyesha kuwa watoto walioasiliwa na wako binafsi.

Imeripotiwa kuwa baadhi ya wanawake walidai walikuwa wajawazito na kwenda Nigeria kabla ya kurejea na watoto wao.

Kamati kuu ya bunge la taifa ambalo linamjumuisha naibu spika na wakuu wengine wa kamati nyinginezo, walikutana Jumatao, na kukubaliana kuwa polisi wanaweza kumkamata na kumhoji bwana Amadou kuhusiana na tuhuma hizo.

Wanasiasa sita wa upinzani walikataa kuhudhuria vikao hivyo ingawa idadi ya wabunge waliofika ilitosha kutoa uamuzi.

Kikao kamili cha bunge kitahitajika kufanyika ili kuondoa uwezekano wa bwana Amadou kushitakiwa.

Inadaiwa watoto 30 wameuzwa katika kashfa hii ambayo imehusisha kutengeza stakabadhi bandia na kubadili vyeti vya kuzaliwa vya watoto waliouzwa. 

Chanzo: ccm blog

MTEMVU: CCM ITAUPUKUTISHA UPINZANI TEMEKE UCHAGUZI WA MITAA, SIYO KWA KUTUMIA NGUVU ILA MATUNDA YA UTEKELEZAJI ILANI



Na Bashir Nkoromo
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ametamba kuwa, CCM itapukutisha kwa kishindo upinzani wote katika jimbo hilo kwa kushinda mitaa yote katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

"Wala hatutatumia nguvu bali tutaichukua mitaa yote hata hiyo michache iliyopo sasa chini ya upinzani, kwa kutumia mtaji wa mafanikio makubwa tuliyoonyesha katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi hiki", alisema Mtemvu.

Mtemvu alitoa tambo hizo wakati akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Jumuia ya Wanawake Tanzania, Kata ya Azimio, kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Sokoine, katika Kata hiyo, Temeke jijini Dar es Salaam.

Alisema, CCM inao uhakika wa kutwaa viti vyote hadi kurejesha vichache vilivyopo sasa chini ya upinzani kwa kuwa mengi ambayo CCM iliahidi kupitia yeye wakati akiomba kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliopita yamefanyika.

Mtemvu alitaja baadhi ya yaliyotekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ambazo karibu zote zimeboreshwa kwa kujengwa kwa kiwngo cha lami tofauti na awali ambapo ilikuwa kero kubwa kwa kuwa zilikuwa hazipitiki kutokana na ubovu tena za vumbi.

"Zamani nilikuwa kila nikisimama jukwaani mnaniolea matatizo na kero lukuki hasa kuhusu hizi barabara, sasa leo hatuzungumzii matatizo ya barabara, tunazungumzia tu sasa kuboresha taa kwenye mitaa na barabara hizi", alisema Mtemvu.

Alisema, kuanzia mwezi huu Septemba, taa zote katika barabara na mitaa kwenye jimbo hilo zitawaka ambapo sasa zinafanyiwa maboresho ili zitumie nishati ya jua (solar) ili kupunguza changamoto ya gharama za malipo ya umeme wa taa hizo.

Mtemvu alisema, kukamilika kwa taa hizo itakuwa janga kwa vibaka ambao wamekuwa wakitumia fursa ya giza kujificha wakati wakivizia kuiba kwenye nyumba za watu na pia kukwapua wapitanjia nyakati za usiku.

Alisema mbali na kuboresha barabara CCM pia kupitia uongozi wake imeweza kuboresha hali za wananchi hasa kina mama na vijana kwa kuviwezesha vikundi vyao vya ujasiriamali kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ambapo sasa zaidi ya vikundi 100 vimenufaika.

Mtemvu aliahidi kuendelea kushirikiana na wabunge wengine wa Temeke na mkoa wa Dar es Salaam kwa jumla kuhakikisha watendaji wabovu serikalini wanakabwa koo ili wawajibike ipasavyo kutumikia wananchi.

Pia aliahidi kuhakikisha anaedelea kupigania kupatikana kwa mazingira bora ya kufanya kazi zao mamalishe na bodaboda kwa kuwa wana mchango mkubwa katika maendeleao ya jamii.

"Najua haiwezekani bodaboda zote zikaingia mjini, lakini tunachofanya ni kupigania kuhakikisha unakuwepo utaratibu mzuri utakaowezesha baadhi kufika mjini bila kuharibu taratibu na sheria zilizopo. Pia Mamalishe kwa kuwa lazima waendelee na shughuli zao tunawatafutia utaratibu bora kufanya shughuli zao kwa amani badala ya kukimzwa kimbizwa na mgambo kila mara", alisema Mtemvu.

Katika mkutano huo, uliosheheni burudani mbalimbali ikiwemo msanii Omari Tego kuimba wimbo maalum wa CCM ambao ulikonga nyoyo za waliohudhuria, Mtemvu aligawa kadi kwa wanachama wapya 45 wa UWT.

HABARI KATIKA PICHA KUHUSU MKUTANO HUO
Mbunge wa Temeke, Abbas  Mtemvu akihutubia mkutano wa hadhara uliofabyika kwenye Uwanja wa shule ya Sokoine, Temeke jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 30, 2014.
Mtemvu akishangiliwa wakati akihutubia mkutano huo wa hadhara
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimpa kadi ya Uanachama wa UWT Maridha Rajabu wakati wa mkutano huo, wanachama wapya 45 wa jumuia hiyo walipewa kadi
Mbunge wa temeke,  Mtemvu akimtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Mbunge wa temeke,  Mtemvu akimpongeza baada ya kumtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Umati wa wananchi ukiwa umefurika wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Azimio, Tatu Hassan akifungua mkutano huo, kwenye Uwanja wa Sokoine Temeke kabla ya kuhutubiwa na Mtemvu
Diwani wa Kata ya Azimio, Hamisi Mzuzuri akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo wakati wa mkutano huo
Ofisa Kutoka Makao Makuu ya CCM, Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Gifti Isaya akipata picha kupitia simu yake kwenye mkutano huo
Waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo. Wapili walioketi kulia ni Ofisa katika Idara ya Mambo ya Nje Makao Makuu ya CCM,  Gift Isaya akifuatilia kwa makini pamoja na wenzake
Msanii Yusuf Peter wa Kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha vimbwanga vyake mbele ya mke wa Mbunge wa Temeke  Mama Mtemvu (kulia)
Msanii Ahmadi Juma wa kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha uhodari wa 'kula' moto wakati kikundi hicho kikitoa burudani wakati wa mkutano huo
Mtemvu akiwatuza wasanii waliotia fora uwanjani wakati wa mkutano huo. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog

Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu Mchakato wa Katiba

Sisi, wajumbe wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, tuliokutana tarehe 27 hadi 28 Agosti, 2014, Dar es Salaam , tumepata fursa ya kutafakari, kujadili na kujielimisha kwa kina yaliyomo katika Rasimu ya pili ya Katiba na mjadala unaoendelea katika Bunge Maalumu la Katiba. Baada ya mjadala wa kina, tunatoa tamko letu kama ifuatavyo:
Tunaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilikusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko hayo na kutuletea Rasimu yenye maoni mengi ya Watanzania bila kujali dini zao, upande wa Muungano walikotoka, hali zao za kimaisha, jinsi na kabila.
Pia tunaipongeza Tume kwa kuandaa nyaraka na kumbukumbu mbalimbali kama Randama, Nyaraka zenye maoni ya wananchi, picha, tafiti mbalimbali na hata orodha ya watu walioshiriki kutoa maoni katika Tume. Tume pia iliweza kuandaa tovuti iliyokuwa na kumbukumbu za Tume na maoni yote yaliyotolewa. Kazi hii ni ushahidi kuwa Tume iliandaa rasimu kwa weledi na kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuzingatia maoni ya wananchi.
Tume imedhihirisha kuwa, ilitenda kizalendo na kwa mantiki hiyo, wajumbe wote bila kujali vyama vyao, dini zao na upande wa Muungano walikotoka, waliweza kujadili kwa uwazi na kweli na mwisho wakaridhiana katika kila Ibara iliyopendekezwa. Hili linatufundisha kuwa Katiba ni maridhiano na si jambo la masilahi ya kisiasa, bali ni suala la masilahi ya wananchi.
Tunaamini kuwa kila mjumbe wa kamati ya kukusanya maoni ya wananchi aliheshimu kiapo chake na hivyo kufanya kazi waliyokabidhiwa kwa uaminifu na uadilifu na ya kwamba hawakushawishiwa au kupokea rushwa kutoka kwa kundi, dini au chama chochote cha siasa wakati wa zoezi hili.
Baada ya Tume kuwasilisha rasimu kwenye Bunge Maalumu la Katiba, Taifa likaanza kushuhudia “uasi wote na uovu wa wanadamu wapingao kweli kwa uovu” (Warumi 1:18). Katika mijadala ya Bunge Maalum la Katiba (BMK) yakaanza kujitokeza mambo mengi yasiyo ya masilahi kwa wananchi, na ukiukwaji wa sheria na kanuni. Mambo kadhaa yanadhihirisha hili:
Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilifungwa bila sababu za msingi kutolewa wakati mchakato unaendelea. Hali hii imefanya zile nyaraka na kumbukumbu zilizoandaliwa kwa ajili ya rejea na kuwezesha mjadala wa Rasimu ya Katiba kuendelea katika mwanga na ufahamu wa nyaraka hizo kutowezekana kabisa. Kwa sababu hiyo, tumeona Bunge Maalumu la Katiba likiendelea kupotosha takwimu na taarifa mbalimbali ambazo wananchi hawawezi kuzipata kwa ajili ya kuoanisha baina ya kinachojadiliwa bungeni na kilichomo katika rasimu na viambatanisho vyake vyote. Tunajiuliza jambo hili limefanywa na nani na kwa masilahi ya nani?
Bunge la Katiba limeshindwa kusimamia kanuni kama ambavyo zilipendekezwa na kuridhiwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba. Kushindwa huku kusimamia kanuni kumesababisha vurugu ndani ya Bunge Maalumu na kumekwamisha matarajio ya wananchi kupata Katiba bora ya nchi yetu. Matumizi ya ubabe na wingi wa wabunge wa Chama Tawala (CCM), badala ya kanuni za Bunge na maridhiano, kumefanya mchakato wa Katiba kuhodhiwa na Chama Tawala dhidi ya maslahi ya wananchi.
Mijadala katika Bunge Maalumu la Katiba imekuwa ya kejeli, matusi, vitisho, ubabe na kupuuza hata kupotosha maoni yaliyotolewa na Wananchi kwa Tume. Hali hii imelifanya Bunge Maalumu la Katiba kupuuzwa na hivyo kupoteza heshima na hadhi yake. Matokeo yake baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wakaamua kususia vikao vya bunge na wengine kuendelea, bila kukumbuka kuwa Katiba ni matokeo ya tendo la maridhiano na si suala la masilahi ya kikundi cha watu wachache.
Hatua iliyofikiwa ni dhahiri, Mjadala wa BMK unaoendelea umeondoa kwa kiasi kikubwa maoni yaliyotolewa na wananchi kuhusu muundo wa Muungano, kupunguza mamlaka ya Rais, uwajibikaji na uwajibishwaji wa wabunge, ukomo wa ubunge, n.k., na kuwezesha maoni na masilahi ya chama tawala kwa uongozi wa kikundi cha wanasiasa wachache wasio na uaminifu na uadilifu wa kutosha kuwekwa kama mapendekezo ya Katiba Mpya kwa nia ya kulinda masilahi binafsi au ya makundi na kuhalalisha ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na maadili ya uongozi bora.
Baada ya kujadili na kuona haya na mengine mengi, Jukwaa la Wakristo Tanzania lina maoni yafuatayo;
1. Kwamba Serikali (Wizara ya Katiba na Sheria) irudishe tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na nyaraka zake zote kwa ajili ya wananchi kuendelea kuona kazi waliyoifanya, kujifunza na kujadili Rasimu ya Katiba kwa uwazi.
2. Kwamba maoni ya wananchi hayawezi kufutwa na kudharauliwa na chama tawala. Hivyo basi, Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea lijadili na kuboresha tu maoni yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na siyo kufanya mabadiliko katika Katiba ya mwaka 1977.
3. Kwamba mchakato wa Katiba usimamishwe ili kupisha majadiliano, maelewano na maridhiano mwafaka, uchaguzi mkuu na wa serikali za mitaa. Na mabadiliko ya Katiba ya 15 ya mwaka 1977 yafanyike kuwezesha chaguzi kufanyika kwa uwazi na haki. Pia, kuweka kifungu kitakacholinda Rasimu ya pili na kumtaka kiongozi ajaye kuendelea na mchakato wa Katiba.
4. Kwamba baada ya Bunge Maalumu la Katiba kuanza shughuli zake tena, Mwenyekiti wa Bunge hilo afanye kazi kwa mujibu wa kanuni na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba badala ya kutumia ubabe na kiburi cha wingi wa wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi katika Bunge la Katiba.5. Kwamba wananchi waendelee kusoma na kujadili maoni yaliyoko katika Rasimu ya pili ya Katiba, na kufuatilia kitakachokuwa kinajadiliwa kwenye Bunge la Katiba ili kuwawezesha kupiga kura ya maoni wakiwa na uelewa wa kutosha kabisa kuhusu ni nini kipo kwenye “Katiba inayopendekezwa”. Wananchi pia wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa nia ya kuwawezesha kupiga kura ya maoni.
6. Kwamba tunaomba Tume ya Mabadiliko ya Katiba ihuishwe na kupewa mamlaka kisheria ili kuiwezesha kujibu maswali yanayojitokeza na kutoa ufafanuzi kwa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa jumla hadi Katiba Mpya itakapokamilika na kukabidhiwa rasmi.
Jukwaa la Wakristo Tanzania na Watanzania wote wanaoitakia nchi yao mema, tunakuomba Mheshimiwa Rais kwamba amani ya nchi yetu sasa imo mikononi mwako hasa katika kipindi hiki cha kuandikwa kwa Katiba Mpya. Tunakuomba uahirishe mchakato unaoendelea ili uepushe ishara za aina mbalimbali za kuanzisha sintofahamu nchini mwetu na hali yoyote inayoweza kuathiri mshikamano, umoja na amani ya Taifa letu.
Ifahamike kuwa wananchi wa Tanzania wako juu ya Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi. Kwa mantiki hiyo, tunakuomba uepushe wananchi wa Tanzania kuhamasishwa kukikataa Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa tu chama hicho kimeyapuuza na kimekataa maoni yao waliyotoa kwa dhati baada ya kuaswa na kuhimizwa kufanya hivyo na viongozi wa nchi.
“Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”. (Rejea Warumi 1: 28-32)
Ikumbukwe kuwa Rasimu ya Pili ya Katiba bni waraka halali na rasmi na ndiyo mawazo ya Watanzania na tunahimiza kuwa Katiba ni ya wananchi na inahitaji maridhiano na sio ubabe.Imetolewa na Tanzania Episcopal Conference (TEC) The Council of Pentecostal Churches of Tanzania (CPCT) Christian Council of Tanzania (CCT) The Seventh Day Adventists (SDA)

Hali hairuhusu kupata Katiba


Mchungaji Antony Lusekelo akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa Mwananchi, kanisani kwake Ubungo Kibangu jana. Picha na Kelvin Matandiko. 
Na Goodluck Eliona na Fidelis Butahe, MwananchiWakati Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakitarajiwa kuendelea na vikao mjini Dodoma kesho, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony Lusekelo, amesema kuwa hali ya kisiasa hairuhusu nchi kupata Katiba Mpya kwa sasa, akishauri Bunge hilo kusitishwa hadi baada ya uchaguzi mkuu mwakani.
Lusekelo pia ameonya wajumbe wa Bunge hilo akisema iwapo wataendelea na mchakato huo, Katiba itakayoandikwa itakataliwa na wananchi baadaye hivyo kuwa wamepoteza muda na fedha za walipakodi bure.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini hapa juzi, Mchungaji Lusekelo alisema kuwa Mchakato wa Katiba Mpya, umevurugika kutokana na wanasiasa kujiona miungu watu na kukataa kusikiliza ushauri wanaopewa.
“Kwa upande wangu, kama viongozi wangekuwa wanatusikiliza, mchakato huu usingefika ulipofika leo. Hii misukosuko isingetokea, wanasiasa wetu wana tatizo hilo. Ni miungu watu, wana shingo ngumu utafikiri Farao,” alisema Mchungaji Lusekelo.
Mchungaji huyo anayefahamika zaidi kwa jina la Mzee wa Upako, alisema kuwa viongozi hawataki kusikiliza ushauri kutoka kwa watu wengine kwa sababu wanaamini kuwa wamesoma, wana hekima, wamesafiri sana na wanaijua nchi kuliko mtu mwingine.
“Kwa hiyo tatizo limeanza baada ya wanasiasa kuweka pamba masikioni. Nchi inahitaji uwanja mpana zaidi wa mawazo ndipo unaweza kuijenga, hasa katika mfumo wa sasa wa uhuru wa habari na vyama vingi. Dunia ya sasa siyo ya mwaka 1970,” alisema na kuongeza:
“Ni busara tu, haihitaji kwenda shule, kusema kuwa sisi tunaijua nchi, nani asiyeijua nchi yake? Kwani sisi ni Wazambia? Kila mtu anaijua nchi yake katika eneo lake.
“Iwapo viongozi watalazimisha kupatikana kwa Katiba Mpya, haitakuwa na uzito, itapoteza heshima muda mfupi kwa kuwa itapingwa na wananchi.
“Kwa hiyo, mtapata hasara kubwa sana kwamba mlitumia Sh75 bilioni kwa Warioba (Jaji Joseph Warioba, Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na bilioni kadhaa kwenye Bunge la Katiba. Atakayeumia sana Katiba Mpya ikianguka ni yule aliyeanzisha wazo. Tanzania haiwezi kuandika Katiba katika mazingira haya.”
Aliongeza kuwa katika hali ya kawaida hauwezi kuanzisha mashindano ya mbio ukiwa peke yako halafu ukajipongeza kwa kushinda.
“Au mpira uko peke yako, unafunga goli, halafu unasema ehhh nimefunga, haiwezekani,”alisema.
Kiongozi huyo, alisema kwamba anaamini Rais ajaye wa awamu ya tano, ataweza kuwaunganisha wananchi waliotofautiana kutokana na Mchakato wa Katiba kwa kuwa mazingira ya sasa hayawezi kuwapa wananchi Katiba wanayoitaka.
“Mwaka 2016 unamwacha rais wa awamu ya tano atusaidie kuirudisha nchi pamoja, tuligawanyika, unaponya majeraha halafu mwaka 2017 Bunge la Katiba linaendelea,” alisema.
Hata hivyo, alieleza kwamba kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kufanyika, Bunge la Jamhuri ya Muungano litapaswa kufanyia marekebisho baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya sasa vinavyolalamikiwa, ambavyo ni suala la mgombea binafsi, Tume ya Uchaguzi na madaraka ya Rais.
“Rais apunguziwe madaraka kidogo kwa sababu Rais wa Tanzania ana madaraka makubwa mno, ukimtoa Mungu anakuja yeye. Bahati, Mungu ametusaidia katika vipindi vinne, tumepata marais ambao tumeishi kwa huruma zao,” alisema.
Vilevile aliwataka wanasiasa kukumbuka kuwa amani na chakula kinachopatikana nchini leo ni matokeo ya mazingira yaliyoandaliwa na viongozi miaka ya 1960 na 1970 na kwamba uamuzi wowote wanaofikia leo lazima ukusudie kulinufaisha taifa kwa miaka mingi ijayo.
“Viongozi wa sasa hivi hawataki kutengeneza mazingira ya miaka 30, 40 ijayo, hawajui jamii lazima ibadilike, sasa wakati wote mabadiliko ukiyasubiri yaje huwa yanajileta na maafa sana,” alieleza.
Joto la uchaguzi
Akizungumzia kuhusu joto la kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2015, Mzee wa Upako alisema unatarajiwa kuwa mgumu kwa kuwa tayari watu wenye majina makubwa wameshaanza kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu nchini.
“Ingekuwa nafuu kama rais huyu anaendelea, lakini tunabadilisha rais na ukisoma hisia, unaona wanaogombea urais hata ndani ya CCM ni wakubwa, siyo watu wadogo, wana makundi makubwa kwenye chama chao,” alisema.
Alibainisha kuwa kutokana na mchakato wa urais kuanza chini kwa chini, baadhi ya wananchi na viongozi wameanza kugawanyika kila mtu akimtaka rais atakayenufaika naye.
Pia, alisema katika uchaguzi huo, siyo vyema kupuuza nguvu ya vyama vya upinzani kwa kuwa vina wafuasi wengi baadhi ya maeneo nchini.
“Unaweza kupuuza nguvu ya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF huku Tanzania Bara, lakini huwezi kupuuza nguvu ya CUF Zanzibar. Wabunge wote wa CUF na wawakilishi wao hawapo kwenye Bunge la Katiba, ukitoa Hamad Rashid hawako wote. Nguvu ya kisiasa Zanzibar kati ya CUF na CCM ni asilimia moja kwa 49,” alisema.
Sifa za Rais ajaye; vijana wakae kando
Akizungumzia kuhusu sifa za rais ajaye, alisema hata ikitokea kijana mwenye miaka 45 akiingia katika kinyang’anyiro hicho, hawezi kupata nafasi kwa kuwa umri huo hautoshi kulifahamu taifa vizuri.
“Naamini katika umri, unaweza kusema Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na miaka 38 alipokuwa Waziri Mkuu, hayo yalikuwa ni mazingira ya wakati ule, lakini siyo kama leo,” alisema na kuongeza:
“Rais anatakiwa kuanzia miaka 50 na kuendelea, huo ndio ukweli hata kama watasema urais ni taasisi kwa miaka 40 umeijua nchi wapi? Hata akina Nyerere (Julius Nyerere) iliwasumbua sana.”
Alizitaja sifa nyingine kuwa ni pamoja na kujua matatizo ya Watanzania ukiwamo umaskini, uzalendo, mwadilifu ambaye hana kashfa, siyo mdini wala mdhehebu, rais ambaye ataendelea kuwaunganisha Watanzania na atakayesimamia Katiba ya nchi.
“Sijajua Katiba ya sasa itaitamkaje Zanzibar, tupate watu wanaosimamia Katiba, sasa unaona Katiba ya Zanzibar imevunja Katiba ya Jamhuri wa Muungano. Tunataka rais wa awamu ya tano ambaye ni jasiri, ukicheza na matendo yanayoshiria uvunjifu wa amani rais anakuwa mkali kwa wahalifu,” alisema.
Kuhusu baadhi ya watu wanaotajwa kutaka kugombea urais, alisema baadhi yao wana sifa alizozitaja isipokuwa wale ambao walishakuwa kwenye madaraka wakashindwa kuleta maendeleo.
“Sasa wewe serikalini ulisahau nini? Ulikaa pale miaka yote, chochote haujaonyesha, sasa unataka kurudi tena kwa njia nyingine, haiwezekani. Hauwezi kupata mabadiliko kwa kutumia watu walewale kwa njia zilezile, kwa hiyo lazima upate watu ambao hawajawahi kushika madaraka makubwa ya nchi au walishika madaraka makubwa walionyesha utendaji.”
Kuhusu maadili ya viongozi wa umma
Mzee wa Upako alisema ingawa hakuna kipimo cha mtu aliyejilimbikizia mali, viongozi wanaofanya hivyo ni wale yenye hofu na wasio na uhakika na maisha yao baada ya kustaafu.
“Sisi hatukatai mtu kuwa na mali, lakini apate katika njia iliyokuwa halali. Haumizi wenzake na kuliingiza taifa kwenye mikataba isiyo na tija. Binadamu anastahili kula, hastahili kuwa mlafi, anastahili kuwa na mali, lakini siyo mali iliyopitiliza katikati ya watu maskini,” alisema.
Akitoa mfano namna maisha ya viongozi wa umma na watoto wao yalivyokuwa miaka ya 1970, alisema: “Mimi nimesoma na watoto wa Mkuu wa Mkoa Mwakabongo, wadogo zake Waziri Mwakawago, watoto wa Makweta shule moja. Wote tulikuwa tunavaa makobazi.”
Alisema hali ni tofauti hivi sasa, ambapo kuna shule za maskini na matajiri. Viongozi waliojilimbikizia mali ni vizuri wakaifikiria zaidi jamii, maana ikisambaratika hata mali yao haitakuwa na thamani.
“Hata ukikimbilia Ulaya kunakuwa kuzuri tu kama nyumbani kuna amani. Nasema wenzetu wenye dhamana wafanye jitihada kulitoa taifa kwenye umaskini.”
Vitega uchumi na amani nchini
Mzee wa Upako, alisema kuwa baada ya miaka 10 Tanzania haipaswi kuwa katika hali ya kiuchumi iliyonayo sasa na kwamba kama hakutakuwa na mabadiliko, amani itatoweka nchini.
“Kama nchi hii itakuwa maskini hivi kwa miaka 10 ijayo usitegemee itakuwa kisiwa cha amani tena. Huku chini kumeshaanza kuteketea, ukipata ajali hapa watu hawakimbilii kukuokoa wanakimbilia kukusachi. Viashiria vimeshaanza kuonyesha kwamba watu wanaendekeza njaa, kuliko utu wao.

Freeman Mbowe apata ‘mbabe’ mwenzake


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk (aliyevaa gwanda) akirudisha fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa wa chama hicho. Waliomzunguka ni walinzi wake. Na Mpigapicha Wetu 
Na Ibrahim Yamola, MwananchiDar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk amejitokeza ‘kupimana kifua’ na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe katika uchaguzi wa ndani unaotarajiwa kufanyika Septemba 14.
Mbarouk alirejesha fomu hizo makao makuu ya Chadema jana mchana huku akikumbana na kizingiti cha kuzuiwa na walinzi kuingia ndani kurejesha fomu akiwa pamoja na waandishi wa habari na hata alipotoka nje hakutakiwa kuzungumza na waandishi hao karibu na jengo hilo.
Ili kuepusha vurugu, Mbarouk alitoka eneo hilo na kuanza kuzungumza na waandishi wa habari kwa kusema, “Hili ambalo limenipata kwa kuzuiwa nisipigwe picha wakati nikirejesha fomu nikiingia madarakani nitahakikisha narejesha usawa ndani ya chama hiki na katiba inazingatiwa.”
Aliongeza, “Jambo la pili kulifanya nitahakikisha wanachama wote ndani ya Chadema wanakuwa na haki sawa, hakuna atakayeonewa na atakayevunja katiba kwa njia zozote zile atachukuliwa hatua kali, hakuna atakayekuwa juu ya katiba ya Chadema.”
Juzi, Mbowe alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’.
“Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
Mbarouk alisema, kulingana na katiba ya chama Mbowe amemaliza muda wake wa uongozi na anatakiwa kukiachia kiti hicho kiongozwe na mtu mwingine.
“Mimi nimekuwa mwenyekiti wa mkoa (Tabora) kwa kipindi cha miaka 10 nikaamua kuachia ili wengine waendeleze vivyo hivyo na Mbowe ameongoza kwa miaka kumi anatakiwa kuachia ngazi, na hii ni nafasi yangu imewadia kuiongoza Chadema kufika Ikulu 2015,” alisema Mbarouk.
Huku akisisitiza alisema, “Kauli aliyoitoa Mbowe ya kusema anayetaka kujipima kifua naye ajitokeze ni ya kuwatisha wanachama wasijitokeze, lakini mimi siwezi kutishika na ndiyo maana nimejitokeza kupimana naye kifua na ninajua nitamshinda kwani katiba ikizingatiwa tu hawezi kunishinda.” Uchaguzi huo utatanguliwa na wa Baraza la Vijana Taifa la Chadema, (Bavicha) utakaofanyika Septemba 10 huku Septemba 11 ukifanyika wa Baraza la Wanawake (Bawacha).
Hadi dirisha la urejeshaji fomu linafungwa jana saa 10.30 makada mbalimbali walikuwa wamejitokeza kuwania nafasi hiyo miongoni ni Daniel Madiba anayewania Mratibu Mhamasishaji taifa wa Bavicha na wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Lutiger Haule nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu kupitia Vijana. Haule alisema anataka kuwatumikia vijana katika kupata haki zao na atatumia nafasi hiyo kuwapigania kwa nguvu zote katika harakati za kusaka ukombozi wa pili unaominywa na CCM.
Ushindani ndani ya Bawacha unatarajiwa kuwa kati ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge Viti Maalum, Chiku Abwao na makada wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda kwa nafasi ya mwenyekiti.
Katika hatua nyingine, nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Baraza la Wanawake ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), imeendelea kupata wagombea baada ya Aisha Yusuf kuchukua fomu na kuirejesha kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza katika ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Aisha alisema kuwa amelazimika kuwania wadhifa huo kutokana na kuwa na uwezo wa kutosha. “Hivi sasa ukiangalia wanawake wengi bado wapo nyuma hivyo ni wakati wa kuondokana na dhana hiyo ndiyo maana nami nimelazimika kuomba nafasi hiyo,” alisema Aisha.
Alisema kuwa tangu alipojiunga na chama hicho mwaka 2007 amepata uzoefu ikiwamo kuwa Mwekahazina wa Bawacha Kata ya Saranga hivyo ameomba ngazi ya juu zaidi ili aweze kuwatumikia wananchi kwa ukaribu.
Aisha alisema kuwa ni vyema wanawake wakatambua wao ni jeshi kubwa linaloweza kuleta mabadiliko ndani ya Tanzania akieleza kwamba sasa taifa lina matatizo makubwa hivyo wanawake wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu ili kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
“Wanawake ni lazima tuwe jasiri ni lazima tuondokane na mifumo dume inayotukandamiza hiyo itatusaidia tupate nafasi za juu za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao,” alisema.
Aisha alisema kuwa anaamini kuwa taifa hili litaweza kupata maendeleo zaidi ikiwa wanawake wengi watapata nafasi nyingi za uongozi.

Mlipuko wamuua mtu mmoja mjini Paris.


Jengo lililolipuliwa

Mlipuko umeharibu jengo moja la ghorofa 4 kazkazini mashariki mwa Paris na kumuua mvulana mmoja huku watu kadhaa wakiwa hawajulikani walipo.
Watano kati ya wale waliotoweka wanadaiwa kuwa watoto.
Afisa mmoja wa huduma ya zima moto katika mji huo mkuu amesema haijulikani ni nini kilichosababisha mlipuko huo.
Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa matibabu wamepelekwa katika eneo hilo.

Bunge Maalumu giza nene


 Rais Jakaya Kikwete.PICHA MAKTABA 
Na Neville Meena, MwananchiDodoma. Kadiri siku zinavyosogea kitendawili kuhusu hatima ya Bunge Maalumu kimeendelea kuwa kigumu na sasa kinachosubiriwa ni matokeo ya mkutano baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa ambavyo ni wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Awali kikao hicho baina ya Rais Kikwete na viongozi hao kilipangwa kufanyika jana mchana, lakini kiliahirishwa hadi leo saa tano asubuhi kutokana na Rais kukabiliwa na majukumu mengine yanayohusiana na ziara yake inayoendelea mkoani Dodoma.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zinasema taarifa ya kuahirishwa kwa kikao hicho ilitolewa juzi usiku kwa wahusika ambao wote ni viongozi wa vyama vya siasa, na kwamba wale walioko Dar es Salaam watasafiri leo kwa ndege maalumu hadi Dodoma ambako watashiriki mkutano huo.
“Mkutano umeahirishwa hadi kesho (leo) saa tano asubuhi na utafanyika hapahapa Dodoma. Ratiba ya Mheshimiwa Rais kwa leo (jana) haikuruhusu kwa hiyo wahusika waliarifiwa tangu jana (juzi) usiku,” kilisema chanzo chetu.
Rais Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani Dodoma na jana ilikuwa siku yake ya tatu alipotembelea Wilaya ya Chamwino. Leo baada ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa, Rais Kikwete atalihutubia taifa pale atakapokuzunguza na wazee wa Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango.
Matokeo ya mkutano wa Rais Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa yanasubiriwa kwa shauku kubwa kwani huenda yakatoa mwelekeo wa nini kinafuata baada ya kuwapo kwa mkwamo wa mchakato wa Katiba, ambao hivi sasa umefikia katika hatua ya Bunge Maalumu.
Licha ya kwamba Kamati za Bunge hilo zimemaliza kazi yake, lakini kuna wasiwasi kwamba kile kilichojadiliwa kitakosa uhalali wa kisiasa kutokana na kutoshirikisha wajumbe ambao ni wanachama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Ukawa walisusia Bunge hilo Aprili 16 mwaka huu kwa madai ya kwamba hawaridhishwi na mambo yanavyokwenda na wameapa kwamba kamwe hawatarejea bungeni kutokana na sababu ambazo hivi sasa zimebadilika tofauti na zile walizokuwa wakizitoa awali.
Awali viongozi hao walikuwa wakidai kwamba walisusia Bunge Maalumu kutokana na CCM kutumia wingi wao kubadili maudhui ya rasimu iliyotungwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini sasa wanasema pamoja na hilo kuendelea na mchakato ni kufuja fedha za umma kwani hakuna uharaka wa kupatikana kwa Katiba mpya.
Badala yake Ukawa kupitia kwa viongozi wao ambao ni wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR Mageuzi, wamesikika mara kadhaa wakidai kwamba hivi sasa taifa linapaswa kujielekeza katika mambo muhimu yakiwamo uandikishaji mpya wa daftari la kudumu la wapigakura, maandalizi ya bajeti ya mwisho ya uongozi wa awamu ya nne na maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015.
Kikao cha leo
Kwa kuzingatia mazingira hayo, kikao cha leo kinaweza kisijikite katika kuwashawishi Ukawa kurejea bungeni, bali kuangalia jinsi ya kusitisha Bunge hilo bila kuleta madhara makubwa ya kisiasa kwa pande zote zinazohusika katika mgogoro unaoendelea.
Kumekuwa na mawazo kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Rais hana uwezo wa kusitisha Bunge, lakini baadhi ya watumishi wa umma wanasema kiongozi wa nchi anaweza kutumia mamlaka yake (prerogative powers) alizopewa na Katiba kusitisha kuendelea kwa taasisi hiyo.
“Pengine kuvunja ni tatizo lakini kwa nafasi yake kama Mkuu wa Nchi, Rais anaweza kusitisha Bunge Maalumu maana ni kama anavyoweza kuteua mawaziri, hakuna mahali amepewa ruhusa ya kuwaondoa, lakini huwa akishateua mwingine maana yake yule aliyepo ameondoka,” alisema mtaalamu mmoja wa masuala ya utumishi serikalini na kuongeza:
“Kwa hiyo hilo Bunge yeye mwenyewe ndiye aliyetoa GN ya kulianzisha na wanasema siku alizotoa ni chache kwa hiyo wanataka huyohuyo atoe GN nyingine kuongeza kwa maana ya kufuta ile ya kwanza. Kwa hiyo anaweza kutoa GN ya kusitisha tu na siyo kosa kisheria”.
Wapinzani kwa upande wao wamekuwa wakijenga hoja kwamba hata kama Katiba itapitishwa hakuna fursa ya kupigiwa kura ya maoni kama sheria inavyoelekeza kutokana na muda kutoruhusu.
Mmoja wa viongozi wa Ukawa, Freeman Mbowe aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba uandikishaji wa wapigakura katika daftari la kudumu ni kazi inayohitaji muda usiopungua miezi sita, ikizingatiwa kwamba tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshaweka bayana kwamba daftari la sasa halifai.
NEC ilipokutana na vyama vya saisa ilitangaza kwamba uandikishaji mpya wa wapigakura ungeanza kesho, Septemba 1, 2014 lakini hadi jana hakukuwa na dalili zozote za kuanza kwa kazi hiyo.
Changamoto ya muda
Habari kutoka ndani ya Serikali zinasema muda ni moja ya mambo yanayoifanya Serikali kuona umuhimu wa kusitisha Bunge kwani mbali na mambo makubwa ya kitaifa yaliyotajwa, vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi vinapaswa kuanza katika muda ambao vinaweza kuingiliana na Bunge Maalumu.

Wakati Bunge la Muungano likitarajiwa kukutana kuanzia Novemba 4, 2014, Katibu wa Bunge Maalumu ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Yahya Khamis Hamad alisema jana kwamba vikao vyake vilipangwa kuanza katikati ya Oktoba.
Kwa kawaida vikao vya Bunge hutanguliwa na wiki mbili za vikao vya kamati za kudumu na ikiwa ratiba itabaki kama ilivyo basi vitaingiliana na vikao vya Bunge Maalumu ambalo ratiba yake imepangwa kuendelea hadi Oktoba 31.
Awali Bunge Maalumu lilipaswa kukutana kwa siku 60 katika awamu yake ya pili kama zilivyoongezwa na Rais Kikwete Julai 28 mwaka huu na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali (GN) namba 254 ya Agosti 1, 2014.
Katika gazeti hilo, Bunge Maalumu lilipaswa kuanza Agosti 5, 2014 na kumalizika Oktoba 4, lakini ratiba rasmi ya Bunge hilo inaonyesha kuwa litamalizika Oktoba 31, baada ya kuhesabiwa kwa siku za kazi tu badala ya siku za kalenda.
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta Jumatatu hadi Ijumaa ndizo kisheria ambazo wajumbe wanapaswa kufanya kazi na kwamba Jumamosi na Jumapili siyo sehemu ya siku 60 zilizoongezwa na Rais.
Kutokana na hali hiyo, kulikuwa na jitihada za kubadilishwa kwa taarifa ya Rais kwenye Gazeti la Serikali ili kuzingatia mabadiliko hayo, lakini hadi jana Hamad alisema walikuwa hawajapokea maelekezo ya ziada tofauti na yale ya awali.
“Bado tunasubiri maelekezo au niseme ufafanuzi kutoka serikalini maana haya mambo ni ya kisheria kwani hadi sasa ile GN ya kwanza bado haijabadilika,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi (BLW).
Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Job Ndugai alisema kwa jinsi ratiba ya Bunge Maalumu ilivyopangwa lazima itaingilia na shughuli za Bunge la Muungano, hivyo lazima uamuzi ufanywe ili kuepusha adha hiyo.
“Sisi tumeishaliona hilo kwamba ni changamoto, tulikuwa tukijaribu kujadiliana kuona kama baadhi ya vikao vya kamati vinaweza kuanza mapema hapa Dodoma, lakini uamuzi bado haujafanyika mpaka sasa,” alisema Ndugai.
Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge la Muungano, kamati zake za kisekta zilipaswa kuanza vikao wiki mbili kabla ambayo ni Oktoba 20 mwaka huu, siku ambayo bado Bunge Maalumu kwa mujibu wa ratiba iliyopo sasa litakuwa bado halijakamilisha kazi yake.

Upinzani wafanya maandamano Pakistan

Maandamano Pakistan
Maafisa wa polisi nchini Pakistan wamekabiliana na waandamanaji wanaopinga serikali wanaoelekea katika makao rasmi ya waziri mkuu Nawaz Sharrif katika mji mkuu wa Islamabad.
Mmoja ya viongozi wa maandamano hayo Tahir Ul-Qadri amesema kuwa maafisa wa polisi waliwafyatulia risasi pamoja na kuwarushia vitoa machozi.
Amesema kuwa watu saba waliuawa.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa maafisa wa polisi walichukua hatua hiyo baada ya waandamanaji kuanza kuelekea katika makaazi ya bwana Shariif huku wakijaribu kuondoa vizuizi vilivyowekwa na polisi.
Amesema kuwa baadhi ya waandamanaji walifaulu kuingia katika jengo hilo.
Waziri wa Ulinzi amesema kuwa viongozi wa maandamano hayo wanajaribu kuchochea hali hiyo ili walaumu serikali kwa mauaji.
Amesema kuwa serikali itatumia nguvu kiasi kuwadhibiti waandamanaji hao.

Mawaziri, wabunge kutimuliwa kwenye nyumba TBA Dodoma


 
Na Beatrice Moses, MwananchiDar es Salaam. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imefanya uamuzi mgumu wa kuwatimua baadhi ya wapangaji wa nyumba zake zilizopo mjini Dodoma ambao ni wadaiwa sugu, wakiwamo mawaziri saba na wabunge 15.
TBA katika kutekeleza uamuzi huo imekabidhi Kampuni ya Yono Action Mart orodha ya majina ya watu hao wanaodaiwa kiasi cha Sh800 milioni, ili waondolewe kwa nguvu kwenye nyumba hizo wanazoishi.
Akizungumza na Mwananchi juzi Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga, alithibitisha kuwa ofisi yake inachukua hatua hiyo kwa mujibu wa sheria kwa sababu wapangaji hao wamekwenda kinyume na mikataba yao.
“ Hatukupenda kuchukua hatua hii, lakini ukweli ni kwamba madeni hayo ni ya muda mrefu, kazi tunayofanya ni kwa manufaa ya maendeleo ya nchi na siyo yetu binafsi, hivyo tulitegemea wangetimiza wajibu wao wa kulipa lakini imekuwa kinyume,” alisema Mwakalinga.
Alisema fedha ambazo TBA inadai hadi sasa zimefikia jumla ya Sh 800 milioni ambazo kama zingekuwa zimelipwa zingewasaidia kutimiza wajibu wao wa kujenga baadhi ya nyumba mpya au kukarabati zile zinazotakiwa kufanyiwa hivyo.
“Walipewa notisi na ofisi yetu kule Dodoma baadhi yao waliitikia wito kwa kulipa madeni yao, wakiwamo hata maofisa wa Ikulu, walitoa ushirikiano mzuri, nafikiri kwa kutambua wajibu tulio nao TBA,” alisema.
Mwakalinga alisema kuwa TBA imeona iwahusishe kampuni ya udalali ya Yono Action Mart kwa sababu wao wana majukumu mengi ya ujenzi wa nyumba mpya za watumishi wa Serikali.
“ Gharama za kumlipa dalali huyo, watatakiwa kulipa hao hao wanaodaiwa kwa mujibu wa sheria, sisi hatuna bajeti hiyo,” alisema Mwakalinga ambaye alikataa kuwataja wadaiwa hao akieleza kuwa jukumu hilo tayari lipo kwa Yono.
Mkurugenzi wa Yono Action Mart, Yono Kevela, kwa upande wake alisema baada ya kupokea kazi hiyo, walitoa notisi ya siku 14 kwa wahusika ili kuwapa nafasi ya kulipa madeni yao.
“ Wale ambao wamelipa kutokana na ile notisi wamejinusuru, lakini wale ambao hawajalipa kwa kweli nimetuma kikosi kazi changu ambacho ninakiamini, kwamba hakina woga katika kutimiza majukumu tuliyopewa, natarajia kesho wataanza kazi, hiyo,” alisema Kevela. Baadhi ya mawaziri waliotajwa kwenye orodha hiyo ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda, anayedaiwa Sh7.5 milioni, ambaye alipohojiwa na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu deni hilo alisema: “Mimi sina habari hiyo nipo Nairobi, Kenya,”.
Mwingine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu anayedaiwa Sh 9.4 milioni, ambaye aliliambia gazeti hili kuwa ana taarifa ya deni hilo, lakini kwa wadhifa wake hawajibiki binafsi.
“ Nakumbuka niliona barua, lakini kwa utaratibu ninaoujua ni kwamba mawaziri wote hatujigharamii kwa hilo , bali tunalipiwa na Serikali sasa nafikiri labda wizara ilijisahau, nakuhakikishia binafsi siwajibiki,” alisema Nyalandu.
Juhudi za gazeti hili kuwasiliana na mawaziri wengine wakiwamo na naibu mawaziri ambao majina tunayo, zilikwama baada ya baadhi yao kushindwa kupatikana ofisini na simu zao kuita bila majibu huku wengine simu hazikupatikana.
Wabunge
Kwa upande wa wabunge ni mbunge wa Bariadi John Cheyo(UDP) ambaye anadaiwa Sh 4.2 milioni, alipohojiwa kuhusu deni hilo alishtuka na kueleza kuwa TBA wamfuate, badala ya kudai kupitia magazeti.
“He! ndiyo unaniambia wewe, sina taarifa kama wana madai, waje tu siyo kudai kwenye magazeti.” alisema.
Mwingine ni mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani (CCM) anayedaiwa zaidi ya Sh2.5 milioni, alipoulizwa na alijitetea kuwa hana taarifa, kwa kuwa alikuwa safarini Masasi Mkoani Mtwara kwenye msiba.
“ Hapa ninapozungumza nawe nipo njiani naelekea Dodoma, sina habari hiyo wewe ndiyo kwanza unaniambia, natoka kuzika,” alisema Makani.
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (CCM), ambaye kwenye orodha hiyo inaonyesha anadaiwa Sh2.4 milioni, alisema kwamba hajawahi kuwa na mkataba na TBA.
“ Eeh! Labda wamekosea sijawahi kuwa na mkataba na TBA mimi,” alijibu Ole Medeye kisha akakata simu.

Man U kumsajili beki Daley Blind

Mchezaji Daley Blind wa Ajax.

Kilabu ya Manchester United ya Uingereza imekubaliana na kilabu ya Uholanzi Ajax Amsterdam kutoa kitita cha pauni millioni 13.8 kumnunua mlinzi wa timu hiyo Daley Blind.
Blind ambaye ana umri wa miaka 24 alikuwa katika kikosi cha Kombe la dunia cha Uholanzi chini ya mkufunzi Louis Van Gaal.
Anaweza kucheza kama beki wa kushoto pamoja na ngome ya kati ya ulinzi.
Iwapo makubaliano hayo yatatiwa sahihi, huyo atakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na kilabu hiyo.
Kilabu ya Manchester tayari imetumia zaidi ya pauni millioni 130 katika msimu huu pamoja na kuvunja rekodi ya Uingereza kwa kusajili Angel Di Maria kwa kitita cha pauni 59.7 kutoa Real Madrid.
Old Trafford pia imemnunua beki wa kushoto Luke Shaw,mchezaji wa kungo cha kati Ander Herrera na Marcos Rojo.

Saturday, August 30, 2014

Okwi arejea Simba


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope akimkabidhi jezi ya timu hiyo mshambuliaji wao mpya Emmanuel Okwi baada ya kumtambulisha jana jioni kwa waandishi wa habari. Picha na Khatimu Naheka      
Na Vicky Kimaro, MwananchiDar es Salaam. Uongozi wa Simba umemrudisha kundini mshambuliaji wake wa zamani, Emmanuel Okwi ukisema umechukua hatua hiyo: “Kumsitiri ili asipoteze kipaji chake” baada ya watani wake wa jadi Yanga, kumshtaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope alisema mbinu ambazo Yanga ilitumia Yanga kumsajili Okwi wakati alipokuwa na mgogoro na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia ndiyo hiyohiyo kamati yake iliyoitumia kumrejesha Simba.
“Yanga walivyowafanyia Watunisia wakati wana mgogoro na Okwi walijiona washindi, sasa na sisi kwa mantiki hiyohiyo tumeamua kumrudisha kundini, “alisema Hans Pope.
Alisema Simba haina mkataba wowote na Okwi na kwamba anaruhusiwa kuondoka muda wowote atakapoamua huku akisema timu hiyo inasubiri uamuzi wa kesi ya mchezaji huyo na Yanga imalizike kukamilisha mchakato.
Habari zilizopatikana jana kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Simba zinasema Okwi amemwaga wino wa kuichezea Simba kwa miaka miwili na kwamba malipo ya awali ya mkataba huo ya Dola za Marekani 10,000 alichukua mwaka jana.
Kauli ya Okwi
Akizungumzia madai yake na Yanga, Okwi alisema juzi alipewa barua na TFF ya kushtakiwa na Yanga.
Alisema katika madai, alisema Yanga inamtuhumu kuchukua fedha za usajili na kushindwa kuitumikia huku akishindwa kuipa ubingwa baada ya kufungiwa michezo minne.
“Mimi naishangaa Yanga, eti inadai fedha za usajili, usajili maana yake nisaini wa wanipe fedha, sasa hizo fedha wanazodai ni zipi? Mbona hawazungumzii mshahara wangu ambao nilikuwa nalipwa kwa kutumia nguvu, nipo tayari kukaa meza moja na Yanga katika kesi wala siogopi chochote na pale naamini kila mmoja atapata haki yake.
“Nawaomba wana Simba wanipokee mimi ni kijana wao, nitaitumikia Simba kwa moyo wangu wote, mimi ni mpya nawaahidi sitakuwa tena msumbufu,” alisema Okwi.
Wakati huo huo, baadhi ya klabu za Ligi Kuu zimelipinga Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kusogeza usajili mbele mpaka leo saa 6 usiku kwa kigezo kuwa ni timu moja tu ndio iliyokuwa imekamilisha usajili wake hadi juzi saa sita usiku.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao wa soka waliitaka TFF kuacha kudanganya umma wa Watanzania na badala yake iseme ukweli kilichofanya wakasogeza mbele usajili.

David Rudisha amaliza wa tatu

Nijel Amos alimzidi nguvu David Rudisha
Katika michuano ya Diamond League ya jana usiku, Nijel Amos alimzidi kasi ya kuufukuza upepo David Rudisha katika michuano ya mita 800 mjini Zurich.
Mshindi huyo wa michuano ya Olympic David Rudisha alimaliza mbio zake katika nafasi ya tatu kwenye mbio hizo za mita 800 wakati mwanariadha mchanga na mwenye ubavu wa kutanua mapafu mbioni Nijel Amos kwa mara ingine tena amejitwalia tena ubingwa huo wa mita 800.
Na hii si mara ya kwanza kwa Amos kumshinda nguvu Rudisha kwani mwezi uliopita katika michuano ya jumuiya ya madola maarufu kama Commonwealth Games na kujitwalia medali ya dhahabu huku akitumia dakika 43. sekunde 77
Naye Ayanleh Souleiman alimshinda Rudisha na kutwaa nafasi ya pili kitendo kilichomlazimisha Rudisha kushika nafasi ya tatu.

Rais atumie fursa hii kuleta maridhiano


Rais Kikwete 
Kwamba Rais Jakaya Kikwete muda wowote kuanzia sasa atafanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge, wakiwamo viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hakika ni habari njema ambazo zimewapa wananchi matumaini makubwa. 
Hivi sasa habari hiyo ndiyo gumzo kuu katika kila kona ya nchi yetu na vyombo vya habari, ikiwamo mitandao ya kijamii ambayo imesheheni maoni ya wananchi wanaounga mkono uamuzi huo wa Rais.
Sisi wa Mwananchi tunaungana na wananchi hao kumpongeza Rais kwa uamuzi huo wa busara wenye lengo la kuwaunganisha wananchi waliogawanyika vipandevipande baada ya mchakato wa kupata Katiba mpya kuvurugwa na wanasiasa.
Bila shaka Rais atakuwa ameona mbali na kutambua madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo cha Bunge la Katiba kuendelea na mchakato wa Katiba bila kuwapo mwafaka wa kitaifa, kwa maana ya kutokuwapo uwakilishi mpana katika kujadili na kuboresha Rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Hakuna asiyejua kwamba mwelekeo hasi wa mijadala katika Bunge hilo linaloandika Katiba mpya ndiyo hasa uliowasukuma wajumbe wake kutoka vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF kususia vikao na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Moja ya sababu za kufanya hivyo ni vitendo vya kibaguzi, kejeli, matusi ya nguoni na vitisho kutoka kwa wajumbe wa chama tawala, CCM, ambacho Ukawa wanasema kiliteka mjadala na mchakato mzima kwa kuweka kando Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kupenyeza yao iliyotayarishwa na chama hicho. Kwa mtazamo wa Ukawa, katiba ambayo itatokana na mazingira hayo haitakuwa ya wananchi, bali itakuwa ya CCM.
Ni jambo la kusikitisha kwamba tangu wajumbe wa Ukawa wasusie Bunge hilo Aprili 16, mwaka huu hawajawahi kusikilizwa na chombo chenye mamlaka ya juu au chombo ambacho hakina masilahi ya moja kwa moja na mgogoro huo.
Wito wao wa mara kwa mara wa kukutana na Rais Kikwete ulibezwa na kupuuzwa na makada wa chama chake ambao walipaswa kumshauri akutane nao ili kupata maridhiano na mwafaka wa kitaifa.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba hakuna mahali popote duniani ambako katiba ya wananchi iliyo nzuri na endelevu ilitokana na mazingira ya ghiliba, hadaa na shari kama ambayo tumeyashuhudia katika Bunge hili.
Katiba yoyote nzuri huhitaji mazingira yenye masikilizano, maelewano na kustahiana.
Mazingira ya matusi ya nguoni, uadui, kebehi, dharau, vitisho na hadaa kama ilivyotokea katika Bunge letu la Katiba huzaa chuki, hivyo katiba inayotokana na mazingira kama hayo kamwe haiwezi kukubalika kwa wananchi kwa sababu hupandikiza chuki na hatimaye kusababisha vurugu.
Ndiyo maana tunampongeza Rais Kikwete kwa kuona hilo na kuridhia kukutana na viongozi wa vyama vyenye wabunge kuzungumzia kadhia hiyo.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliandaa Rasimu ya Katiba kwa kuzingatia maoni ya wananchi. Bahati mbaya Bunge la Katiba limetekwa na wanasiasa wanaopigania masilahi binafsi.
Ndiyo maana, pamoja na mambo mengine wamekataa uwepo ukomo wa vipindi vyao vya ubunge, wamekataa wapigakura kuwawajibisha wabunge wao na pia wamekataa pendekezo la mawaziri kutokuwa wabunge.
Katika hali kama hiyo, Rais atafanya vyema iwapo atasitisha Bunge hilo hadi mwafaka wa kitaifa utakapopatikana.

Mbowe: Anayetaka kupima kifua na mimi aje Chadema

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’.
“Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
Makada wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiongozwa na kada maarufu, Athuman Mzigo (Mapigo Saba) kutoka Kigoma, walikutana na Mbowe na kuwasilisha maombi yao ya kumtaka awanie tena nafasi hiyo.
“Kutokana na sifa za mwenyekiti wetu, tumechangishana Sh200 kila mmoja hadi zikafika Sh50,000,” alisema Mapigo Saba huku akishangiliwa na makada wenzake alioambatana nao na kuongeza:
“Tumemwomba mwenyekiti agombee nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa; kwanza anaijua vizuri idadi ya Watanzania na matatizo yao, pili anaungwa mkono na watu wengi na amekisaidia chama kukua. Tulikuwa na madiwani 40 leo wamefika 500, wabunge watano leo 48. Halafu hana ubaguzi ndiyo maana ameunganisha vyama vya upinzani na kuunda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”
Huku akichomekea maneno ya lugha ya Kiha, Mapigo Saba alisema kuwa maombi ya kumtaka Mbowe agombee pia yametolewa katika mikoa ya Rukwa, Manyara, Iringa, Njombe, Jimbo la Same Magharibi, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.
Hotuba ya Mapigo Saba ilifuatiwa na salamu kutoka kwa wazee wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, Baraza la Wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).
Akitoa salamu za Bavicha, mwenyekiti wa baraza hilo Njombe, Emmanuel Masonga alisema Mbowe ni sawa na Joshua aliyemalizia kuwaongoza wana wa Israel kuingia nchi ya Kanaani:
“Sisi Wakristo tunajua kuwa Mussa alianzisha safari ya Waisrael kwenda Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (Edwin), Kimesera (Victor), Bob Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu,” alisema Masonga.
Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Susan Lymo alimsifu Mbowe akisema ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa katika chama hicho.
“Mwaka 2000, kulikuwa na mwanamke mmoja katika viti maalumu, mwaka 2005 waliongezeka na kufikia sita na mwaka 2010 wamefikia 26. Mwenyekiti pia ameufanya mwaka huu kuwa wa wanawake kitaifa na ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa,” alisema Lymo.
Mbali na viongozi wa chama, alikuwapo pia Sheikh Rajab Katimba kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambaye alimsifu Mbowe na kuomba agombee tena nafasi hiyo.
Mbowe akubali
Baada ya Mratibu wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Nickson Tugara kummwagia sifa Mbowe, Mapigo Saba alimkabidhi fomu, huku makada wakiimba, ‘Jembe, jembe, jembe…”
Mbowe aliishukuru Kamati Kuu ya chama hicho kwa kupanga uchaguzi Septemba 14, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa huku akiahidi kujenga chama imara.
“Mtaiona Chadema mpya ifikapo Septemba 14. Hiki chama hakitakufa na hatutamvumilia mtu yeyote wa kabila lolote atakayekivuruga,” alisema.
Mbowe alisema hajawahi kuomba kugombea uenyekiti wa chama hicho tangu aliponza mwaka 2000... “Napata wakati mgumu ninapofikia wakati huu.
Chadema ina watu mbalimbali wenye taaluma na uzoefu, kwa nini mimi? Makundi haya yaliyojitokeza kunichukulia fomu yanaweza kutafsiriwa na wapenda majungu kuwa nimepanga mimi.
“Leo ni mara ya tatu naombwa kugombea uenyekiti, sijawahi kuomba. Mwaka 2004, Mzee Makani aliniomba nikamkatalia, lakini akaunda kikundi cha wazee walionichukulia fomu.
Mwaka 2005, chama hakikuwa na mgombea urais, awali alijitokeza Profesa Mwesiga Baregu lakini akajitoa, nikaambiwa nibebe mzigo. Mwaka 2009 nikaombwa tena kugombea.”
Alisema amedhamiria kujenga chama kimtandao na kimfumo ili kuondokana na mfumo wa kienyeji... “Huko nyuma wakati wa uchaguzi watu walipeana tu nyadhifa kiundugu tukadhani chama kimeongezeka. Lakini wakati huu uchaguzi umefanyika kwa miezi tisa.
Tulisema hatuwezi kufanya uchaguzi wa Taifa bila kupata viongozi wa mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa, kitongoji na shina.
Tumefanya uchaguzi, watu wamepima na kuona mambo magumu, mara unasikia wanakimbia wakisema wameacha uenyekiti, uache wakati chama kinakua?”

Mgawanyo wa mapato watikisa Bunge Maalumu


Samwel Sitta akifafanua jambo 
Na Neville Meena na Habel Chidawali, MwananchiDodoma. Hoja kuhusu mgawanyo wa mapato ya muungano imeendelea kulitikisa Bunge Maalumu la Katiba na jana watendaji wakuu wa wizara za fedha wa muungano na Zanzibar pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu walitua Dodoma kuweka mambo sawa.
Vigogo hao wa fedha jana walikutana na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu, kujaribu kupata mwafaka wa jinsi suala hilo litakavyowekwa kwenye Katiba Mpya.
Bunge la Katiba limelazimika kuwaita Dodoma watendaji hao ili kusaidia kukwamua mgogoro wa mapato ya muungano, ambao uliwagawa wajumbe wa kamati za Bunge hilo wakati wa mjadala wa sura ya 14 kwenye Rasimu ya Katiba.
Pamoja na Profesa Ndulu, wengine waliokuwapo ni Katibu Mkuu Hazina, Dk Servacius Likwelile na mwenzake kutoka Zanzibar, Mussa Omar ambao walikuwa na kibarua kigumu cha kupunguza ufa uliowatenga wajumbe wa Bunge hilo katika misingi ya Ubara na Uzanzibari.
Sura ya 14 ya rasimu ndiyo inayozungumzia masuala ya mapato ya muungano na mgawanyo wake.
Suala la mgawanyo wa mapato ni moja ya mambo manne magumu yaliyosababisha mvutano mkubwa katika kamati za Bunge hilo kiasi cha kusababisha Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu kuunda kamati ndogo ili kulifanyia kazi.
Kutokana na kusababisha mivutano hiyo, Kamati Namba Moja iliamua kutolijadili kabisa suala hilo na badala yake, kuomba uongozi wa Bunge uwalete watendaji wakuu wa masuala ya fedha ili watoe mwongozo wa kuwawezesha wajumbe kujadili na kupata mwafaka wa jinsi fedha zitakavyoweza kusimamiwa na kugawanywa. Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Waziri - Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu alisema walishindwa kupigia kura sura ya 14 baada ya kuona ina utata.
“Ni kweli hatukupigia kura sura ya 14 pekee, tuliona ina utata mkubwa ambao unahitaji ufafanuzi wa kina na bila shaka baada ya semina ya leo (jana) tutakutana kufanya uamuzi,” alisema Mwalimu.
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Hamis Hamad alisema: “Kamati zote zimemaliza kazi, isipokuwa Namba Moja haikupigia kura sura ya 14 wakitaka ufafanuzi wa kitaalamu, ndiyo maana tumewaleta wataalamu leo.”
Alisema pamoja na kupigia kura sura hiyo, lakini hata kamati nyingine zilionekana kutoelewa vizuri sura hiyo, hivyo ujio wa wataalamu ulilenga kuwawezesha kujadili sehemu hiyo ya Katiba wakiwa na uelewa mpana.
Habari zinasema sura iliyojitokeza kwenye mijadala ya kamati zote 12 ilihamia kwenye semina hiyo, ambako ufa ulidhihirika baina ya wajumbe wa pande hizo mbili za muungano, lakini watendaji hao kwa kushirikiana na wataalamu wengine walifanikiwa kutoa mwelekeo wenye matumaini.
Hoja zilizojiri
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema hoja kubwa zilizojitokeza zilihusu uwiano wa mgawanyo wa mapato, kuanzishwa kwa tume ya pamoja ya kusimamia mapato na Zanzibar kuruhusiwa kukopa fedha nje na katika mashirika ya kimataifa bila kupata ridhaa ya Hazina.
Hivi sasa Zanzibar inapata asilimia 4.5 ya mapato ya muungano huku Tanzania Bara ikipata asilimia 95.5 kutokana na wingi wa idadi ya watu na eneo lake kijiografia, suala ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na Wazanzibari kwamba wananyonywa.
Hata hivyo, mmoja wa wajumbe alinukuliwa akizungumza katika kikao hicho kwamba kanuni ya mgawanyo wa mapato inayotumiwa sasa ilitokana na ushauri wa kitaalamu uliotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na kwamba unaweza kupitiwa upya ikiwa kutakuwa na haja hiyo. Mmoja wa wajumbe kutoka Zanzibar alinukuliwa akihoji kwa nini upande huo wa muungano ambao ni nchi kamili usipewe asilimia 50 ya mapato yatakayopatikana katika mfuko huo.
“Katibu Mkuu (Likwelile) aliposimama kujibu hakukataa lakini alisema kiwango cha asilimia pia kinazingatia uwekezaji kwenye mfuko husika na kwamba kama uwekezaji ni sawa, basi hakuna shaka kwamba hiyo asilimia 50 inawezekana,” kilisema chanzo chetu.
Kuhusu suala la mfuko wa pamoja, habari zinasema wajumbe wengi walionekana kuwa na mwelekeo wa pamoja lakini walikosoa kutoanzishwa kwake hadi sasa, licha ya kwamba suala hilo liliamuliwa miaka 14 iliyopita.
Katika Kamati Namba Mbili, suala la tume ya pamoja limeongezwa na kupewa Ibara ya 221B, huku ikipendekezwa kwamba tume ya pamoja ya fedha iwe na wajumbe wasiozidi saba watakaoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar. Watatu watatoka Zanzibar na wanne Tanzania Bara.
Tume hiyo, pamoja na mambo mengine inapendekezwa iwe na jukumu la kuchambua mapato na matumizi yanayotokana au yanayohusu utekelezaji wa mambo ya Muungano na kutoa mapendekezo kwa serikali zote mbili kuhusu mchango na mgawo wa kila mojawapo wa serikali hizo.
Hata hivyo, ndani ya kamati kadhaa, wajumbe kutoka Tanzania Bara walikuwa na msimamo kwamba lazima Zanzibar ipate idhini ya Hazina kabla ya kukopa fedha nje kwani Serikali ya Muungano ndiyo mdhamini mkuu wa mikopo hiyo.
“Hatuwezi kuruhusu Zanzibar wakope wanavyotaka, lazima Serikali ya Muungano ijiridhishe kwamba masharti yote kuhusu ukopaji yamezingatiwa, vinginevyo tunaweza kuiingiza nchi katika matatizo makubwa,” kilisema chanzo kingine.
Akizungumzia kikao hicho, Mwalimu alisema semina waliyoipata itawawezesha kufanya uamuzi sahihi watakapokuwa wakijadili sura hiyo ya 14.
Mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi alisema kuwa semina hiyo imemsaidia kwa kiasi kikubwa ingawa ilikuja kwa kuchelewa.
Kwa upande wake Mbunge wa Dimani, Abdallah Sharia Ameir alisema semina ya jana ingawa imechelewa itatoa mabadiliko makubwa.

Rasimu ya Warioba sasa mifupa mitupu


Mjumbe  wa  Bunge la Katiba Andrew  Chenge(kulia), akifurahia jambo  na wajumbe wenzake, Salehe Pamba (wa pili kushoto),  Adam Malima na Vita Kawawa nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman 
Na Neville Meena, MwananchiDodoma. Kamati za Bunge Maalumu, zimekamilisha kazi ya kujadili na kuchambua Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, huku ikiwa imefanyiwa mabadiliko makubwa tofauti na ilivyokuwa awali.
Wajumbe wanatarajiwa kuanza kukutana kama Bunge zima kuanzia Jumanne ijayo, Septemba 2, 2014 wakati kamati zitakaposoma taarifa zake baada ya kufanya uchambuzi wa sura 15 za Rasimu ya Katiba kwa zaidi ya wiki tatu, huku yakitarajiwa mabadiliko makubwa.
Mabadiliko yaliyofanywa yameondoa mambo makubwa yaliyokuwa yakiifanya rasimu hiyo kuonekana mpya, hivyo sasa baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaiona rasimu kama ‘Katiba ya 1977 iliyofanyiwa marekebisho.’
Mwelekeo wa kubadili karibu misingi yote muhimu iliyojengwa na tume iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba akiwa mwenyekiti, ilianza baada ya kuwekwa kando kwa mfumo wa muungano wa Serikali tatu uliopendekezwa na badala yake kurejea katika muundo wa sasa wa serikali mbili.
Uamuzi huo uliathiri mtiririko na muundo mzima wa sura na ibara za rasimu hiyo, kwani sasa wajumbe wa Bunge Maalumu walilazimika kutengeneza Katiba yenye mwelekeo wa serikali mbili na siyo tatu tena zilizokuwa zimependekezwa na tume.
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba mwelekeo wa uchambuzi wa rasimu kwa sura hizo 15, lazima ufuate kile ambacho kamati zilikiamua katika uchambuzi wa awali wa sura ya kwanza na ya sita.
Miongoni mwa mambo ambayo yameachwa baada ya kurejesha mfumo wa serikali mbili ni muundo wa uongozi wa juu wa nchi hususan nafasi ya Makamu wa Rais, muundo wa Bunge la Jamhuri, kupunguzwa mamlaka ya Rais, uwajibikaji na uwajibishwaji wa wabunge na ukomo wa ubunge.
Kadhalika, habari kutoka ndani ya kamati zilisema suala la kuwekwa kwa maadili ya uongozi kwenye Katiba nalo lilizua mjadala mkali kutokana na baadhi ya wajumbe kutaka liondolewe kwa maelezo kwamba linapaswa litajwe kwenye sheria na siyo Katiba.
Mambo ya muungano
Miongoni mwa mambo ambayo kuna kila dalili kwamba yatabadilika ni Bunge Maalumu kuongeza mambo ya muungano kutoka saba yaliyopendekezwa na tume na huenda idadi yake ikazidi 22 yaliyomo kwenye Katiba ya sasa.
 Uchunguzi wa gazeti hili uliofanywa katika baadhi ya kamati za Bunge hilo na kuthibitishwa na baadhi ya wenyeviti wake, umebaini kuwa yapo mapendekezo ya mambo ya muungano kuongezwa, tofauti na mtazamo wa awali kwamba yangepungua kama moja ya njia za kuondoa kero za muungano.
Tume ya Jaji Warioba ilipendekeza mambo saba tu kwenye orodha ya muungano chini ya mfumo wa Serikali tatu, mfumo ambao hata hivyo ni dhahiri umeshawekwa kando na Bunge Maalumu na kurejesha muundo wa serikali mbili.
Mambo yaliyopendekezwa na tume hiyo ambayo yapo kwenye sura ya 17 ya Rasimu ya Katiba inayohusu masharti ya mpito ni pamoja na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uraia na Uhamiaji.
 Mengine ni Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje, Usajili wa Vyama vya Siasa na Ushuru wa Bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
 Mapendekezo hayo yaliyaacha nje mambo mengine 15 yaliyopo kwenye Katiba ya sasa ambayo ni polisi, mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, mikopo na biashara ya nchi za nje, utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu na leseni ya viwanda na takwimu.
Pia yamo elimu ya juu, maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa na gesi asilia, Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania, usafiri na usafirishaji wa anga, utafiti, utafiti wa hali ya hewa na  Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
 Baadhi ya wenyeviti wa kamati za Bunge Maalumu wamesema kuna kila dalili kwamba baadhi ya mambo yaliyoachwa yatarejeshwa huku kukiwa na mtazamo kwamba mengine yanaweza kuongezwa kutoka nje ya orodha ya sasa.
 Mwenyekiti wa Kamati Namba Tano, Hamad Rashid Mohamed alisema orodha iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba ina upungufu mkubwa kwani imeacha mambo mengi ya msingi yenye sura ya muungano.
“Mathalani huwezi kuzungumzia kwamba usalama ni suala la muungano halafu ukaacha mambo ya anga, au ukaacha suala la mitihani, yaani Baraza la Mitihani limeachwa pia suala la utafiti nalo huwezi kuliacha, kwa hiyo orodha itaongezeka,” alisema Mohamed.
Mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita, Stephen Wassira alisema kuna mambo mengi ya muungano yaliyotajwa kwenye Rasimu ya Katiba lakini hayako katika orodha iliyowekwa kama moja ya nyongeza kwenye rasimu hiyo.
“Ngoja nikwambie kwamba mambo hayo yataongezeka, hilo halina ubishi na kamati yangu tulijadili kidogo na kesho (leo) tutakutana kumalizia. Ukisoma vizuri ibara kwa ibara, utagundua kuwa kuna mambo mengi kama vile Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo ni chombo cha muungano hata ukiangalia muundo wake,” alisema Wassira.
Alitaja mambo mengine kuwa mahakama ya juu inayopendekezwa kuanzishwa lakini haimo kwenye orodha pamoja na masuala ya elimu ya juu na utafiti.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati Namba nne, Christopher Ole Sendeka alisema kuna kazi kubwa ya kutazama upya orodha ya mambo ya muungano na kwamba suala la usalama wa anga ni moja ya mambo hayo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati Namba Moja, Ummy Mwalimu alisema, licha ya kwamba kamati yake haikujadili suala hilo lakini orodha hiyo inaweza kuongezeka kwani kuna mambo mengi yameachwa.
“Leo tulikuwa tunaangalia suala la fedha na kuna mambo ukichuguza humo yanagusa sehemu zote mbili, sisi hatukujadili sehemu hiyo kutokana na kwamba haikuwa kwenye orodha ya kazi tulizopewa ila nadhani tukipata fursa bungeni lazina mambo hayo yaangaliwe,” alisema Mwalimu.
Kamati nyingine ambayo haikujadili suala hilo ni namba tatu ambayo mwenyekiti wake, Dk Francis Michael alisema orodha ya mambo ya muungano iko kwenye sura ya 17 ambayo haikuwa sehemu ya kazi za kamati.

Ebola:Ivory Coast kususia mechi


Ivory Coast kususia mechi na Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola
Shirikisho la soka la Ivory Coast limesema kuwa huenda likasusia mechi ya kufuzu kwa dimba la mabingwa barani Afrika dhidi ya wapinzani wao Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola.
Mchuano huo ambao umeratibiwa kuchezwa mjini Abidjan tarehe 6 Septemba umeibua taharuki miongoni mwa maafisa wa Afya na serikali kuu inatishia kuipiga marufuku.
Hofu hiyo inatokana na kuenea kwa homa ya Ebola katikamataifa 5 kanda ya Afrika Magharibi ikiwemo Sierra.

Ivory Coast kususia mechi na Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola
"Kwa mujibu wa msemaji wa shirikisho la soka la Ivory Coast Malick Tohe, ikiwa wataruhusiwa kuihamisha mechi hiyo hadi taifa la tatu iwapo CAF itaruhusu.
Tayari Sierra Leone imetaja kikosi cha wachezaji wanaocheza nje ya Sierra Leone ilikuepusha hatari ya kueneza Ebola Ivory Coast .
Sierra Leone imeagiza maafisa wote wa ukufunzi kufanyiwa uchunguzi wa kutosha kabla ya kuingia Ivory Coast .

Ivory Coast kususia mechi na Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola
Shirikisho la soka barani Afrika limekataa katakata kubadilisha kutakapoandaliwa mechi za kufuzu licha ya hatari ya maambukizi .
Hadi kufikia sasa haijulikani iwapo CAF itaichukulia hatua zaidi Ivory Coast iwapo itasusia kuchuana na Sierra Leone au itaruhusiwa kuendelea na mechi za kufuzu.