Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, September 30, 2013

DAYOSISI ZASHEREHEKEA SIKUKUU YA MIKAEL NA WATOTO NA HAPA NI KATIKA DAYOSISI YA IRINGA JIMBO LA KASKAZINI USHARIKA WA KIHESA

    HAPA NI MKUU WA JIMBO LA KASKAZINI MCHG.DONALD KIWANGA AKIWA NA MSAIDIZI WA ASKOFU WA DAYOSISI YA KUSINI(NJOMBE) MCHG.DR. GERGE FIHAVANGO

 WATOTO WAKISOMA ZABURI TOKA  ZABURI 103:1-6


 MSAIDIZI WA ASKOFU WA DAYOSISI YA KUSINI (NJOMBE) MCHG.DR. GERGE FIHAVANGO AKITANGAZA MSAMAHA WA DHAMBI
     MTOTO ONESMO MBILINYI AKISOMA SOMO LA PILI TOKA UFUNUO WA YOHANA 12:7-12







                         MKUU WA JIMBO LA ILEMBULA TOKA DAYOSISI YA KUSINI AKITOA SALAM
    PICHANI WA KWANZA NI MCHUNGAJI BARODA MKUU WA JIMBO LA ZANZIBAR NA MKUU WA ENEO LA ZANZIBAR AKIWA NA MCHUNGAJI YUSTO KINYOA WA USHARIKA WA KIHESA
MKUU WA JIMBO LA KASKAZINI MCHG.DONALD KIWANGA

           MSAIDIZI WA ASKOFU WA DAYOSISI YA KUSINI(NJOMBE) MCHG.DR. GERGE FIHAVANGO AKITOA  MAFUNDISHO MAALUM LA IMANI NA UJASIRIAMALI

          MSAIDIZI WA ASKOFU WA DAYOSISI YA KUSINI(NJOMBE) MCHG.DR. GERGE FIHAVANGO
 HAPA NI MKUU WA JIMBO LA KASKAZINI MCHG.DONALD KIWANGA AKIWA NA MSAIDIZI WA ASKOFU WA DAYOSISI YA KUSINI(NJOMBE) MCHG.DR. GERGE FIHAVANGO
 HAPA NI MKUU WA JIMBO LA KASKAZINI MCHG.DONALD KIWANGA AKIWATAKIA WASHARIKA BARAKA ZA BWANA ZIWE NAO WANAPOTAWANYIKA

Makabiliano yazuka mjini Kidal, Mali

Makabiliano makali yameibuka kati ya wanajeshi wa Mali na watu wanaoshukiwa kuwa waasi katika eneo la Kidal Kaskazini mwa Mali na kusababisha hofu kuwa ghasia huenda zikakithiri.
Wapiganaji wa MNLA Kaskazini mwa Mali
Waasi hao waliwashambulia wanajeshi waliokuwa wanalinda benki mjini humo na ambao waliwafyatulia riasi.
Mkataba wa amani uliofikiwa mwezi Juni, ulikuja baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano ambao ulisababisha jeshi la Ufaransa kuingilia kati.Wenyeji walioshuhudia tukio hilo na maafisa ambao hawakutajwa, walisema kuwa waasi kutoka kundi la Tuareg ambao walisema wanapuuzilia mbali makubaliano ya amani waliyoafikia na serikali.
Majeshi hayo yangali yanashika doria Kaskazini mwa Mali na jeshi la Mali limerejea mjini Kidal katika hali isiyoeleweka.
Mji huo ulikuwa mikononi mwa waasi wa (MNLA) kwa miezi mingi.
Gavana wa eneo hilo Adama Kamissoko aliambia shirika la habari la AFP mjini Kidal kuwa walisikia milio mingi ya risasi, na kwamba wanajeshi wa Mali walilemewa na kuondoka sehemu hiyo ingawa alisema hangeweza kuwatambua wapiganaji hao.
Hapakuwa na taarifa zozote kuhusu majeruhi kwenye makabiliano hayo.
Vurugu za Jumapili ndizo za hivi punde kutokea katika eneo hilo. Mnamo Ijumaa wanajeshi wawili walijeruhiwa mjini Kidal wakati waliporushiwa guruneti.

Ujasusi hautajwi hadharani yasema Kenya

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi, waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa Kenya alitupilia mbali swala kwamba serikali ya Kenya ingefaa kuzindukana baada ya kupata habari mapema kwamba kuna uwezekano wa shambulio kubwa la kigaidi kutokea katika mji mkuu.
Joseph Ole Lenku
Waziri Joseph Ole Lenku alilitoa maanani swala hilo la mwandishi wa BBC na kusema kuwa taarifa za ujasusi, yaani intelijensi, ni swala la serikali:
"Sifikiri kama weye ndie wa kuniambia mimi nini serikali ingefaa kusema au la.
Kuhusu taarifa na ujasusi wetu, hilo halijakuhusu.
Tumeonesha hapa, na tunaendelea kusema, kuwa taarifa za ujasusi zitabaki hivohivo, habari za ujasusi; na hatutasema hadharani.
Kwa hivo intelijensia yetu ni siri na siyo kitu tutakizungumza hadharani."
Waziri huyo wa Kenya piya alizilaumu nchi, pamoja na Marekani, ambazo zimeonya wananchi wao wasiende Kenya.
Alisema ilani kama hizo hazihitajiki na wala si za kirafiki na hazisaidii katika kupambana na ugaidi wa kimataifa.
Alisema Kenya haitawaachia magaidi kuwatia khofu watu wa Kenya.

Chuo kilichovamiwa Nigeria kilikosa ulinzi

Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
mauaji ya Nigeria
Wanafunzi waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu katika mabweni yao katika jimbo la Yobe , Kaskzini Mashariki mwa Nigeria.
Afisa mmoja aliambia BBC kuwa serikali itashirikiana na jeshi kuhakikisha kuna ulinzi katika shule.
Serikali ya Nigeria ilisema kuwa haitafunga shule zingine kutokana na shambulio lililowaua wanafunzi 50 katika chuo kikuu cha mafunzo ya kilimo.
Shambulio hilo linashukiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram siku ya Jumapili.Wavamizi walishambulia kwa risasi chuo hicho kilichoko jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Afisa mmoja wa serikali Abdullahi Bego, ameambia BBC kuwa serikali na idara ya jeshi zitaongeza usalama katika taasisi zote za elimu.
Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limewekwa katika hali ya hatari kufuatia mashambulio yanayofanywa kila mara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Boko Haram wanadaiwa kupigana kwa lengo la kuiondoa serikali iliyoko na badala yake kuweka utawala wa kiislamu. Tayari wamefanya mashambulio kadhaa katika shule.

Vyombo vya usalama

Mwandishi wa BBC wa idhaa ya Hausa, Mansur Liman, anasema kuwa huenda jeshi la Nigeria imelegeza juhudi zake kufuatia kufanikiwa kwao katika siku za hivi punde kuwaondosha wapiganaji wa Boko Haram kutoka maeneo mengi kaskazini mashariki.
Hata hivyo wapiganaji hao wameripotiwa kuiba sare za kijeshi katika siku kadhaa zilizopita na magari ya kivita. Inadaiwa wanatumia vifaa hivi kupenya maeneo yaliyowekwa ulinzi mkali.
Mshauri mkuu wa serikali katika Jimbo la Yobe, Abdillahi Bego, ameambia BBC, Jumatatu, kuwa hakukuwepo walinzi katika eneo hilo wakati shambulio lilifanywa katika chuo kikuu.
Amesema kuwa maafisa wa usalama wa Nigeria walistahili kuimarisha doria katika taasisi za elimu zote.
Amesisitiza kuwa shule zingine hazitafungwa kwani hilo ndilo hao ''magaidi'' wanataka.

Idadi ya waliopotea yapungua Kenya

Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa idadi ya watu waliopotea kutokana na shambulizi la kigaidi la Westgate, imepungua hadi 39 kutoka 61, idadi iliyotangazwa awali na shirika hilo awali.
Vikosi vya Kenya vilifanikiwa kuwaua magaidi watano
Kati ya watu hao, 14 wamepatikana wakiwa hai na miili saba ikipatikana katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Kwa mujibu wa serikali, watu 67 waliuawa baada ya wanamgambo wa Al Shabaab kuvamia jengo la Westgate mjini Nairobi, tarehe 21 Septemba.
Wabunge wameanza kuchunguza taarifa za ulegevu upande wa maafisa wa ujasusi na wa serikali.
Shirika la Red Cross linasema kuwa baadhi ya jamaa za wale waliokuwa wameripotiwa kupotea kwa jamaa zao, hawakutoa taarifa wakati walipowapata.
Afisaa mmoja wa shirika hilo, ameambia BBC kuwa baadhi ya ripoti walizokuwa nazo zilikuwa kutoka kwa jamaa waliokuwa na wakati mgumu kuwapata watu wao.
Serikali ilisema kuwa hadi sasa hakuna watu wowote ambao wanasemekana kupotea baada ya kutokea shambulizi hilo na kuwa hakuna mateka wowote waliouawa wakati jengo la Westgate lilipoporomoka.
Hata hivyo, vifusi vingali vinaondolewa na kwa hilo waziri wa usalama akasema kuwa miili zaidi huenda ikapatikana.
Magaidi watano waliuawa na vikosi vya usalama, wakati wa uvamizi huo wakati watu tisa wakikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo la kigaidi.
Kundi la kigaidi la Al Shabaab lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo kulipiza kisasi hatua ya Kenya kujihusisha na vita nchini Somalia.

TAMASHA LIKEIELEKEA UKINGONI NI KWAYA ZA AWAMU YA PILI SASA BAADA YA MATOLEO NA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA HILI NA KUSAIDIA ENEO LA MISIONI LILILOPO RUAHA MBUYUNI IRINGA

Wakiwa wenye furaha ni Msaidizi wa Askofu wa Datyosisi ya iringa Mchungaji Blastone Gavile akiwa na Binti yake Eresi Blastone  wakifuatilia Tamasha la uimbaji uliofanyika katika Usharika wa Mkwawa jana 29.09.2013

Serikali ya Syria yatangaza utayari wake wa kushirikiana na Umoja wa Mataifa UN juu ya azimio la kuteketeza silaha zake za kemikali

Rais wa Syria Bashar Al Assad ambaye ametangaza utayari wa nchi yake kutoa ushirikiano kwa Umoja wa Mataifa UN juu ya kutetekeza silaha zake za kemikali
Rais wa Syria Bashar Al Assad ambaye ametangaza utayari wa nchi yake kutoa ushirikiano kwa Umoja wa Mataifa UN juu ya kutetekeza silaha zake za kemikali
Na Nurdin Selemani Ramadhani
Serikali ya Syria imesema ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Umoja wa Mataifa UN katika kuhakikisha azimio lililopitishwa juma lililopita la kutaka kuangamiza silaha za kemikali wanazozimiliki linafanikiwa na kutekelezwa kwa namna ambavyo Umoja huo inaona ni sahihi.
Serikali ya Syria chini ya rais Bashar Al Assad imesema itafanya kila linalowezekana katika kuhakikisha azimio hilo linatekelezwa iapsavyo na wapo tayari kuwapokea Waatalam wa Masuala ya Silaha za kemikali ambao wanaelekea Damascus kuanza kazi hiyo.
Rais Assad amesema watashirikiana na Umoja wa Mataifa UN ili kuhakikisha azimio hilo linafanywa kazi kutokana na wao kuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya silaha za kemikali ndani ya mipaka yake kwa kuwa wanafahamu madhara yake ni makubwa kwa wananchi.
Serikali ya Syria imesema hakuna sababu yoyote kwa wao kuzuia kufanyika kwa shughuli hiyo ya kuangamiza silaha za kemikali wanazozimiliki kutokana na kuonekana ni hatari kwa usalama wa wananchi wake.
Kauli ya Serikali inakuja ikiwa ni majuma mawili tangu Rais Assad aweke bayana suala la kuangamiza silaha za kemikali wanazozimiliki litachukua zaidi ya mwaka mmoja sanjari na gharama zake ambazo ni dola za Marekani bilioni moja.
Haya yanakuja huku Wataalam ishirini wa Masuala ya Silaha za Kemikali wakitarajiwa kuwasili Damascus kwa ajili ya kuanza kuangalia namna amnavyo itafanyika ili kuhakikisha silaha hizo zote zinateketezwa haraka iwezekanavyo.
Kazi ya kwanza ya wataalam hao itakuwa ni kufanya uchunguzi na kubaini maeneo yote ambayo silaha hizi zimehifadhiwa ikiwa ni pamoja na idadi yake kabla hawajatoa ushauri wa namna nzuri ya kuhakikisha silaha hizo zote zinaangamizwa kwa wakati.
Zoezi hili linaendelea kipindi hiki kumekuwa na juhudi za kuhakikisha pande zinazohasimiana kwenye mgogoro wa Syria zinarejea kwenye meza ya mazungumzo ili kusaka suluhu kwa njia ya majadiliano badala ya kutumia nguvu za kijeshi.
Kiongozi wa Upinzani Ahmad Jarba alikutana kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ambapo alimhakikishia watapeleka ujumbe wao kwenye mazungumzo ya Geneva.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Walid Muallem amesisitiza kuwa wataenda kwenye mazungumzo ya Geneva lakini hakuna sharti linalomtaka Rais Assad aondokea madarakani ndiyo majadiliano hayo yafanyike.
Chanzo:www.kiswahili.rfi.fr

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers asema washambuliaji wake Suarez na Sturridge ndiyo bora zaidi Uingereza

Washambuliaji wa Klabu ya Liverpool Daniel Sturridge na Luis Suarez wakishangilia moja kati ya magoli matatu waliyoshinda dhidi ya Sunderland
Washambuliaji wa Klabu ya Liverpool Daniel Sturridge na Luis Suarez wakishangilia moja kati ya magoli matatu waliyoshinda dhidi ya Sunderland
Na Nurdin Selemani Ramadhani
Kocha Mkuu wa Liverpool Brendan Rodgers ameibuka na kusifu timu yake ndiyo yenye safu hatari zaidi ya ushambuliaji na hili limekuja kutokana na ushindi alioupata kwenye mchezo dhidi ya Sunderland huku washambuliaji wake wawili wakifunga magoli yao matatu. Rodgers amethubutu kutamka hadharani ushirikiano kati ya washambuliaji wake Luis Suarez na Daniel Sturridge ndiyo hatari zaidi kwa sasa na ana uhakika wachezaji hao wawili wataleta mafanikio makubwa sana msimu huu.

Suarez alirejea dimbani baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa michezo kumi na katika mchezo wa kwanza dhidi ya Manchester United kwenye mashindano ya Capital One hakuweza kufunga ila jana alipachika magoli mawili kati ya matatu.
Liverpool imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1 mbele ya Sunderland huku Suarez akipiga magoli mawili na mwenzake Sturridge akifunga goli moja na kuifanya timu hiyo kuzoa pointi tatu muhimu.
Rodgers amewaambia wanahabari hana uhakikika kama kuna ushirikiano bora zaidi ya washambuliaji wake hao wawili kwenye Ligi Kuu nchin Uingereza na kusema maneno yake yataonekana ya kweli kadri michezo itakavyokua inaendelea.
Liverpool imefanikiwa kurejea kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza nyuma ya vinara Arsenal wakitofautiana kwa pointi mbili baada ya kucheza michezo sita hadi sasa.
Rodgers amekiri amefikia uamuzi wa kusema washambuliaji hao wawili ndiyo bora kwa sasa kutokana na umahiri waliouonesha kwenye mchezo dhidi ya Sunderland na hilo lilionekana kwa kila mtu aliyefuatilia mchezo huo.
Kocha huyo ambaye ameshaondolewa kwenye Kombe la Capital One ameendelea kufarijika na kurejea kwa Suarez anayeonekana kuongeza makali ya safu yake ya ushambuliaji kitu kinachomfanya aamini kutakuwa na mapinduzi kwenye safu yake ya ushambuliaji.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi ya Kenya kumhoji Mkuu wa Usalama juu ya shambulizi la kigaidi kwenye Jumba la Biashara la Westgate

Jengo la Biashara la Westgate ambalo lilitekwa na kushambuliwa na Wanamgambo wa Al Shabab
Jengo la Biashara la Westgate ambalo lilitekwa na kushambuliwa na Wanamgambo wa Al Shabab
Na Nurdin Selemani Ramadhani
Maofisa wa Juu wa Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Usalama wa Taifa nchini Kenya wanatarajiwa kuwa na wakati mgumu pale ambapo watakuwa wanahojiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi wakituhumiwa kushindwa kufanyia kazi taarifa za kijasusi walizokuwa nazo juu ya kupangwa kwa Shambulizi la kigaidi katika Jumba la Biashara la Westgate. Mkuu wa Usalama wa Taifa atakuwa na kibarua cha kujibu ni kwa nini alishindwa kuwa na taarifa za kutosha ambazo zingesaidia kuzuia kutokea kwa shambulizi hilo la kigaidi linalotajwa kupangwa na kutekelezwa na Wanamgambo wa Kundi la Al Shabab wenye uhusiano na Mtandao wa Al Qaeda.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi nchini kenya imefikia uamuzi huo wa kumhoji Mkuu wa Usalama wa Taifa kutokana na uwepo wa taarifa zilizovuja na kueleza Kitengo cah Usalama wa Taifa kilikuwa na taarifa za kutokea kwa shambulizi hilo tangu mwaka 2011 lakini walishindwa kuchukua hatua madhubuti kulidhibiti.
Taarifa zimeendelea kuzagaa na kuanisha Kundi la Al Shabab lilishatoa tishio la kushambulia Jumba la Biashara la Westgate pamoja na Kanisa la Mtakatifu Bsilica lililopo Jijini Nairobi lakini hakuna hatua za haraka zilizochukuliwa kuhakikisha kitisho hicho kinafanyiwa kazi kwa wakati.
Vyombo vya Habari zimekuwa vikivujisha taarifa zinazoeleza kuwa Usalama wa Taifa wa Kenya ulivyopata taarifa hizo za onyo la kufanyika kwa mashambulizi walichukua hatua za kuifahamisha Marekani na Israel ili kuhakikisha wanawasaidia kuchukua hatua kukabiliana nalo.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku kwa upande wake amekanusha madai ya kwamba Serikali ilikuwa na taarifa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kutokwa kwa shambulizi hilo na kusema hizo ni taarifa zisizona ukweli wowote na kama wangepata onyo hilo wangelifanyia kazi.
Lenku amewaambia wanahabari Serikali imekuwa makani katika kuhakikisha wanaimarisha hali ya usalama katika nchi yote ya Kenya kwa hiyo wanapopata taarifa kama hizo hawawezi kukaa kimya kwani wanafahamu madhara yanayoweza kutokea ni makubwa.
Katika hatua nyingine Waziri Lenku amekanusha taarifa zilizokuwa zimezagaa ya kwamba zaidi ya watu sabini wamefukiwa kwenye vifusi vilivyochangiwa na kulipuliwa kwa jengo hilo na amesisitiza hakuna mtu mwengine aliyeuawa zaidi ya wale sitini na saba waliotolea maelezo.
Kumekuwa na taarifa na hali ya wasiwasi nchini Kenya kutokana na watu kadhaa kuendelea kusaka ndugu zao ambao hawajulikani walipo huku taarifa ya mwisho ya Shirika la Msalaba Mwekundu likisisitiza watu wanaokadiriwa kufikia sitini hawajulikani walipo.
Serikali nchini Kenya imesisitiza kwenye shambulizi hilo la kigaidi la huko Westgate walifanikiwa kuwaua Wanamgambo watano waliokuwa wamewashikilia mateka na kuwaua wananchi waliokuwa kwenye Jumba hilo.
Chanzo:www.kiswahili.rfi.fr

Watu wapatao 40 wamepoteza maisha nchini Iraq kwenye wimbi la mashambulizi ya kujitoa mhanga

Mabaki ya gari yaliyotumika kwenye shambulizi la kujitoa mhanga Jijini Baghdad nchini Iraq

Baghdad hit by wave of deadly car bombs
Mabaki ya gari yaliyotumika kwenye shambulizi la kujitoa mhanga Jijini Baghdad nchini Iraq
Na Nurdin Selemani Ramadhani

Watu wanaofikia arobaini wamepoteza maisha kwenye wimbo jipya la mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyotekeleza leo nchini Iraq na kuwaacha watu zaidi ya mia moja hamsini na sita wakijeruhiwa wengi wao vibaya.
Mashambulizi hayo ya kujitoa mhanga yametekelexzwa kwa kutumia mabomu tisa yaliyokuwa yametekewa kwenye magari tisa tofauti na kulenga zaidi Jiji la Baghdad katika maeneo yanayokaliwa zaidi ya Waumini wa Kishia.
Taarifa kutoka Jijini Baghdad zinaweka bayana mashambulizi hayo ya mabomu yamepiga sehemu nane tofauti na kuleta madhara kwenye soko la mbogamboga na kusababisha vifo vya polisi saba wakiwemo wanajeshi wawili na wengine kumi na sita wakijeruhiwa.
Maeneo yaliyoathirika zaidi na mashambulizi hayo mabaya zaidi kutekelezwa katika siku za hivi karibuni ni viunga vilivyopo kwenye Jiji la Baghdad ikiwemo Habibiya, Sabaa Al Bour na Kazimiyah.
Sehemu hizo zilizoshambuliwa huwa zinakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu na ngome imara ya waumini wa Kishia ambao wamekuwa walengwa wakubwa wa mashambulizi yanayofanywa na makundi ya Kisunni.
Vyombo vya usalama nchini Iraq vimethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo baya na juhudi za kuwaska waliohusika vimeazishwa huku usalama ukiendelea kuimarishwa katika Jiji lote la Baghdad.
Hadi kufika sasa hakuna Kundi lolote lililotangaza kuhusika kupanga na hatimaye kutekeleza shambulizi hilo lililoongeza hali ya wasiwasi juu ya usalama wa wananchi wa Taifa la Iraq.
Shambulizi lenyewe limekuwa likitajwa kama la kulipiza kisasi kutokana na Ijumaa kutekelezwa kwa mashambulizi mawili ya mabomu jirani kabisa na Msikiti Mkubwa wa Sunni uliopo kwenye Jiji la Baghdad na kuchangia vifo vya waumini sita.
Matukio haya yanafanya idadai ya watu waliopoteza maisha kwenye mashambulizi yaliyofanyika nchini Iraq mwezi Septemba kuzidi kuchupa kwani takwimu zinaonesha mwezi Agosti watu zaidi ya mia nane walipoteza maisha.

Waziri Mkuu wa Israeli Netanyahu kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani Obama juu ya mpango wa nyuklia wa Iran na amani ya Mashariki ya Kati

Rais wa Marekani Barack Obama akijadiliana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Rais wa Marekani Barack Obama akijadiliana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Na Nurdin Selemani Ramadhani

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameelekea nchini Marekani kwa ajili ya kukutana na Rais Barack Obama katika mazungumzo ambayo yanatarajiwa kujiegemeza juu ya mpango wa nyuklia wa Iran na mazungumzo ya kusaka amani ya kudumu ya Mashariki ya Kati. Netanyahu anatarajiwa kukutana na Rais Obama kwa faragha baadaye jumatatu kabla ya jumanne kuhutubia Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa UN huku suala kubwa linalotarajiwa kuzingira mazungumzo hayo ni mpango wa Marekani kutaka kulegeza vikwazo vyake kwa Iran.

Waziri Mkuu Netanyahu amesema atatumia nafasi yake ya mazungumzo na Rais Obama kumueleza ukweli juu ya hatua iliyopigwa na Iran katika mkakati wake wa kutengeneza bomu la nyuklia licha ya taifa hilo kuendelea kukana haijafikia hatua hiyo kwenye mpango wake wa nyuklia.
Netanyahu akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Tel Aviv amesisitiza ukweli wake ataueleza hadi kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa UNGA ili Viongozi wa mataifa mbalimbali waweze kutambua ukweli wa kile kinachoendelea na kufanywa na Serikali ya Tehran kwa siri.
Mazungumzo kati ya Netanyahu na Rais Obama yanakuja kipindi hiki Rais wa Iran Hassan Rouhani akiwa amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kiongozi huyo wa Serikali ya Washington na kumueleza nia yao ya kuhakikisha suluhu inafikiwa juu ya mpango wa nyuklia wa Tehran.
Netanyahu ameendelea kuonesha wasiwasi wake iwapo Iran itatekeleza kwa vitendo kauli yake ya kuwa tayari kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa juu ya mpango wake wa nyuklia huku mwenyewe akisisitiza kinachotakiwa kufanywa na Tehran ni kutangaza kusitisha mkakati wake wa kutengeneza mabomu ya nyuklia.
Waziri Mkuu Netanyahu alikosoa vikali hotuba ya Rais Rouhani aliyoitoa katika Mkutano Mkuu wa Sitini na Nane wa Umoja wa Mataifa UNGA na kusema ilijaa ubinafsi na haikuweza kueleza ni lini watasitisha mchakato wao wa kutengeza mabomu ya nyuklia ambayo ni hatari kwa usalama wa Mashariki ya Kati.
Rais Rouhani alipokelewa na maelfu ya wananchi wa Iran wakimpongeza kwa uamuzi wake aliochukua wa kukubali kushirikiana na mataifa ya magharibi juu ya mpango wake wa nyuklia wakiamini hiyo itasaidia kuondokana na vikwazo vilivyochangia kulemaza ukuaji wa uchumi wao.
Netanyahu kwa upande wake ameendelea kusisitiza kinachofanywa na Rais Rouhani hakina baraka za Kiongozi Mkuu wa Kidini Ayatollah Ali Khamenei ambaye ndiye amekuwa akisisitiza kuendelea kwa mpango wa nyuklia wa Tehran wenyewe lengo la kutengeneza silaha za maangamizi.
Chanzo:www.kiswahili.rfi.fr

MHE. RAIS KIKWETE AHUTUBIA BARAZA KUU UMOJA WA MATAIFA (UN)

Matukio zaidi ya Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye Jukwaa la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Rais Kikwete akihutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mjini New York ambapo katika hotuba hiyo alielezea masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafasi ya Tanzania katika kuchangia walinzi wa Amani, Mageuzi katika Umoja wa Mataifa, Utekelezaji wa Malengo ya Milenia na pia alitoa salamu za rambirambi kwa Serikali ya Kenya kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea tarehe 23 Septeba, 2013 mjini Nairobi.
Mhe. Membe akiwa na Mhe. Haroun Suleiman, Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar wkimsikiliza Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Ramadhan Mwinyi, Naibu Balozi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York akifuatilia hotuba ya Mhe. Rais kwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy huku Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York akisikiliza kwa makini hotuba hiyo.
Balozi Tuvako Manongi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York akiteta jambo na Mhe. Membe.
Mhe. Membe akimpongeza Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kumaliza kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mama Dorcas Membe naye akifurahia mara baada ya kumpongeza Mhe. Rais Kikwete.
Balozi Manongi akimpongeza Mhe. Rais kwa hotuba nzuri.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri, Wabung na Watendaji mbalimbali kutoka Serikalini mara baada ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Rais Kikwete katika mahojiano na Bw. Joseph Msami, Mtangazaji kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kulihutubia Braza Kuu la Umoja wa Mataifa.
chanzo cha habari http://michuzi-matukio.blogspot.com/

TOZO ZA LAINI: WAMILIKI SIMU KUKATWA 3,00/-

TOZO ZA LAINI: WAMILIKI SIMU KUKATWA 3,00/-

  • KUANZIA JULAI MWAKA HUU,TRA YATOA SIKU 14
  • WATEJA WENGI KUKOSA MAWASILIANO HASA VIJIJINI


 Na Mwandishi Wetu

  Kilio cha Watanzania wengi kutaka tozo ya sh. 1,000 kila mwezi kwa laini moja ya simu ifutwe, bado kipo mashakani baada ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuzitaka kampuni za simu nchini kulipa tozo hiyo kuanzia Julai mwaka huu ndani ya siku 14.


 Awali tozo hiyo ilitakiwa kuanza kulipwa Julai mwaka huu, lakini kutokana na malalamiko ya wadau, utekelezwaji huo ulisubiri mapendekezo ya Tume Maalumu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia tatizo hilo.

 Hivi karibuni, Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Simu nchini (MOAT) ulisema asilimia 48 ya Watanzania ndio wanaotumia simu za mkononi sawa na watu milioni 22.Kutokana na tozo hiyo, zaidi ya asilimia 40 hadi 45 watafungiwa simu zao na kudai takribani Watanzania milioni nane, hushindwa kuweka sh. 1,000 kwa mwezi katika laini za simu zao.

MOAT waliongeza kuwa, kuendelea kukua kwa sekta ya mawasiliano hasa maeneo ya vijijini, kutakuwa na mashaka kwani wengi wao watashindwa kumudu gharama za simu hivyo kukwamisha malengo ya Umoja wa Kimataifa katika maendeleo ya mawasiliano. Tume iliyoundwa na Rais Kikwete ilijumuisha wajumbe kutoka TRA, Wizara ya fedha na wawakilishi wa kampuni za simu

 Julai 19 mwaka huu, Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, alisema Serikali imekubali kupitia mawazo na maoni ya MOAT kuhusu kufutwa kwa tozo hiyo ambayo imelalamikiwa na wadau wengi wa sekta ya mawasiliano.

Hali hiyo ilitokana na kauli za baadhi ya viongozi wa Serikali, wabunge na wananchi wanaopinga tozo hiyo wakidai huo ni mzigo kwa watumiaji simu hasa wa kipato cha chini.

Dkt. Mgimwa alisema walikutana na MOAT na kupokea mapendekezo yao ambayo wanayafanyia kazi ili tupunguze makali ya kodi hiyo kwa wananchi wa hali ya chini. Alionya kusiwepo na jazba kwani suala hilo ni la kisheria kwa sababu lilipitishwa bungeni hivyo ili kuondolewa lazima ufuatwe utaratibu kwani hakuna mtu anayelenga kumkamua mwananchi.

  Alisema kodi hiyo ilitokana na mapendekezo 67 yaliyotolewa na Kamati ya Bajeti kuwa chanzo cha mapato kinachotekelezeka lakini kama inaonekana kikwazo, wataliangalia jinsi ya kukabiliana nalo

 Aliongeza kuwa lengo la tozo hiyo ni kupata fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi ya maji, barabara na umeme hasa vijijini ambako kuna changamoto nyingi za maendeleo.

Alisisitiza kuwa, hakuna mtumiaji wa simu ambaye ameanza kukatwa tozo hiyo kutokana na mchakato huo kuwa bado unaendelea katika utekelezaji wake

 Naye Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alisema Serikali itahakikisha mwananchi hapati mzigo usiokuwa na sababu.

Aliongeza kuwa, Serikali ni sikivu na inawasikiliza wananchi wake, hivyo kupitia mawazo na mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa, yatafanyiwa kazi ili kutokuathiri pande zote.

Afrika yadai nafasi yake Baraza la Usalama UN

AFRIKA imesisitiza kuwa haitochoka kudai haki ya kufanyika kwa mageuzi ya msingi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), ili iwe na uwakilishi wa kudumu katika Baraza hilo. ...
Kwa habari zaidi ingia http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/17009-afrika-yadai-nafasi-yake-baraza-la-usalama-un

JK AKOSOA UTENDAJI ICC

 Rais Jakaya Kikwete, amesema mwenendo wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kuhusu Bara la Afrika na viongozi wake, unainyima mahakama hiyo nafasi kubwa ya kuungwa mkono barani Afrika
. Alisema kuanzishwa kwa ICC kumetokana na Mkataba wa Rome ambao ulikuwa ni hatua muhimu katika mfumo wa kimataifa kupambana na makosa ya jinai.Rais Kikwete alitoa msimamo huo mwishoni mwa wiki wakati akilihutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), katika Makao Makuu ya umoja huo, New York, Marekani. 

Katika hotuba yake, Rais Kikwete pia alilaani mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya vikosi vya kimataifa vya kulinda amani katika nchi mbalimbali duniani vikiwemo kutoka Tanzania."Kwa hakika, kuundwa kwa mahakama hii kuliweka mfumo mzuri wa kuondokana na watu kutenda vitendo vya jinai, hata hivyo mwongo mmoja baada ya kuanzishwa mahakama hii, mvutano umezuka kati ya ICC na Bara la Afrika.
"Sasa mahakama hii inaonekana kama taasisi isiyojali maoni na msimamo wa Afrika kwa mambo ambayo kwa maoni yangu ni hofu halali ya Waafrika," alisema Rais Kikwete.Aliongeza kuwa, bado mahakama hiyo inaendelea kupuuza maombi ya mara kwa mara ya Umoja wa Afrika, hivyo ni jambo la kutia huzuni kuwa maombi ya kubadilisha muda wa kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya; na Naibu Rais William Ruto yalipuuzwa na hayakujibiwa.
"Tabia hii imekuwa ni tatizo kubwa linaloleta kikwazo kwa ICC kushindwa kutimiza wajibu wake wa kupambana na tabia ya watu wanaofanya makosa ya jinai kutokuchukuliwa hatua."Kwa hakika, kugangamara kwa ICC hata katika masuala yaliyo wazi, kumethibitika kuwa kunainyima mahakama hii nafasi ya kuendelea kuungwa mkono Barani Afrika," alisema.
Rais alisema Tanzania ni moja ya nchi zinazoshiriki shughuli za kimataifa za kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa ikiwa na zaidi ya walinda amani 2,500 Darfur, nchini Sudan, Lebanon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Alisema Tanzania ni nchi ya sita katika Afrika na 12 duniani kwa kutoa walinzi wa amani duniani ikiridhishwa na mchango mdogo wanaoutoa katika shughuli hiyo.Aliongeza kuwa, wakati mwingine Tanzania inalipa gharama kubwa na maisha ya vijana wake katika shughuli hizi kama ilivyotokea Darfur na DRC ambapo askari wake ambao ni walinda amani walipoteza maisha. Rais Kikwete alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani na Canada na atarejea nchini leo.

Kamati ya Moyo yacharuka Zanzibar

Hassan Nassor Moyo 
Na Mwinyi Sadallah
Zanzibar. Kamati ya Maridhiano Zanzibar imetangaza maazimio sita yanayotakiwa kuzingatiwa katika mchakato wa kupata Katiba Mpya kabla ya Bunge la Katiba kujadili rasimu ya mwisho na kufanyika kura ya maoni mwakani.
Maazimio hayo yametangazwa na Kamati hiyo pamoja na Baraza la Katiba Zanzibar (Bakaza) katika mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika, Shangani mjini Zanzibar jana.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hassan Nassor Moyo alisema Marekebisho ya sheria hiyo yaliyofanywa na Serikali na kupitishwa na Bunge yana upungufu makubwa katika utaratibu kuandaa muswada huo na uchukuaji wa maoni yake.
Alisema kabla ya Rais kusaini muswada huo, wadau kutoka Zanzibar wapewe nafasi ya kutoa maoni yao na urudishwe upya bungeni kujadiliwa na kupitishwa kwa manufaa ya pande mbili za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Aidha, alisema kifungu kinachotoa nafasi kwa wabunge wa Bunge la Katiba kupitisha Katiba kwa wingi wa kura kama theluthi mbili itashindikana kupatikana muafaka, kifutwe na badala yake utaratibu wa awali wa kupitisha kwa kutumia theluthi mbili ubakie kutumika kwa manufaa pande mbili za Muungano.
“Tunapinga kifungu kinachoweka ukomo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya kuwasilisha Rasimu ya mwisho ya Katiba kwa Rais,”alisema Moyo ambaye ni aliwahi kuwa Waziri wa Sheria wa Serikali ya Muungano.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapaswa kuendelea na kazi yake ya kutetea rasimu ndani ya Bunge la Katiba badala ya kuitwa kama waalikwa kama kutaonekana na haja ya kufanya hivyo wakati wa mjadala wa Bunge hilo.
Mambo mengine yaliyopendekezwa na Kamati hiyo ni wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba wawe idadi sawa baina ya Zanzibar na Tanzania Bara hasa kwa kuzingatia Katiba inayopitishwa ni ya Jamhuri ya Muungano unaotokana washirika wawili waliokuwa na sifa sawa kabla ya kuungana mwaka 1964.
Alisema wajumbe 166 wa Bunge la Katiba kutoka makundi mbalimbali ya kijamii na asasi za kiraia wachaguliwe na makundi na taasisi zenyewe badala ya kazi hiyo kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  kushirikiana na Rais wa Zanzibar.
Hata hivyo, alisema Kamati yake inaunga mkono ushauri wa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba wa kutaka  viongozi wa kisiasa na makundi ya kijamii kukutana na kukaa pamoja kuzungumzia mvutano uliyojitokeza baada ya kufanyika kwa marekebisho ya muswada huo.

Hamad: Kikwete usisaini muswada

Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad 
Tanga. Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad amesema mgogoro wa Muungano uliopo unatokana na kufichwa kwa makubaliano yaliyowekwa na waasisi wa Muungano na kusema kero hizo hazitakwisha hadi kutakapoundwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba.
Alisema hayo juzi wakati wa kongamano la Wazanzibar waishio Bara na kusema Muungano uliotiwa saini na waasisi wa Muungano huo umefichwa na kusema dawa yake ni Serikali tatu na  Muungano wa mkataba.
Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013 kwa maelezo kuwa una kasoro.
“Wazanzibari wenzangu na mimi pia ni mmoja wao ambao tunataka Muungano wa mkataba, nilipoulizwa na tume nilisema nataka Muungano wa mkataba nadhani nanyi pia mawazo yenu ni kama mimi,” alisema Hamad.
Hamad aliisifu Serikali ya Kikwete kwa kuwaachia wananchi wenyewe kuiandika katiba yao na kumwomba asikubali kutia saini muswada huo wa sheria.
Alisema Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kama ilivyo kwa nchi nyingine hivyo inahitaji kurejeshewa mamlaka yake na kuwa na uamuzi ikiwa na pamoja kurejeshewa kiti chake katika Baraza la Umoja wa Kimataifa.
“Zanzibar iko na haki ya kuingia mikataba na jumuiya za kimataifa kama ilivyo nchi nyingine, tunataka dola ya Zanzibar iliyo nchi kamili kama ilivyokuwa zamani, Muungano umeifuta Zanzibar katika ramani ya kimataifa,” alisema na kuongeza:
“Hivi sasa Zanzibar haina haki ya kusema inajiunga na jumuiya yoyote ya kimataifa, kikwazo hiki ni kufichika kwa makubaliano ya Muungano kutoka kwa waasisi wetu."

Rais Kikwete ahutubia Baraza Kuu UN

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete akihutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York 
Na Mwandishi Wetu
New York. Rais Jakaya Kikwete juzi alihutubia kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (Unga), New York, Marekani na kusema kama nchi tajiri duniani zingetoa fedha za kutosha kama zilivyokuwa zimeahidi, ni dhahiri kuwa dunia ingeweza kufanikisha utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) na malengo yake yote katika kipindi cha miaka 15 kama ilivyokuwa imeamuliwa mwaka 2000.
Aidha, Rais Kikwete alisema Afrika haitochoka kudai haki ya kufanyika kwa mageuzi ya msingi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), ili kuliwezesha bara hilo lenye idadi kubwa zaidi ya wanachama kwenye Umoja wa Mataifa (UN) kuwa na uwakilishi wa kudumu.
Katika hotuba yake ya dakika 15, Rais Kikwete alisema ni jambo lisiloelezeka kuwa dunia ya leo inaendelea kushuhudia umasikini wakati kuna raslimali na utajiri wa kutosha wa kumaliza tatizo hilo ikiwa kuna utashi wa kisiasa kumaliza tatizo hilo.
Rais Kikwete alikiambia kikao hicho ambacho mada yake kuu ilikuwa `Mjadala Kuhusu Ajenda ya Maendeleo Duniani baada ya mwaka 2015' kuwa pamoja na kwamba umasikini mkali zaidi duniani umepunguzwa kwa nusu katika kipindi cha utekelezaji wa MDG, bado zaidi ya watu bilioni 1.2 wanaishi katika mtego wa umasikini mkubwa.
Alisema kuwa mbali na watu hao, bado kiasi cha watoto wanaokadiriwa kufikia 19,000 chini ya umri wa miaka mitano na wanawake 800 hupoteza maisha kila siku kwa magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika na kutibika.
“Hili ni jambo ambalo halikubaliki kabisa katika dunia iliyojaa neema ya kila aina tunamoishi leo ambako kuna maendeleo ambayo hayajapata kuonekana katika historia ya binadamu ya sayansi na teknolojia ambayo yanaweza kutumika kumaliza changamoto zote za maendeleo zinazokabili jamii ya binadamu sasa.
“Katika dunia ambako kuna chakula cha kutosha kumlisha kila mtu, hakuna sababu ya mtu yeyote kulala na njaa na kukabiliwa na ukosefu wa lishe. Katika dunia yenye utajiri mkubwa kama wa sasa, hakuna sababu kwa nini umasikini, njaa na dhiki viendelee kuleta dhiki na kusababisha shida kubwa kwa watu wengi kiasi hiki.”
Rais Kikwete alisisitiza: “Katika hali hiyo, ni jambo lisiloingia akilini kwa nini Malengo ya Milenia hayakufanikiwa kwa kiwango cha juu kabisa.
“Kama nchi tajiri na zilizoendelea duniani zingekuwa zimetoa fedha na rasilimali za kutosha kama ilivyokuwa imekubaliwa chini ya lengo la nane kwa mipango hiyo kwa mujibu wa makubaliano na ahadi zao katika mikutano ya nchi tajiri duniani ya G8 na G20, tungefanikiwa kutekeleza mipango hiyo,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Kwa maana hiyo, litakuwa ni jambo la kujidanganya kama tulijadili nini tufanye kuhusu Malengo ya Maendeleo ya Milenia Baada ya 2015 bila kujadili na kukubaliana kuhusu jambo la msingi la jinsi ya kugharimia mipango hii.”
Mapema leo, Rais Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na baadaye alikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani (anayeshughulikia siasa), Wendy R Sherman.

Watu 8 bado wanashikiliwa na polisi Kenya

Polisi wa Kenya na wananchi wengine katika jengo la Westgate huko Nairobi September 21, 2013.
Polisi wa Kenya na wananchi wengine katika jengo la Westgate huko Nairobi September 21, 2013.
Maafisa wa Kenya wanasema bado wanawashikilia watu wanane kuhusiana na shambulizi la siku nne lililosababisha vifo kwenye jengo la maduka ya kifahari mjini Nairobi.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya, Joseph Ole Lenku aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kwamba maafisa wamewaachia washukiwa wengine watatu.

Mwanzoni mwa wiki hii maafisa walisema washukiwa wanamgambo watano waliuwawa wakati wanajeshi na polisi walipokuwa wakifanya operesheni ya kukomboa jengo la Westgate. Idadi rasmi ya vifo kutokana na shambulizi hilo imefikia 72.

Wachunguzi wanaendelea kupekua kwenye vifusi vya jengo hilo lililoanguka Ijumaa ya wiki iliyopita. Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya lilisema watu 59 bado hawajulikani walipo kutokana na shambulizi hilo.

Lenku alisema hakuna miili yeyote iliyopatikana kutoka kwenye eneo la tukio. “kwa mujibu wa rekodi za polisi, hakuna ripoti rasmi ya watu waliopotea ambao yawezekana walikuwa kwenye jengo hilo wakati shambulizi likitokea”.
 
Kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia lilidai kuhusika kwa shambulizi na linaapa kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Kenya.
 
Katika mtandao wa Twitter Ijumaa kundi hilo la wanamgambo lilisema shambulizi lake kwenye jengo la Westgate lilikuwa ni mwanzo wa mashambulizi yanayotarajiwa kufanywa nchini humo.