Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, August 31, 2013

Somalia yakaribisha TED-X

Wasomi, wasanii na wafanya-biashara wa Somalia wamekuwa wakizungumza katika mji mkuu, Mogadishu, kwenye ile mikutano inayofanywa sehemu mbali-mbali za dunia iitwayo TED-EX.
Barabara ya Mogadishu
Mazungumzo hayo yaliyofanywa kwenye ukumbi wa mikutano chini ya ulinzi mkubwa, yalihusu mapendekezo na ubunifu wa kuijenga tena Somalia.
Hotuba katika vikao vya TED-EX zimetolewa katika nchi zaidi ya 150.
Imewekwa na Happy Adam

Mandela hakutolewa hospitali

Serikali ya afrika Kusini imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba aliyekuwa kiongozi wa afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye amelazwa hospitali tangu mwezi wa Juni, kwamba alirejeshwa nyumbani Johannesburg Ijumaa usiku.
Picha ya Mandela ikipambana ukuta Johannesburg siku yake ya kuzaliwa, 18th July
Taarifa ya serikali imesema kuwa Bwana Mandela bado yuko hospitali mjini Pretoria na kwamba bado mahtuti, lakini hali yake imetulia.
Kulazwa kwa muda mrefu kwa kiongozi huyo kumewatia wasiwasi raia wa taifa hilo na ulimwengu kwa jumla.
Mandela ambaye ana umri wa miaka 95, alikuwa Muafrika wa kwanza kuwa rais wa taifa la Afrika Kusini, na anaheshimiwa na wengi kama baba wa taifa.

Imewekwa na Happy Adam

Museveni aombwa kumaliza mgogoro Rwanda, Tanzania

\ Rais wa Uganda, Yoweri Museveni 
Dodoma. Mgogoro wa kidiplomasia ulioibuka kati ya Rwanda na Tanzania, jana ulitinga bungeni huku Rais Jakaya Kikwete, akimuomba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuwa msuluhishi wa mgogoro huo.
Hata hivyo, Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alionyesha kutoafiki kuombwa kwa Rais Museveni akisema naye yuko katika kundi linaloitenga Tanzania.
Kauli ya kwamba Tanzania kupitia kwa Rais Kikwete imemuomba Rais Museveni kuwa msuluhishi wa mgogoro huo,ilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la papo kwa hapo aliloulizwa na Mbowe akitaka kupata kauli ya Serikali juu ya kuibuka kwa mgogoro huo wa kidiplomasia na dalili za Tanzania kutengwa.
Katika swali lake la msingi, Mbowe alisema mvutano huo wa kidiplomasia umesababisha Tanzania kutengwa katika shughuli ambazo zilipaswa kuwa za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alikiri kuwapo kwa hali ya  kutoelewana na kwamba hata baada ya kauli ya Rais Kikwete kuwa Tanzania haina uhasama na Rwanda, mvutano unaendelea.
“Mimi ninavyojua Rais (Kikwete) amemuomba Rais wa Uganda Yoweri Museveni ajaribu kuona ni namna gani jambo hili linaweza kusuluhishwa na maneno haya yakapungua,” alisema Pinda.
Waziri Mkuu alisema anaamini busara zitatumika ili kuona jambo hilo linakwisha vizuri lakini kama litaendelea na kuonekana dalili za Tanzania kutengwa busara zaidi itahitajika. Katika swali la nyongeza, Mbowe alisema kinachoonekana, Rwanda wameweza kuwavuta Waganda na Wakenya katika mikakati ya kiuchumi ambao kwa hali ya kawaida ingekuwa ni ya jumuiya
Alisema viongozi wa mataifa hayo wamekutana Kampala na Kenya bila kuwapo kwa Tanzania.
Habari kutoka kwa Daniel Mjema, Mwananchi  (email the author
Imewekwa na Happy Adam

KKKT DAYOSISI YA IRINGA JIMBO LA KUSINI MASHARIKI LASIKITIKA KUONDOKEWA NA MMOJA WA WAZEE WAZAMANI WAANZILISHI WA USHARIKA WA IDETE (MTAA WA LUKOSI) AFARIKI DUNIANI.














 


















M23 wataka mazungumzo baada ya kushindwa Goma.

Jeshi la Congo FADRC baada ya kusambaratisha vikosi vya M23 huko Kibati..
Jeshi la Congo FADRC baada ya kusambaratisha vikosi vya M23 huko Kibati..
Kundi la M23 la jamhuri ya kidemokrasi ya kongo linasema linasitisha mapigano na jeshi la Congo na kuondoka kwenye eneo ambalo mapigano yalikuwa makali katika siku za karibuni ili kuruhusu uchunguzi huru ufanyikwe kuhusiana na mizinga iliyoshambulia Rwanda .

Rwanda jana imeituhumu majeshi ya serikali ya congo kwa kufyetua mizinga na roketi ndani ya ardhi yake , lakini umoja wa mataifa na serikali ya Kigali wanakilaumu kundi la M23 kwa mashambulio hayo.

Kiongozi wa kundi la M23  Bertrand Bisimwa aliiambia VOA kwamba wapiganaji wake wanaondoka kwenye maeneo yao katika kijiji cha Kanyaruchinya , karibu na Goma kwenye mpaka wa Congo na Rwanda ili kuruhusu uchunguzi ufanyike  kuamua nani hasa alihusika.
Jeshi la Congo

Naye msemaji wa majeshi ya serikali FARDC Olivia Amuli  akizungumza na VOA  amesema kwamba wanajeshi wa serikali wamerudisha nyuma wapiganaji wa M23 jana na M23 wameondoka kwasababu ya kupata pigo kubwa aliongeza kuwa baada ya mapambano ya siku 9 hatimaye  wamedhibiti  maeneo ya Kibati  na Kilimanyoka na kusema waasi hao wamekimbia huku wakiwa wameacha magari yao yaliopigwa na mabomu.

Wakati huo huo msemaji wa jeshi la Congo alishiriki kwenye mjadala na idhaa ya Kiswahili ya VOA msemaji huyo wa serikali alieleza kwamba M23 wamepiga mabomu huko Goma na nchini Rwanda ili wapate usaidizi wa Rwanda huko Congo na sasa wameondolewa huko Kibati akidai kuwa M23 wanadanganya wananchi . Kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa.

Imewekwa na Happy Adam


IGP aibiwa upanga wa dhahabu

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said Mwema 
Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.
Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.
IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.
Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi husika.
Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.
Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.

Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo.
Imewekwa na Happy Adam

Friday, August 30, 2013

PICHA ZA MKESHA WA MSIBA WA ASKOFU KULOLA KANISANI TEMEKE

Angalia baadhi ya picha kutoka kanisa la E.A.G.T Temeke jijini Dar es salaam ambako ndiko ulipo msiba wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa hilo la Evangelistic Assemblies of God, marehemu Dkt. Moses Kulola aliyefariki dunia jana asubuhi jijini Dar es salaam.

Mchungaji Florian Katunzi wa City Centre ambaye anahusika na taratibu za msiba, akizungumza na wenzake msibani hapo.

Watu wakibadilishana mawazo.
Kina mama nao wapo msibani hapo kumsindikiza askofu Kulola.
Waombolezaji wakipata chakula msibani hapo.
Askofu Bruno Mwakibolwa mwenye shati ya kitenge akiwa na mwenzake katika kikao.
Kikao cha baadhi ya watumishi wa E.A.G.T jimbo la Temeke.
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Flora Mbasha ambaye pia ni mjukuu wa marehemu Kulola akirejea msibani hapo usiku akitokea hospitalini ambako alikuwa amepelekwa baada ya kuzimia msibani hapo.
Emanuel Mbasha kushoto akizungumza na wafiwa wengine msibani hapo.

Mjane wa askofu Kulola akimuuliza mjukuu wake Flora anaendeleaje baada ya mwimbaji huyo kuingia ndani.
Flora akiwa na bibi yake mke wa marehemu askofu Kulola.


Wafiwa wakiwa ndani msibani hapo.
Mwimbaji Rebecca Imagaba akimtukuza Mungu.

New Jerusalem Choir watoto wa Mito ya baraka wakiimba msibani hapo.



Innocent hakuwa nyuma katika kumsifu Mungu.
Mambo ya muziki na vipaza sauti yalikuwa sawa.
Ambilikile akimsifu Mungu mahali hapo, anaushuhuda mzito wa maisha yake na jinsi Mungu alivyomtumia askofu Kulola kumponya.

Uimbaji ulikuwa mwema na mzuri usiku wa kumakia leo.
Picha na Gospel Kitaa