Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, October 7, 2013

Fifa yapambana na ubaguzi

Uwanja wa klabu ya AC Milan wa San Siro umefungwa kwa mashabiki kwa mechi ijayo kama adhabu kwa matusi walioangua wakati wa mechi hapo jana.
Hii ni mara ya pili kwa Milan kukumbwa na hatua kama hii iliyoidhinishwa na Jaji wa Ligi ya Serie A.
San Siro
San Siro
Hukumu hio itaanza kwenye mechi ijayo dhidi ya Udinese iliyopangwa tareh 19 Octoba. Pamoja na marufuku hio klabu imetozwa faini ya takriban dola za Marekani $68,000).
Kwingine Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michezl Platini amesema kua mchezo huo unafaa kuongoza juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi katika michezo.
Kiongozi huyo aliyasema hayo kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa FIFA kutoka Afrika kusini Tokyo Sexwale amesema kwenye mkutano huo unaojadili ubaguzi wa rangi na mchezo wa mpira kwamba utandawazi wa vipimo vya ubaguzi wa rangi ni muhimu katika juhudi zake kupambana na ubaguzi wa rangi.
Mwanaharakati huyo wa ANC amesema kua FIFA ina mipango ya kuandaa mkutano wa kilele juu ya ubaguzi wa rangi kwa ushirikiano na Wkfu wa Mandela mapema mwaka ujao.''
FIFA litatoa maelezo zaidi kuhusu mpango wake wa kupambana na ubaguzi rangi kwenye mkutano wake huko Qatar mwezi Disemba.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment