Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, April 29, 2014

Obama praises influence of Saints John XXIII, John Paul II

President Barack Obama gives his weekly address, May 5, 2012. Credit: White House.
President Barack Obama gives his weekly address, May 5, 2012. Credit: White House.
U.S. president Barack Obama issued a statement Monday noting the canonization of both John XXIII and John Paul II over the weekend, paying tribute to their work in the Church and society.

“Today, Michelle and I join Catholics around the world in celebrating the canonization of Pope John XXIII and Pope John Paul II,” he said April 28. “The work and witness of both Pope John XXIII and Pope John Paul II shaped not only the Catholic Church but the world.”

He noted John XXII’s advocacy “in the cause of global peace and justice,” and said that in calling Vatican II, “he revolutionized not only aspects of worship but the Catholic Church’s relationship with other faith communities.”

Obama discussed John Paul II’s role in inspiring the Solidarity movement, which “eventually helped to end communism in Eastern Europe,” and his forceful words against apartheid in South Africa and the Rwandan genocide.

“He had a special rapport with young people, drawing many of them to the Church’s work and teachings,” Obama stated.

The two late Popes were canonized April 27 during a Mass said by Pope Francis in St. Peter’s Square.

During his homily at the Mass, Pope Francis said, “At the heart of this Sunday, which concludes the Octave of Easter and which Saint John Paul II wished to dedicate to Divine Mercy, are the glorious wounds of the risen Jesus.”

“Saint John XXIII and Saint John Paul II were not afraid to look upon the wounds of Jesus, to touch his torn hands and his pierced side,” Pope Francis preached.

“They were not ashamed of the flesh of Christ, they were not scandalized by him, by his cross; they did not despise the flesh of their brother, because they saw Jesus in every person who suffers and struggles,” the Pope said. “These were two men of courage, filled with the parrhesia of the Holy Spirit, and they bore witness before the Church and the world to God’s goodness and mercy.”

Obama, concluding his statement, said: “We celebrate these Saints and the leadership of His Holiness Pope Francis, and we look forward to continuing to work with Pope Francis and Catholics around the world to advance peace and justice for all people.”

Poor Brazilian parish becomes first to take St. John Paul II's name

Pope John Paul II.
Pope John Paul II.
 A small parish in the poor neighborhood of Alagados in Salvador de Bahia, Brazil, has become the first in the world to be named after St. John Paul II, after the late pontiff’s canonization April 27.

Sara Gomes, spokesperson for the Archdiocese of Salvador, told AFP that the “small church of Notre Dame of Alagados will now be called 'Notre Dame of Alagados and of St. John Paul II.' It is the first in the world to be named after the new saint.”

The official name change took place the morning of April 27 after Mass at the parish. Pope John Paul II was declared a saint alongside Pope John XXIII at a Vatican Mass earlier that day.

Archbishop Murilo Krieger signed a decree authorizing the new title for the parish, which was inaugurated in 1980 by John Paul II during the first of three trips he made to Brazil.

Capuchin Father Jorge Rocha recalled meeting St. John Paul II at the parish three decades ago.

“The saints live among us,” he told the Globo website. “The Church does not invent them, she recognizes what already exists.”

Masses of Thanksgiving offered in Rome for new Pope saints

Cardinal Angelo Comastri celebrated a Mass of thanksgiving for Pope St. John Paul II in St. Peter's Square on April 28, 2014. Credit: Daniel Ibáñez/CNA.
Cardinal Angelo Comastri celebrated a Mass of thanksgiving for Pope St. John Paul II in St. Peter's Square on April 28, 2014. Credit: Daniel Ibáñez/CNA.
.- Following the canonization of Popes John Paul II and John XIII, Church officials presided over two Masses of Thanksgiving, drawing attention to the saints’ enormous contributions to the Church and to society.

Taking place April 28 at 10 a.m. in St. Peter’s Square, where the day before huge numbers of pilgrims crowded for the canonization of the ecclesial giants, Cardinal Angelo Comastri led the congregation in giving thanks for the 27-year pontificate of John Paul II.

In his homily, Cardinal Comastri – who is Archpriest of St. Peter’s Basilica and Vicar General for the Vatican City State – emphasized the courage John Paul II had in proclaiming the Gospel, especially during a time when the world pretended as if God no longer existed.

Observing how the pontiff’s witness became stronger, even as his body became weaker, the cardinal reflected that his faith was “authentic and free from fear or compromise.”

He then highlighted the saint’s untiring defense of the family and the dignity of human life, also drawing attention to his firm opposition to the Gulf Wars and his efforts in establishing peace among peoples and nations.

Cardinal Comastri concluded his reflections by emphasizing the special attention the pontiff gave for the youth, as well as his devotion to Mary, into whose hands he had entrusted himself and his whole life.

Present for the April 27 canonization of the Polish saint was a young man named Nicholas and his father, who recounted to CNA an encounter they had with the pontiff in Rome when Nicholas was just a toddler.

Explaining how they had come for the beatification of three nuns, Nicholas’ father recalled that “We didn’t have tickets” for the Mass, but were still able to get in.

“Some nuns that were there from Brazil asked us to get on the end of the bench,” he continued, adding that the nuns told him “that John Paul II was going to stop and that he was going to touch” his son’s head.

“And that’s what happened. Nicolas really stopped the Pope who touched his little head and he was one-and-a-half years old.”

Reflecting on what it meant for him to be in the square again for the canonization of the pontiff who had stopped to bless him, Nicholas said that “being here today is very special because all of that.”

“I think it marked my life a lot. And I think he has helped me in all the moments of my life,” the youth noted, emphasizing that he has “never” lost his faith because “he has always been up there. So today it’s going to be interesting.”

At the same time as pilgrims were giving thanks in St. Peter’s Square, others expressed gratitude for the life and witness of Saint John XXIII, gathering at the Church of San Carlo al Corso, which is the same church where the pontiff had received his episcopal ordination.

Bishop Francesco Beschi, who currently oversees the pontiff’s former diocese of Bergamo, presided over the ceremony, during which he responded to Pope Francis’ April 24 letter thanking the diocese for the gift of John XXIII to the Church.

In his letter, Pope Francis referred to the diocese of Bergamo, Italy as “a land of profound faith lived in daily life, of poor families but united in love of the Lord, of a community capable of sharing in simplicity.”

He affirmed to the people there his certainty that “civil society will always be able to find inspiration in the life of the Pope of Bergamo and of the atmosphere he generated, seeking new ways and adapting to the times in order to build a life based on the perennial values of fraternity and solidarity.”

Referring to the Pope’s statements, Bishop Beschi expressed that such encouragement would help all in the Church there to guard the values of generosity, simplicity, and solidarity which characterized so much of the young Angelo Roncalli, as well as his later pontificate.

The letter also assists Bergamo to respond to the current challenges and signs of the times with the same spirit of obedience espoused by “Good Pope John,” the bishop went on to say.

Concluding, he affirmed that Pope Francis’ words to them will help the diocese to faithfully adhere to the path set by the Second Vatican Council, which was opened by John XXIII in 1962, and during which he called for a renewal in the life of the Church, which would revitalize the faith of all Christians.

Jaji Samatta, Prof Lumumba kutumika kuwarejesha Ukawa bungeni

Huwezi kuwalazimisha watu kuamua jambo ambalo hawalitaki kama ni muundo wa Muungano tunaomba wananchi ndiyo waamue, lakini yote hayo Katiba yetu inatakiwa kubainisha mambo mbalimbali yanayohusu watu wenye ulemavu na haki zao zote,”PICHA|MAKTABA 
Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Wiki hii Bunge Maalumu la Katiba limeahirishwa, kupisha Bunge la Bajeti kuanza vikao vyake vya bajeti kwa mwaka mpya wa fedha wa 2014/15.
Hata hivyo, Bunge hilo limeahirishwa likiwa limegawanyika vipande, baada ya wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutoka nje ya Bunge hilo Aprili 16, wakipinga kejeli, matusi na mambo mengine ya ukiukwaji wa taratibu yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya mawaziri nje ya Bunge.
Kutoka kwa Ukawa nje unaojumuisha vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, DP na wajumbe 25 kutoka kundi la 201 hakukuzuia Bunge hilo kuendelea na vikao vyake. Bunge hilo limeahirishwa Agosti 5, litakapokutana tena mjini Dodoma kuendelea na majadala wa kuijadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba.
Kundi la Tanzania Kwanza linalojumuisha wajumbe wengi wa CCM, wamekuwa wakiwapiga vijembe kuwa warudi bungeni kuendelea na mjadala huo kwani Katiba haitengenezwi nje ya Bunge.
Jukata yasaka suluhu
Kutokana na mgawanyiko huo kuonyesha kuligawa taifa na kuwaacha wananchi wakiwa njiapanda juu ya hatima ya kupata Katiba Mpya, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) linajipambanua kutaka kusaka suluhu ya mvutano huo.
Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba anasema, Jukwaa hilo linajitolea kusaka suluhu kwa kuratibu maridhiano ya makundi yanayovutana ya Ukawa na la Tanzania Kwanza.
Anasema lengo la kusaka maridhiano hayo ni kuhakikisha kabla ya Bunge hilo kuanza Agosti 5, kunakuwapo maridhiano, yatakayowezesha wajumbe wote wanakuwa kitu kimoja katika kujadili maudhui ya rasimu, licha ya tofauti zao za kiitikadi na kimisimamo.
Kibamba anasema wameamua kuwaalika wataalamu ambao wana uzoefu wa siku nyingi katika masuala ya sheria kusimamia maridhiano hayo, yatakayojenga umoja na mshikamano katika taifa.
Wataalamu hao kwa mujibu wa Kibamba ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta anayekuwa mwenyekiti, Profesa Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msuluhishi mwenza sambamba na uwepo wa makundi ya viongozi kutoka Ukawa, Tanzania Kwanza, vyama vya siasa, asasi za wananchi na taasisi zote muhimu zilizoguswa na mchakato huu.
“Katika kujenga Katiba yenye kuwajali wananchi, tunaomba kila upande kuridhia kukutana na kutokuwa na misimamo mikali ili kuhakikisha tunawaunganisha na kuendelea na mchakato huo kama kawaida,” anasema Kimbamba.
Kuhusu uhalali wa Bunge hilo kuendelea na mijadala licha ya Ukawa kutoka nje, anasema sheria za Jumuiya ya Madola kwa mabunge ya Katiba kundi moja linapotoka nje kwa tamko, Bunge hilo hutakiwa kusitishwa.
“Ukawa wametoka nje tena wakiwa zaidi ya 190, Bunge lilitakiwa kusitishwa na kupata maridhiano kwanza si kama wanavyotumia akidi vibaya kuliendesha Bunge hilo,” anasema Kibamba.
Aliongeza: “Jukata bado inaamini kwamba mwaka 2014 Katiba Mpya haitapatikana, hivyo kunahitajika kufanyiwa marekebisho makubwa Katiba ya sasa hasa vifungu vinavyohusu uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi ujao unafanyika kwa amani.”
Maoni ya wadau
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania, Felician Mkude anasema, maridhiano yanahitajika ili kuweza kupata uwakilishi ndani ya Bunge hilo kwa ufasaha.
Anasema, kuendelea na mvutano kuhusu aina gani ya Muungano, si jambo la maana na kinachotakiwa kufanyika ni wananchi kupiga kura ya muundo gani unaostahili.
“Huwezi kuwalazimisha watu kuamua jambo ambalo hawalitaki kama ni muundo wa Muungano tunaomba wananchi ndiyo waamue, lakini yote hayo Katiba yetu inatakiwa kubainisha mambo mbalimbali yanayohusu watu wenye ulemavu na haki zao zote,” anasema Mkude.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Idd Makombe anasema mvutano uliokuwa ukiendelea bungeni kuhusu muundo wa Muungano haukuuimarisha bali unauvuruga.
Dk Makombe anasema, uwazi na maridhiano ndio utakaowezesha kuipata Katiba Mpya yenye kuwajali Watanzania wote.
“Kunahitajika kufanyika kwa kura ya maoni kuhusiana aina gani ya Muungano wananchi wanataka, kwani hivi sasa watu hatuaminiani na huwezi kumlazimisha mtu jambo ambalo halitaki, hivyo pande zote mbili zifikie maridhiano kwa amani,” anasema Dk Makombe.
Mhadhiri wa Chuo Kiuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi na Utawala, Richard Mbunda anasema nchi inapitia katika kipindi kigumu kutokana na kauli na mienendo mbalimbali inayoendelea kujitokeza.
Mbunda anasema viongozi wa kidini na Serikali wanapotoa kauli wanatakiwa kuwa makini, kwani zinaweza kuliingiza taifa katika vurugu za kidini au za kisiasa.
Kauli ya Rais Kikwete
Akizungumza na Vijana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Tanzania Bara na Visiwani juzi kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete amewataka Ukawa kurejea bungeni kuendelea na mjadala wa kutunga Katiba.
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limeingilia kati mpasuko uliojitokeza katika Bunge Maalumu la Katiba kwa kusaka wasuluhishi watakaorejesha maridhiano ya pande mbili zinazokinzana.
Rais Kikwete anasema, katika kuandika Katiba ya Watanzania kunahitajika kufanya maridhiano ili kuhakikisha mchakato huo unamalizika salama kwa wananchi kupata Katiba yenye kujali masilahi yao.
MWISHO

Ushirikiano huu wa ‘Ukawa’ uwe endelevu


Hakuna ubishi kwamba upinzani wenye nguvu huisukuma serikali ichape kazi na kuwatumikia wananchi kwa kutambua kwamba ikiboronga itaondolewa madarakani na serikali kivuli ambayo ni vyama vya upinzani. 
Na Mwananchi
Bila shaka kila mwananchi anayeitakia mema nchi yetu amevutiwa na habari zilizochapishwa katika gazeti hili jana kwamba vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeamua kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
Viongozi wakuu wa vyama hivyo tayari wamekubaliana kuanza mchakato huo na wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.
Sisi tunaona kitendo hicho cha vyama vinavyounda Ukawa kuwa ni hatua muhimu ya kuongeza nguvu ili kuongeza ushindani ambao ni muhimu katika mustakabali wa nchi yetu kisiasa na hivyo kusaidia nyanja nyingine za kiuchumi na kijamii.
Tangu kuruhusiwa tena kwa siasa huru karibu miaka 22 sasa, bado nchi haijashuhudia ushindani wa kweli unaoweza kuwafanya watawala kuwajibika kwa wananchi kutokana na kuona hatari ya kuondolewa madarakani na vyama pinzani.
Hii imetokana na vyama shindani katika siasa kukumbwa na mifarakano ya kisiasa ambayo imekuwa ikiwagawa na hivyo kuingia kwenye chaguzi vikiwa dhaifu na hivyo kushindwa vibaya na chama tawala na matokeo yake yamekuwa ni wananchi wengi kukata tamaa na hivyo kusababisha idadi ya wanaoshiriki kupiga kura kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na kutoona faida ya siasa za ushindani.
Pengine hiyo ndiyo sababu iliyofanya wananchi wapendekeze kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba vyama viruhusiwe kuunganisha nguvu wakati wa chaguzi kwa kuwa wameona bila ya nguvu ya vyama shindani, watawala wawataendelea kuongoza kwa mazoea na matokeo yake ni wananchi kuendelea na umaskini wao na kuona uhuru wa vyama vya kisiasa hausaidii kuwa kuboresha maisha yao.
Si nia yetu kuona chama tawala kikiondolewa madarakani na vyama shindani, lakini tunachotaka kuona na ushindani wa dhati, makini na wa kweli ambao, kwa taifa lolote lile, ni afya kwa ustawi wa wa taifa kwa kuwa huongeza uwajibikaji kwa watawala.
Hakuna ubishi kwamba upinzani wenye nguvu huisukuma serikali ichape kazi na kuwatumikia wananchi kwa kutambua kwamba ikiboronga itaondolewa madarakani na serikali kivuli ambayo ni vyama vya upinzani.
Vyama legelege vya upinzani huogopa kivuli cha serikali na kufifisha maendeleo na kuzima matumaini ya wananchi wanaotaka kuona uwajibikaji serikalini, kwani huwa chachu ya kuendeleza tawala za kiimla zisizothamini demokrasia na zisizowajibika kwa wananchi.
Ndiyo maana tunawapongeza viongozi wa Ukawa kwa kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu na kuwa wamoja ili kuweka ushindani wa kweli katika mazingira ya kisiasa tuliyomo.
Tunachoweza kuwashauri viongozi wa Ukawa ni kuwa makini na kuondoa tofauti zinazowatenganisha. Ukawa isitarajie kwamba kila kitu kitakuwa mteremko, kwani bado sheria kandamizi ambazo zimekuwa zikikwaza shughuli za upinzani bado hazijafutwa.
Ni matarajio yetu kwamba serikali na chama tawala kitachukulia hatua hiyo ya Ukawa kuwa changamoto ya kuongeza ufanisi katika kuwatumikia wananchi na si kuanza kujenga chuki na kutafuta mbinu za kuikwamisha.
Serikali haina budi kuhakikisha kuwa vyama vyote vinapewa nafasi sawa ya ushindani na kujengewa mazingira ya kukua ili kukifanya chama chochote kinachopewa madaraka kiwajibike kwa wananchi na kuwaletea maendeleo.

Nape abeza Ukawa kuungana

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.PICHA|MAKTABA 
Na Raymond Kaminyoge, Mwananchi
Dar es Salaam. Siku moja baada ya vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutangaza kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais na ubunge majimboni, CCM kimebeza hatua hiyo kikisema viongozi hao hawawezi kukaa zizi moja.
Akizungumza jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema viongozi wa Ukawa ni genge la wasaka madaraka hivyo hawawezi kuungana kwa hilo.
Nnauye alisema viongozi wa vyama vya upinzani waliungana kwa lengo la kutafuta Katiba bora, lakini wamebadilisha ajenda na sasa wanazungumzia urais mwaka 2015.
“Hawa kumbe ni waongo, malengo yao siyo Katiba, bali ni kutafuta madaraka, muungano wa kutafuta madaraka hauwezi kufanikiwa kwa sababu viongozi wote wa Ukawa ni wapenda madaraka,” alisema Nnauye.
Alisema wananchi watashuhudia umoja huo ukisambaratika kwa sababu viongozi wa Ukawa hawawezi kuvumiliana na kuachiana madaraka.
“Kuungana ni jambo zuri, lakini sababu za kuungana zinapotajwa kuwa ni kumsimamisha mgombea mmoja wa urais mwaka 2015, watasambaratika kabla ya muda huo kufika,” alisema.
Alisema Ukawa wamewadanganya wananchi kwamba wanasimamia Katiba bora kumbe ajenda kuu ni kuongoza nchi.
Gazeti hili jana liliripoti kuwa Ukawa pia wanataka kusimamisha mgombea mmoja wa ubunge katika kila jimbo la uchaguzi.
Katika habari hiyo, Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia walikiri kuwapo mpango huo.
Taarifa za kuwapo mpango, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri Kivuli ambalo litawajumuisha wabunge wa vyama vya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa bajeti unaoanza Mei 6, mwaka huu.

Sunday, April 27, 2014

Waziri mkuu nchini Korea Kusini ajiuzulu

Waziri mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la ferry iliozama siku kumi na moja zilizopita.
ferry ya Korea kusini iliozama
Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.Bwana Chung alizomwa alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.

JWTZ wadaiwa kutembeza kipigo, wajeruhi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura.PICHA|MAKTABA 
Na Kalunde Jamal, Mwananchi
Wakazi wawili wa eneo la Kiluvya Gogoni, Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, Barnabas Swai (33), Pendo Mchaki (26) na Lugano Kalinga, wamejeruhiwa kutokana na kipigo cha watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWT) na mmoja wao akilazwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Tukio hilo lilitokea juzi na inadaiwa kuwa chanzo cha kipigo hicho ni mmoja wa maofisa wa jeshi hilo aliyefika kwenye baa na mkewe na baadaye ulizuka ugomvi uliodaiwa kuzuka kutokana na mke wa ofisa huyo kudhulumiwa nyama choma, lakini walizidiwa nguvu na kupigwa.
Habari zinasema baada ya tafrani kutokea ofisa huyo wa jeshi aliondoka, baadaye walifika askari na kuanza kupiga watu ovyo njiani, kwenye maduka na baa za eneo hilo na kujeruhi baadhi ya watu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura jana aliliambia gazeti hili kuwa hajapata taarifa za tukio hilo.
“Ofisini kwangu sina taarifa kama hiyo, nashukuru kwa kunifahamisha nitazifanyia kazi,” alisema Wambura. Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Eric Komba hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, baada ya simu yake kutokuwa hewani.
Barnabas inaelezwa amepata majeraha katika maeneo mbalimbali ya mwili na damu imevujia kwenye mapafu, wakati Pendo ambaye ni mkewe alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi na kuruhusiwa.
Hata hivyo, akizungumza kwa shida kutokana na maumivu katika Wodi namba 5A, Hospitali ya Mwananyamala alikolazwa, Swai alisimulia kwamba yeye na mkewe walikuwa kwenye Baa ya Gogoni Inn na waliona watu wanakimbia ovyo eneo hilo na nao walipoamua kukimbia, walivamiwa na wanaodhania kuwa ni askari wa JWTZ kutokana na kuvaa suruali za jeshi na mashati ya kiraia.
Alisema kuwa walipigwa kwa kutumia mikanda ya jeshi iliyokuwa na vyuma, virungu na vitu vya ncha kali na wakati akipigwa alitobolewa eneo la mgongoni na kupata maumivu makali huku akipumua kwa shida.
Hivyo yeye na majeruhi wengine walipelekwa Hospitali ya Tumbi Kibaha kabla ya kuhamishiwa Mwananyamala.
“Walinifanyia upasuaji na kuniweka mpira wa kutoa damu iliyoanza kuganda, lakini kwa sasa naendelea vizuri, ingawa nahisi maumivu makali sehemu ya mgongoni,” alisema Swai huku akiomba apatiwe dawa ya maumivu kutokana na maumivu makali anayoyahisi.
Daktari wa zamu katika wodi namba 5A, katika Hospitali ya Mwananyama Daktari Brian Minja alisema: “Kulingana na faili lake, ‘mgonjwa huyo alipokewa usiku na daktari mwingine, inaonyesha alikuwa na tatizo la kupumua kutokana na damu kuvujia kwenye mapafu. Karibu lita mbili za damu ilitolewa.”
Naye Upendo Swai alisema kwamba mume wake aliumizwa kwa sababu alikuwa akimkinga yeye kuzuia asipigwe zaidi na askari hao na kufafanua kwamba katika kipigo hicho, yeye aliumizwa usoni kwa kukanyagwa na viatu pamoja na kuchomwa na kitu chenye ncha kali eneo la kwapani.
Kwa upande wake Lugano Kalinga ambaye ni mkazi wa eneo hilo, alisema alipigwa na askari hao, ingawa alifanikiwa kukimbia na hakupata majeraha makubwa.
Alisema kilichosababisha wapate kipigo hicho ni ofisa mmoja wa jeshi kugombana na muuza chipsi baada ya kukataa kumlipa fedha zake, ndipo kijana huyo alipigana na ofisa huyo pamoja na mkewe lakini aliwazidi nguvu.
“Baada ya kutoka pale, ndiyo maaskari wakavamia eneo hilo na kuanza kumpiga kila waliyemwona, hali inayoonekana ni kupata maelekezo kutoka kwa huyo ofisa aliyepigana kwenye baa ya Kiluvya, ”alisema Kalinga.

Wafuasi 11 wa Morsi wahukumiwa jela


Mahakama moja nchini Misri imewahukumu wafuasi 11 wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi kifungo cha kati ya miaka mitano hadi minane jela kwa kufanya maandamano.
Wafuasi wa aliyekuwa raia wa Misri Mohammed Morsi
Washtakiwa hao walikamatwa kufuatia msururu wa ghasia zilizozuka baada ya kundolewa madarakani kwa Mohammed Morsi mwaka uliopita.
Mnamo mwezi Machi, zaidi ya wafuasi 500 wa Mohammed Morsi walihukumiwa kifo katika mahakama hiyo hiyo.
kesi hiyo inajiri wakati ambapo kuna msako dhidi ya waislamu wenye itikadi kali wanaomuunga mkono Mohammed Morsi.

Tsvangirai asimamishwa uongozi MDC

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change MDC kimesema kimemsimamisha kiongozi wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.
Morgan Tsvangirai
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti kufuatia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika mji Mkuu Harare.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia kikomo mwezi julai mwaka 2013 baada ya Rais Mugabe kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa rais na Tsvangirai kususia uchaguzi kwa madai ya udanganyifu.Tangu mwaka 2009 hadi 2013 Bwana Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya Waziri Mkuu katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa kwa pamoja na Rais wa sasa Robert Mugabe.
Kushindwa kwake kulipunguza nguvu yake kama kiongozi ambaye alikuwa mshindani mkuu wa Rais Mugabe.
Waangalizi wanasema ndani ya MDC kumekuwa na mgogoro wa kiuongozi kwa miezi kadhaa.
Viongozi wengine wa ngazi za juu wameripotiwa kusimamishwa katika mkutano huo uliofanyika siku ya jumamosi na wanachama wengine wa chama hicho watachukua nafasi zao.

Warioba atunukiwa nishani iliyotukuka

Rais Jakaya Kikwete  akimvisha  Jaji Mstaafu, Joseph Warioba nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la kwanza  wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo hizo iliyofanyika Ikulu jijini  Dar es Salaamu juzi usiku. Picha na Salim Shao 
Na Elias Msuya, Mwananchi
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba juzi usiku alikuwa miongoni mwa viongozi na watu mashuhuri waliotunukiwa nishani na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika maelezo ya kutoa nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la kwanza, ilielezwa kuwa Jaji Warioba, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuenzi na bado anauenzi Muungano huo.
“Katiba kipindi chako, pamoja na nyadhifa nyingine, ulikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani…katika kipindi hicho na hadi sasa umeendelea kuwa mwaminifu, umeutunza, umeulinda na umeuenzi Muungano,” ilisema sehemu ya taarifa ya kutoa nishani.
Hivi karibuni, Jaji Warioba amekuwa akishambuliwa na baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Maalumu la Katiba, pia baadhi ya wanaCCM kutokana na Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiongoza, kupendekeza muundo wa Muungano wa Serikali tatu.
Hata hivyo, upande mwingine wajumbe wanaojitambulisha kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamekuwa wakiunga mkono mapendekezo ya rasimu hiyo.
Mbali na Jaji Warioba, wengine waliopewa nishani katika daraja hilo ni Aboud Jumbe Mwinyi aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Aman Karume, John Malecela, Cleopa Msuya na Dk Salmin Amour Juma.
Wengine ni Omar Ali Juma na Idrissa Abdul Wakil, ambao sasa ni marehemu.
Walioanza kupata tuzo na nishani hizo ni waasisi wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume(wote ni marehemu) na walioendeleza ambao ni Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
Wengine waliopewa tuzo ni pamoja na viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama akiwemo Mkuu wa Jenshi la Wananchi (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Wakuu wa JWTZ wastaafu pia walikumbukwa akiwemo, Jenerali Mirisho Sarakikya, Jenerali David Musuguri.
Katika nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne lilikuwa na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume, Bendi ya Msondo Ngoma pia ilipewa tuzo kwa kuuenzi Muungano.
Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi alipewa tuzo maalumu akiwa raia wa Tanzania aliyetoa mchango muhimu katika huduma za jamii.
Wasifu
Joseph Warioba aliingia serikalini mwaka 1966, akiwa mwanasheria wa mji wa Dar er Salaam, nafasi aliyoitumikia kwa muda wa miaka miwili, kisha kuhamia kuwa mwanasheria wa Baraza la Jiji mpaka mwaka 1970.
Kuanzia mwaka 1976 mpaka 1983 Warioba alitumikia taifa kwa wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Warioba pia aliwahi kuwa Waziri wa Sheria katika awamu ya kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere.
Mwaka 1984 aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 1990.
Mwaka 1996 Rais Benjamin Mkapa alimteua kuongoza tume ya kupambana na rushwa.
Mwaka 2007 alioongoza jopo la waangalizi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola katika uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Nigeria.
Mwaka 2012 Rais wa awamu ya nne alimteua Warioba kuongoza Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Saturday, April 26, 2014

HONGERA TANZANIA KWA KUTIMIZA MIAKA 50 YA MUUNGANO

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, wanatoa hongera kwa Watanzania wote kwa kuadhiumisha kwa kishindo miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, leo.

MWEMBE ULIOPANDWA NA NYERERE NA KARUME KATIKA IKULU YA DAR ES SALAAM WATIMIZA MIAKA 50 LEO

Wakati wa Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili 1964, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Zanzibar Abeid Amaan Karume ambao sasa wote ni marehemu,  walipanda katika shimo moja miembe miwili mmoja kutoka Zanzibar na mwingine kutoka Tanganyika. Miembe hiyo imekuwa na kustawi pamoja na kufanya shina moja 'through grafting' .Leo hii mti huo wa mwembe umestawi vyema katika bustani ya Ikulu, Dar es Salaam, kama unavyoonekana leo Aprili 26, 2014 ambayo ni Siku ya miaka 50 ya Muungano.

Kingunge apinga matusi, kejeli dhidi ya Warioba

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza katika kikao cha Bunge hilo, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi  
Na Habel Chidawali, Mwananchi
Dodoma. Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale-Mwiru amekemea kauli za kejeli na matusi dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Akichangia mjadala wa Rasimu ya Katiba, alisema wanaombeza Warioba wanapaswa kuacha mara moja tabia hiyo kwa kuwa hawamtendei haki.
“Siyo sawa hata siku moja kumshambulia Warioba eti kwa sababu ya misimamo yenu ya vyama, hata mimi japo nimestaafu lakini bado ni mwanaCCM kwa hiyo tabia hii ni mbaya na haileti heshima,” alisema Kingunge.
Alisema kuwa misimamo ya vyama inapotokea kuwatukanisha watu tena wenye heshima zao inakuwa ni aibu kwa chama pamoja na jamii kwa jumla na inaondoa heshima ya mtu.
Kauli ya Kingunge imekuja zikiwa zimepita siku chache baada ya kujitokeza kwa hali ya mashambulizi ya matusi ndani ya Bunge ambayo yalikuwa yakielekezwa kwa Warioba kuhusu tuhuma za kuchakachua maoni ya wananchi.
Tuhuma za hivi karibuni zilitoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia ambaye alimtaka Waziri Mkuu huyo wa zamani kufunga mdomo wake kwa kuwa kazi yake imekwisha.
Mbali na huyo, Mbunge wa Mbinga Mashariki, John Komba alimfananisha Warioba na Adam na Hawa ambao waliasi katika Bustani ya Edeni.
Akizungumzia Rasimu, mkongwe huyo alisema Katiba haitapatikana pasipokuwapo na maridhiano na makubaliano na akawataka wajumbe wa kundi la Umoja wa Katiba warudi bungeni ili waweze kujadiliana na kutengeneza katiba ya wananchi.
Kingunge aliwasifia waganga wa tiba za jadi kwa kumpendekeza kama mlezi wao tangu 1998 ili aweze kuwawakilisha hivyo akasema hakubebwa wala kupita njia za panya kama ambavyo wengine wanasema.
Pinda awaomba Ukawa warudi bungeni
Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana alitumia dakika 13 alizopewa na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kuwaomba wajumbe wa kundi la Ukawa kurejea bungeni ili waweze kukubaliana katika utungwaji wa katiba ya wananchi.
Pinda alisema, “Yaliyopita si ndwele, naomba nitumie nafasi hii kuwasihi sana hawa ndugu zetu waliosusia Bunge, warudi tukubaliane pamoja katika kutengeneza katiba ya wananchi.”
Hata hivyo, alikiri ofisi yake kutuma maoni kuhusu muundo wa serikali tatu lakini akakanusha kuwa yeye hakuhusika bali waliotuma ni watumishi katika ofisi yake na walifanya hivyo kwa utashi wao.
Kwa mujibu wa Pinda yeye, alipeleka mawazo yake kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu ambayo hayakuzungumzia serikali tatu kwa hiyo mawazo ya watumishi ofisini kwake yasibebeshwe kuwa ndiyo mawazo yake.
Sitta asita kutoa adhabu
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta alitoa sababu za kutowachukulia hatua baadhi ya wajumbe ambao walionekana kuwa na shida ndani ya bunge akisema ilitokana na busara za kiti chake kuepusha migogoro zaidi.
Sitta alisema katika kutoa uamuzi, walikubaliana na Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan kwamba kama wangechuka uamuzi wowote huenda wangesababisha migogoro zaidi  kwa wajumbe.
“Tulishauriana na Makamu wangu kuwa tutasababisha mambo mengi hapa ikiwamo kuongeza matusi na kwa hiyo busara tulizitanguliza mbele,” alisema Sitta.
Mwenyekiti huyo aliahirisha shughuli za Bunge la Katiba hadi Agosti 5 mwaka huu ili kupisha Bunge la Bajeti ambalo linatarajiwa kuanza vikao vyake Mei 5 mjini Dodoma.

Warioba: Matusi, uongo vinaniumiza

Jaji Joseph Warioba 
Na Goodluck Eliona, Mwananchi
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wametumia vibaya Bunge hilo kwa kumshambulia na kumsingizia mambo ya uongo kwa makusudi, akisema matusi yanayotolewa dhidi yake yanamuumiza.
Aidha, Warioba amesema ingawa haelewi kwa nini wanaomshambulia wameamua kutumia lugha za matusi dhidi yake binafsi, hatajutia kuchaguliwa kuiongoza tume hiyo kwa kuwa ilikusudia kuwaletea maendeleo wananchi wote kwa kuwapatia Katiba wanayoitaka.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja wakati baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na viongozi wa CCM wakiikosoa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba kwa maneno makali,huku wakimshutumu na kumkejeli yeye na baadhi ya wajumbe wa tume aliyoiongoza.
Akizungumza kwa mifano katika mahojiano na gazeti hili jana, Warioba alisema kuwa anawashashangaa wajumbe hao na viongozi wa CCM kwa kuacha kuijadili Rasimu ya Katiba, badala yake wanamkosoa yeye na kumsingizia maneno yasiyo ya kweli.
“Bulembo (Abdallah Bulembo mjumbe wa Bunge na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM) amenitukana, amenitukana… amesema niliwahi kupokea rushwa huku akijua kabisa kuwa ni uongo. Yeye ni kiongozi wa Kamati Kuu ya CCM, anasema uongo akijua ni uongo. Kwanza mimi simjui wala sijawahi kumwona huyu mtu naambiwa tu anatoka Mara,” alisema Jaji Warioba kwa sauti ya upole iliyoashiria kuumizwa.
Aliongeza kwamba siyo mara ya kwanza kwa Bulembo kumshambulia kwa lugha za matusi, kwani aliwahi kufanya hivyo tena kwenye moja ya mikutano ya CCM mkoani Tanga.
“Alifanya hivyo Tanga, anachokifanya siyo kitu cha mzaha kwa sababu anafahamu kilichotokea,” alisema.
Akizungumzia kauli aliyoitoa Waziri Hawa Ghasia wakati akichangia mjadala wa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba aliyemtaka Jaji Warioba kufunga mdomo kutokana na kazi yake ya kuwasilisha Rasimu kumalizika, Jaji Warioba alisema: “Wao wanataka waseme uongo, mtu mwingine asiseme kitu.”
Warioba alieleza kuwa tangu lugha za matusi na kejeli zilipoanza kutolewa dhidi yake, baadhi ya watu walimshauri kwenda mahakamani kufungua kesi, lakini alikataa kwa kile alichodai kuliheshimu Bunge.
Alisema Bunge ndiyo lenye mamlaka ya kufuatilia na kudhibiti kauli zinazotolewa bungeni, kama wahusika hawafanyi hivyo hawezi kuchukua hatua yoyote.
“Kama kinga ya Bunge inatumika vibaya unafikiri mimi nitafanya nini? Sina nia ya kuchukua hatua, watu walipendekeza niende mahakamani, kuna wanasheria walisema hata nisipokwenda, wao watakwenda mahakamani nikawazuia,” alisema Warioba ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu.
Akisimulia kuhusu uchaguzi wa ubunge wa mwaka 1995 ambapo aligombea na kutuhumiwa kupokea rushwa na kufungiwa kwa miaka minne, Warioba alisema taarifa hizo siyo sahihi kwa kuwa aliyepokea rushwa ni aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya NCCR Mageuzi (wakati huo), Stephen Wassira ambaye sasa yuko CCM na ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu.
“Uchaguzi ule ulikuwa umejaa sana rushwa, tukaenda mahakamani, Wassira akafungiwa asigombee,” alisema.
Akizungumzia maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Warioba alisema: “Mimi ni muumini wa muungano, kwa miaka 50 taifa limekaa kwa amani, mshikamano na umoja. Ni kweli tumekuwa na matatizo lakini yanaweza kutafutiwa ufumbuzi.”

Palestina kulitambua taifa la Israel

Rais wa Palestina Mohmuoud Abbas
Rais wa Palestina, Mahmuoud Abbas amesema serikali ya pamoja itakayowajumuisha kundi la Hamas, italitambua taifa la Israel na wajibu wa kitaifa pamoja na kutangaza kusimamisha machafuko.
Bwana Abbas amelimbia baraza kuu la chama cha kisiasa cha PLO, kwamba bado angelipenda kuendelea na mazungumzo ya amani na Israel.
Israil imesimamisha mazungumzo hayo baada ya kutangazwa kwa serikali ya pamoja ambayo itaongozwa na bwana Abbas na Hamas wanaotawala himaya ya ukanda wa Gaza.
Rais wa Palestina ametetea makubaliano hayo ya serikali ya pamoja na kusema hawezi kuwabana na kuwakana raia wake walioko Gaza na wala kukataa kuendelea na mazungumzo ya amani na Israil.

Tanzania yagonga miaka 50

“Nakerwa  zaidi na Zanzibar kuwa na Katiba yao , wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Zanzibar ni sehemu ya nchi yake pia. Wakati wa Sherehe za Muungano, Rais wa Zanzibar ndiye anaonekana mwenye nguvu, kitu ambacho siyo sahihi. Rais wa Tanzania ndiye apewe hadhi kubwa,” Padri Francis Shawa 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar/ Mikoani.  Wakati leo ni maadhimisho ya  miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa taifa la Tanzania, wasomi, viongozi wa dini, watendaji wa Serikali na wananchi wa kawaida wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu uhai wa Muungano huo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi walitaka Muungano huo uvunjike kwa madai ya kutokuwa na manufaa yoyote, au uwe wa Serikali moja, huku wengine wakitaka uenziwe kwa sababu ndiyo chachu ya amani, umoja na mshikamano uliopo sasa.
Moshi
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St. Augustine, Padri Francis Shawa alisema: “Muungano uendelee ila kuwe na serikali moja kama ilivyokuwa awali na Rais akitoka Zanzibar makamu atoke Bara na kusiwe na marais wawili.”
Alisema  wadhifa wa Rais wa Zanzibar na makamu wake viondolewe na pande zote zikubali baadhi ya vitu kutoa sadaka kwa kuvipoteza.
“Nakerwa  zaidi na Zanzibar kuwa na Katiba yao , wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Zanzibar ni sehemu ya nchi yake pia. Wakati wa Sherehe za Muungano, Rais wa Zanzibar ndiye anaonekana mwenye nguvu, kitu ambacho siyo sahihi. Rais wa Tanzania ndiye apewe hadhi kubwa,” alisema.
Diwani wa Kata ya Kilema Kusini, Kawawa Lubega alipendekeza Serikali mbili na alitoa sababu kuwa hata Serikali mbili za sasa bado wananchi hawajazifahamu vizuri. Lubega alisema kwamba shirikisho la serikali tatu litasababisha Rais atakayekuwapo madarakani akose nguvu kiuchumi na kiutawala.
Ofisa Elimu wa Shule za Sekondari za Wilaya ya Moshi, George Jidamva alipendekeza kuwapo kwa serikali mbili, lakini akashauri Katiba zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar, ziwekwe mezani ili dosari zilizopo zirekebishwe akitaja kipengele cha madaraka ya Rais.
Mwanasheria wa Serikali, Wilaya ya Moshi, Glorian Issagya alipendekeza pia serikali mbili ziendelee, lakini akasema wabunge waliojitoa bungeni, warudi ili changamoto zinazojitokeza ziweze kufanyiwa kazi zisije zikaleta athari hapo mbeleni.
Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, mwanasheria huyo alipendekeza ungepitia kwenye Halmashari za Wilaya na hali hiyo ingekuwa rahisi kwa kila mtu kutoa maoni yake kwani atakuwa amepata elimu kupitia vitongoji, vijiji hadi kata.
Songea
Naye mwanasiasa, Asha Kitambuli mkazi wa Wilaya ya Tunduru alisema kuwa binafsi anapenda Muungano uendelee kuwapo akieleza kuwa una faida nyingi na kwamba  wanaopenda uvunjike ni waroho wa madaraka na wabinafsi, akataka waache kuvuruga Muungano.
Kwa habri zaiddi ingia http://www.mwananchi.co.tz/

Tuesday, April 22, 2014

Waasi wa Sudan Kusini wakana mauaji

Waasi wa Sudan Kusini wamekana mauaji ya raia kwa misingi ya ukabila
Waasi nchini Sudan Kusini wamekanusha madai yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuwa waliwaua watu kwa misingi ya ukabila.
Msemaji wa waasi, Brigedia Lul Ruai Koang, ameambia BBC kuwa wanajeshi wa serikali ndio waliowaua raia walipokuwa wanaondoka mji wa Bentiu uliotekwa wiki jana na waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar.
Jeshi la Sudan Kusini linasema kuwa linakabiliana vikali na waasi hao katika majimbo matatu nchini Sudan Kusini.Umoja wa Mataifa katika ripoti yake iliyotolewa Jumatatu, ulisema kuwa takriban watu miambili waliokuwa wamepewa hifadhi msikitini na wengine wengi wakiwa wanahifadhiwa hospitalini na makanisani waliuawa kwa sababu ya kabila lao.
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuondoka makwao tangu mapigano kuanza Disemba mwaka jana.
Mgogoro huo ni kati ya Rais Salva Kir wa kabila la Dinka na Riekl Machar aliyekuwa makamu wa Rais anayetoka kabila la Nuer
Pande zote mbili zinasemekana kufanya mauaji.
Lakini mauaji yaliyofanywa na waasi mjini Bentiu, Bor na Malakal, umewafanya watu kumchukia kiongozi wa waasi Riek Machar.
Mapigano huenda yakaanza tena ingawa pia mazungumzo ya kusitisha vita yanatarajiwa kuanza nchini Ethiopia katika wiki chache zijazo.
Kumekuwa na taarifa za jeshi kuwalenga watu wa kabila la Nuer huku waasi wakiwalenga watu wa jamii ya Dinka.

David Moyes atimuliwa na Manchester U

Moyes amekuwa na Man U kwa miezi kumi pakee
Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini.

Wakulima wa nyanya Iringa watakiwa kuunda vikundi


Na Geofrey Nyang’oro,Mwananchi
Iringa. Wakulima wa nyanya mkoani Iringa, wameshauriwa kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na misaada mbalimbali pamoja na mikopo kutoka katika taasisi za fedha ikiwamo benki na vicoba ili kuinua thamani ya mazao wanayozalisha.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gelard Guninita wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Nyanya iliyofanyika katika Kijiji cha Nzih Tarafa ya Kalenga mkoani hapa.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Muunganisho wa Ujasilimali Vijijini (Muvi) kwa ushirikiano na wadau wa kilimo kutoka sekta binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa za taasisi hiyo, zao la nyanya katika mkoa huo limeongezeka kutoka tani 100,009 mwaka 2010 na kufikia tani 100,400 kwa kipindi cha mwaka 2013 katika maeneo ambayo taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Guninita, ambaye alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alisema ikiwa wakulima hao wataunda vikundi na kusajili, watakuwa wametambuliwa na kuwa na sifa za kupata mikopo katika taasisi za fedha jambo linaloweza kuwasaidia kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli zao. “Ninaomba mjiunge katika vikundi na sisi serikalini tunasaidia pale itakapoonekana kuna ulazima,” alisema.

Mbowe: Hakuna aliyemtusi Mwalimu Nyerere, wala anayetaka kuvunja Muungano

Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa), Freeman Mbowe, amesema uamuzi wao wa kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge ni sahihi kwa kuwa ni njia ambayo imeonekana kwao kuwa inafaa kudai haki ya Watanzania wote.
Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa ndani wa Ukawa.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulijadili mikakati mbalimbali inayohusu umoja huo ambao sasa wanapeleka masuala yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa wananchi.
Ukawa pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka kundi la 201, walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini wakidai kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo lenye lengo la kutengeneza Katiba Mpya.
“Kuendelea kushiriki mchakato huu, ni kuubariki na kuupa uhalali udhalimu unaoendelea ndani ya Bunge Maalumu, hatuwezi kushiriki mjadala wenye matusi, kejeli, dharau na unaopotosha umma, kwa kupindisha kauli zilizowahi kutolewa na viongozi wetu,’ anaeleza Mbowe.
Mbowe anasema wajumbe wa upande wao kila walipotoa mtazamo wao, wakieleza ukweli, wajumbe wa upande wa pili wanapopata nafasi ya kuchangia mjadala badala ya kutoa mapendekezo yao na kuyatetea kwa hoja, wanageuza ukweli wa maoni yaliyotolewa na wale wa upande wa Ukawa, anasema ni karaha ambayo ni vigumu kuielezea ikaeleweka.
Akahoji wanaodai wamekosea kujitoa katika mijadala hiyo ikiwa wanafurahishwa na udhalilishaji ambao wamefanyiwa tangu kuanza mjadala unaohusu sura ya kwanza na sita za Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.
Anataka pia watu wajiulize, je kwa mchakato wa aina hii kitapatikana kile wanachotaka? Anasema kazi yao kama vyama vya siasa ni kuweka shinikizo na kujenga hoja zenye kushinikiza kupatikana kile kinachohitajika kwa masilahi ya taifa.
Anasema hawawezi kuwa sehemu ya mijadala inayopuuza maoni ya wananchi ambayo yamepatikana kwa kukusanywa na chombo (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) kilichoundwa na serikali na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria iliyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Mbowe anabainisha kuwa baada ya kubaini kutokuwapo uwezekano wa kubadili nyendo za wenzao bungeni, wakaafikiana kuwa kinachofuata ni kuunda busara yoyote ambayo wanaweza kuitumia kuokoa taifa dhidi ya genge la watu kama wale, ambao wamekaririshwa maneno.
“Wao wanatulaumu Ukawa tunaweka misimamo, lakini wao wanakuja na mambo ambayo wameyajadili katika mikutano yao ya ndani na Waziri Mkuu akiwa miongoni mwao. Wanaweka mikakati ya kuzomea, watu wanazomewa pale, kauli za utenganisho zinatajwa na watu wanashangilia bila kujali kuwa wanapasua taifa - hatuwezi kuendelea kuwa sehemu ya wapasua taifa,” anasema Mbowe.
Anasema wameamua kwenda kwa wananchi kuwaambia kinachoendelea bungeni, wao ndiyo wataamua anasema kadhalika waliobaki siku za usoni wanaweza wakapata busara wakaona kuwa kutunga Katiba peke yao ni jambo lisilo na uhalali.

DC Chang’a kuzikwa Iringa kesho

Waombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a aliyefariki dunia juzi wakimpa pole mtoto wa marehemu, Chiku (katikati) nyumbani kwake, Mbagala-Kibonde Maji, Dar es Salaam. Picha na Salhim Shao 
Na Raymond Kaminyoge na Musa Mwangoka, Mwananchi
Dar/Rukwa. Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Moshi Chang’a aliyefariki dunia juzi atazikwa kesho Kihesa mkoani Iringa.
Chang’a alifariki juzi saa 10.15 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa tangu Machi 29, mwaka huu kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Mdogo wa marehemu, Faustine Kikove alisema jana kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa leo saa 10.00 jioni kwa gari kwenda Iringa.
Alisema kabla ya kusafirishwa, mwili wa Chang’a utaagwa nyumbani kwake Mbagala Kibondemaji kuanzia saa 8.00 mchana na utazikwa kesho baada ya swala ya adhuhuri.
Akimzungumzia marehemu, alisema wakati akiwa Kalambo, alimpigia simu akimweleza kuwa hajisikii vizuri na kwamba alikuwa anakwenda Muhimbili kwa ajili ya kuchunguza afya yake.
“Hatukujua kwamba hali yake ingebadilika ghafla, tulijua anakwenda kuchunguzwa afya na angerejea salama kuendelea na majukumu ya kitaifa lakini haikuwa hivyo,” alisema .
Akizungumzia kifo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema ni pigo kwa Wanakalambo na mkoa mzima kwa jumla.
“Tumepoteza kiongozi ambaye alikuwa mwongoza njia ambaye wananchi aliowaongoza walimpenda kwa ucheshi wake na uchapakazi,” alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema katika vikao vya wakuu wa wilaya, Chang’a alikuwa mwalimu kutokana na uzoefu wake wa kutumikia nyadhifa mbalimbali za Serikali.
“Alitufundisha mambo mengi kutokana na uzoefu wake, pia kwa sababu ni mwalimu kitaaluma na kiongozi wa muda mrefu CCM,” alisema Rugimbana.
Nyumbani kwa marehemu viongozi walifika kutoa pole kwa wafiwa, wakiwamo Manyanya na Rugimbana ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.